URAIA STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023

SOMO: URAIA NA MAADILI DARASA: VII 

MUDA: SAA 1:30 

  SEHEMU A: 

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa

1. Ni kiongozi yupi wa kata kati ya wafuatao huchaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge?__

A. ofisa mtendaji wa kata B. diwani C. mwenyekiti wa kijiji D. wajumbe wa kata [     ]

2. Mwajiriwa wa serikali na mtendaji mkuu wa shughuli zote za kata ni yupi? ______

A. afisa elimu kata B. afisa maendeleo jamii C. ofisa mtendaji wa kata D. diwani wa kata [     ]

3. Bendera ya taifa imepambwa na rangi kuu nne ambazo hubeba maana nzito kwa taifa letu. Je, ni rangi ipi huwakilisha madini yanayopatikana nchini? _____ 

A. nyekundu B. njano C. nyeusi D. bluu [     ]

4. Chombo cha kitaifa ambacho huwaunganisha Watanzania katika kuwasiliana ni ______ 

A. Wimbo wa taifa B. redio C. lugha ya Kiswahili D. simu za mkononi [     ]

5. Kati ya vifuatavyo kipi hutumika kuhifadhi na kulinda sheria zote zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania? ______

A. mahakama zote nchini B. magereza C. jeshi la polisi D. katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania [     ]

6. Unapoona mtu mwenye asili ya India anaongea Kiswahili inamaanisha nini? ____ 

A. Hajui lugha yake ya kihindi B. Anakipenda Kiswahili kuliko kihindi C. Anaichukia lugha ya kihindi D. Anaimarisha uhusiano wa kiutamaduni na nchi yetu [     ]

7. Taifa letu lina historia ndefu kabla na baada ya uhuru. Kila tarehe 7 Aprili huwa tunaadhimisha _____ 

A. kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa B kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar C. siku ya uhuru wa taifa D. maonesho ya biashara ya kimataifa [     ]

8. Mwenendo wa maisha unaohusisha mila, desturi, jadi na asili ya watu hujulikana kama: ______ 

A. jamii B. itikadi C. utamaduni D. mazoea [     ]

9. Kati ya zifuatazo zipi ni miongoni mwa tunu za taifa letu? ________ 

A. lugha ya kiswahili, umoja, mshikamano, upendo na utu B. katiba, bendera ya taifa C. fedha za nchi, wimbo wa taifa na lugha ya taifa D. utamaduni, ndege za taifa na umoja na mshikamano [     ]

10. Katika ukuaji wa mtoto kuna mambo yanapaswa kuzingatia kati ya mtoto wa kike na wa kiume; ambapo _____ 

 1. mtoto wa kiume kupewa kipaumbele kuliko wa kike kwa kuwa ni shujaa 
 2. mtoto wa kike afunzwe kazi za nyumbani pekee 
 3. wapewe elimu ya jinsia kulingana na mabadiliko wanayopitia 
 4. watengwe, wasikaribiane kuwaepusha na shewrati [     ] 

11. Zifuatazo ni idara zinazosimamia majukumu mbalimbali katika serikali ya mkoa isipokuwa: ______ 

A. mipango na uratibu B. afya na ustawi wa jamiii C. uchumi, uzalishaji na idara ya elimu D. sensa ya watu na makazi kwa taifa [     ]

12. Kamati ya ushauri ya mkoa ni kikao cha juu cha mkoa kinachojadili na kutoa uamuzi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo katika mkoa, je kikao hiki hufanyika mara ngapi kwa mwaka? ______

A. mara mbili B. mara nne C. mara tatu D. mara moja [     ]

13. Wakuu wa idara katika halmashauri za wilaya huwajibika kwa nani? _____

A. mkuu wa wilaya B. mkurugenzi wa halimashauri C. mkuu wa wilaya D. idara husika [     ]

14. Matendo yasiyofaa katika jamii kama vile ubakaji, ulawiti, ajira za utotoni na kunyimwa mahitajhi muhimu mara nyingi hufanywa na ndugu au wazazi katika familia. Je, ipi ni njia sahihi ya kupambana na tatizo hili? _______ 

 1. wanao fanyiwa matendo haya kukaa kimya kuepuka kuadbibiwa 
 2. kuondoka katika familia hiyo
 3. kuwatilia sumu kwenye chakala waliofanya ukatili huo
 4. kutoa taarifa kwenye sehemu stahiki ili kupata haki zao [     ]

15. Kwanini tunashauriwa kuwatembelea majirani, kuwajulia hali, na kushirikiana katika shughuli za maendeleo? ____ 

A. kupata mikopo kutoka kwa majirani zete B. kujipendekeza kwao C. kukuza mahusianao bora katika jamiii D. ili kuwaelimisha juu ya mambo yanayotokea [     ]

16. Moja ya faida ya kujiunga na klabu mbalimbali shuleni ni: ___

A. kukuza umahiri wa majibizano kwa kupaza sauti B. kukuza uelewa na kujiamini C. kuwa maarufu na kuimarisha utengano katika jamii D. kuongeza ujanja [     ]

17. Waathirika wa UKIMWI, walemavu, na wanaotumia madawa ya kulevya tunapaswa ______ katika jamii. 

A. kuwatenga B. kuwashauri, kuwajali, na kuwasaidia C. kukaa mbali nao D. kuwakashifu [     ]

18. Kati ya yafuatayo yapi ni madhara ya vitendo vya ukatili katika familia au jamii? _____

A. kuenea kwa magonjwa, vifo na kuongezeka kwa watoto wa mtaani B. kukosa ajira katika mda stahiki C. kujenga jamii iliyobora kwa adhabu kali D. hakuna madhara [     ]

19. Serikali ya kidemokrasia huongozwa na nani? _____

A. watu wachache B. wananchi wote C. wanajeshi D. wawakilishi wa wananchi [     ] 

20. Yapi ni majanga ya asili yanayoweza kupelekea uharibifu wa miundombinu na mazingira?

A. uzalishaji wa viwandani na vyombo vya usafiri B. uchimbaji wa madini na shughuli za kilimo C. mafuriko, milipuko ya volcano na kimbunga D. ukataji miti ovyo na vita [     ]

21. Jukumu la kusimamia utunzaji wa mazingira lipo chini ya: _________ 

A. ofisi ya tamisemi B. taasisi ya mazingira ya taifa C. ofisi ya Rais D. ofisi ya makamu wa Rais Jamhuri ya muungano [     ]

22. Ipi kati ya hizi zifuatazo SIYO faida ya kuwa na subira? ______ 

A. Kupata hekima B. Kuchukua uamuzi sahihi C. Kuogopa D. Kupata utulivu wa akili [     ]

23. Jamii tegemezi husababishwa na ________ 

A. taifa kuwa na watu wengi B. vijana kutoshiriki katika shughuli za maendeleo C. kua na ombaomba wengi D. kukosa misaada kutokas nchi zilizoendelea [     ]

24. Kati ya zifuatazo ni rasilimali gani hupatikana nchini Tanzania tu? ________

A. bahari ya Hindi B. madini ya Tanzanite C. ziwa Tanganyika D. mizazi yenye oksijeni [     ]

25. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia uharibifu wa rasilimia aridhi?____ 

A. kilimo cha matuta kukinga mteremko B. kutumia mbolea za viwandani C. kubadilisha mazao kila msimu D. kilimo cha umwagiliaji [     ]

26. Kati ya zifuatazo ni ipi njia sahihi ya kuepusha migogoro katika jamii? _____ 

A. kuwafunga jela watu wakorofi B. kuzuia uvutaji wa bangi C. kuzingatia sheria na haki katika jamii D. kujenga kituo cha polisi [     ]

27. Kiongozi mzuri ni yule anaefata _____ 

A. matakwa ya watu wake B. mtazamo wa watu wengi C. maono kutoka kwa wadau wa siasa D. misingi ya utawala [     ]

28. Kitendo cha kujifanya mwema machoni mwa watu lakini kiuhalisia siyo mwema hujulikana kama _____ 

A. Unafiki B. Uvumilivu C. Ukatili D. Uwazi [     ]

29. Unaposhuhudia vitendo vya ukatili uwapo shuleni unapaswa kutoa taarifa wapi? _______

A. Polisi B. Mahakamani C. Mwalimu wa ushauri nasaha au kwa mwalimu yeyote D. Serikali ya mtaa [     ]

30. Katika familia ikitokea changamoto nani hufanya maamuzi? _____ 

A. baba na watoto wa kuime pekee B. baba na mama C. wanafamilia wate hushauriana na kufikia muafaka D. baba peke ake [     ]

31. Saikolojia ni sayansi ya kuchunguza tabia, mtazamo na imani walizonazo watu inavyoathiri mambo watendayo. Je, ni zipi athari za kisaikolojia? __ 

A. ulemavu, upofu na uziwi B. kuwa na hofu, kutojiamini, na kupata mshituko C. wizi, kuvaa nguo fupi, na uvutaji wa madawa D. yote ni majibu sahihi [     ]

32. Wanafunzi wenye nidhamu njema ndio hufanya vizuri kwenye masomo. Unafikiri ni kwanini? ______ 

A. wanapendelewa na walimu B. wanatumia muda wote kusoma tu

C. wanatekeleza majukumu yao kwa wakati na kujifunza kwa bidii D. wanakuwa na akili nyingi [     ]

33. Kutumia mitandao bila kufuata tamaduni na maadili ya watanzania kuna athari zifuatazo:______ 

 1. kukosa fedha za kigeni, kupunguza utalii nchini na kukuza lugha 
 2. mmmomonyoko wa maadili, uharibifui wa mila na tamaduni za mtanzania 
 3. kujenga jamii iliyo bora kwa kuiga wazuingu
 4. ongezeko la joto duniani [     ]

34. Nini maana halisi ya sheria? _______ 

A. kanuni zinazoongoza taasisi au nchi B. hukumu kwa wahalifu C. ni mwongozo wa kitamaduni D. tuzo apewayo aliyefanyiwa makosa [     ]

35. Ipi ni haki ya mtoto?__

A. haki ya kupata ajira B. haki ya kuolewa C. haki ya kutoa mawazo D. kusoma kwa bidii [     ]

36. Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ina sura ngapi?_ 

A. 20 B. 15 C. 12 D. 10 [     ]

37. Ipi ni kazi ya vyama vya siasa nchini? ______ 

 1. kuelimisha na kushawishi watu kuhusu sera na malengo yao
 2. kukosoa serikali iliyopo madarakani 
 3. Kufanya kampeni wakati wa Harakati za uchaguzi 
 4. kuibua magaidi waliopo nchini na kuwashitaki [     ]

38. Moja ya wajibu wa kila raia wa tanzania ni: ___ 

A. kulinda amani, umoja, na uhuru wa taifa B. kuweka bendera ya taifa nyumbaniu C. kujua kuimba wimbo wa taifa D. kuunga mkono chama cha CCM [     ]

39. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina mgawanyo wa madaraka. Hii husaidia ______ 

 1. mtu mwenye madaraka kunyenyekewa 
 2. kuepusha mwingiliano katika kutekeleza majukumu 
 3. kusaidia serikali iliopo madarakani kutawala kwa muda mrefu 
 4. kuongeza umakini [     ]

40. Uraia wa Tanzania hupatikana kwa njia tatu ambazo ni: _____ 

 1. kutumia kitambulisho cha mpiga kura, cha nida na kuzaliwa 
 2.  kununua, kurithi na kujiandikisha 
 3. kuzaliwa, kurithi na kuandikishwa 
 4. kuzaliwa, kusoma na kurithi [     ]

SEHEMU B: Jaza nafasi zilizoachwa wazi.

