MAARIFA YA JAMII 2010
URAIA, JOGRAFIA NA HISTORIA
SEHEMU A
Chagu jibe hullo sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya kilo swali katika karatasi ya kujibia uhyopewa.
1. Ukoo ni muungano wa:
- familia zinazokaa karibu
- familia nyingi zenye asili moja
- familia nyingi zilizo rafiki
- baba, mama na watoto.
- familia zilizoungana kufanya kazi pamoja.
Chagua Jibu
2. Utamaduni maana yake ni
- imani, desturi, mila na miiko ya jamii ya watu
- kuimba na kucheza kwa pamoja
- namna ya kufanya matambiko katika jamii
- desturi na mila za jamii Fulani
- utaratibu wa kuishi
Chagua Jibu
3. Kiongozi wa serikali ngazi ya kata ni
- Diwani
- Afisa mtendaji wa kata
- Mwenyekiti wa kata
- Katibu kata
- Afisa mifugo wa kata
Chagua Jibu
4. Ili Afrika ijitegemee kiuchumi inahitaji
- misaada toka nje
- Ongezeko kubwa la watu
- sayansi na teknolojia
- mikopo ya masharti nafuu
- wawekezaji wa kiafrika.
Chagua Jibu
5. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Madola lilikuwa
- kupata makoloni zaidi barani Afrika
- kuimarisha uhusiano baina ya Uingereza na nchi ilizozitawala
- kuoongeza kiasi cha malighafi zilizokuwa zinahitajiwa na wazungu.
- kuwaachia watumwa ambao bado walikuwa hawajawa huru
- kumfanya malkia wa Uingereza aogopwe na ulimwengu mzima.
Chagua Jibu
6. Mahakama inayotoa hukumu ya kesi za mauaji ni
- Mahakama ya mwanzo
- Mahakama ya wilaya
- Mahakama kuu
- Mahakama ya hakimu mkazi
- Mahakama ya Rufaa
Chagua Jibu
7. Nchi zinazopakana na Tanzania upande wa kusini ni
- Msumbiji na Malawi
- Msumbiji na Zimbabwe
- Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na Malawi
- Burundi na Malawi
- Rwanda na Malawi
Chagua Jibu
8. Nini tofauti kati ya nyota na sayari?
- Nyota humweka wakati sayari hazimweki
- Nyota zinatoa mwanga mweupe, wakati sayari hutoa mwanga wa rangi ya njano.
- Sayari huonekana mchana lakini nyota huonekana usiku tu.
- Nyota hazina mwanga wakati sayari zina mwanga
- Sayari zote zina viumbe hai wakati nyota hazina viumbe hai
Chagua Jibu
9. Bonde la ufa limegawanyika sehemu ya Mashariki na Magharibi katika nchi gani?
- Kenya
- Uganda
- Tanzania
- Burundi
- Ethiopia
Chagua Jibu
10. Vifuatavyo vilikuwa ni vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika isipokuwa
- ANC
- PAC
- SWAPO
- KANU
- UNITA
Chagua Jibu
11. Mkusanyiko wa shughuli zinazohusisha wafanyabiashara na walaji au watumiaji huitwa
- Soko
- duka
- Bidhaa
- mteja
- fedha
Chagua Jibu
12. Bara la pili kwa ukubwa ulimwenguni ni
- Asia
- Afrika
- Australia
- Amerika ya Kaskazini
- Amerika ya kusini
Chagua Jibu
13. Rais wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika lililoanzishwa Machi 2004 ni
- Dr. Salim Salim
- Dr. Emek Anyauko
- Mh. Getrude Mongela
- William Erek
- Peter Omu
Chagua Jibu
14. Mtanzania anaruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu anapofikia umri wa miaka
- 15
- 25
- 40
- 21
- 18
Chagua Jibu
15. Hapo awali mabara yote yalikuwa yameshikana na kuwa bara moja lililojulikana kama
- Andes
- Pangaea
- Australia
- Eurasia
- Antaktika
Chagua Jibu
16. Tabaka la ozone huweza kuharibiwa na
- kuongezeka kwa gesi ya oksijeni
- Kuongezeka kwa gesi ya haidrojeni kwenye anga
- moshi wenye kemikali unaotoka viwandani na kwenye magari
- kupungua kwa gesi ya kaboni daioksaidi kwenye anga
- vumbi linalosambaa angani kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini
Chagua Jibu
17. Rhoda anachemsha maji ya kunywa kila siku kwa sababu maji yaliyochemshwa
- ni safi na salama
- yana ladha nzuri
- hukata kiu haraka
- huua wadudu walioko katika matumbo yetu
- huwa na virutubisho vingi
Chagua Jibu
18. Lengo mojawapo la michezo shuleni ni
- kutumia viwanja vya shule vizuri
- kuleta umoja na ushirikiano
- kuwapa zawadi washiriki
- kutambua shule zisizo na viwanja vya michezo
- kupata wachezaji wa kulipwa
Chagua Jibu
19. Serikali za mitaa zina aina ......za Halmashauri
- moja
- nne
- tano
- tatu
- sita
Chagua Jibu
20. Idadi kubwa ya wakimbizi katika bara la Afrika inasababishwa na
- umaskini katika nchi nyingi za Afrika
- migogoro ya kifamilia
- miundo mbinu duni
- upungufu wa ajira
- machafuko ya kisiasa
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |