2016 - MAARIFA YA JAMII
SEHEMU A
Chagua jibu herufiyake kwenye karatariya
1. Katibu kata anachaguliwa na:
- Wanachama wa chama tawala
- Mkutano mkuu wa kata
- Wananchi wa kata ile
- Mkutano wa kijiji wa mwaka
- Kamati ya kijiji
Chagua Jibu
2. Kamati ya maendeleo ya kata inaundwa na wafuatao isipokuwa:
- Katibu kata
- Afisa mtendaji wa Kata
- Katibu Kata wa viti maalumu
- Afisa mtendaji wa Mkoa
- Kamanda wa Polisi wa Mkoa
Chagua Jibu
3. Mwakilishi wa Rais katika ngazi ya mkoa ni:
- Katibu tawala wa Mkoa
- Mkurugenzi mtendaji wa manispaa
- Mkuu wa Mkoa
- Afisa mtendaji wa Mkoa
- kamanda wa Polisi wa mkoa
Chagua Jibu
4. Kauli mbiu ya Tanzania iliyopo kwenye nembo ya taifa ni:
- uhuru na maendeleo
- uhuru na kazi
- uhuru na umoja
- uhuru na amani
- umoja na amani
Chagua Jibu
5. Wimbo wa taifa una beti ngapi?
- Tatu
- Mbili
- Nne
- Tano
- Sita
Chagua Jibu
6. Mambo yote ambayo watu wote wanastahili bila ya kujali kabila, utaifa au jinsia ya huitwa:
- utawala bora
- haki za binadamu
- utawala wa sheria
- demokrasia
- usawa wa kijinsia
Chagua Jibu
7. Ushiriki wa wanafunzi kwenye kuchagua viongozi wao shuleni huimarisha:
- uongozi wa kikatiba shuleni
- kiongozi mkuu wa uongozi wa shule
- ukiritimba shuleni
- usalama shuleni
- uongozi bora shuleni
Chagua Jibu
8. Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora ilianzishwa Tanzania mwaka:
- 2005
- 1995
- 1992
- 2001
- 1977
Chagua Jibu
9. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ni:
- Kamanda wa Polisi wa Mkoa
- Katibu Tawala wa mkoa
- Afisa Usalama wa Mkoa
- Afisa Upelelezi wa makosa ya jinai wa Mkoa
- Mkuu wa Mkoa
Chagua Jibu
10. Umuhimu wa kivuko cha pundamilia ni:
- kupunguza msongamano wa magari barabarani
- kuwezesha walemavu kuvuka barabara kwa usalama
- kuwezesha watembea kwa miguu kuvuka barabara kwa usalama
- kutoa ishara ya kuwepo kwa mifugo karibu na barabara
- kuashiria uwepo wa reli karibu na barabara
Chagua Jibu
11. Uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania ni:
- kilimo
- ujasiriamali
- biashara
- utandawazi
- madini
Chagua Jibu
12. Ujumla wa taratibu za maisha ya kila siku ya mwanadamu huitwa:
- mila
- desturi
- sanaa
- utamaduni
- kazi za mikono
Chagua Jibu
13. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huchaguliwa na:
- wananchi
- wabunge
- mawaziri
- madiwani
- Jaji Mkuu
Chagua Jibu
14. Wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni:
- Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China
- Marekani, Uingereza, Ujerumani, Urusi na China
- Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na Italia
- Marekani, Uingereza, Urusi, Kanada na Ujerumani
- Marekani, Uingereza, Urusi, Japani na Ujerumani
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chagua jibu herufi yake kwenye karatariya
15. Chimbuko la familia ni:
- babu na bibi
- baba na mama
- shangazi na mjomba
- watoto na wazazi
- kaka na dada
Chagua Jibu
16. Kiongozi mkuu wa shule ni:
- mwalimu mkuu msaidizi
- mwalimu wa taaluma
- kiranja mkuu
- mwalimu mkuu
- mwalimu wa nidhamu
Chagua Jibu
17. Nini faida ya mgawanyo wa kazi katika familia?
- Hudhoofisha familia
- Huchochea utengano
- Huleta udikteta
- Huleta maendeleo
- Huleta mitafaruku
Chagua Jibu
18. Moto uligunduliwa katika:
- Zama za Mawe za Kale
- Zama za Mawe za Kati
- Zama za Chuma
- Zama za Mawe za Mwisho
- Zama za Viwanda
Chagua Jibu
19. Uchoraji wa wanyama katika mapango ulianza kufanywa na binadamu katika:
- Zama za Chuma
- Zama za Mawe za Kati
- Zama za Mawe za Kale
- Zama za Mawe za Mwisho
- Zama za Mavve za Mwanzo
Chagua Jibu
20. Mabaki ya Zinjanthropus yaliyopatikana katika bonde la Olduvai mwaka 1959 yaligunduliwa na:
- David Livingstone
- Fredrick Lugard
- Louis Leakey
- Carl Peters
- Charles Darwin
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |