HISABATI STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

MKOA WA SIMIYU HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI 

MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU KATA - FEBRUARI 2023 

DARASA LA SABA HISABATI

Muda : Saa 2:00 

Maelekezo 

 1.  Maelekezo Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).
 2. Jibu maswali yote.
 3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).
 4.  Jaza taarifa zote katika fomu ya OMR.
 5.  Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.
 6. Weka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:
 1.  Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hiclto kwa umakini kwa kutumia kifutio sail kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.
 2. Tumia penseli ya HR to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi 45.
 3.  Onesha wazi njia iliyotumika katika kujibu swali Ia 41 hadi 45 katika nafasi iliyotolewa kwenyc fomu ya OMR.
 4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO

Kwa swali la 1-40, kokotoa majibu, kisha chagua jibu sahihi na usilibe herufi yake kwenye karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Ni lipi kati ya majibu yafuatayo linalandana na Mia tisa sabini elfu mia nne arobaini na moja?

A: 9070441 B. 900000+400+70000+1+40

C. 700000+90000+400+40+1+40 D. 9000000+70000+0+400+40+1 E. 900000+70000+0+4000+1+40

2. John alibeba mzigo wenye uzani wa tani 0.75. Je, ni kilogram ngapi alizobeba John?

A: kg 750 B. kg 7500 C. kg 0.7500 D. kg 725 E. kg 705

3. Uzani wa ng’ombe 200 ni kilogramu 250.763. Ni tarakimu ipi katika uzito ulio rekodiwa iko katika nafasi ya thamani iliyo juu ya mia moja?

A: 0 B. 2 C. 7 D. 6 E. 3

4. Sadala alitembea umbali wa hektomita 50. Umbali huu ni sawa na umbali upi kati ya vizio vifuatavyo?

A: km 0.5 B. dam 5000 C. m 5000 D. dg 50500 E. sm 30000

5.Yafuatayo ni makundi yenye fedha za noti 100 za shilingi elfu kumi kama zilivyo hesabiwa na Salome. Je, ni kiasi gani cha fedha hizi zote kwa ujumla katika tarakimu?

 1. 100,000,000/=
 2. 1,000,000/=
 3. 10,000,000/=
 4. Shilingi milioni 200
 5. 1,000.000,000/=

6. Ng’ombe mmoja anaweza kutoa lita 5 na mililita 500 za maziwa kwa siku. Je, ng’ombe huyo atatumia siku ngapi kutoa lita 22 za maziwa ?

A: Siku 8 B. Siku 2 C. Siku 4 D. Siku 5 E. Siku 3

7. Idadi ya mbegu za ngano zilikusanywa na wanafunzi saba katika makundi ya mbegu; 7000000, 6000, 500000, 10, 30000, 100, 600000000 kwa kila mmoja. Je, ni jumla ya mbegu ngapi zilikusanywa kama namba moja?

A: 6007536110 B. 607536110 C.760536110 D. 670536110 E. 670563110

8. Sarafina hulipwa kiasi cha shilingi 204000 zaidi ya rafiki yake Ulimwengu. Ikiwa Ulimwengu hulipwa na kampuni kiasi cha shilingi 500500, ni kiasi gani cha fedha Sarafina hulipwa na kampuni?

A: 745000/= B. 704500/= C. 296500/= D. 296000/= E. 754000/=

9. Philemon alitakiwa aandike namba ndogo kuliko zote inayoweza kugawanywa kwa 6,9 na 12 bila baki. Unafikiri ni namba ipi aliyoiandika ni sahihi kati ya zifuatazo?

A: 3 B. 36 C. 48 D. 24 E. 120

10. Bosco ni mwanafumzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Mkanyageni. Alipewa na mwalimu wake jumla ya shilingi 3055000 kwa ajili ya kununulia ng’ombe. Ikiwa Bosco alinunua ng’ombe wanne(4) kwa jumla ya shilingi 2700500, Je ni kiasi gani cha fedha alibakiwa nacho?

A: 354500/= B. 435000/= C. 543500/= D. 435500/= E. 345500/=

11. Douglas alirekodi jumla ya uzito wa watoto wawili wenye jumla ya kilogram 57.8563. Ni kwa namna gani namba hii inaweza kuandikwa katika nafasi mbili za desimali?

A: Kg 58.00 B. Kg 50.85 C. Kg 578.56 D. Kg 75.86 E. Kg 57.86

12. Shule imesajili wanafunzi 200 katika mwaka wa masomo 2023. Ikiwa 35% ya wanafunzi waliosajiliwa wamesha wasili shuleni, Je ni wanafunzi wangapi bado hawajawasili shuleni?

