MAARIFA STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)
OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

 SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI DARASA: VII 

MUDA: SAA 1:30 

SEHEMU A:

 Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa  

1. Shughuli ipi kati ya hizi zifuatazo husababisha uharibifu wa mazingira? ______ 

A. Kupanda miti B. Ukataji miti ovyo C. Kilimo cha matuta D. Urejeleaji wa takataka E. kilimo mseto [       ]

2. Dunia hutumia muda gani kujizungusha nyuzi 15 za longitudo? ______

A. Dakika 4 B. saa 1 C. siku 1 D. mwaka mmoja E. saa 24 [       ]

3. Mkutano wa berlin ni mkutano uliojumuisha mataifa ya kibeberu kwa lengo la kugawana makoloni barani Afrika. Mkutano huu uliitishwa na nani?________ 

A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. Kansela Otto von Bismark D. umoja wa mataifa E. Sultani Seyyid Said [       ]

4. Ni sayari ipi katika mfumo wa Jua ambayo ipo karibu sana na Jua? ______ 

A. Zebaki B. Sumbula C. Zuhura D. Kausi E. Dunia [       ]

5. Yafuatayo ni matokeo ya dunia kujizungusha kwenye mhimili wake isipokua _____ 

A. kutokea kwa usiku na mchana B.madbadiliko ya muda kati ya longitudo moja na nyingine C. kupwa na kujaa kwa maji D. mabadiliko ya uelekeo wa upepo na mikondo ya bahari E. majira ya mwaka [       ]

6. Serikali ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro iliwashauri wakazi wake waishio maeneo ya mabondeni wahame kuepuka majanga yatokanayo na mvua. Lipi kati ya yafuatayo ni janga litokanalo na mvua kubwa?

A. mafuriko B. tetemeko la ardhi C. ukame D. mlipuko wa volkano E. vita [       ]

7. Mifugo mingi katika eneo dogo hupelekea: _______ 

A. Nyasi kuwa nyingi B. mimea kunawiri C. mmomonyoko wa udongo D. utajiri mkubwa kwa wafugaji E. ukosefu wa barabara [       ]

8. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa rasilimali nyingi sana yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo hupatikana Tanzania pekee. Madini ya Tanzanite hupatikana wapi? __ 

A. Mwadui Mkoani Shinyanga B. Uvinza mkoani

Kigoma C. Bagamoyo mkoani Pwani D. Manyoni mkoani Singida E. Mererani mkoani Manyara [       ]

9. Kiongozi wa koloni katika utawala wa Waingereza na Wajerumani aliitwa Gavana. Yupi kati wa wafuatao ni gavana katika utawala wa Wajerumani? _____

A. Horace Byatt B. Donald Kameroon C. Edward Twining D. Richard Turnbl E. Julius Von Soden [       ]

10.Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita kuu vya kwanza vya dunia, eneo la Tanganyika liliwekwa chini ya utawala wa Waingereza kwa udhamini wa umoja wa mataifa uliofahamika kwa jina la _____

A. UN B. League of Nations C. UNO D. UNHCR E. EAC [       ]

11.Mkataba uliofanyika mwaka 1890 kati ya serikali ya Uingereza na Ujerumani wenye madhumini ya kurekebisha mipaka ya mwaka 1886 ulijulikana kama _______

A. mkataba wa Hamaton B. mkataba wa freire C. mkataba wa Berlin D. mkataba wa Heligoland E. mkataba wa Vienna [       ]

12.Mfumo wa kwanza wa kiuchumi na kiutawala ambapo watu waliishi na kushirikiana pamoja uliitwa _____

A. Ujima B. Ujamaa C. Ubepari D. Ukabaila E. Umwinyi [       ]

13.Viongozi wa mwanzo wa bara la Afrika waliopinga uvamizi wa wakoloni katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii hujulikana kama: ______

A. magavana wa Afrika B. waafrika C. Mashujaa wa Afrika D. maliwali E. Wafadhili wa Afrika [       ]

14.Nani kati ya wafuatao siyo shujaa wa nchi yetu? _______ 

A. Mtwa Mkwawa B. Jomo Kenyatta C. Bibi Titi Mohamed D. Mwalimu J.K. Nyerere E. Mtemi Isike [       ]

15.Mtwa Mkwawa Mkwavinyika alijiua mwenyewe kwa kujipiga risasi baada ya kuona anakaribia kukamatwa na Wajerumani mwaka gani? ___ 

A. 1898 B. 1905 C. 1907 D. 1888 E. 1961 [       ]

16.Joseph alitaka kupata taarifa kuhusu matukio ya kihistoria ya nchi yetu. Unafikiri ni mahali gani angeweza kwenda ili lengo lake litimie?___

A. Maabari B. mbuga za wanyama C. makumbusho D. ikulu E. mgodini [       ]

17.Fuvu la binadamu wa kwanza liligunduliwa katika bonde la Olduvai Gorge mkoani Arusha mwaka 1959. Ni nani waliogundua fuvu hilo? _____ 

A. Dkt Mary George na Dkt George Lincolin B. Dkt. Louis Leakea na Dkt Mary Leakey C. Dkt George Louis na Dkt Mary Leakey D. Vasco Da Gama E. Carl Peters [       ]

18.Hali ya angahewa iliyorekodiwa katika kipindi cha muda mfupi hujulikana kama _____ A. Jotoridi C. Unyevunyevu B. mabadiliko ya tabianchi D. Tabia ya nchi E. Hali ya hewa [       ]

19.Ni mataifa yapi kati ya yafuatayo yaliitawala Tanganyika katika vipindi tofauti?__ 

A. Marekani na Ujerumani B. Ujerumani na Uingereza C. Ufaransa na Uingereza D. Ureno na Marekani E. Italia na uingereza [       ]

20.Kipi kati ya hivi vifuatavyo siyo kipengele cha hali ya hewa? ____ 

A. Jotoridi B. Kipimajoto C. Mvua D. Unyevuanga E. upepo [       ]

21.Fedha anazobakiwa nazo mfanyabiashara baada ya kuuza bidhaa na kutoa kiasi cha mtaji hujulikana kama:_

A. kodi B. hasara C. tozo D. akiba E. faida [       ]

22.Mambo ya kawaida yanayofanywa mara kwa mara na wanajamii ambayo huweza kubadilika kulingana na mahali na wakati hujulikana kama ____ 

A. mila B. miiko C. tambiko D. desturi E. lugha [       ]

23.Ufundi anaotumia mtu ili kuwasilisha fikra au mawazo yake katika namna inayoburudisha na kufikirisha huitwa ____ 

A. mila B. desturi C. tambiko D. Sanaa E. vinyago [       ]

24.Mfalme Leopold wa Ubelgiji alitambuliwa kuwa mtawala wa __________ 

A. Kongo B. Tanganyika C. Senegal D. Zimbabwe E. Lesotho [       ]

25.Bwana na Paulo amefunga ndoa mwaka 2021 na Bibi Sijali na hadi sasa wanaishi pamoja katika kijiji cha Mzogole wakiwa bado hawajapata mtoto. Hii ni aina gani ya familia? ____ 

A. Familia ya awali B. Familia pana C. Familia ya mke na mume D. familia ya watoto yatima E. familia ya mzazi mmoja [       ]

26.Mikoa ambayo ina ranchi za taifa ni ____

A. Dodoma, Tanga na Pwani B. Iringa, Njombe na Rukwa

C. Kilimanjaro, Morogoro na Iringa D. Lindi na Shinyanga E. Ruvuma, Kigoma na Njombe [       ]

27.Aina ya njia ambayo vitu vyenye maumbo ya kijometriki kama vile maumbo ya pembe tatu, piramidi na pembe nne hufinyangwa huitwa:__

A. njia pindi B. michoro pacha C. maumbo ya pembe tatu D. njia bapa [       ]

28.Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ilijengwa na Wareno kuanzia mwaka 1593 na kukamilika mwaka 1596. Je, ngome hii ilijengwa katika mji gani?__ 

A. Malindi B. Kilwa C. Mombasa D. Bagamoyo E. Pangani [       ]

29.Kundi lipi linawakilisha wamisionari kati ya haya yafuatayo? _______

A. Vasco Da Gama na Dr. Livingstone B. Vasco Da Gama na Otto Von Bismark C. Karl Petters na Vasco Da Gama D. Karl petters na Dr. Livingstone E. Johann Ludwig Krapf na Johannes Rebmann [       ]

30.Mjumbe wa kwanza wa wafanyabiashara kutoka ujerumani aliyetumwa kuja kufanya mikataba na machifu alikuwa ni nani?__ A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. William Mackinoon D. Dr. Livingstone E. Isike [       ]

31.Umwinyi ni mfumo wa kinyonyaji uliyokuwa umeshamiri katika sehemu gani ya Tanzania? _____ 

A. Kigoma B. maeneo ya pwani C. magharibi mwa ziwa Viktoria D. maeneo ya Kusini E.Singida [       ]

32.Mreno wa kwanza kufika Pwani ya Afrika Mashariki alikuwa ni yupi? _____ 

A. Karl Peters B. Vasco Da Gama C. William Mackinoon D. Dr. Livingstone E. Julius Von Soden [       ]

33.Tanganyika ilianza kutawaliwa na waingereza mwaka 1918. Hii ni baada ya tukio gani?

A. Vita vya Maji maji B. Vita vya pili vya dunia C. Vita vya Sangu Bena D. Vita vya kwanza vya dunia E. mkutano wa Berlin na mkataba wa Heligoland [       ]

34.Ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na wafanyakazi, wakoloni walijenga miundombinu ya usafirishaji hapa Tanganyika. Bandari za tanga na Dar es Salaam zilijengwa na wakoloni wa taifa gani? _____

A. Waigereza B. Wareno C. Wajerumani D. Wafaransa E. Wabelgiji [       ]

35.Reli ya Tanga hadi Moshi ilianza kujengwa mwaka 1893 na kumalizika mwaka gani? _____ 

A. 1899 B. 1897 C. 1900 D. 1911 E. 1918 [       ]

36.Vita vya Maji maji vilianza kupiganwa mwaka 1905 na kumalizika mwaka _____ 

A. 1960 B. 1914 C. 1940 D. 1945 E. 1907 [       ]

37.Mganga wa jadi kutoka kabila la Wamatumbi aliyeongoza vita vya Maji maji dhidi ya Wajerumani alijulikana kwa jina la _____ 

A. Chifu Mangungo B. Mtwa Mkwawa C. Mtemi Isike Mwana Kiyungi D. Abushiri Bin Sultani E. Kinjekitile Ngwale [       ]

38.Vitu vyote katika ramani hutafsiriwa katika sehemu ya ramani ijulikanayo kama ______ 

A. ufunguo B. dira C. kipimio D. kichwa cha ramani E. mipaka ya ramani [       ]

39.Sanaa imegawanyika katika makundi mangapi? ___

A.mawili B. matatu C. manne D. matano E. sita [       ]

40.Nyuzi moja (1o) ya longitudo ni sawa na _______ 

A. dakika 15 B. dakika 4 C. saa 24 D. dakika 60 E. siku 3651/4 au 366 [       ]

SEHEMU B: Jaza nafasi zilizoachwa wazi

41.Taja vipindi viwili tu vya majira ya mwaka. i. . . . . . . . . . . . ... . . . . .. ii. . . . . . . . . . . . . . ..

42.Kabla ya kuingia kwa wakoloni katika Pwani ya Afrika Mashariki, walitanguliza vitangulizi vyao. Taja vitangulizi viwili tu vya wakoloni waliokuja Tanganyika. 

i. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

ii. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

43.Kuna aina kuu mbili za ramani ambazo ni ramani ya . . . . . . . . . . . . . na . . . . . . . . . . . . . . .

44.Jumuiya inayojumuisha nchi zilizopo upande wa Mashariki mwa Afrika ambayo Tanzania ni mwanachama hujulikana kwa jina la: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

45.Kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine kilitokea mwaka . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 22  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 22  

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo

 1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
 2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.
 3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalumu ya kujibia (OMR).
 4. Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
 5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
 6. Weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

 1. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
 2. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40 na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.
 3. Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

Kwa swali 1-40, tafuta majibu kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi ya jibu hilo katika karatasi maalumu ya OMR uliyopewa.

1. Inaelezwa kwamba mwanadamu amezungukwa na vitu mbalimbali. Ni istilahi ipi kati ya zifuatazo inasadifu vitu vyote vinavyomzunguka mwanadamu?

A: Uoto B: Anga hewa C: Makazi D: Mazingira E: Milima [       ]

2. Mwaka jana tulitembelea kituo cha hali ya hewa, lengo letu kuu lilikuwa kujifunza kuhusu vipengele vya hali ya hewa na vipimio vyake. Mmoja wa wataalamu wa hali ya hewa alituambia kuwa kuna vipimio mbalimbali vya vipengele vya hali ya hewa. Unadhani ni kipimio gani alituambia kuwa kinatumika kupimia kasi ya upepo?

A: Kipima mvua B: Anemomita C: Baromita D: Kipimajoto E: Kipima mwelekeo wa upepo [       ]

3. Nini mchango wa misitu katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la ozoni unaosababishwa na moshi wa viwandani?

A: Misitu inasaidia kunyonya gesi zinayosababisha uharibifu wa ozoni. B: Misitu inachangia kasi ya ongezeko la gesi zinazoharibu tabaka la ozoni. C: Misitu ni vyanzo vya moshi unaoharibu tabaka la ozoni. D: Misitu haihusishwi katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la ozoni. E: Misitu huimarisha tabaka la ozoni. [       ]

4. Umepewa vipengele muhimu kuhusu mzunguko wa maji; Upozaji, Maji tiririka ardhini, Mvua na Uvukizi. Bainisha mtiririko sahihi wa vipengele hivi kutoka cha kwanza hadi cha mwisho.

 1. Mvua > Upozaji > Maji tiririka ardhini > Uvukizi
 2. Upozaji > Uvukizi > Mvua > Maji tiririka ardhini
 3. Maji tiririka ardhini > Uvukizi > Upozaji > Mvua
 4. Uvukizi > Upozaji > Mvua> Maji tiririka ardhini
 5. Maji tiririka ardhini > Uvukizi> Upozaji > Mvuke [       ]

5. Mimi na Bello tulikuwa na majadiliano kuhusu madhara ya wingi wa watu. Rafiki yangu Bello alijitahidi kuorodhesha madhara mengi kadiri alivyoweza. Unadhani ni lipi kati ya yafuatayo hakulitaja?

A: Uchafuzi unaosababishwa na ongezeko la uzalishaji na utumiaji. B: Matumizi ya rasilimali kupita kiasi C: Ukosefu wa ajira D: Upungufu wa ardhi na rasilimali nyinginezo E: Maendeleo kutokana na matumizi sahihi ya rasilimali. [       ]

6. Afrika Mashariki ni moja ya sehemu za bara la Afrika ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali za asili kama vile; madini, vyanzo vya maji na milima. Unadhani Ndulu alitoa jibu gani alipotakiwa kutaja mto mrefu kuliko yote Afrika?

A: Mto Malagarasi B: Mto Rufiji C: Mto Kongo D: Mto Tana E: Mto Nile [       ]

7. Bw. Bakari anaishi katika kijiji cha Kilolo ambacho kipo mita 2700 juu ya usawa wa bahari. Bw. Buli anaishi katika mji wa Kyala uliopo mita 111 juu ya usawa wa bahari. Wanapokutana Bw. Buli hulalamika kwamba katika mji wake kuna kiwango cha juu cha joto wakati Bw. Bakari hueleza kwamba katika mji wake kuna kiwango cha chini cha joto. Unadhani ni kwa nini Bw. Bakari anapata kiwango hicho cha joto?

A: Kwa sababu anaishi nyanda za chini B: Kwa sababu anaishi nyanda za juu zaidi C: Hasemi ukweli D: Hana sweta E: Anaumwa [       ]

8. Wakati wanadamu wakipambania uhai wao, wanajikuta wakiharibu mazingira bila kujua. Kwa kufanya hivyo baadhi ya watu kama vile wakulima wanachoma vichaka kwa ajili ya kilimo na wafugaji kufuga wanyama wengi kwenye eneo dogo. Unafikiri shughuli hizo zina madhara gani?

A: Uwepo wa mvua nyingi B: Ongezeko la ujazo wa maji katika vyanzo vya maji C: Husababisha mmomonyoko wa ardhi D: Kuganda kwa maji katika mito na maziwa E: Ongezeko la uoto wa asili [       ]

9. Shalibu ni mwalimu mzoefu anayefundisha katika shule ya msingi Mtakuja. Alialikwa na mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii aje kutuelezea mambo muhimu yanayoathiri hali ya hewa Tanzania. Ni jambo lipi kati ya yafuatayo unadhani halikutajwa na mwalimu Shailibu?

A: Upepo B: Uoto wa asili C: Umbali kutoka baharini D: Mvua E: Latitudo [       ]

10. Tulipotembelea Mlima Kilimanjaro, tuliarifiwa na wenyeji kuwa mlima huo unatokana na volkano. Mlima huo umezungukwa na wakazi ambao wengi wao ni wakulima. Bw. Bilu ambaye ni mwalimu wetu alitaka kujua ni kwa nini upande mmoja wa mlima ni mkame karibia mwaka mzima. Je, ni jibu gani sahihi alipata kutoka kwa wenyeji hao?

A: Upande huo upo juu sana B: Ni upande wa mwelekeo wa upepo C: Wanyama wengi wanaishi upande huo D: Watu waishio upande huo huharibu mazingira E: Ni upande wa mlima unaopokea pepo kavu. [       ]

11. Dunia ni sayari ya tatu katika mfumo wa jua. Ni sayari pekee inayosemekana kuwa na viumbe hai. Ina aina mbili za mizunguko ambayo ni kulizunguka jua na kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake. Yafuatayo ni matokeo ya dunia kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake ISIPOKUWA.

A: Kutokea kwa afelioni na perihelioni B: Kutokea kwa mchana na usiku C: Kupwa na kujaa kwa maji baharini D: Uwepo wa utofauti wa muda sehemu mbalimbali E: Mabadiliko ya siku [       ]

12. Tanzania ni nchi mojawapo Afrika inayotumia bidhaa za kitamaduni kuvutia watu mbalimbali kutoka nchi za Ulaya na kwingineko. Watu hao wanapotembelea nchi hii hununua bidhaa hizo hivyo kukuza pato la taifa. Ni kabila gani nchini Tanzania ni maarufu katika uchongaji wa vinyago?

A: Wamasai B: Wamakonde C: Wakurya D: Wahadzabe na Watindiga E: Wazaramo [       ]

13. Mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii darasa la tatu alimtaka mwanafunzi ataje baadhi ya makabila yanayopatikana Tanzania, chimbuko na ngoma zao za asili.

A: Wachaga, Kilimanjaro, Mdundiko B: Wanyakyusa, Dodoma, Mdumange C: Wapogoro, Morogoro, Sangula D: Wapare, Kilimanjaro, Iringi E: Wangoni, Ruvuma, Sindimba [       ]

14. Moja ya ajenda inayojadiliwa duniani kwa sasa hasa katika nchi zinazoendelea ni ajira kwa watoto. Imeenea sana kiasi cha kuwanyima watoto haki yao ya elimu. Ukiwa kama ni mtaalamu wa kutetea haki za watoto, ungewezaje kutatua tatizo hilo nchini Tanzania?

A: Kuwa na misingi imara ya mila na desturi hizo. B: Kwa kuanzisha maeneno ya kilimo C: Kuwatenga watoto hao na jamii. D: Kuelimisha jamii juu ya madhara ya tamaduni hiyo. E: Kuwaita waajiri wa jamii husika ofisini kwako. [       ]

15. Tunaiitaje hali ya nchi huru kuendelea kutawaliwa kijamii, kisiasa na kiuchumi na koloni lake?

A: Ubeberu B: Ukoloni C: Ukoloni mamboleo D: Utandawazi E: Ubepari [       ]

16. Shitundu aliambiwa ataje jina la vuguvugu la waafrika duniani kote lililokuwa na lengo la kupinga ukandamizaji na unyonyaji. Unadhani lipi lilikuwa ni jibu lake sahihi?

A: Ukoloni mamboleo B: Uafrika C: Muungano wa Afrika (Pan Afrika) D: Utandawazi E: Ukombozi [       ]

17. Kama ungeambiwa utoe sababu kwanini juhudi za waafrika za kupinga uvamizi wa kikoloni zilishindwa. ungetoa jibu gani?

A: Wazungu walikuwa wengi kuliko waafrika B: Waafrika walikuwa ni wazee sana C: Waafrika walitumia silaha duni na mbinu hafifu za kivita D: Wazungu walitumia uchawi E: Kulikuwa na baa la njaa Afrika [       ]

18. Zama za mawe ziligawanyika katika vipindi mbalimbali. Maisha ya binadamu yalitofautiana kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ni katika zama ipi ambapo binadamu aliacha kula vyakula vibichi?

A: Zama za kati za mawe B: Zama za mwisho za mawe C: Zama za chuma D: Zama za mawe za kale E: Zama za teknolojia ya kisasa ya kidigitali [       ]

19. Kwa sasa dunia imegubikwa na muingiliano wa watu unaofanya dunia kuonekana kama kijiji kimoja. Je, hali hiyo inaitwaje?

A: Utandawazi B: Kupanda kwa joto duniani C: Uundaji wa vijiji D: Mahusiano E: Ukoloni mamboleo [       ]

20. Wakati wa mapambano ya kukomesha biashara ya utumwa Afrika Mashariki. Upi kati ya mikataba ifuatayo ulijulikana kihistoria kama mkataba wa kubadilishana suruali na kifungo?

A: Mkataba wa Frere wa 1873 B: Mkataba wa Moresby wa 1822 C: Mkataba wa Hermarton wa 1845 D: Mkataba wa mipaka wa 1886 E: Mkataba wa Heligoland wa 1890 [       ]

21. Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Wakati huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza. Je, ni Gavana yupi wa kingereza aliyemkabidhi madaraka?

A: Horace Byatt B: Donald Cameron C: Julius Von Soden D: Richard Turnbull E: Edward Twinning [       ]

22. Ni tukio gani liliathiri awamu ya pili ya maendeleo ya kiuchumi Tanzania kati ya 1967 na 1985? 

A: Mapokeo ya itikadi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa. B: Kung’atuka kwa mwalimu Nyerere kutoka madarakani C: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar D: Kutangazwa kwa Azimio la Arusha E: Vita ya Tanzania na Uganda [       ]

23. Mkutano wa Berlin ulifanyika nchini Ujerumani toka mwezi Novemba 1884 hadi Februari 1885. Lengo la mkutano huo ambao uliongozwa na Otto Von Bismarck lilikuwa ni kuligawa bara la Afrika. Ni mwaka gani Zanzibar ilikabidhiwa kwa Uingereza?

