MAARIFA YA JAMII - 2018
SEHEMU A
URAIA
Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibuhullosahihi katika fornu maaLÂkujibia.
1. Mtu anayedhibiti mwenendo wa wanafunzi shuleni ni..
- Mwenyekiti wa kamati ya shule
- Mwalimu wa nidhamu
- Mwalimu mkuu msaidizi
- Mwalimu wa taaluma
- Mwalimu wa somo
Chagua Jibu
2. Chombo cha juu katika maamuzi kwenye serikali ya kijiji ni ..................
- Serikali ya kijiji
- Kamati ya ulinzi na usalama
- Mkutano mkuu wa kijiji
- Afisa Mtendaji wa kijiji
- Kamati ya Maendeleo ya kijiji
Chagua Jibu
3. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya huchaguliwa na...................
- Mkurugenzi mtendaji wa wilaya
- Baraza la madiwani
- Waziri katika ofisi ya Rais
- Afisa Mtendaji wa Kata
- Wenyeviti wa vijiji
Chagua Jibu
4. Ipi kati ya sarafu zifuatazo ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar?.................
- Sarafu ya shilingi mia moja
- Sarafu ya shilingi mia mbili
- Sarafu ya shilingi hamsini
- Sarafu ya silingi ishirini
- Sarafu ya shilingi kumi
Chagua Jibu
5. Maliasili zinazovutia watalii na kuchangia katika kukuza uchumi wa Tanzania ni..................
- ardhi
- mito
- mifugo
- madini
- mbuga za wanyama
Chagua Jibu
6. Wajibu wa serikali katika kujenga maadili ya viongozi ni....................
- Kuwakopesha magari viongozi wote
- Kuimarisha mfumo wa chama kimoja cha siasa
- Kusimamia sheria za utumishi wa umma
- Kuhamisha watumishi wasio waadilifu
- Kuajiri watumishi wenye elimu ya juu to
Chagua Jibu
7.Tofauti kati ya mila na desturi ni....
- Mila hubadilika mara kwa mara kuliko desturi
- Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mila
- Mila ni mazoea wakati desturi ni vitendo
- Mila ni mazoea na huweza kubadilika na kuwa desturi
- Desturi hubadilika mara kwa mara kuliko mazoea
Chagua Jibu
8. Matumizi ya ofisi ya umma kwa manufaa binafsi huitwa.................
- takrima
- rushwa
- uzalendo
- ubinafsi
- ujasiriamali
Chagua Jibu
9. Zipi kati ya nchi zifuatazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola?................
- Botswana na Burundi
- Botswana na Zambia
- Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Malawi na Burundi
- Zambia na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo
Chagua Jibu
10. Moja ya matukio yanayokiuka Haki za Binadamu nchini Tanzania ni.............
- Mauaji ya vikongwe na maalbino
- Ukataji na upandaji mid
- kuwafungulia mashtaka wahalifu
- kufukuzwa kazi viongozi wasio waadilifu
- Serikali kusimamia ukusanyaji kodi
Chagua Jibu
11. Mojawapo ya njia ambazo wananchi wanaweza kushiriki katika ulinzi na usalama ni...............
- kupiga wahalifu
- kufanya mazoezi ya viungo
- kuwaua wahalifu
- kuwafichua wahalifu
- kuwa rafiki na wahalifu
Chagua Jibu
12.Viashiria vya utandawazi ni pamoja na...............
- kupungua kwa tofauti ya kipato
- uchumi wa soko huria
- kupungua kwa umaskini
- kuwepo kwa ushindani wa kutengeneza silaha
- kuwepo kwa bidhaa nyingi toka viwanda vya ndani
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
:hagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu h u b sahihi katika karatasi ya kujibia.
13. Baba wa baba yako anaitwa
- baba
- mjukuu
- mjomba
- babu
- mpwa
Chagua Jibu
14.Ni Taifa lipi la kibepari liliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1891 hadi 1918?
- Ujerumani
- Uingereza
- China
- Ureno
- Ufaransa
Chagua Jibu
15. Kwa nini Berlin ni miongoni mwa miji maarufu katika historia?
- Ni Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa
- Ni Makao Makuu wa Jumuiya ya Madola
- Ni mji uliokuwa kitovu cha biashara ya utumwa
- Ni mji wa Ufaransa ambao uliendesha utawala wa kulisha kasumba
- Ni mji ambao mgawanyo wa Bara la Afrika ulifanyika
Chagua Jibu
16.Mataifa makubwa ya kibepari yaliyogombania Bara la Afrika yalikuwa
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Ureno
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uchina, Uhispania na Marekani
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Japani, Uhispania na Ubelgiji
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Japani
- Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Italia na Uchina
Chagua Jibu
17. Mwanzilishi wa Kampuni wa Kibiashara ya Kiingereza ya Afrika Mashariki anaitwa
- David Livingstone
- Karl Peters
- Mungo Park
- William Mackinnon
- Seyyid Said
Chagua Jibu
18. Julius Von Soden alikuwa nani?................
- Gavana wa kwanza wa kiingereza katika Tanganyika
- Gavana wa kwanza wa kijerumani katika Tanganyika
- Gavana wa mwisho wa kijerumani katika Tanganyika
- Gavana wa mwisho wa Kiingereza katika Tanganyika
- Gavana aliyeanzisha utawala wa moja kwa moja katika Tanganyika
Chagua Jibu
19. Mtaalamu wa mambo wa kale aliyevumbua fuvu la binadamu wa kwanza Olduvai aliitwa
- Charles Darwin
- Zinjathropus
- Homo Habilis
- David Livingstone
- Louis Leakey
Chagua Jibu
20. Ni lini binadamu alianza kuchoma misitu iii kuwafukuza wanyama wakali?.................
- Wakati wa Zama za Chuma
- Wakati wa Zama za Mwanzo za Mawe
- Wakati wa Zama za Kale za Mawe
- Wakati wa Zama za Mwisho za Mawe
- Wakati wa Zama za Kati za Mawe
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |