SAYANSI DARASA LA NNE 2016
SEHEMU A
Jibu swali la 1 - 10 kwa kuchagua jibu sahihi na kisha andika herufi yake katika karatasi ya kujibia.
1. Ni hewa ipi inayotumiwa na mimea kusanisi chakula chao wakati wa mchana?
- Kabondayoksaidi
- Oksijeni
- Naitrojeni
- Biogesi
Chagua Jibu
2. Ni ugonjwa upi unaotokana na ukosefu wa madini joto (ayodini) mwilini?
- Surua
- Goita
- UKIMWI
- Matege
Chagua Jibu
3. Ni kundi lipi linalowakilisha vyakula vinavyoupa mwili nguvu na joto......
- Mkate, maziwa na mboga za majani
- Maembe, karoti na mboga za majani
- Mihogo, viazi mviringo na mahindi
- Nyama, mahindi na maharagwe
Chagua Jibu
4. Ni kiungo kipi katika mwili kinachotumika kutambua ladha ya vitu?
- Ngozi
- Mdomo
- Pua
- Ulimi
Chagua Jibu
5. VVU ni kifupi cha . . . . . .
- Virusi Vinavyozaliana
- Virusi Vya Ukimwi
- Via Vya Uzazi
- Viungo Vya UKIMWI
Chagua Jibu
6. Ipi ni kazi ya matamvua katika samaki?
- Kufyonza chakula
- Kuwinda
- Kupumua
- Kutoa uchafu
Chagua Jibu
7. Lipi kati ya makundi yafuatayo ya wanyama huishi majini na nchi kavu?
- Chura na bata
- Samaki na chura
- Mamba na chura
- Kiboko na samaki
Chagua Jibu
8. Makundi yafuatayo ya wanyama hutaga mayai isipokuwa
- wadudu, samaki na ndege
- ndege, mamba na nyoka
- popo, fisi na mbuzi
- samaki, mjusi na kenge
Chagua Jibu
9. Huduma ya kwanza hutolewa .......
- kwenye zahanati
- ajali inapotokea
- kabla ya ajali kutokea
- na wataalamu wa afya
Chagua Jibu
10. Nini kitatokea iwapo miche miwili ya sumaku iliyooneshwa hapo chini itasogezwa ili kukaribiana?
- Itakimbiana
- Itavutana
- Itaharibika
- Itapata kutu
Chagua Jibu
Jibu swali la 11 - 15 kwa kuoanisha maneno yaaliyo katika "Fungu A" na yaliyo katika "Fungu B"
FUNGU A
- Ugonjwa unaosambazwa na mbu jike aina ya Anopheles
- Ugonjwa unaosababisha upotevu wz maji mwilini
- Ugonjwa unaoathiri kibofu cha mkojo
- Ugonjwa unaoambukukizwa ngono zembe.
- Ugonjwa unaosababisha upofu.
FUNGU B
- Minyoo
- B. Trakoma
- Kuharisha/kuhara
- Malaria
- Homa
- Kichocho
- UKIMWI
Fungua Jibu
SEHEMU C
Jibu swali 16 - 22 kwa kujaza jibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi.
16. Maji, mswaki na dawa ya meno ni muhimu kwa kusafisha . . . . . . . .
Fungua Jibu
17. Maji salama kwa kunywa yanapaswa yachemshwe na. . . . . . . .
Fungua Jibu
18. Kitendo cha maji kubadilika kutoka half ya kimiminika na kuwa katika hail ya gesi huitwa. . . . . . . .
Fungua Jibu
19. Chanzo kikuu cha nishati duniani ni. . . . . . . .
Fungua Jibu
20. Virutubisho vinavyoongeza kinga mwilini huitwa ..........
Fungua Jibu
21. Macho, ngozi, ulimi, sikio na pua ni ......
Fungua Jibu
22. Hewa huingia na kutoka katika mmea kwa kupitia. . . . . . . .
Fungua Jibu
SEHEMU D
Andika Ndio au Hapana
23. Sehemu kubwa ya mwili wa binadamu ni maji . . . . . . . .
Fungua Jibu
24. VVU/UKIMWI husambazwa kwa kushirikiana nyembe na mswaki........
Fungua Jibu
25. Mawimbi ya sauti husafiri katika mstari mnyoofu tu. . . . . . . .
Fungua Jibu