A: 1890 B:1886 C: 1885 D:1980 E: 1887 [       ]

24. Unaishi katika mazingira yenye uhaba wa mvua. Ni mazao yapi kati ya haya yafuatayo utawashauri watu wanaoishi katika eneo hilo wayapande ili kuepukana na uhaba wa chakula?

A: Mihogo, Mtama na Ulezi B: Ulezi, Maharage na Mahindi C: Mtama, Maharge na Kahawa D: Pamba, Mihogo na Mpunga E: Mpunga, Mtama na Ulezi [       ]

25. Kuna aina mbalimbali za madini zinazopatikana nchini Tanzania. Madini haya huwezesha nchi kukua kiuchumi. Ni madini gani yapatikanayo mkoani Manyara ambayo huingizia nchi yetu fedha za kigeni?

A: Dhahabu B: Shaba C: Almasi D: Chuma E: Tanzanite [       ]

26. Mnamo mwaka 2022 nchi yetu ya Tanzania iliendesha sensa ya watu na makazi kwa lengo la kujua idadi ya watu nchini. Endapo utatakiwa kutaja mwaka ambao sensa inayofuata itafanyika, lipi litakuwa ni jibu lako?

A: 2032 B: 2025 C: 2030 D: 2042 E: 2026 [       ]

27. Bw. Chebo ambaye ni mwalimu wa somo la Maarifa ya Jamii, aliwaagiza wanafunzi wa darasa la saba wachore ramani ya bara la Afrika. Ni aina gani ya kipimio cha ramani kati ya hivi vifuatavyo kitawafaa kuchora ramani hiyo?

A: Kipimio cha mstari B: Kipimio cha sentenso C: Kipimio kidogo D: Kipimio cha kati E: Kipimio kikubwa [       ]

28. Wakati wa somo la Maarifa ya Jamii, Bi. Limbo aliwafundisha wanafunzi wake kwamba mistari ya latitudo ina majina tofauti kulingana na nyuzi na maeneo husika. Je, latitudo yenye nyuzi 66½ kusini mwa ikweta hujulikana kwa jina gani?

A: Ikweta B: Meridiani Kuu C: Tropiki ya Kansa D: Duara la antaktiki E: Duara la aktiki [       ]

29. Mojawapo ya vitendo haramu katika ujasiriamali ni kuuza bidhaa ambazo zipo chini ya kiwango ambazo zinaweza kusababisha madhara kwa watumiaji. Ni mamlaka ipi ya serikali inahusika katika kusimamia viwango vya bidhaa za wajasiriamali nchini Tanzania?

A: TMAA B: TRA C: TBC D: TCRA E: TBS [       ]

30. Tausi amehitimu elimu ya Chuo Kikuu na kwa bahati mbaya hajaajiriwa na serikal hivyo ameamua kuanzisha biashara. Unafikiri ni kitu gani kitakuwa ni cha kwanza kuzingatiwa na Tausi?

A: Faida B: Mpango biashara C: Barabara D: Hatari E: Bima [       ]

31. Kwa nini tunashauriwa kuepuka kutumia vyombo vya chuma kuhifadhia sharubati?

A: Vinapoza sharubati B: Vinaharibu sharubati C: Vinaharibu ladha ya sharubati D: Vinabadili matunda matamu kuwa machungu E: Vina ujazo mdogo [       ]

32. Bwana Mbimbi alitaka kujua Rwanda na Burundi zilikuwa chini ya utawala gani wa kikoloni kabla ya vita kuu ya dunia. Ni jibu gani sahihi angetakiwa kupewa?

A: Utawala wa Kiarabu B: Utawala wa Kijerumani C: Utawala wa Kiingereza D: Utawala wa Kibelgiji E: Utawala wa Kifaransa [       ]

33. Mwanafunzi wa darasa la tatu alitakiwa kutaja faida tano za kupanda miti katika mazingira yetu. Endapo angelitoa majibu yafuatayo, ni herufi gani inaonesha jibu lisilo sahihi?

A: Kupata kivuli kwa ajili ya mifugo na watu B: Kupata madini C: Kuzuia mmomonyoko wa udongo D: Kuongeza rutuba kwenye udongo E: Kusaidia kuleta mvua [       ]

34. Wakati wa somo la Maarifa ya Jamii darasa la sita, nilitaka wanafunzi wangu wataje faida ambazo nchi ya Tanzania imezipata kutokana na kupanuka kwa biashara ya kimataifa na walizitaja. Ni ipi kati ya hizi zifuatazo ilikuwa sahihi zaidi kuliko nyingine?

A: Kupungua kwa wajasiriamali wa ndani B. Kupungua kwa mikataba ya kibiashara C: Kuongezeka kwa uzalishaji D. Watu watatembelea nchi nyingi E: Kuongezeka upatikananji wa fedha za kigeni [       ]

35. Jamii za kitanzania kabla ya ukoloni zilikuwa na mila na desturi zake. Lipi kati ya haya yafuatayo halikuwa lengo mahususi katika jamii hizo?

A: Kuwafanya watu wajenge nyumba kubwa na kufuga wanyama wengi B: Kuendeleza kufanya kazi kwa bidii C: Kuimarisha usawa katika uzalishaji na mgawanyo wa rasilimali D: kuheshimu na kukuza tabia njema E: Kuhimiza malezi ya wazazi katika jamii [       ]

36. Upatikanaji wa uhuru katika mataifa mbalimbali ya Afrika, ulitokana na juhudi za mashujaa wengi wa Afrika. Nani kati ya hawa wafuatao hawakuwa kati ya viongozi waliopigania uhuru katika nchi za kiafrika?

A: Jomo Kenyata and Robert Mugabe B: Samora Machel and Patrick Lumumba C: Kwame Nkrumah and Julius K. Nyerere D: Milton Obote and Nelson Mandela E: Mobutu Seseseko and Yoweri Museveni [       ]

37. Ili kuwatawala waafrika, wazungu walitumia mbinu anuai. Ni ipi kati ya njia zifuatazo ilitumiwa na wazungu ili kuanzisha utawala wa kikoloni barani Afrika?

A: Kutoa huduma mbalimbali za kijamii B: Kuanzisha biashara ya utumwa C: Kugawa vyakula na mavazi D: Kusaini mikataba ya uongo E: Kujenga reli na barabara [       ]

38. Wakati Bi. Chedo anamuelekeza binti yake namna ya kunyoosha nguo, Alimuonesha hatua zifuatazo, isipokuwa moja. Hatua hiyo ni ipi?

A: Kulowesha nguo kwenye maji B: Kuwasha pasi C: Kunyoosha mikono D: Kunyoosha mapindo E: Kunyoosha mbele na nyuma ya nguo [       ]

39. Mwanafunzi wa darasa la saba alitaka kujua kutoka kwa mwalimu wake wa somo la Stadi za Kazi, ni kwa nini wauzaji wengi wa viatu huweka karatasi au matambara ndani ya viatu. Unadhani mwanafunzi huyu alipewa jibu gani?

A: Husaidia kung’arisha viatu B: Ili viuzike kwa urahisi C: Ili kurahisisha uning’inizaji wa viatu juu D: Huvifanya viatu vibakie na mwonekano wake wa asili E: Hufanya viatu visitoboke [       ]

40. Kitanda ni mojawapo ya vitu muhimu vinavyohitajika katika sehemu ya kulala. Kitanda kizuri na imara ni muhimu kwa afya ya binadamu yeyote. Katika muktadha huo, kuna umuhimu gani wa mtu kulala akiwa amenyooka? 

A: Inamfanya mtu aonekane safi B: Inasaidia kulinda uti wa mgongo na viungo vingine ndani ya mwili wa mwanadamu C: Inatengeneza mahusiano mazuri ya kifamilia D: Inafanya mwili kuwa na nguvu E: Inamfanya mtu afurahie usingizi [       ]

SEHEMU B: (Alama 10)

Andika jibu sahihi kwa kila swali la 41-45 katika nafasi iliyoachwa wazi nyuma ya karatasi ya OMR. Tumia kalamu ya wino mweusi au wa buluu.

 

41. Kipindi nafanya kazi katika Baraza la Taifa la Mzingira (NEMC) Niliwashauri wananchi wa kijiji cha Nkisi kutumia vyanzo vya nishati mbadala kama njia mojawapo ya kupambana na uharibifu wa mazingira. Taja vyanzo mbadala viwili nilivyowaelekeza kuvitumia.

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

42. Wanafunzi wa darasa la saba walimuuliza mwalimu wao wa somo la Maarifa ya Jamii kwa nini Afelioni na Periherioni hutokea wakati dunia ikilizunguka jua. Unadhani jibu gani ni sahihi?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

43. Chiwili ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita alitakiwa na mwalimu wake wa somo la Stadi za Kazi ataje faida moja wapo ya kutandaza majani shambani.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

44. Ni miaka mingapi iliyopita toka binadamu alipoanza kutengeneza historia yake duniani?

45. Bw. Saliboko mjasiriamali mdogo toka katika kijiji cha Mabuku, alitaka kujua maana ya neno “biashara” kutoka kwa Lanja ambaye ni mfanyabiashara mkubwa. Unadhani ni jibu gani alipewa?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 18  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 18  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

 1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
 2. Jibu maswali yote
 3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
 4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
 5. Tumia penseli ya HB tu.
 6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Mr. Msabila aliishi kwa miaka 130. Lipi kati ya kauli zifuatazo ni sahihi kuhusu Bw. Msabila

(A) aliishi miaka elfu moja na karne 13 (B) aliishi miongo 130 (C) aliishi kwa karne moja na miongo 3 (D) aliishi kwa karne 13 (E) aliishi kwa karne moja na miongo 30 [     ] 

2. Miundo mbinu maana yake ni barabara, reli na mawasiliano,.Ni mikoa gani ya Tanzania imepitiwa na reli ya TAZARA. 

(A) Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Tabora na Kigoma (B) Kilimanjaro, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam (C) Morogoro, Manyara, Tanga na Pwani (D) Mbeya, Dar es Salaam, Njombe, Morogoro, Songwe na Iringa (E) Kigoma, Mbeya na Tanga [     ]

3. Wanafunzi wa darasa la tatu walifundishwa kuhusiana na hali ya hewa. Ni kifaa gani wanafunzi hutumia kupima miale ya jua? 

(A) Oktas (B) Barometa (C) Anemometa (D) Haigrometa (E) Compbell stock [     ]

4. Wanafunzi wa shule ya Msingi Azimio walipewa zoezi la kurekodi jotoridi kwa siku tano. Matokeo ya siku ya kwanza hadi ya tano yalikuwa kama ifuatayo; 19.5oC, 25.3oC, 30oC, 27.2oC na 20.5oC. Tafuta wastani wa jotoridi. 

(A) 21.5oC (B) 23.5 oC (C) 24.5 oC (D) 19.5 oC (E) 25.5 oC [     ]

5. Kuna aina tofauti za majanga yanayotokea katika mazingira yetu. Lipi kati ya yafuatayo limesababishwa na nguvu za asili na shughuli za binadamu? 

(A) kimbumba (B) mmomonyoko wa udongo (C) tsunami (D) tetemeko la ardhi (E) mlipuko wa volcano [     ]

6. Mazingira yanaundwa na vitu mbalimbali ni aina gani ya mazingira ambayo vitu hivyo hupatikana chaki, ubao na madaftari. 

(A) dukani (B) nyumbani (C) mahakamani (D) sokoni (E) shuleni[     ] 

7. Tetemeko la ardhi, tsunami, moto, mafuriko na ukame ni baadhi ya majanga ya asili. Ni janga lipi kati ya yafuatayo linasababishwa na ukataji wa miti

(A) tetemeko la ardhi (B) ukame (C) mafuriko (D) tsunami (E) moto [     ]

8. Ili ramani ikamilike inatakiwa iwe na vipengele vitano muhimu, kipengele kipi kinaonyesha mipaka ya ramani 

(A) jina la ramani (B) pambizo (C) ufunguo (D) dira (E) kipimio [     ] 

9. Yapo makundi matatu ya vitangulizi vya ukoloni kundi lipi lilikuwa la pili kuwasili Afrika

Mashariki? (A) makabuni (B) wamisionari(C) mapebari (D) wapelelezi(E) wafanya biashara[     ] 

10. Vita vya majimaji vilianza kupiganwa mwaka 1905 – 1907. Dhidi ya wajerumani, nani alikuwa kiongozi wa vita hivyo? 

(A) Kinjekitile ngwale (B) Chifu Mirambo (C) Hassani Makunganya (D) Abushiri (E) Mkwawa [     ]

11. Zifuatazo ni sehemu za kihistoria zipatikanazo Tanzania isipokuwa__________

(A) Rusinga (B) Olduvai (C) Engaruka (D) Kondoa Irangi (E) Kaole [     ]

12. Shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mto Msimbazi zinaathari kwa jamii inayozunguka mto huo, ni athari gani husababishwa kwa kukata miti pembezoni mwa mto?

(A) uhaba wa maji kwa matumizi ya binadamu (B) uchafunzi wa hali ya hewa (C) ardhi kupoteza rutuba (D) kukauka kwa vyanzo vya maji (E) kushuka kwa uzalishaji samaki [     ]

13. Bwana Hatibu hutoka jasho kwa wingi wakati wa msimu wa joto. Je utamshauri avae nguo za rangi gani? 

(A) nyeupe (B) nyeusi (C) blue (D) njano (E) kijani [     ]

14. Bwana Salimu ni mfugaji ambaye huhama hama na idadi kubwa ya mifugo. Ni madhara gani husababishwa na aina hii ya ufugaji? 

(A) mafuriko (B) kustawi kwa uoto wa asili (C) kufa kwa mifugo (D) kupotea kwa misitu (E) uharibifu wa mazao [     ]

15. Bwawa la Nyerere ni mojawapo ya chanzo kinachotarajiwa kuzalisha nishati ya umeme wa maji nchini Tanzania. Je bwawa hili limejengwa katika mto gani?

(A) Ruaha (B) Ruvuma (C) Ruvu (D) Rufiji (E) Pangani [     ]

16. Mtalamu wa madini alitembelea wanafunzi wa darasa la saba na kuwafundisha aina ya madini na kazi zake. Je madini gani hutumika kukatia vioo?

(A) dhahabu (B) almasi (C) fedha (D) Tanzanite (E) Shaba [     ]

17. Maji ni maendeleo kwa jamii na kiuchumi nchini Tanzania. Bainisha vyanzo vikuu vitatu vya rasilimali hiyo? 

(A) mvua, bahari na maziwa (B) bahari, visima na mito (C) mvua, maji yaliyo juu ya nchi ya ardhi (D) maziwa, mito na chemuchemu (E) visima, chemchem na mvua [     ]

18. Kupungua kwa theluji katika mlima Kilimanjaro kumesababishwa na ongezeko la joto katika uso wa dunia. Ni shughuli ipi inaweza kutumika kukabiliana na tatizo hilo?

(A) kuchoma misitu na kukata miti (B) kulima kandokando ya mlima (C) kupanda miti na kutunza mazingira (D) uvunaji ovyo wa misitu (E) kufuga mifugo mingi kwenye eneo dogo [     ]

19. Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa michezo kama nyenzo ya kuburudisha na kuunganisha raia wake. Ni taasisi ipi inayohusika katika kusimamia na kuendeleza michezo nchini Tanzania? 

(A) BASATA (B) BAKITA (C) TUKI (D) BMT (E) TFF [     ]

20. Kila jamii nchini Tanzania ina michezo yake ya asili kulingana na mazingira, muda na utamaduni. Ipi ni mifano ya michezo hiyo? 

(A) mpira wa miguu, ngumi na kukimbia (B) kukimbia, kuogelea na mpira wa miguu (C) kurusha mkuki, kuruka kamba na kukimbia (D) mpira wa miguu, pete na kuogelea (E) mpira wa kikapu, mguu na pete [     ]

21. Katika uso wa dunia kuna pepo zinazovuma kutoka eneo moja kwenda jingine. Je ni upepo gani unavuma kutoka kusini kuelekea kaskazini? (A) upepo wa kusi (B) upepo wa kaskazini (C) upepo mkavu (D) upepo wa magharibi (E) upepo wa unyevu [     ]

22. Tanzania ina makabila mengi yenye mila nzuri na potofu. Ni mila ipi yenye madhara kwa jamii?

(A) kuruhusu wanawake wajawazito kula mayai (B) kukeketa watoto wa kike (C) kufundisha wavulana pamoja na wasichana maadili (D) kutahiri wavulana (E) kuwapa wanawake haki sawa na wanaume [     ]

23. Kuongezeka kwa joto duniani unasababishwa na shughuli za kibinadamu. Ipi si madhara yanayosababishwa na ongezeko la joto nchini Tanzania? 

(A) kuyeyuka kwa theluji katika mlima Kilimanjaro (B) kupotea kwa bayoanuai (C) kuongezeka kwa kina cha maji baharini (D) kuongezeka kwa uoto wa asili (E) kutokea kwa ukame [     ]

24. Ni kwa namna gani jamii inaweza kukabiliana na mila na tamaduni zilizopitwa na wakati?

(A) kudumisha umoja wa taifa (B) kudumisha misingi ya uzalendo (C) kuwa na misingi ya mila na desturi zinazofanana (D) kupenda jamii na taifa (E) kufanya majadiliano na jamii inayohusika [     ]

25. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anatambulika kama “baba wa taifa” aliyestaafu kwa hiyari mwaka 1985. Je, alistaafu karne ya ngapi? 

(A) 19 (B) 21 (C) 20 (D) 22 (E) 18 [     ]

26. Yafuatayo yaweza kutokea kwa taifa linalokuza utamaduni wake isipokuwa________

(A) kudumisha misingi ya uzalendo (B) kuiga tamaduni za kigeni (C) kudumisha umoja (D) kulinda asili yake (E) kuwepo kwa uhusiano mzuri katika jamii [     ]

27. Magret anaipenda nchi yake ana moyo wa kujitoa kwa taifa lake na ni mtunzaji mzuri wa rasilimali za taifa. Magreti anaweza kuwa na sifa ipi kwa taifa lake?

(A) mlinzi wa rasilimali za nchi (B) mzalendo kwa taifa lake (C) mtunzi wa miiko ya jamii (D) mlinda usalama wa jamii (E) msimamizi wa umoja wa wananchi [     ]

28. Licha ya kugawanywa kwa bara la Afrika katika mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 – 1885 Afrika iligawanywa tena baada vita vya kwanza vya dunia miongono mwa mataifa ya ulaya isipokuwa______

(A) ufaransa (B) haha (C) ubelgiji (D) ureno (E) ujerumani [     ]

29. Katika ujasiriamali neno thubutu linamaanisha nini?

(A) kuwa na maamuzi magumu (B) uzembe katika kufanya maamuzi (C) uwe tayari kujitolea (D) kusababisha hasara kwa makusudi (E) kuwa jasiri kuchukua hatua [     ]

30. Kitu gani kinaweza kuchangia kukua kwa uzalishaji mali nchini Tanzania?

(A) uwepo wa mifumo rafiki ya kisera na kisheria (B) uwapo wa viwanda vingi nchini (C) kukaribisha uwekezaji kutoka nje ya nchi (C) kuwa na amani na utulivu mijini (D) kutangaza vivutio vya ulaya [     ]

31. Viatu ni sehemu ya sare ya shule. Kwa nini wanafunzi wanashauriwa kutovaa viatu vyenye visigino virefu? 

(A) husababisha maumivu ya tumbo (B) husababisha maumivu ya magoti (C) husababisha maumivu ya kichwa (D) husababisha maumivu ya misuli (E) husababisha maumivu ya kifua [     ]

32. Familia inapokuwa na wazazi na watoto hujulikana kama familia ya baba, mama na watoto (nyuklia family). Familia hii itaitwaje endapo wazazi hapo watafariki

(A) familia pana (B) familia ya watoto (C) failia ya watoto yatima (D) familia tegemezi (E) familia ya watoto wa mtaani [     ]

33. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa na madini tofautitofauti ni kundi lipi linajumuisha madini yatumikayo kwa urembo? 

(A) dhahabu, chumvi na chuma (B) almasi ruby na tanzanaiti (C) almasi, dhahabu na chuma (D) kobati, rubi na tanzanaiti (E) chumvi, dhahabu na chuma [     ]

34. Umemtembelea shangazi yako na umepewa chumba kichafu. Ni ugonjwa gani unaweza kukupata ukilala chumba hicho? 

(A) kuharisha na kutapika (B) kukohoa na kutapika [     ] (C) mafua na maumivu ya kifua (D) kuharisha na mafua (E) homa na maumivu ya kifua

35. Mwalimu wa somo la stadi za kazi aliwaongoza wanafunzi kuunda chungu na kuwapa mbinu namna ya kukikausha chungu hicho. Kwa nini ni muhimu kukausha chungu hicho?

(A) kukifanya kiwe imara (B) kukifanya kiwe na rangi nyeusi (C) kukipendezesha (D) kukifanya kiwe na harufu nzuri (E) kukifanya kiwe chepesi [     ]

36. Mimi ni mbunifu, mthubutu na mchapakazi kwa ajiliya kutimiza malengo yangu mimi ni nani?

(A) mjasiriamali (B) mbunifu (C) mfanyabiashara (D) mnunuzi (E) muuzaji [     ]

37. Rangi nyekundu kwenye nembo ya taifa huwakilisha nini? 

(A) maliasili (B) uhuru na umoja (C) mipaka ya nchi (D) uoto wa asili (E) udongo wenye rutuba [     ]

38. Maisha ya binadamu yamepitia zama ngapi? 

(A) 3 (B) 5 (C) 2 (D) 4 (E) 6 [     ]

39. Chama gani cha siasa kilichokipinga chama cha TANU wakati wa harakati za kudai uhuru hapa Tanzania? 

(A) TAA (B) ASP (C) ZPPP (D) AA (E) UTP [     ]

40. Ipo mifumo minne ya tawala za kikoloni Afrika. Je nani alikuwa mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma? 

(A) Fredrick Lugard (B) Donald Cameroon (C) Fredrick De Clark (D) Richard Turnbull (E) Karl Peters [     ]

SEHEMU B:

ANDIKA MAJIBU SAHIHI KATIKA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI KWENYE FOMU MAALUMU YA OMR KWA KUTUMIA KALAMU YA WINO

41. Je! ni jina gani ambalo linaelezea mahali ambapo mjasiriamali anaweza kuweka na kutoa fedha kwa ajili ya biashara?  ___________________________________________________________

42.Ni nyota gani ambayo ipo karibu zaidi na dunia?  ______________________________________

43.Ni zao gani ambalo hutumiwa kutengeneza sumu ya kuulia wadudu? ______________________

44. Mkusanyiko wa matone madogomadogo ya maji angani ni  ______________________________

45. Umoja wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, limetangazwa tarehe 7 Julai kila mwaka kwa siku ya Kiswahili duniani, eleza kwa kifupi umuhimu wa siku ya Kiswahili katika nchi ya Tanzania

 ______________________________________________________

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 8  

STANDARD SEVEN MAARIFA EXAM SERIES 8  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256