JINA LA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . .
NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . .
OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA
MTIHANI WA UTAMILIFU WA DARASA LA SABA,APRIL, 2024
SOMO : HISABATI
Muda: Saa 2:00
Maelekezo:
SEHEMU A: MATENDO YA KIHISABATI (ALAMA 10)
Katika kila kipengele, jibu maswali yote katika sehemu hii
SWALI LA 1
i. 4021 + 7929=
ii. 30045-869=
iii. 792 × 48=
iv. 8888÷88=
v. 7 1/7+4 ½ =
vi. 4 5/8+1 4/5
vii. 7.263+6.96=
viii. 0.00075÷0.03=
(ix) Tafuta kipeuo cha pili cha 7921
(x) Zidisha km 6 m 350 kwa 25
SEHEMU B: MAFUMBO ( ALAMA30)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
SWALI LA 2
(i) Eneo la la shamba la shule ya lupeta lina ukubwa wa hekari 89738. Kadiria hekari hizo katika maelfu yaliyo karibu
(ii) Katiak namba 983084 tarakimu 8 huwakilisha kiwango gani cha namba
(iii) Ng`ombe wa mwajuma hutoa maziwa lita 14 ¾ za maziwa kila siku. Je kwa siku 16 ngombe huyo atatoa lita ngapi za maziwa?
(iv) Wastani wa vimo vya wavuala 6 na sm 143. Wastani wa vimo vya wavulana watano kati ya hao n ism 142. Nini uregu wa kimo cha mvulana wa sita?
(v) Umeagizwa na mwalimu wa Hisabati kutafuta namba kubwa ambayo inaweza kuzigwa 12,18,na 24 kwa wakati mmoja.Wewe kama Mtaalam wa Hisabati, Je namba hiyo ni ipi?
(vi) Punguza miaka 3 na miezi 9 kwenye miaka 12 na miezi 4
SWALI LA 3
(i) Majira ya nukta A(1,-3) B(1,-1) C4,-1) ukiunganisha A ,B, na C utapata umbo gani?
(ii) Umri wa mtoto na 1/5 ya umri wa mama yake . ikiwa jumla ya umri wao ni miaka 40,tafuta umri wa mama,.
(iii) John aliuza magunia sita ya mtama akapata wastani wa shilingi 56,000/= kwa gunia moja . Ikiwa alipata sh 282000/=kwa magunia matano . Gunia la sita aliuza kwa bei gani?
SWALI LA 4.
(i) Mfanayabiashara alipata faida sh 25000/=kwa siku kwa kuuza mayai Je atapata sh ngapi kwa mwezi Februari 2025?
(ii) Kijiji cha chunyu kina jumla ya wakazi 3000 ikiwa kuna wanaume 1700. Je sehemu gani ya wakazi ni wanawake?
(iii) Bei ya simu ni shilingi 96000/= baada ya kutolewa punguzo la 20% je simu hiyo ilikuwa inauzwa sh. Ngapi kabla ya punguzo?
SWALI LA 5.
(i) Kigomba aliweka fedha benki sh 400,000/= benki hiyo hutoa faida ya 10% kwa mwaka mmoja. Tafuta jumla ya fedha baada ya mwaka mmoja na miezi sita.
(ii) Umbali wa kutoka arusha hadi tanga ni km 455 iwapo basi liliondoka tanga saa 1530 na kufika arusha saa 2200 siku hiyo hiyo nini wastani wa mwendokasi wa basi hilo.
(iii) Said aliuza vitenge kw ash. 42000 na akapata hasara ya 16% tafuta thamani ya vitenge hivyo.
SWALI LA 6.
(i) Swaumu aliwagawia watoto wake watatu Ali,Juma na Amin ash 6000/= katika uwiano wa 4:6:2 kwa mfuatano huo. Tafuta kiasi cha fedha alichopata Amina?
(ii) Mwaluko alitumia 0.25 ya fedha zake kununua chakula 1/6 ya fedha zilizobaki alinunua nguo. Iwapo alibakiwa n ash 10,000/= je mwanzoni Mwaluko alikuwa ni sh ngapi?
(iii) Salama alikwenda dukani kununua vitu vifuatavyo:- maharage kg 1 ½ @sh 3500/= sukari kg 2 @ sh 2800/=, nyama kg 1 ½ @ sh 9000/=na mafuta lita 2 @ sh 3000/= . Iwapo alimpatia mwenye duka note 4 za sh 10000/= alirudishiwa kiasi gani cha fedha?
SEHEMU C: MAUMBO NA TAKWIMU( ALAMA 10)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
SWALI LA 7
(i) Mchoro kwa njia ya pai ufuatao unaonyesha idadi ya wafugaji na wakulima katika kijiji cha Godegode iwapo kijiji kina wafugaji 800 tafuta idadi ya wakulima katika kijiji cha Godegoge.
(ii) Grafu ifuatayo inaonyesha kiasi cha mvua kilichonyesha katika kijiji cha Kyamba kwa mwezi January hadi Machi. Tafuta wastani wa mvua iliyonyesha kwa miezi yote mitatu.
SWALI LA 8.
(i) Tafuta eneo la umbo hili (Tumia pai 22/7)
(ii) Eneo la mstatili ABCD ni sm2 120. Tafuta mzingo wake.
(iii) Tafuta ukubwa wa pembe q
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 44
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 44
MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI
MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023
DARASA LA SABA HISABATI
Muda : Saa 2:00
Maelekezo
SEHEMU A: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO
Kwa swali la 1-40, kokotoa majibu, kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi yake kwenye karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa.
1. Ni lipi kati ya majibu yafuatayo linalandana na Mia tisa sabini elfu mia nne arobaini na moja?
A: 9070441 B. 900000+400+70000+1+40
C. 700000+90000+400+40+1+40 D. 9000000+70000+0+400+40+1 E. 900000+70000+0+4000+1+40
2. John alibeba mzigo wenye uzani wa tani 0.75. Je, ni kilogram ngapi alizobeba John?
A: kg 750 B. kg 7500 C. kg 0.7500 D. kg 725 E. kg 705
3. Uzani wa ng’ombe 200 ni kilogramu 250.763. Ni tarakimu ipi katika uzito ulio rekodiwa iko katika nafasi ya thamani iliyo juu ya mia moja?
A: 0 B. 2 C. 7 D. 6 E. 3
4. Sadala alitembea umbali wa hektomita 50. Umbali huu ni sawa na umbali upi kati ya vizio vifuatavyo?
A: km 0.5 B. dam 5000 C. m 5000 D. dg 50500 E. sm 30000
5.Yafuatayo ni makundi yenye fedha za noti 100 za shilingi elfu kumi kama zilivyo hesabiwa na Salome. Je, ni kiasi gani cha fedha hizi zote kwa ujumla katika tarakimu?
|
6. Ng’ombe mmoja anaweza kutoa lita 5 na mililita 500 za maziwa kwa siku. Je, ng’ombe huyo atatumia siku ngapi kutoa lita 22 za maziwa ?
A: Siku 8 B. Siku 2 C. Siku 4 D. Siku 5 E. Siku 3
7. Idadi ya mbegu za ngano zilikusanywa na wanafunzi saba katika makundi ya mbegu; 7000000, 6000, 500000, 10, 30000, 100, 600000000 kwa kila mmoja. Je, ni jumla ya mbegu ngapi zilikusanywa kama namba moja?
A: 6007536110 B. 607536110 C.760536110 D. 670536110 E. 670563110
8. Sarafina hulipwa kiasi cha shilingi 204000 zaidi ya rafiki yake Ulimwengu. Ikiwa Ulimwengu hulipwa na kampuni kiasi cha shilingi 500500, ni kiasi gani cha fedha Sarafina hulipwa na kampuni?
