SAYANSI DARASA LA IV 2015
SEHEMU A
Jibu swali la 1 -10 kwa kuchagua herufiya jibu sahihi na kuandika katika kiratasi ya kujibia.
1. Ni muhimu kusafisha mazingira iii ........
- kuzuia mmomonyoko wa udongo
- kuruhusu mimea iongezeke
- kulinda afya na hewa safi
- kuleta magonjwa na harufu mbaya
Chagua Jibu
2. Nyama, vyenye samaki na mayai ni vyakula
- wanga
- vitamini
- protini
- madini
Chagua Jibu
3. Sehemu ya mwili inayohusika na kuhisi ni
- ulimi
- ngozi
- macho
- pua
Chagua Jibu
4. Kipimajoto ni kifaa kinachotumika kupima
- ujazo wa maada
- hewa angani
- uzito wa maada
- jotoridi la mwili
Chagua Jibu
5. Viumbe hai vyote hupumua, hula, hukua na
- kucheza
- kuimba
- kufa
- kulia
Chagua Jibu
6. Mwathirika wa VVU/UKIMWI anaweza kuthibitishwa kwa njia ipi?
- Kupima damu yake hospitali ni
- Kumtazama use wake
- Kuangalia tabia yake
- Kupima uzito wake
Chagua Jibu
7. Chuma kikipata joto ......
- . husinyaa
- hutanuka
- huungua
- hupata kutu
Chagua Jibu
8. Sehemu kuu za mmea ni .....
- majani, shina na maua
- shina, matawi na mizizi
- majani, shina na mizizi
- mizizi, shina na maua
Chagua Jibu
9. Kipi kati ya vifuatavyo hutumika kutambua sauti ya kengele?
- Macho
- Ngozi
- Ulimi
- Masikio
Chagua Jibu
10. Kipitisho kizuri cha umeme kati ya vitu vifuatanyo ni:
- Plastiki
- shaba
- mti mkavu
- Binadamu
Chagua Jibu
SEHEMU B
Jibu swali 11 - 15 kwa kuoanisha maneno yallyo katika "Fungu A" na yallyo katika "Fungu B":
FUNGU A
- Gesi itokanayo na taka za wanyama
- Hewa itolewayo wakati wa upumuaji
- Gesi ambayo ni muhimu kwa uhai wa viumbe na moto kuwaka
- Hewa iliyo kwenye mwendo
- Mvuke unaoganda na kusababisha mvua.
FUNGU B
- Hewa
- Upepo
- Mawingu
- Kabonidayoksaidi
- Oksijeni
- Gesi vunde
- Haidrojeni
Fungua Jibu
SEHEMU C
Jaza nafasi iliyoachwa wazi
16. Kifaa kinachotumika kukuza vitu vidogo sana visivyoonekana kwa macho huitwa . . . . .
Fungua Jibu
17. Mchakato wa kugomboa chumvi kwenye husababisha myeyuko wa chumvi huitwa.....
Fungua Jibu
18. Kabohaidreti imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni sukari na . . . . . .
Fungua Jibu
19. Kutapika na kuhara husababisha mwili wa binadamu kupoteza . . . . . . .
Fungua Jibu
20. Vitu vyenye asili ya chuma huweza kuvutwa kwa kutumia . . . . . . . . .
Fungua Jibu
21. VVU vinapoingia kwenye mwili wa binadamu hushambulia . . . . . . . .
Fungua Jibu
22. Gesi inayohitajika na mmea katika utengenezaji wa chakula huitwa .........
Fungua Jibu
SEHEMU D:
Andika Kweli ama Si Kweli
23. "Kifua kikuu huambukizwa kwa kunywa maji yasiyo salama" . . . .
Fungua Jibu
24. "Kutunza mazingira wakati wote husababisha magonjwa mbali mbali . . . . . . .
Fungua Jibu
25. "Huduma ya kwanza hutolewa kutegemea aina ya tatizo" ........
Fungua Jibu