SAYANSI STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

MTIHANI WA KUJIANDAA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023

SOMO: SAYANSI NA TEKNOLOJIA DARASA: VII 

MUDA: SAA 1:30   

 SEHEMU A: 

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa

1. Chakula ni moja ya hitaji la msingi sana la viumbe hai. Lipi kati ya yafuatayo siyo umuhimu wa chakula kwa binadamu? ___ 

A. Husaidia kukua B. husaidia kujikinga na magonjwa C. hutupatia nguvu D. hutupatia joto mwilini E. hutupatia watoto [     ]

2. Takamwili zote zitolewazo na viumbe hai hupatikana katika hali za maada zifuatazo _____

A. gesi na vimiminika B. yabisi, gasi na kimiminika C. vimiminika na yabisi D. gesi na yabisi E. kimiminika tu [     ]

3. Samaki ni viumbe waishio majini ambao wana ute kiini juu ya miili yao. Kazi ya ute huu ni: ____ 

A. huwasaidia kupumua B. huwasaidia kuona C. huwasaidia kupunguza ukinzani wanapoogelea D. huwasaidia kupata kona E. huwasaidia kuhisi miguso [     ]

4. Ni mamalia yupi hana tezi za jasho? ___ 

A. ng’ombe B. mbwa C. binadamu D. popo E. nyangumi [     ]

5. Zifuatazo ni sifa za taswira katika kiioo mbinuko isipokuwa: ______ A. taswira ni ndogo ukilinganisha na kiolwa B. taswira kuwa wima C. taswira kutokea nyuma ya kioo

D. taswira hugeuza upande wa kulia kuwa upande wa kishoto E. taswira hugeuzwa juu chini [     ]

6. Kitendo cha mmea kupoteza maji kwa njia ya mvuke kupitia kwenye majani huitwa ______

A. usanishaji B. fotosinthensisi C. transilokesheni D. uyeyushaji E. transipiresheni [     ]

7. Ngamia ni mnyama ambaye anauwezo wa kuishi sehemu kame sana ni kitu gani kina msaidia kumudu kuishi sehemu kame? _____ 

A. kwato B. tumbo C. kichwa D. nundu E. shingo [     ]

8. Zifuatazi ni sifa za taswira ya kioo bapa isipokuwa? ___

  1. taswira kuiwa wima 
  2. aswira kutokea mbele ya kioo bapa 
  3. taswira kutokea nyuma ya kio bapa 
  4. ukubwa wa taswira ni sawa unakubwa wa kiolwa 
  5. umbali wa kiolwa kutoka kwenye kioo ni sawa na taswira kutoka kwenye kioo na taswira hugeuzwa upande wa kiolwa kuwa upande wa kushoto wa kiolwa [     ]

9. Mimea inayozaliana kwa kutegemea gameti uke na gameti ume lazima: ________ 

A. iwe mifupi B. iwe mirefu C. ipaliliwe D. iwe inayotoa maua E. iwe isiyotoa maua [     ]

10. Saitimila za magari hutengenezwa kwa kutumia _______

A. vioo mbonyeo B. vioo bapa C. vioo mbinuko D. Lenzi mbonyeo E. lenzi mbinuko [     ]

11. Zifuatazo ni njia mbalimbali zitumiwazo na mimea kudhibiti upotevu wa maji isipokuwa: ______ 

A. kupukutisha majani B. unene na unyororo wa majani C. ukubwa wa majani na unene wa shina D. kunyooka kwa majani E. kukauka kwa shina [     ]

12. Ni seti ya mimea ambayo huzaliana kwa kutumia machipukizi: _____ 

A. viazi mviringo B. karanga na maharage C. mkonge na migomba D. mihogo na viazi vitamu E. miwa na mihogo

13. Gamba gumu katika kichwa cha samaki ambalo hufunika matamvua huitwa: _______ 

A. mapezi B. matamvua C. mabawa D. opekyulamu E. mstari wa neva [     ]

14. Selemani ni mlinzi wa duka la mzee Sultani ni kifaa gani kinamwezesha kumsaidia katika kazi yake ya ulinzi kati ya hivi? _____ 

A. kioo mbonyeo B. lenzi mbonyeo C. lenzi mbinuko D. kioo mbinuko E. kioo bapa [     ]

15. Mirija ambayo huunganisha 0vari na uterasi huitwa: _____ 

A. mirija ya manii B. zaigoti C. mirija ya falopia D. urethira E. ureta [     ]

16. Mashine ya kielektroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadshi taarifa na kutoa matokea ya kazi kwa haraka kulingana na maelezo ni: ______

A. ngoma B. gari C. cherehani D. jenereta au kangavuka E. tarakilishi au kompyuta [     ]

17. Tarakilishi ina kazi kuu nne za msingi ambazo ni hizi zifuatazo isipokuwa: ____

A. kuingiza na kupokea data au taarifa B. kuchakata data au taarifa mbalimbali C. kuhifadhia data au taarifa D. kutoa au kuonesha matokeo ya kazi au taarifa E. kutengeneza mitambo mbalimbali [     ]

18. Sehemu yakinifu za tarakilishi zinazoshikika na zinazoonekana kama kiteuzi, monita, kipaza sauti, kichakato kikuu na printa huitwa: ____ 

A. program B. kashamfumo C. kichakatokikuu D. maunzi E. kingavirusi [     ]

19. Ni kiumbe yupi kati ya wafuatao huweza kujitengenezea chakula chake? ______ 

A. binadamu B. kuku C. ng’ombe D. mmea E. uyoga [     ]

20. Ni pea ipi ya makundi ya wanyama ni homeothemia ______ 

A. samaki na ndege B. amfibia na reptilia C. mamalia na samaki D. ndege na amfibia E. ndege na mamamlia [     ]

21. Stomata ni vitundu vidogovidogo vilivyopo kwenye jani la mmea ambavyo hutumiwa na mimea kupumua vitundu hivyo hupatikana katika sehemu ipi ya jani? _______

A. epidemisi ya juu B. seli safu za kati C. vifereji pitishi D. epidemisi ya chini E. nafasi ya hewa [     ]

22. Mrija mwembamba unaosafirisha chavua au poleni kutoka kwenye stigima kwenda kwenye ovari unaitwa: ____

A. ovuli B. sepali C. kikonyo D. filament E. staili [     ]

23. Ni mdudu yupi hupitia metamofisisi pungufu? ____ 

A. mbu B. mende C. kipepeo D. nyuki E. nzi [     ]

24. Kitu kipi kati ya vifuatavyo kina umbo maalumu? _____

A. soda B. hewa ya oksijeni C. maji D. kipange cha chuma E. hewa ya kabonidayoksaidi [     ]

25. Mwalimu mkuu amenunua tarakilishi ambayo vifaa vyake vyote ikiwemo kibodi, kiteuzi na monita vimeunganishwa ndani ili kurahisissha ubebaji na matumizi mahali popote. Je, hii ni aina gani ya tarakilishi? _____

A. tarakilishi ya mezani B. tarakilishi mfumo C. tarakilishi mpakato D. tarakilishi kuu E. tarakilishi endeshi [     ]

26. Kama mwalimu atakuomba uende ukazime tarakilishi ya mezani iliyopo ofisini ni sehemu ipi utaanza kuzima?____

A. swichi ya ukutani B. kebo ya umeme C. skrini D. kidhibiti umeme E. kasha mfumo [     ]

27. Sumaku huweza kutumika katika maeneo yafuatayo isipokuwa:________ 

A. kunyanyua na kutenganisha vtu B. kutengenezaa kengerele ya umeme C. kutengeneza dira D. kuzalisha umeme E. kukata vioo [     ]

28. ______ ni mkusanyiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vya tarakilishi vifanye kazi na kutoa matokeo kulingana na maelekezo. 

A. Programu B. Paunzi C. Kiteuzi na kibodi D. Kiteuzi na skrini E. Kingavirusi [     ]

29. Elimu ya uhusiano wa viumbe hai na mazingira inajulikana kama _____ 

A. Biolojia B. Mazingira C. Ikolojia D. Metamofosisi E. Bioanuai [     ]

30. Kitu chochote kinachotumika kurahisisha kazi huitwa _______

A. Tarakilishi B. nishati C. mashine D. umeme E. kazi [     ]

31. Wafuatao ni mawakala wa uchavushaji isipokuwa ______

A. wadudu B. upepo C. ndge D. maji E. mwanga [     ]

32. Vifuatavyo ni vitu ambavyo huunda sakiti ya umeme isipokuwa: ________

A. kipitisha umeme B. kikinza umeme C. swichi D. chanzo E. nguzo ya umeme [     ]

33. Usanishaji wa chakula hufanyika katika sehemu ipi ya jani? _____

A. ncha B. kingo C. mishipa jani D. lamina E. kikonyo [     ]

34. Ni kitendo kipi kati ya vifuatavyo ni badiliko la kiumbo? _____ 

A. chuma kupata kutu B. kuungua kwa nta C. Maziwa kuganda D. kuungua kwa karatasi E. majani kuoza [     ]

35. Mamalia hutumia ogani ipi kupumua? ______

A. pua B. ngozi C. mdomo D. mapafu E. moyo [     ]

36. Mtiririko wa elekroni au chaji hasi kwenye kipitishio kutoka kwenye chanzo hadi kitumia umeme huitwa: ___ 

A. waya B. nishati C. sakiti D. kikinza E. umeme [     ]

37. Sehemu ya ua ambayo ikikomaa huwa tunda huitwa ________ 

A.ovuli B. stigma C. petali D. ovari E. stameni [     ]

38. Mtandao janibu ni aina ya mtandao ambao huunganisha tarakilishi: _____ 

A. katika eneo kubwa la kijografia B. zote duniani C. katika eneo dogo la kijografia D. na printa E. Na ruta [     ]

39. Zikitumika mashine rahisi zaidi ya moja kuunda mashine moja mashine hiyo huitwa: ______ 

A. roda tuli B. mashine mchanganyiko C. mashine tata D. nyenzo E. muunganiko [     ]

40. Mche wa sumaku wenye ncha ya KUS na KAS ukining’inizwa hewani ncha ya KAS itaelekea upande gani wa dunia?_ 

A. Kusini B. Mashariki C. Magharibi D. Kaskazini E. Uelekeo wa jua [     ]

SEHEMU B: Jaza nafasi wazi

41. Hewa iliyo katika mwendo huitwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

42. Kitendo cha mimea ya kijani kujitengenezea chakula chake huitwa: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

43. Mojawapo ya sehemu tatu za wenzo ni mzigo. Taja zingine mbili: i . . . . . . . . .. . . . .. ii. . . . . . . . . . ...

44. Nini kinatokea katika mchoro huo hapo chini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

45. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu kipengele i na ii


i. Hii ni aina gani ya sakiti?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

ii. Ikiwashwa swichi C nini kitatokea kwa glopu namba 2 endapo glopu namba 1 itaungua?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 24  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 24  

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA SAYANSI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
  4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
  5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
  6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

  1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
  2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
  3. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: (Alama 40)

Kwa swali 1-40, tafuta majibu kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya OMR uliyopewa.

1. Mwalimu aliwaambia wanafunzi wa darasa la saba kuwa baadhi ya vyombo vya usafiri wa majini vinaweza kuzama au kuelea kama nahodha ameamua kufanya hivyo. Unadhani ni sababu gani huviwezesha kufanya hivyo?

A: Vinabadilisha maumbo B: Manahodha wana mafunzo ya kutosha C: Densiti hubadilika kutegemea aina ya maji D: Mwendokasi huviwezesha kufanya hivyo E: Vina matanki ambayo hujazwa maji au hewa [       ]

2. Yona alipanda mmea chumbani, mmea ulipoota alishangaa kuona majani yake yanaelekea dirishani kadiri ulivyozidi kukua. Je, kitendo hicho kinaitwaje kisayansi?

A: Haidropizimu B: Fototropizimu C: Kemotropizimu D: Jeotropizimu E: Tropizimu [       ]

3. Mwalimu aliwafundisha wanafunzi wake kuwa baadhi ya wadudu hufuata hatua nne za ukuaji. Jeni alipouliza kama wadudu wote hufuata hatua nne za ukuaji, mwalimu aliwapa kazi ya kufanya utafiti wa kujua ni wadudu gani hawafuati hizo hatua. Kama ungekuwa mwalimu ungemjibu nini Jeni?

A: Kipepeo–Nzi-Panzi B: Senene-panzi-mchwa C: Mchwa-kereng’ende-panzi D: Nyigu-kereng’ende-kipepeo E: Nzige-senene-panzi [       ]

4. Jerome ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba aliambiwa apange makundi ya alama za usalama kwa usahihi. Je, alama ifuatayo ilipangwa katika kundi gani?


A: Alama ya amri B: Alama ya kukataza C: Alama ya dharura D: Alama ya tahadhari E: Alama ya hatari [       ]

5. Msukumo wa mkondo wa umeme katika sakiti ni volti 6. Je ni kiasi gani cha mkondo wa wa umeme huzalishwa ikiwa kinzani ni ohm 0.5?

A: Ampia 3 B: Ampia 12 C: Ampia 0.6 D: Ampia 0.025 E: Ampia 25 [       ]

6. Ukiambiwa na mama yako uandike kanuni ya kutafuta ukinzani, lipi kati ya majibu yafuatayo litakuwa jibu lako?

A: V=I/R B: I=VxR C: R=V/I D: V=I/R E: V=IxR [       ]

7. Selemani ni mwanaume tajiri anayeishi Kilwa ambaye anataka kulinda nyumba mpya isipigwe na radi. Je, atalazimika kununua kitu gani kati ya vifuatavyo ili akiunganishe na waya wa Ethi?

A: Mtaimbo wa chuma B: Mtaimbo wa shaba C: Madini ya Zinki D: Mtambo wa Aluminum E: Mtaimbo wa zebaki [       ]

8. Kombe aliambiwa na baba yake kuorodhesha vyanzo vya nishati mbadala. Kama mojawapo ya vyanzo alivyooorodhesha hakikuwa sahihi, chanzo hicho ni kipi??

A: Mkondo wa maji B: Paneli ya jua C: Makaa ya mawe D: Umeme wa Kidatu E: Upepo [       ]

9. Wakati wa ujenzi wa barabara, mzigo wa nyutoni 100 uliinuliwa kwa kutumia jitihada ya kilogramu 5 kwa umbali wa mita 8. Je, mashine hiyo ilikuwa na ufanisi kiasi gani?

A: 50% B: 75% C: 0.5% D: 100% E: 200% [       ]

10. Wafanyakazi watano waliulizwa na mwanafunzi swali kama ifuatatvyo: ‘Ni nani kati yenu kazi yake inahusisha badiliko la kikemikali? Unadhani ni nani alitoa jibu sahihi?

A: Mwashi B: Fundi cherehani C: Mpishi D: Fundi bomba E: Mkata vioo [       ]

11. Tulipokuwa tunajifunza hali za maada, tuligundua kuwa mabadiliko ya hali za maada hutegemea mabadiliko ya joto katika mazingira husika. Je, ni badiliko gani hutegemea ongezeko la joto katika maji?

A: Kuganda kwa maji B: Kubadili mvuke kuwa maji C: Utangaenezaji wa mvua kwenye mawingu D: Uvukizaji E: Kutengeneza barafu [       ]

12. Wakati wa shughuli za kila siku za shule, Asha alikuwa anasoma kitabu cha sayansi na tekinolojia kuhusu vyanzo vya nishati vinavyotumia tabaini kuzalisha umeme. Ni chanzo kipi hakikusomwa na Asha?

A: Umeme wa Kidatu B: Paneli ya jua C: Joto ardhi D: Uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo E: Jenereta ya mafuta [       ]

13. Mabadiliko ya gesi hufanyika katika mapafu wakati wa upumuaji wa wanyama ambapo Oksijeni huingia na hewa ya ukaa hutoka nje. Ni kipi kati ya vifuatavyo huwezesha hewa ya ukaa kutoka nje?

A: Osmosisi B: Usambaaji C: Uenezaji D: Uvukizaji E: Tropizimu [       ]

14. Robina alisukuma mkokoteni umbali wa sentimeta 500. Kama kazi aliyoifanya ilikuwa joule 100, atakuwa ametumia kani ngapi katika kukamilisha zoezi lote?

A: N 0.2 B: Kg 20 C: N 20 D: N 500 E:N 50000 [       ]

15. Baraka alitakiwa na mtaalam wa elimu ya mawasiliano aandike jina linalojumuisha mikeka kazi. Unadhani alijibu nini kati ya machaguo haya?

A: Kitabu kazi B: Seli C: Ekseli D: Programu jedwali E: Mkusanyiko wa mikeka [       ]

16. Muunganiko wa safu wima na safu mlalo katika programu jedwali huitwaje?

A: Kitufe B: Kiteuzi C: Seli D: Kanuni E: Kiolesura [       ]

17. Doto ana shule ya msingi nchini Kanada na rafiki yake Collins ana shule ya sekondari nchini Uingereza. Ikiwa watu hawa huwasiliana kwa kutumia simu ili kupeana uzoefu wa kuendesha shule, ni aina gani ya mtandao watatakiwa kutumia ili kurahisisha mawasiliano?

A: MJA B: Mtandao wa nchi C: Mtandao wa simu D: Mtandao wa tarakilishi E: MTAPA [       ]

18. Ignas amechoka sana kwa sababu amekuwa akichapa kwa kutumia tarakilishi kwa muda wa saa tano. Je, ni hatua gani itakuwa ya kwanza katika kuzima tarakilishi hiyo?

A: Kubofya paumenyu B: Bonyeza kitufe cha kuanzia C: Bonyeza Microsoft word D: Bofya Microsoft Excel E: Bonyeza kitufe cha kufungua [       ]

19. Mwalimu alifundisha vitu vingi kuhusu marekebisho ya data. Alisema kuwa kurekebisha data inahusisha kuzibadili kwa jinsi mhusika anavyotoka na anaweza kutoa au kuongeza vitu anavyohitaji katika data hizo. Ni njia ipi itatumika kutunza data?

A: Kuhifadhi B: Kupigia mistari C: Kuongeza ukubwa wa maandishi D: Kukoleza maandishi E: Kuzalisha vitini [       ]

20. Rehema ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano alimuuliza baba yake ni sehemu gani ya tarakilishi huonesha picha?

A: Spika B: Kicharazio C: Kiteuzi D: CPU E: Skrini [       ]

21. Kuna programu nyingi zinazotumika katika tarakilishi. Endapo Majaliwa atatumia programu jedwali, ataitumia kufanya kazi ipi kati ya zifuatazo?

A: Uchoraji B: Kuandaa matokeo ya mitihani C: Kuandika barua D: Kucheza michezo E: Kuchora picha [       ]

22. Pareto hutumia seli kavu na taa ili kuwasha umeme chumbani kwake. Unafikiri anatumia aina gani ya umeme?

A: Mkondo geu B: Mkondo mnyoofu  C: Mkondo geu na mkondo mnyoofu D: Mkondo wa umeme E: Mkondo wa seli kavu [       ]

23. Kielelezo kifuatacho kinaonesha aina gani ya roda?


A: Roda moja B: Roda huru C: Wenzo tuli D: Roda E: Wenzo huru [       ]

24. Wanaume watano wenye uzito wa kilogramu 70 kila mmoja walisukuma mti mkubwa kwa muda wa saa nne lakini haukusogea. Wanaume hao walichoka na kila mmoja akaenda kwake. Je, walifanya kazi kwa kiasi gani?

A: J4000 B: J4 C: J400 D: Kazi kubwa E:J 0 [       ]

25. Penford aliainisha mashine zifuatazo. Endapo lengo lake lingekuwa ni kuainisha mashine rahisi tu, ni mashine ipi iliainishwa kimakosa?

A: Wenzo B: Nyundo C: Stepla D: Skrubu E: Mtelemko [       ]

26. Rukia ana lenzi ambayo akiielekeza kwenye mwanga , mwanga hutawanyika. Je, unadahani hii ni aina gani ya lenzi?

A: Lenzi mbinuko B: Lenzi mbonyeo C: Lenzi nusu duara D: Lenzi bapa E: Lenzi mviringo [       ]

27. Ukienda hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa mwili, joto, mapigo ya moyo na uzito hupimwa kwanza. Je, kimiminika kilichomo katika mashine ya kupimia joto la mwili kinaitwaje?

A:Maji safi B: Spiriti C: Ayodini D: Zebaki E: Petroli [       ]

28. Lenzi hutumika katika vifaa mbalimbali vinavyotumika na macho katika nyanja mbalimbali katika maisha.Tumia ujuzi ulioupata darasa la tano kubaini kifaa kinachofanya kazi kama jicho la binadamu ?

A: Kamera B: Hadubini C: Darubini D: Periskopu E: Teleskopu [       ]

29. Tulipomwomba mwalimu atutajie faida za kufanya mazoezi ya viungo alieleza faida nyingi sana. Kulingana na ufahamu ulio nao, ipi ni moja kati ya faida alizotaja mwalimu?

A: Kunenepa B: Kujenga misuli C: Kujenga misuli na mifupa D: Kuimarisha meno E: Kuongeza joto la mwili [       ]

30. Malaria ni ugonjwa hatari sana unaoua mamilioni ya watu duniani. Wiki iliyopita Adamu alipelekwa hospitalini na baada ya uchunguzi wa damu daktari aligundua kuwa alikuwa na vimelea vinavyosababisha malaria. Je, ni aina gani ya mbu ilimuuma Adamu?

A: Kuleksi B: Plasmodiamu C: Mbung’o D: Anofelesi E: Mbu wa malaria [       ]

31. Kisumu aliunguzwa na metali ya moto lakini alipata madhara kidogo sana. Je, ni ipi kati ya huduma zifuatazo ilikuwa ni huduma ya kwanza kwake ?

A: Kutumia hewa ya ukaa B: Kummwagia maji ya baridi C: Kutumia blanketi zito D: Kuita Zimamoto E: Kwa kutumia feni [       ]

32. Ni kiungo gani huathirika moja kwa moja na kilevi na kupelekea mlevi kupoteza uwezo wa kuweka mwili katika usawazo?

A: Tumbo B: Figo C: Utumbo D: Ubongo E: Moyo [       ]

33. Wanakijiji wa Dogma hawatumii vyoo bali wanajisaidia porini karibu na nyumba zao za makazi. Je, wanakijiji hawa wanaweza kushambuliwa na ugonjwa gani?

A: Uti wa mgongo B: Kuhara damu C: Saratani D: Hemofilia E: Vidonda vya tumbo [       ]

34. Rupia alishauriwa na tabibu kula vyakula vyenye protini kwa sababu anaonekana kuwa na dalili za unyafuzi. Je, ni chakula gani kati ya hivi kinalandana na ushauri wa daktari?

A: Maziwa B: Asali C: Embe D: Mahindi E: Mchicha [       ]

35. Dawa tunazomeza husharabiwa pamoja na madini katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kisha husafirishwa katika sehemu mbalimbali za mwili. Je, ni seli gani za damu huhusika katika usafirishaji huo?

A: Seli hai nyekundu B: Seli hai nyeupe C: Chembe sahani D: Vakyuli E: Saitoplazimu [       ]

36. Watu wanapaswa kuelimishwa kuhusu njia za kujikinga na magonjwa ili tuwe na taifa lenye afya bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa sababu baadhi ya magonjwa huambukiizwa na mengine hayaambukizi. Je, ni upi kati ya haya siyo ugonjwa wa kuambukiza?

A:Malaria B: Kipindipindu C: Pumu D:Kuhara E: Kisonono [       ]

37. Lofa na Kayeye ni marafiki ambao wanapenda kula chakula kwa pamoja. Jana walikula mayai na karanga. Unadhani mmeng’ enyo wa kikemikali ulianzia katika kiungo gani?

A: Tumbo B: Utumbo mpana C: Mdomo D: Utumbo mwembamba E: Iliamu [       ]

38. Kuzaliana ni kitendo kinachofanywa na viumbe hai wote. Amina alitaja viungo vinavyotumika katika mfumo wa uzazi wa binadamu. Ni kiungo kipi ambacho hakukitaja?

A: Tezi ya Cowper B: Tezi dume C: Plasenta D: Kibofu E: Mirija ya manii [       ]

39. Baada ya mzunguko wa damu mwilini kukamilika, damu huelekea kwenye moyo ili isukumwe kwenda katika viungo vyote vya mwili. Je, ni mshipa upi husafirisha damu toka kwenye mapafu hadi kwenye moyo?

A: Vena kava B: Aota C: Vena ya ini D: Vena ya mapafu E: Ateri ya mapafu [       ]

40. Utungwaji wa mimba ni matokeo ya kukutana kwa gameti ya kiume na gameti ya kiume. Njidi alitakiwa na mwalimu wake wa somo la sayansi kutaja sehemu ambayo gameti hizi hukutana. Unadhani alitoa jibu gani kati ya haya?

A: Ukeni B: Kwenye ovari C: Katika mirija ya falopio D: Katika mji wa mimba E: Katika mlango wa uzazi [       ]

SEHEMU B: (Alama 10)

Andika jibu sahihi kwa kila swali la 41-45 katika nafasi iliyoachwa wazi nyuma ya karatasi ya OMR. Tumia kalamu ya wino mweusi au wa buluu.

 41. Mmeng’enyo wa chakula ni mfumo mmojawapo kati ya mifumo mingine katika mwili wa binadamu. Je, ni sehemu gani katika mfumo huo mmeng’enyo huishia?

42. Ni aina gani ya seli za damu hulinda mwili dhidi ya magonjwa?

43. Daima anataka kubadili mkondo mnyofu wa umeme kuwa mkondo geu. Je, atatumia kifaa gani?

44. Chunguza ua hili kwa makini kisha utaje herufi inayowakilisha sehemu inayopokea chavulio kutoka sehemu ya kuime ya ua.


45. Chunguza kwa makini kielelezo kifuatacho kisha ujibu swali linalofuata.


Kama mkondo wa umeme unaopita katika sakiti ni Ampia 4, kokotoa ukinzani.

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 19  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 19  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

SAYANSI DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
  2. Jibu maswali yote
  3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
  4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
  5. Tumia penseli ya HB tu.
  6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Mwanafunzi wa darasa la 7 alikuwa anatembea barabarani, mara akaona alama hii, ambayo hakujua maana yake. Je! unaweza kumwambia alama hii inahusu nini? 


(A) hatari (B) inamomonyoa na kuunguza (C) hakuna njia (D) inalipuka (E) maji salama [     ]

2. Mwalimu wa darasa la tano aliwafundisha wanafunzi kuwa ili maisha ya viumbe hai yaendelee lazima kuwe na uwiano mzuri katika idadi ya viumbe hai wanaotegemeana. Je! unafikiri elimu inayohusu kutegemeana kwa viumbe hai katika mazingira inaitwaje?

(A) baiolojia (B) usanisinuru (C) ikolojia (D) akiolojia (E) amfolopojia [     ]

3. Afisa kilimo alitoa elimu kwa wananchi kuhusu aina ya udongo unaofaa kwa kilimo. Ni aina gani ya udongo Afisa kilimo alitaja? 

(A) kichanga (B) tifutifu (C) mfinyanzi (D) tope (E) sanyi [     ]

4. Bwana shamba hutumia gesi maalum inayofaa kutengeneza mbolea za chumvichumvi za viwandani kama Yurea, DAP, NPK na CAN. Taja jina la gesi hiyo

(A) posforasi (B) kalisi (C) haidrojeni (D) naitrojeni (E) uranium [     ]

5. Katika jaribio la kubaini ncha za sumaku, sumaku ilining’inizwa hewani, nini kilitokea?

(A) ncha ya kaskazini huelekea kaskazini (B) ncha za kaskazini na kus huelekea kusini (C) ncha ya KAS huelekea kusini (D) huzunguka wakati wote (E) itatulia [     ]

6. Ni kawaida kuwa volteji ya umeme inapoongezeka katika sakiti ya umeme__________nayo huongezeka kama ukinzani haubadiliki. 

(A) mkondo (B) ukinzani wa umeme (C) sakiti ya umeme (D) omu ya umeme (E) sumaku ya umeme [     ]

7. Wanafunzi wa darasa la 6 walipokuwa maabara waliambiwa wakokotoe kiasi cha mkondo wa umeme unaopita katika sakiti yenye volteji 20V na ukinzani wenye omu 0.4. Walipata jibu gani?

(A) 50A (B) 50VA (C) 150A (D) 8A (E) 18A [     ]

8. Kwa nini katika uzalishaji wa gesivunde gesi ya kabonidayoksaidi huondolewa?

(A) ili methane iongezeke (B) ili methane ipungue (C) ili methane iwe safi (D) ili methane iwe nzito (E) methane isiathiriwe [     ]

9. Umbali wa Kiolwa kwenda kwenye kioo bapa ni sm 5. Je! umbali wa taswira kutoka kwenye kioo bapa itakuwa sm ngapi? (A) sm 15 (B) sm 5 (C) sm 50 (D) sm 10 (E) sm 2.5 [     ]

10. Juma alifanya jaribio la kuzama na kuelea kwa vitu, akachukua jiwe lenye uzito wa newton 80 likiwa hewani na kulitumbukiza kwenye maji ambayo uzito wake ukawa ni newton 50. Tafuta kanielezi iliyosukuma jiwe hilo 

(A) 20N (B) 30N (C) 130N (D) 50N (E) 45N [     ]

11.Zifuatazo ni faida za osmosis isipokuwa____________ 

(A) husaidia kuhifadhi vyakula (B) huifanya mimea kuwa imara (C) mizizi ya mimea kufyonza maji yaliyo ardhini (D) husambaza virutubisho na gesi ya oksijeni katika mwili (E) kuwezesha harufu kuenea [     ]

12. X inawakilisha nini katika mlinganyo wa upatikanaji kutu ufuatao;

Maj + X + Chuma Kutu

(A) kabonidayoksaidi (B) kabonimonoksaidi (C) naitrojeni (D) oksijeni (E) agoni [     ]


13. Kama densiti ya kitu ni ndogo kuliko ya maji, nini kitatokea ukidondosha kitu hicho kwenye maji? 

(A) kitazama (B) kitazama na kuelea (C) kitakuwa hewani (D) kitaelea (E) kitaanguka [     ]

14. Kusambaa kwa tone la wino katika beseni lenye maji husababishwa na _________

(A) osimosisi (B) difyusheni (C) mweneo (D) uyeyushaji (E) ukolevu [     ]

15. Katika mpangilio wa molekyuli za maada hizi ni ipi inawakilisha maada yenye umbo maalum?


(A) B (B) C (C) A (D) A na B (E) A na C [     ]

16. Wanakijiji wa songambele hufuatilia sana matangazo ya utabiri wa hali ya hewa ili kupata taarifa sahihi za mvua kwa ajili ya kilimo. Unafikiri ni antenna gani hutumika kunasa mawimbi ya utabiri wa hali ya hewa? 

(A) antenna mchirizo akisi au dishi (B) antenna kidoa (C) antenna yagi-uda (D) antenna kitanzi (E) antenna kipenyo [     ] 

17. Mwalimu wa somo la sayansi alikuwa anataka kuandaa matokeo ya wanafunzi wake. Ungemshauri atumie programu gani katika tarakilishi?

(A) andishi (B) programu seli (C) jedwali (D) kiku (E) kiteuzi [     ] 

18. Mwalimu Mkuu alitaka kuandika barua za wito wa wazazi. Je! atatumia programu gani katika tarakilishi? 

(A) intaneti (B) kisakuzi (C) watsapp (D) maunzi (E) andishi [     ] 

19. Mzee Masanja alifungua akaunti katika benki ya NMB iliyoko Dar es Salaam akapata safari ya kibiashara kwenda Dodoma, akatoa pesa katika tawi la NMB lililopo Dodoma. Ni mtandao gani uliomuwezesha?

 (A) JANIBU (B) Mtandao wa eneo (C) MTAPA (D) MTANDAO WA INTANET (E) Mtandao pekuzi [     ] 

20. Zifuatazo ni athari za matumizi mabaya ya simu isipokuwa___________

(A) kuelimisha jamii (B) wizi mtandaoni (C) uraibu wa matumizi ya simu (D) uhalifu (E) kuvuruga mile na desturi [     ] 

21. Kipi kati ya vifuatavyo hutumika kuingiza data kwenye tarakilishi__________

(A) skrini (B) kibodi (C) kipaza sauti (D) printa (E) spika [     ] 

22. Sehemu ya kutumbukiza ufunguo katika kitasa ina mashine sahili aina ya_________

(A) gurudumu (B) skrubu (C) springi (D) nyenzo (E) gurudumu na ekseli [     ] 

23. Mwajuma alisaga juisi kwa kutumia blenda. Ni sehemu gani ya mashine hiyo inayobadili nishati ya umeme kuwa ya kimakanika?

(A) pangaboi (B) bapa (C) ekseli (D) mota (E) bolti [     ] 

24. Mashine ilinyanyua mzigo wenye uzito wa kilogramu 180 kwa kutumia jitihada ya kilogramu 45. Tafuta manufaa ya kimakanika

(A) 135 (B) 225 (C) 4 (D) 6 (E) 8100 [     ] 

25. Zainabu alisukuma ukuta kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 7 mchana, kwa kani ya newtoni 80, lakini ukuta haukusogea. Je alifanya kazi kiasi gani?

(A) juli 80 (B) juli 160 (C) juli 84 (D) juli 40 (E) hakuna kazi iliyofanyika [     ] 

26. Mwanafunzi alikuwa anafagia uwanja kwa kutumia ufagio wa wima. Alitumia nyenzo daraja la ngapi? 

(A) nne (B) tatu (C) kwanza (D) pili (E) mashine tata [     ] 

27. Mzee kazimoto anaota moto wakati wa baridi. Unafikiri joto hilo lilimfikia kwa njia gani?

(A) mnururisho (B) msafara (C) mpitisho (D) mpitisho na msafara (E) msafirisho [     ] 

28. Katika madaraja ya moto, ni daraja lipi linalozimwa kwa maji? 

(A) moto daraja A (B) moto daraja B (C) moto daraja C (D) moto daraja D (E) moto daraja F [     ] 

29. Katika shughuli zao za uwindaji, wanakijiji walitaka kuwasha moto lakini hawakuwa na kiberiti. Walitumia lenzi ya aina gani kuwasha moto?

(A) mbonyeo (B) duara (C) mbinuko (C) bapa (D) nusu duara [     ] 

30. Wataalamu wa sayansi hutumia njia mbalimbali kuzuia vyuma visipate kutu. Katika njia zifuatazo ipi ni sahihi? 

(A) kuviweka kwenye maji (B) kuvipaka rangi (C) kuviongezea oksijeni (D) kuvipaka majivu (E) kuvilaza nje [     ] 

31. John alichovya kipande cha karatasi ya Litmas katika juisi ya limao, karatasi hiyo ilibadilika kutoka rangi ya___________kuwa________ 

(A) nyekundu kuwa njano (B) kijani kuwa njano (C) bluu kuwa nyekundu (D) nyekundu kuwa bluu (E) nyeupe kuwa nyekundu [     ] 

32. Ni zipi kati ya taka zifuatazo zipo kwenye kundi la taka zinazooza?

(A) vyuma chakavu na glasi (B) plastiki na makaratasi (C) vigae na mabaki ya vioo (D) mabaki ya vyakula na makaratasi (E) vyuma na makaratasi [     ] 

33. Ugonjwa wa Ukimwi unaweza kudhibitiwa. Mgonjwa anatakiwa dawa zipi ili kfubaza makali ya virusi? 

(A) VR (B) VAR (C) CD4 (D) RVA (E) ARV [     ] 

34. Tunashauiwa kula vyaula vya vitamin A kwa wingi ili kuimarisha nini katika mwili?

(A) nywele (B) mifupa (C) macho (D) sikio (E) ulimi [     ] 

35. Afisa ustawi alitembelea kituo cha kulelea wazee na kuwashauri watumie vyakula vyenye______ ili kurejesha chembechembe hai na tishu zilizokufa.

(A) protini (B) vitamin (C) wanga (D) madini (E) mafuta [     ] 

36. Moja kati ya zifuatazo ni dalili ya ugonjwa wa Anaemia selimundo__________

(A) damu kutoka mfululizo kwenye jeraha (B) kupungukiwa damu mara kwa mara [     ]  (C) kupata choo chenye damu (D) kupasuka kwa mishipa ya damu (E) damu kutoka polepole

37. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa gani? Homa kali, kutokwa damu sehemu zilizo wazi, uchovu wa mwili, maumivu ya kichwa 

(A) kipindupindu (B) kaswende (C) ebola (D) homa ya uti wa mgongo (E) kisukari [     ] 

38. Mke wa mchapakazi ni mjamzito, utamshauri afanye aina gani ya mazoezi?

(A) kulala (B) kutembea (C) kuruka kamba (D) kukimbia (E) kucheza mpira [     ] 

39. Jumanne alikunywa sumu kimakosa. Je! ni kiungo gani kilichomsaidia kupambana na sumu hiyo?

(A) kongosho (B) figo (C) moyo (D) ini (E) mapafu [     ] 

40. Gameti uke X ikirutubishwa na gamete ume Y na kugawanyika mara mbili tunapata aina gani ya watoto? 

(A) mapacha wanaofanana wa kiume (B) mapacha wanaofanana wa kike (C) mapacha wasiofanana (D) jinsia ya kike (E) jinsia ya kiume [     ] 

SEHEMU B: JAZA NAFASI ZILIZO WAZI 

41. Mishipa yote ya Ateri husafirisha damu yenye oksijeni isipokuwa__________________________

42. Sehemu gani ya ubongo inayoongoza matendo yasiyo ya hiari? ___________________________

43. Tafuta thamani ya X katika wenzo msawazo ufuatao?


44. Ubadilishanaji wa gesi ya oksijeni na kabonidayoksaidi hufanyika sehemu gani ya mapafu? _________________________________________________________________

45. Taja kazi mbili za korodani katika mfumo wa uzazi wa mwanaume

(i) __________________________ 

(ii) _________________________________

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 7  

STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 7  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256