41. Jumuiya ya madola ni umoja wa mataifa huru yaliyokuwa makoloni ya uingereza ikiwemo uingereza yenyewe

Jumuiya hii ilianzishwa mwaka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

42. Kitendo cha watu wawili au zaidi kufanya kazi pamoja huitwa: . . . . . . . .... . . . . . . . . ....

43. Kitendo cha kumwambia mtu alichokifanya sio sahihi ni . . . .... . . . . . . . . . . . . ..............

44. Mfumo wa utawala ambapo wananchi hushirikishwa katika maamuzi . . . . . . .. . ... . . . . . .

45. Mfumo ambao huwaunganisha watu katika ulimwengu na kuifanya dunia kama kijiji kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano unaitwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 25  

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 25  

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA URAIA NA MAADILI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo

 1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
 2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
 3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
 4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
 5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
 6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

 1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
 2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
 3. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: (Alama 40)

Kwa swali 1-40, tafuta majibu kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya OMR uliyopewa.

1. Kuna vitu vingi tunaweza kusema kuhusu shule yetu kwa sababu tunaipenda sana na tungetamani watu wengi wafahamu jinsi tunavyojisikia kwajili ya shule yetu. Kipi kati ya yafuatayo ni kitu sahihi tunaweza kufanya ili kuwaonyesha watu kwamba tunajivunia shule yetu?

A: Kutembelea maktaba ya shule mara kwa mara B: Kutunga nyimbo na mashairi kuhusu shule yetu C: Kutoa msaada kwa wahitaji. D: Kufanya vizuri katika mitihani yetu E: Kuheshimu walimu wetu.[       ]

2. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi. Ipi kati ya njia zifuatazo inaweza kutumiwa na wahusika kuitangaza?

A: Kuimba winbo wa taifa B: Kushiriki katika shughuli za michezo mbalimbali C: Kuwa na idadi kubwa ya watu D: Kuongeza idadi ya mabasi ya umma E: Kuepuka kuwa na inchi marafiki

3. Ni jambo la wazi kwamba upendo baina ya watu katika jamii ndiyo msingi wa maendeleo kijamii na kiuchumi. Bainisha moja kati ya machaguo yafuatayo ambalo ni umuhimu wa kusaidia wahitaji A: Inawafanya wajione ni sehemu ya jamii. B: Inaongeza idadi ya wahitaji. C: Inaongeza idadi ya wafadhili. D: Inaongeza kiburi kwa wahitaji. E: Inaongeza idadi ya watu tegemezi katika jamii.

4. Shule ina alama mbalimbali zinazoitambulisha na kuitofautisha na shule zingine. Ni kipengele gani katika nembo ya shule hutumika kama kichocheo kwa mwanafunzi kuongeza juhudi shuleni na baada ya kuhitimu shule?

A: Rangi ya nembo hiyo B: Jina la shule C: Alama zilizomo D: Kaulimbiu ya shule E: Nembo ya shule. [       ]

5. Kaka yangu ni naibu waziri katika Wirara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Ni kauli ipi kati ya zifuatazo si ya kweli kuhusu kaka yangu?

A: Ni mbunge B: Ni mteule wa raisi C: Ni mjumbe wa baraza la mawaziri D: Ni msaidizi wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia E: Ni msimamizi mkuu wa wizara ya elimu Sayansi na Teknologia. [       ]

6. Moja ya majukumu ya kiongozi ni kuhakikisha kwamba watu wa wa eneo lake wako salama dhidi ya tishio lolote la usalama wao. Je ni nani kati ya viongozi wafuatao ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa?

A: Kamanda wa polisi wa mkoa B: Katibu tawala wa mkoa C: Mkuu wa mkoa D: Mganga mkuu wa mkoa E: Afisa elimu mkoa. [       ]

7. Umeteuliwa kama mjumbe wa kamati inayoishauri serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Lipi kati ya mabo yafuatayo halitakuwa miongoni mwa mambo muhimu utakayoshauri yaendelezwe ili kulinda uhuru na umoja wa nchi?

A: Kuheshimu haki za binadamu B: Kulinda mipaka ya nchi C: Kukemea matendo maovu D: Kujenga uhusiano mwema na nchi jirani E: Kufunga mipaka yote ili kuepuka wageni [       ]

8. Kuna mihimili mitatu ya nchi ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge. Lipi kati ya yafuatyo siyo jukumu la Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania?

A: Kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi B: Kuthibitisha uteuzi wa waziri mkuu C: Kuchagua spika D: Kuchunguza matendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi E: Kutafsiri sheria [       ]

9. Jamii tunayoishi ina watu wenye tabia tofauti tofauti. Lipi kati ya yafuatayo unaweza kulitumia kuwawasaidia rafiki zako kuacha kufanya matendo maovu katika jamii?

A: Michezo B: Makundi rika C: Maeneo ya kupumzikia D: Fedha nyingi E: Urafiki [       ]

10. Kuna matendo mbalimbali yanayotendeka katika jamii yetu. Baadhi yanakubalika na mengine yanafaa kukemewa. Ni tendo lipi kati ya haya utalikemea ikiwa utakuta rafiki yako akilifanya?

A: Majadiliano shuleni B: Ukandamizaji C: Kazi za nyumbani D: Kujisomea E: Kusaidia wahitaji. [       ]

11. Kuna changamoto mabalimbali ambazo mwanadamu anapitia na hata zina mfanya apoteze matumaini. Unadhani nini kinatakiwa ili mtu huyo astahilimili changamoto na hatimaye kupata mwelekeo wa maisha yake?

A: Moyo wa kuMoyo wa kukata tama B: Huduma ya unasihi C: Huduma za kifedha D: Kuwa muwazi kwa kila moja E: Makundi rika. [       ]

12. Mwanakijiji mmoja wa kijiji cha Kapemba alitaka kujua kitu kimojawapo kati ya vitu vinavyounda mazingira ya kijiji ambacho kikiharibiwa husababisha upungufu wa mvua . Unafikiri lipi lilikuwa jibu sahihi kwa mwanakijiji huyo?

A: Ardhi B: Maji C: Msitu D: Wanyama E: Mvua. [       ]

13. Kila mmoja anahitaji marafiki katika kazi zake za kila siku. Lipi kati ya yafuatayo linaweza kuimarisha uhusiano baina ya watu wa jamii fulani?

A: Kutembeleana B: Kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii C: Kushiriki katika michezo D: Kusaidiana E: Kudhoofisha mwingiliano wa kijamii. [       ]

14. Tunashauriwa kuendelea kutathmini utendaji kazi wetu binafsi au kundi kwa kila hatua katika kazi zetu za kila siku. Je kujitathmini kuna umuhimu gani katika maisha ya mwanafunzi?

 1. Inamwezesha kuelewa masomo shuleni
 2. Inamwezesha kufahamu walimu wote shuleni
 3. Inamwezesha kulipa ada kwa wakati
 4. Inamwezesha kuona matatizo ya wanafunzi wengine katika masomo yao
 5. Inamwezesha kuelewa madhaifu yake na kuchukua hatua stahiki. [       ]

15. Kuna jamii za kitanzania ambazo bado zinakabiliwa na matatizo kama mimba na ndoa za utotoni. Unafikiri ni lipi kati ya yafuatayo linaweza kusaidia vijana wa jamii hizo kumaliza tatizo hilo?

A: Elimu ya afya ya uzazi B: Kushiriki kwenye mikutano ya hadhara C: Hali ya kiuchumi ya jamii ile D: Ushauri wa wazazi wa jamii ile E: Kutenga vijana na jamii ile

16. Kuna majukumu mbalimbali ambayo yanafanywa na wazazi au watoto katika familia zetu. Bainisha kati ya yafuatayo wajibu wa mtoto katika familia.

A: Kutoa elimu B: Kufariji familia C: Heshima na Nidhamu D: Kulinda familia E: Kuonesha njia kwa wanafamilia wengine. [       ]

17. Wakati wa somo kuhusu kutetea haki za binadamu, mwalimu wetu alimuuliza Julius ataje mila na desturi zinazokiuka haki za binadamu. Lipi kati ya yafuatayo halikuwa jibu sahihi ambalo Julius alitoa?

A: Ndoa za utotoni B: Ukeketaji C: Kutokuwapo usawa wa kijinsia D: Kurithi wajane E: Jinsi zote kufanya kazi za nyumbani. [       ]

18. Nani ni mwenyekiti wa kamati ya taaluma kwa mujibu wa majukumu ya viongozi shuleni?

A: Mwalimu Mkuu B: Mwalimu Mkuu Msaidizi C: Mwalimu wa taaluma D: Mwalimu wa darasa E: Kiranja Mkuu. [       ]

19. Udanganyifu hutokea pale mtu anapoweka mbele maslahi binafsi. Hii inaweza kudhihirika katika miundo tofauti kama vile hongo, ubadhilifu na matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Lipi kati ya machaguo yafuatayo ni suluhisho la tatizo kama hilo katika jamii yetu?

A: Uadilifu B: Viongozi matajiri C: Ujuzi wa uongozi D: Viongozi wenye ushirikiano hafifu E: Viongozi wenye elimu nzuri. [       ]

20. Kuwa Kiongozi katika jamii, mtu anatakiwa kujitolea muda wake wote kuhudumia watu katika jamii hiyo bila kuweka maslahi yake mbele. Kama raia, ni sifa ipi kati ya zifuatazo inaweza kukuongezea imani kuwaamini viongozi wa jamii yako?

 1. Kupewa pesa na viongozi hao 
 2. Kuhusishwa na wizi wa rasilimali za umma.
 3. Uwazi wa viongozi wa jamii yako 
 4. Kupewa kipaumbele na viongozi katika kupewa huduma 
 5. Kupewa tenda za miradi kwenye kijiji chenu. [       ]

21. Ni kawaida kuwasikia viongozi wetu wakihimiza matumizi bora ya fedha za umma. Unadhani nini kitatokea endapo fedha za umma zitatumika vizuri?

 1. Wananchi watapata gawio lao kila mwaka.
 2. Huduma za jamii zitaboreshwa.
 3. Viongozi watapata magari mazuri. 
 4. Kutakuwa na huduma duni za jamii.
 5. Viongozi watakuwa maskini. [       ]

22. Kuna rasilimali mbalimbali nchini kwetu. Baadhi ya ya rasilimali hizo zimetengenezwa na binadamu wakati nyingine ni za asili. Ni rasilimali ipi kati ya zifuatazo inawezesha nyingikuwepo?

A: Hewa B: Ardhi C: Madini D: Mwanadamu E: Maji. [       ]

23. Uwazi, uwajibikaji, umoja na uzalendo ni baadhi tu ya njia ambazo mtu anaweza kuzitumia kuzuia rushwa. Unadhani ni wapi unaweza kuripoti vitendo vya rushwa mara tu unapovishuhudia?

A: CCM B: TAMWA C: TAKUKURU D: JWTZ E: CHRGG [       ]

24. Kama mwanafunzi, unadhani utafanya nini ili kuepuka adhabu za mara kwa mara shuleni?

 1. Kujenga urafiki na walimu wote
 2. Kuwapa zawadi walimu wote
 3. Kutii sheria na miongozo ya shule
 4. Kujificha mara tu baada ya kufanya kosa
 5.  Kuwaambia wazazi au walezi [       ]

25. Ipi kati ya zifuatazo ni njia bora ya kuhifadhi mazingira?

A: Kulima karibu na vyanzo vya maji B: Kuelekeza maji taka mtoni C: Kukata miti D: Kubadili taka kuwa bidhaa E: Kuchimba mchanga kwenye kingo za mto [       ]

26. Unatumia simu ya mkononi na imeunganishwa na intaneti. Ni lipi kati ya mambo yafuatayo utaepuka kusambaza kwa rafiki yako?

A: Taarifa za siri B: Picha zenye staha C: Ujumbe wa salamu kwa rafiki yako D: Taarifa ya uhakika E: Ujumme juu ya kuzuia UVIKO-19 [       ]

27. Tuna vyama vya siasa zaidi ya 17 ncini kwetu na bado wanachama wa vyama hivyo wanaishi kwa amani ijapokuwa wana itikadi tofauti. Ni kipi kati ya hivi vifuatavyo kinasaidia kuwepo kwa maisha haya ya uelewano baina ya watanzania pamoja na uwepo wa itikadi tofauti?

A: Heshima B: Utiifu C: Uwajibikaji D: Uadilifu E: Uvumilivu [       ]

28. Tunaweza kuzungumza mambo mengi kuhusu malengo ikiwemo namna tunavyotakiwa kupangilia. Kwa uelewa wako, lipi kati ya machaguo yafuatayo SI umuhimu wa kuweka malengo katika maisha ya mtu?

 1. Inasaidia kufanya maamuzi sahihi 
 2. Inaongeza ubunifu
 3. Inamuongezea mtu ari ya kufanya kazi kwa bidii 
 4. Inasaidia kutambua mahitaji 
 5. Inachelewesha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa. [       ]

29. Mwalimu wetu huwa anauliza maswali wakati anapofundisha somo la Uraia na maadili. Hii inaweza kufanyika kwa mdomo au kwa maandishi. Nini dhumuni la kuuliza maswali katiaka maisha ya kila siku?

A: Kuweka mipango mingi B: Kuongeza matatizo C: Kuwafanya watu wasifikiri D: Kupunguza maswali kutoka kwa wengine E: Kutafuta suluhisho la matatizo mbalimbali. [       ]

30. Mtu anasemekana kuwa na subira ikiwa ana uwezo wa kusubiri au kuendelea kufanya jambo fulani. Unadhani subira inamsaidia nini mtu katika maisha?

A: Inajenga mahusiano mazuri na jamii B: Inaongeza mwanya wa kutokea kwa migogoro C: Inamaliza muda wa shughuli nyingine D: Inadhalilisha watu wengine E: Inaweza kufelisha mipango ya watu. [       ]

31. Tabia ya kuficha hisia halisi za mtu hujulikana kama unafiki. Ipi kati ya haya yafuatayo ni madhara ya tabia hiyo?

A: Urafiki imara B: Mahusiano hafifu ya kijamii C: Upendo baina ya wanajamii D: Kujiamini E: Ubunifu. [       ]

32. Demokrasia ni serikali ya watu kwa watu na kwa ajili ya watu. Ni kanuni ipi ya kidemocrasia inamuwezesha kiongozi kueleza juu ya maamuzi ya utekelezaji wa majukumu yake?

A: Haki za binadamu B: Uwazi C: Uwajibikaji D: Usawa E: Utawala wa sheria. [       ]

33. Matumizi ya intaneti yana upande mzuri na mbaya. Ni lipi kati ya haya yafuatayo ni upande mbaya kwa mwanafunzi anaetumia intaneti?

A: Kujifunza maneno ya kashfa B: Kujifunza njia za kukokotoa hesabu C: Kujifunza njia mbalimbali za kupika vyakula D: Kujifunza njia za kucheza michezo E: Kuuza bidhaa kupitia intanet. [       ]

34. Shule ina chombo ambacho kinajulikana kama Baraza la wanafunzi. Viongozi wa chombo hiki ni wanafunzi wenyewe . Unafikiri kuna umuhimu gani wa kuwa na chombo hiki shuleni?

 1. Kinawasaidia wanafunzi kujadili mambo yao wenyewe na kuyawasilisha kwa uongozi wa shule.
 2. Inawasaidia wanafunzi kujadili tabia za walimu.
 3. Inawasaidia wanafunzi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya walimu wao.
 4. Inawawezesha wanafunzi kutengeneza sheria na kanuni za shule. 
 5. Inasaidia kujadili hali ya maisha ya wazazi wa wanafunzi. [       ]

35. Biashara ya kimataifa ni kitu muhimu katika kudumisha mahusiano mema na watu kutoka mataifa mengine. Ni kitu gani kingine kati ya hivi vifuatavyo kinaweza kudumisha mahusiano mazuri na watu wengine kutoka mataifa mbaimbali?

A: Michezo B: Mawasiliano hafifu C: Ukosefu wa viongozi wazuri D: Watu wakorofi E: Elimu nzuri. [       ]

36. Lipi kati ya haya yafuatayo ni njia bora ya kuepuka kushuka kwa viwanda vya ndani kunakosababishwa na athari za utandawazi?

 1. Kuwahimiza wananchi kutumia bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini
 2. Kuingiza bidhaa za viwandani kutoka nje
 3. Kuongeza wageni nchini
 4. Kuepuka kutumia bidhaa zilizotengenezwa hapa nchini
 5. Kuhimiza wananchi kwenda kufanya kazi nchi za nje. [       ]

37. Tanzania ina uhusiano mzuri na nchi jirani. Hali hii imefanya nchi nyingi kutumia bandari ya Dar es Salaam. Ni nchi zipi hutumia bandari ya Dar es salaam kuingiza bidhaa kutoka ughaibuni?

A: Zambia na Malawi B: Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Zimbabwe C: Kenya na Zimbabwe D: Sudani na Zimbabwe E: Namibia na Zambia. [       ]

38. Ni nchi zipi zilifufua Jumuiya ya Afrika Mashariki? Hili lilikuwa swali kutoka kwa mmoja wa wanafunzi katika darasa letu. Unadhani ni jibu gani sahihi lingefaa kwa mwanafunzi huyo?

A: Tano B: Sita C: Tatu D: Saba E: Nne. [       ]

39. Kipi kati ya vyama vifuatavyo ni chama cha siasa kilichosajiliwa na kwa sasa kinafanya shughuli zake nchini Tanzania?

A: ANC B: NCCR – MAGEUZI C: TANU D: NEC E: UTP. [       ]

40. Ndoto ya Ibrahimu ni kuwa kiongozi katika kata yetu. Kwa sasa ana miaka 15. Unafikiri ni baada ya miaka mingapi atakuwa na sifa ya kugombbea nafasi ya udiwani?

A: Miaka saba B: Miaka mitatu C: Miaka sita D: Miaka tisa E: Miaka kumi na nane. [       ] 

SEHEMU B: (Alama 10)

Andika jibu sahihi kwa kila swali la 41-45 katika nafasi iliyoachwa wazi nyuma ya karatasi ya OMR. Tumia kalamu ya wino mweusi au wa buluu.

41. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ni aina gani ya uraia mtu anatakiwa kuwa nao kama kigezo muhimu cha kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania?

42. Matokeo ya hisia ni mihemuko ambayo isipodhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa. Elezea kwa kifupi faida mbili za kuthibiti hisia na mihemko.

43. Tanzania inafaidika vipi kiuchumi na kupanuka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

44. Elezea kwa kifupi namna anavyopatikana kiranja mkuu shuleni kwenu.

45. Eleza kwa kifupi namna kodi isiyo ya moja kwa moja inavyolipwa serikalini.

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 20  

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 20  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

URAIA NA MAADILI DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

 1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
 2. Jibu maswali yote
 3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
 4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
 5. Tumia penseli ya HB tu.
 6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotawala kwa kufuata misingi ya kidemokrasia. Ipi mojawapo kati ya sababu zifuatazo ni lengo la kuanzisha mfumo wa vyama vingi Tanzania?

(A) kutokuwa na umoja (B) kudumisha amani miongoni mwa watu (C) kuongeza migogoro (D) kudumisha demokrasia (E) kuongeza matabaka [     ]

2. Urafiki ni uhusiano wenye afya kati ya mtu na mtu. Lipi kati ya matendo yafuatayo huharibu uhusiano kwa wengine? 

(A) uchangiaji wa vitu (B) kushiriki mambo ya kijamii (C) kuungana katika michezo

(D) kujadli mambo kwa pamoja (E) kujitenga na wengine [     ]

3. Ni tarehe ipi wanawake husherekea siku yao duniani?

(A) 24 Februari (B) Machi 8 (C) Machi 6 (D) Machi 7 (E) Machi 9 [     ]

4. Kauli mbiu ya shule hueleza mambo yaliyoko shuleni na kuhamasisha wanafunzi wa shule husika. Kati ya yafuatayo lipi sio mfano wa kauli mbiu ya shule? 

(A) elimu ni mwanga wa baadae (B) elimu ni ufunguo wa mafanikio (C) elimu ni msingi wa utajiri (D) elimu ni mwanga (E) elimu ni mlango wa baadaye [     ]

5. Yapi sio maelezo sahihi kuhusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

(A) ni nchi huru isiyohitaji urafiki na nchi nyingine (B) ni nchi ya kidemokrasia (C) ni nchi inayofuata utawala wa sheria (D) ni nchi huru yenye watu huru (E) ni nchi mwanachana wa mashirika ya kikanda [     ]

6. Tunaishi na watu tofauti katika jamii zetu na familia zetu. Wafuatao ni makundi ya watu wenye mahitaji maalum na uangalizi makini isipokuwa___________

(A) wazee (B) wanawake wajawazito (C) mlevi (D) kipofu (E) kiziwi [     ]

7. Kobelo ni kiongozi wa kata ya Magila ambaye alishinda uchaguzi mwaka 2020. Vilevile akawa mwenyekiti wa kamati mbalimbali katika kata na kwa hiyo anatarajia kuchaguliwa tena baada ya miaka mitano kutokana na uongozi wake mzuri. Je! Kobelo anaweza kuwa na cheo gani? 

(A) afisa mkuu (B) afisa mtendaji wa kijiji (C) afisa mtendaji wa kata (D) afisa wa mahakama ya kata (E) diwani [     ]

8. Mwalimu wa somo la Uraia na Maadili aliwaambia wanafunzi wa darasa la sita wataje sifa za shule bora. Ipi kati ya sifa zifuatazo haikuwa sifa sahihi ya shule bora? 

(A) wanafunzi na walimu kuwa wasafi mara zote (B) walimu na wanafunzi kutimiza majukumu yao (C) kuwepo kwa migogoro kila mara na wazazi kwa sabasbu ya malipo ya ada (D) walimu na wanafunzi kushirikiana pamoja (E) wazazi na walimu kushirikiana katika kuinua ufaulu wa shule [     ]

9. Wajibu wa kudumisha ulinzi wa Taifa letu la Tanzania ni kazi ya kila raia lakini vipo vyombo maalum vya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kipi kati ya vifuatavyo sio chombo cha ulinzi na usalama? 

(A) jeshi la uokozi na zimamoto (B) jeshi la wananchi wa Tanzania

(C) Mfumo wa mahakama wa Tanzania (D) idara ya upelelezi na usalama wa Tanzania

(E) Jeshi la polisi [     ]

10. Naomi ni mwanafunzi wa darasa la tano anaejitolea kufanya kazi nyingi shuleni na nyumbani. Kati ya kazi zifuatazo ipi inaweza kuwa kazi anayojitolea kufanya ndani ya darasa? (A) kupanga meza na madawati

(B) kuwapa walimu zawadi (C) kuosha vyombo (D) kulala walimu wasipokuwepo (E) kuwa kimya darasani [     ]

11. Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huundwa na viongozi wakuu wa serikali kuu. Ni kiongozi gani kati ya hawa sio miongoni mwa baraza la mawaziri? 

