STD VII HISABATI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2022

JAMHURI VA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 

04 HISABATI 

Muda: Saa 2:00 Mwaka : 2022 

1. Maelekezo Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45)

2. Jibu maswali yote. 

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR). 

4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR. 

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo: 

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hiclto kwa umakini kwa kutumia kifutio sail kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya. 

8. Tumia penseli ya HR to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi 45. 

9. Onesha wazi njia iliyotumika katika kujibu swali Ia 41 hadi 45 katika nafasi iliyotolewa kwenyc fomu ya OMR. 

10. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani. 

SEHEMU A: MATENDO YA KIHISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO 

Katika swali la 1 — 40, kokotoa swill ulilopewa na kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa. 

1. Thamani ya nafasi ya tarakimu iliyopigiwa mstari katika namba 504251 ni

  1. Makumi
  2. Maelfu 
  3. Mamia elfu 
  4. Mamia 
  5. Makumi elfu
Chagua Jibu


2. Jedwali lifuatato linaonesha mauzo ya lita za petroli katika siku tano za wiki. Je, ni siku ipi lita nyingi zaidi za mafuta ziliuzwa? 

  1. Jumatatu 
  2. Jumanne 
  3. Jumatano 
  4. Alhamisi 
  5. Ijumaa 
Chagua Jibu


3. Ipi kati ya sehemu 13/14, 15/14, 12/13, 16/17 , na 19/20 ni sehemu guni? 

  1. 13/14
  2. 15/14
  3. 12/13
  4. 16/17
  5. 19/20
Chagua Jibu


4. Ufaulu wa mwanafunzi iwa Darasa la Saba katika masomo matano ulikuwa kama ifuatavyo: somo la Hisabati alipata 14/25 Kiswahili alipata 5/8, English Language alipata 1/2 Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi alipata 3/5 na Uraia na Maadili alipata 31/50 . Ni somo lipi alipata alama ndogo kuliko zote? 

  1. Hisabati 
  2. Kiswahili 
  3. English Language 
  4. Maarifa ya Jamii na Stadi za kazi 
  5. Uraia na Maadili 
Chagua Jibu


5. Mtungi wa gesi una ujazo wa lita 10. Iwapo lita 1.5 zimetumika, ni sehemu gani ya ujazo imebakia? 

  1. 17/2
  2. 21/20
  3. 17/20
  4. 3/2
  5. 3/20
Chagua Jibu


6. Upendo alimpa 0.1 ya kilogramu za sukari dada yake na ? shangazi yake. Ikiwa alibakiwa na kilogram 35, zipi kati ya zifuatazo ni jumla ya kilogramu za sukari alizokuwa nazo awali? 

  1. kg 500 
  2. kg 50 
  3. kg 35.3 
  4. kg 38 
  5. kg 45 
Chagua Jibu


7. Shule ya Msingi Mwenge ina jumla ya wanafunzi 560, ambapo kati yao ? ni wanachama wa skauti. Ikiwa ? ya wanachama wa skauti watilipa ada ya shule, ni asilimia ngapi ya wanafunzi hawakulipa ada? 

  1. 60%
  2. 25%
  3. 37.5%
  4. 62.5%
  5. 40% 
Chagua Jibu


8. Mpeliialipewa kazi ya kupanga namba nzima zote zilizopo kati ya 2 na 55 ambazo ni vigawe vya 9. Upi ni mpangilio sahihi wa namba hizo ikiwa alianza na namba ndogo? 

  1. 27, 35, 49, 54 
  2. 27, 42, 51, 54 
  3. 27, 45, 51, 54 
  4. 27, 36, 45, 54 
  5. 27, 32, 45, 54 
Chagua Jibu


9. Mkulima alipanda michungwa kwenye mistari sita kwa mpangilio uluatao: 90, 81, 72,. . . .  , . . . . . . 45. Michungwa iliyopandwa kwcnyc mstari wa nne na wa tano haikuota. .lc, ni idadi ipi inawakilisha jumla ya michungwa ambayo haikuota? 

  1. 141 
  2. 147 
  3. 93 
  4. 87 
  5. 117 
Chagua Jibu


10.  Maria alimwomba kaka yake amsaidie kupanga namba XC, IV, LV, CI na VI kuanzia kubwa kwenda ndogo. Upi ni mpangilio sahihi? 

