MAARIFA STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JINA LA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . 

NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . . 

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024

SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1:30

Maelekezo:

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali saba (07).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi.
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa.
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika.
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele cha (i)-(xv), chagua jibu sahihi kisha andika herufi hiyo katika kisanduku.

(i) Kupungua kwa kasi kwa misitu hapa Tanzania kunasababishwa na. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

A. Joto kali la kiangazi B. Ukatji miti kwa ajili ya mkaa, kilimo na kuni C. Serikali kutokuwa na sera ya upandaji miti D. Kufyeka miti ili kufukuza wanyama wakali E. Mvua kubwa zenye mafuriko. [     ]

(ii) Janga la kimazingira linalosababishwa na nguvu za asili pekee linaitwa. . . . . . . . . . . . . .

A. Ukame B. Tetemeko la ardhi C. Mmomonyoko wa udongo D. Njaa E. Uchafu wa mazingira [     ]

(iii) Mwalimu alikuwa akiwafundisha wanafunzi vipengele vya hali ya hewa , alipomaliza mwanafunzi mmoja alitaka kufahamufaida za utabiri wa hali ya hewa . Je unafikiri lipi lilikuwa jibu sahihi kati ya haya?

A. Kuzuia majanga B. Kulima C. Kuchukua tahadhari ya majanga D. Kuepuka mafuriko E. Kujenga nyumba imara [     ]

(iv) Mzee Pondamali anaishi mjini na ana eneo la ekari moja, pia anafuga ng’ombe mia saba katika eneo hilo,unafikiri eneo hilo litapata madhara gani?

A. Jangwa B. Mazao bor ya mifugo C. Mmomonyoko wa udongo D. Utajiri E. Umaarufu [     ]

(v) Njia mojawapo iliyotumiwa na wakoloni katika kuimarisha utawala wa hapa Afrika Mashariki ilikuwa.

A. Kusajili wanafunzi wengi wa kiafrika katika vyuo vya elimu B. Kueneza dini ya kikristo C. Kuoana na watawaliwa D. Kujenga maboma katika wilaya E. Kuanzisha uislamu [     ]

(vi) Mhimili wa dunia ni . . . . . . . . .

A. Mstari maalumu wa Latitudo B. Mstari wa kufikirika unaoanzia kaskazini hadi kusini C. Meridiani kuu D.Ni mstari unaoneshwa kwa darubini tu E. Ni longtudo ndefu kuliko zote [     ]

(vii) Mfumo wa kwanza kabisa wa uzalishaji mali katika maisha ya binadamu ulikuwa.

A. Ukabaila B. Ujima C.Utumwa D. Ujamaa E. Ubepari [     ]

(viii) Ni mashirika yapi ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia elimu na afya duniani?

A. WHO na ILO B. WMO na UNDS C. UNDP na IMF D. UNICEF na IMF E. UNESCO na WHO[     ]

(ix) Kuweka kwa majira ya mwaka kunatokana na nini?

A. Dunia kulizunguka jua B. Kuvuma kwa upepo C. Dunia kujizungusha kwenye mhimili wake D. Kupatwa kwa mwezi E. Usiku na mchana [     ]

(x) Mkoa wetu wa Dodoma una tabia nchi ya nusu jangwa, Je, kwa sifa za mkoa huu tunatakiwa kupanda mazao yenye sifa gani?

A. inayostahili ukame B. ya mizizi C. yanayohitaji mbolea nyingi D. Mbogamboga E. Maji mengi [     ]

(xi) Wanafunzi wa Darasa la Tano walikuwa na ziara ya kimasomo ya siku moja, mwalimu aliwaelekeza waandae vyakula kwa ajili ya safari yao, Je, kipi kilikuwa chakula cha safari kati ya hivi?

A. Mihogo ya kuchemsha B. Wali nyama C. Supu ya kuku D. Viazi vya kukaanga E. Mayai ya kuchemsha [     ]

(xii) Sayari ambayo viumbe hai huishi na Dunia, Je, sayari hii ina mizunguko mingapi?

A. Mmoja B.Sita C. 24 D. Kumi na mbili E. Miwili [     ]

(xiii) Tanganyika ilipata Uhuru wake mwaka 1961, wakati huo Hayati Mwl. J.K . Nyerere akawa Waziri mkuu wa kwanza . Je, ni Gavana yupi wa Kiingereza alikabidhi madaraka kwa wazalendo

A. Horace Byatt B. Donald Cameroon C. Julius Von Soden D. Richard Turn Bull E. Edward Twining [     ]

(xiv) Kazi mojawapo ya sanaa za maonesho katika jamii ni.

A. Kuwatenga B. Kuburudisha C. Kuibia jamii D. Kuitumikisha jamii E. Kuigiza [     ]

(xv) Waasisi wa Muunganonwa Tanzania walikuwani ..

A. Karume na J.K. Nyerere B. Mfaume Kawawa C. Kikwete D. Mkapa E. Majaliwa na Karume [     ]

2. OANISHA KIFUNGU A NA KIFUNGU B ILI KULETA MAANA

FUNGU A

MAJIBU

FUNGU B

I. Shinyanga na Mwanza

[     ]

A. Makumbusho ya Vita vya Maji maji

Ii. Karl Peters

[     ]

B.Kilimo cha Pamba

Iii. Kuundwa kwa jeshi la wananchi wa Tanzania

[     ]

C.Madini ya Chumvi

Iv. Songea

[     ]

D.William Macknon

V. Uvinza

[     ]

E. Mwaka 1964

F.Kampuni ya kibiashara ya Kijerumani Afrika Mashariki

SEHEMU B ( Alama 20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (i) Ni zama zipi binadamu alianza kutembea kwa miguu miwili? . . . . . . . . . .

(ii) Kupwa na kujaa kwa maji ya Bahari husababishwa na nini? . . . . . . . . ...

(iii) Soko kuu la Watumwa hapa Afrika Masharikililikuwa wapi? . . . . . . . . ..

4. (i) Taja taasisi ya kitaifa ambayo husimamia utunzaji wa Mazingira . . . . . . . .

(ii) Mji wa kwanza Afrika Mashariki kujitengenezea sarafu yake ulikuwa . . . . . . .

(iii) Taja aina mbili za taka (a) . . . . ... (b) . . . . . . . ..

5.(i) Taja athari chanya mbili za mlipuko wa volkano (a) . . . . . . . (b) . . . . . . ..

(ii) . Ni mto gani uliotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia? . . . . . . . . . ..

(iii) Taja maziwa mawili tu yaliyopitiwa na bonde la ufa nhini Tanzania ambayo yapo tawi la Magharibi (a) . . . . . . . (b) . . . . . . . . . . . .

6. Bitana ni nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

SEHEMU C( Alama 10)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

7 (i) Ikiwa dunia hutumia saa 1 kuzunguka nyuzi 150. Je, itachukua muda gani kuzunguka nyuzi 900? . . . . . . . . . . .

(ii) Badili Sentigredi 400 kuwa Farenhaiti . . . . . . . . . . . ..

CHUNGUZA KIELELEZO KIFUATACHO KWA MAKINI KISHA JIBU MASWALI YANAYOFUATA.

(iii). Ni kanda gani ya tabia nchi hapa Tanzania unahusika na kilimo cha hilo katika kielelezo hapo juu? . . . . . . . . . . . . . . ...

(iv). Taja aina mbili za zao linaloonekana katika kielelezo ambazo zinalimwa hapa Tanzania (a) . . . . . . . . . ... (b) . . . . . . . . . . ...

(v). Taja mikoa miwili tu maarufu kwa zao hili nchini Tanzania (a) . . . .. (b) . . . . . . ...

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 48  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 48  

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA MACHI 2024 

SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1:30

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali saba (07)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua jibu sahihi na kisha uandike herufi ya jibu sahihi hilo katika nafasi uliyopewa

(i) Mpenja ni mjasiliamali ambaye ameajiri watu nane katika shughuli zake. Je, yupo katika kundi gani la ujasiriamali? A. mdogomdogo B. kati C. mkubwa D. wastani E. mdogo [     ]

(ii) Wanafunzi wa darasa la sita walijifunza kuhusu mistari ya kufikirika inayochorwa katika ramani. Je, ni mistari ipi huchorwa kutoka upande wa magharibi kuelekea mashariki? A. mstarihi B. kontua C. longitudo D. Ikweta E. latitudo [     ]

(iii) Ni kwa jinsi gani Misri na Zanzibar zilipata uhuru wake? A. vita vya msituni B. katiba C. mapinduzi C. mapinduzi na vita D. Mapinduzi na vita E. katiba na vita [     ]

(iv) Kwanini ni muhimu kuwa na wimbo wa shule? `A. hukuza vipaji B. huenzi utamaduni wa taifa C. huleta uzalendo katika shule D. ni utambulisho wa shule E. utambulisho wa wazazi na walezi [     ]

(v) Katika kujifunza stadi za ramani, wanafunzi wengi walishindwa namna ya kuanza kusoma mistari ya gridi. Je, ni kwa namna gani mistari ya gridi huanza kusomwa? A. mistari ya ulalo halafu latitudo B. mistari ya ulalo halafu wima C. mistari ya latitudo halafu longitudo D. mistari ya ulalo tu E. mistari ya wima halafu ulalo [     ]

(vi) Ni kiongozi yupi kati ya hawa wafuatao aliongoza serikali dhalimu ya makaburu nchini Afrika Kusini mwaka 1989 – 1994? A. Nelson Mandela B. Keneth Kaunda C. Idd Amin D. De Clerk E. Desmond Tutu [     ]

(vii) Bunge lina viongozi mbalimbali. Yupi kati ya wafuatao ni kiongozi wa sekretarieti ya bunge? Waziri Mkuu B. Spika C. Katibu Kiongozi D. Kiongozi wa upinzani E. Katibu wa bunge [     ]

(viii) Wanafunzi walitakiwa kumtaja kiongozi ambaye huhakikisha kuwa shughuli za kila siku shuleni zinatekelezwa, lipi lilikuwa ni jibu sahihi? A. mwalimu wa zamu B. mwenyekiti wa kamati ya shule C. mwalimu mkuu D. kaka na dada mkuu E. mwalimu wa darasa [     ]

(ix) Lipi kati ya matukio yafuatayo lilitokea Ulaya kati ya karne ya 18 na 19? A. kuzuka kwa ugonjwa wa ebola B. uvamizi katika nchi za kiafrika C. kukua kwa mapinduzi ya viwanda D. kuzuka kwa vita kuu ya dunia E. Hitler kuitawala dunia [     ]

(x) Wafuatao ni wadudu waharibifu wanaopatikana nyumbani isipokuwa;- A. kunguni, panya na viroboto viroboto, nzi na mbu C. mbu, mende na kunguni D. mende, nzi na chawa E. chawa, viroboto na kunguni [     ]

(xi) Ni katika tabianchi ipi kati ya zifuatazo ambapo hali ya joto hujitokeza katika miezi ya Juni, Septemba, Novemba na Aprili? A. tropiki B. jangwa C. Ikweta D. pwani E. nusu jangwa [     ]

(xii) Katika mfumo wa jua, ni gimba lipi ambalo robotatu ya eneo lake limefunikwa na maji? A. Kausi B. Bahari C. Mirihi D. Zohari E. Dunia [     ]

(xiii) Majanga ya moto huweza kusababishwa na moto wa asili au shughuli za binadamu. Je, kipi ni chanzo kikubwa cha moto kwenye maeneo yenye misitu minene? A. urinaji wa asali B. uwindaji C. umeme wa radi D. milipuko ya radi E. uvutaji wa sigara [     ]

(xiv) Ni tukio lipi kati ya haya yafuatayo ni matokeo ya nguvu ya mvutano kati ya dunia na mwezi? A. kupatwa kwa mwezi B. kupatwa kwa dunia C. kupwa na kujaa kwa maji D. mwezi kukaa henamu E. dunia kujizungusha katika mhimili wake [     ]

(xv) Kitendo cha kutekeleza wazo jipya kwa lengo la kutengeneza au kuboresha bidhaa au huduma huitwaje? A. ujasiriamali B. akili C. ubunifu D. usanii E. utundu [     ]

2. Katika swali hili umepewa sehemu A na Sehemu B. Oanisha sehemu hizo ili kupata maelezo yenye mantiki.

Sehemu A

Sehemu B

(i) Tsunami [     ]

(ii) Umeme wa radi na joto kali [     ]

(iii) Tetemeko la ardhi na mlipuko wa volkano [     ]

(iv) Athari za janga la moto [     ]

(v) Magma [     ]

  1. Nguvu za asili na shughuli za binadamu
  2. Moto wa asili
  3. Lava
  4. Mawimbi makubwa ya bahari yanayosababishwa na tetemeko la ardhi la chini ya bahari
  5. Aina za majanga
  6. Hewaukaa kuongezeka
  7. Miamba iliyoyeyuka kwa joto kali chini ya ardhi

SEHEMU B: (ALAMA 20)

3. Mwishoni mwa mwaka 2023 wilaya ya Hanang iliyopo mkoani Manyara ilikumbwa na moja ya majanga ya asili ambalo lilipelekea kutokea kwa madhara mbalimbali.

  1. Je, ni janga gani liliikumba wilaya ya Hanang?                                
  2. Taja madhara mawili yaliyosababishwa na janga hilo                                 na                                       
  3. Bainisha njia mbili ambazo jamii inaweza kuzitumia kama tahadhari ili kuzuia kutokea kwa janga kama hilo                                    na                                       

4. Maendeleo ya binadamu yamepitia katika vipindi mbalimbali ambavyo ni zama za mawe, zama za chuma na zama za teknolojia ya kisasa ya kidigitali.

  1. Je, ni kitu gani huitambulisha zama husika?  
  2. Zama za mawe zimegawanyika katika zama za kale, za kati na za mwisho. Taja shughuli kuu mbili za kiuchumi ambazo binadamu alianza kuzifanya katika zama za mawe za mwisho. na 
  3. Katika zama za kati za mawe binadamu aliweza kusafiri na kuishi maeneo mbalimbali yenye baridi kali duniani; je, ni nini kilimwezesha kuweza kuishi maeneo hayo?  

5. Tabianchi ni wastani wa hali ya hewa ya eneo fulani iliyorekodiwa kwa kipindi kisichopungua miaka 30.

  1. Kuna mambo makuu matatu yanayoathiri tabianchi,taja mambo mawili                              na                                           
  2. Ukataji wa miti na matumizi ya fueli za kisukuku huweza kusababisha ongezeko la kitu gani duniani?                                      

6. Kuanzia karne ya 20 Tanganyika iliwekwa chini ya utawala wa Kiingereza;-

  1. Taja tukio kubwa la kihistoria ambalo lilitokea duniani na athari zake zikapelekea Tanganyika kuwa chini ya utawala wa Kiingereza                                           
  2. Bainisha aina ya utawala waliotumia Waingereza katika kuitawala Tanganyika                                             

SEHEMU C : ALAMA 10

7. Chunguza jedwali ulilopewa likiwa linaonesha matukio ya kihistoria Tanzania kisha jibu maswali kipengele cha a-e

Mwaka

Matukio ya Kihistoria

1961

Tanganyika ilipata uhuru

1967

Azimio la Arusha

1978-1979

Vita vya Kagera

1999

Kifo cha Rais wa kwanza wa Tanzania

2021

Kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania

2024

Kifo cha Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania

  1.  Taja angalau vifaa viwili vinavyoweza kutumika katika kukusanya taarifa za kihistoria                                        na                                           
  2. Wanahistoria hutumia vyanzo mbalimbali katika ukusanyaji na utunzaji wa kumbukumbu, taja angalau vyanzo viwili.                                                 na                                           
  3. Ikiwa umetembelea kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam ili kujifunza zaidi kuhusiana na tukio la kihistoria lililotokea mwaka 1961, bainisha njia mbili utakazotumia katika kukusanya taarifa hizo.                                                   ,                                                        
  4. Ni sehemu gani ya makumbusho ambako zinapatikana kumbukumbu za hayati Julius K. Nyerere tu?                                                                      
  5. Bainisha mataifa ambayo yalihusika katika tukio la kihistoria la mwaka 1978 – 1979.                                                                  


STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 40  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 40  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024 

SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1:30

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali saba (07). 
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele cha (i) – (xv), chagua jibu sahihi kisha andika herufi hiyo katika parandesi ulizopewa. 

i. Endapo ungetakiwa kubaini chanzo au njia ya kupata habari za kihistoria kwa njia kuchunguza mabaki ya mwanadamu, jibu lako lingekuwa lipi?

A: Anthropolojia B: Akiolojia C: Sayansi ya lugha D: Chanzo cha kielektroniki E: Kumbukumbu za maandishi [     ]

ii. Zifuatazo zote ni njia na visababishi vya uharibifu wa mazingira ISIPOKUWA;

A: Kuchoma misitu B: Ukataji miti kwa ajili ya kilimo C: Ufugaji wa wanyama wachache kwenye eneo kubwa D: Kukata miti kwa ajili ya mbao na mkaa E: Ufugaji wa wanyama wengi kwenye eneo dogo [     ]

iii. Jamii za kitanzania zina aina tofauti za vyakula vya asili. Ni kwanini watanzania huandaa na kula vyakula wakati wa misiba na mazishi?

A: Kuwafanya watu wafurahie tukio B: Huwakumbusha watu kuwa kifo kipo. C: Siyo mila ya kizamani D: Kuwafanya watu wapate nguvu E: Kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii [     ]

iv. Rundu ambaye ni mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii darasa la saba alisema kwamba uhifadhi wa mazingira ni kitendo cha kulinda, kujali na kutunza mazingira. Kwanini ni muhimu kuhifadhi mazingira?

A: Kuruhusu mzunguko huru wa vumbi B: Huleta usawa C: Ili kufuga wanyama wengi D: Ili kuweka uwiano E: Ili kuwezesha viumbe hai kuishi [     ]

v. Mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii alituambia kwamba kadiri mtu alivyo juu kwenye mwinuko toka usawa wa bahari, ndivyo mkandamizo wa hewa unavyoongezeka na jotoridi kupungua na kinyume chake. Mwalimu huyu alikuwa anazungumzia jambo gani?

A: Longitudo B: Milima na mito C: Mkandamizo wa upepo D: Mwinuko unavyoathiri hali ya hewa E: Mvuke anga unavyoathiri hali ya hewa [     ]

vi. Ipi ni kauli sahihi kati ya hizi zifuatazo?

A: Tunafua nguo kabla ya kuziloweka kwenye maji B: Hatutumii sabuni wakati wa kufua nguo C: Tunaloweka nguo kwenye maji kabla ya kuzifua D: Tunapiga nguo pasi kabla ya kuzifua E: Viatu vya ngozi havitakiwi kuoshwa kabisa [     ]

vii. Ipi kati ya hizi zifuatazo HAIKUWA sababu ya kushindwa kwa Watanganyika wakati wa harakati za kujikomboa?

A: Majanga ya asili B: Silaha duni za kiafrika C: Usaliti D: Kukosa umoja E: Kukosekana kwa maarifa [     ]

viii. Ni tukio lipi kati ya haya yafuatayo lilisababisha uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

A: Mapinduzi B: Kifo cha Mwl. Nyerere C: Muungano waTanganyika na Zanzibar D: Uhuru wa Tanganyika E: Siku ya Tanganyika kuwa Jamhuri [     ]

ix. Zifuatazo zote ni faida za maeneo yanayotunza kumbukumbu za kihistoria ISIPOKUWA;

A: Yanavutia watalii B: Yanatoa ajira C: Yanatoa taarifa zinazowasaidia watafiti D: Hutunza utamaduni wa eneo husika E: Hutunza wanyama pori [     ]

x. Mtaalam wa mazingira aliwashauri wanakijiji wa kijiji cha Njinji wilayani Lidi kuacha kuharibu mazingira na kuchafua hewa. Ni ipi kati ya shughuli zifuatazo walishauriwa kuacha?

A: Ufugaji wa wanyama B: Kuchoma misitu kwa ajili ya kilimo C: Kupanda miti D: Kupanda mazao ya chakula E: Kusafisha mazingira [     ]

xi. Mfumo wa jua ni mkusanyiko wa sayari nane pamoja na jua katikati. Ni sayari ipi ni ya kipekee ambayo imezungukwa na kitu mithili ya pete?

A: Mirihi B: Sarateni C: Dunia D: Sumbula E: Zohari [     ]

xii. Chifu Mkwawa alikuwa kiongozi wa kabila la Wahehe ambaye alipigana kupinga utawala wa Wajerumani mkoani Iringa. Alipofariki fuvu la kichwa chake lilipelekwa Ujerumani na kisha kurejeshwa nchini Tanzania mwaka 1954. Je, fuvu hilo limehifadhiwa wapi?

A: Bonde la Olduvai B: Ruaha C: Kalenga D: Amboni E: Isimila [     ]

xiii. Kwa kawaida mavazi yamewekewa lebo ambazo huonesha namna ya kufua, kukausha na hata kuyapiga pasi. Kuna umuhimu gani wa kufuata lebo hizo?

A: Kuepuka kuchanganya mavazi B: Hurahisisha kazi ya kufua C: Husaidia kuzuia uharibifu wa mavazi D: Huwatangaza watengenezaji wa lebo E: Huwavutia wateja [     ]

xiv. Jando na unyago ambavyo huwaandaa wavulana na wasichana kuelekea utu uzima ni mila ya zamani sana katika jamii nyingi za kitanzania. Yafuatayo ni mafuzo yanayosisitizwa ISIPOKUWA;

A: Elimu na stadi za maisha B: Kujitegemea C: Upendo na heshima kwa wengine D: Kutowajibika E: Unadhifu na usafi wa mazingira [     ]

xv. Ingawa mvua ni muhimu katika maisha ya viumbe hai, kwa upande mwingine kipengele hiki cha hali ya kina madhara. Unadhani mvua husababisha madhara gani kwa mwanadamu?

A: Husaidia kwenye kilimo B: Husababisha mafuriko C: Huleta Uviko D: Ni chanzo cha ukame E: Ni chanzo cha maji [     ]

2. Katika kipengele cha (i) – (v), chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku kisha uliandike kwenye nafasi iliyo wazi.

Ukataji miti, 1977, Utafiti, 1972, Wazo la biashara, Upandaji miti

(i). Lintu angependa kuanzisha biashara na amekuja kwako kama msomi kuomba ushauri. Ni mambo gani mawili ambayo ungemshauri ayafanye kabla ya kuanzisha biashara?
a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

ii. Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea tarehe 12 Januari 1964 yaliongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume. Je,shujaa huyo aliuawa mwaka gani? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

iii. Eneo la kati la nchi ya Tanzania limeathirika sana na ukame kutokana na wakazi wa eneo hilo kukata miti kwa ajili ya shughuli anuai. Ungewashauri watu hao wafanye nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
iv. Jumuiya ya mwanzo ya Afrika Mashariki iliundwa na nchi tatu wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.Ilivunjika mwaka gani? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

v. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa theluji iliyopo juu ya mlima Kilimanjaro inapungua.Unadhani ni kitu gani ambacho ni moja ya sababu zinazosababisha hali hiyo?
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

SEHEMU B (Alama20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (i) Rafiki yangu Zube huwa anasikia watu wakiongea kuhusu tabaka la ozoni lakini hajui umuhimu wake. Ukiwa kama msomi, ni faida zipi mbili za tabaka hilo unaweza kumpatia Zube?

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... .
b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

(ii) Salum ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita aliulizwa na mwalimu wa somo la Stadi za Kazi atoe maana ya neno ‘Urejelezaji’Unadhani alitoa jibu lipi sahihi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iii) Kwa kuzingatia pande nane za dunia, kijiji chetu kipo kati ya upande wa Kusini na Mashariki. Unafikiri kijiji chetu kipo katika upande upi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

4. (i) Njilo ana mazoea ya kuvaa viatu vyenye unyevuunyevu. Anaweza kupata tatizo gani la kiafya? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

(ii) Mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii alipokuwa anasahihisha daftari ya Bahati alishindwa kujua ramani ilikuwa inahusu nini. Unadhani ni kitu gani kilikosekana kwenye ramani hiyo? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iii) Kuna aina kuu tatu za pasi. Ni aina ipi ya pasi hutumika zaidi kwenye maeneo ya mijini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

5.(i) Bibi Mbuda anatarajia kuandaa chapati kwa ajili ya safari kwa sababu atasafiri juma lijalo. Unadhani atatumia njia ipi ya mapishi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(ii)  Njudu alitakiwa kuchora ramani ya Afrika. Unadhani atatumia kipimio kipi kitakachofaa kwa kazi hiyo? . . . . . . . . . . . . . . . . . .

6. (i) Mkataba wa kwanza wa kukomesha biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki ulisainiwa mwaka 1822. Ni mwaka upi sultani wa Zanziba aitwaye Bargashi alisimamisha usafirishaji wa watumwa kuvuka bahari ya Hindi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(ii) Ni mwaka gani Sultani Seyyid Said alihamisha makao yake kutoka Oman Kwenda Zanzibar? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

SEHEMU C (Alama10)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

7. Chunguza kwa makini mchoro ufuatao , kisha ujibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi zilizo wazi.

i. Mstari B una nyuzi 00. Je, mstari huo unaitwaje? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

ii. Herufi D katika mchoro huo inawakilisha eneo gani katika uso wa Dunia ? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

iii. Herufi C ipo upande wa Kusini wa herufi B. Je, herufi Cinawakilisha nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

iv. Ni wakati gani eneo linalopitiwa na mstari C hupata Jua la utosi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

v. Herufi Z ipo upande wa Kaskazini mwa herufi B. Je, herufi Z inawakilisha nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 35  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 35  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA FEBRUARI 2024 

SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1:40

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu mbili: A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A

Kwa swali la 1 – 40, chagua jibu sahihi kisha siliba herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Bwana Bokoboko ambaye ni mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii alipima kipengele kimojawapo cha hali ya hewa ambacho matokeo yake hupatikana kwa asilimia. Ni kipengele kipi hicho?

A: Jua B: Mvua C: Jotoridi D: Unyevuanga E: Mgandamizo wa hewa

2. Ramani zinaweza kutumiwa na makundi tofauti ya watu kwa malengo tofauti. Ni kundi lipi kati ya haya yafuatayo ramani siyo muhimu?

A: Marubani B: Manahodha C: Wacheza muziki D: Maaskari E: Wapimaji ardhi

3. Bonde la Olduvai ni sehemu maarufu ya kihistoria nchini Tanzania na hata duniani kwa sababu ndipo fuvu la binadamu wa kale lilikogunduliwa. Ni nani aligundua fuvu la binadamu wa kale mnamo mwaka 1959?

A: Dr. Charles Darwin B: Dr. Livingstone C: Vasco da Gama D: Carl Peters E: Dr. Louis Leakey

4. Uharibifu wa mazingira ni moja kati ya changamoto zinazoikabili nchi yetu. Ni ipi kati ya njia zifuatazo inapunguza kiwango cha uharibifu wa mazingira?

A: Upandaji miti B: Ukataji miti C: Utupaji ovyo wa taka D: Uchomaji mkaa E: Ufugaji wa wanyama wengi kwenye eneo dogo

5. Mafuriko ni moja kati ya majanga ya asili ambapo sehemu kavu ya ardhi hujaa maji ghafla. Ni ipi kati ya njia zifuatazo inaweza kusaidia kupunguza matokeo hasi ya mafuriko?

A: Ukataji miti B: Ufugaji wa wanyama wengi kwenye eneo dogo C: Uchomaji misitu D: Uchomaji vichaka E: Upandaji miti

6. Wanafunzi wa darasa la sita walipanga kutembelea eneo lenye michoro ya mapangoni lililopo katika ukanda wa kati nchini Tanzania kipindi cha likizo yao ya mwezi Juni. Unafikiri watatembelea kituo gani?

A: Kondoa Irangi – Dodoma B: Isimila – Iringa C: Kaole – Pwani D: Engaruka - Arusha E: Olduvai Gorge – Arusha

7. Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi tofauti. Ni ipi kati ya hizi zifuatazo siyo rasilimali za asili?

A: Ardhi na maji B: Misitu na madini C: Gesi asilia D: Bandari na viwanja vya ndege E: Wanyama pori

8. Mmoja wa wanafunzi wa darasa la saba alitakiwa kutaja misimu ya kudumu ya mwaka nchini Tanzania. Ni lipi kati ya yafuatayo lilikuwa jibu sahihi?

A: Kipupwe na kiangazi B: Kavu na Kiangazi C: Masika na kiangazi D: Kiangazi na unyevunyevu E: Kipupwe na vuli

9. Ngoma ya asili ya Wasukuma hujulikana kama Bugobogobo. Je, ngoma ya asili ya Wangoni huitwaje?

A: Mdundiko B: Lizombe C: Mganda D: Enhuma E: Akasimbo

10. Nani walikuwa waasisi wa awali wa ushirikiano kati ya Tanzania na mataifa mengine ya Afrika?

A: Mwalimu J. K. Nyerere and Sheikh Abeid Karume B: Ali Hassani Mwinyi and B. W. Mkapa C: Jakaya Kikwete and Rashid Mfaume Kawawa D: Mwalimu J.K. Nyerere and Jakaya Kikwete E: Kwame Nkurumah and Dr. John Pombe Magufuli

11. Ili kuleta ukoloni barani Afrika, wakoloni waliwatanguliza mawakala wao amabao walijulikana kama watangulizi wa wakoloni. Ni mawakala gani walikuwa wa kwanza kuwasili barani Afrika?

A: Wafanyabiashara B: Wapelelezi C: Wakristo D: Wamisionari E: Mbaharia

12. Tanzania ni nchi mwanachama wa makundi ya kikanda na kimataifa. Ni kundi lipi kati ya haya yafuatayo Tanzania SIYO nchi mwanachama?

A: SEDC B: COMESA C: EAC D: WHO E: UNO

13. Umoja wa nchi huru za Afrika uliundwa tarehe 25 Mei 1963 na baadaye ukabadilishwa kuwa Umoja wa Afrika mnamo tarehe 9 Julai 2002. Je, ni nani alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa Afrika?

A: Mwl. Julius K. Nyerere B: Yoweri K. Museven C: Haile Sellasie D: Paul Kagame E: Thabo Mbeki

14. Mtwa Mkwawa alikuwa mmoja kati ya mashujaa wa Afrika waliopinga uvamizi wa kikoloni wa Wajerumani nchini Tanganyika. Je, alikuwa kiongozi wa kabila gani kati ya haya yafuatatyo?

A: W a n yamwezi B: Wahehe C: Wayao D: Wagogo E: Wazigua

15. Dunia hutumia muda gani kukamilisha mzunguko mmoja wa nyuzi 360? Ungeulizwa swali hili jibu lako lingekuwa lipi?

A: S i k u 365.5 B: Saa 1 C: Saa 24 D: Saa 96 E: Saa 8760

16. Nchi za Angola, Msumbiji, Kenya, Algeria na Namibia zilipata uhuru wake kupitia mtutu wa bunduki. Zifuatazo ni sababu zilizosababisha nchi hizo kutumia njia hiyo ISIPOLKUWA;

A: Ukatili, ukandamizaji na unyonyaji uliopitiliza kwa waafrika
B: Uwepo wa taasisi za kisiasa zenye nguvu za kikoloni
C: Uwepo wa walowezi wengi kwenye makoloni hayo
D: Wakoloni walitegemea rasilimali za Afrika kuendeleza uchumi wa nchi zao.
E: Wakoloni walichukulia makoloni kama majimbo ya nchi zao yaliyoko ughaibuni.

17. Mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wake, “ Leo dunia ipo kwenye perihelioni. Unadhani ilikuwa tarehe ngapi?

A: Mei, 21 B: Julai, 4 C: Juni,21 D: Januari, 3 E: Desemba, 22

18. Dunia ina mizunguko ya aina mbili; Dunia kujizungusha kwenye mhimili wake na Dunia kulizunguka jua. Dunia ikiwa inajizungusha kwenye mhimili wake hutokea upande gani na kuelekea upande upi?

A: Mashariki kwenda Mgharibi B: Magharibi kwenda Mashariki C: Kaskazini kwenda Kusini D: Kusini kwenda Kaskazini E: Kusini kwenda Mashariki

19. Taifa lolote lina utamaduni wake ambao unatakiwa kusimamiwa na kuendelezwa. Ni mamlaka ipi kati ya hizi zifuatazo inahusika katika kulinda kazi za sanaa nchini Tanzania?

A: TANAPA B: BASATA C: TANESCO D: TBS E: BAKITA

20. Ni shughuli ipi ya uzalishaji kati ya hizi zifuatazo inachukuliwa kama uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kwa kuwa inaajiri idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na shughuli nyingine za uzalishaji mali?

A: Kilimo B: Uchimbaji wa madini C: Uvuvi D: Utalii E: Biashara

21. Mojawapo ya vipengele vinavyoifanya Tanzania iwe kivutio kwa nchi za nje ni uwepo wa uoto wa asili na usio wa asili. Ni upi kati ya hii ifuatayo ni msitu wa kupandwa ulio mkubwa kuliko yote nchini Tanzania?

A: Mazumbai B: Nyumbnitu C: Rungwe D: Ruaha E: Sao Hill

22. Habalibi alitakiwa kutaja faida za utamaduni katika nchi yetu. Ni lipi kati ya haya yafuatayo lingekuwa jibu sahihi?

A: Chanzo cha uhalifu B: Uharibifu wa maadili C: Ubaguzi wa rangi D: Huendeleza umoja na ushirikiano E: Husababisha ubaguzi wa kijinsia

23. Rasilimali za asili na zisizo za asili zinaweza kutengwa na kuwa rasilimali zinazoweza kurejeshwa na zisizoweza kurejeshwa. Ni zipi kati ya hizi zifuatazo ni rasilimali zisizoweza kujrejeshwa?

A: Makaa ya mawe na gesi asilia B: Maji na ardhi C: Misitu na ardhi D: Hewa na ardhi E: Viwanja vya ndege na bandari

24. Bibi Bella ni mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii katika shule ya Msingi Mapinduzi. Mmoja wa wanafunzi wake alitaka kujua jibu la swali “ Ni lini Tanganyika ilijiunga na umoja wa forodha Afrika Mashariki?

A: 1948 B: 1963 C: 1929 D: 1961 E: 1927

25. Shughuli ya uzalishaji ni shughuli yoyote halali aifanyayo binadamu kwa lengo la kujipatia kipato.Ni ipi kati ya shughuli hizi zifuatazo za uzalishaji hujihusisha na kununua na kuuza bidhaa na huduma?

A: Utalii B: Biashara C: Kilimo D: Uchimbaji madini E: Uvuvi

26. Ninini kitatokea endapo Salum aishiye karibu na bahari ya Hindi atatembea umbali wa meta 100 toka usawa wa bahari?

A: Jotoridi litaongezeka kwa 0.6 B: Jotoridi litaongezeka kwa sentigredi 6 C: Jotoridi litapungua kwa sentigredi 0.6 D: Kutakuwa na hali ya ujoto E: Kutakuwa na upepo mkali

27. Masheba ni mkulima wa mazao kama mihogo, viazi, mahindi na ndizi. Mazao haya huitwaje?

A: Mazao ya biashara B: Mazao ya chakula C: Mazao mazuri D: Mazao ya nafaka E: Mazao mabaya

28. Bwana Ntabindi alikuwa anaangalia mechi ya mpira wa miguu kati ya timu za Kumas na timu ya Asante Kotoko iliyokuwa ikichezwa Accra Ghana 00 saa 10:00 jioni. Utakuwa ni muda gani kwa Afrika Mashariki iliyopo 450 Mashariki?

A: Saa 07:00 Usiku B: Saa 01:00 Asubuhi C: Saa 04:00 Usiku D: Saa 07:00 Mchana E: Saa 01:00 Usiku

29. Kumbukumbu za kihistoria hutunzwa kwa kutumia njia anuai. Ni njia ipi ya utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria inafaa kwa watu wasijua kusoma?

A: Masimulizi B: Makumbusho C: Vitabu D: Vifaa vipya E: Matukio mapya

30. Mfumo wa jua ni mkusanyiko wa sayari nane na jua likiwa katikati. Ni sayari ipi kati ya hizi zifuatazo ni ya joto sana.

A: Ya kwanza B: Ya tano C: Ya sita D: Ya pili E: Ya nane

31. Kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki imeundwa nan chi saba. Je, makao makuu ya jumuiya hii yapo wapi?

A: Arusha – Tanzania B: Addis Ababa - Ethiopia C: Lusaka - Zambia D: Gaborone – Botswana E: Cairo – Misri

32. Kuna vipengele tofauti vya hali ya hewa ambavyo hupimwa kwa vifaa anuai.Ni mamlaka ipi inahusika kupima hali ya hewa ya hewa nchini Tanzania?

A: Mamlaka ya hali ya hewaTanzania B: Mamlaka ya Mapato Tanzania C: Taasisi ya hewa D: Mamlaka ya Mawasiliano E: Taasisi ya kupima mvua

33. Zifuatazo ni baadhi ya hatua za kufuata wakati wa kuosha mwili. Zisome kwa makini kisha jibu swali linalofuata.

i. Kupaka mafuta, kuchana nywele kisha kuvaa nguo zilizonyooshwa
ii. Kuosha mwili mzima kwa sabuni, maji na brashi laini
iii. Kausha mwili kwa taulo safi na kavu
iv. Paka mafuta au losheni ili kutenegneza ngozi laini yenye afya na inayong’aa.

Ni chaguo lipi kati ya haya linaonesha mtiririko sahihi wa kuosha mwili?

A: i, iii, iv, ii B: iii, ii, iv, i C: ii, iii, iv, i D: iv, iii, ii, i E: ii, iii, i, iv

34. Wanafunzi wa darasa la sita walitembelea eneo la Mererani-Manyara kwa lengo la kufanya ziara ya mafunzo.

A: Almasi B: Dhahabu C: Tanzanite D: Makaa ya mawe E: Chokaa

35. Bibi Njele aliandaa mlo maalum kwa ajili ya familia na akaaamua kutumia njia ya kupikia kwa kutumia mafuta mengi. Ni kipi kati ya vyakula vifuatavyo hakikupikwa?

A: Maandazi B: Chips C: Donati D: Samaki wa kukaanga E: Chapati

36. Johnson alitakiwa kupima kiwango cha jotoridi katika angahewa ya Dunia ambapo vipimo vyake ni sentigredi. Ni kifaa kipi kinafaa kati ya vifuatavyo alikitumia?

A: Hygrometa B: Kipimajoto C: Kipimamvua D: Anemometa E: Barometa

37. Mwalimu wetu wa somo la Stadi za kazi aliorodhesha vitu vifuatavyo ambavyo vinatakiwa kufundishwa mwaka 2024. Nyimbo, dansi, maigizo na sarakasi

A: Sanaa nzuri B: Sanaa za kuongea C: Sanaa na ufundi D: Sanaa za maonesho E: Ushairi

38. Utamaduni ni jumla ya maisha ya watu katika jamii fulani.Ni ipi kati ya mila na desturi zifuatazo imepitwa na wakati na inatakiwa ikomeshwe?

A: Harusi B: Mazishi C: Sanaa za maonesho D: Ukeketaji E: Kula uagali

39. Tunakiitaje kitendo cha kuondoa matawi ya zamani na yasiyotakiwa kutoka kwenye mmea ili mmea ukue vizuri?

A; Kukata B: Kupogoa C: Kuondoa D: Kufyeka E: Kupalilia

40. Harakati za ukombozi katika nchi za Afrika zililenga kuleta uhuru na utawala binafsi katika nchi hizo ili kuondokana na utawala wa kikoloni.Je, harakati hizi zilianza lini?

A: Baada ya kuundwa umoja wa kiafrika B: Wakati wa vita ya pili ya Dunia C: Baada ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa D: Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi E: Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia

SEHEMU B

Kwa swali la 41 – 45, andika majibu katika nafasi uliyopewa kwenye karatasi ya kujibia kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.

41. Bwana Piedro alipanga kuanzisha biashara ya mtaji wa shilingi milioni kumi. Ni kundi lipi la ujasiriamali atawekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia mtaji huo? . . . . . . . . ...

42. Wanafunzi wa darasa la saba walifanya majadiliano kuhusu vipimio vya ramani wakati wa somo la Maarifa ya Jamii

i. Je, walijadiliana kuhusu vipimio vingapi vya ramani? . . . . . . . . . .

ii. Endapo wangeamua kupima eneo la shamba la shule wangetumia aina gani ya kipimio kwa kuzigatia jibu lako hapo juu? . . . . . . . . . . . . . ..

43. Mabadiliko ya hali ya hewa ni tatizo kubwa sana duniani. Onesha njia moja ambayo inaweza kutumika ili kupunguza madhara ya tatizo hili kwenye jamii. . . . . . . . . . . . . ...

44. Mto Bulindo unapungua kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu karibu na mto huo. Bainisha mambo mawili wanajamii wa eneo hilo wanatakiwa kufanya ili kutatua tatizo hilo. . . . ... . . .

45. Mlima Oldonyo Lengai ni mmoja kati ya milima ya volkano nchini Tanzania. Je, mlima huo upo katika kundi gani la milima? . . . . . . . . . . ..

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 31  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 31  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

 SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI DARASA: VII 

MUDA: SAA 1:30 

SEHEMU A:

 Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa  

1. Shughuli ipi kati ya hizi zifuatazo husababisha uharibifu wa mazingira? ______ 

A. Kupanda miti B. Ukataji miti ovyo C. Kilimo cha matuta D. Urejeleaji wa takataka E. kilimo mseto [       ]

2. Dunia hutumia muda gani kujizungusha nyuzi 15 za longitudo? ______

A. Dakika 4 B. saa 1 C. siku 1 D. mwaka mmoja E. saa 24 [       ]

3. Mkutano wa berlin ni mkutano uliojumuisha mataifa ya kibeberu kwa lengo la kugawana makoloni barani Afrika. Mkutano huu uliitishwa na nani?________ 

A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. Kansela Otto von Bismark D. umoja wa mataifa E. Sultani Seyyid Said [       ]

4. Ni sayari ipi katika mfumo wa Jua ambayo ipo karibu sana na Jua? ______ 

A. Zebaki B. Sumbula C. Zuhura D. Kausi E. Dunia [       ]

5. Yafuatayo ni matokeo ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake isipokua _____ 

A. kutokea kwa usiku na mchana B.madbadiliko ya muda kati ya longitudo moja na nyingine C. kupwa na kujaa kwa maji D. mabadiliko ya uelekeo wa upepo na mikondo ya bahari E. majira ya mwaka [       ]

6. Serikali ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro iliwashauri wakazi wake waishio maeneo ya mabondeni wahame kuepuka majanga yatokanayo na mvua. Lipi kati ya yafuatayo ni janga litokanalo na mvua kubwa?

A. mafuriko B. tetemeko la ardhi C. ukame D. mlipuko wa volkano E. vita [       ]

7. Mifugo mingi katika eneo dogo hupelekea: _______ 

A. Nyasi kuwa nyingi B. mimea kunawiri C. mmomonyoko wa udongo D. utajiri mkubwa kwa wafugaji E. ukosefu wa barabara [       ]

8. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa rasilimali nyingi sana yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo hupatikana Tanzania pekee. Madini ya Tanzanite hupatikana wapi? __ 

A. Mwadui Mkoani Shinyanga B. Uvinza mkoani

Kigoma C. Bagamoyo mkoani Pwani D. Manyoni mkoani Singida E. Mererani mkoani Manyara [       ]

9. Kiongozi wa koloni katika utawala wa Waingereza na Wajerumani aliitwa Gavana. Yupi kati wa wafuatao ni gavana katika utawala wa Wajerumani? _____

A. Horace Byatt B. Donald Kameroon C. Edward Twining D. Richard Turnbl E. Julius Von Soden [       ]

10.Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita kuu vya kwanza vya dunia, eneo la Tanganyika liliwekwa chini ya utawala wa Waingereza kwa udhamini wa umoja wa mataifa uliofahamika kwa jina la _____

A. UN B. League of Nations C. UNO D. UNHCR E. EAC [       ]

11.Mkataba uliofanyika mwaka 1890 kati ya serikali ya Uingereza na Ujerumani wenye madhumini ya kurekebisha mipaka ya mwaka 1886 ulijulikana kama _______

A. mkataba wa Hamaton B. mkataba wa freire C. mkataba wa Berlin D. mkataba wa Heligoland E. mkataba wa Vienna [       ]

12.Mfumo wa kwanza wa kiuchumi na kiutawala ambapo watu waliishi na kushirikiana pamoja uliitwa _____

A. Ujima B. Ujamaa C. Ubepari D. Ukabaila E. Umwinyi [       ]

13.Viongozi wa mwanzo wa bara la Afrika waliopinga uvamizi wa wakoloni katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii hujulikana kama: ______

A. magavana wa Afrika B. waafrika C. Mashujaa wa Afrika D. maliwali E. Wafadhili wa Afrika [       ]

14.Nani kati ya wafuatao siyo shujaa wa nchi yetu? _______ 

A. Mtwa Mkwawa B. Jomo Kenyatta C. Bibi Titi Mohamed D. Mwalimu J.K. Nyerere E. Mtemi Isike [       ]

15.Mtwa Mkwawa Mkwavinyika alijiua mwenyewe kwa kujipiga risasi baada ya kuona anakaribia kukamatwa na Wajerumani mwaka gani? ___ 

A. 1898 B. 1905 C. 1907 D. 1888 E. 1961 [       ]

16.Joseph alitaka kupata taarifa kuhusu matukio ya kihistoria ya nchi yetu. Unafikiri ni mahali gani angeweza kwenda ili lengo lake litimie?___

A. Maabari B. mbuga za wanyama C. makumbusho D. ikulu E. mgodini [       ]

17.Fuvu la binadamu wa kwanza liligunduliwa katika bonde la Olduvai Gorge mkoani Arusha mwaka 1959. Ni nani waliogundua fuvu hilo? _____ 

A. Dkt Mary George na Dkt George Lincolin B. Dkt. Louis Leakea na Dkt Mary Leakey C. Dkt George Louis na Dkt Mary Leakey D. Vasco Da Gama E. Carl Peters [       ]

18.Hali ya angahewa iliyorekodiwa katika kipindi cha muda mfupi hujulikana kama _____ A. Jotoridi C. Unyevunyevu B. mabadiliko ya tabianchi D. Tabia ya nchi E. Hali ya hewa [       ]

19.Ni mataifa yapi kati ya yafuatayo yaliitawala Tanganyika katika vipindi tofauti?__ 

A. Marekani na Ujerumani B. Ujerumani na Uingereza C. Ufaransa na Uingereza D. Ureno na Marekani E. Italia na uingereza [       ]

20.Kipi kati ya hivi vifuatavyo siyo kipengele cha hali ya hewa? ____ 

A. Jotoridi B. Kipimajoto C. Mvua D. Unyevuanga E. upepo [       ]

21.Fedha anazobakiwa nazo mfanyabiashara baada ya kuuza bidhaa na kutoa kiasi cha mtaji hujulikana kama:_

A. kodi B. hasara C. tozo D. akiba E. faida [       ]

22.Mambo ya kawaida yanayofanywa mara kwa mara na wanajamii ambayo huweza kubadilika kulingana na mahali na wakati hujulikana kama ____ 

A. mila B. miiko C. tambiko D. desturi E. lugha [       ]

23.Ufundi anaotumia mtu ili kuwasilisha fikra au mawazo yake katika namna inayoburudisha na kufikirisha huitwa ____ 

A. mila B. desturi C. tambiko D. Sanaa E. vinyago [       ]

24.Mfalme Leopold wa Ubelgiji alitambuliwa kuwa mtawala wa __________ 

A. Kongo B. Tanganyika C. Senegal D. Zimbabwe E. Lesotho [       ]

25.Bwana na Paulo amefunga ndoa mwaka 2021 na Bibi Sijali na hadi sasa wanaishi pamoja katika kijiji cha Mzogole wakiwa bado hawajapata mtoto. Hii ni aina gani ya familia? ____ 

A. Familia ya awali B. Familia pana C. Familia ya mke na mume D. familia ya watoto yatima E. familia ya mzazi mmoja [       ]

26.Mikoa ambayo ina ranchi za taifa ni ____

A. Dodoma, Tanga na Pwani B. Iringa, Njombe na Rukwa

C. Kilimanjaro, Morogoro na Iringa D. Lindi na Shinyanga E. Ruvuma, Kigoma na Njombe [       ]

27.Aina ya njia ambayo vitu vyenye maumbo ya kijometriki kama vile maumbo ya pembe tatu, piramidi na pembe nne hufinyangwa huitwa:__

A. njia pindi B. michoro pacha C. maumbo ya pembe tatu D. njia bapa [       ]

28.Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ilijengwa na Wareno kuanzia mwaka 1593 na kukamilika mwaka 1596. Je, ngome hii ilijengwa katika mji gani?__ 

A. Malindi B. Kilwa C. Mombasa D. Bagamoyo E. Pangani [       ]

29.Kundi lipi linawakilisha wamisionari kati ya haya yafuatayo? _______

A. Vasco Da Gama na Dr. Livingstone B. Vasco Da Gama na Otto Von Bismark C. Karl Petters na Vasco Da Gama D. Karl petters na Dr. Livingstone E. Johann Ludwig Krapf na Johannes Rebmann [       ]

30.Mjumbe wa kwanza wa wafanyabiashara kutoka ujerumani aliyetumwa kuja kufanya mikataba na machifu alikuwa ni nani?__ A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. William Mackinoon D. Dr. Livingstone E. Isike [       ]

31.Umwinyi ni mfumo wa kinyonyaji uliyokuwa umeshamiri katika sehemu gani ya Tanzania? _____ 

A. Kigoma B. maeneo ya pwani C. magharibi mwa ziwa Viktoria D. maeneo ya Kusini E.Singida [       ]

32.Mreno wa kwanza kufika Pwani ya Afrika Mashariki alikuwa ni yupi? _____ 

A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. William Mackinoon D. Dr. Livingstone E. Julius Von Soden [       ]

33.Tanganyika ilianza kutawaliwa na waingereza mwaka 1918. Hii ni baada ya tukio gani?

A. Vita vya Maji maji B. Vita vya pili vya dunia C. Vita vya Sangu Bena D. Vita vya kwanza vya dunia E. mkutano wa Berlin na mkataba wa Heligoland [       ]

34.Ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na wafanyakazi, wakoloni walijenga miundombinu ya usafirishaji hapa Tanganyika. Bandari za tanga na Dar es Salaam zilijengwa na wakoloni wa taifa gani? _____

A. Waigereza B. Wareno C. Wajerumani D. Wafaransa E. Wabelgiji [       ]

35.Reli ya Tanga hadi Moshi ilianza kujengwa mwaka 1893 na kumalizika mwaka gani? _____ 

A. 1899 B. 1897 C. 1900 D. 1911 E. 1918 [       ]

36.Vita vya Maji maji vilianza kupiganwa mwaka 1905 na kumalizika mwaka _____ 

A. 1960 B. 1914 C. 1940 D. 1945 E. 1907 [       ]

37.Mganga wa jadi kutoka kabila la Wamatumbi aliyeongoza vita vya Maji maji dhidi ya Wajerumani alijulikana kwa jina la _____ 

A. Chifu Mangungo B. Mtwa Mkwawa C. Mtemi Isike Mwana Kiyungi D. Abushiri Bin Sultani E. Kinjekitile Ngwale [       ]

38.Vitu vyote katika ramani hutafsiriwa katika sehemu ya ramani ijulikanayo kama ______ 

A. ufunguo B. dira C. kipimio D. kichwa cha ramani E. mipaka ya ramani [       ]

39.Sanaa imegawanyika katika makundi mangapi? ___

A.mawili B. matatu C. manne D. matano E. sita [       ]

40.Nyuzi moja (1o) ya longitudo ni sawa na _______ 

A. dakika 15 B. dakika 4 C. saa 24 D. dakika 60 E. siku 3651/4 au 366 [       ]

SEHEMU B: Jaza nafasi zilizoachwa wazi

41.Taja vipindi viwili tu vya majira ya mwaka. i. . . . . . . . . . . . ... . . . . .. ii. . . . . . . . . . . . . . ..

42.Kabla ya kuingia kwa wakoloni katika Pwani ya Afrika Mashariki, walitanguliza vitangulizi vyao. Taja vitangulizi viwili tu vya wakoloni waliokuja Tanganyika. 

i. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

ii. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

43.Kuna aina kuu mbili za ramani ambazo ni ramani ya . . . . . . . . . . . . . na . . . . . . . . . . . . . . .

44.Jumuiya inayojumuisha nchi zilizopo upande wa Mashariki mwa Afrika ambayo Tanzania ni mwanachama hujulikana kwa jina la: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

45.Kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine kilitokea mwaka . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 22  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 22  

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
  4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
  5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
  6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

  1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
  2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
  3. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

Kwa swali 1-40, tafuta majibu kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya OMR uliyopewa.

1. Inaelezwa kwamba mwanadamu amezungukwa na vitu mbalimbali. Ni istilahi ipi kati ya zifuatazo inasadifu vitu vyote vinavyomzunguka mwanadamu?

A: Uoto B: Anga hewa C: Makazi D: Mazingira E: Milima [       ]

2. Mwaka jana tulitembelea kituo cha hali ya hewa, lengo letu kuu lilikuwa kujifunza kuhusu vipengele vya hali ya hewa na vipimio vyake. Mmoja wa wataalamu wa hali ya hewa alituambia kuwa kuna vipimio mbalimbali vya vipengele vya hali ya hewa. Unadhani ni kipimio gani alituambia kuwa kinatumika kupimia kasi ya upepo?

A: Kipima mvua B: Anemomita C: Baromita D: Kipimajoto E: Kipima mwelekeo wa upepo [       ]

3. Nini mchango wa misitu katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la ozoni unaosababishwa na moshi wa viwandani?

A: Misitu inasaidia kunyonya gesi zinayosababisha uharibifu wa ozoni. B: Misitu inachangia kasi ya ongezeko la gesi zinazoharibu tabaka la ozoni. C: Misitu ni vyanzo vya moshi unaoharibu tabaka la ozoni. D: Misitu haihusishwi katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la ozoni. E: Misitu huimarisha tabaka la ozoni. [       ]

4. Umepewa vipengele muhimu kuhusu mzunguko wa maji; Upozaji, Maji tiririka ardhini, Mvua na Uvukizi. Bainisha mtiririko sahihi wa vipengele hivi kutoka cha kwanza hadi cha mwisho.

  1. Mvua > Upozaji > Maji tiririka ardhini > Uvukizi
  2. Upozaji > Uvukizi > Mvua > Maji tiririka ardhini
  3. Maji tiririka ardhini > Uvukizi > Upozaji > Mvua
  4. Uvukizi > Upozaji > Mvua> Maji tiririka ardhini
  5. Maji tiririka ardhini > Uvukizi> Upozaji > Mvuke [       ]

5. Mimi na Bello tulikuwa na majadiliano kuhusu madhara ya wingi wa watu. Rafiki yangu Bello alijitahidi kuorodhesha madhara mengi kadiri alivyoweza. Unadhani ni lipi kati ya yafuatayo hakulitaja?

A: Uchafuzi unaosababishwa na ongezeko la uzalishaji na utumiaji. B: Matumizi ya rasilimali kupita kiasi C: Ukosefu wa ajira D: Upungufu wa ardhi na rasilimali nyinginezo E: Maendeleo kutokana na matumizi sahihi ya rasilimali. [       ]

6. Afrika Mashariki ni moja ya sehemu za bara la Afrika ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali za asili kama vile; madini, vyanzo vya maji na milima. Unadhani Ndulu alitoa jibu gani alipotakiwa kutaja mto mrefu kuliko yote Afrika?

A: Mto Malagarasi B: Mto Rufiji C: Mto Kongo D: Mto Tana E: Mto Nile [       ]

7. Bw. Bakari anaishi katika kijiji cha Kilolo ambacho kipo mita 2700 juu ya usawa wa bahari. Bw. Buli anaishi katika mji wa Kyala uliopo mita 111 juu ya usawa wa bahari. Wanapokutana Bw. Buli hulalamika kwamba katika mji wake kuna kiwango cha juu cha joto wakati Bw. Bakari hueleza kwamba katika mji wake kuna kiwango cha chini cha joto. Unadhani ni kwa nini Bw. Bakari anapata kiwango hicho cha joto?

A: Kwa sababu anaishi nyanda za chini B: Kwa sababu anaishi nyanda za juu zaidi C: Hasemi ukweli D: Hana sweta E: Anaumwa [       ]

8. Wakati wanadamu wakipambania uhai wao, wanajikuta wakiharibu mazingira bila kujua. Kwa kufanya hivyo baadhi ya watu kama vile wakulima wanachoma vichaka kwa ajili ya kilimo na wafugaji kufuga wanyama wengi kwenye eneo dogo. Unafikiri shughuli hizo zina madhara gani?

A: Uwepo wa mvua nyingi B: Ongezeko la ujazo wa maji katika vyanzo vya maji C: Husababisha mmomonyoko wa ardhi D: Kuganda kwa maji katika mito na maziwa E: Ongezeko la uoto wa asili [       ]

9. Shalibu ni mwalimu mzoefu anayefundisha katika shule ya msingi Mtakuja. Alialikwa na mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii aje kutuelezea mambo muhimu yanayoathiri hali ya hewa Tanzania. Ni jambo lipi kati ya yafuatayo unadhani halikutajwa na mwalimu Shailibu?

A: Upepo B: Uoto wa asili C: Umbali kutoka baharini D: Mvua E: Latitudo [       ]

10. Tulipotembelea Mlima Kilimanjaro, tuliarifiwa na wenyeji kuwa mlima huo unatokana na volkano. Mlima huo umezungukwa na wakazi ambao wengi wao ni wakulima. Bw. Bilu ambaye ni mwalimu wetu alitaka kujua ni kwa nini upande mmoja wa mlima ni mkame karibia mwaka mzima. Je, ni jibu gani sahihi alipata kutoka kwa wenyeji hao?

A: Upande huo upo juu sana B: Ni upande wa mwelekeo wa upepo C: Wanyama wengi wanaishi upande huo D: Watu waishio upande huo huharibu mazingira E: Ni upande wa mlima unaopokea pepo kavu. [       ]

11. Dunia ni sayari ya tatu katika mfumo wa jua. Ni sayari pekee inayosemekana kuwa na viumbe hai. Ina aina mbili za mizunguko ambayo ni kulizunguka jua na kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake. Yafuatayo ni matokeo ya dunia kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake ISIPOKUWA.

A: Kutokea kwa afelioni na perihelioni B: Kutokea kwa mchana na usiku C: Kupwa na kujaa kwa maji baharini D: Uwepo wa utofauti wa muda sehemu mbalimbali E: Mabadiliko ya siku [       ]

12. Tanzania ni nchi mojawapo Afrika inayotumia bidhaa za kitamaduni kuvutia watu mbalimbali kutoka nchi za Ulaya na kwingineko. Watu hao wanapotembelea nchi hii hununua bidhaa hizo hivyo kukuza pato la taifa. Ni kabila gani nchini Tanzania ni maarufu katika uchongaji wa vinyago?

A: Wamasai B: Wamakonde C: Wakurya D: Wahadzabe na Watindiga E: Wazaramo [       ]

13. Mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii darasa la tatu alimtaka mwanafunzi ataje baadhi ya makabila yanayopatikana Tanzania, chimbuko na ngoma zao za asili.

A: Wachaga, Kilimanjaro, Mdundiko B: Wanyakyusa, Dodoma, Mdumange C: Wapogoro, Morogoro, Sangula D: Wapare, Kilimanjaro, Iringi E: Wangoni, Ruvuma, Sindimba [       ]

14. Moja ya ajenda inayojadiliwa duniani kwa sasa hasa katika nchi zinazoendelea ni ajira kwa watoto. Imeenea sana kiasi cha kuwanyima watoto haki yao ya elimu. Ukiwa kama ni mtaalamu wa kutetea haki za watoto, ungewezaje kutatua tatizo hilo nchini Tanzania?

A: Kuwa na misingi imara ya mila na desturi hizo. B: Kwa kuanzisha maeneno ya kilimo C: Kuwatenga watoto hao na jamii. D: Kuelimisha jamii juu ya madhara ya tamaduni hiyo. E: Kuwaita waajiri wa jamii husika ofisini kwako. [       ]

15. Tunaiitaje hali ya nchi huru kuendelea kutawaliwa kijamii, kisiasa na kiuchumi na koloni lake?

A: Ubeberu B: Ukoloni C: Ukoloni mamboleo D: Utandawazi E: Ubepari [       ]

16. Shitundu aliambiwa ataje jina la vuguvugu la waafrika duniani kote lililokuwa na lengo la kupinga ukandamizaji na unyonyaji. Unadhani lipi lilikuwa ni jibu lake sahihi?

A: Ukoloni mamboleo B: Uafrika C: Muungano wa Afrika (Pan Afrika) D: Utandawazi E: Ukombozi [       ]

17. Kama ungeambiwa utoe sababu kwanini juhudi za waafrika za kupinga uvamizi wa kikoloni zilishindwa. ungetoa jibu gani?

A: Wazungu walikuwa wengi kuliko waafrika B: Waafrika walikuwa ni wazee sana C: Waafrika walitumia silaha duni na mbinu hafifu za kivita D: Wazungu walitumia uchawi E: Kulikuwa na baa la njaa Afrika [       ]

18. Zama za mawe ziligawanyika katika vipindi mbalimbali. Maisha ya binadamu yalitofautiana kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ni katika zama ipi ambapo binadamu aliacha kula vyakula vibichi?

A: Zama za kati za mawe B: Zama za mwisho za mawe C: Zama za chuma D: Zama za mawe za kale E: Zama za teknolojia ya kisasa ya kidigitali [       ]

19. Kwa sasa dunia imegubikwa na muingiliano wa watu unaofanya dunia kuonekana kama kijiji kimoja. Je, hali hiyo inaitwaje?

A: Utandawazi B: Kupanda kwa joto duniani C: Uundaji wa vijiji D: Mahusiano E: Ukoloni mamboleo [       ]

20. Wakati wa mapambano ya kukomesha biashara ya utumwa Afrika Mashariki. Upi kati ya mikataba ifuatayo ulijulikana kihistoria kama mkataba wa kubadilishana suruali na kifungo?

A: Mkataba wa Frere wa 1873 B: Mkataba wa Moresby wa 1822 C: Mkataba wa Hermarton wa 1845 D: Mkataba wa mipaka wa 1886 E: Mkataba wa Heligoland wa 1890 [       ]

21. Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Wakati huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza. Je, ni Gavana yupi wa kingereza aliyemkabidhi madaraka?

A: Horace Byatt B: Donald Cameron C: Julius Von Soden D: Richard Turnbull E: Edward Twinning [       ]

22. Ni tukio gani liliathiri awamu ya pili ya maendeleo ya kiuchumi Tanzania kati ya 1967 na 1985? 

A: Mapokeo ya itikadi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa. B: Kung’atuka kwa mwalimu Nyerere kutoka madarakani C: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar D: Kutangazwa kwa Azimio la Arusha E: Vita ya Tanzania na Uganda [       ]

23. Mkutano wa Berlin ulifanyika nchini Ujerumani toka mwezi Novemba 1884 hadi Februari 1885. Lengo la mkutano huo ambao uliongozwa na Otto Von Bismarck lilikuwa ni kuligawa bara la Afrika. Ni mwaka gani Zanzibar ilikabidhiwa kwa Uingereza?

A: 1890 B:1886 C: 1885 D:1980 E: 1887 [       ]

24. Unaishi katika mazingira yenye uhaba wa mvua. Ni mazao yapi kati ya haya yafuatayo utawashauri watu wanaoishi katika eneo hilo wayapande ili kuepukana na uhaba wa chakula?

A: Mihogo, Mtama na Ulezi B: Ulezi, Maharage na Mahindi C: Mtama, Maharge na Kahawa D: Pamba, Mihogo na Mpunga E: Mpunga, Mtama na Ulezi [       ]

25. Kuna aina mbalimbali za madini zinazopatikana nchini Tanzania. Madini haya huwezesha nchi kukua kiuchumi. Ni madini gani yapatikanayo mkoani Manyara ambayo huingizia nchi yetu fedha za kigeni?

A: Dhahabu B: Shaba C: Almasi D: Chuma E: Tanzanite [       ]

26. Mnamo mwaka 2022 nchi yetu ya Tanzania iliendesha sensa ya watu na makazi kwa lengo la kujua idadi ya watu nchini. Endapo utatakiwa kutaja mwaka ambao sensa inayofuata itafanyika, lipi litakuwa ni jibu lako?