(A) Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (B) Waziri mkuu (C) Jaji mkuu (D) Mwanasheria mkuu (E) Rais wa Zanzibar. [     ]

12. Kupunguza watoto wa mitaani na mmomonyoko wa Maadili Tanzania kunaweza kufanikiwa endapo_

(A) kukua kwa uchumi (B) watu wakiishi maisha mazuri (C) serikali ikitumia nguvu (D) familia zikiwa imara (E) elimu ikitolewa kwa watu wote [     ]

13. Chombo cha umma kinachoonesha mgawanyiko wa mamlaka na mipaka yake ni ________

(A) katiba (B) chama cha siasa (C) vyombo vya habari (D) Rais (E) bunge [     ]

14. ________ni mhusika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na wadhifa na cheo chake. (A) Raisi (B) waziri mkuu (C) spika (D) mwanasheria mkuu (E) jaji mkuu [     ]

15. Madam Jokate Mwegelo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Korogwe hakuwepo kazini kwake kwa siku tano. Ukiwa kama mwanafunzi unayeelewa itifaki za uongozi, nani atakaimu nafasi yake kwa siku hizo tano?

(A) Mkurugenzi mtendaji wa wilaya (B) meya mkuu (C) mbunge wa wilaya (D) katibu tawala wa wilaya (E) diwani [     ]

16. Kulingana na sheria ya Tanzania, kuchapisha picha zenye maudhui ya uamsha hisia za ngono ni kosa la uhalifu. Je! sheria inayohusiana na udhibiti wa makosa ya aina hii ilitungwa mwaka gani na bunge la Tanzania?

(A) 2007 (B) 2020 (C) 2005 (D) 2015 (E) 2016 [     ]

17. Lipi kati ya haya yafuatayo ni jukumu la msingi la Bw. Malema Lukindo ambaye ni mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gereza? 

(A) kuandaa ratiba ya shule (B) kuandaa kitabu cha zamu cha walimu (C) kutoa adhabu kwa wafanyakazi (D) kuongoza kikao cha kamati ya shule (E) kusimamia kazi zote za shule za kila siku [     ]

18. Lipi kati ya yafuatayo sio tendo rafiki kwa mazingira? 

(A) kubadili taka kuwa nyenzo itakayotumika (B) kuvua samaki kwa wavu wenye matundu makubwa (C) utupaji mbaya wa taka (D) ulimaji wa kufuata kontua katika miteremko (E) kupunguza uhifadhi wa mazao [      ]

19. Ni nchi zipi kati ya hizi zifuatazo zina nguvu ya kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa? 

(A) China, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na Italia (B) Ufaransa, Marekani, Urusi, China na Uingereza (C) Ureno, Hispania, China, Urusi na Marekani (D) Italia, Dernmark, Afrika Kusini, Ujerumani na Ubelgiji (E) Uholanzi, Marekani, Brazil, Uingereza na Ufaransa [     ]

20. Shirika lisilo la serikali linaloonesha changamoto mbalimbali unaokumba mfumo wa elimu wa Tanzania hujulikana kama___

(A) TAMWA (B) BASATA(C) BAKITA (D) HAKI ELIMU (E) WIZARA YA ELIMU [     ]

21. Nani anayehusika katika uandaaji wa ratiba za vikao vya bunge? (A) spika wa bunge (B) jaji mkuu (C) mwenyekiti wa bunge (D) katibu wa bunge (E) mwanasheria mkuu [     ]

22. Ni ujumbe gani hutolewa na alama ya pundamilia kwa madereva wa magari?

(A) yawezekana kuna magari megine yanavuka barabara au kusubiri kuvuka barabara (B) kuna watembea kwa miguu wanavuka barabara au wanasubiri kuvuka barabara (C) punguza mwendo kuna kivuko cha reli mbele (D) punguza mwendo kuna hifadhi mbele (E) kuna askari wa barabarani wanaodhibiti mwendo [     ]

23. Kituo cha sheria za haki za binadamu kilianzishwa mwaka gani?

(A) 1996 (B) 1989 (C) 2005 (D) 1995 (E) 2001 [     ]

24. Mtu ambaye ni mwaminifu na huweza kuaminika kwa wengine huitwa________

(A) mnafiki (B) mtu mwaminifu (C) mtu asie na maadili (D) mtu mvumilivu (E) msaliti [     ]

25. Ni katika kipindi gani bendera ya Taifa ya Tanzania hupepea nusu mlingoti?

(A) tunapotembelewa na wageni kutoka nchi nyingine (B) Rais anapotangaza hali ya hatari (C) kunapokuwa na janga la kitaifa au tukio la huzuni (D) kumbukumbu ya kitaifa ya mashujaa (E) Rais anapokuwa nje ya nchi [     ]

26. Mtindo wa kujifunza wenye lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuhusisha walichokisoma darasani na uhalisia hufahamika kama________ 

(A) kujifunza kwa uchambuzi (B) kujifunza kwa kurudia (C) kujifunza kwa mwendelezo (D) kujifunza kwa haraka (E) kukariri mambo mbalimbali [     ]

27. Vitu vya thamani vinavyoweza kutuletea utajiri au kipato katika taifa hufahamika kama_(A) alama za taifa (B) rasilimali za taifa (C) tunu za taifa (D) malighafi (E) heshima ya taifa [     ]

28. Malengo au matarajio yanayopangwa kutimizwa katika muda fulani huitwa_________

(A) mipango (B) mikakati (C) misheni (D) changamoto (E) malengo [     ]

29. Nandala aligundua kuwa rafiki yake kinumbo anajihusisha na madawa ya kulevya. Je! lipi kati ya haya ni tendo sahihi kwa Nandala kulifanya? 

