2013 -MAARIFA YA JAMII
SEHEMU A
URAIA
1. Majukumu ya kiongozi wa wanafunzi katika shule ni pamoja na:
- kusimamia maendeleo ya taaluma katika shule
- kuandaa ripoti za maendeleo ya wanafunzi
- kuwa kiungo kati ya wanafunzi na walimu
- kusimamia nidhamu ya walimu
- kuadhibu wanafunzi wanaovunja sheria za shule
Chagua Jibu
2. Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hufanyika kila baada ya miaka:
- minne
- miwili
- mitano
- mitatu
- sita
Chagua Jibu
3. Lengo kuu Ia kuanzisha Serikali za Mitaa Tanzania ni
- kuimarisha demokrasia
- kukusanya kodi ya maendeleo
- kuimarisha polisi jamii
- kuboresha usafi wa miji
- kuongeza ajira
Chagua Jibu
4. Bendera ya Taifa ina rangi ngapi?
- Nne.
- Tatu.
- Tano.
- Sita.
- Mbili
Chagua Jibu
5. Ni chombo kipi chenye mamlaka ya kusimamia utoaji wa sarafu na noti hapa Tanzania?
- Wizara ya Fedha.
- Benki ya Dunia.
- Benki Kuu ya Tanzania.
- Benki ya Rasilimali ya Tanzania.
- Wizara ya Mambo ya N dani.
Chagua Jibu
6. Jukumu mojawapo Ia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni:
- kukosoa chama tawala
- kuchagua Wabunge
- kusajili vyama vya siasa
- kuteua Spika
- kusimamia kuhesabu kura
Chagua Jibu
7. Mfumo wa utawala unaotumika Tanzania ni wa:
- Kimila.
- Kidemokrasia
- Kibeberu.
- Kimapinduzi
- Kifashisti.
Chagua Jibu
8. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa lini?
- 2000
- 1992
- 1996
- 1977
- 2005
Chagua Jibu
9. Faida ya ushirikiano kati ya shule na jumuiya inayozunguka shule ni pamoja na:
- ulinzi na usalama wa shule kuimarika
- ongezeko Ia idadi ya watoto wanaoandikishwa shule
- nafasi za ajira kwa jamii inayozunguka shule kuongezeka
- shughuli za biashara kuzunguka eneo Ia shule kuongezeka
- walimu wengi kupata nyumba za kupanga jirani na shule
Chagua Jibu
10. Ni hatua zipi wanafunzi wanatakiwa kuchukua wanapoona katika eneo la shule wageni wanaowatilia shaka?
- Kutoa taarifa kwa jeshi la Wananchi la Tanzania.
- Kutaarifu Kamati ya Shule kuhusu uwepo wa wageni.
- Kuwapiga wageni kabla ya kuwafikisha Mahakamani.
- Kuwakamata wageni na kuwahoji.
- Kutaarifu Walimu kuhusu uwepo wa wageni.
Chagua Jibu
11. Uchumi wa soko huria, ushindani wa kidemokrasia katika siasa na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano ni viashiria vya
- ujasiriamali
- utawala bora
- utawala wa sheria
- utandawazi
- haki za binadamu
Chagua Jibu
12. Ni aina gani ya madini yaligunduliwa kwa wingi nchini Tanzania mwaka 2007?
- Dhahabu
- Uraniamu
- Almasi
- Shaba
- Chuma.
Chagua Jibu
13. Makubaliano ya kuanzisha Umoja wa Mataifa yalifanyika
- New York
- San Francisco
- C. San Diego
- Washington
- Los Angeles
Chagua Jibu
14. Chombo kinachohusika na kuhakikisha kuwa raia anapata haki yake anayostahili ni:
- Polisi
- Magereza
- Mahakama
- Jeshi la Wananchi
- Bunge
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
15. Jukumu la ulinzi katika familia ni la nani?
- Baba na watoto.
- Baba, jamaa na marafiki.
- Watoto, mama na jirani
- Kila mtu katika familia
- Watoto, jamaa na marafiki
Chagua Jibu
16. Waziri Mkuu wa Dola ya Buganda aliitwa:
- Kabaka
- Katikiro
- Mukama
- Lukiko
- Bakungu
Chagua Jibu
17. Moja ya mbinu iliyotumika kudhoofisha teknolojia ya Waafrika wakati wa ukolono ni
- kufundisha masomo ya sayansi.
- kuanzisha viwanda vya kisasa katika Afrika.
- kubinafsisha viwanda vya Afrika.
- kuleta bidhaa za viwandani kutoka ulaya.
- kufundisha Waafrika teknolojia ya Ulaya.
Chagua Jibu
18. Moja ya malengo ya elimu ya kikoloni ilikuwa:
- kupambana na ujinga na umaskini
- kupunguza uzalishaji wa mazao ya biashara
- kupata watumishi wa ngazi za chini
- kuongeza ajira kwa vijana
- kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi
Chagua Jibu
19. Gavana aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria nchini Tanganyika aliitwa
- Donald Cameron
- Richard Turnbull
- Horrace Byatt
- Edward Twinning
- John Scott
Chagua Jibu
20. Chama cha TANU kilianzishwa nchini Tanganyika ili
- kuboresha maisha ya Watanganyika
- kuongeza kipato cha wafanyakazi
- kupigania uhuru wa Tanganyika
- kutetea mas?ahi ya walowezi
- kutetea haki za wakulima
Chagua Jibu
21. Mpelelezi wa kikoloni aliyeweka mikataba ya ulaghai na Chifu Mangungo wa Msovero aliitwa
- De Brazza
- Carl Peters
- Dr. Livingstone
- Mungo Park
- Henry Stanley
Chagua Jibu
22. Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea:
- 12 Februari 1964
- 12 Desemba 1964
- 26 Januari 1964
- 12 Januari 1964
- 26 Aprili 1964
Chagua Jibu
23.Makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) yapo:
- New York
- San Francisco
- San Diego
- Washington
- Los Angeles
Chagua Jibu
24. M?oto wa shangazi yako ni:
- mjomba
- kaka
- binamu
- dada
- mpwa
Chagua Jibu
25. Rais wa kwanza wa nchi ya Msumbiji alikuwa:
- Edwardo do Santos
- Samora Machel
- Edward Mondlane
- Joachim Chissano
- Grace Machel
Chagua Jibu
26. Wafanyabiashara wa mwanzo kutoka Ulaya walifika Tanganyika katika karne ya ngapi?
- Karne ya 15
- Karne ya 8
- Karne ya 19
- karne ya 18
- Karne ya 9
Chagua Jibu
27. Mfumo wa ukabaila katika jamii ya Waha uliitwa:
- Umwinyi
- Ntemi
- Ubugabire
- Nyarubanja
- Mvunjo
Chagua Jibu
28. Wanadamu walianza kujihusisha na biashara katika zama za:
- Mwanzo za Mawe
- Mwisho za Mawe
- Mapinduzi ya viwanda
- Kati za Mawe
- Chuma
Chagua Jibu
29. Mfumo wa uzalishaji mali ambao msingi wake mkubwa ulikuwa ardhi uliitwa:
- Ujamaa
- Ujima
- Ubepari
- Ubeberu
- Uka
Chagua Jibu
30. Yupi kati ya wafuatao ni msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku shuleni?
- Mwalimu wa nidhamu.
- Mwalimu wa zamu.
- Mwalimu Mkuu.
- Mwenyekiti wa kamati ya shule.
- Kiranja mkuu.
