MAARIFA YA JAMII 2006
SEHEMU A
URAIA, JIOCRAFIA NA HISTORIA
Chagua jibu lililo sahihi na kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasiyako ya kujibia.
1. Familia yetu inaweza kupata maendeleo mazuri ya kiuchumi ikiwa:
- mama atajishughulisha na kazi za ndani ya nyumba tu
- baba ataachiwa ashughulikie kazi ya ajira tu
- watoto hawatajihusisha na kazi yoyote isipokuwa kwenda shule na tuisheni
- kila ndugu anayeomba msaada atapewa
- kila mwanafamilia atashiriki kikamilifu kutimiza majukumu aliyopangiwa
Chagua Jibu
2. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Bunge ni nani?
- Waziri Mkuu
- Spika wa Bunge
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Jaji Mkuu
- Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Chagua Jibu
3. Madhumuni ya kuundwa kwa serikali za mitaa nchini ni:
- kuongeza nafasi za kazi kwa wasomi
- kuharakisha maendeleo ya wananchi
- kuinua maendeleo ya wanawake
- kupanua biashara ndogondogo
- kuimarisha ukusanyaji wa kodi
Chagua Jibu
4. Latitudo ndogo kuliko zote ni:
- ncha ya Kusini na Kaskazini
- muhimili wa dunia
- Tropiki ya Kansa
- Ikweta
- Grinwichi
Chagua Jibu
5. Ramani iliyokamilika inakuwa na mambo yafuatayo:-
- barabara, miji, dira, uoto na mipaka
- kichwa, ufunguo, kipimio, dira na pambizo
- uoto, barabara, reli, miji na ufunguo
- mazao, pambizo, kipimio, kichwa na dira
- dira, ufunguo, kipimio, mipaka na kichwa
Chagua Jibu
6. Mabwawa makubwa yanayozalisha umeme kwa wingi Tanzania ni:
- Pangani na Kidatu
- Kihansi na Mtera
- Nyumba ya Mungu na Hale
- Mtera na Kidatu
- Kidatu na Nyumba ya Mungu
Chagua Jibu
7. Wapelelezi wa kwanza waliofika Afrika ya Mashariki karne ya 19 walikuwa:
- Burton na Speke
- Rebman na Grant
- Rebman na Krapf
- Krapf na Burton
- Speke na Livingstone
Chagua Jibu
8. Makaburu walivamia ncha ya Kusini mwa Afrika chini ya uongozi wa nani?
- Jan Van Riebelk
- Bartholomew Diaz
- Rebman na Kruger
- Von Letton
- Vasco Da Gama
Chagua Jibu
9. Jamii ya watu waliohamia Afrika ya Mashariki kati ya mwaka 100 na 500 baada ya Kristo kutoka Magharibi ya Afrika walikuwa:
- Wanaoiloti
- Wahabeshi
- Mbilikimo
- Wabantu
- Wakush
Chagua Jibu
10. Sababu kubwa ya kutokea kwa familia za mzazi mmoja ni nini?
- Kutozingatia uzazi wa mpango
- Matatizo ya kiuchumi
- Ukosefu wa ajira
- Kuiga mila za kigeni
- Wazazi kutelekeza watoto
Chagua Jibu
11. Chanzo cha nishati ya nyuklia ni madini ya:
- uraniamu
- platiniamu
- beriliamu
- vanadiamu
- titaniamu
Chagua Jibu
12. Idadi ya watu katika nchi hujulikana kwa njia ya:
- kupiga kura
- kujua idadiya wanawake wenye umri wa kuzaa
- kuhesabu idadi ya vijana
- sensa ya watu
- kusajili wahamiaji na wahamaji
Chagua Jibu
13. Katika muundo wa mahakama, hakimu mkazi ni hakimu katika mahakama . . . . . .
- ya Wilaya
- ya Mwanzo
- ya Mkoa
- Kuu
- ya Rufaa
Chagua Jibu
14. Kazi kubwa zilizokuwa zikifanywa na wazee wa ukoo katika jamii nyingi za Kiafrika zilikuwa . . . . . . . . .
- kulinda mila na desturi, kufanya matambiko na kukata mashauri;
- kupanga mahari, kukata mashauri, na kupigana katika vita;
- kulinda mila na desturi, kutembelea koo zingine na kupigana katika vita;
- kulisha mifugo, kukata mashauri na kufanya tambiko;
- kulima mashamba, kuwinda na kulisha mifugo.
Chagua Jibu
13 Wajibu wa Serikali katika kusimamia biashara ya ndani ni
- kupanga bei za bidhaa mbalimbali
- kukagua bidhaa madukani
- kugawa maeneo ya kufanyia biashara
- kutunga sheria za kusimamia biashara
- kutoa mitaji kwa wafanyabiashara
Chagua Jibu
16. Maana halisi ya familia ni ipi?
- Mama, baba, watoto na jamaa wote katika ukoo
- Mama, baba na watoto
- Mama, baba, watoto na rafiki wa karibu wote
- Baba, mama, watoto, bibi na babu
- Baba, mama, watoto, bibi, babu, shangazi na mjomba
Chagua Jibu
17. Teknolojia ya kale ya umwagiliaji maji mashambani barani Afrika ilihusisha .
- shadoof
- mifereji
- mnyama aina ya punda
- ngamia
- mabomba
Chagua Jibu
18. Soko kuu la biashara ya watumwa Zanzibar lilifungwa mwaka .
- 1840
- 1900
- 1890
- 1884
- 1873
Chagua Jibu
19. Sehemu zenye mvua kidogo sana, joto jingi mchana na baridi sana usiku ni za hali ipi ya nchi?
- Kimediteranean
- Kisavanna
- Jangwa
- Kiikweta
- Kitropiki
Chagua Jibu
20. Uchumi wa nchi ya Libya unategemea zaidi:
- tende
- dhahabu
- almasi
- mafuta
- gesi
Chagua Jibu
BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA
Try Another Test |