MAARIFA JAMII 2013
SEHEMU A
HISTORIA
Kwa swali la 1-4 chaguajibu sahihi na andika herufi yake kwenye nafasi ya kujibia
1. Kuna aina ngapi za familia? .
- Moja
- Tano
- Sita
- Mbili
Chagua Jibu
2. Dada wa baba yako ni .........
- mpwa
- bibi
- shangaz
- binamu
Chagua Jibu
3. Hatua au zama iliyoonesha maendeleo ya kijamii ya mwanadamu inaitwa .........
- Zama za mawe za kale
- Zama za mawe za kati
- Zama za mawe za mwisho
- Ubepari
Chagua Jibu
4. Mfumo wa kwanza wa uzalishaji mali ambao haukuwa na matabaka ya watu uliitwa .
- Ujima
- ukabaila
- Ujamaa
- Ubepari
Chagua Jibu
Jibu swali la 5 - 7 kwa kuandika Ndiyo au Hapana
5. Sababu mojawapo iliyofanya jamii za Kitanzania hapo kale zibadilishane bidhaa ni kutokuwa na fedha za kununua bidhaa .........
Fungua Jibu
6. Shughuli nyingi za mwanadamu huboresha mazingira .........
Fungua Jibu
7. Uchoraji ni mojawapo ya namna/fani ya kueleza hisia au mawazo .........
Fungua Jibu
SEHEMU B
URAIA
Jibu swali namba 8 hadi 9 kwa kuchagua jibu sahihi na kuandika herufi yake.
8. Mtoto asiyejua namna ya kudai haki zake
- hupata msaada haraka
- hupendwa na watoto wenzake
- husahauliwa na kutojaliwa
- huliwazwa na wengine
Chagua Jibu
9. Hasara mojawapo ya kutowahusisha wanafunzi katika kufanya maamuzi
- matatizo wanafunzi hayatatambuliwa.
- huhamasisha mahusiano
- huchochea upendo na umoja
- huleta vurugu kwenye familia.
Chagua Jibu
Chagua majibu katika kifungu B yanayojibu maswali katika kifungu A.
Kifungu A | Kifungu B |
10. Mwenyekiti wa serikali ya kijiji au mtaa. 11. Wimbo wa taifa. 12. Wizi, ajali za barabarani, moto, umeme, wadudu na wanyama. 13. Kuingia darasani na kusoma ipasavyo. 14. Njia mojawapo ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi | - Vitu vinavyoweza kusababisha mazingira yasiyo salama shuleni.
- Sikukuu za kitaifa.
- Jukumu la wanafunzi shuleni.
- Alama mojawapo ya taifa.
- Huongoza mikutano yote ya kijiji au mtaa.
- Ishara ya uongozi bora
- Kuwa na idadi ndogo ya mifugo.
|
Fungua Jibu
SEHEMU C
JIOGRAFIA
Jibu swali la 15 hadi la 19 kwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi.
15. Kila kitu kinachomzunguka mwanadamu katka maisha yake huitwa ...........
Fungua Jibu
16. Misitu ya asili huzalisha ......... zitumikazo kutengeneza meza na viti.
Fungua Jibu
17. Umbo la kitu Iililochorwa na Iinalofanana na kitu chenyewe huitwa . . . . . . .
Fungua Jibu
18. Je, kuna pande kuu ngapi za dunia? . . . . . . . .
Fungua Jibu
19. Kifaa kinachofanana na saa ambacho huwawezesha wasafiri kujua uelekeo huitwa . . . . . . .
Fungua Jibu
Jibu swali la 20 hadi 23 kwa kuchaguajibu sahihi katika mabano.
20. Misitu, majani na vichaka ni .. . . . . .(bonde la ufa, uoto wa asili, matabaka ya hewa)
Fungua Jibu
21. Mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Katavi, Njombe na Iringa ni maarufu kwa kilimo cha . . . . . . .
Fungua Jibu
22. Madini yanayotumika kutengeneza urembo, kukata vioo na kutoboa miamba huitwa . . . . . . . . .(dhahabu, chumvi, rubi, almasi)
Fungua Jibu
23. Hewa iliyo katika mwendo huitwa . . . . . . . . .(unyevu, upepo, mvua, mawingu)
Fungua Jibu
Tazama ramani ifuatayo kisha utambue nchi zilizowakilishwa kwa herufu A na B
24. Nchi A ni? .
Fungua Jibu