STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2017

11. Ipi kati ya mila zifuatazo inaweza kueneza ITVU/UKIMWI?........

 1.  Ngoma za asili 
 2.  Miiko ya chakula
 3.  Kuzaa watoto wengi 
 4.  Kurithi wajane
 5.  Mahari
Choose Answer :


12. Kuna makundi mangapi ya uoto wa asili?

 1.  Matatu 
 2.  Manne 
 3.  Mawili 
 4.  Matano 
 5.  Sita
Choose Answer :


13. Lengo kuu la mabadiliko ya katiba ya Tanzania mwaka 1962 yalikuwa

 1. kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
 2. kuunda serikali ya shirikisho
 3. kuunda serikali ya mtaa
 4. kuunda serikali ya jamhuri
 5. kuunda serikali ya mpito.
Choose Answer :


14. Umoja wa Afrika ulianzishwa rasmi mwaka gani?

 1.  2002 
 2.  2001 
 3.  1963 
 4.  1945 
 5.  1999
Choose Answer :


SEHEMU B
HISTORIA        

Chagua jibu sahihi kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililosahihi katika fomu maalumu(OMR) ya kujibia.

15. Familia ya ndugu na jamaa inakaribia kufanana na kundi la jamii inayojulikana kama: 

 1.  kabila 
 2.  jamii 
 3.  ukoo 
 4.  jirani 
 5.  kijiji
Choose Answer :


16. Ubugabire ni mfumo wa Umwinyi uliajengwa juu ya umiliki wa:

 1.  ngombe 
 2.  viwanda 
 3.  ardhi
 4.  wafanyakazi wa kigeni 
 5.  watumwa
Choose Answer :


17. Mfumo wa kwanza ambapo jamii ilimiliki njia zote za uzalishaji kijamaa huitwa:.............

 1.  Umwinyi 
 2.  Ukomunisiti 
 3.  Ujamaa
 4.  Urafiki 
 5.  Ujima
Choose Answer :


18. Mkataba upi uliharamisha biashara ya utumwa Afrika Mashariki mwaka 1873?

 1.  Mkataba wa Moresby 
 2.  Mkataba wa Hamerton
 3.  Mkataba wa Berlin 
 4.  Mkataba wa Heligoland
 5.  Mkataba wa Frere
Choose Answer :


19. Mwenendo mzima wa maisha ya binadamu unaitwa

 1.  historia 
 2.  utamaduni 
 3.  Desturi 
 4.  demokrasia 
 5.  mila
Choose Answer :


20. Utandawazi umebadili dunia na kuwa kama aliitwa..................

 1.  nchi 
 2.  wilaya 
 3.  mpira 
 4.  kijiji 
 5.  kata
Choose Answer :


21. Umoja wa Mataifa ulianzishwa mwaka:

 1.  1955 
 2.  1945 
 3.  1995 
 4.  1885 
 5.  1950
Choose Answer :


22. Mreno wa kwanza kufika sehemu ya Kusini mwa Afrika:

 1.  King Henry 
 2.  Bartholomew Diaz
 3. Vasco Da Gama 
 4.  David Livingstone
 5.  Cecil Rhodes
Choose Answer :


23. Sababu mojawapo ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa ilikuwa:

 1.  Huruma ya wazungu juu ya mateso ya watumwa
 2.  Waafrika kupigania uhuru wao
 3.  Kupata masoko ya bidhaa za ulaya
 4.  Wazungu kujali juu ya usawa wa watu wote
 5. Udhaifu wa watumwa kutoka Afrika.
Choose Answer :


24. Makundi makuu ya mawakala wa ukoloni waliokuja Tanganyika na Zanzibar yalikuwa:

 1. askari, wamisionari na watendaji
 2. wamisionari, waandishi wa habari na wafanyabiashara
 3. wapelelezi, watendaji na wafanyabiashara
 4. waandishi wa habari, wapelelezi na Askiari
 5. wapelelezi, wamisionari na wafanya biashara
Choose Answer :


25. Mkataba wa 1890 uliogawanya Afrika Mashiriki kwa Wajerumani na Waingereli.ulijulikana kama:

 1.  Mkataba wa Hamerton 
 2.  Mkataba wa Haligoland
 3.  Mkataba wa Moresby 
 4.  Mkataba wa Afrika Mashariki
 5.  Mkataba wa Frere
Choose Answer :


26. Makoloni ya Kifaransa Afrika yalikuwa pamoja na:

 1.  Togo na Morocco 
 2.  Senegal na Ghana
 3.  Nigeria na Tunisia 
 4.  Senegal na Morocco
 5.  Angola na Tunisia
Choose Answer :


27. Kiongozi wa Banyoro aliyewaongoza wafuasi wake kuwapiga Waingereza Uganda alikuwa 

 1.  Kabaka Mwanga 
 2.  Kabarega 
 3.  Lobengula
 4.  Lewanika 
 5.  Samora Toure
Choose Answer :


28. Azimio la Arusha lilisisitiza kwamba maendeleo ya nchi lazima yajengwe juu ya :

 1.  Utegemezi wa misaada 
 2.  Biashara ya kimataifa
 3.  Ujamaa na kujitegemea 
 4.  Chama kimoja cha demokrasia
 5.  Ubinafsishaji na uwekezaji.
Choose Answer :


29. Tanzania ilipitisha mfumo wa vyama vingi kwa mara ya pili mwaka:

 1.  1995 
 2.  1992 
 3.  1963 
 4.  1985 
 5.  1965
Choose Answer :


30. Nini faida ya mfumo wa chama kimoja?

 1. unawafanya baadhi ya viongozi wa Kiafrika kuwa madikteta.
 2. unawawezesha wananchi kuwa na uhuru wa kuzungumza.
 3. unaruhusu watu wengi kushiriki shughuli za kisiasa.
 4. unapunguza migogoro inayotokana na tofauti za kimtazamo.
 5. inawawezesha watu kukosoa serikali yao wakati wowote.
Choose Answer :


31.Ipi siyo sahihi kuhusu sifa za elimu ya Tanzania kabla ya Uhuru?

 1. Ilitolewa kwa watu wote.
 2. Iliwatenga watoto wa kike.
 3. Iliangalia matabaka.
 4. llikuwa ya nadhalia zaidi kuliko vitendo.
 5. Ilitolewa kwa kuzingatia dini.
Choose Answer :


32. Kurudishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania kulipendekezwa na :

 1.  Tume ya Kisanga 
 2.  Tume ya Nyalali
 3.  Tume ya Makweta 
 4.  Tume ya Karume
 5.  Tume ya Warioba
Choose Answer :


SEHEMU B

JIOGRAFIA

Magua jibu sahihi na uzungushie herufi katika karatasi yako ya kujibia.

33. Mazingira ni:

 1. Viumbe hai na visivyo hai
 2. Viumbe hai, nyumba na maji
 3. Vitu vyote vinavyomzunguka binadamu
 4. Ardhi, Majengo na bahari
 5. Mimea, wanyama wa kufugwa na nyumba
Choose Answer :


34. Matumizi sahihi ya mistari ya gridi kwenye ramani ni

 1. kuonesha mahali katika ramani
 2. kuonesha uelekeo wa Mashariki
 3. kuonesha umbali
 4. kupata muda
 5. kuonesha mwelekeo wa Kaskazini.
Choose Answer :


35. Chanzo kikuu cha mnishati katika fumo wa jua ni:

 1.  Dunia 
 2.  Sayari 
 3.  jua 
 4.  Mwezi 
 5.  Nyota
Choose Answer :


36. Vifuatavyo ni vyanzo vya maji isipokuwa:

 1.  visima 
 2.  chemichemi 
 3.  mita 
 4.  mabomba ya maji 
 5. . maziwa
Choose Answer :


37. Uchafuzi wa hewa katika maeneo ya makazi unaweza kuthibitiwa kwa: 

 1.  matumizi ya vyoo 
 2.  kuchoma takataka
 3.  kumwaga maji taka mitaani 
 4. kuchemsha maji ya kunywa
 5.  kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki
Choose Answer :


38. Pitio ni sehemu ya ardhi inayoonyesha:

 1.  eneo lenye bonde la ufa 
 2.  sehemu yenye milima
 3.  vilele vya milima 
 4.  mandhari tambarare
 5.  nafasi kati ya safu za milima miwili
Choose Answer :


39. Tafuta umbali halisi katika kilometa kati ya sehemu A" na "S" ikiwa umbali wa ramani ni sentimeta 15 na skeli ya ramani ni 1:100,000

 1.  50km 
 2.  0.15km 
 3.  100,000 km
 4.  7.5km 
 5.  15km
Choose Answer :


40. Mikoa inayolima zao la ndizi Tanzania ni:

 1. Kagera, Kilimanjaro na Mbeya
 2. Mbeya, Kagera na Lindi
 3. Kagera, Singida na Shinyanga
 4. Arusha, Morogoro na Shinyanga
 5. Singida, Lindi na Kagera
Choose Answer :


41. Wastani wa mvua wa milimita 500 kwa mwaka, joto kali kutoka 28° - 39° waka:mchana na hali ya baridi kali wakati wa usiku ni tabia za:

 1.  Hali ya hewa ya kitropiki
 2.  Hall ya hewa ya Jangwa
 3.  Nusu jangwa 
 4.  Hall ya hewa ya Ikweta
 5. Hali ya hewa ya Mediteraniani
Choose Answer :


42. Soma picha ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali namba 42 na 43.

Shughuli kuu za kiuchumi zinazoweza kufanyika katika eneo hili ni:

 1.  kilimo 
 2.  ufugaji 
 3.  uvuvi
 4.  utalii 
 5.  viwanda
Choose Answer :


43. Faida mojawapo ya wanyama wanaoonekana kwenye picha hii ni:

 1. kuongezeka kwa idadi ya wanyama
 2. uhifadhi wa mazingira
 3. kuongezeka kwa pato la taifa
 4. kuongezeka kwa misitu
 5. kuongezeka kwa mvua
Choose Answer :


44. Lipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na binadamu

 1. Vita
 2. Ukame
 3. Milipuko ya volkano
 4. Tetemeko la ardhi
 5. Kimbunga
Choose Answer :


45. Katani, chaff na kahawa ni: 

 1.  mazao ya chakula
 2. mazao ya biashara  
 3.  mimea ya jamii ya kunde 
 4. mazao ya msimu
 5.  mazao ya kuuza nje 
Choose Answer :


46. Ranchi ni eno lililotengwa kwa:

 1.  kilimo cha mazao
 2.  machinjio ya ngombe 
 3.  ufugaji wa ngombe
 4.  josho la ngombe
 5.  kuotesha majani
Choose Answer :


47. Katika Afrika ufugaji wa kondoo hufanyika zaidi:

 1.  Namibia 
 2.  Tanzania 
 3.  Afrika Kusini
 4.  Lesotho 
 5.  Botswana
Choose Answer :


48. Uvuvi usio endelevu hufanyika kwa kutumia:

 1. Mitego
 2. Meli kubwa
 3. Nyavu mraba ndogo
 4. Ugwe
 5. Nyavu mraba kubwa
Choose Answer :


49. Ni madini yapi yanayopatikana Tanzania pekee?

 1.  Dhahabu 
 2.  Urani
 3.  Almasi
 4. Tanzanaiti 
 5.  Makaa ya mawe
Choose Answer :


50. Kuhama kwa watu na bidhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine inaitwa: 

 1. Usafirishaji 
 2.  Utalii 
 3.  Biashara
 4.  Mawasiliano 
 5.  Uhamiaji.
Choose Answer :


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)
GO TO NECTA EXAMS