Chagua Jibu
31. Jamii ya watu wa Zambia iliyofanya biashara na Wayao iliitwa
- Wakamba
- Wasumbwa
- Waluo
- Wanyamwezi
- Walunda
Chagua Jibu
32. Mojawapo ya athari ya utawala wa Wareno katika Afrika Mashariki ilikuwa:
- kuanzishwa kwa uislamu
- kukomeshwa kwa biashara ya utumwa
- kuharibiwa kwa miji ya pwani
- kusaini mikataba ya ulaghai
- kuanzisha mashamba ya katani
Chagua Jibu
SECTION C
JOGRAFIA
33. Kipi kati ya vifuatavyo ni chanzo kikuu cha maji?
- Mito
- Maziwa
- Mabwawa
- Visima
- Mvua
Chagua Jibu
34. Chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira barani Afrika ni
- ongezeko la watu
- silaha za nyuklia
- kilimo cha mazao ya chakula
- kilimo cha mazao ya biashara
- kilimo cha matuta kwenye miinuko
Chagua Jibu
35. Miji ya Dar es Salaam na Tanga ina joto kuliko miji ya Arusha na fringa kwa sababu joto:
- hupungua kwa wastani wa 0.6 0 C unapopanda meta 100
- huongezeka kwa wastani wa 0.60 C unapopanda meta 100
- hupungua kwa wastani wa 0.60 C unapopanda meta 1000
- huongezeka kwa wastani wa 0.6 0 C unapopanda meta 1000
- hupungua kwa wastani wa 6,5 0 C unapopanda meta 100
Chagua Jibu
36. Nchi kubwa kuliko zote barani Afrika ni
- Afrika ya Kusini
- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Nigeria
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Algeria
Chagua Jibu
37. TPC Moshi, Kagera, Mtibwa na Kilombero ni mfano wa viwanda vinavyozalisha:
- Saruji
- Sukari
- Sigara
- Mabati
- Kahawa
Chagua Jibu
38. Kipimo kidogo cha ramani hutumika kuchorea
- maeneo madogo
- maeneo makubwa
- maeneo ya kati tu
- maeneo madogo na ya kati
- maeneo madogo na makubwa
Chagua Jibu
39. Mstari wa Tarehe wa Kimataifa HAUKO mnyoofu kwa sababu ya :
- kuepuka majanga yanayoweza kutokea duniani.
- kuepuka nchi moja kuwa na nyakati tofauti.
- kuzuia tsunami na matetemeko ya ardhi.
- kupunguza milipuko ya volcano.
- kufanya ncha za dunia kuwa karibu.
Chagua Jibu
40. Miamba Iaini inayopatikâfia katika pwani ya Afrika Mashariki inaitwa
- Matumbawe
- Geu
- Jiwe moto
- Mfinyanzi
- Makaa ya mawe
Chagua Jibu
41. Tabia ya nchi ya nusu jangwa na ukame wa kitropiki hupatikana sehemu zipi za Afrika Mashariki?
- Kaskazini mwa Uganda
- Kaskazini Mashariki mwa Kenya na sehemu ya kati ya Tanzania.
- Kusini Mashariki mwa Tanzania.
- Magharibi mwa Kenya
- Kusini mwa Tanzania na Kusini Mashariki mwa Kenya
Chagua Jibu
42. Nchi za Kusini mvva Afrika ni pamoja na:
- Angola, Afrika Kusini na Namibia
- Afrika Kusini, Burundi na Malawi
- Malawi, Msumbiji na Rwanda
- Zimbabwe, Botswana na Tanzania
- Swaziland, Lesotho na Nigeria
Chagua Jibu
43. Ni mikoa ipi nchini Tanzania imeonesha dalili za kuenea kwa jangwa?
- Shinyanga, Tabora na Mwanza
- Kilimanjaro, Iringa na Mbeya
- Lindi, Morogoro na Tabora
- Shinyanga, Dodoma na Singida
- Arusha, Ruvuma na Manyara
Chagua Jibu
44. Kundi lipi linaonesha sayari?
- Zebaki, Mwezi na Zuhura
- Dunia, Nyota na Mihiri
- Zebaki, Serateni na Zohari
- Zuhura, Dunia na Kimondo
- Utaridi, Jua na Mwezi
Chagua Jibu
Soma kwa makini ramani ifuatayo kishajiba maswaliyafuatayo 45, 46 and 47
45. Mlima maarufu unaopatikana katika eneo lenye herufi C huitwa:
- Kilimanjaro
- Rungwe
- Meru
- Usambara
- Uluguru
Chagua Jibu
46. Mto uliooneshwa kwa herufi E unaitwa:
- Tana
- Galana
- Naili
- Malagarasi
- Ruaha
Chagua Jibu
47. Nchi inayooneshwa kwa herufi B ni maarufu kwa uzalishaji wa madini yanayoitwa:
- Dhahabu
- Tanzanaiti
- Makaa ya Mawe
- Almasi
- Shaba
Chagua Jibu
48. Ongezeko Ia joto duniani, ukame, mafuriko na vimbunga ni matokeo ya athari zitokanazona
- uharibifu wa mazingira
- tsunami iliyotoka Asia
- ongezeko kubwa Ia watu katika nchi za Ulaya
- matumizi ya mabomu ya nyuklia
- Mvua nyingi
Chagua Jibu
49. Ni maziwa yapi yanapatikana katika Bonde la Ufa la upande wa Mashariki?
- Turkana, Rukwa na Kyoga.
- Nyasa, Victoria na Eyasi.
- Turkana, Natroni na Eyasi
- Victoria, Eyasi na Kyoga.
- Albert, Edward na Kivu
Chagua Jibu
50. Chunguza RAMANI kisha jibu swali linalofuata
Mchoro huu unaonesha mpangilio wa makazi wa aina gani?
- Mkusanyiko
- Mtawanyiko
- Kimstari
- Yasiyo na mpangilio
- Kiasili
Chagua Jibu
Try Another Test |