A: 70 B. 230 C. 130 D. 103 E. 170

13. Odhiambo aliandika orodha ya namba tasa tano zinazofuatana. Kama mtaalamu wa Hisabati, orodha ipi ni sahihi kati ya hizi zifuatazo?

A: 1,2,3,5,7 B. 2,5,7,11,13 C. 7,11,13,15,17 D. 5,7,9,11,13 E. 3,5,7,11,13

14. Shulala alipanda miti katika mistari mitatu, ambapo kila mstari una mashimo 21. Ikiwa kila shimo alipanda miti minne, je alipanda jumla ya miti mingapi kwa pamoja?

A: 252 B. 84 C. 63 D. 225 E. 522

15. Baraka alikuwa na noti za shilingi 1000. Noti ya kwanza ilikua na namba 136700201 wakati noti ya mwisho ilikuwa na namba 136700300. Ikiwa noti hizo zilikuwa zimepangwa kwa namba zenye mtiririko mzuri, je Baraka alikua na jumla ya noti ngapi?

A: 99 B. 89 C. 100 D. 98 E. 101

16. Umbali wa barabara ni kilometa 270.007. Serikali ina tarajia kujenga umbali wa kilometa 198.13 kwa kiwango cha lami. Ni kilometa ngapi za barabara zitabaki bila lami baada ya ujenzi huo?

A: Km 70.807 B. Km 71.87 C. Km 877.71 D. Km 71.877 E. Km 7.1877

17. Kalunde aliambiwa na mwalimu wake aandike namba ndogo kuliko zote ambayo hutokana na tarakimu sita. Lipi unafikiri ni jibu lililokusudiwa na mwalimu kati ya majibu yafuatayo?

A: 210010 B. 102345 C. 110100 D. 012345 E. 1012345

18. Shule inamiliki theluthi ya ardhi ya kijiji. Ikiwa shule inamiliki kilomita za mraba 60, ni kiasi gani cha eneo la kilomita za mraba za ardhi linamilikiwa na Peter ikiwa anamiliki moja ya tisa ya eneo la kijiji?

A: 40 B. 80 C. 90 D. 20 E. 180

19. Watu watano walihudhuria mkutano wa kijiji. Walikaa kwenye viti vilivyokuwa vimewekwa namba kwa mpangilio wa 5, 7, 11, 13, _____ Je, ni namba ipi ya kiti iliwekwa kwenye kiti cha mtu wa tano?

A: 15 B. 14 C. 19 D. 23 E. 17

20. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya vitabu kwa masomo matano yanayofundishwa darasa la tano. Tafuta wastani wa idadi ya vitabu katika shule hiyo.

Jina la kitabu

Sayansi

Kiswahili

English

M/Jamii

Idadi

35

30

40

15

A: 82 B. 104 C. 20 D. 28 E. 140

21. Mkulima alipanda mbegu katika mashimo matano ya bustani yake. Ikiwa katika mashimo manne ya kwanza, kila moja lilikua na mbegu 4, 9, 16 na 25 kwa mpangilio huo. Je ni ipi ilikua jumla ya mbegu zilizopandwa katika mashimo yote matano?

A: 90 B. 360 C. 36 D. 63 E. 49

22. Bw. Kidulo alichora pembe nyuma ya kitabu chake ambayo ukubwa wake ulikua ni 63°. Kama mtaalamu wa Hisabati, ni lipi ni jina la pembe hiyo iliyochorwa na Bw. Kidulo?

A: Pembe butu B. Pembe kuu C. Pembe kali D. Pembe mraba E. Pembe nyoofu

23. Wakati wa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Singida United dhidi ya Mwadui FC, magoli yalikua yakifungwa kila baada ya dakika 18 ya mchezo. Ikiwa mchezo uliendeshwa kwa dakika 90 bila ya mapumziko, ni magoli mangapi yalifungwa kwa muda wote wa mchezo?

A: 10 B. 6 C. 19 D. 8 E. 5

24. Katika umbo, ukubwa wa pembe ya nje ni mara mbili ya ukubwa wa pembe ya ndani. Ni ipi kati ya pembe zifuatazo itakua ni ukubwa wa pembe ya nje?

A: 45° B. 120° C. 90° D. 60° E. 240°

25. Hidaya alijaribu kupanga namba katika machaguo yafuatayo kutoka ndogo kwenda kubwa. Kati ya namba hizi ni ipi alipaswa aanzie?

A: 2001 B. CMXCIX C. 1526 D. MCXIX E. MDCCCLXXXIII

26. Upande mmoja wa kasha la mche mraba ni sm 10. Ikiwa Bwana Heri atatumia kasha hilo kununulia maziwa, ni kiasi cha lita ngapi Bwana Heri atabeba?

A: L 10 B. L1.2 C. L 2.0 D. L 1000 E. L 1

27. Ngombola alikwenda sokoni na jumla ya shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kununulia bidhaa zifuatazo;-

 • Kilogramu 4 za sukari @ shilingi 5,000
 • Mifuko10 ya saruji @ shilingi 20,000
 • Dazani 5 za daftar @ shilingi 40,000 na
 • Simu 2 za mkononi @ shilingi 90,000.

Ni kiasi gani cha fedha alibakiwa nacho katika asilimia?

A: 60% B. 20% C. 75% D. 40% E. 30%

28. Umbo lifuatalo linalandana na umbo la nyumba ya Bw. Msemakweli. Ni kwa namna gani tunaweza kulitaja jina la umbo hili kuhusianisha na elimu ya maumbo (jiometri)?


A: Pentagon B. Hexagon C. Heptagon D. Octagon E. Decagon

29. Baba yangu alilima shamba kwa siku 2 na saa tano. Je, baba alitumia dakika ngapi?

A: 3180 B. 3420 C. 3080 D. 1440 E. 1280

30.

Gaucho alifunga magoli 240 pungufu ya rafiki yake Neymar ambaye alifunga magoli 890 katika kipindi cha maisha yake ya soka. Ni magoli mangapi walifunga wote kwa pamoja?

A: 650 B. 560 C. 1540 D. 1130 E. 1450

31.

Garimoshi liliondoka Kilosa majira ya saa 1945. Dakika 25 baadae, basi ambalo lilikuwa njiani likitokea Dumila likawasili Kilosa. Ni muda gani basi hilo liliwasili Kilosa katika mtindo wa saa 12?

A: 2:10 mchana B. 2010 hrs C. 8:45 usiku D. 8:10 asubuhi E. 2:10 usiku

32. Endapo Monica atatembea mara moja kuzunguka uwanja uliochorwa hapo chini, ni umbali gani atakuwa ametembea? (Tumia pai = 3.14)


A: m 741 B. m 614 C. m 740 D. m 714 E. m 7140

33. Kama Halima angeuza gauni lake kwa shilingi 1,200,000 angepata hasara ya shilingi 240,000. Ipi ilikuwa ni thamani halisi ya gauni hilo?

A: 2400000/= B. 960000/= C. 1440000/= D. 1040000/= E. 1240000/=

34. Zinduna alitumia jumla ya shilingi 25,500 kama matumizi yake ya kila siku katika mwezi Februari mwaka 2016. Ni kiasi gani cha fedha alikitumia kwa mwezi mzima?

A: 714000/= B. 741000/= C. 739500/= D. 765000/= E. 756000/=

35. Kitabu chenye kurasa mia moja kinaweza kusomwa na Ashura kwa saa 2 na dakika 12. Ashura atatumia muda gani kusoma vitabu 9 vya aina hiyo?

A: saa 19 dk 40 B. dk 1188 C. saa 18 dk 48 D. saa 19 dk 108 E. dk 1088

36. Kwenye uchaguzi wa kata mwaka 2014, Zidane alipata kura 378, Shumbana kura MXIX wakati Suzan akapata kura 608. Ni kura ngapi zilipigwa na wajumbe wa kata wakati wa uchaguzi huo?

A: MCV B. MCMXCV C. MMV D. MCIV E. MCV

37. Mfanyabiashara alikuwa na gunia moja la mahindi na akaliuza kwa faida ya 20%. Ikiwa aliliuza kwa kiasi cha shilingi 240,000, ni kiasi gani cha fedha alitumia kununulia hilo gunia la mahindi?

A: 200000/= B. 140000/= C. 40000/= D. 220000/= E. 20000/=

38. Galaga alikuwa na kamba yenye urefu wa mita 8 2/3 . Ikiwa aliamua kumpatia rafiki yake Mrope kipande chenye urefu wa mita 4 1/24 , ni mita ngapi ambazo Galaga alibakiwa nazo?

A: m 4 B. m 6 3/8 C. m 4 3/8 D. m 5 3/8 E. m 4 5/8

39. Bukuru alinunua kg 46 na dag 5 za unga wa mahindi. Akataka kuwapatia watu watano (5) ambao aliwaahidi kama zawadi ya kufanya kazi kwa bidii.

Je, kila mtu alipata kiasi gani?

A: kg 21 dag 9 B. kg9 dag 105 C. g9 dg 21 D. kg9 dag 21 E. dag 12 kg 9

40. David alirahisisha mtajo ufuatao hapo chini kama ilivyokua inahitajika urahisishwe. Lipi ni jibu sahihi kati ya yafuatayo ikiwa mtajo wenyewe ulikuwa 16x – x + 13 ?

A: 3x B. 2x C. 15x-13 D. 15x+13 E. 13x-x

SEHEMU B: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO

Kwa swali la 41-45, Tumia kalamu ya wino wa buluu au mweusi kukokotoa majibu katika nafasi ya karatasi maalumu ya kujibia (OMR) uliyopewa kwa kuonyesha kazi yako kwa usahihi.

41.  75% ya wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kibondo wanajua kusoma kwa ufasaha. Idadi ya wanafunzi iliyobaki hawawezi kusoma kwa ufasaha. Je, darasa hilo lina wanafunzi wangapi ikiwa idadi ya wanafunzi ambao hawawezi kusoma vizuri ni wanafunzi 40 ?

42.  Kwenye mzani wa uzito barabarani tani 250 na kg 750 zilirekodiwa kwa kipindi cha siku moja. Je, ni kiasi gani cha uzani wa magari kitarekodiwa kwa kipindi cha siku nne (4) ikiwa uzani wa siku hautobadilika?

43.  Fundi Saudi alianza kujenga kona ya nyumba ya Mwashamba katika majira ya nukta yaliyowakilishwa na herufi C. Andika majira ya nukta ya herufi ambapo fundi Saudi alianzia kujenga nyumba hiyo.


44.  Mchoro ufuatao unaonesha mgawanyo wa tani za zao la tumbaku zilizokusanywa mkoani Tabora kutoka wilaya mbalimbali. Ikiwa idadi ya tani zote zilizo kusanywa kutoka wilaya zote ni tani 720, Je ni tani ngapi zilikusanywa kutoka katika wilaya ya Sikonge?


45.  Katika mgawanyo fulani, Gatuka alipata 4080 pungufu ya rafiki yake Mponjoli ambaye alipata 19008. Ni kiasi gani Gatuka alipatiwa?

STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 17  

STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 17  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

MTIHANI WA UTAMILIFU KATA

HISABATI DARASA LA SABA – MACHI, 2023

MUDA: MASAA 2

MAELEKEZO

 1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
 2. Jibu maswali yote
 3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
 4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
 5. Tumia penseli ya HB tu.
 6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: MASWALI YA KUCHAGUA

1. Mika alivuna magunia 56 ya mahindi. Kama aliuza magunia yote kwa shilingi 140,000/=, je! kila gunia moja la mahindi aliliuza kwa shilingi ngapi?

(A) sh. 140,000 (B) 25,000 (C) 40,000 (D) 15,000 (E) 78,400 [     ]

2. Andika “milioni saba laki tisa na mia nane” kwa tarakimu

(A) 79,000,800 (B) 7,009,800 (C) 7,900,800 (D) 7,090,800 (E) 700,900,800 [     ]

3. Darasa la saba katika shule ya msingi Ndala ina wavulana 16 na wasichana 28. Je! uwiano wa wavulana kwa idadi ya wasichana ni upi?

(A) 16:28 (B) 28:16 (C) 4:7 (D) 4:11 (E) 11:16 [     ]

4. Kama Jerry alikula 5/7 ya mkate na Tonny akala 1/8 ya mkate huohuo. Je! sehemu ya mkate uliobakia ni ipi? 

(A) 9/56 (B) 33/56 (C) 1/13 (D) 23/56 (E) 13/15 [     ]

5. Wanafunzi wa darasa la saba waliulizwa na mwalimu wao kurahisisha algebra ifuatayo;


 Je! walipata jibu gani?

