2015 - MAARFA
SEHEMU A
URAIA
Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.
1. Mwenyekiti wa kikao cha maendeleo katika kata ni .
- Diwani wa kata
- Afisa Huduma za ugani
- Afisa Maendeleo wa kata
- Mratibu Elimu wa kata
- Afisa Mtendaji wa kata
Chagua Jibu
2. Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa kwa pamoja zipo chiniya .
- Bunge la Tanzania
- Serikali ya Mtaa
- Serikali Kuu
- Wabunge wa kuchaguliwa
- Chama Tawala
Chagua Jibu
3. Jukumu la kutunga sheria ndogondogo katika Halmashauri ya Wilaya ni la
- Mkuu wa Wilaya
- Afisa Sheria na Usalama wa Wilaya
- Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
- Baraza la Madiwani
- Wabunge wa Wilaya husika
Chagua Jibu
3. Jukumu la kutunga sheria ndogondogo katika Halmashauri ya Wilaya ni la
- Mkuu wa Wilaya
- Afisa Sheria na Usalama wa Wilaya
- Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
- Baraza la Madiwani
- Wabunge wa Wilaya husika
Chagua Jibu
5. Katika Nembo ya Taifa alama inayowakilisha maliasili ya taifa ni
- mlima Kilimanjaro
- mkuki
- karafuu
- pembe za ndovu
- mawimbi ya bahari
Chagua Jibu
6. Ni muhimu kwa wapiga kura wenye sifa kushiriki katika uchaguzi wa Rais na Wabunge kwa sababu
- ni njia ya amani ya kubadili uongozi wa nchi
- ni njia pekee ya kuimarisha utandawazi
- ni kanuni ya kuimarisha mshikamano
- ni kanuni ya mfumo wa vyama vingi
- ni njia pekee ya kuleta mabadiliko ya Katiba ya nchi
Chagua Jibu
7. Kuzingatia sheria, haki za bianadamu, ukweli na uwazi, na uhuru wa vyombo vya habari ni misingi ya
- Urasimu
- Utawala wa sheria
- Ujamaa wa kiafrika
- Demokrasia ya Uwakilishi
- utawala bora
Chagua Jibu
8. Ipi kati ya orodha zifuatazo inawakilisha makundi ya kutetea haki za wanawake ?
- UWT, TAWLA na TAMWA.
- TAMWA, TGNP na TAWALA.
- MEWATA, TGNP na TAWLA
- UWT, TGNP na TAMWA.
- MEWATA, TGNP na UWT.
Chagua Jibu
9. Jukumu la kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao lipo mikononi mwa
- Jeshi la Wananchi la Tanzania
- Idara ya Usalama wa Taifa
- Jeshi la Magereza
- Jeshi Ia Mgambo
- Jeshi la Polisi
Chagua Jibu
10. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa mwaka
- 1961
- 1962
- 1964
- 1963
- 1965
Chagua Jibu
11. Ni muhimu kwa Tanzania kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa sababu ni lugha
- inayozungumzwa na watu wengi Afrika Mashariki
- ya mawasiliano katika Umoja wa Mataifa.
- ya kufundishia shuleni.
- inayowaunganisha Watanzania
- ya mawasiliano katika Bunge la Tanzania.
Chagua Jibu
12. Zipo aina tatu za mipango ya uchumi ambayo ni mipango ya ...
- miaka kumi, kumi na tano na ishirini na tano
- Taifa, Mkoa na Wilaya
- kilimo, biashara na viwanda
- muda mrefu, dharura na muda mfupi
- muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu
Chagua Jibu
13. Moja ya athari mbaya ya utandawazi kwa Tanzania ni ...
- kuongezeka kwa idadi ya wageni nchini
- kumomonyoka kwa maadili katika jamii
- kuongezeka kwa uhasama baina ya vyama vya siasa
- kuongezeka kwa uhuru wa vyombo vya habari
- ongezeko la matumizi ya teknolojia ya habari
Chagua Jibu
14. Utawala wa sheria maana yake ni ...
- wananchi kujichukulia sheria mkononi
- polisi kuadhibu wanaovunja sheria
- sheria kuchukua mkondo wake
- mahakama kukamata wanaovunja sheria
- mamlaka ya mahakama kutunga sheria
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chaguajibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatariya kujibia.
