KISWAHILI STANDARD SEVEN REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JINA LA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . 

NAMBA YA MTAHINIWA . . . . . . . . . . . . . . 

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA 

MTIHANI WA UTAMILIFU DARASA LA SABA APRIL 2024

SOMO: 01 - KISWAHILI

Muda: Saa 1:40

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali sita (06)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa na msimamizi wako kisha jibu kipengele cha i-v kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi

(i) Msimuliaji alipokuwa juu ya mti aliona nini? 

A. Mbwamwitu B. Majani C. Matawi D. Nyoka E. Mto [     ]

(ii) Msimuliaji alipotupa jicho pembeni mwa mti aliona nini? 

A. Kibanda B. Nyumba C. Mto D. Mtu E. Simba [     ]

(iii) Msimuliaji alikuwa anaelekea kijiji gani? 

A. Mtini B. Kibandani C. Nyumbani D. Mkoka E. Shambani [     ]

(iv) Mnyama gani alikaa karibu na kibanda chakavu? A. Nyoka B. Mbwamwitu C. Mamba D. Kima E. Simba [     ]

(v) Nahau “tupa jicho” maana yake ni nini? A. Sikia B. Angalia C. toa jicho D. Kodoa macho E. Kimbia [     ]

2. Chagua jibu sahihi kisha uandike herufi ya jibu hilo katika visanduku ulivyopewa ili kukamilisha kipengele cha (i )-(x)

(i) Mama alipanga vyombo kabatini. Kinyume cha neno panga ni ipi kati yafuatayo? 

A. Pangisha B. Pangusa C. Pangua D. Panua E. Pango [     ]

(ii) Nomino ipi inatokana na kubadilishwa kwa kitenzi lima? 

A. Limisha B. Limiana C. Limika D. Mkulima E. Kalime [     ]

(iii) Mama amekwenda safari atafika kesho jioni . Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno? 

A. Nomino B. Kielezi C. Kiwakilishi D. Kitenzi E. Kiunganishi [     ]

(iv) Mtoto alinunuliwa zawadi. Kitenzi alinunuliwa kipo katika kauli gani? 

A. Kutendana B. Kutendwa C. Kutenda D. Kutendwa E. Kutendesha [     ]

(v) Yupi kati ya wafuatao anafanya kazi ya kuazimisha vitabu katika maktaba? 

A. Mkutubi B. Muhtasi C. Mhandisi D. Nahodha E. Mhadhiri [     ]

(vi) Pale . . . . . . panapofuka moshi. 

A. Ndio B. Ndiyo C. Ndivyo D. Ndimo E. Ndipo [     ]

(vii) Katika neno “ Shanga” Mzizi wa neno ni upi? 

A. shanga B. sha C. sha D. shang E. a [     ]

(viii) Sisi ni wanafunzi wa darasa la saba. Neno sisi linawakilisha nafsi ya na ngapi? 

A.Nafsi ya kwanza umoja B. Nafsi ya tatu wingi C. Nafsi ya tatu umoja D. Nafsi ya kwanza wingi E. Nafsi ya pili wingi [    ]

(ix) Baba alimwagiza Juma, “ Nenda kanunue mbuzi sokoni”. Sentensi hii ipo katika kauli gani? 

A. Tata B. Taarifa C. Mazoea D. Halisi E. Desturi [    ]

(x) Katika maneno yafuatayo neno lipi halilandani na mengine ? 

A. Ndovu B. Mbogo C. Faru D. Korongo E. Nyumbu [     ]

3. Oanisha Sehemu A na sehemu B ili kukamilisha kazi ya fasihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika kipengele cha (i )- (v)

NA

SEHEMU A

JIBU

SEHEMU B

i .

Piga maji

A. Anajua

ii .

Methali inayotumika kuonya mtu asiyesikiliza ushauri wa wakubwa

B. Maji na Maziwa

iii .

Kiti cha dhahabu akikaliwi na watu

C. Maziwa na tui la nazi

iv .

Asiyeuliza

D.Kunywa maji

V .

Ukiona njigi utadhani njege, ukiona njege utadhani njigi.

E .Jua

F. Hana ajifunzalo

G. Moto

H. Kunywa Pombe

I. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

J. Kunywa chai

SEHEMU B: ( Alama 20)

4. Panga sentensi zifuatazo kwa mtiririko sahihi ili zilete maana kamili iliyokusudiwa kwa kuzipa herufi A,B,C,D na E.

  1. Kijiji hicho kipo karibu na hifadhi ya wanyama ya Mkomanzi.
  2. Siku moja, Busara na bibi yake walijihimu kuelekea shambani.
  3. Anaishi na bibi yake katika kijiji cha Mwendokasi
  4. Wakiwa wanakaribia kufika shambani, waliona wanyama wawili wakitembea kuelekea upande waliokuwa wanaelekea wao.
  5. Busara ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya msingi Tumaini.

5. Soma Shairi lifuatalokisha jibu maswali kipengele cha i -- v.

 Shairi

1. La mgambo likilia, ujue kuna jambo,

Ndugu kwenye familia, hutakiwi kenda kombo, 

Vijana wazee pia, lisikilize hili jambo,

Ni hatari kutumia dawa hizi za kulevya.


2. Dawa tukizitumia, haifai asilani, 

Jamii inakataa, hata vitabu vya dini,

Madhara yameshajaa, Kila pembe duniani, 

Ni hatari kutumia dawa hizi za kulevya.

MASWALI

  1. Taja vina vya kati na vina vya mwisho katika ubeti wa pili . . . . . . . . . . . .
  2. Mtu anayetunga mashairi anaitwa malenga. Je mwalimu wa malenga anaitwaje? . . . . . . . . . . .
  3. Shairi hili lina jumlaya beti ngapi? . . . . . . . . . . . .
  4. Kituo cha shairi ni kipi? . . . . . . . . . . . . . . . . .
  5. Pendekeza kichwa cha shairi hili . . . . . . . . . . . . . .

SEHEMU C: UTUNGAJI (Alama 10)

6. Andika simu ya maandishi kwa Kaka yako anayeitwa Juma Sioni S.L.P 2015 Shinyanga, ukimtaarifu kuwa Mama yenu mgonjwa amelazwa. Wewe tumia jina la Chausiku Sioni

JUMA SIONI, S.L.P 2015, SHINYANGA

i. .. . . . . . . . . . . . . . . . . .

ii. .. . . . . . . . . . . . . . . . . .

iii. .. . . . . . . . . . . . . . . . .

iv. .. . . . . . . . . . . . . . . . .

v. .. . . . . . . . . . . . . . . .

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 46  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 46  

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA MACHI 2024 

SOMO: 01 - KISWAHILI

Muda: Saa 1:40

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali sita (06)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa na msimamizi wako kisha jibu kipengele cha i-v kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi

(i) Kwa mujibu wa habari uliyosikiliza nini maana ya maisha? A. Maisha ni silaha B. Maisha ni vita C. Maisha ni uhai D. Maisha ni kuishi E. Maisha ni kusoma [     ]

(ii) Kwanini mwanafunzi upo shuleni? A. ili kupambana B. ili kunoa silaha C. ili ukue vyema D. ili uweze kujua maana ya maisha E. ili kucheza na wenzako [     ]

(iii) Ni wapi mtu huweza kujifunza maana ya maisha? A. shuleni B. chuoni C. hakuna sehemu yoyote D. chuoni na shuleni E. kanisani [     ]

(iv) Ikiwa mtu anatamani kuwa na nyumba,gari au mali yampasa kufanya nini? A. kuishi B. kwenda shule C. kuhamia mjini D. kuanzisha biashara E. kupambana [     ]

(v) Kwanini mnasisitizwa kutumia vyema muda wenu muwapo shuleni? A. ili kufaulu vyema B. ili kuepuka maisha C. ili kuyashinda maisha D. ili kutojuta baadaye E. ili kukua vyema

2. Chagua jibu sahihi na kisha uandike herufi ya jibu sahihi hilo katika sehemu ya kujibia.

(i) Walifanya kazi ile bega kwa bega hadi ilipokamilika. Nahau “bega kwa bega” inafafanuliwa na kifungu kipi cha maneno? A. kujituma sana B. walishirikiana kwa pamoja C. walitumia nguvu nyingi D. walifanya kwa uzalendo E. walitumia maarifa sana [     ]

(ii) Nahau ipi yenye maana ya “kuzama au kuogelea majini?” A. piga maji B. zama maji C. piga mbizi  D. piga kumbo E. piga zengwe [     ]

(iii) “Utakapowasili hapa utahutubia wananchi”. Mzungumzaji ametumia nafsi gani kati ya hizi? A. nafsi ya pili umoja B. nafsi ya kwanza wingi C. nafsi ya kwanza umoja D. nafsi ya tatu umoja E. nafsi ya tatu wingi [     ]

(iv) “Yanga wamefuzu katika hatua ya mtoano”. Kauli hiyo inawakilisha nafsi ipi kati ya hizi zifuatazo? A. nafsi ya kwanza wingi B. nafsi ya pili wingi C. nafsi ya kwanza umoja D. nafsi ya tatu umoja E. nafsi ya tatu wingi [     ]

(v) “Aminata amefaulu mtihani”, mwalimu alisema. Hiyo ni aina gani ya kauli kati ya hizi zifuatazo? A. mazoezi B. halisi C. tata D. taarifa E. tendwa [     ]

(vi) “Juma anasoma ingawa Neema anacheza”. Neno “ingawa” ni aina gani ya neno? A. kitenzi B. kihisishi C. kiiunganishi D. kielezi E. kiwakilishi [     ]

(vii) Rehema mama yake Mary. Neno linalokamilisha sentensi hii ni lipi? A. siyo B. sio C. sie D. siye E. si [     ]

(viii) Hapa alipozikwa hayati Ali Hassan Mwinyi. A. ndiko B. ndimo C. nipo D. ndipo E. ndicho [     ]

(ix) “Sitakubali kuondoka”. Neno “sitakubali” liko katika hali gani? A. ukanushi B. mazoea C. timilifu D. endelevu E. halisi [     ]

(x) “Damu ni nzito kuliko maji”. Methali hii inahusiana na ipi kati ya hizi zifuatazo? A. mchumia juani hulia kivulini B. penye nia pana njia C. mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe D. mbio za sakafuni huishia ukingoni E. baada ya dhiki faraja [     ]

3. Katika sehemu hii oanisha methali zinazofanana kutoka sehemu A na B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi

Sehemu A

Sehemu B

  1. Usipoziba ufa, utajenga ukuta [     ]
  2. Mchumia juani, hulia kivulini [     ]
  3. Mvumilivu hula mbivu [     ]
  4. Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo [     ]
  5. Mchagua nazi huambulia koroma [     ]
  1. Mdharau mwiba, mguu huota tende
  2. Mchagua jembe, si mkulima
  3. Samaki mkunje, angali mbichi
  4. Polepole ndio, mwendo
  5. Jembe halimtupi, mkulima
  6. Kidole kimoja hakivunji, chawa
  7. Umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu

SEHEMU B (ALAMA 20)

4. Katika sehemu hii kamilisha sentensi kadri ulivyoulizwa kwenye kipengele husika

(i) Meza, kabati, kiti na kitanda kwa neno moja huitwaje?                                                

(ii) Abdalah alitapanya mali za urithi. Kinyume cha neno tapanya ni nini?                                                

(iii) “Kazi ya Halima ni ya kijungujiko”. Kazi ya kijungujiko ni kazi ya aina ipi?                                                

(iv) Kitoto hiki kinacheza kitoto. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina ipi ya maneno?                                                    

(v) Nashon hufanya kazi ya kuhifadhi na kuazimisha vitabu kwa wasomaji katika maktaba ya mkoa. Je, Nashon ni nani?                                               

5. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata

Kaitwa mahakamani, popo kujibu shitaka, 

Hakimu naye makini, hadhira shauku tua, Atakiwa abaini, 

kwa ulimi kutamka, 

Ajitetee bayana, ni mnyama au ndege

Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea, 

Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea, 

Sina jadi na kunguru, ila na pundamilia,

Mimi ni mnyama huru, amini ninakwambia,

Tukidaiwa ushuru, kwa Wanyama nalipia.

Ni kweli popo napaa, na mabawa nimepata, 

Lakini mimi nazaa, hilo halina utata,

Nazaa na kunyonyesha, sina undugu na bata

Wale wanaopotosha , niwaonyeshe matiti.

 Maswali

(i) Ni sababu ipi inayomfanya popo akatae ya kuwa yeye si ndege?                                      

(ii) Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi huitwaje?                                   

(iii) Katika ubeti wa pili popo anasema, “sina jadi na kunguru”, usemi “sina jadi” una maana gani?                                          

(iv) Kutokana na shairi hili, unadhani ni tuhuma gani zilikua zinamkabili popo?                                                    

(v) “Hakimu makini, hadhira shauku tua”. Unaelewa nini kuhusiana na neno hadhira?                                             

SEHEMU C : UTUNGAJI (ALAMA 10)

6. Ichunguze barua rasmi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata;-

Tafadhali husika na barua hii.


Shule ya Msingi Ugele,

S.L.P. 165,

RINGO

Mimi ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule yako. Ninaomba ruhusa ya kushiriki mashindano ya kanda ambayo yatafanyikia katika uwanja wa Samora siku ya Alhamis. Mashindano hayo yataanza mnamo saa 2:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 8:30 mchana.

Ahsante

Baada ya kukamilisha kuiandika barua hiyo Lashack aliambiwa na mwalimu wake kuwa barua yake ina mapungufu mengi na kuifanya ikose sifa za kuitwa barua rasmi. Taja vipengele vitano vinavyokosekana katika barua hii.

  1.                                                    
  2.                                                    
  3.                                                    
  4.                                                    
  5.                                                    

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 43  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 43  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA APRIL 2024 

SOMO: 01 - KISWAHILI

Muda: Saa 1:40

Maelekezo: 

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye maswali saba (06). 
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika kila swali iii kujibu vipengele husika kwa usahihi. 
  4. Jaza taarifa zako (jina, shule nk) katika nafasi uliyopewa hapo juu. na kwenye nafasi uliyopewa katika kila ukurasa. 
  5. Tumia penseli kuchora kama kutakua na swali la kuchora, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa maj ibu yote ya kuandika. 
  6. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha upimaji.

SEHEMU A (Alama 20 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu kipengele cha (i)- (v), kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na uiandike katika parandesi.

i) Mutalemwa ni kijana mwenye umri wa miaka mingapi?

A: Miaka kumi B: Miaka nane C: Miaka tisa D: Miaka saba E: Miezi kenda [     ]

ii) Nini maana ya msemo “aghalabu” kama ulivyotumika katika habari?

A: Mara nyingi B: Mara chache C: Mara moja D: Angalau E: Kwa hasira [     ]

ii) Nani alimuokoa Mutalemwa alipokuwa akiraruliwa na mbwa?

A: Mama yake B: Mutashobya C: Mutahaba D: Kokubanza E: Kyaruzi [     ]

iv) Mutalemwa alitibiwa kwa muda gani?

A: Siku sita B: Siku mbili C: Wiki tatu D: miezi mitatu E: Siku tatu [     ]

v) Mbwa alimrarua Mutalemwa maeneo gani ya mwili wake?

A: Miguuni na usoni B: Miguuni na mikononi C: Miguuni na shingoni D: Mikononi na kichwani E: Miguuni na kiunoni [     ]

2. Katika kipengele cha (i) – (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha iandike katika parandesi.

i) Hapo kabla Fatuma na Musa walikuwa ni marafiki wakubwa. Ila ilitokea siku moja Musa alimnyima peremende Fatuma. Tangu siku hiyo Fatuma alimkasirikia sana Musa wakawa hawapikiki chungu kimoja. Msemo wenye ukolezo una maana gani?

A: Hawaishi pamoja B: Hawatembei pamoja C: Hawali pamoja D: Hawaelewani E: Hawazungumzi pamoja [     ]

ii) Wenyewe wangeweza kwenda hata ninyi pia mngekwenda. Katika sentensi hii maneno wenyewe na ninyi yametumika kama aina ipi za maneno?

A: Nomino B: Viunganishi C: Viwakilishi D: Vivumishi E: Vielezi [     ]

iii) Watoto wanaopenda kukimbizana barabarani wanaweza kugongwa na magari. Kiarifu cha sentensi hii kipo katika kauli gani?

A: Kutendana B: Kutendwa C: Kendewa D: Kutenda E: Kutendea [     ]

iv) Viongozi wengi walikuwa wakila mlungula ili kutoa huduma ambayo wananchi walipaswa kuipata bure. Lakini tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuwatumbua. Nini maana ya nahau kula mlungula?[     ]

A: Kula pesa B: Kula fadhila C: Kutoa huduma bora D: Kupokea rushwa E: Kutoza hela

v) Watoto wanapenda kutazama vikaragosi kwenye runinga. Tungo hiyo ipo katika nafsi gani?