A: 745000/= B. 704500/= C. 296500/= D. 296000/= E. 754000/=
9. Philemon alitakiwa aandike namba ndogo kuliko zote inayoweza kugawanywa kwa 6,9 na 12 bila baki. Unafikiri ni namba ipi aliyoiandika ni sahihi kati ya zifuatazo?
A: 3 B. 36 C. 48 D. 24 E. 120
10. Bosco ni mwanafumzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Mkanyageni. Alipewa na mwalimu wake jumla ya shilingi 3055000 kwa ajili ya kununulia ng’ombe. Ikiwa Bosco alinunua ng’ombe wanne(4) kwa jumla ya shilingi 2700500, Je ni kiasi gani cha fedha alibakiwa nacho?
A: 354500/= B. 435000/= C. 543500/= D. 435500/= E. 345500/=
11. Douglas alirekodi jumla ya uzito wa watoto wawili wenye jumla ya kilogram 57.8563. Ni kwa namna gani namba hii inaweza kuandikwa katika nafasi mbili za desimali?
A: Kg 58.00 B. Kg 50.85 C. Kg 578.56 D. Kg 75.86 E. Kg 57.86
12. Shule imesajili wanafunzi 200 katika mwaka wa masomo 2023. Ikiwa 35% ya wanafunzi waliosajiliwa wamesha wasili shuleni, Je ni wanafunzi wangapi bado hawajawasili shuleni?
A: 70 B. 230 C. 130 D. 103 E. 170
13. Odhiambo aliandika orodha ya namba tasa tano zinazofuatana. Kama mtaalamu wa Hisabati, orodha ipi ni sahihi kati ya hizi zifuatazo?
A: 1,2,3,5,7 B. 2,5,7,11,13 C. 7,11,13,15,17 D. 5,7,9,11,13 E. 3,5,7,11,13
14. Shulala alipanda miti katika mistari mitatu, ambapo kila mstari una mashimo 21. Ikiwa kila shimo alipanda miti minne, je alipanda jumla ya miti mingapi kwa pamoja?
A: 252 B. 84 C. 63 D. 225 E. 522
15. Baraka alikuwa na noti za shilingi 1000. Noti ya kwanza ilikua na namba 136700201 wakati noti ya mwisho ilikuwa na namba 136700300. Ikiwa noti hizo zilikuwa zimepangwa kwa namba zenye mtiririko mzuri, je Baraka alikua na jumla ya noti ngapi?
A: 99 B. 89 C. 100 D. 98 E. 101
16. Umbali wa barabara ni kilometa 270.007. Serikali ina tarajia kujenga umbali wa kilometa 198.13 kwa kiwango cha lami. Ni kilometa ngapi za barabara zitabaki bila lami baada ya ujenzi huo?
A: Km 70.807 B. Km 71.87 C. Km 877.71 D. Km 71.877 E. Km 7.1877
17. Kalunde aliambiwa na mwalimu wake aandike namba ndogo kuliko zote ambayo hutokana na tarakimu sita. Lipi unafikiri ni jibu lililokusudiwa na mwalimu kati ya majibu yafuatayo?
A: 210010 B. 102345 C. 110100 D. 012345 E. 1012345
18. Shule inamiliki theluthi ya ardhi ya kijiji. Ikiwa shule inamiliki kilomita za mraba 60, ni kiasi gani cha eneo la kilomita za mraba za ardhi linamilikiwa na Peter ikiwa anamiliki moja ya tisa ya eneo la kijiji?
A: 40 B. 80 C. 90 D. 20 E. 180
19. Watu watano walihudhuria mkutano wa kijiji. Walikaa kwenye viti vilivyokuwa vimewekwa namba kwa mpangilio wa 5, 7, 11, 13, _____ Je, ni namba ipi ya kiti iliwekwa kwenye kiti cha mtu wa tano?
A: 15 B. 14 C. 19 D. 23 E. 17
20. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya vitabu kwa masomo matano yanayofundishwa darasa la tano. Tafuta wastani wa idadi ya vitabu katika shule hiyo.
Jina la kitabu | Sayansi | Kiswahili | English | M/Jamii |
Idadi | 35 | 30 | 40 | 15 |
A: 82 B. 104 C. 20 D. 28 E. 140
21. Mkulima alipanda mbegu katika mashimo matano ya bustani yake. Ikiwa katika mashimo manne ya kwanza, kila moja lilikua na mbegu 4, 9, 16 na 25 kwa mpangilio huo. Je ni ipi ilikua jumla ya mbegu zilizopandwa katika mashimo yote matano?
A: 90 B. 360 C. 36 D. 63 E. 49
22. Bw. Kidulo alichora pembe nyuma ya kitabu chake ambayo ukubwa wake ulikua ni 63°. Kama mtaalamu wa Hisabati, ni lipi ni jina la pembe hiyo iliyochorwa na Bw. Kidulo?
A: Pembe butu B. Pembe kuu C. Pembe kali D. Pembe mraba E. Pembe nyoofu
23. Wakati wa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Singida United dhidi ya Mwadui FC, magoli yalikua yakifungwa kila baada ya dakika 18 ya mchezo. Ikiwa mchezo uliendeshwa kwa dakika 90 bila ya mapumziko, ni magoli mangapi yalifungwa kwa muda wote wa mchezo?
A: 10 B. 6 C. 19 D. 8 E. 5
24. Katika umbo, ukubwa wa pembe ya nje ni mara mbili ya ukubwa wa pembe ya ndani. Ni ipi kati ya pembe zifuatazo itakua ni ukubwa wa pembe ya nje?
A: 45° B. 120° C. 90° D. 60° E. 240°
25. Hidaya alijaribu kupanga namba katika machaguo yafuatayo kutoka ndogo kwenda kubwa. Kati ya namba hizi ni ipi alipaswa aanzie?
A: 2001 B. CMXCIX C. 1526 D. MCXIX E. MDCCCLXXXIII
26. Upande mmoja wa kasha la mche mraba ni sm 10. Ikiwa Bwana Heri atatumia kasha hilo kununulia maziwa, ni kiasi cha lita ngapi Bwana Heri atabeba?
A: L 10 B. L1.2 C. L 2.0 D. L 1000 E. L 1
27. Ngombola alikwenda sokoni na jumla ya shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kununulia bidhaa zifuatazo;-
Ni kiasi gani cha fedha alibakiwa nacho katika asilimia?
A: 60% B. 20% C. 75% D. 40% E. 30%
28. Umbo lifuatalo linalandana na umbo la nyumba ya Bw. Msemakweli. Ni kwa namna gani tunaweza kulitaja jina la umbo hili kuhusianisha na elimu ya maumbo (jiometri)?
A: Pentagon B. Hexagon C. Heptagon D. Octagon E. Decagon
29. Baba yangu alilima shamba kwa siku 2 na saa tano. Je, baba alitumia dakika ngapi?
A: 3180 B. 3420 C. 3080 D. 1440 E. 1280
30.
Gaucho alifunga magoli 240 pungufu ya rafiki yake Neymar ambaye alifunga magoli 890 katika kipindi cha maisha yake ya soka. Ni magoli mangapi walifunga wote kwa pamoja?
A: 650 B. 560 C. 1540 D. 1130 E. 1450
31.
Garimoshi liliondoka Kilosa majira ya saa 1945. Dakika 25 baadae, basi ambalo lilikuwa njiani likitokea Dumila likawasili Kilosa. Ni muda gani basi hilo liliwasili Kilosa katika mtindo wa saa 12?
A: 2:10 mchana B. 2010 hrs C. 8:45 usiku D. 8:10 asubuhi E. 2:10 usiku
32. Endapo Monica atatembea mara moja kuzunguka uwanja uliochorwa hapo chini, ni umbali gani atakuwa ametembea? (Tumia pai = 3.14)
A: m 741 B. m 614 C. m 740 D. m 714 E. m 7140
33. Kama Halima angeuza gauni lake kwa shilingi 1,200,000 angepata hasara ya shilingi 240,000. Ipi ilikuwa ni thamani halisi ya gauni hilo?
A: 2400000/= B. 960000/= C. 1440000/= D. 1040000/= E. 1240000/=
34. Zinduna alitumia jumla ya shilingi 25,500 kama matumizi yake ya kila siku katika mwezi Februari mwaka 2016. Ni kiasi gani cha fedha alikitumia kwa mwezi mzima?
A: 714000/= B. 741000/= C. 739500/= D. 765000/= E. 756000/=
35. Kitabu chenye kurasa mia moja kinaweza kusomwa na Ashura kwa saa 2 na dakika 12. Ashura atatumia muda gani kusoma vitabu 9 vya aina hiyo?
A: saa 19 dk 40 B. dk 1188 C. saa 18 dk 48 D. saa 19 dk 108 E. dk 1088
36. Kwenye uchaguzi wa kata mwaka 2014, Zidane alipata kura 378, Shumbana kura MXIX wakati Suzan akapata kura 608. Ni kura ngapi zilipigwa na wajumbe wa kata wakati wa uchaguzi huo?
A: MCV B. MCMXCV C. MMV D. MCIV E. MCV
37. Mfanyabiashara alikuwa na gunia moja la mahindi na akaliuza kwa faida ya 20%. Ikiwa aliliuza kwa kiasi cha shilingi 240,000, ni kiasi gani cha fedha alitumia kununulia hilo gunia la mahindi?
A: 200000/= B. 140000/= C. 40000/= D. 220000/= E. 20000/=
38. Galaga alikuwa na kamba yenye urefu wa mita 8 2/3 . Ikiwa aliamua kumpatia rafiki yake Mrope kipande chenye urefu wa mita 4 1/24 , ni mita ngapi ambazo Galaga alibakiwa nazo?
A: m 4 B. m 6 3/8 C. m 4 3/8 D. m 5 3/8 E. m 4 5/8
39. Bukuru alinunua kg 46 na dag 5 za unga wa mahindi. Akataka kuwapatia watu watano (5) ambao aliwaahidi kama zawadi ya kufanya kazi kwa bidii.
Je, kila mtu alipata kiasi gani?
A: kg 21 dag 9 B. kg9 dag 105 C. g9 dg 21 D. kg9 dag 21 E. dag 12 kg 9
40. David alirahisisha mtajo ufuatao hapo chini kama ilivyokua inahitajika urahisishwe. Lipi ni jibu sahihi kati ya yafuatayo ikiwa mtajo wenyewe ulikuwa 16x – x + 13 ?
A: 3x B. 2x C. 15x-13 D. 15x+13 E. 13x-x
SEHEMU B: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO
Kwa swali la 41-45, Tumia kalamu ya wino wa buluu au mweusi kukokotoa majibu katika nafasi ya karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa kwa kuonyesha kazi yako kwa usahihi.
41. 75% ya wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kibondo wanajua kusoma kwa ufasaha. Idadi ya wanafunzi iliyobaki hawawezi kusoma kwa ufasaha. Je, darasa hilo lina wanafunzi wangapi ikiwa idadi ya wanafunzi ambao hawawezi kusoma vizuri ni wanafunzi 40 ?
42. Kwenye mzani wa uzito barabarani tani 250 na kg 750 zilirekodiwa kwa kipindi cha siku moja. Je, ni kiasi gani cha uzani wa magari kitarekodiwa kwa kipindi cha siku nne (4) ikiwa uzani wa siku hautobadilika?