(A) 4a2b (B) 4a2b2 (C) 4a3b2 (D) a2b2 (E) 4ab2 [     ]

6. Ali anasoma darasa la tano, rafiki yake mmoja alimuuliza jina la umbo hilo hapo chini. Je! jina sahihi ni lipi?


(A) pembetatu mraba (B) pembe tatu gunia (C) pembetatu sawa (D) pembetatu msambamba (E) pembetatu pacha [     ]

7. Tafuta eneo la kabati hili ikiwa juu lipo wazi


(A) 1670m(B) 217m(C) 1150m(D) 2170cm(E) 1670cm2 [     ]

8. Bei ya gari imeongezeka kutoka shilingi 3,000,000 hadi shilingi 4,500,000. Tafuta asilimia ya bei iliyoongezeka. (A) 33.3% (B) 30% (C) 25% (D) 66.6% (E) 50% [     ]

9. Ni mchoro upi unaoweza kuunganisha majira ya nukta yafuatayo? A (5,3) B(4,5) C(0,3) D (1,1)

(A) mstatili (B) trapeza (C) duara (D) msambamba (E) mraba [     ]

10. Upi kati ya michoro ifuatayo sio pembe nne?

(A) trapeza (B) mraba (C) pembe tatu (D) msambamba (E) mstatili [     ]

11. Mwalimu Beni ametuambia tutafute K.K.S cha 56,117 na 6 kwa kutumia njia yoyote. Je! lipi ni jibu sahihi? 

(A) 9 (B) 1 (C) 13 (D) 11 (E) 17 [     ]

12. Sheila alichelewa kulala na kuamka saa 05:45. Andika muda huo kwa masaa kumi na mbili. 

(A) 5:45 asbh (B) 5:45 mchana (C) 17:45 asbh (D) 17:45 jioni (E) 5:17 [     ]

13. Mwalimu wako wa hesabu amekuuliza jibu la swali hili, (x-y) toa (x+y). Je! lipi ni jibu sahihi?

(A) -2y (B) +2y (C) 2x (D) 0 (E) 2xy [     ]

14. Taja namba shufwa zote zinazogawanyika kwa 6 zilizopo kati 20 – 40

(A) 24, 30, 36 (B) 32, 34, 36 (C) 22, 24, 28, 30 (D) 24, 30, 36, 40 (E) 30,24, 36, 38 [     ]

15. Babu alivuna matikiti maji 8 kwenye shamba lake na kuwagawia yatima. Siku moja alikula 31/2 na kuwapa yatima 17/8. Je! alibakiwa na matikiti maji mangapi?

(A) 23/8 (B) 2 (C) 25/8 (D) 45/8 (D) 5/8 [     ]

16. Darasa la sita walipewa mfululizo wa namba 1, 8, 27, 64, ____. Je! namba inayofuata ni ipi?

(A) 81 (B) 101 (C) 125 (D) 119 (E) 72 [     ]

17. Tafuta eneo la shamba lifuatalo


(A) 36m(B) 112m(C) 768m(D) 112m (E) 36m2 [     ]

18. Andika majira ya nukta X


(A) x (-2,-1) (B) x (0,2) (C) x (2,0) (D) x (2,1) (E) x (-0, +0) [     ]

19. Kuna mistari mingapi linganifu katika umbo hili la pembe tatu?


(A) 1 (B) 2 (C) 3 (D) 4 (E) 5 [     ]

20. Tafuta ujazo wa lita uliojaza chombo hapo chini (Lita 1 – 1000cm3)


(A) 8L (B) 8cm3 (C) 80L (D) 8000L (E) 800 cm[     ]

21. Badilisha 60% kuwa katika sehemu (a/b)

(A) 6/10 (B) 3/2 (C) 6/100 (D) 12/(E) 3/[     ]

22. Kuna lita 2/5 ngapi kwenye lita 10 za mafuta ya kupikia?

(A) 25 (B) 100 (C) 4 (D) 8 (E) 1/25 [     ]

23. Kipi ni kipeuo cha pili cha 9 kati ya namba zifuatazo?

(A) 1 (B) 3 (C) 81 (D) 29 (E) 9 [     ]

24. Katika takwimu 345.97 namba ipi inaonyesha makumi?

(A) 3 (B) 4 (C) 5 (D) 9 (E) 7 [     ]

25. Badili 608,864 kwenda kwenye maelfu

(A) 609,00 (B) 608,900 (C) 608,860 (D) 618,000 (E) 600,000 [     ]

26. Wakulima watatu wamechanga shilingi 80,000/= katika uwiano wa 2:5:9. Je! mkulima wa kwanza alipata kiasi gani? (A) 45,000 (B) 5000 (C) 25000 (D) 2000 (E) 10,000 [     ]

27. Wafanyakazi 12 walivuna heka 8 kwa siku 8. Wafanyakazi 18 wakaongezeka. Je! watavunakwa siku ngapi katika heka hizo? (A) siku 1 (B) siku 3 (C) siku 4 (D) siku 5 (E) siku 2 [     ]

28. Tafuta thamani ya “y” katika swali hili 3y+3 = 2y-2

3 (A) 5/2 (B) -3 (C) 3 (D) -5 (E) 4/3 [     ]

29. Jenereta lina uwezo wa kubeba lita 80 za dizeli. Ikiwa 40% ya dizeli yametumika, Je! sehemu ya ujazo wa dizeli uliobakia kwenye tanki ni kiasi gani?

(A) 32 (B) 48 (C) 2/5 (D) ½ (E) 3/5 [     ]

30. Benard ana pipi 24 na Ally ana pipi 72. Je! ni kiasi gai cha pipi Benard anatakiwa kukipata toka kwa Ally ili wawe na idadi sawa ya pipi? 

(A) 27 (B) 18 (C) 24 (D) 16 (E) 20 [     ]

31. Ikiwa 7/8 ya namba iliyofichwa ni 21, Je! ¾ ya namba hiyo ni ipi?

(A) 24 (B) 18 (C) 12 (D) 28 (E) 14 [     ]

32. Darasa la tano njano walipewa kazi ya kutafuta jumla ya namba zilizopo kati ya 12 na 20. Lipi ni

jibu sahihi? (A) 49 (B) 32 (C) 30 (D) 64 (E) 45 [     ]

33. Andika 3.0695 katika nafasi mbili ya desimali. (A) 0.36 (B) 3.68 (C) 3.16 (D) 3.07 (E) 3.67[     ]

34. Namba fulani ukiizidisha yenyewe unapata 6561. Tafuta kipauo cha pili cha namba hiyo.

(A) 9 (B) 81 (C) 3 (D) 39 (E) 33 [     ]

35. Baba yake na Hadija alizaliwa mwaka 1944. Andika mwaka aliozaliwa kwa kirumi.

(A) MCMXCIV (B) MMXMLV (C) MCMXLIV (D) MCDXLIV (E) MCMXCIX [     ]

36. Wastani wa uzito wa wanafunzi watano ni kilogram 42. Kama uzito wa wanafunzi wane ni 54kg, 18kg, 48kg na 60kg. Tafuta uzito wa mwanafunzi wa tano kwa gramu.

(A) 35000g (B) 30000g (C) 50000kg (C) 40000g (E) 29000g [     ]

37. Gari lina viti 50. Kama 15 ni rangi nyekundu, tafuta sehemu inayowakilisha viti visivyo na rangi nyekundu. (A) ¾ (B) 5/7 (C) 3/5 (D) 7/10 (E) 3/10 [     ]

38. Ikiwa jumla ya mfululizo wa namba tatu witirini 57. Tafuta zao la namba hizo tatu.

(A) 21 (B) 14 (C) 784 (D) 6873 (E) 6783 [     ]

39. Badili 11/2% kuwa desimali 

(A) 0.015 (B) 1.15 (C) 0.15 (D) 0.05 (E) 1.5 [     ]

40. Tafuta jumla ya 121/2 na 33/4 

(A) 154/6 (B) 161/4 (C) 151/4 (D) 11/4 (E) 134/6 [     ]

 SEHEMU B: MATENDO YA HISABATI, MAUMBO NA MAFUMBO

Kokotoa kwa makini kisha andika jibu sahihi

41. Grafu ifuatayo inaonyesha idadi ya wanafunzi waliohudhuria shuleni Jumanne hadi Ijumaa. Tafuta wastani wa siku tatu za mwanzo kisha kadiria jibu lako katika namba kamili.


42. Kama mzunguko wa mstatili ABCD hapo chini ni 26cm. Tafuta eneo la sentimita za mraba


43. Jumla ya pembe za ndani za umbo mraba ni 2x. Pembe nyingine mbili ni 70o na 80o. Tafuta thamani ya “X”

44. Siku moja mwalimu Yusufu aliwapa kazi wavulana wa darasa la saba wachimbe shimo, walipokuwa wanachimba na kufika urefu fulani walikutana na mwamba mgumu kama umbo la eneo lililotiwa kivuli katika mchoro hapo chini. Tafuta eneo lililotiwa kivuli katika mchoro hapo chini.


45. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha namna Mzee Mbwiga alivyoutumia mashahara wake wa mwezi. Kama alipokea shilingi 720,000 baada ya makato ya kodi, je! alitumia kiasi gani kwa chakula?


STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 9  

STANDARD SEVEN HISABATI EXAM SERIES 9  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256