15. Familia hujumuisha
- marafiki, watoto na ndugu
- baba, mama na watoto
- majirani, ndugu na watoto
- majirani watoto na marafiki
- baba, mama na majirani
Chagua Jibu
16. Mahitaji ya lazima ya familia ni pamoja na ...
- chakula, malazi na magari
- chakula, mavazi na televisheni
- mavazi, malazi na chakula
- chakula, malazi na televisheni
- mavazi, chakula na magari
Chagua Jibu
17. Binadamu wa kale alianza ufugaji katika zama za
- kati za mawe
- mwisho za mawe
- mwanzo za mawe
- chuma
- shaba
Chagua Jibu
18. Michoro ya mapangoni iliyoko Kondoa Irangi inasadikiwa kuchorwa wakati wa zama za
- mwanzo za mawe
- Kati za mawe
- Mwisho za mawe
- Chuma
- Ugunduzi wa moto
Chagua Jibu
19. Mkataba wa kufunga soko la watumwa la Zanzibar ulisainiwa mwaka
- 1822
- 1845
- 1885
- 1884
- 1873
Chagua Jibu
20. Moja ya faida ya uhusiano wa kibiashara kati ya Tanganyika na jamii nyingine ilikuwa
- kukua kwa miji ya pwani ya Afrika Mashariki kama Kilwa na Lagos
- kukua kwa dola za Afrika Mashariki kama vile Buganda na Songhai
- kupatikana kwa bidhaa zilizokuwa hazizalishwi nchini
- kuingizwa kwa silaha Tanganyika
- kukomeshwa kwa biashara ya utumwa
Chagua Jibu
21. Nani alikuwa Gavana wa kwanza wa Kijerumani katika Tanganyika?
- Julius Von Soden
- Albert Von Rechenberg
- Herman Von Wissman
- Friedrich Von Schele
- Carl Peters
Chagua Jibu
22. Mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma katika Afrika alikuwa ...
- Horace Byatt
- Friedrick Lugard
- Richard Turnbull
- Donald Cameroon
- Edward Twinning
Chagua Jibu
23. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885 uliitishwa na ..
- Carl Peters
- Johann Krapf
- Henry Stanley
- David Livingstone
- Otto Von Bismarck.
Chagua Jibu
24. Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka
- 1964
- 1961
- 1962
- 1977
- 1963
Chagua Jibu
25. Azimio la Arusha lililenga:
- kuboresha maisha ya matajiri vijijini
- kutaifisha mali za wazungu na kuzigawa kwa maskini
- kupunguza tofauti ya kipato miongoni mwa raia
- kukomesha ubaguzi wa rangi nchini
- kudumisha amani katika nchi jirani
Chagua Jibu
26. Ipi kati ya nchi zifuatazo ilipata uhuru kwa njia ya Vita?
- Zimbabwe.
- Tanganyika
- Ghana.
- Malawi.
- Zambia.
Chagua Jibu
27. Lengo mojawapo la kuanzishwa kwa UNO lilikuwa....
- kuunganisha nchi zinazoendelea
- kuleta umoja wa Waafrika
- kupinga ukoloni mambo leo
- Kudumisha amani
- kutengeneza silaha bora.
Chagua Jibu
28. Mji wa Katanga ulikuwa maarufu kwa utoaji wa ....
- dhahabu.
- shaba.
- ulanga.
- almasi.
- petroli.
Chagua Jibu
29. Kabla ya utawala wa Waingereza, Zanzibar ilikuwa ikitawaliwa na
- Kansela
- Gavana
- Malkia
- Sultani
- Mtemi
Chagua Jibu
30. Kampuni ya biashara ya Kijerumani ilishindwa kuitawala Tanganyika kutokana na
- kuja kwa Wareno
- upinzani kutoka kwa Waafrika
- miundombinu bora iliyokuwepo
- mikataba ya ulaghai
- kuondoka kwa Waingereza.