STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2022
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
03 MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI
Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2022
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu maalum (OMR) uliyopewa.
1. Ubunifu ni kipengele muhimu katika ujasiriamali. Je, nini kitatokea endapo ubunifu utakosekana?
Wajasiriamali kukosa motisha
Polisi kuingilia kati biashara
Wajasiriamali kupoteza wateja
Wajasiriamali kuongeza wateja
Serikali kutunga sheria
Chagua Jibu
2. Je, mjasiriamali ni mtu wa namna gani?
Mwenye kukata tamaa upesi
Mwenye kutegemea mawazo ya wengine
Mwenye matumaini ya kuwa tajiri kwa haraka
Mwenye kukasirika haraka apatapo hasara
Mwenye kutumia fursa vizuri
Chagua Jibu
3. Amani ni mjasiriamali ambaye ameajiri watu wanne kwenye biashara zake. Je, huo ni aina gani ya ujasiriamali?
Kati
Mdogomdogo
Mdogo
Mkubwa
Makini
Chagua Jibu
4. Ardhi ni rasilimali ambayo isipotunzwa vizuri inaweza kusababisha hatari katika maisha ya viumbe hai na rasilimali nyingine. Ipi ni njia bora itakayotumika kutunza rasilimali hiyo?
Kuongeza idadi ya wakulima mashambani
Kutoa elimu juu ya uhifadhi na utunzaji wa ardhi
Wananchi kuhimizwa kutumia mbolea za viwandani
Kuacha kupanda miti katika maeneo ya wazi
Kuhimiza wafugaji kuongeza idadi ya mifugo
Chagua Jibu
5. Tanzania imebahatika kuwa na rasilimali nyingi, mojawapo imebeba nyinginezo katika mazingira. Rasilimali hiyo ni ipi?
Madini
Misitu
Mifugo
Mbuga za wanyama
Ardhi
Chagua Jibu
6. Mwalimu Kasese aliwaambia wanafunzi wake wataje madini na mikoa yanapopatikana nchini Tanzania. Je, walitaja mkoa gani makaa ya mawe yanapatikana?
Manyara
Mbeya
Kagera
Morogoro
Mara
Chagua Jibu
7. Wakati wa kipindi, mwalimu aliwataka wanafunzi wataje fursa za kibiashara zinazoweza kupatikana pembezoni mwa bahari ya Hindi. Lipi kati ya yafuatayo lingekuwa jibu lao?
Kutengeneza mikanda ya ngozi
Kuzalisha maziwa
Kuuza madawa ya mifugo
Kuuza ngozi za wanyama
Utalii
Chagua Jibu
8. Mwalimu Timamu alifundisha kuhusu kilimo cha mazao ya biashara kilichofanywa Tanganyika kabla ya uhuru. Je wanafunzi walifundishwa mazao yapi?
Zabibu, kahawa, chai na maharage
Mahindi, kahawa, chai na pareto
Kahawa, pareto, mkonge na chai
Pareto, korosho, chai na mahindi
Korosho, maharage, mkonge na pareto
Chagua Jibu
9. Inapendekezwa kuwa shughuli za kibinadamu ziwe rafiki kwa mazingira iii kuzuia kuharibika
kwa tabaka la ozoni. Ni shughuli ipi sahihi katika kulinda tabaka hilo?
A Kufuga mifugo mingi katika eneo dogo B Kuvua kwa kutumia baruti
C Uchimbaji wa madini D Upandaji wa miti
Kutumia mbolea za viwandani kwa wingi
Chagua Jibu
10. Mwalimu alifundisha umuhimu wa tabaka la ozoni kwa maisha ya viumbe hai na vitu vinavyoathiri uimara wa tabaka la ozoni. Je mwalimu alitaja kitu gani kinachoathiri uimara wa tabaka la ozoni?
Upepo
Hewa ya oksijeni
Radi
Mvua
Gesi ya kloroflorokaboni
Chagua Jibu
11. Meli ya mizigo iliyoko mji wa Brasilia 450 Magharibi huanza safari siku ya Jumatatu saa 4:00 usiku. Muda huo utakuwa ni saa ngapi katika mji wa Kabul ulioko 75° Mashariki?
Jumatatu 6:00 usiku
Jumanne 5:00 usiku
Jumanne 12:00 asubuhi
Jumatatu 6:00 mchana
Jumanne 12:00 jinni
Chagua Jibu
12. Mwalimu Kulwa aliwafundisha wanafunzi wake kuhusu mistari ya kufikirika inayochorwa katika ramani. Je, ni mistari ipi aliwafundisha kuwa huchorwa kutoka upande wa Kaskazini kuelekea Kusini?
Tropiki
Latitudo
Mstarihi
Longitudo
Ikweta
Chagua Jibu
13. Jasiri anayeishi katika mji wa Handani, alianza kuangalia mechi katika televisheni saa 9:00 alasiri na rafiki yake Juhudi anayeishi katika mji wa Mikoko uliopo longitudo 40° Mashariki, alianza kuangalia mechi hiyo saa 7:00 mchana. Je, mji wa Handani upo longitudo ngapi?
70° Magharibi
30° Magharibi
90° Mashariki
70° Mashariki
30° Mashariki
Chagua Jibu
14. Bara la Afrika lina mashujaa wengi ambao walipinga ukoloni mamboleo. Mashujaa gani wa Afrika Mashariki waliopinga ukoloni huo?
Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na Samora Machel
Julius K. Nyerere, Kwame Nkrumah na Nelson Mandela
Jomo Kenyatta, Julius. K. Nyerere na Milton Obote
Patrice Lumumba, Julius. K. Nyerere na Kwame Nkrumah
Jomo Kenyatta, Kamuzu Banda na Samora Machel
Chagua Jibu
15. Tanzania imeongozwa na Mawaziri wakuu wengi tangu uhuru. Je, Mawaziri wapi walishika nyazifa wakati wa Mwalimu Nyerere?
Rashid Mfaume Kawawa na Joseph Sinde Warioba
Rashid Mfaume Kawawa na Edward Moringe Sokoine
John Samweti Malecela na Mizengo Kayanza Pinda
Edward Ngoyai Lowassa na Cleopa David Msuya
Edward Moringe Sokoine na Fredrick Sumaye
Chagua Jibu
16. Ni kwa jinsi gani Uganda ilipata uhuru wake?
Kupitia vita vya msituni
Kupitia mapinduzi
Kupitia vita
Kupitia njia ya Katiba
Kupitia ushirikiano
Chagua Jibu
17. Kiongozi yupi aliongoza mapambano ya kudai uhuru wa watu weusi nchini Afika ya Kusini?
Julius Kambarage Nyerere
De Clerk
Keneth Kaunda
Nelson Mandela
Kwame Nkurumah
Chagua Jibu
18. Katika karne ya 19, Pwani ya Afrika Mashariki ilitembelewa na wageni wengi kutoka Sara la Asia. Nini lilikuwa lengo lao kuu?
Shughuli za kijeshi
Shughuli za kisiasa
Shughuli za kiutamaduni
Shughuli za kiuchumi
Shughuli za kijamii
Chagua Jibu
19. Kwa nini Wareno walijenga ngome nyingi maeneo ya Pwani?
Kuwalinda Waafrika dhidi ya Waarabu
Kulinda maslahi yao ya kibiashara
Kuwalinda Waarabu wasivamiwe na Waafrika
Kuonyesha nguvu zao za kijeshi kwa Waafrika
Kuwafundisha Waafrika mbinu za kijeshi
Chagua Jibu
20. Fatuma ni binti wa kaka yangu, Casmir ni mtoto wa kiume wa dada wa baba yake Fatuma. Je, Fatuma atamwitaje Casmir?