A: 2032 B: 2025 C: 2030 D: 2042 E: 2026 [       ]

27. Bw. Chebo ambaye ni mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii, aliwaagiza wanafunzi wa darasa la saba wachore ramani ya bara la Afrika. Ni aina gani ya kipimio cha ramani kati ya hivi vifuatavyo kitawafaa kuchora ramani hiyo?

A: Kipimio cha mstari B: Kipimio cha sentenso C: Kipimio kidogo D: Kipimio cha kati E: Kipimio kikubwa [       ]

28. Wakati wa somo la Maarifa ya Jamii, Bi. Limbo aliwafundisha wanafunzi wake kwamba mistari ya latitudo ina majina tofauti kulingana na nyuzi na maeneo husika. Je, latitudo yenye nyuzi 66½ kusini mwa ikweta hujulikana kwa jina gani?

A: Ikweta B: Meridiani Kuu C: Tropiki ya Kansa D: Duara la antaktiki E: Duara la aktiki [       ]

29. Mojawapo ya vitendo haramu katika ujasiriamali ni kuuza bidhaa ambazo zipo chini ya kiwango ambazo zinaweza kusababisha madhara kwa watumiaji. Ni mamlaka ipi ya serikali inahusika katika kusimamia viwango vya bidhaa za wajasiriamali nchini Tanzania?

A: TMAA B: TRA C: TBC D: TCRA E: TBS [       ]

30. Tausi amehitimu elimu ya Chuo Kikuu na kwa bahati mbaya hajaajiriwa na serikal hivyo ameamua kuanzisha biashara. Unafikiri ni kitu gani kitakuwa ni cha kwanza kuzingatiwa na Tausi?

A: Faida B: Mpango biashara C: Barabara D: Hatari E: Bima [       ]

31. Kwa nini tunashauriwa kuepuka kutumia vyombo vya chuma kuhifadhia sharubati?

A: Vinapoza sharubati B: Vinaharibu sharubati C: Vinaharibu ladha ya sharubati D: Vinabadili matunda matamu kuwa machungu E: Vina ujazo mdogo [       ]

32. Bwana Mbimbi alitaka kujua Rwanda na Burundi zilikuwa chini ya utawala gani wa kikoloni kabla ya vita kuu ya dunia. Ni jibu gani sahihi angetakiwa kupewa?

A: Utawala wa Kiarabu B: Utawala wa Kijerumani C: Utawala wa Kiingereza D: Utawala wa Kibelgiji E: Utawala wa Kifaransa [       ]

33. Mwanafunzi wa darasa la tatu alitakiwa kutaja faida tano za kupanda miti katika mazingira yetu. Endapo angelitoa majibu yafuatayo, ni herufi gani inaonesha jibu lisilo sahihi?

A: Kupata kivuli kwa ajili ya mifugo na watu B: Kupata madini C: Kuzuia mmomonyoko wa udongo D: Kuongeza rutuba kwenye udongo E: Kusaidia kuleta mvua [       ]

34. Wakati wa somo la Maarifa ya Jamii darasa la sita, nilitaka wanafunzi wangu wataje faida ambazo nchi ya Tanzania imezipata kutokana na kupanuka kwa biashara ya kimataifa na walizitaja. Ni ipi kati ya hizi zifuatazo ilikuwa sahihi zaidi kuliko nyingine?

A: Kupungua kwa wajasiriamali wa ndani B. Kupungua kwa mikataba ya kibiashara C: Kuongezeka kwa uzalishaji D. Watu watatembelea nchi nyingi E: Kuongezeka upatikananji wa fedha za kigeni [       ]

35. Jamii za kitanzania kabla ya ukoloni zilikuwa na mila na desturi zake. Lipi kati ya haya yafuatayo halikuwa lengo mahususi katika jamii hizo?

A: Kuwafanya watu wajenge nyumba kubwa na kufuga wanyama wengi B: Kuendeleza kufanya kazi kwa bidii C: Kuimarisha usawa katika uzalishaji na mgawanyo wa rasilimali D: kuheshimu na kukuza tabia njema E: Kuhimiza malezi ya wazazi katika jamii [       ]

36. Upatikanaji wa uhuru katika mataifa mbalimbali ya Afrika, ulitokana na juhudi za mashujaa wengi wa Afrika. Nani kati ya hawa wafuatao hawakuwa kati ya viongozi waliopigania uhuru katika nchi za kiafrika?

A: Jomo Kenyata and Robert Mugabe B: Samora Machel and Patrick Lumumba C: Kwame Nkrumah and Julius K. Nyerere D: Milton Obote and Nelson Mandela E: Mobutu Seseseko and Yoweri Museveni [       ]

37. Ili kuwatawala waafrika, wazungu walitumia mbinu anuai. Ni ipi kati ya njia zifuatazo ilitumiwa na wazungu ili kuanzisha utawala wa kikoloni barani Afrika?

A: Kutoa huduma mbalimbali za kijamii B: Kuanzisha biashara ya utumwa C: Kugawa vyakula na mavazi D: Kusaini mikataba ya uongo E: Kujenga reli na barabara [       ]

38. Wakati Bi. Chedo anamuelekeza binti yake namna ya kunyoosha nguo, Alimuonesha hatua zifuatazo, isipokuwa moja. Hatua hiyo ni ipi?

A: Kulowesha nguo kwenye maji B: Kuwasha pasi C: Kunyoosha mikono D: Kunyoosha mapindo E: Kunyoosha mbele na nyuma ya nguo [       ]

39. Mwanafunzi wa darasa la saba alitaka kujua kutoka kwa mwalimu wake wa somo la Stadi za Kazi, ni kwa nini wauzaji wengi wa viatu huweka karatasi au matambara ndani ya viatu. Unadhani mwanafunzi huyu alipewa jibu gani?

A: Husaidia kung’arisha viatu B: Ili viuzike kwa urahisi C: Ili kurahisisha uning’inizaji wa viatu juu D: Huvifanya viatu vibakie na mwonekano wake wa asili E: Hufanya viatu visitoboke [       ]

40. Kitanda ni mojawapo ya vitu muhimu vinavyohitajika katika sehemu ya kulala. Kitanda kizuri na imara ni muhimu kwa afya ya binadamu yeyote. Katika muktadha huo, kuna umuhimu gani wa mtu kulala akiwa amenyooka? 

A: Inamfanya mtu aonekane safi B: Inasaidia kulinda uti wa mgongo na viungo vingine ndani ya mwili wa mwanadamu C: Inatengeneza mahusiano mazuri ya kifamilia D: Inafanya mwili kuwa na nguvu E: Inamfanya mtu afurahie usingizi [       ]

SEHEMU B: (Alama 10)

Andika jibu sahihi kwa kila swali la 41-45 katika nafasi iliyoachwa wazi nyuma ya karatasi ya OMR. Tumia kalamu ya wino mweusi au wa buluu.

 

41. Kipindi nafanya kazi katika Baraza la Taifa la Mzingira (NEMC) Niliwashauri wananchi wa kijiji cha Nkisi kutumia vyanzo vya nishati mbadala kama njia mojawapo ya kupambana na uharibifu wa mazingira. Taja vyanzo mbadala viwili nilivyowaelekeza kuvitumia.

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

42. Wanafunzi wa darasa la saba walimuuliza mwalimu wao wa somo la Maarifa ya Jamii kwa nini Afelioni na Periherioni hutokea wakati dunia ikilizunguka jua. Unadhani jibu gani ni sahihi?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

43. Chiwili ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita alitakiwa na mwalimu wake wa somo la Stadi za Kazi ataje faida moja wapo ya kutandaza majani shambani.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

44. Ni miaka mingapi iliyopita toka binadamu alipoanza kutengeneza historia yake duniani?

45. Bw. Saliboko mjasiriamali mdogo toka katika kijiji cha Mabuku, alitaka kujua maana ya neno “biashara” kutoka kwa Lanja ambaye ni mfanyabiashara mkubwa. Unadhani ni jibu gani alipewa?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 18  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 18  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
  2. Jibu maswali yote
  3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
  4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
  5. Tumia penseli ya HB tu.
  6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Mr. Msabila aliishi kwa miaka 130. Lipi kati ya kauli zifuatazo ni sahihi kuhusu Bw. Msabila

(A) aliishi miaka elfu moja na karne 13 (B) aliishi miongo 130 (C) aliishi kwa karne moja na miongo 3 (D) aliishi kwa karne 13 (E) aliishi kwa karne moja na miongo 30 [     ] 

2. Miundo mbinu maana yake ni barabara, reli na mawasiliano,.Ni mikoa gani ya Tanzania imepitiwa na reli ya TAZARA. 

(A) Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Tabora na Kigoma (B) Kilimanjaro, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam (C) Morogoro, Manyara, Tanga na Pwani (D) Mbeya, Dar es Salaam, Njombe, Morogoro, Songwe na Iringa (E) Kigoma, Mbeya na Tanga [     ]

3. Wanafunzi wa darasa la tatu walifundishwa kuhusiana na hali ya hewa. Ni kifaa gani wanafunzi hutumia kupima miale ya jua? 

(A) Oktas (B) Barometa (C) Anemometa (D) Haigrometa (E) Compbell stock [     ]

4. Wanafunzi wa shule ya Msingi Azimio walipewa zoezi la kurekodi jotoridi kwa siku tano. Matokeo ya siku ya kwanza hadi ya tano yalikuwa kama ifuatayo; 19.5oC, 25.3oC, 30oC, 27.2oC na 20.5oC. Tafuta wastani wa jotoridi. 

(A) 21.5oC (B) 23.5 oC (C) 24.5 oC (D) 19.5 oC (E) 25.5 oC [     ]

5. Kuna aina tofauti za majanga yanayotokea katika mazingira yetu. Lipi kati ya yafuatayo limesababishwa na nguvu za asili na shughuli za binadamu? 

(A) kimbumba (B) mmomonyoko wa udongo (C) tsunami (D) tetemeko la ardhi (E) mlipuko wa volcano [     ]

6. Mazingira yanaundwa na vitu mbalimbali ni aina gani ya mazingira ambayo vitu hivyo hupatikana chaki, ubao na madaftari. 

(A) dukani (B) nyumbani (C) mahakamani (D) sokoni (E) shuleni[     ] 

7. Tetemeko la ardhi, tsunami, moto, mafuriko na ukame ni baadhi ya majanga ya asili. Ni janga lipi kati ya yafuatayo linasababishwa na ukataji wa miti

(A) tetemeko la ardhi (B) ukame (C) mafuriko (D) tsunami (E) moto [     ]

8. Ili ramani ikamilike inatakiwa iwe na vipengele vitano muhimu, kipengele kipi kinaonyesha mipaka ya ramani 

(A) jina la ramani (B) pambizo (C) ufunguo (D) dira (E) kipimio [     ] 

9. Yapo makundi matatu ya vitangulizi vya ukoloni kundi lipi lilikuwa la pili kuwasili Afrika

Mashariki? (A) makabuni (B) wamisionari(C) mapebari (D) wapelelezi(E) wafanya biashara[     ] 

10. Vita vya majimaji vilianza kupiganwa mwaka 1905 – 1907. Dhidi ya wajerumani, nani alikuwa kiongozi wa vita hivyo? 

(A) Kinjekitile ngwale (B) Chifu Mirambo (C) Hassani Makunganya (D) Abushiri (E) Mkwawa [     ]

11. Zifuatazo ni sehemu za kihistoria zipatikanazo Tanzania isipokuwa__________

(A) Rusinga (B) Olduvai (C) Engaruka (D) Kondoa Irangi (E) Kaole [     ]

12. Shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mto Msimbazi zinaathari kwa jamii inayozunguka mto huo, ni athari gani husababishwa kwa kukata miti pembezoni mwa mto?

(A) uhaba wa maji kwa matumizi ya binadamu (B) uchafunzi wa hali ya hewa (C) ardhi kupoteza rutuba (D) kukauka kwa vyanzo vya maji (E) kushuka kwa uzalishaji samaki [     ]

13. Bwana Hatibu hutoka jasho kwa wingi wakati wa msimu wa joto. Je utamshauri avae nguo za rangi gani? 

(A) nyeupe (B) nyeusi (C) blue (D) njano (E) kijani [     ]

14. Bwana Salimu ni mfugaji ambaye huhama hama na idadi kubwa ya mifugo. Ni madhara gani husababishwa na aina hii ya ufugaji? 

(A) mafuriko (B) kustawi kwa uoto wa asili (C) kufa kwa mifugo (D) kupotea kwa misitu (E) uharibifu wa mazao [     ]

15. Bwawa la Nyerere ni mojawapo ya chanzo kinachotarajiwa kuzalisha nishati ya umeme wa maji nchini Tanzania. Je bwawa hili limejengwa katika mto gani?

(A) Ruaha (B) Ruvuma (C) Ruvu (D) Rufiji (E) Pangani [     ]

16. Mtalamu wa madini alitembelea wanafunzi wa darasa la saba na kuwafundisha aina ya madini na kazi zake. Je madini gani hutumika kukatia vioo?

(A) dhahabu (B) almasi (C) fedha (D) Tanzanite (E) Shaba [     ]

17. Maji ni maendeleo kwa jamii na kiuchumi nchini Tanzania. Bainisha vyanzo vikuu vitatu vya rasilimali hiyo? 

(A) mvua, bahari na maziwa (B) bahari, visima na mito (C) mvua, maji yaliyo juu ya nchi ya ardhi (D) maziwa, mito na chemuchemu (E) visima, chemchem na mvua [     ]

18. Kupungua kwa theluji katika mlima Kilimanjaro kumesababishwa na ongezeko la joto katika uso wa dunia. Ni shughuli ipi inaweza kutumika kukabiliana na tatizo hilo?

(A) kuchoma misitu na kukata miti (B) kulima kandokando ya mlima (C) kupanda miti na kutunza mazingira (D) uvunaji ovyo wa misitu (E) kufuga mifugo mingi kwenye eneo dogo [     ]

19. Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kuburudisha na kuunganisha raia wake. Ni taasisi ipi inayohusika katika kusimamia na kuendeleza michezo nchini Tanzania? 

(A) BASATA (B) BAKITA (C) TUKI (D) BMT (E) TFF [     ]

20. Kila jamii nchini Tanzania ina michezo yake ya asili kulingana na mazingira, muda na utamaduni. Ipi ni mifano ya michezo hiyo? 

(A) mpira wa miguu, ngumi na kukimbia (B) kukimbia, kuogelea na mpira wa miguu (C) kurusha mkuki, kuruka kamba na kukimbia (D) mpira wa miguu, pete na kuogelea (E) mpira wa kikapu, mguu na pete [     ]

21. Katika uso wa dunia kuna pepo zinazovuma kutoka eneo moja kwenda jingine. Je ni upepo gani unavuma kutoka kusini kuelekea kaskazini? (A) upepo wa kusi (B) upepo wa kaskazini (C) upepo mkavu (D) upepo wa magharibi (E) upepo wa unyevu [     ]

22. Tanzania ina makabila mengi yenye mila nzuri na potofu. Ni mila ipi yenye madhara kwa jamii?

(A) kuruhusu wanawake wajawazito kula mayai (B) kukeketa watoto wa kike (C) kufundisha wavulana pamoja na wasichana maadili (D) kutahiri wavulana (E) kuwapa wanawake haki sawa na wanaume [     ]

23. Kuongezeka kwa joto duniani unasababishwa na shughuli za kibinadamu. Ipi si madhara yanayosababishwa na ongezeko la joto nchini Tanzania? 

(A) kuyeyuka kwa theluji katika mlima Kilimanjaro (B) kupotea kwa bayoanuai (C) kuongezeka kwa kina cha maji baharini (D) kuongezeka kwa uoto wa asili (E) kutokea kwa ukame [     ]

24. Ni kwa namna gani jamii inaweza kukabiliana na mila na tamaduni zilizopitwa na wakati?

(A) kudumisha umoja wa taifa (B) kudumisha misingi ya uzalendo (C) kuwa na misingi ya mila na desturi zinazofanana (D) kupenda jamii na taifa (E) kufanya majadiliano na jamii inayohusika [     ]

25. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anatambulika kama “baba wa taifa” aliyestaafu kwa hiyari mwaka 1985. Je, alistaafu karne ya ngapi? 

(A) 19 (B) 21 (C) 20 (D) 22 (E) 18 [     ]

26. Yafuatayo yaweza kutokea kwa taifa linalokuza utamaduni wake isipokuwa________

(A) kudumisha misingi ya uzalendo (B) kuiga tamaduni za kigeni (C) kudumisha umoja (D) kulinda asili yake (E) kuwepo kwa uhusiano mzuri katika jamii [     ]

27. Magret anaipenda nchi yake ana moyo wa kujitoa kwa taifa lake na ni mtunzaji mzuri wa rasilimali za taifa. Magreti anaweza kuwa na sifa ipi kwa taifa lake?

(A) mlinzi wa rasilimali za nchi (B) mzalendo kwa taifa lake (C) mtunzi wa miiko ya jamii (D) mlinda usalama wa jamii (E) msimamizi wa umoja wa wananchi [     ]

28. Licha ya kugawanywa kwa bara la Afrika katika mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 – 1885 Afrika iligawanywa tena baada vita vya kwanza vya dunia miongono mwa mataifa ya ulaya isipokuwa______

(A) ufaransa (B) haha (C) ubelgiji (D) ureno (E) ujerumani [     ]

29. Katika ujasiriamali neno thubutu linamaanisha nini?

(A) kuwa na maamuzi magumu (B) uzembe katika kufanya maamuzi (C) uwe tayari kujitolea (D) kusababisha hasara kwa makusudi (E) kuwa jasiri kuchukua hatua [     ]

30. Kitu gani kinaweza kuchangia kukua kwa uzalishaji mali nchini Tanzania?

(A) uwepo wa mifumo rafiki ya kisera na kisheria (B) uwapo wa viwanda vingi nchini (C) kukaribisha uwekezaji kutoka nje ya nchi (C) kuwa na amani na utulivu mijini (D) kutangaza vivutio vya ulaya [     ]

31. Viatu ni sehemu ya sare ya shule. Kwa nini wanafunzi wanashauriwa kutovaa viatu vyenye visigino virefu? 

(A) husababisha maumivu ya tumbo (B) husababisha maumivu ya magoti (C) husababisha maumivu ya kichwa (D) husababisha maumivu ya misuli (E) husababisha maumivu ya kifua [     ]

32. Familia inapokuwa na wazazi na watoto hujulikana kama familia ya baba, mama na watoto (nyuklia family). Familia hii itaitwaje endapo wazazi hapo watafariki

(A) familia pana (B) familia ya watoto (C) failia ya watoto yatima (D) familia tegemezi (E) familia ya watoto wa mtaani [     ]

33. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa na madini tofautitofauti ni kundi lipi linajumuisha madini yatumikayo kwa urembo? 

(A) dhahabu, chumvi na chuma (B) almasi ruby na tanzanaiti (C) almasi, dhahabu na chuma (D) kobati, rubi na tanzanaiti (E) chumvi, dhahabu na chuma [     ]

34. Umemtembelea shangazi yako na umepewa chumba kichafu. Ni ugonjwa gani unaweza kukupata ukilala chumba hicho? 

(A) kuharisha na kutapika (B) kukohoa na kutapika [     ] (C) mafua na maumivu ya kifua (D) kuharisha na mafua (E) homa na maumivu ya kifua

35. Mwalimu wa somo la stadi za kazi aliwaongoza wanafunzi kuunda chungu na kuwapa mbinu namna ya kukikausha chungu hicho. Kwa nini ni muhimu kukausha chungu hicho?

(A) kukifanya kiwe imara (B) kukifanya kiwe na rangi nyeusi (C) kukipendezesha (D) kukifanya kiwe na harufu nzuri (E) kukifanya kiwe chepesi [     ]

36. Mimi ni mbunifu, mthubutu na mchapakazi kwa ajiliya kutimiza malengo yangu mimi ni nani?

(A) mjasiriamali (B) mbunifu (C) mfanyabiashara (D) mnunuzi (E) muuzaji [     ]

37. Rangi nyekundu kwenye nembo ya taifa huwakilisha nini? 

(A) maliasili (B) uhuru na umoja (C) mipaka ya nchi (D) uoto wa asili (E) udongo wenye rutuba [     ]

38. Maisha ya binadamu yamepitia zama ngapi? 

(A) 3 (B) 5 (C) 2 (D) 4 (E) 6 [     ]

39. Chama gani cha siasa kilichokipinga chama cha TANU wakati wa harakati za kudai uhuru hapa Tanzania? 

(A) TAA (B) ASP (C) ZPPP (D) AA (E) UTP [     ]

40. Ipo mifumo minne ya tawala za kikoloni Afrika. Je nani alikuwa mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma? 

(A) Fredrick Lugard (B) Donald Cameroon (C) Fredrick De Clark (D) Richard Turnbull (E) Karl Peters [     ]

SEHEMU B:

ANDIKA MAJIBU SAHIHI KATIKA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI KWENYE FOMU MAALUMU YA OMR KWA KUTUMIA KALAMU YA WINO

41. Je! ni jina gani ambalo linaelezea mahali ambapo mjasiriamali anaweza kuweka na kutoa fedha kwa ajili ya biashara?  ___________________________________________________________

42.Ni nyota gani ambayo ipo karibu zaidi na dunia?  ______________________________________

43.Ni zao gani ambalo hutumiwa kutengeneza sumu ya kuulia wadudu? ______________________

44. Mkusanyiko wa matone madogomadogo ya maji angani ni  ______________________________

45. Umoja wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, limetangazwa tarehe 7 Julai kila mwaka kwa siku ya Kiswahili duniani, eleza kwa kifupi umuhimu wa siku ya Kiswahili katika nchi ya Tanzania

 ______________________________________________________

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 8  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 8  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256