STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
03 MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI
Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2021
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
9. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu maalum kujibia (OMR) uliyopewa.
1. Maji ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania. Bainisha vyanzo vikuu vitatu vya rasilimali hiyo.
Mvua, maziwa na bahari
Bahari, visima na mito
Mvua, maji yaliyo juu na Chini ya ardhi
Maziwa, mito na chemchemi
Visima, chemchemi na mvua
Chagua Jibu
2. Kupungua kwa theluji katika mlima Kilimanjaro kumesababishwa na ongezeko la joto katika uso wa dunia. Ni shughuli ipi inaweza kutumika kukabiliana na tatizo hilo?
Kuchoma misitu na kukata miti
Kulima kandokando ya milima
Kupanda miti na kutunza mazingira
Uvunaji ovyo wa misitu
Kufuga mifugo mingi katika eneo dogo
Chagua Jibu
3. Mtaalamu wa masuala ya mazingira aliwaasa wanakijiji waishio kando ya mto Mzinga kuacha tabia ya uharibifu na uchafuzi wa chanzo cha maji. Je, ni vitendo gani aliwashauri kuviacha?
Kupanda miti, kuchoma misitu na kutupa taka katika mto
Kulisha mifugo, kupanda nyasi na kutupa taka katika mto
Umwagiliaji, kutengeneza matuta na kutiririsha maji taka.
Kulima, kulisha mifugo na kukata miti
Kuchakata malighafi, kuoga na kupozea mitambo
Chagua Jibu
4. Mtaalamu wa madini aliwatembelea wanafunzi wa Darasa la Saba na kuwafundisha aina mbalimbali za madini na kazi zake. Je ni madini yapi hutumika kukatia vioo?
Dhahabu
Almasi
Fedha
Tanzanaiti
Shaba
Chagua Jibu
5. Mzee Mahiya ni mfugaji ambaye huhamahama na idadi kubwa ya mifugo. Ni madhara yapi husababishwa na aina hii ya ufugaji?
Mafuriko
Kustawi kwa uoto wa asili
Kufa kwa mifugo
Kupotea kwa misitu
Kuharibika kwa mazao
Chagua Jibu
6. Bwawa la Nyerere ni mojawapo ya chanzo kinachotarajiwa kuzalisha nishati ya umeme wa maji nchini Tanzania. Je, bwawa hili limejengwa katika mto gani?
Ruaha
Ruvuma
Ruvu
Rufiji
Pangani
Chagua Jibu
7. Musa hutoka jasho kwa wingi wakati wa msimu wa joto. Je, utamshauri avae nguo ya rangi gani?
Nyeupe
Nyeusi
Bluu
Njano
Kijani
Chagua Jibu
8. Kuongezeka kwa joto duniani kunakosababishwa na shughuli za kibinadamu kama Vile uchomaji wa misitu, uzalishaji wa gesiukaa kutoka viwandani na uchomaji wa mkaa husababisha madhara yafuatayo isipokuwa
kuyeyuka kwa theluji katika mlima kilimanjaro.
kupotea kwa bayoanuai.
kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari.
kuongezeka kwa uoto wa asili.
kutokea kwa ukame.
Chagua Jibu
9. Mtaalamu wa hali ya hewa alisoma kiwango cha juu cha jotoridi la siku kama nyuzi joto 420C na kiwango cha Chini 200C. Upi ni utofauti wa kiwango cha jotoridi kwa siku?
620C
620F
220F
220C
1340F
Chagua Jibu
10. Wanafunzi wa Darasa la Nne walijifunza juu ya uhusiano uliopo kati ya jua, mimea na maji juu ya uso wa dunia. Yapi ni matokeo ya uhusiano huo?
Kutokea kwa upepo
Kufanyika kwa mvua
Kuganda kwa maji
Kutokea kwa kimbunga
Kuyeyuka kwa barafu
Chagua Jibu
11. Katika uso wa Dunia kuna pepo zinazovuma kutoka eneo moja kwenda jingine. Je, ni upepo gani unavuma kutoka Kusini kuelekea Kaskazini?
Upepo wa Kusi
Upepo wa Kaskazini
Upepo mkavu
Upepo wa Magharibi
Upepo unyevu
Chagua Jibu
12. Tanzania ina makabila mengi yenye mila nzuri na potofu. Ni mila ipi yenye madhara kwa jamii?
Kuruhusu wanawake wajawazito kula mayai
Kukeketa watoto wa kike
Kufundisha wavulana na wasichana kuhusu maadili
Kutahiri wavulana
Kuwapa wanawake haki sawa na wanaume
Chagua Jibu
13. Kila jamii inchini Tanzania ina michezo yake ya asili kulingana na mazingira, muda na utamaduni. Ipi ni mifano ya michezo hiyo?
Mpira wa miguu, ngumi na kukimbia
Kukimbia, kuogelea na mpira wa miguu
Kurusha mkuki, kuruka kamba na kukimbia
Mpira wa miguu, pete na kuogelea
Mpira wa kikapu, miguu na pete
Chagua Jibu
14. Ni kwa namna gani jamii inaweza kukabiliana na tamaduni zilizopitwa na wakati?
Kudumisha umoja wa kitaifa
Kudumisha misingi ya uzalendo
Kuwa na misingi ya mila na desturi zinazofanana
Kupenda jamii na taifa
Kufanya majadiliano na jamii inayohusika
Chagua Jibu
15. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kuburudisha na kuwaunganisha raia wake. Ni taasisi ipi inayohusika zaidi katika kusimamia na kuendeleza michezo inchini Tanzania?
Baraza la Sanaa la Taifa
Baraza la Kiswahili la Taifa
Baraza la Michezo ya Ridhaa la Taifa
Baraza la Michezo la Taifa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Chagua Jibu
16. Yafuatayo huweza kutokea kwa taifa linalokuza utamaduni wake isipokuwa
kudumisha misingi ya uzalendo
kuiga tamaduni za kigeni
kudumisha umoja
kulinda asili yake
kuwepo kwa uhusiano mzuri katika jamii.
Chagua Jibu
17. Kasuku anaipenda nchi yake, ana moyo wa kujitoa kwa Taifa lake na ni mtunzaji mzuri wa rasilimali za Taifa. Kasuku anaweza kuwa na sifa ipi kwa taifa lake?
Mlinzi wa rasilimali za nchi
Mzalendo kwa taifa lake
Mtunzaji wa miiko ya jamii
Mlinda usalama wa jamii
Msimamizi wa umoja wa wananchi
Chagua Jibu
18. Katika mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika, vyama vingi vilishiriki kwa malengo tofauti. Ni chama gani kiliungwa mkono na serikali ya kikoloni ili kukidhoofisha chama cha TANU?
Tanganyika African Association (TAA)
Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP)
Afro Shirazi Party (ASP)
African National Congress (ANC)
United Tanganyika Party (UTP)
Chagua Jibu
19. Jumuiya ya Afrika Mashariki ina makao makuu yake ambapo taasisi zake zote huwepo na kazi muhimu zote hufanyika hapo. Je, makao makuu yanapatikana wapi?
Mombasa nchini Kenya
Kigali nchini Rwanda
Juba nchini Sudan Kusini
Entebbe nchini Uganda
Arusha nchini Tanzania
Chagua Jibu
20. Licha ya kugawanywa kwa Bara la Afrika katika mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885, Afrika iligawanywa tena baada ya vita vya kwanza vya dunia miongoni mwa mataifa ya Ulaya isipokuwa