  1. CI, XC, LV, VI, IV 
  2. XC, CI, LV, IV, VI 
  3. CI, XC, VI, IV, LV 
  4. XC, LV,C1,1V,.V1 
  5. CI, XC, LV, IV, VI 
Chagua Jibu


11. Wanafunzi watano walipewa kazi ya kuorodhesha vigawe vya 6 vilivyopo kati ya 30 na 60. Je, ipi ni orodha sahihi? 

  1. 36, 48, 54, 56 
  2. 36,48,54,60 
  3. 36, 42, 54, 60 
  4. 36,42,48,54 
  5. 36, 40, 42, 48 
Chagua Jibu


12. Wanafunzi watano waliorodhesha vigawe vitatu vya shirika vya namba 4 na 6 vilivyopo kati ya 10 na 40. Ipi ni sahihi kati ya orodha zi fuatazo? 

  1. 16, 24, 36 
  2. 12, 24, 36 
  3. 12, 18, 36 
  4. 16, 28, 36 
  5. 12. 30, 36 
Chagua Jibu


13. Dotto ana jumla ya sh 1,260,000. Iwapo ? ya fedha za Dotto ni sawa na ½ ya fedha za Kulwa, je, kati yao wawili mwenyc kiasi kikubwa cha fedha kuliko mwenzake ana shilingi ngapi? 

  1. sh 800,000 
  2. sh 600,000 
  3. sh 400,000 
  4. sh 1,600,000 
  5. sh 1,200,000 
Chagua Jibu


14. Katika mojawapo ya hifadhi za Taifa kuna jumla ya wanyama 2,400,000. lkiwa 0.3 ya wanyama wote ni Simba, 0.4 ni Swab, 0.2 ni Twiga na 0.1 ni Tembo, je, kuna tofauti ya wanyama wangapi kati ya kundi lenye wanyama wengi na kundi lenye wanyama wachache? 

  1. 720,000 
  2. 240,000 
  3. 1,200,000 
  4. 480,000 
  5. 960,000 
Chagua Jibu


15. Zuhura ana uzito wa kilogramu 70.5 na Hamis ana uzito wa kilogramu 68.15. Je, jumla ya uzito wao ni kiasi gani? 

  1. 2.35 kg 
  2. 148.65 kg 
  3. 138.65 kg 
  4. 1.35 kg 
  5. 138.2 kg 
Chagua Jibu


16.  Jafari alipewa machungwa 789,951 na miezi wake. Pia, alipata machungwa mengine 226,783 kutoka kwa rafiki yake. Je, jafari alipata jumla ya machungwa mangapi? 

  1. 563,232 
  2. 1,016,734 
  3. 563,168 
  4. 1,016,634 
  5. 916,734 
Chagua Jibu


17.  Jumla ya magari 834,223 yaliingizwa nchini mwaka 2020 kutoka Japani na nchi nyingine. Ikiwa magari 436,756 yalitoka Japan, je, magari mangapi yalitoka nchi nyingine? 

  1. 1,270,979 
  2. 1,260,979 
  3. 397,467 
  4. 4,085,757 
  5. 402,533 
Chagua Jibu


18.  Shamba la ng'ombe wa maziwa huzalisha lita 254,567 za maziwa kwa siku. Ni kiasi gani  cha maziwa kitazalishwa kwa siku 43? 

  1. Lita 10,947,381 
  2. Lita 10,846,381
  3. Lita 254,524 
  4. Lita 254,610 
  5. Lita 10,946,381 
Chagua Jibu


19. Tatu alikuwa na shilingi 5,500 alizopata katika biashara yake. Ikiwa alitumia ? ya fedha hizo kununua matunda alibakiwa na kiasi gani cha fedha? 

  1. sh 2,200 
  2. sh 7,700 
  3. sh 3,300 
  4. sh 1,100 
  5. sh 4,400 
Chagua Jibu


20.  Sharifa alikuwa na shilingi 47,200 kwenye akaunti yake. Ikiwa alinunua suruali 3 za watoto wake kwa bei ya shilingi 12,900 kila moja, je, alibakiwa na kiasi gani cha fedha? 

  1. sh 38,700 
  2. sh 12,900 
  3. sh 34,300 
  4. sh 8,500 
  5. sh 60,100 
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256