2014 - MAARIFA YA JAMII
SEHEMU A
URAIA
Chagua jibu lililo sahihi kisha andika herufi yake mkabala na namba ya swali kwenye karatasi ya kujibia.
1. Kazi ya kamati ya shule ni:
- Kusimamia maendeleo ya taaluma
- Kutoa ushauri juu ya maambukizi ya UKIMWI
- Kuidhinisha uteuzi wa waalimu
- Kusimamia nidhamu ya waalimu
- Kusimamia ujenzi na maendeleo ya shule.
Chagua Jibu
2. Vyanzo vya mapato ya serikali za mitaani pamoja na:
- kodi ya kichwa na kodi ya rasilimali
- ruzuku, kodi na michango mingine
- kodi ya ardhi, na kodi ya rasilimali
- tozo katika mazao ya mali asili
- tozo za leseni za biashara
Chagua Jibu
3. Katika muundo wa kiutawala wa serikali za mitaa, wilaya na manispaa zinaongozwa na:
- Chama tawala
- Mkurugenzi mtendaji
- Mkuu wa wilaya
- Kamati yenyewe
- Afisa utawala wa wilaya
Chagua Jibu
4. Rangi nyeusi katika bendera yetu huwakilisha:
- Mimea
- Madini
- Watu
- Ardhi
- Mbuga za wanyama
Chagua Jibu
5. Ngaoya taifa inawakilisha:
- umoja, uhuru, uwezo na mamlaka ya taifa
- uhuru, umoja na rasilimali za taifa
- uwezo, uhuru, uoto wa asili na mamlaka ya taifa
- uhuru, umoja na mamlaka ya taifa
- uhuru na umoja
Chagua Jibu
6. Sababu kubwa ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania ni:
- kutekeleza matakwa ya wahisani
- kulinda haki za makundi maalumu katika jamii
- kuvutia wawekezaji wa nje
- kutekeleza maelekezo ya Umoja wa Mataifa
- kupanua demokrasia
Chagua Jibu
7. Chombo chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania ni:
- Jeshi la polisi
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi
- Mahakama Kuu
- Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
- Ofisi ya Waziri Mkuu
Chagua Jibu
8. Haki ya kumiliki mali iko katika kipengele kipi cha haki za binadamu?
- Kijamii na kiuchumi
- Kisiasa na kiuchumi
- Kikatiba na kisiasa
- Kijamii na Kisiasa
- Kijamii na Kiutamaduni
Chagua Jibu
9. Ulinzi na usalama wa taifa letu ni jukumu la:
- Jeshi Wananchi wa Tanzania
- kitengo cha Usalama wa Taifa
- Jeshi la Polisi
- mgambo
- kila mwananchi
Chagua Jibu
10.Mojawapo ya kazi za mgamboni:
- kukamata wahalifu na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi
- kuadhibu wanaovunja sheria mijini
- kuzuia ajali za moto
- kukusanya kodi ya maendeleo mijini
- kuzuia na kupambana na rushwa
Chagua Jibu
11. Utandawazi ni mfumo unao hamasisha:
- teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi zinazoendelea
- haki sawa kwa kila mmoja duniani
- mfumo wa vyama vingi katika nchi zinazoendelea
- biashara huria baina ya mataifa
- sekta binafsi katika nchi zinazoendelea .
Chagua Jibu
12.Nini maana ya ujasiriamali?
- Bishara yoyote yenye faida
- Uwekezaji kwenye biashara
- Biashara ndogondogo
- Sekta binafsi
- Ujasiri wa kumiliki mali
Chagua Jibu
13.Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni:
- kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi
- Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa
- baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu
- kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu
- kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama
Chagua Jibu
14.Jaji Mkuu waTanzania huteuliwa na:
- Bunge
- Waziri Mkuu
- Rais
- Makamu wa rais
- Mwanasheria Mkuu
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
15. Wafanyabiashara kutoka bara la Asia walifika Tanganyika kwa mara ya kwanza mnamo
- Karne ya 15
- Karne ya 19
- Karne ya 8
- Karne ya 9
- Karne ya 12
Chagua Jibu
16. Kabla ya ukoloni majukumu ya kiongozi wa ukoo yalikuwa ni pamoja na:
- kutatua migogoro
- kusaini mikataba na wakoloni
- kuongeza idadi ya mifugo
- kujenga nyumba
- kuanzisha vijiji vya ujamaa
Chagua Jibu
17. Mkutano wa kuligawa bara la Afrika ulifanyika:
- Berlin
- London
- Roma
- Paris
- New York
Chagua Jibu
18. Azimio la Arusha lililenga zaidi:
- uhuru na kazi
- siasa na kilimo
- elimu kwa wo?e
- ujamaa na kujitegemea
- mfumo wa vyama vingi
Chagua Jibu
19. Katika zama za mawe za mwisho ugawanyaji majukumu katika jamii ulifanyika kwa misingi ya:
- hekima na utajiri
- hekima na umri
- uzoefu na hekima
- umri na jinsia
- utajiri na umri
Chagua Jibu
20.Mwanadamu alianza kutembea kwa miguu miwili katika hatua gani ya mabadiliko?
- Primate
- Homo sapiens
- Homo habilis
- Zinjanthropus
- Homo erectus
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |