MAARIFA YA JAMII 2012
SEHEMU A
URAIA
Chaguajibu sahihi kisha andika katika karatasiyakoya kujibia.
1. Mwakilishi wa wananchi katika vikao vya Wilaya vya Serikali za Mitaa ni ....
- Mkuu wa Wilaya.
- Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji.
- Afisa Mtendaji Kata.
- Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama Tawala.
- Diwani wa Kata.
Chagua Jibu
2. Mojawapo ya majukumu ya Halmashauri ya Wilaya ni kutoa ruzuku kwa .....
- Serikali za Kata.
- Serikali Kuu.
- Vyama vya siasa.
- Serikali za Vijiji.
- Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Chagua Jibu
3. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya au Manispaa huteuliwa na .....
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Baraza la Madiwani la Halmashuri au Manispaa husika.
- Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
- Katibu Mkuu Kiongozi.
Chagua Jibu
4. Katika Bendera ya Taifa rangi ya kijani kibichi inawakilisha ...
- madini
- maji
- uoto wa asili
- kilimo
- ardhi
Chagua Jibu
5. Ni wakati gani Bendera ya Taifa hupeperushwa nusu mlingoti?
- Wakati wa ziara za viongozi wa mataifa mengine.
- Rais anapotangaza hali ya hatari.
- Linapotokea janga la kitaifa au tukio la huzuni.
- Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa.
- Rais anapokuwa nje ya nchi.
Chagua Jibu
6. Uchaguzi wa Rais na Wabunge hapa Tanzania hufanyika kila baada ya
- miaka 10
- miaka 3
- miaka 4
- miaka 5
- miaka 6.
Chagua Jibu
7. Haki za binadamu zinapaswa kutolewa kwa watu wote bila kujali .
- vyama vya siasa.
- katiba ya nchi.
- haki za makundi maalumu.
- umri wa mtu.
- rangi, dini, jinsi na kabila.
Chagua Jibu
8. Kazi mojawapo ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni .........
- kupokea na kuhakiki taarifa ya rasilimali na madeni ya viongozi wa umma
- kusuluhisha migogoro baina ya viongozi wa umma
- kufanya utafiti na kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu na utawala bora
- kuchunguza tuhuma zozote dhidi ya Afisa wa serikali anayehusishwa na rushwa
- kuthibitisha uteuzi wa mawaziri.
Chagua Jibu
9. Ni chombo gani chenye jukumu la kulinda nchi yetu na mipaka yake?
- Jeshi la Polisi Tanzania.
- Jeshi la Magereza la Tanzania.
- Jeshi la Kujenga Taifa.
- Jeshi la Wananchi la Tanzani.
- Jeshi la Mgambo.
Chagua Jibu
10. Lengo kuu la Polisi jamii ni .........
- kufundisha raia kazi za Polisi.
- kujenga mahusiano ya kirafiki baina ya Polisi na raia.
- kuwezesha Maafisa wa Polisi kuishi na raia.
- kuwafanya raia kuwa wakakamavu kama polisi.
- kuzuia matumizi ya dawa za kulevya katika jamii.
Chagua Jibu
11. Mila zinazoathiri afya ya uzazi wa kinamama ni pamoja na .........
- mahari na uzazi wa mpango.
- ukeketaji wanawake na uzazi wa mpango.
- ndoa za utotoni na mahari.
- ukeketaji wanawake na ndoa za utotoni.
- kunyonyesha watoto kwa muda mrefu.
Chagua Jibu
12. Mojawapo ya changamoto wanazozipata wajasiriamali ni pamoja na .......
- ukosefu wa leseni za biashara.
- kutokuwepo kwa benki na taasisi za fedha.
- upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma.
- uwepo wa askari polisi na mgambo wengi maeneo ya mijini.
- kutokuwepo sera ya uwekezaji.
Chagua Jibu
13. Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
- Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa.
- Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
- Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
- Mahakama Kuu ya Kimataifa.
Chagua Jibu
14. Mtumishi wa umma ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa nafasi yake katika utumishi wa umma ni ....
- Jaji Mkuu
- Katibu Mkuu Kiongozi
- Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
- Msajili wa vyama vya siasa.
- Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chagua jibu sahihi uliandike katika karatasi yakoya kujibia.
15. Mabaki ya Zinjanthropus yaligunduliwa .........
- Kondoa Irangi.
- Kalenga.
- Olduvai.
- Isimila.
- Engaruka.
Chagua Jibu
16. Wafanyabiashara wa mwanzo wa kigeni kuja Tanganyika walitoka .........
- Amerika.
- Amerika Kaskazini.
- Asia
- Ulaya.
- Amerika Kusini.
Chagua Jibu
17. Mojawapo ya athari ya utawala wa Waingereza katika visiwa vya Unguja ilikuwa ....
- kukomesha biashara ya utumwa.
- kuanzishwa kwa dini ya kikristu.
- kuondoa umaskini.
- kuanzisha kilimo cha karafuu.
- kuanzisha vyama vya siasa.
Chagua Jibu
18. Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi vya siasa katika Tanzania ulifanyika mwaka
- 1992
- 1990
- 1961
- 2005
- 1995.
Chagua Jibu
19. Elimu kwa wote (UPE) nchini Tanzania ilianzishwa mwaka ...
- 1974
- 1970
- 1972
- 1980
- 1977
Chagua Jibu
20. Nchi ya Afrika iliyokuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1980 ni .....
- Zimbabwe.
- Tanzania.
- Botswana.
- Ghana.
- Ethiopia.
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |