STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2005

MAARIFA YA JAMII 2005

URAIA, JIOGRAFIA NA HISTORIA

Chagua jibu sahihi na kisha andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasiyakoya kujibia.

1. Kabla ya ujio wa wageni, jamii za Kiafrika zilitumia njia zifuatazo katika kurithisha maarifa kwa vizazi vilivyofuata:

  1. kusoma, kuandika na kuhesabu
  2. kuchora, kusoma na kuandika
  3. kazi za mikono, nyimbo na hadithi
  4. mashairi, riwaya na sinema
  5. Sanaa, kusoma na kuandika
Chagua Jibu


2. Uhuru, haki na udugu ni misingi ya nini?

  1. Demokrasia
  2. Azimio la Arusha
  3. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  4. Utawala wa sheria
  5. Mfumo wa siasa ya vyama vingi nchini
Chagua Jibu


3. Kiongozi aliyekuwa na wajibu wa kugawa mashamba na kuongoza ufyekaji wa mapori kwa ajili ya kilimo katika jamii ya Wanyamwezi aliitwa

  1. Mtemi 
  2. Rugaruga 
  3. Chifu 
  4. Nyapara 
  5. Nyungu wa mawe
Chagua Jibu


4. Pepo za Harmattan huvuma katika jangwa lipi kati ya haya?

  1. Namibia 
  2. Kalahari 
  3. Uarabuni 
  4. Gobi 
  5. Sahara
Chagua Jibu


5. Uchaguzi wa Madiwani husimamiwa na chombo kipi kati ya hivi vifuatavyo?

  1. ofisi ya Waziri Mkuu 
  2. Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  3. jeshi la polisi 
  4. tume ya Taifa ya Uchaguzi
  5. ofisi ya Rais
Chagua Jibu


6. Ili shughuli za biashara ziweze kuimarika vizuri hapana budi pawe na:

  1. maduka na soko
  2. maji na umeme wa kuaminika
  3. huduma muhimu za jamii 
  4. majengo imara na njia za uchumi
  5. masoko ya kuaminika na njia za uchukuzi
Chagua Jibu


7. Umaarufu wa mji wa Kilwa katika karne ya kumi na tano ulitokana na "Husuni Kubwa" ambayo ilikuwa:

  1. meli ya kifahari 
  2. ikulu ya Su?tani wa Kilwa
  3. soko kuu la watumwa
  4. sanamu ya dhahabu ya Su?tani wa Kilwa
  5. ngome kuu ya Wareno
Chagua Jibu


8. Ikiwa ni saa 4:30 asubuhi katika mji wa Mtwara ulioko nyuzi 30 Mashariki je, itakuwa saa ngapi katika mji wa Kigali ulioko nyuzi 15 Mashariki? 

  1. saa 3:30 asubuhi 
  2. saa 3:30 usiku
  3. saa 5:30 asubuhi
  4. saa 5:30 usiku 
  5. saa 4:30 usiku
Chagua Jibu


9. Michezo ni muhimu kwa vijana kwa sababu:

  1. hujenga ukakamavu wa afya
  2. huwajengea umaarufu miongoni mwa jamii
  3. huwapatia zawadi
  4. huwawezesha kwenda nje ya nchi
  5. huwaepusha na madawa ya kulevya
Chagua Jibu


10. Kitendo cha nchi changa kulazimika kuzingatia matakwa na maslahi ya nchi za kibeberu huitwaje?

  1. ukoloni mkongwe 
  2. ukoloni mamboleo
  3. ubepari
  4. umangimeza 
  5. utandawazi
Chagua Jibu


11. Nchi zinazolima mpunga kwa wingi katika Bara la Asia ni zipi?

  1. Burma, Thailand, India na China
  2. Japani, Iran, Afghanistan na Indonesia
  3. Austraria, China, Israel na Japan
  4. Burma, India, China na Kuwait
  5. Sri Lanka, Malasia, Japan na Burma
Chagua Jibu


12. Madini maarufu yanayochimbwa katika eneo la Uvinza hapa Tanzania ni:

  1. chuma 
  2. dhahabu 
  3. chumvi
  4. makaa ya mawe 
  5. tanzanite
Chagua Jibu


13. Mmoja wa viongozi wa wapigania uhuru aliyeuawa kwa njama za mabeberu ili kudhoofisha harakati za ukombozi wa Afrika ni:

  1. Edward Mondlanae 
  2. Tom Mboya
  3. Abeid Aman Karume 
  4. Jonas Savimbi 
  5. Edward Moringe Sokoine
Chagua Jibu


14. Majaji wa Mahakama wanaweza kutengua sheria iliyotungwa na Bunge iwapo sheria hiyo:

  1. haikuungwa mkono na Rais
  2. haimsaidii mwanachi wa kawaida
  3. haitambuliki kimataifa 
  4. haikubaliki kikatiba 
  5. haina sheria ndogo zake
Chagua Jibu


15. Ni mbinu ipi inaweza kupunguza tatizo la wakimbizi katika Afrika?

  1. kuruhusu kuwepo kwa majeshi ya kigeni
  2. kuwa na serikali imara zilizochaguliwa na wananchi
  3. kuanzisha jumuiya za kiuchumi za kanda
  4. kuondoa vikwazo vya uhamiaji toka nchi moja hadi nyingine 
  5. kuanzisha sera za ubinafsishaji
Chagua Jibu


16. Reli ya TAZARA husafirisha mizigo kwenda na kutoka katika bandari ipi?

  1. Mombasa 
  2. Mwanza 
  3. Dar es Salaam
  4. Tanga 
  5. Kapiri Mposhi
Chagua Jibu


17. Moja ya mambo yafuatayo si kweli kuhusu mambo ambayo mgonjwa wa ukimwi anapaswa kutendewa:

  1. kustaafishwa kazini 
  2. kula pamoja
  3. kucheza naye 
  4. kujadiliana naye kuhusu maendeleo yake
  5. kupewa tiba kwa magonjwa nyemelezi
Chagua Jibu


18. Nchi nyingi za kiafrika zilianza kupata mwamko wa kudai uhuru baada ya

  1. vita kuu ya kwanza ya Dunia 
  2. kuanzishwa chama cha TANU
  3. Ghana kupata Uhuru 
  4. vita kuu ya Pili ya Dunia
  5. kuibuka kwa mataifa ya kijamaa
Chagua Jibu


19. Maziwa yafuatayo yako ndani ya Bonde la Ufa katika Afrika Mashariki

  1. Victoria, Tanganyika na Eyasi 
  2. Turkana, Natron na Magadi
  3. Manyara, Rukwa na Victoria 
  4. Kyoga, Albert na Naivasha
  5. Rukwa, Victoria na Magadi
Chagua Jibu


20. Bunge la Jamhuri ya Muungano lina sehemu kuu mbili ambazo ni

  1. Rais na Wabunge 
  2. Waziri Mkuu na Wabunge
  3. Spika na Wabunge 
  4. Wabunge wa CCM na wa Upinzani
  5. Mawaziri na Wabunge
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256