SAYANSI 2005
Chaguajibu sahihi na andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasiya kujibia.
1. Zilizoorodheshwa hapa chini ni sehemu za jicho la binadamu isipokuwa
- siliari
- retina
- mboni
- shata
- irisi
Chagua Jibu
2. Usambazaji wa chakula mwilini hufanywa na:
- damu
- maji
- hewa
- misuli
- neva
Chagua Jibu
3. Kemikali inayotumika kutambua iwapo chakula Fulani ni cha aina ya wanga ni:
- besi
- alkoholi
- aside
- alkali
- ayodini
Chagua Jibu
4. Ombwe katika chupa ya chai (kielelezo namba 1) huzuia upotevu wa joto kwa njia ya:
|
Kielelezo Na. 1 |
- kuakisi
- mpitisho
- msafara na mpitisho
- mnururisho
- msafara na mnururisho
Chagua Jibu
5. Taswira halisi hufanywa na vitu vyenye tabia ya:
- kutupa mwanga kwenye kiwambo
- kukusanya mwanga
- kutawanya mwanga
- kuruhusu mwanga kupenya
- kuzuia kupinda kwa mwanga
Chagua Jibu
6. Mbung'o husababisha ugonjwa uitwao
- matende
- surua
- kipindupindu
- malale
- malaria
Chagua Jibu
7. Maji magumu aushi yanaweza kubadilishwa kuwa maji laini kwa
- kuyachemsha
- kuyachuja
- kuyatonesha
- kuyagandisha
- kuyapasha joto
Fungua Jibu
8. Kiini cha ugonjwa kinachooneshwa katika kielelezo namba 2 kinaitwa
|
Kielelezo Na. 2 |
- bacteria
- plasmodiamu
- kirusi
- amiba
- fungi
Chagua Jibu
9. Uga wa sumaku ni eneo
- lililoko kwenye sumaku
- ambalo unga wa chuma huonekana
- ambalo nguvu ya sumaku hupatikana
- linaloonesha sehemu za kaskazini na kusini za sumaku
Chagua Jibu
10. Wakati wa kiangazi mimea hupukutisha majani kwa sababu ya:
- kuruhusu majani mapya yaote
- kukomaa sana
- kuongeza rutuba ardhini
- kuruhusu maua yaote
- kupunguza upotevu wa maji
Chagua Jibu
11. Shinikizo la damu hutokana na:
- mafuta
- ateri kuwa kubwa
- kupasu a kwa vena
- mgandamizo wa mishipa
- vena ku kubwa
Chagua Jibu
12. Ni muhimu kuchukua tahadhari zifuatazo wakati wa vita isipokuwa:
- kusafisha mazingira kwa kukata miti
- kujenga nyumba imara
- kuhifadhi chakula
- kuchimba mahandaki
- kuhamia mahali pengine
Chagua Jibu
13. Mlo kamili ni ule wenye mchanganyiko ufuatao:
- muhogo, maharage, mayai, maziwa na tunda
- tunda, mayai, wali, karanga na nyama
- mkate, mchicha, kunde, karanga na tunda
- ugali, mayai, samaki, wali na tunda
- mchicha, karanga, mayai, maharage na tunda.
Chagua Jibu
14. Sayari hutofautiana na nyota kwasababu sayari:
- ni kubwa kuliko nyota
- zina mwanga wa asili
- zipo katika hali ya gesi
- hazizunguki jua
- huzungukwa na mwezi au miezi
Chagua Jibu
15. Ulinganifu wa rula inayooneshwa katika kelelezo namba 3 utapatikana tu iwapo uzito wa P utakuwa gm .
|
Kielelezo 3 |
- 46
- 16
- 10
- 40
- 24
Chagua Jibu
16. Watu wanaofanya mazoezi ya viungo wanapaswa kula chakula chenye wingi wa:
- protini
- kabohaidreti
- vitamin D
- vitamini C
- madini
Chagua Jibu
17. Herufi J katika kielelezo namba 4 inawakilisha mshipa unaotoa damu kutoka kwenye moyo unaoitwa:
|
Kielelezo Na. 4 |
- venakava
- auriko
- ventriko
- vena
- aorta
Chagua Jibu
18. Roda aina ya abedari na kamba husahilisha kazi zaidi kwasababu:
- nguvu nyingi hutokana na mashine yenyewe
- huongeza nusu ya nguvu ya kubebea mzigo
- husaidia kubadili uelekeo wa nguvu
- wingi wa kamba huongeza msuguano
- mzigo hufungwa mwisho
Fungua Jibu
19. Nyakati za joto kali, si vema kuvaa nguo nyeusi kwasababu nguo hizo:
- huakisi mwanga
- hukinga joto
- huakisi joto
- husharabu joto
- hupindisha nuru.
Chagua Jibu
20. Kitumi cha umeme kinachobadili mkondogeu wa umeme kuwa mkondo mnyofu huitwa:
- rektifaya
- transista
- amplifaya
- resista.
- transfoma
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |