STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2023
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHAINII LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
01KISWAHILI
Muda: Saa 1:40Mwaka: 2023
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
Jibu maswali yote.
Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
Andika Namba yako ya Mtihani kisha weka kivuli kwenye tarakimu za namba hiyo mahali panapohusika kwenye karatasi yako ya kujibia.
Weka kivuli kwenye herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali 1 — 40. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 — 40; na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41 hadi 45.
Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.
SEHEMU A (Alama 35)
Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la 1 - 5, kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia.
Maswali
1. Nini kilisababisha kifo cha wazazi wake Baraka?
Uhaba wa hospitali kijijini
Ajali ya ndege
Maisha ya anasa ya wazazi wake D Ajali ya gari
Maisha duni ya wazazi wake
Chagua Jibu
2. Nani alimlea Baraka baada ya kufiwa na wazazi wake?
Wanakijui
Bibi yake mzaa mama
Bibi yake mzaa baba
Walimu wake
Mganga Mkuu wa Zahanati
Chagua Jibu
3. Baraka alipataje fedha za kuMpeleka bibi yake hospitali?
Aliomba kwa wanakijiji
Alifanya kibarua cha kufyatua matofali
Alipewa na walimu wake
Alipata kutoka vya jirani
Alipewa na mganga mkuu
Chagua Jibu
4. Baraka alisoma kozi gani baada ya kuhitimu masomo ya sekondari?
Uashi
Urubani
Uuguzi
Udereva
Udaktari
Chagua Jibu
5. Kwa nini wanalajui walimuona Baraka ni lulu kwao?
Alifaulu vizuri mitihani yake
Alikuwa msaada mkubwa sana
Aliwapa pesa nyingi
Alifyatua matofali na kuwapatia
Alifanya biashara na kuwanufaisha
Chagua Jibu
Katika swali la 6 - 35, weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika fomu yako ya kujibia
6. "Jino langu linang'aa." Wingi wa sentensi hii ni upi kati ya sentensi zifuatazo?
Meno zangu yanang'aa.
Meno yangu linang'aa.
Meno yangu yanang'aa.
Majino yangu yanang'aa.
Jino zangu zinang'aa.
Chagua Jibu
7. "Manamba angalimsikiliza baba yake ____________mguu." Neno lipi kati ya yafuatayo linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?
asingeliumia
angaliumia
asingaliumia
asingeumia
angeliumia
Chagua Jibu
8. Makuli walisikika wakisema, "kidole kimoja hakivunji chawa." Je, ni methali ipi kati ya zifuatazo inafanana na methali hiyo?
Mchonga mwiko huukimbiza mkono wake.
Chanda chema huvishwa pete.
Kidole chako kibaya kitakufaa siku mbaya.
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
Kidole chako kibaya usikikate.
Chagua Jibu
9. "Tunashauriwa kuwalea watoto katika maadili mema." Methali ipi kati ya zifuatazo inaendana na kauli hiyo?
Ugambi ni wa wenye ndumba.
Udongo uwahi ungali maji.
Tone na tone hujaza ndoo.
Tone na'tone huwa mchirizi.
Ubishi mwingi huvuta matendo.
Chagua Jibu
10. Kisongo alipoumia Kajiru alimpeleka hospitali kwa matibabu. Methali ipi kati ya zifuatazo ingefaa kutumiwa na Kisongo kwa jambo alilotendewa na Kajiru?
Asiyekubali kushindwa si mshindani.
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli.
Shukurani ya punda ni mateke.
Hakuna marefu yasiyo na ncha. -
Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
Chagua Jibu
11. Wao walikuwa hawana furaha. Neno "wao" lipo katika nafsi ipi kati ya hizi zifuatazo?
Nafsi ya tatu wingi
Nafsi ya pili wingi
Nafsi ya tatu umoja
Nafsi ya kwanza wingi
Nafsi ya pili umoja
Chagua Jibu
12. "Alivyoendelea kukanusha__________hasira zilivyozidi kumpanda yule askari." Neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?
Ndipo
Ndiko
Ndivyo
Ndio
Ndiyo
Chagua Jibu
13.Nikitoka bustanini nitawapikia watoto chakula. Neno "nitawapikia" lipo katika kauli gani?
Kutendwa
Kutendeana
Kutendea
Kutendana
Kutendewa
Chagua Jibu
14. Mwalimu wa somo la Kiswahili alipigwa butwaa baada ya kuambiwa mwanafunzi wa Darasa la Saba ameacha shule. Nahau "pigwa butwaa" ina maana gani?
Kukubaliana
Kushangaa
Kufurahi
Kuchukizwa
Kukataa
Chagua Jibu
15. Juhudi za Suli kufanya kazi serikalini ziligonga mwamba baada ya kukosa cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi. Nahau "gonga mwamba" katika sentensi hii ina maana gani?
Kufika mwisho kabisa
Kupasua mwamba mgumu
Kufika kikomo
Kufanya jambo bila mafanikio
Kupata suluhu ya kazi
Chagua Jibu
16. Tabia ya wanafunzi kuchelewa shuleni imeota mizizi. Nahau "ota mizizi" ina maana gani?
Kufanikiwa kufika shuleni
Kujificha ili wasionekane
Kustawi na kudumu sana
Kupenda kuishi shuleni
Kutodumu kwa muda mrefu
Chagua Jibu
17. Neno jumuishi linaloundwa kutokana na maneno "kuku, njiwa, kunguru na bata" ni lipi?
Wadudu
Ndege
Mboga
Wanyama
Kitoweo
Chagua Jibu
18. Chikoyo alihuzunika sana aliposikia taarifa ya kifo cha Babu yake. Katika neno "aliposikia" kiambishi kipi huwakilisha wakati uliopita?
a-
-po-
-sik-
-ki-
-li-
Chagua Jibu
19. "Mwanafunzi alicheza vizuri." Ukanushi wa sentensi hii ni upi?
Mwanafunzi hakucheza vizuri.
Mwanafunzi hakuchezaga vizuri.
Mwanafunzi hatacheza vizuri.
Mwanafunzi hucheza vizuri.
Mwanafunzi hajacheza vizuri.
Chagua Jibu
20. Maneno haya hayajapangwa katika utaratibu wa kialfabeti: "dada, kisu, andika, cheza, zuhura." Yakipangwa kwa utaratibu wa kialfabeti seti sahihi itakuwa ipi kati ya zifuatazo?