5. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu hililo sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.
Yoya na Bura wanaishi katika Kipp cha Ulanga. Watoto hao walikuwa na tabia ya ukaidi. Kila walipoonywa na wazazi wao hawakutii. Walimu pia walitimiza wajibu wao wa malezi, hivyo mara kwa mara waliwashauri kuacha tabia ya ukaidi. japokuwa walionywa na walimu pamoja na wazazi lakini hawakubadilika.
Walipofika Darasa la Nne, watoto hao walianza tabia ya utoro na hatimaye waliacha shule. Walikubaliana kuanza biashara ya kuuza mkaa. Kila siku walikwenda msituni kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa. Wazazi wao waliwaonya kwa kuwakumbusha katazo la serikali kuhusu ukataji wa miti ovyo.
Siku moja walipokwenda kukata miti msituni, viongozi wa serikali ya waliwavizia na kuwakamata. Waliwapeleka kwenye ofisi ya Kulp. Huko walipata adhabu kali na kuamriwa kupanda miti ishirini kila mmoja. Walijutia ukaidi wao na kuomba radhi kwa wazazi na walimu wao. Walisamehewa na walirudi shuleni kuendelea na masomo. Toka wakati huo watoto hao walikuwa na heshima na watiifu sana.