MAARIFA YA JAMII DARASA LA IV 2014
SEHEMU A : HISTORIA
Jibu swali la 1 - 4 kwa kuchagua herufi sahihi na kuandika katika kisanduku
1. Sifa kubwa ya Ukabaila ni ....
- Kumiliki ardhi
- Kugawana ardhi
- Kukusanya kodi
- Kuwa na watumwa
Chagua Jibu
2. jamii za siku hizi hazibadilishani bidhaa kwa bidhaa kwa sababu .......
- hakuna bidhaa za kubadilishana
- watu wamechoka kufanya biashara hiyo
- bidhaa zilizopo ni nzito kuzibeba
- fedha hutumika kununua bidhaa
Chagua Jibu
3. Mojawapo ya mila na desturi za zamani ni
- kuogopa kazi za shambani
- kuwafunza watoto maadili mema
- kuchoma misitu ovyo
- kuchafua nyumba na mazingira
Chagua Jibu
4. Nasaba ni hali ya kuwa na...........
- uhusiano wa karibu sana
- watoto wa karibu sana
- uhusiano baina ya watu katika familia
- urafiki mzuri baina ya watu
Chagua Jibu
Jibu swali la 5 - 7 kwa kuandika neno "Kweli"au "si kwelf:
5. Umasikini wakati wa ujima ulisababishwa na vitendea kazi duni..................
Fungua Jibu
6. Kumwaga takataka za viwandani katika bahari na mito huongeza mazalia ya samaki . . . .
Fungua Jibu
7. Kabila linalodumisha vazi lake la asili ni Wamakonde . . . . .
Fungua Jibu
SEHEMU B : URAIA
Jibu swali la 8 - 9 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuandika katika karatariya kujibia.
8. Katika muundo wa serikali ngazi amhayo raia wote wanaweza kushiriki ni katika mkutano mkuu wa
- Mtaa au kijip
- Mkoa
- Wilaya
- Taifa
Chagua Jibu
9. Taja maeneo ambayo huwekwa nembo ya Taifa
- Shuleni na mahakamani
- Mahakamani na uwanja wa Taifa
- Gari la Rais na kwenye fedha
- Kofia ya polisi na fulana za shule
Chagua Jibu
Chagua jibu sahihi kutoka kwenye mabano na liandike kwenye karatasi ya kujibia
10. Sikukuu ya wafanyakazi ni ..........
(Sikukuu ya kitaifa, sikukuu ya kidini, sikukuu ya kisiasa).
Fungua Jibu
11. Tarehe ambayo Tanzania ilipata uhuru wake ilikuwa . . . . . . .
(12/01/1964, 09/12/1961, 26/04/1964)
Fungua Jibu
12. Wajibu wa mtoto ni ..........
(kucheza, kuwa na tabia njema, kufanya kazi)
Fungua Jibu
13. Mambo yanayoathiri utawala bora ni......
(ushirikishwaji, rushwa, maslahi bora)
Fungua Jibu
14. Jukumu la ulinzi ni la...
(watu wote, watoto peke yao, walezi peke yao
Fungua Jibu
SEHEMU C : JOGRAFIA
Jibu swali la 15 - 18 kwa kujaza jibu sahihi :
15 ..... ni tabaka la gesi linaloikinga dunia dhidi ya mionzi hatati ya jua.
Fungua Jibu
16. Kuna aina kuu ..... za uoto
Fungua Jibu
17. Madini aina ya .. . . . . . hupatikana Mererani mkoani Arusha.
Fungua Jibu
18 . . . . . . . . hupenda kutembelea mbuga wanyama, milima mirefu na makumbusho ya kihistoria
Fungua Jibu
Jibu swali 19 - 23 kwa kuoanisha maneno yaliyo katika "Fungu A" no yaliyo katika "Fungu
FUNGU A
19. Haigrometa
20. Uoto wa asili
21. Ufunguo
22. Majira ya mwaka
23. Ramani