SAYANSI STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JINA LA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . .  

NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . .  

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MPWAPWA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024 

SOMO: 05 - SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:40

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali nane (08).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali ili kujibu vipengele husika kwa usahihi.
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa.
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika.
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi (alama 10)

(i) Mwanafunzi wa darasa la tano aliulizwa swali na mwalimu wake ataje kitu ambacho hakiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa bali kinaweza kubadilishwa kutoka hali moja kwenda hali nyingine. Je, unafikiri alitaja jibu gani?

A. Jua B. Maji C. Nishati D. Elementi E. Sumaku [     ]

(ii) Seli hai nyekundu za damu hudumu mwilini kwa muda gani?

A. Siku 120 B. Siku 90 C. Siku 60 D. Siku 180 E. Siku 360 [     ]

(iii) Sehemu ya kutumbukiza funguo katika kitasa ina mashine sahili aina gani?

A. Springi B. Skrubu C. Bolti D. Gurudumu na Ekseli E. Nyenzo [     ]

(iv) Yafuatayo ni aina ya mazoezi ya mwili isipokuwa . .

A. Kutembea B. Kucheza mpira C. Kuruka Kamba D. Kusikiliza muziki E. Kuogelea [     ]

(v) Ni aina gai ya madini husaidia kuimarisha mifupa na meno?

A. Ayani na sodiamu B. Magneziamu na chuma C. Kalsiamu na Fosiforasi D. Potasiamu na Zinki E. Ayodini na Zinki [     ]

(vi) Virusi vya Ukimwi hushambulia seli zipi za damu?

A. Nyekundu B. Njano C. Chembe sahani D. Plazma E. Nyeupe [     ]

(vii) Ateri zote hubeba damu yenye oksijeni isipokuwa

A. Aota B. Vena kava C. Ateri ya palmonari D. Ateri kuu E. Vena ya palmonari[     ]

(viii) Sumaku imeundwa na nini? A. Chuma B. Zebaki C. Kioo D. Manganizi E. Zinki [     ]

(ix) Kuiva kwa tunda ni badiliko gani la maada? A. Kikemikali B. Kibaolojia C. Kiumbo D. Kimakanika E. Kifizikia [     ]

(x) Ni kifaa gani kinaweza kurekebisha kasoro ya jicho taswira kufanyika nyuma ya Retina?

A. miwani B. Lenzi mbonyeo C. Lenzi mbinuko D. Kioo bapa E. Hadubini[     ]

2. Oanisha Orodha A na Orodha B ili kupata maana sahihi na kisha herufi ya jibu sahihi katika nafasi ulizopewa.

Orodha A

Majibu

Orodha B

I. Msawazo asilia

[     ]

A. Bwawa lenye maji, samaki,majani madogo madogo, vyura na magugu maji, bakteria na fangasi

Ii. Ikolojia

[     ]

B. Huozesha mimea na wanyama na kurutubisha udongo

Iii. Transipiresheni

[     ]

C. Elimu ya viumbe hai na mazingira

Iv. Bakteria na Fangasi

[     ]

D. Hali asilia ya urekebishaji wa idadi ya viumbe hai katika mazingira

V. Mfano mfumo wa Ikolojia

[     ]

E. Kitendo cha mmea kupoteza maji kwa njia ya mvuke kupitia stomata za kwenye majani

F. Huozesha udongo wa tifutifu.

3. Kamilisha kipengele cha i -v kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku, kisha kuliandika kuliandika katika nafasi iliyoachwa wazi.

Barua pepe, Kicharazio, Skrini, Kichakato kikuu, prorgramu tumizi

i. . . . . . . . . . . . . . . . . hupokea na kuchakata kazi zote zinazoingia kwenye tarakirishi

ii. . . . . . . . . . . . . . . . hutumika kuingiza data au taarifa kwenye tarakilishi

iii. . . . . . . . . . . . . . . hutumika kuonesha kazi inayofanyika au taarifa ndani ya tarakilishi

iv. . . . . . . . . . . . . . . hujumisha programu andishi na jedwali

v. . . . . . . ni ujumbe unaotayarishwa kwa kutumia tarakilishi na kusambaza kwa njia ya intaneti

SEHEMU B (Alama 20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

4. (i). Sehemu ya programu andishi inayotumika kusahihisha makosa katika waraka hujulikana kama . . . . . . . . . . .

(ii). Mtu anayekula vyakula vyenye mafuta kwa wingi anaweza kupata . . . . . . . . .

(iii). Ugonjwa unaosababisha na hitilafu katika chembe hai nyekundu za damu ni . . . . . . .

5. (i) Sehemu ipi ya mfumo wa umeng’enyaji chakula inahusika na umeng’enyaji wa protini? . . . . . . . . .

(ii). Huduma ya afya anayepewa majeruhi kabla hajapelekwa hospitalini ni . . . . . . . . .

Iii. Saratani ya damu ambayo hujulikana kama Leukemia huathiri tishu za mwili zinazohusika na uzalishaji wa aina ipi ya seli za damu? . . . . . . . . . .

6. (i) . Eleza ni kwa nini cherehani ni mashine tata? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(ii). Ni kwa nini waathirika wa VVU au UKIMWI hushambuliwa na magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu? . . . . . . . . . .

Iii. Dainamoo ni kifaa ambacho huzalisha umeme kwenye baiskeli kwa kutumia aina gani ya nishati? . . . . . . . . . . .

Iv. Kaswende ni mojawapo ya magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya kujamiana. Ugonjwa huu husababishwa bakteria yupi? . . . . . . . . . . . .

SEHEMU C( Alama 10)

Jibu maswali yote katika sehemu hii( michoro, ukokotoaji wa dhana za kisayansi)

7. (i) Densiti ya jiwe ni Kg/m380 na tungamo lake ni Kg 240. Kokotoa ujazo wake

(ii) Tafuta ufanisi wa mashine, ikiwa manufaa ya kimakanika 4 na uwiano wa mwendo dhahiri ni 16

(iii) Katika sakiti ya umeme yenye Ukinzani wa omu 8. Ikiwa voltimita inasoma volti 4. Nini kiasi cha umeme kinachopita katika waya? . . . . . . .

8. Chunguza mchoro ufuatao hapo chini kisha jibu maswalu yafuatayo:

  1. . Herufi “D” inaonesha kitu gani? . . . . . . . . . . . . . . . . . .
  2. . Tafuta thamani ya pembe “n” katika mchoro hapo juu . . . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 47  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 47  

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024 

SOMO: 05 - SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:40

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali nane (08).  
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.  
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali ili kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi (alama 10)

(i) Mfumo wa utoaji takamwili katika mwili wa binadamu umeundwa na ogani kuu nne. Ogani ipi inahusika na kuondoa sumu pamoja na kusaga vyakula vyenye mafuta na protini? 

A. meno B. figo C. ini D. mapafu E. ngozi [     ]

(ii) Viumbe hai wamegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni mimea na wanyama. Je, ni sifa zipi zinahusu makundi yote hayo mawili kwa pamoja? 

A. ukuaji, respiresheni na fotosinthesisi B. mjongeo, uzaaji na transpiresheni C. respiresheni, uzaaji na ukuaji D. respiresheni, transpiresheni na ukuaji E. respiresheni na fotosinthesisi [     ]

(iii) Ni mmea upi kati ya hii ifuatayo unaweza kubadili naitrojeni na kuwa naitreti? A. mhindi B. maharage C. mpunga D. kahawa E. pamba [     ]

(iv) Baada ya kupata ajali ya pikipiki mwili wa Rahma umeshindwa kuwa katika hali ya msawazo ambapo humpelekea kuyumbayumba kama mlevi pindi atembeapo barabarani. Je, ni sehemu gani ya sikio lake imeathirika? 

A. koklea B. vifereji nusuduara C. neva za akustika D. ngoma ya sikio E. miatus [     ]

(v) Sifa mojawapo ya mimea ni kutawanya mbegu zake baada ya kukomaa. Je, ni kwanini mimea hufanya hivyo? 

A. ili mbegu zichukuliwe na wanyama B. ili mbegu ziongeze virutubisho C. ili mimea iendelee kustawi vizuri D. ili kupunguza uzazi E. ili mbegu ziote haraka [     ]

(vi) Zuhura ana tatizo la kutokwa na vidonda mdomoni mara kwa mara. Je, unafikiri Zuhura ana ukosefu wa vitamini ipi? 

A. C B. K C. B1 D. B12 E. D [     ]

(vii) Walimu wa shule ya msingi Maendeleo wanahitaji mashine ya kielektroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadhi na kutoa taarifa za maendeleo ya wanafunzi. Je, utawashauri wanunue nini? 

A. program jedwali B. runinga C. tarakilishi D. printa E. kisimbuzi [     ]

(viii) Ni sifa ipi ya wanyama katika kundi la amfibia inawatofautisha na ndege? 

A. kutaga mayai B. kuishi majini C. kuishi nchi kavu D. kuwa na damu moto E. kuwa na mifupa mifupi [     ]

(ix) Wanafunzi wa darasa la nne walijifunza vifaa mbalimbali vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Je, ni kifaa kipi hupokea mawimbi ya sumakuumeme ya runinga kutoka kwenye satelaiti? 

A. runinga B. kisimbuzi C. dishi D. plagi E. waya [     ]

(x) Kuna aina kuu tano za alama za usalama ambazo hutofautishwa kwa mfumo wa rangi, maelekezo na sifa. Je, alama za onyo au tahadhari huwakilishwa kwa rangi ipi? A. bluu B. njano C. nyekundu D. kijani E. kijivu [     ]

2. Oanisha sehemu A na sehemu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi (Alama 05)

Sehemu A Majibu Sehemu B
(i) Mfumo wa utoaji takamwili
A. Mfumo wa uzazi wa mwanamke
(ii) Kasoro katika mmeng’enyo wa chakula
B. Mishipa ya damu, tezijasho na tezi mafuta
(iii) Mrija wa manii, urethira na tezi za kopa
C. Ubongo, ugweuti na neva
(iv) Sehemu ya ndani ya ngozi
D. Kuhara na kutapika
(v) Mfumo wa fahamu
E. Ini, mapafu, figo na ngozi


F. Mfumo wa uzazi wa mwanaume


G. Kiungulia na vidonda vya tumbo

3. Katika kipengele cha i-v jibu maswali kwa kujaza jibu sahihi kwa kuchagua kwenye kisanduku cha maneno uliyopewa. (Alama 05)

(i) Hakikisha umeweka kichwa cha ujumbe, funga akaunti yako baada ya kuitumia na kamwe usiruhusu kisakuzi kukumbuka nywila yako. Je, hayo ni mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia nini?  

(ii) Hitilafu katika tezi ya kongosho husababisha ugonjwa gani? 

(iii) Wanafunzi wa darasa la saba waliulizwa swali kuhusiana na uchambuzi na uwasilishaji wa data zilizo katika namba. Je, swali hilo lilijikita katika kufafanua dhana gani?  

(iv) Asia alipopimwa na daktari iligundulika kuwa na tatizo katika uzalishaji wa chembehai za damu mwilini. Je, ni nini huhusika na utengenezaji wa chembehai za damu mwilini?  

(v) Start → All programs → Microsoft Office → word 2016 =                                               

SEHEMU B : MAJIBU MAFUPI (ALAMA 20)

Jibu maswali kwa kifupi

4. (i).Ni rangi ipi hutokea kama zao la mpambano wa gesi ya kabonidioksidi na maji ya chokaa?                                                 

(ii). Baada ya panga kusahaulika nje asubuhi tulipoamka tuliona panga likiwa na kutu. Je, kutu ni matokeo ya mchanganyiko wa nini?                                                 

(iii). H + O2 → Y. Je, herufi katika mlinganyo huu inawakilisha nini?                                              

5. (i). Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa yanayoenea kwa haraka sana. Je, viini vya ugonjwa wa kipindupindu huingia mwilini kwa kupitia njia ipi?                                        

(ii). Kila jaribio la kisayansi lina hatua muhimu za kufuatwa. Itaje hatua ya mwisho ya jaribio la kisayansi                                        

(iii). Utabiri kuhusu chanzo cha tatizo linalotarajiwa kufanyiwa uchunguzi hujulikanaje?                                          

6. (i). Hewa, chuma na maji ni vitu vinavyoweza kupitisha joto tofauti na plastiki. Je, ni kwanini plastiki haipitishi joto?                                                    

(ii) Katika kujifunza aina mbalimbali za vioo tuligundua ya kuwa viio vinavyotumika kwenye vyombo vya usafiri kama vile magari huonesha eneo kubwa na taswira zake ni wima. Je, hizo ni sifa ya aina gani ya kioo?                                                

(iii) Tulipowasili kwenye maabara ya uchunguzi wa vimelea vya magonjwa mbalimbali tulikuta kifaa ambacho hutumika kuchunguza vimelea hivyo ambavyo kwa macho ya kawaida haviwezi kuonekana. Je, kifaa hicho kinaitwaje?                                                              

(iv) Tunashauriwa kutunza vyema sumaku ili ziweze kubaki na ubora wake wa awali. Taja vitendo viwili vinavyosababisha kusumakua sumaku a)                                                             b)                                                

SEHEMU C: PICHA, MICHORO NA DHANA MBALIMBALI ZA KISAYANSI (Alama 10)

7. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu kipengele cha i-iii

(i) Katika mchoro huo hapo juu unaonesha kitendo gani kinachofanywa na mmea?                                 

(ii) Je, kitendo hicho kinachooneshwa na mmea huo kisayansi huitwaje?                                      

(iii) Unafikiri mmea huo umehifadhiwa sehemu yenye sifa ipi hadi uoneshe hali hiyo?                                  

8. Chunguza kwa makini alama za wanafunzi wa darasa la saba


A

B

C

D

E

F

1

Jina la Mwanafunzi

Hisabati

Sayansi

Maarifa

Jumla

Wastani

2

Dibe

45

35

40



3

Anganile

12

5

23



4

Tufyage

45

45

45



(i) Taja jina la programu unayohitaji kuitumia ili kukamilisha matokeo hayo?                                                          

(ii) Andika jina la seli lilipoandikwa jina la Anganile                                                                               


STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 41  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 41  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024 

SOMO: 05 -SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali nane (08)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Kwa kipengele cha swali la i – x, chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika parandesi ulizopewa.

i. Deus alishangaa kuona miti yenye majani membamba kama sindano alipomtembelea kaka yake Ulaya. Ni sifa ipi kati ya sifa hizi inalandana na miti hiyo?

A: Miti yenye majani ya kijani B: Miti inayoota jangwani C: Miti inayorutubisha udongo D: Miti aina ya monokotiledoni E: Miti isiyotoa maua [     ]

ii. Julius alitufundisha kwamba, reptilia, amfibia na ndege hutaga mayai wakati mamalia huzaa. Je, nini tofauti kati ya vyura wa Kihansi na vyura wengine?

A: Wana damu baridi B: Wana rangi ya kijani C: Hutaga yai moja D: Hukaa majini tu E: Huzaa kama mamalia [     ]

iii. Agness alichimba shimo kwenye kiazi kisha akajaza chumvi kwenye shimo hilo na akakiweka kwenye beseni yenye maji. Je, alikuwa anafanya jaribio gani?

A: Kuyeyusha chumvi B: Uwepo wa protini C: Osmosisi D: Difyusheni E: Uwezo wa chumvi kunyonya maji [     ]

iv. Mimea imegawanyika katika makundi makuu mawili. Mimea inayotoa maua na mimea isiyotoa maua. Mimea isiyotoa maua ina njia mbalimbali za kuzaliana. Je, ni mmea upi unaweza kuzaliana pasipo kutoa maua?

A: Nyasi B: Mnazi C: Haragwe D: Mpapai E: Pumpkin [     ]

v. Mkondo wa umeme unaopita katika sakiti ni ampia 4. Tafuta ukinzani kama volteji ni 24.

A: Ohm 6 B: Ampia 4 C: Ohm 4 D: Ohm 96 E: Ohm 2 [     ]

vi. Mji wa Kimanga una watu wengi sana hivyo umeme hautoshi kwa kuwa hutumiwa na watu wengi unapowashwa. James ambaye ni mhandisi katika fizikia aliwashauri wakazi wa mji huo kutumia kifaa kinachoongeza volteji ili kukabiliana na tatizo hilo. Je, kifaa hicho ni kipi?

A: Amita B: Galvanomita C: Inveta D: Transfoma E: Paneli ya jua [     ]

vii. Mashine tata huundwa na mashine rahisi nyingi ili ziwe na ufanisi wa kurahisisha kazi zaidi. Je, ni aina gani ya mashine rahisi kati ya hizi huunda baskeli?

A: Gurudumu kapi na ekseli, nyenzo na breki B: Nyenzo, skrubu na pedali C: Gurudumu kapi, nyenzo na roda D: Gurudumu, mnyororo na pedali E: Wenzo, mnyororo na gurudumu [     ]

viii. Wakati wa uchimbaji wa madini, viongozi waliwalazimisha wachimbaji kutumia taa zinazosambaza mwanga ili waweze kuona eneo kubwa. Je, taa hizo zinatumia aina gani ya vioo?

A: Vioo bapa B: Vioo mbonyeo na mbinuko C: Vioo mbonyeo D: Vioo mviringo E: Vioo duara dufu [     ]

ix. Kuna aina mbili za mkondo wa umeme, mkondo geu na mkondo mnyoofu kutokana na aina ya chanzo cha umeme kilichotumika. Tumia ujuzi wako kubaini kundi lenye vyanzo vya mkondo mnyoofu pekee.

A: Dainamo, paneli ya jua na seli kavu. B: Betri ya gari, paneli ya jua na seli kavu C: Paneli ya jua, dainamo na umeme wa kidatu D: Betri ya gari, jenereta na jotoardhi. E: Seli kavu, mota ya redio na umeme wa kidatu [     ]

x. Tumia ujuzi uliopata darasani kuhusu tabia za tindikali na nyongo kubaini maada yenye nyongo.

A: Limau B: Sabuni C: Siki D: Dawa ya kuua wadudu E: Mkojo [     ]

2. Oanisha kifungu A na kifungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku cha majibu.

KIFUNGU A
KIFUNGU B

i. Chakula kinachotakiwa kwa wingi na wafanyakazi wakati wa kazi ngumu za mikono.

ii. Aina ya chakula kinachojenga mwili

iii. Chakula kinachoongeza joto mwilini

iv. Chakula kinachotakiwa kwa wingi na wafanyakazi wa ofisini

v. Chakula kinachojenga meno na mifupa

A. Mafuta

B. Wanga

C. Vitamini

D. Madini

E. Protini

Kifungua A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
Kifungu B





3. Chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku kisha ulijaze kwenye nafasi wazi.

Kifua kikuu, Hemofilia, Kifaduro, Ebola, Surua, UKMWI

i. Ugonjwa wenye sifa ya mgonjwa kutokwa na damu nyingi akipata jeraha . . . . . . . . . .
ii. Ugonjwa unaoshambulia mapafu na kusababisha mgonjwa kushindwa kupumua vizuri . . . . . ..
iii. Ugonjwa unaoambukiza kwa njia ya damu kugusana pekee . . . . . . . . . . . . . . .. .
iv. Ugonjwa unaomfanya mgonjwa kutokwa na damu masikioni, puani na machoni . . . .. . . . .
v. Ugonjwa unaosababisha vipele kwenye ngozi . . . . . . . . . . .

SEHEMU B (Alama 20)

Majibu mafupi

4. i. Bibi yangu alipougua alipelekwa hospitali, kabla ya kupima damu alipimwa joto la mwili na mapigo ya moyo. Je, ni kifaa gani kilitumika kupima joto la mwili . . . . . . . . . . . . . . .
ii. Fatuma alifanya jaribio kuhusu osmosisi akagundua kuwa dhanio lake halikuwa sahihi. Je, ni katika hatua gani ya jaribio alitupilia mbali dhanio? . . . . . . . . .. . . .
iii. Watumiaji wa mtandao wa intaneti hutumia vifupisho kama GPS,www, MJA na MTAPA. Nini kirefu cha MTAPA? . . . . . . . . . . . . . . ..

5. i. Kisayansi kazi hufanyika kama kani imesogeza mzigo umbali fulani. Mariamu alisukuma mzigo fulani umbali fulani. Andika kizio kilichotumika kufafanua kani hiyo? . . . . . . . . . . . .
ii. Taka lazima zidhibitiwe katika mazingira ili kuepuka madhara yatokanayo na mlundikano wa taka. Je, taka kama vile vipande vya chuma huhifadhiwa katika chombo cha rangi gani? . . . . . . ..
iii. Mbu ni wadudu hatari sana, husambaza ugonjwa unaoua mamilioni ya watu duniani kote. Je, ni hatua ipi ya ukuaji wa mbu inayofaa zaidi kuwaangamiza ili kuwepo na mafanikio makubwa . . . . . . . .. . .. . . .

6. i. Magonjwa ya kurithi husambaa kutoka kizazi kizazikimoja hadi kingine kwa kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi, Je, ni ugonjwa gani wa kurithi una uhusiano na ukosefu wa vitamini K? . . . . ..
ii. Wanyama huhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kupata mahitaji katika mazingira. Je, ni mnyama gani husaidiwa na mwangwi kujongea . . . . . . . . . . . . . . . . . ...
iii. Sikio ni ogani ya fahamu ambayo kazi zake kuu ni kusikia na kuweka mwili katika msawazo. Je, ni sehemu gani ya sikio hunasa mawimbi ya sauti? ........................................
iv. Mfumo wa mzunguko wa damu umeundwa na moyo, damu na mishipa ya damu. Kuna aina kuu tatu za mishipa ya damu ambazo ni vena, ateri na kapilari. Vena zote husafirisha damu yenye kabondayoksaidi ISIPOKUWA ..............................................................

SEHEMU C (Alama 10)

7. Jibu kulingana na swali uliloulizwa.

i. Rhoda alitumia roda ifuatayo kurahisisha kazi. Tafuta manufaa ya kimakanika ya roda hiyo. . . . .


ii. Je, hii ni aina gani ya roda? . . . . . . . . . . . . . . . .
iii. Je, nini matumizi ya roda katika mazingira ya kila siku? . . . . . . . . . . ...
8. i. Chunguza kielelezo kifuatacho kisha tafuta thamani ya pembe E . . . . . . . . . . . ..


ii. Je, kielelezo hiki kinawakilisha nini? . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 37  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 37  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA FEBRUARI 2024 

SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:40

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu mbili: A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A

Kwa swali la 1 – 40, chagua jibu sahihi kisha siliba herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Mwalimu alitufundisha kuwa, ua la mmea lina sehemu za kiume na sehemu za kike. Tumia ujuji ulionao kubaini sehemu mojawapo inayounda sehemu ya kike ya ua.

A: Filamenti B: Chavulio C: Petali D: Staili E: Sepali

2. Magonjwa yanaweza kuwekwa katika makundi kwa kuzingatia visababishi na njia za uenezaji za magonjwa hayo. Je, ni ugonjwa upi hausababishwi na vimelea vya magonjwa kati ya magonjwa haya?

A: Polio B: Kiseyeye C: Kipindupindu D: Mafua E: Uti wa mgongo

3. Mimea inahitaji mahitaji muhimu kama vile hewa, madini, maji, mwanga wa jua na mengineyo ili iishi. Kwa kutumia ujuzi ulionao kuhusu virutubisho, ni kirutubisho kipi ni kirutubisho kikuu kati ya hivi?

A: Chuma B:Salfa C: Nikeli D: Haidrogeni E:Potasi

4. Utoajitaka ni moja kati ya sifa saba za viumbe hai. Ni kiungo gani kinahusika na kuchuja damu?

A: Pafu B: Moyo C: Figo D: Urethira E: Kibofu cha mkojo

5. Binadamu ni moja kati ya wanyama ambao joto lao halibadiliki. Ikiwa Musa alitumia kipimajoto kumpima mgonjwa, je aliandika kizio gani katika kumbukumbu?

A:C B:F C: oT D: oF E: Co

6. Ni dhahiri kuwa mtu huumwa ugonjwa wa kisukari kama kiungo kinachodhibiti sukari hakifanyi kazi kwa usahihi. Je, kiungo hicho ni kipi?

A:Figo B: Ini C: Moyo D: Kongosho E: Utumbo

7. Kwa kawaida damu hupata oksijeni katika mapafu. Je, ni mshipa upi husafirisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye mapafu hadi kwenye atriamu ya kushoto?

A: Ateri ya palmonari B: Vena ya palmonari C: Vena kuu D: Aota E: Mshipa wa palmonari

8. Kama unafahamu vema sifa za mamalia, baini sifa isiyo sahihi kuhusu mamalia.

A: Halijoto la mwili haibadiliki B: Hunyonyesha C: Huzaa D: Wana damu baridi E: Hula

9. Mwalimu alitufundisha kuwa electroni husafiri katika sumaku ya mche kwa kufuata uelekeo maalumu. Je, ni uelekeo gani ni sahihi kuhusu taarifa hiyo?

A: KAS kuelekea KUS B: KUS kuelekea KAS C: Mashariki kuelekea Magharibi D: Magharibi kuelekea KAS E: KAS kuelekea Mashariki

10. Kisayansi KAZI hufanyika kama kani fulani imesukuma kitu fulani katika umbali fulani. Ikiwa Neema alifanya kazi ya joule 60 baada ya kusogeza jiwe lenye uzito wa kg 1. Je, alilisogeza umbali gani katika mita?

A: 1 B:60 C: 10 D: 0.5 E: 6

11. Kulingana na ujuzi ulionao kuhusu tarakilishi na kazi zake muhimu inazofanya. Je, tarakilishi ina aina kuu ngapi za programu?

A: 2 B: 3 C:4 D:5 E:6

12. Ni aina gani ya kitumi cha tarakilishi kimewakilishwa na mchoro ufuatao?

A: Kitumi ingizi B: Kitumi kipanya C: Kitumi cha kubofya D: Kitumi cha kielektroniki E: Kitumi ingizi

13. Kamau alitumia kipima umeme kupima waya wa umeme na akaandika jibu kama 5Ώ. Je alipima nini?

A: Mkondo wa umeme B: Volteji C: Ukinzani D: Umeme E: Mwendo wa umeme

14. Ni kifaa kinacholinda vifaa vya umeme kwa KUYEYUKA volteji inapozidi. Je, unadhani kifaa hicho ni kifaa gani?

A: Fyuzi B: Taa C: Kikingaradi D: Seli E: Kikata sakiti

15. Damu huzunguka katika mwili kwa msaada wa moyo unaoisukuma kwenda sehemu zote za mwili. Je, moyo una vali ngapi?

A: 4 B: 2 C: 5 D: 3 E: 5

16. Je, ni sifa ipi kati ya sifa zifuatazo siyo sifa ya mmea unaostahimili ukame?

A: Kuwa na majani makubwa B: Kuwa na mizizi mirefu C: Kupukutisha majani D: Kuwa na majani membamba E: Kuwa na shina nene.

17. Kwa kawaida urutubishwaji hufanyika katia mirija ya falopio katika mamalia. Je, urutubishwaji hufanyika katika sehemu gani ya ua?

A: Staili B: Stigma C: Stameni D: Filamenti E: Ovari

18. Ikiwa Mashaka atakula mayai na maharage, je matokeo ya chakula hicho yatakuwa nini baada ya mmeng`enyo?

A: Glukozi B: Asidi za fati C: Asidi za amino D: Proteni E: Chakula kimiminika

19. Lucy kwa bahati mbaya alipoteza sindano yake katika mchanga. Je, ni njia ipi inaweza kuwa rahisi sana kupata sindano hiyo?

A: Kutumia watu wengi kuitafuta B: Kutumia sumaku C: Kutumia ufagio D: Kutumia tochi E: Kuiokota

20. Hewa imeundwa na gesi mbalmbali. Baadhi ya gesi ni muhimu katika maisha yetu. Haruna anafanya kazi katika maabara ya hospitali ya taifa, anatunza seli za binadamu, damu na tishu hai zinazotumiwa
na wagonjwa. Je, ni gesi gani anayotumia katika kazi yake?

A: Haidrojeni B: Naitrojeni C: Kabondayoksaidi D: Oksijeni E: Agoni

21. Kupumua ni moja kati ya sifa za viumbe hai. Je, ni sehemu gani ya samaki hutumika kupumua?

A: Opekyulamu B: Pezi C: Matamvua D: Pua E: Ngozi

22. Mimea hupoteza maji katika hali ya mvuke inapopumua. Je, kitendo hicho kinajulikanaje kisayansi?

A: Translokesheni B: Evaporesheni C: Usafirishaji D: Transpiresheni E: Transfyusheni

23. Katika nchi zilizoendelea, mawimbi ya maji hutumika kuzalisha umeme kama mkondo wa maji unavyotumika. Je, nini chanzo cha mawimbi ya maji baharini?

A: Joto B: Baridi C: Mtetemo wa vyombo vya majini D: Kujaa na kupwaa kwa maji E: Mabadiliko ya hali ya hewa

24. Umefundishwa alama za usalama nyingi zinazotumika katika mazingira kuelekeza njia bora vitu na miundombinu vinavyoweza kutumika. Ikiwa Makani aliona alama ya pembe tatu yenye alama ya msongo mkubwa wa umeme, unadhani ilikuwa na rangi gani?

A: Njano B: Bluu C: ijani D: Nyekundu E: Nyeupe

25. Je, ni mdudu gani kati ya hawa wafuatao anafuata metamofosisi kamili?

A: Panzi B: Mchwa C: Mbu D: Mende E: Jongoo

26. Nishati jadidifu ni rafiki kwa mazingira. Ni chanzo kipi si chanzo cha nishati jadidifu kati ya hivi?

A: Maji B: Jua C: Makaa ya mawe D: Gesivunde E: Jotoardhi

27. Tedy alitumia mikono yake kuinua vitabu vitatu hewani. Je, alitumia nyenzo daraja la ngapi kufanya kazi hiyo?

A: La pili B: La tatu C: La kwanza D: La nne E: La tano

28. Programu jedwali ni programu ya tarakilishi inayotumika kukokotoa mahesabu. Je, ni data ipi haiwezi kuandikwa na programu hiyo?

A: Matini B: Number ya kirumi C: Namba nzima D: Alama ya kujumlisha E: Namba kipeo

29. Mtu anayeharisha hupoteza maji mengi, virutubisho na nishati. Inashauriwa apewe mchanganyiko wa maji, sukari na chumvi. Je, ni kipi si sababu ya kumpa huduma hiyo ya kwanza?

A: Kurudisha maji yaliyopotea B: Kuokoa maisha yake C: Kurudisha virutubisho D: Kurudisha joto E: Kuupa mwili nguvu

30. Watu wanaovuta sigara wako katika hatari ya kuumwa saratani ya mapafu. Je, kitu gani kwenye sigara kinachosababisha madhara mwilini?

A: Kokeini B: Rami C: Kafeini D: Nikotini E: Sumu

31. Watu wawili wa familia moja wanaweza kuwa na ngozi zenye rangi tofauti. Hii inaonyesha kuwa wana homoni inayosababisha rangi. Je, hiyo homoni inaitwaje?

A: Ualubino B: Adrenalaini C: Testosteroni D: Projesteroni E: Melanini

32. Je, ni kifaa gani hutumia zebaki kufanya kazi?

A: Kipimajoto B: Mizani C: Saa D: Hadubini E: Barometa

33. Umefundishwa gesi mbalimbali zinazounda hewa katika tabaka la hewa. Je, ni hewa ipi huchukua 78% ya hewa yote?

A: Kabondayoksaidi B :Oksijeni C: Agoni D:Neoni E: Naitrojeni

34. Tausi alitaka kulima mahindi katika eneo la Katubuka lakini alishauriwa na mtaalamu wa kilimo kuwa angetumia mbolea nyingi ili apate mazao. Je, kuna aina gani ya udongo Katubuka?

A: Kichanga B: Tifutifu C: Mfinyanzi D: Tifutifu na mfinyanzi E: Mchanga na mfinyanzi

35. Jiwe lenye gramu 60 lilizamishwa katika maji yenye ukubwa wa sm3 80 katika beseni. Baada ya kulizamisha ukubwa uliongezeka na kuwa sm3 100. Je, nini ilikuwa densiti ya jiwe hilo?

A: g/sm3 60 B: g/sm3 80 C: g/sm3 3 D: g/sm3 30 E: g/sm3 1

36. Katumbi ni mfanyakazi ambaye kazi yake ni kufyeka majani katika mazingira yetu ya shule. Je, mashine anayotumia kufyeka majani ni nyenzo daraja la ngapi?

A: La kwanza B: La pili C: La tatu D: La nne E: La tano

37. Bakari alizamisha karatasi ya litmasi nyekundu katika kimiminika fulani kisha ikabadilika rangi na kuwa bluu. Unadhani hicho kimiminika kilikuwa kitu gani?

A: Damu B: Juisi ya maembe C: Maji yenye majivu D: Maji ya maganda ya chungwa E: Maji ya betri

38. Urutubishaji ni moja kati ya vitendo muhimu katika kutungwa kwa mimba. Je, kitendo hicho hufanyika katika sehemu gani katika mfumo wa uzazi wa mwanamke?

A: Ovari B: Uterasi C: Mirija ya falopio D: Uke E: Shingo ya kizazi

39. Anemia ni mmoja kati ya magonjwa hatari yanayoua watoto chini ya miaka mitano. Je, ni madini gani yakikosekana mwilini hupelekea kuugua ugonjwa huo?

A: Potasiamu B: Ayodini C: Kalsiamu D: Chuma E: Fosforasi

40. David ana umri wa miaka thelathini. Anafanya kazi shambani kwake masaa matano kila siku. Je, ni chakula gani kinamfaa kutokana na kazi yake?

A: Vitamini B: Mafuta C: Wanga D: Protini E: Ugali

SEHEMU B: (Alama 10)

Kwa swali la 41 – 45, andika majibu katika nafasi uliyopewa kwenye karatasi ya kujibia (OMR) kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.

41. Rehema ana kibanda kikubwa Karume. Aliajiri wanaume saba wanofanya kazi katika kibanda chake kunyoa nywele. Je, ni aina gani ya kioo hutumika katika kibanda hicho? . . . . . . . . .

42. Kwa kifupi, eleza KANUNI YA KUELEA . . . . . . . . ..

43. Moto ni muhimu katika maisha ya kila siku lakini unaweza kusababisha ajali usipotumiwa kwa uangalifu. Je, ni daraja gani la moto huongeza athari ukizimwa kwa kutumia maji?....................

44. Kinzani mbili zenye ohm 2 kila moja zimepangwa katika sakiti sambamba yenye Ampia 2. Tafuta volteji. . . . . . . . . ..

45. Andika makundi mawil ya wanyama wenye uti wa mgongoambao jotoridi hubadilika. . . . . . .

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 32  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 32  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

MTIHANI WA KUJIANDAA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023

SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA DARASA: VII 

MUDA: SAA 1:30   

 SEHEMU A: 

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa

1. Chakula ni moja ya hitaji la msingi sana la viumbe hai. Lipi kati ya yafuatayo siyo umuhimu wa chakula kwa binadamu? ___ 

A. Husaidia kukua B. husaidia kujikinga na magonjwa C. hutupatia nguvu D. hutupatia joto mwilini E. hutupatia watoto [     ]

2. Takamwili zote zitolewazo na viumbe hai hupatikana katika hali za maada zifuatazo _____

A. gesi na vimiminika B. yabisi, gasi na kimiminika C. vimiminika na yabisi D. gesi na yabisi E. kimiminika tu [     ]

3. Samaki ni viumbe waishio majini ambao wana ute kiini juu ya miili yao. Kazi ya ute huu ni: ____ 

A. huwasaidia kupumua B. huwasaidia kuona C. huwasaidia kupunguza ukinzani wanapoogelea D. huwasaidia kupata kona E. huwasaidia kuhisi miguso [     ]

4. Ni mamalia yupi hana tezi za jasho? ___ 

A. ng’ombe B. mbwa C. binadamu D. popo E. nyangumi [     ]

5. Zifuatazo ni sifa za taswira katika kiioo mbinuko isipokuwa: ______ A. taswira ni ndogo ukilinganisha na kiolwa B. taswira kuwa wima C. taswira kutokea nyuma ya kioo

D. taswira hugeuza upande wa kulia kuwa upande wa kishoto E. taswira hugeuzwa juu chini [     ]

6. Kitendo cha mmea kupoteza maji kwa njia ya mvuke kupitia kwenye majani huitwa ______

A. usanishaji B. fotosinthensisi C. transilokesheni D. uyeyushaji E. transipiresheni [     ]

7. Ngamia ni mnyama ambaye anauwezo wa kuishi sehemu kame sana ni kitu gani kina msaidia kumudu kuishi sehemu kame? _____ 

A. kwato B. tumbo C. kichwa D. nundu E. shingo [     ]

8. Zifuatazi ni sifa za taswira ya kioo bapa isipokuwa? ___

  1. taswira kuiwa wima 
  2. aswira kutokea mbele ya kioo bapa 
  3. taswira kutokea nyuma ya kio bapa 
  4. ukubwa wa taswira ni sawa unakubwa wa kiolwa 
  5. umbali wa kiolwa kutoka kwenye kioo ni sawa na taswira kutoka kwenye kioo na taswira hugeuzwa upande wa kiolwa kuwa upande wa kushoto wa kiolwa [     ]

9. Mimea inayozaliana kwa kutegemea gameti uke na gameti ume lazima: ________ 

A. iwe mifupi B. iwe mirefu C. ipaliliwe D. iwe inayotoa maua E. iwe isiyotoa maua [     ]

10. Saitimila za magari hutengenezwa kwa kutumia _______

A. vioo mbonyeo B. vioo bapa C. vioo mbinuko D. Lenzi mbonyeo E. lenzi mbinuko [     ]

11. Zifuatazo ni njia mbalimbali zitumiwazo na mimea kudhibiti upotevu wa maji isipokuwa: ______ 

A. kupukutisha majani B. unene na unyororo wa majani C. ukubwa wa majani na unene wa shina D. kunyooka kwa majani E. kukauka kwa shina [     ]

12. Ni seti ya mimea ambayo huzaliana kwa kutumia machipukizi: _____ 

A. viazi mviringo B. karanga na maharage C. mkonge na migomba D. mihogo na viazi vitamu E. miwa na mihogo

13. Gamba gumu katika kichwa cha samaki ambalo hufunika matamvua huitwa: _______ 

A. mapezi B. matamvua C. mabawa D. opekyulamu E. mstari wa neva [     ]

14. Selemani ni mlinzi wa duka la mzee Sultani ni kifaa gani kinamwezesha kumsaidia katika kazi yake ya ulinzi kati ya hivi? _____ 

A. kioo mbonyeo B. lenzi mbonyeo C. lenzi mbinuko D. kioo mbinuko E. kioo bapa [     ]

15. Mirija ambayo huunganisha 0vari na uterasi huitwa: _____ 

A. mirija ya manii B. zaigoti C. mirija ya falopia D. urethira E. ureta [     ]

16. Mashine ya kielektroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadshi taarifa na kutoa matokea ya kazi kwa haraka kulingana na maelezo ni: ______

A. ngoma B. gari C. cherehani D. jenereta au kangavuka E. tarakilishi au kompyuta [     ]

17. Tarakilishi ina kazi kuu nne za msingi ambazo ni hizi zifuatazo isipokuwa: ____

A. kuingiza na kupokea data au taarifa B. kuchakata data au taarifa mbalimbali C. kuhifadhia data au taarifa D. kutoa au kuonesha matokeo ya kazi au taarifa E. kutengeneza mitambo mbalimbali [     ]

18. Sehemu yakinifu za tarakilishi zinazoshikika na zinazoonekana kama kiteuzi, monita, kipaza sauti, kichakato kikuu na printa huitwa: ____ 

A. program B. kashamfumo C. kichakatokikuu D. maunzi E. kingavirusi [     ]

19. Ni kiumbe yupi kati ya wafuatao huweza kujitengenezea chakula chake? ______ 

A. binadamu B. kuku C. ng’ombe D. mmea E. uyoga [     ]

20. Ni pea ipi ya makundi ya wanyama ni homeothemia ______ 

A. samaki na ndege B. amfibia na reptilia C. mamalia na samaki D. ndege na amfibia E. ndege na mamamlia [     ]

21. Stomata ni vitundu vidogovidogo vilivyopo kwenye jani la mmea ambavyo hutumiwa na mimea kupumua vitundu hivyo hupatikana katika sehemu ipi ya jani? _______

A. epidemisi ya juu B. seli safu za kati C. vifereji pitishi D. epidemisi ya chini E. nafasi ya hewa [     ]

22. Mrija mwembamba unaosafirisha chavua au poleni kutoka kwenye stigima kwenda kwenye ovari unaitwa: ____

A. ovuli B. sepali C. kikonyo D. filament E. staili [     ]

23. Ni mdudu yupi hupitia metamofisisi pungufu? ____ 

A. mbu B. mende C. kipepeo D. nyuki E. nzi [     ]

24. Kitu kipi kati ya vifuatavyo kina umbo maalumu? _____

A. soda B. hewa ya oksijeni C. maji D. kipange cha chuma E. hewa ya kabonidayoksaidi [     ]

25. Mwalimu mkuu amenunua tarakilishi ambayo vifaa vyake vyote ikiwemo kibodi, kiteuzi na monita vimeunganishwa ndani ili kurahisissha ubebaji na matumizi mahali popote. Je, hii ni aina gani ya tarakilishi? _____

A. tarakilishi ya mezani B. tarakilishi mfumo C. tarakilishi mpakato D. tarakilishi kuu E. tarakilishi endeshi [     ]

26. Kama mwalimu atakuomba uende ukazime tarakilishi ya mezani iliyopo ofisini ni sehemu ipi utaanza kuzima?____

A. swichi ya ukutani B. kebo ya umeme C. skrini D. kidhibiti umeme E. kasha mfumo [     ]

27. Sumaku huweza kutumika katika maeneo yafuatayo isipokuwa:________ 

A. kunyanyua na kutenganisha vtu B. kutengenezaa kengerele ya umeme C. kutengeneza dira D. kuzalisha umeme E. kukata vioo [     ]

28. ______ ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vya tarakilishi vifanye kazi na kutoa matokeo kulingana na maelekezo. 

A. Programu B. Paunzi C. Kiteuzi na kibodi D. Kiteuzi na skrini E. Kingavirusi [     ]

29. Elimu ya uhusiano wa viumbe hai na mazingira inajulikana kama _____ 

A. Biolojia B. Mazingira C. Ikolojia D. Metamofosisi E. Bioanuai [     ]

30. Kitu chochote kinachotumika kurahisisha kazi huitwa _______

A. Tarakilishi B. nishati C. mashine D. umeme E. kazi [     ]

31. Wafuatao ni mawakala wa uchavushaji isipokuwa ______

A. wadudu B. upepo C. ndge D. maji E. mwanga [     ]

32. Vifuatavyo ni vitu ambavyo huunda sakiti ya umeme isipokuwa: ________

A. kipitisha umeme B. kikinza umeme C. swichi D. chanzo E. nguzo ya umeme [     ]

33. Usanishaji wa chakula hufanyika katika sehemu ipi ya jani? _____

A. ncha B. kingo C. mishipa jani D. lamina E. kikonyo [     ]

34. Ni kitendo kipi kati ya vifuatavyo ni badiliko la kiumbo? _____ 

A. chuma kupata kutu B. kuungua kwa nta C. Maziwa kuganda D. kuungua kwa karatasi E. majani kuoza [     ]

35. Mamalia hutumia ogani ipi kupumua? ______

A. pua B. ngozi C. mdomo D. mapafu E. moyo [     ]

36. Mtiririko wa elekroni au chaji hasi kwenye kipitishio kutoka kwenye chanzo hadi kitumia umeme huitwa: ___ 

A. waya B. nishati C. sakiti D. kikinza E. umeme [     ]

37. Sehemu ya ua ambayo ikikomaa huwa tunda huitwa ________ 

A.ovuli B. stigma C. petali D. ovari E. stameni [     ]

38. Mtandao janibu ni aina ya mtandao ambao huunganisha tarakilishi: _____ 

A. katika eneo kubwa la kijografia B. zote duniani C. katika eneo dogo la kijografia D. na printa E. Na ruta [     ]

39. Zikitumika mashine rahisi zaidi ya moja kuunda mashine moja mashine hiyo huitwa: ______ 

A. roda tuli B. mashine mchanganyiko C. mashine tata D. nyenzo E. muunganiko [     ]

40. Mche wa sumaku wenye ncha ya KUS na KAS ukining’inizwa hewani ncha ya KAS itaelekea upande gani wa dunia?_ 

A. Kusini B. Mashariki C. Magharibi D. Kaskazini E. Uelekeo wa jua [     ]

SEHEMU B: Jaza nafasi wazi

41. Hewa iliyo katika mwendo huitwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

42. Kitendo cha mimea ya kijani kujitengenezea chakula chake huitwa: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

43. Mojawapo ya sehemu tatu za wenzo ni mzigo. Taja zingine mbili: i . . . . . . . . .. . . . .. ii. . . . . . . . . . ...

44. Nini kinatokea katika mchoro huo hapo chini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

45. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu kipengele i na ii


i. Hii ni aina gani ya sakiti?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

ii. Ikiwashwa swichi C nini kitatokea kwa glopu namba 2 endapo glopu namba 1 itaungua?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 24  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 24  

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA SAYANSI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
  4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
  5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
  6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

  1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
  2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
  3. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: (Alama 40)

Kwa swali 1-40, tafuta majibu kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya OMR uliyopewa.

1. Mwalimu aliwaambia wanafunzi wa darasa la saba kuwa baadhi ya vyombo vya usafiri wa majini vinaweza kuzama au kuelea kama nahodha ameamua kufanya hivyo. Unadhani ni sababu gani huviwezesha kufanya hivyo?

A: Vinabadilisha maumbo B: Manahodha wana mafunzo ya kutosha C: Densiti hubadilika kutegemea aina ya maji D: Mwendokasi huviwezesha kufanya hivyo E: Vina matanki ambayo hujazwa maji au hewa [       ]

2. Yona alipanda mmea chumbani, mmea ulipoota alishangaa kuona majani yake yanaelekea dirishani kadiri ulivyozidi kukua. Je, kitendo hicho kinaitwaje kisayansi?

A: Haidropizimu B: Fototropizimu C: Kemotropizimu D: Jeotropizimu E: Tropizimu [       ]

3. Mwalimu aliwafundisha wanafunzi wake kuwa baadhi ya wadudu hufuata hatua nne za ukuaji. Jeni alipouliza kama wadudu wote hufuata hatua nne za ukuaji, mwalimu aliwapa kazi ya kufanya utafiti wa kujua ni wadudu gani hawafuati hizo hatua. Kama ungekuwa mwalimu ungemjibu nini Jeni?

A: Kipepeo–Nzi-Panzi B: Senene-panzi-mchwa C: Mchwa-kereng’ende-panzi D: Nyigu-kereng’ende-kipepeo E: Nzige-senene-panzi [       ]

4. Jerome ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba aliambiwa apange makundi ya alama za usalama kwa usahihi. Je, alama ifuatayo ilipangwa katika kundi gani?


A: Alama ya amri B: Alama ya kukataza C: Alama ya dharura D: Alama ya tahadhari E: Alama ya hatari [       ]

5. Msukumo wa mkondo wa umeme katika sakiti ni volti 6. Je ni kiasi gani cha mkondo wa wa umeme huzalishwa ikiwa kinzani ni ohm 0.5?

A: Ampia 3 B: Ampia 12 C: Ampia 0.6 D: Ampia 0.025 E: Ampia 25 [       ]

6. Ukiambiwa na mama yako uandike kanuni ya kutafuta ukinzani, lipi kati ya majibu yafuatayo litakuwa jibu lako?

A: V=I/R B: I=VxR C: R=V/I D: V=I/R E: V=IxR [       ]

7. Selemani ni mwanaume tajiri anayeishi Kilwa ambaye anataka kulinda nyumba mpya isipigwe na radi. Je, atalazimika kununua kitu gani kati ya vifuatavyo ili akiunganishe na waya wa Ethi?

A: Mtaimbo wa chuma B: Mtaimbo wa shaba C: Madini ya Zinki D: Mtambo wa Aluminum E: Mtaimbo wa zebaki [       ]

8. Kombe aliambiwa na baba yake kuorodhesha vyanzo vya nishati mbadala. Kama mojawapo ya vyanzo alivyooorodhesha hakikuwa sahihi, chanzo hicho ni kipi??

A: Mkondo wa maji B: Paneli ya jua C: Makaa ya mawe D: Umeme wa Kidatu E: Upepo [       ]

9. Wakati wa ujenzi wa barabara, mzigo wa nyutoni 100 uliinuliwa kwa kutumia jitihada ya kilogramu 5 kwa umbali wa mita 8. Je, mashine hiyo ilikuwa na ufanisi kiasi gani?

A: 50% B: 75% C: 0.5% D: 100% E: 200% [       ]

10. Wafanyakazi watano waliulizwa na mwanafunzi swali kama ifuatatvyo: ‘Ni nani kati yenu kazi yake inahusisha badiliko la kikemikali? Unadhani ni nani alitoa jibu sahihi?

A: Mwashi B: Fundi cherehani C: Mpishi D: Fundi bomba E: Mkata vioo [       ]

11. Tulipokuwa tunajifunza hali za maada, tuligundua kuwa mabadiliko ya hali za maada hutegemea mabadiliko ya joto katika mazingira husika. Je, ni badiliko gani hutegemea ongezeko la joto katika maji?

A: Kuganda kwa maji B: Kubadili mvuke kuwa maji C: Utangaenezaji wa mvua kwenye mawingu D: Uvukizaji E: Kutengeneza barafu [       ]

12. Wakati wa shughuli za kila siku za shule, Asha alikuwa anasoma kitabu cha sayansi na tekinolojia kuhusu vyanzo vya nishati vinavyotumia tabaini kuzalisha umeme. Ni chanzo kipi hakikusomwa na Asha?

A: Umeme wa Kidatu B: Paneli ya jua C: Joto ardhi D: Uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo E: Jenereta ya mafuta [       ]

13. Mabadiliko ya gesi hufanyika katika mapafu wakati wa upumuaji wa wanyama ambapo Oksijeni huingia na hewa ya ukaa hutoka nje. Ni kipi kati ya vifuatavyo huwezesha hewa ya ukaa kutoka nje?

A: Osmosisi B: Usambaaji C: Uenezaji D: Uvukizaji E: Tropizimu [       ]

14. Robina alisukuma mkokoteni umbali wa sentimeta 500. Kama kazi aliyoifanya ilikuwa joule 100, atakuwa ametumia kani ngapi katika kukamilisha zoezi lote?

A: N 0.2 B: Kg 20 C: N 20 D: N 500 E:N 50000 [       ]

15. Baraka alitakiwa na mtaalam wa elimu ya mawasiliano aandike jina linalojumuisha mikeka kazi. Unadhani alijibu nini kati ya machaguo haya?

A: Kitabu kazi B: Seli C: Ekseli D: Programu jedwali E: Mkusanyiko wa mikeka [       ]

16. Muunganiko wa safu wima na safu mlalo katika programu jedwali huitwaje?

A: Kitufe B: Kiteuzi C: Seli D: Kanuni E: Kiolesura [       ]

17. Doto ana shule ya msingi nchini Kanada na rafiki yake Collins ana shule ya sekondari nchini Uingereza. Ikiwa watu hawa huwasiliana kwa kutumia simu ili kupeana uzoefu wa kuendesha shule, ni aina gani ya mtandao watatakiwa kutumia ili kurahisisha mawasiliano?

A: MJA B: Mtandao wa nchi C: Mtandao wa simu D: Mtandao wa tarakilishi E: MTAPA [       ]

18. Ignas amechoka sana kwa sababu amekuwa akichapa kwa kutumia tarakilishi kwa muda wa saa tano. Je, ni hatua gani itakuwa ya kwanza katika kuzima tarakilishi hiyo?

A: Kubofya paumenyu B: Bonyeza kitufe cha kuanzia C: Bonyeza Microsoft word D: Bofya Microsoft Excel E: Bonyeza kitufe cha kufungua [       ]

19. Mwalimu alifundisha vitu vingi kuhusu marekebisho ya data. Alisema kuwa kurekebisha data inahusisha kuzibadili kwa jinsi mhusika anavyotoka na anaweza kutoa au kuongeza vitu anavyohitaji katika data hizo. Ni njia ipi itatumika kutunza data?

A: Kuhifadhi B: Kupigia mistari C: Kuongeza ukubwa wa maandishi D: Kukoleza maandishi E: Kuzalisha vitini [       ]

20. Rehema ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano alimuuliza baba yake ni sehemu gani ya tarakilishi huonesha picha?

A: Spika B: Kicharazio C: Kiteuzi D: CPU E: Skrini [       ]

21. Kuna programu nyingi zinazotumika katika tarakilishi. Endapo Majaliwa atatumia programu jedwali, ataitumia kufanya kazi ipi kati ya zifuatazo?

A: Uchoraji B: Kuandaa matokeo ya mitihani C: Kuandika barua D: Kucheza michezo E: Kuchora picha [       ]

22. Pareto hutumia seli kavu na taa ili kuwasha umeme chumbani kwake. Unafikiri anatumia aina gani ya umeme?

A: Mkondo geu B: Mkondo mnyoofu  C: Mkondo geu na mkondo mnyoofu D: Mkondo wa umeme E: Mkondo wa seli kavu [       ]

23. Kielelezo kifuatacho kinaonesha aina gani ya roda?


A: Roda moja B: Roda huru C: Wenzo tuli D: Roda E: Wenzo huru [       ]

24. Wanaume watano wenye uzito wa kilogramu 70 kila mmoja walisukuma mti mkubwa kwa muda wa saa nne lakini haukusogea. Wanaume hao walichoka na kila mmoja akaenda kwake. Je, walifanya kazi kwa kiasi gani?

A: J4000 B: J4 C: J400 D: Kazi kubwa E:J 0 [       ]

25. Penford aliainisha mashine zifuatazo. Endapo lengo lake lingekuwa ni kuainisha mashine rahisi tu, ni mashine ipi iliainishwa kimakosa?

A: Wenzo B: Nyundo C: Stepla D: Skrubu E: Mtelemko [       ]

26. Rukia ana lenzi ambayo akiielekeza kwenye mwanga , mwanga hutawanyika. Je, unadahani hii ni aina gani ya lenzi?

A: Lenzi mbinuko B: Lenzi mbonyeo C: Lenzi nusu duara D: Lenzi bapa E: Lenzi mviringo [       ]

27. Ukienda hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa mwili, joto, mapigo ya moyo na uzito hupimwa kwanza. Je, kimiminika kilichomo katika mashine ya kupimia joto la mwili kinaitwaje?

A:Maji safi B: Spiriti C: Ayodini D: Zebaki E: Petroli [       ]

28. Lenzi hutumika katika vifaa mbalimbali vinavyotumika na macho katika nyanja mbalimbali katika maisha.Tumia ujuzi ulioupata darasa la tano kubaini kifaa kinachofanya kazi kama jicho la binadamu ?

A: Kamera B: Hadubini C: Darubini D: Periskopu E: Teleskopu [       ]

29. Tulipomwomba mwalimu atutajie faida za kufanya mazoezi ya viungo alieleza faida nyingi sana. Kulingana na ufahamu ulio nao, ipi ni moja kati ya faida alizotaja mwalimu?

A: Kunenepa B: Kujenga misuli C: Kujenga misuli na mifupa D: Kuimarisha meno E: Kuongeza joto la mwili [       ]

30. Malaria ni ugonjwa hatari sana unaoua mamilioni ya watu duniani. Wiki iliyopita Adamu alipelekwa hospitalini na baada ya uchunguzi wa damu daktari aligundua kuwa alikuwa na vimelea vinavyosababisha malaria. Je, ni aina gani ya mbu ilimuuma Adamu?

A: Kuleksi B: Plasmodiamu C: Mbung’o D: Anofelesi E: Mbu wa malaria [       ]

31. Kisumu aliunguzwa na metali ya moto lakini alipata madhara kidogo sana. Je, ni ipi kati ya huduma zifuatazo ilikuwa ni huduma ya kwanza kwake ?

A: Kutumia hewa ya ukaa B: Kummwagia maji ya baridi C: Kutumia blanketi zito D: Kuita Zimamoto E: Kwa kutumia feni [       ]

32. Ni kiungo gani huathirika moja kwa moja na kilevi na kupelekea mlevi kupoteza uwezo wa kuweka mwili katika usawazo?

A: Tumbo B: Figo C: Utumbo D: Ubongo E: Moyo [       ]

33. Wanakijiji wa Dogma hawatumii vyoo bali wanajisaidia porini karibu na nyumba zao za makazi. Je, wanakijiji hawa wanaweza kushambuliwa na ugonjwa gani?

A: Uti wa mgongo B: Kuhara damu C: Saratani D: Hemofilia E: Vidonda vya tumbo [       ]

34. Rupia alishauriwa na tabibu kula vyakula vyenye protini kwa sababu anaonekana kuwa na dalili za unyafuzi. Je, ni chakula gani kati ya hivi kinalandana na ushauri wa daktari?

A: Maziwa B: Asali C: Embe D: Mahindi E: Mchicha [       ]

35. Dawa tunazomeza husharabiwa pamoja na madini katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kisha husafirishwa katika sehemu mbalimbali za mwili. Je, ni seli gani za damu huhusika katika usafirishaji huo?

A: Seli hai nyekundu B: Seli hai nyeupe C: Chembe sahani D: Vakyuli E: Saitoplazimu [       ]

36. Watu wanapaswa kuelimishwa kuhusu njia za kujikinga na magonjwa ili tuwe na taifa lenye afya bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa sababu baadhi ya magonjwa huambukiizwa na mengine hayaambukizi. Je, ni upi kati ya haya siyo ugonjwa wa kuambukiza?

A:Malaria B: Kipindipindu C: Pumu D:Kuhara E: Kisonono [       ]

37. Lofa na Kayeye ni marafiki ambao wanapenda kula chakula kwa pamoja. Jana walikula mayai na karanga. Unadhani mmeng’ enyo wa kikemikali ulianzia katika kiungo gani?

A: Tumbo B: Utumbo mpana C: Mdomo D: Utumbo mwembamba E: Iliamu [       ]

38. Kuzaliana ni kitendo kinachofanywa na viumbe hai wote. Amina alitaja viungo vinavyotumika katika mfumo wa uzazi wa binadamu. Ni kiungo kipi ambacho hakukitaja?

A: Tezi ya Cowper B: Tezi dume C: Plasenta D: Kibofu E: Mirija ya manii [       ]

39. Baada ya mzunguko wa damu mwilini kukamilika, damu huelekea kwenye moyo ili isukumwe kwenda katika viungo vyote vya mwili. Je, ni mshipa upi husafirisha damu toka kwenye mapafu hadi kwenye moyo?

A: Vena kava B: Aota C: Vena ya ini D: Vena ya mapafu E: Ateri ya mapafu [       ]

40. Utungwaji wa mimba ni matokeo ya kukutana kwa gameti ya kiume na gameti ya kiume. Njidi alitakiwa na mwalimu wake wa somo la sayansi kutaja sehemu ambayo gameti hizi hukutana. Unadhani alitoa jibu gani kati ya haya?

A: Ukeni B: Kwenye ovari C: Katika mirija ya falopio D: Katika mji wa mimba E: Katika mlango wa uzazi [       ]

SEHEMU B: (Alama 10)

Andika jibu sahihi kwa kila swali la 41-45 katika nafasi iliyoachwa wazi nyuma ya karatasi ya OMR. Tumia kalamu ya wino mweusi au wa buluu.

 41. Mmeng’enyo wa chakula ni mfumo mmojawapo kati ya mifumo mingine katika mwili wa binadamu. Je, ni sehemu gani katika mfumo huo mmeng’enyo huishia?

42. Ni aina gani ya seli za damu hulinda mwili dhidi ya magonjwa?

43. Daima anataka kubadili mkondo mnyofu wa umeme kuwa mkondo geu. Je, atatumia kifaa gani?

44. Chunguza ua hili kwa makini kisha utaje herufi inayowakilisha sehemu inayopokea chavulio kutoka sehemu ya kuime ya ua.


45. Chunguza kwa makini kielelezo kifuatacho kisha ujibu swali linalofuata.


Kama mkondo wa umeme unaopita katika sakiti ni Ampia 4, kokotoa ukinzani.

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 19  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 19  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

SAYANSI DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
  2. Jibu maswali yote
  3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
  4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
  5. Tumia penseli ya HB tu.
  6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Mwanafunzi wa darasa la 7 alikuwa anatembea barabarani, mara akaona alama hii, ambayo hakujua maana yake. Je! unaweza kumwambia alama hii inahusu nini? 


(A) hatari (B) inamomonyoa na kuunguza (C) hakuna njia (D) inalipuka (E) maji salama [     ]

2. Mwalimu wa darasa la tano aliwafundisha wanafunzi kuwa ili maisha ya viumbe hai yaendelee lazima kuwe na uwiano mzuri katika idadi ya viumbe hai wanaotegemeana. Je! unafikiri elimu inayohusu kutegemeana kwa viumbe hai katika mazingira inaitwaje?

(A) baiolojia (B) usanisinuru (C) ikolojia (D) akiolojia (E) amfolopojia [     ]

3. Afisa kilimo alitoa elimu kwa wananchi kuhusu aina ya udongo unaofaa kwa kilimo. Ni aina gani ya udongo Afisa kilimo alitaja? 

(A) kichanga (B) tifutifu (C) mfinyanzi (D) tope (E) sanyi [     ]

4. Bwana shamba hutumia gesi maalum inayofaa kutengeneza mbolea za chumvichumvi za viwandani kama Yurea, DAP, NPK na CAN. Taja jina la gesi hiyo

(A) posforasi (B) kalisi (C) haidrojeni (D) naitrojeni (E) uranium [     ]

5. Katika jaribio la kubaini ncha za sumaku, sumaku ilining’inizwa hewani, nini kilitokea?

(A) ncha ya kaskazini huelekea kaskazini (B) ncha za kaskazini na kus huelekea kusini (C) ncha ya KAS huelekea kusini (D) huzunguka wakati wote (E) itatulia [     ]

6. Ni kawaida kuwa volteji ya umeme inapoongezeka katika sakiti ya umeme__________nayo huongezeka kama ukinzani haubadiliki. 

(A) mkondo (B) ukinzani wa umeme (C) sakiti ya umeme (D) omu ya umeme (E) sumaku ya umeme [     ]

7. Wanafunzi wa darasa la 6 walipokuwa maabara waliambiwa wakokotoe kiasi cha mkondo wa umeme unaopita katika sakiti yenye volteji 20V na ukinzani wenye omu 0.4. Walipata jibu gani?

(A) 50A (B) 50VA (C) 150A (D) 8A (E) 18A [     ]

8. Kwa nini katika uzalishaji wa gesivunde gesi ya kabonidayoksaidi huondolewa?

(A) ili methane iongezeke (B) ili methane ipungue (C) ili methane iwe safi (D) ili methane iwe nzito (E) methane isiathiriwe [     ]

9. Umbali wa Kiolwa kwenda kwenye kioo bapa ni sm 5. Je! umbali wa taswira kutoka kwenye kioo bapa itakuwa sm ngapi? (A) sm 15 (B) sm 5 (C) sm 50 (D) sm 10 (E) sm 2.5 [     ]

10. Juma alifanya jaribio la kuzama na kuelea kwa vitu, akachukua jiwe lenye uzito wa newton 80 likiwa hewani na kulitumbukiza kwenye maji ambayo uzito wake ukawa ni newton 50. Tafuta kanielezi iliyosukuma jiwe hilo 

(A) 20N (B) 30N (C) 130N (D) 50N (E) 45N [     ]

11.Zifuatazo ni faida za osmosis isipokuwa____________ 

(A) husaidia kuhifadhi vyakula (B) huifanya mimea kuwa imara (C) mizizi ya mimea kufyonza maji yaliyo ardhini (D) husambaza virutubisho na gesi ya oksijeni katika mwili (E) kuwezesha harufu kuenea [     ]

12. X inawakilisha nini katika mlinganyo wa upatikanaji kutu ufuatao;

Maj + X + Chuma Kutu

(A) kabonidayoksaidi (B) kabonimonoksaidi (C) naitrojeni (D) oksijeni (E) agoni [     ]


13. Kama densiti ya kitu ni ndogo kuliko ya maji, nini kitatokea ukidondosha kitu hicho kwenye maji? 

(A) kitazama (B) kitazama na kuelea (C) kitakuwa hewani (D) kitaelea (E) kitaanguka [     ]

14. Kusambaa kwa tone la wino katika beseni lenye maji husababishwa na _________

(A) osimosisi (B) difyusheni (C) mweneo (D) uyeyushaji (E) ukolevu [     ]

15. Katika mpangilio wa molekyuli za maada hizi ni ipi inawakilisha maada yenye umbo maalum?


(A) B (B) C (C) A (D) A na B (E) A na C [     ]

16. Wanakijiji wa songambele hufuatilia sana matangazo ya utabiri wa hali ya hewa ili kupata taarifa sahihi za mvua kwa ajili ya kilimo. Unafikiri ni antenna gani hutumika kunasa mawimbi ya utabiri wa hali ya hewa? 

(A) antenna mchirizo akisi au dishi (B) antenna kidoa (C) antenna yagi-uda (D) antenna kitanzi (E) antenna kipenyo [     ] 

17. Mwalimu wa somo la sayansi alikuwa anataka kuandaa matokeo ya wanafunzi wake. Ungemshauri atumie programu gani katika tarakilishi?

(A) andishi (B) programu seli (C) jedwali (D) kiku (E) kiteuzi [     ] 

18. Mwalimu Mkuu alitaka kuandika barua za wito wa wazazi. Je! atatumia programu gani katika tarakilishi? 

(A) intaneti (B) kisakuzi (C) watsapp (D) maunzi (E) andishi [     ] 

19. Mzee Masanja alifungua akaunti katika benki ya NMB iliyoko Dar es Salaam akapata safari ya kibiashara kwenda Dodoma, akatoa pesa katika tawi la NMB lililopo Dodoma. Ni mtandao gani uliomuwezesha?

 (A) JANIBU (B) Mtandao wa eneo (C) MTAPA (D) MTANDAO WA INTANET (E) Mtandao pekuzi [     ] 

20. Zifuatazo ni athari za matumizi mabaya ya simu isipokuwa___________

(A) kuelimisha jamii (B) wizi mtandaoni (C) uraibu wa matumizi ya simu (D) uhalifu (E) kuvuruga mile na desturi [     ] 

21. Kipi kati ya vifuatavyo hutumika kuingiza data kwenye tarakilishi__________

(A) skrini (B) kibodi (C) kipaza sauti (D) printa (E) spika [     ] 

22. Sehemu ya kutumbukiza ufunguo katika kitasa ina mashine sahili aina ya_________

(A) gurudumu (B) skrubu (C) springi (D) nyenzo (E) gurudumu na ekseli [     ] 

23. Mwajuma alisaga juisi kwa kutumia blenda. Ni sehemu gani ya mashine hiyo inayobadili nishati ya umeme kuwa ya kimakanika?

(A) pangaboi (B) bapa (C) ekseli (D) mota (E) bolti [     ] 

24. Mashine ilinyanyua mzigo wenye uzito wa kilogramu 180 kwa kutumia jitihada ya kilogramu 45. Tafuta manufaa ya kimakanika

(A) 135 (B) 225 (C) 4 (D) 6 (E) 8100 [     ] 

25. Zainabu alisukuma ukuta kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 7 mchana, kwa kani ya newtoni 80, lakini ukuta haukusogea. Je alifanya kazi kiasi gani?

(A) juli 80 (B) juli 160 (C) juli 84 (D) juli 40 (E) hakuna kazi iliyofanyika [     ] 

26. Mwanafunzi alikuwa anafagia uwanja kwa kutumia ufagio wa wima. Alitumia nyenzo daraja la ngapi? 

(A) nne (B) tatu (C) kwanza (D) pili (E) mashine tata [     ] 

27. Mzee kazimoto anaota moto wakati wa baridi. Unafikiri joto hilo lilimfikia kwa njia gani?

(A) mnururisho (B) msafara (C) mpitisho (D) mpitisho na msafara (E) msafirisho [     ] 

28. Katika madaraja ya moto, ni daraja lipi linalozimwa kwa maji? 

(A) moto daraja A (B) moto daraja B (C) moto daraja C (D) moto daraja D (E) moto daraja F [     ] 

29. Katika shughuli zao za uwindaji, wanakijiji walitaka kuwasha moto lakini hawakuwa na kiberiti. Walitumia lenzi ya aina gani kuwasha moto?

(A) mbonyeo (B) duara (C) mbinuko (C) bapa (D) nusu duara [     ] 

30. Wataalamu wa sayansi hutumia njia mbalimbali kuzuia vyuma visipate kutu. Katika njia zifuatazo ipi ni sahihi? 

(A) kuviweka kwenye maji (B) kuvipaka rangi (C) kuviongezea oksijeni (D) kuvipaka majivu (E) kuvilaza nje [     ] 

31. John alichovya kipande cha karatasi ya Litmas katika juisi ya limao, karatasi hiyo ilibadilika kutoka rangi ya___________kuwa________ 

(A) nyekundu kuwa njano (B) kijani kuwa njano (C) bluu kuwa nyekundu (D) nyekundu kuwa bluu (E) nyeupe kuwa nyekundu [     ] 

32. Ni zipi kati ya taka zifuatazo zipo kwenye kundi la taka zinazooza?

(A) vyuma chakavu na glasi (B) plastiki na makaratasi (C) vigae na mabaki ya vioo (D) mabaki ya vyakula na makaratasi (E) vyuma na makaratasi [     ] 

33. Ugonjwa wa Ukimwi unaweza kudhibitiwa. Mgonjwa anatakiwa dawa zipi ili kfubaza makali ya virusi? 

(A) VR (B) VAR (C) CD4 (D) RVA (E) ARV [     ] 

34. Tunashauiwa kula vyaula vya vitamin A kwa wingi ili kuimarisha nini katika mwili?

(A) nywele (B) mifupa (C) macho (D) sikio (E) ulimi [     ] 

35. Afisa ustawi alitembelea kituo cha kulelea wazee na kuwashauri watumie vyakula vyenye______ ili kurejesha chembechembe hai na tishu zilizokufa.

(A) protini (B) vitamin (C) wanga (D) madini (E) mafuta [     ] 

36. Moja kati ya zifuatazo ni dalili ya ugonjwa wa Anaemia selimundo__________

(A) damu kutoka mfululizo kwenye jeraha (B) kupungukiwa damu mara kwa mara [     ]  (C) kupata choo chenye damu (D) kupasuka kwa mishipa ya damu (E) damu kutoka polepole

37. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa gani? Homa kali, kutokwa damu sehemu zilizo wazi, uchovu wa mwili, maumivu ya kichwa 

(A) kipindupindu (B) kaswende (C) ebola (D) homa ya uti wa mgongo (E) kisukari [     ] 

38. Mke wa mchapakazi ni mjamzito, utamshauri afanye aina gani ya mazoezi?

(A) kulala (B) kutembea (C) kuruka kamba (D) kukimbia (E) kucheza mpira [     ] 

39. Jumanne alikunywa sumu kimakosa. Je! ni kiungo gani kilichomsaidia kupambana na sumu hiyo?

(A) kongosho (B) figo (C) moyo (D) ini (E) mapafu [     ] 

40. Gameti uke X ikirutubishwa na gamete ume Y na kugawanyika mara mbili tunapata aina gani ya watoto? 

(A) mapacha wanaofanana wa kiume (B) mapacha wanaofanana wa kike (C) mapacha wasiofanana (D) jinsia ya kike (E) jinsia ya kiume [     ] 

SEHEMU B: JAZA NAFASI ZILIZO WAZI 

41. Mishipa yote ya Ateri husafirisha damu yenye oksijeni isipokuwa__________________________

42. Sehemu gani ya ubongo inayoongoza matendo yasiyo ya hiari? ___________________________

43. Tafuta thamani ya X katika wenzo msawazo ufuatao?


44. Ubadilishanaji wa gesi ya oksijeni na kabonidayoksaidi hufanyika sehemu gani ya mapafu? _________________________________________________________________

45. Taja kazi mbili za korodani katika mfumo wa uzazi wa mwanaume

(i) __________________________ 

(ii) _________________________________

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 7  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 7  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256