(A) kukaa mbali na Kinumbo (B) kumpeleka Kinumbo polisi (C) kumuadhibu Kinumbo (D) kumpeleka kwenye ushauri na unasihi (E) kujiunga naye katika matumizi ya madawa ya kulevya [     ]

30. Wanafunzi katika shule ya Msingi Sambweni walizoea kutoa maoni yao na matatizo kupitia masanduku ya maoni ambayo hutundikwa kwenye madarasa yao. Nini umuhimu wa kuwa na masanduku ya maoni shuleni? (A) kufichua siri za wanafunzi (B) kutoa maoni kwa siri (C) kuadhibu wanafunzi (D) kupokea ada za shule (E) huvutia wageni [     ]

31. Katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulingana na katiba kiongozi wa juu wa mfumo wa mahakama ni jaji mkuu ambaye huapishwa na mtu mwenye cheo cha kati ya hivi vifuatavyo;

(A) Rais wa Zanzibar (B) Mwanasheria Mkuu (C) Katibu wa bunge (D) Waziri mkuu (E) Amiri jeshi Mkuu [     ]

32. Amina anaishi katika familia ya kiislamu, siku moja aligombana na mume wake na akaamua kupeleka kesi mahakamani kwa ajili ya maamuzi. Je ni mahakama gani iliyosimamia kesi hii na kutoa maamuzi?

(A) mahakama ya mwanzo (B) Mahakama kuu (C) mahakama ya kadhi (D) mahakama ya rufaa (E) mahakama ya hakimu mkazi [     ]

33. Kasuwi alizaliwa tarehe 9 Disemba 1962. Ni tukio gani la kihistoria lilitokea siku hiyo?

(A) Tanganyika ilipata rais wake wa kwanza (B) Tanzania ilipata rais wake wa kwanza (C) Tanzania iliingia kwenye mfumo wa chama kimoja(D) Tanzania ilijiunga na shirika la fedha duniani na benki ya dunia (E) Tanganyika ilipata uhuru.[     ] 

34. Wanafunzi wa kike wa darasa la saba waliambiwa waeleze kwa nini ni muhimu wao kujua zaidi kuhusu elimu ya afya ya uzazi? Je! kati ya haya lipi lilikuwa jibu sahihi?

(A) huchangia ndoa za utotoni (B) huchochea vijana kujiunga na makundi hatari (C) huongeza idadi ya watoto wa mitaani (D) inawasaidia kuwakinga kutokana na mimba zisizotarajiwa (E) inawajengea mfumo mzuri wa kujieleza [     ]

35.Maendeleo ya uchumi wa Taifa hutegemea__________ 

(A) idadi ya viongozi ambao nchi inayo

(B) jinsi gani mali asili zinavyotumika na kutunzwa (C) matumizi mabaya ya mali asili (D) madini pekee (E) kuwa na Rais bora [     ]

36. Mimi ni msaidizi mkuu wa Mkuu wa Mkoa. Mimi pia ni kiongozi wa watumishi katika ngazi ya mkoa na ni katibu wa sekretarieti ya Mkoa, ninateuliwa na Rais. Mimi ni nani?

(A) mkuu wa Mkoa (B) kamanda wa polisi wa mkoa (C) katibu tawala wa mkoa

(D) afisa wa trafiki wa mkoa (E) mkaguzi wa ndani wa mkoa [     ]

37. Nini hutokea kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakusaini mswada wa sheria?

(A) hutupwa na hauna kazi tena (B) huwa karatasi ya mawaziri na hujadili na hujadiliwa katika baraza la mawaziri (C) hurudishwa bungeni na kujadiliwa zaidi (D) Rais anaweka ndani ya brifukesi yake

(E) yote ni Majibu sahihi [     ]

38. Kitendo cha kuwa tayari kupokea kushindwa na kuwa tayari kukosolewa wakati wa uchaguzi na viongozi wa vyama vingine vya siasa hali hii huitwa__________

(A) mapambano ya kisiasa (B) uvumilivu wa kisiasa

(C) utawala bora (D) demokrasia (E) utawala wa kisheria [     ]

39. Matumizi mabaya ya fedha au utajiri uliokabidhiwa kuutunza huitwa__________

(A) uchafuzi (B) utapeli (C) ubadhilifu (D) upendeleo (E) ubinafsi [     ]

40. Ni chombo gani Zanzibar hufanya kazi sawa na tume ya Taifa ya uchaguzi ya Tanzania bara?

(A) NEMC (B) ZEMC (C) ASP (D) CABINET (E) ZEC [     ]

SEHEMU B

41. Bw. Mazuko ameteuliwa kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sambu ambayo ipo maeneo ya vijijini lakini shule yake ina ukosefu wa vifaa na vitendea kazi muhimu kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji. Taja njia mbili anazoweza kuzitumia ili kupata fedha kwa maendeleo ya shule

(i) __________________________________ 

(ii) ______________________________

42. Ubalozi ni makazi maalumu au ofisi ya balozi katika nchi nyingine. Orodhesha kazi mbili za mabalozi

(i) _______________________________ (ii) _______________________________

43. Kutokana na Katiba ya Tanzania, majukumu ya kila kiongozi yameainishwa na kuandikwa. Ikiwa kuna maombolezo ya kitaifa wapo viongozi wawili wanaoweza kutangaza tukio hilo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo. Taja viongozi hao

(i) _________________________________________________________

(ii) _________________________________________________________

44. Nani ni kiongozi wa kazi za serikali za kila siku bungeni?

_____________________________________________________________________________

45. Mwaka 2022 Tanzania ilifanya sensa ambayo ilikuwa tukio muhimu sana. Wewe kama raia wa Tanzania unafikiri ni kwa nini sensa ni muhimu? Toa sababu mbili.

(i) _________________________________________________________

(ii) _________________________________________________________

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 5  

STANDARD SEVEN URAIA EXAM SERIES 5  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256