STD VII HISABATI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2021

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

04 HISABATI

Muda: Saa 2:00 Mwaka : 2021

Maelekezo

l. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4.Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali Ia 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali Ia 1 hadi 40 na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi 45.

9. Onesha wazi njia iliyotumika katika kujibu swali Ia 41 hadi 45 katika nafasi iliyotolewa kwenye fomu ya OMR.

10. Simu za mkononi, vikokotozi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: MATENDO YA KIHISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO

Katika swali la 1 — 40, kokotoa swali ulilopewa na kisha weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

l . Wanafunzi watano walipewa kazi ya kuandika namba ubaoni, kila mtoto namba moja. Ipi kati ya zifuatazo ni namba ndogo kati ya namba zilizoandikwa na wanafunzi hao?

  1. 0.457
  2. ?
  3. 40%
  4. 0.53 
  5. 0.80
Chagua Jibu


2. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya wanafunzi wa Darasa la Saba kwa Kirumi na vinywaji wanavyopenda zaidi:

Vinywaji Fanta
Pepsi Chai Maji Maziwa
Idadi Ya Wanafunzi XCI XC CIX CVI CX

Ni kinywaji kipi kinapendwa na wanafunzi wengi zaidi?

  1. Fanta 
  2. Pepsi 
  3. Chai 
  4. Maji 
  5. Maziwa
Chagua Jibu


3. Nafasi ya thamani ya tarakimu iliyopigiwa mstari katika numerali 504251 ni

  1. makumi
  2. maelfu
  3. makumi elfu
  4. mamia
  5. mamia elfu
Chagua Jibu


4. Mtungi uliojaa gesi una ujazo wa lita 10. Iwapo lita 1.5 zimetumika, ni sehemu gani ya gesi imebaki?

  1. 3/20
  2. 20/23
  3. 17/20
  4. 3/23
  5. 3/17
Chagua Jibu


5. Katika shule ya msingi ya Uhuru wanafunzi 60 wa Darasa la Nne walihudhuria darasani wakati wa kujisomea. Ikiwa wanafunzi 20 hawakuhudhuria, je, asilimia ngapi ya wanafunzi wote hawakuhudhuria darasani?

  1. 33.3% 
  2. 80% 
  3. 25%
  4. 75% 
  5. 66.7%
Chagua Jibu


6. Kijiji kimoja kilikuwa na jumla ya mifugo 3,845 ,308. Ipi ni jumla ya mifugo hiyo katika makumi elfu yaliyo karibu?

  1. 3,854,310
  2. 3,845,300
  3. 3,846,000
  4. 3,850,000
  5. 3,845,000
Chagua Jibu


7. Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961. Iwapo Mwanakwetu alikuwa na miaka miwili kwa wakati huo, je, mwaka 2020 alikuwa na umri gani? (Toa jibu katika namba za Kirumi).

  1. LIX 
  2. LXI 
  3. XLI
  4. ILX 
  5. XIL
Chagua Jibu


8. Maneno alipewa namba 21, 29, 37, 45, 49, 51, 53, 57, 59 na 61 ili abaini namba tasa. Ikiwa aliandika namba tasa kwa usahihi, je, aliandika namba zipi kati ya zifuatazo? 

  1. 21, 45, 51 na 57 
  2. 29, 37, 51, 59 na 61
  3. 29, 37, 53, 59 na 61 
  4. 29, 49 na 59
  5. 21, 51 na 61
Chagua Jibu


9. Umri wa watoto wanne ulipangwa katika mfululizo wa miaka 13, 18, 23 na  . . . . . Je, mtoto wa nne ana umri gani?

  1. 28 
  2. 24 
  3. 22
  4. 12 
  5. 41
Chagua Jibu


10. Makusanyo ya mapato kwa miaka mitano mfululizo yaliorodheshwa kwa namba 2, 4, 7, 12 na 19 Ni namba ipi ya mapato ya mwaka wa Sita katika mfululizo huo?

  1. 18 
  2. 28
  3. 20
  4. 31
  5. 30
Chagua Jibu


I l . Mpangilio ufuatao unawakilisha uzito wa wanafunzi waliosimama kwenye mstari kulingana na uzito wao:

59, 55, 51, ___, 43, 39, 35.

Upi ni uzito wa mwanafunzi uliotakiwa kuandikwa kwenye nafasi iliyoachwa wazi?

  1. 52
  2. 47
  3. 44
  4. 42 
  5. 50
Chagua Jibu


12. Mahudhurio ya wanafunzi wa Darasa la Kwanza katika Shule ya Msingi Mtakuja yalipungua kwa siku tano mfululizo kutokana na sababu mbalimbali kama ifuatavyo; 78, 75, 72, 69, Je, wanafunzi wangapi walihudhuria siku ya tano?

  1. 70 
  2. 68
  3. 66
  4. 79
  5. 77
Chagua Jibu


13. Wanakijiji cha Mshikamano walichanga shilingi 325 ,500 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule. Kama kila mwanakijiji alichanga shilingi 500, je, wanakijiji wangapi walichanga?

  1. 6,051
  2. 6,501
  3. 32,600
  4. 651
  5. 325,000
Chagua Jibu


14. Tanganyika ilipata uhuru mwaka MCMLXI na Zimbabwe ilipata uhuru wake mwaka MCMLXXX. Je, miaka mingapi ilipita tangu Tanganyika ipate uhuru mpaka Zimbabwe ilipopata uhuru?

  1. XXI 
  2. XIX
  3. XXIX
  4. IX
  5. XVIIII
Chagua Jibu


15. Mwalimu aliwagawa wanafunzi katika makundi matano na kuwapa kazi ya kutafuta jumla ya namba katika abakasi mbili kama inavyoonekana katika mchoro ufuatao:

Je, lipi ni jibu sahihi kati ya yafuatayo?

  1. 280,281
  2. 280,271
  3. 270,231
  4. 270,271
  5. 280,291
Chagua Jibu


16. John alipata faida ya sh 600,000 baada ya kuuza kuku na mayai. Faida ya kuku mmoja ilikuwa sh 1,500 na faida ya trei moja ya mayai ilikuwa sh 1,000. Je, John aliuza trei ngapi za mayai ikiwa aliuza kuku 300?

  1. 400 
  2. 450 
  3. 300
  4. 150
  5. 100
Chagua Jibu


17. Ashura ana maembe 43 na Asha ana maembe 17. Asha anahitaji maembe mangapi kutoka kwa Ashura ili wote wawe na idadi sawa ya maembe?

  1. 26
  2. 13
  3. 60
  4. 30
  5. 43
Chagua Jibu


18. Jeri ana wafanyakazi 208 katika kiwanda chake. Ikiwa kila mfanyakazi hulipwa shilingi 55,460 kila siku, je, Jeri hutumia kiasi gani cha fedha kuwalipa wafanyakazi wake kwa siku moja?

  1. sh. 11,435,680
  2. sh. 10,435,680
  3. sh. 55,252
  4. sh. 55,668
  5. sh. 11,535,680
Chagua Jibu


19. Watoto watano walitakiwa kutafuta tofauti kati ya kura 998,999 na kura 819,937. Je, ipi ni tofauti ya kura hizo kati ya zifuatazo?

  1. 1,818,936
  2. 181,062
  3. 179,062
  4. 189,062
  5. 1,708,936
Chagua Jibu


20. Darasa la Saba katika shule ya msingi Maendeleo lina wanafunzi 480. Iwapo 7/12 ya wanafunzi hao ni wasichana, je, ipi ni tofauti kati ya idadi ya wasichana na wavulana?

  1. 280
  2. 760
  3. 40
  4. 80
  5. 200
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256