43. Fundi Saudi alianza kujenga kona ya nyumba ya Mwashamba katika majira ya nukta yaliyowakilishwa na herufi C. Andika majira ya nukta ya herufi ambapo fundi Saudi alianzia kujenga nyumba hiyo.
44. Mchoro ufuatao unaonesha mgawanyo wa tani za zao la tumbaku zilizokusanywa mkoani Tabora kutoka wilaya mbalimbali. Ikiwa idadi ya tani zote zilizo kusanywa kutoka wilaya zote ni tani 720, Je ni tani ngapi zilikusanywa kutoka katika wilaya ya Sikonge?
45. Katika mgawanyo fulani, Gatuka alipata 4080 pungufu ya rafiki yake Mponjoli ambaye alipata 19008. Ni kiasi gani Gatuka alipatiwa?
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 17
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 17
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
MTIHANI WA UTAMILIFU KATA
HISABATI DARASA LA SABA – MACHI, 2023
MUDA: MASAA 2
MAELEKEZO
SEHEMU A: MASWALI YA KUCHAGUA
1. Mika alivuna magunia 56 ya mahindi. Kama aliuza magunia yote kwa shilingi 140,000/=, je! kila gunia moja la mahindi aliliuza kwa shilingi ngapi?
(A) sh. 140,000 (B) 25,000 (C) 40,000 (D) 15,000 (E) 78,400 [ ]
2. Andika “milioni saba laki tisa na mia nane” kwa tarakimu
(A) 79,000,800 (B) 7,009,800 (C) 7,900,800 (D) 7,090,800 (E) 700,900,800 [ ]
3. Darasa la saba katika shule ya msingi Ndala ina wavulana 16 na wasichana 28. Je! uwiano wa wavulana kwa idadi ya wasichana ni upi?
(A) 16:28 (B) 28:16 (C) 4:7 (D) 4:11 (E) 11:16 [ ]
4. Kama Jerry alikula 5/7 ya mkate na Tonny akala 1/8 ya mkate huohuo. Je! sehemu ya mkate uliobakia ni ipi?
(A) 9/56 (B) 33/56 (C) 1/13 (D) 23/56 (E) 13/15 [ ]
5. Wanafunzi wa darasa la saba waliulizwa na mwalimu wao kurahisisha algebra ifuatayo;
Je! walipata jibu gani?
(A) 4a2b (B) 4a2b2 (C) 4a3b2 (D) a2b2 (E) 4ab2 [ ]
6. Ali anasoma darasa la tano, rafiki yake mmoja alimuuliza jina la umbo hilo hapo chini. Je! jina sahihi ni lipi?
(A) pembetatu mraba (B) pembe tatu gunia (C) pembetatu sawa (D) pembetatu msambamba (E) pembetatu pacha [ ]
7. Tafuta eneo la kabati hili ikiwa juu lipo wazi
(A) 1670m2 (B) 217m2 (C) 1150m2 (D) 2170cm2 (E) 1670cm2 [ ]
8. Bei ya gari imeongezeka kutoka shilingi 3,000,000 hadi shilingi 4,500,000. Tafuta asilimia ya bei iliyoongezeka. (A) 33.3% (B) 30% (C) 25% (D) 66.6% (E) 50% [ ]
9. Ni mchoro upi unaoweza kuunganisha majira ya nukta yafuatayo? A (5,3) B(4,5) C(0,3) D (1,1)
(A) mstatili (B) trapeza (C) duara (D) msambamba (E) mraba [ ]
10. Upi kati ya michoro ifuatayo sio pembe nne?
(A) trapeza (B) mraba (C) pembe tatu (D) msambamba (E) mstatili [ ]
11. Mwalimu Beni ametuambia tutafute K.K.S cha 56,117 na 6 kwa kutumia njia yoyote. Je! lipi ni jibu sahihi?
(A) 9 (B) 1 (C) 13 (D) 11 (E) 17 [ ]
12. Sheila alichelewa kulala na kuamka saa 05:45. Andika muda huo kwa masaa kumi na mbili.
(A) 5:45 asbh (B) 5:45 mchana (C) 17:45 asbh (D) 17:45 jioni (E) 5:17 [ ]
13. Mwalimu wako wa hesabu amekuuliza jibu la swali hili, (x-y) toa (x+y). Je! lipi ni jibu sahihi?
(A) -2y (B) +2y (C) 2x (D) 0 (E) 2xy [ ]
14. Taja namba shufwa zote zinazogawanyika kwa 6 zilizopo kati 20 – 40
(A) 24, 30, 36 (B) 32, 34, 36 (C) 22, 24, 28, 30 (D) 24, 30, 36, 40 (E) 30,24, 36, 38 [ ]
15. Babu alivuna matikiti maji 8 kwenye shamba lake na kuwagawia yatima. Siku moja alikula 31/2 na kuwapa yatima 17/8. Je! alibakiwa na matikiti maji mangapi?
(A) 23/8 (B) 2 (C) 25/8 (D) 45/8 (D) 5/8 [ ]
16. Darasa la sita walipewa mfululizo wa namba 1, 8, 27, 64, ____. Je! namba inayofuata ni ipi?
(A) 81 (B) 101 (C) 125 (D) 119 (E) 72 [ ]
17. Tafuta eneo la shamba lifuatalo
(A) 36m2 (B) 112m2 (C) 768m2 (D) 112m (E) 36m2 [ ]
18. Andika majira ya nukta X
(A) x (-2,-1) (B) x (0,2) (C) x (2,0) (D) x (2,1) (E) x (-0, +0) [ ]
19. Kuna mistari mingapi linganifu katika umbo hili la pembe tatu?
(A) 1 (B) 2 (C) 3 (D) 4 (E) 5 [ ]
20. Tafuta ujazo wa lita uliojaza chombo hapo chini (Lita 1 – 1000cm3)
(A) 8L (B) 8cm3 (C) 80L (D) 8000L (E) 800 cm3 [ ]
21. Badilisha 60% kuwa katika sehemu (a/b)
(A) 6/10 (B) 3/2 (C) 6/100 (D) 12/5 (E) 3/5 [ ]
22. Kuna lita 2/5 ngapi kwenye lita 10 za mafuta ya kupikia?
(A) 25 (B) 100 (C) 4 (D) 8 (E) 1/25 [ ]
23. Kipi ni kipeuo cha pili cha 9 kati ya namba zifuatazo?
(A) 1 (B) 3 (C) 81 (D) 29 (E) 9 [ ]
24. Katika takwimu 345.97 namba ipi inaonyesha makumi?
(A) 3 (B) 4 (C) 5 (D) 9 (E) 7 [ ]
25. Badili 608,864 kwenda kwenye maelfu
(A) 609,00 (B) 608,900 (C) 608,860 (D) 618,000 (E) 600,000 [ ]
26. Wakulima watatu wamechanga shilingi 80,000/= katika uwiano wa 2:5:9. Je! mkulima wa kwanza alipata kiasi gani? (A) 45,000 (B) 5000 (C) 25000 (D) 2000 (E) 10,000 [ ]
27. Wafanyakazi 12 walivuna heka 8 kwa siku 8. Wafanyakazi 18 wakaongezeka. Je! watavunakwa siku ngapi katika heka hizo? (A) siku 1 (B) siku 3 (C) siku 4 (D) siku 5 (E) siku 2 [ ]
28. Tafuta thamani ya “y” katika swali hili 3y+3 = 2y-2
3 (A) 5/2 (B) -3 (C) 3 (D) -5 (E) 4/3 [ ]
29. Jenereta lina uwezo wa kubeba lita 80 za dizeli. Ikiwa 40% ya dizeli yametumika, Je! sehemu ya ujazo wa dizeli uliobakia kwenye tanki ni kiasi gani?
(A) 32 (B) 48 (C) 2/5 (D) ½ (E) 3/5 [ ]
30. Benard ana pipi 24 na Ally ana pipi 72. Je! ni kiasi gai cha pipi Benard anatakiwa kukipata toka kwa Ally ili wawe na idadi sawa ya pipi?
(A) 27 (B) 18 (C) 24 (D) 16 (E) 20 [ ]
31. Ikiwa 7/8 ya namba iliyofichwa ni 21, Je! ¾ ya namba hiyo ni ipi?
(A) 24 (B) 18 (C) 12 (D) 28 (E) 14 [ ]
32. Darasa la tano njano walipewa kazi ya kutafuta jumla ya namba zilizopo kati ya 12 na 20. Lipi ni
jibu sahihi? (A) 49 (B) 32 (C) 30 (D) 64 (E) 45 [ ]
33. Andika 3.0695 katika nafasi mbili ya desimali. (A) 0.36 (B) 3.68 (C) 3.16 (D) 3.07 (E) 3.67[ ]
34. Namba fulani ukiizidisha yenyewe unapata 6561. Tafuta kipauo cha pili cha namba hiyo.
(A) 9 (B) 81 (C) 3 (D) 39 (E) 33 [ ]
35. Baba yake na Hadija alizaliwa mwaka 1944. Andika mwaka aliozaliwa kwa kirumi.
(A) MCMXCIV (B) MMXMLV (C) MCMXLIV (D) MCDXLIV (E) MCMXCIX [ ]
36. Wastani wa uzito wa wanafunzi watano ni kilogram 42. Kama uzito wa wanafunzi wane ni 54kg, 18kg, 48kg na 60kg. Tafuta uzito wa mwanafunzi wa tano kwa gramu.
(A) 35000g (B) 30000g (C) 50000kg (C) 40000g (E) 29000g [ ]
37. Gari lina viti 50. Kama 15 ni rangi nyekundu, tafuta sehemu inayowakilisha viti visivyo na rangi nyekundu. (A) ¾ (B) 5/7 (C) 3/5 (D) 7/10 (E) 3/10 [ ]
38. Ikiwa jumla ya mfululizo wa namba tatu witirini 57. Tafuta zao la namba hizo tatu.
(A) 21 (B) 14 (C) 784 (D) 6873 (E) 6783 [ ]
39. Badili 11/2% kuwa desimali
(A) 0.015 (B) 1.15 (C) 0.15 (D) 0.05 (E) 1.5 [ ]
40. Tafuta jumla ya 121/2 na 33/4
(A) 154/6 (B) 161/4 (C) 151/4 (D) 11/4 (E) 134/6 [ ]
SEHEMU B: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO
Kokotoa kwa makini kisha andika jibu sahihi
41. Grafu ifuatayo inaonyesha idadi ya wanafunzi waliohudhuria shuleni Jumanne hadi Ijumaa. Tafuta wastani wa siku tatu za mwanzo kisha kadiria jibu lako katika namba kamili.
42. Kama mzunguko wa mstatili ABCD hapo chini ni 26cm. Tafuta eneo la sentimita za mraba
43. Jumla ya pembe za ndani za umbo mraba ni 2x. Pembe nyingine mbili ni 70o na 80o. Tafuta thamani ya “X”
44. Siku moja mwalimu Yusufu aliwapa kazi wavulana wa darasa la saba wachimbe shimo, walipokuwa wanachimba na kufika urefu fulani walikutana na mwamba mgumu kama umbo la eneo lililotiwa kivuli katika mchoro hapo chini. Tafuta eneo lililotiwa kivuli katika mchoro hapo chini.
45. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha namna Mzee Mbwiga alivyoutumia mashahara wake wa mwezi. Kama alipokea shilingi 720,000 baada ya makato ya kodi, je! alitumia kiasi gani kwa chakula?
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 9
STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 9