A: Nafsi ya I umoja B: Nafsi ya II umoja C: Nafsi ya III umoja D: Nafsi ya II wingi E: Nafsi ya III wingi [     ]

vi) Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana sawa na isemayo;- “Mchakacho ujao haulengwi jiwe”

A: Jiwe moja moja hujenga nyumba ya mawe. B: Jiwe la kutupa ngomani humpiga wako

C: Jina jema hung’aa gizani D: Jino la pembe si dawa ya pengo E: Jina jema ni hazina [     ]

vii) “Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke.” Mwalimu Manjia aliwataka wanafunzi wategue kitendawili hicho kwa kutumia picha. Ungekuwepo darasani ungechagua picha gani kati ya hizi?

[     ]

viii) Mchomoeni nyoka shimoni. Kuna silabu ngapi katika neno lililopigiwa mstari?

A: Tisa B: Tano C: Sita D: Nane E: Nne [     ]

(ix) Uliponifanyia ubaya ulifurahia sana na kunicheka, sasa na mimi nimekufanyia ubaya huo huo kama ulionifanyia unaona nimekuonea. Ama kweli wahenga walituambia;- . . ...

A: Shukurani ya punda ni mateke B: Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki C: Hakuna masika yasiyokuwa na mbu D: Mtaka cha uvunguni sharti ainame E: Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu [     ]

x) “Lala chini la sivyo nitakupasua kichwa chako.” Badili kauli hiyo kuwa taarifa.

A: Aliambiwa kuwa lala chini la sivyo angepasuliwa kichwa chake.
B: Aliambiwa kwamba alale chini la sivyo atapasuliwa kichwa chake.
C: Aliambiwa kuwa alale chini vinginevyo angepasuliwa kichwa.
D: Aliambiwa kuwa alale chini vinginevyo angepasuliwa kichwa chake.
E: Aliambiwa kwamba lala chini vinginenvyo nitalipasua kichwa chako. [     ]

3. Oanisha msamiati uliopo katika Orodha A na maana yake iliyopo kutoka Orodha B, kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika nafasi ya majibu.

Na. Orodha A Majibu Orodha B
(i) Mtu anayefanya biashara ya kuuza vitu rejareja
A. Kuli
(ii) Mtu anayetangaza bei na kuuza vitu wakati wa mnada
B. Utingo
(iii) Mtu anayefanya kazi ya kupakia na kupakua mizigo bandarini au forodhani
C. Kondakta
(iv) Chete ifanywayo mara moja kwa juma au mwezi
D. Mpagazi
(v) Mtu anayefanya kazi ya kupakia na kupakua mizigo
kwenye gari.

E. Mchuuzi



F. Mnadi



G. Mnuni



H. Gulio

SEHEMU B (Alama 20)

4. Chunguza picha zifuatazo kisha jibu maswali yote katika kipengele cha (i) – (v) kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi.


i) Jina la tunda linalowakiliswa na herufi A limeundwa na konsonanti ngapi? . . . . . . .
ii) Kuna silabi ngapi katika jina la tunda linalowakilishwa na herufi C? . . . . . . . . .
iii) Zipo irabu ngapi katika jina la tunda linalowakilishwa na herufi B? . . . . . . . . . .
iv) Kuna aina ngapi za irabu katika jina la mnyama anayewakilishwa na herufi D? . . . . . . ...
v) Ukidondosha silabi moja ya jina la samaki anayewakilishwa na herufi E, utapata jina la aina gani ya kifaa? . . . . . . . . . . . . .

5. Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali katika kipengele cha (i) - (v) kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

Omari na Sara wanasoma katika shule ya msingi Kiloleni. Siku moja Omari aliona makala kwenye gazeti la Mwananchi. Akamwita rafiki yake Sara ili waisome pamoja. Makala yenyewe ilihusu utunzaji wa mazingira. Kwa pamoja walisoma vizuri na kujionea umuhimu wa utunzaji wa mazingira. Pia waliona madhara yanayoweza kuwapata ikiwa hawatatunza mazingira kama vile kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

Katika Makala hiyo, kulikuwa na tangazo la mashindano ya uandishi wa insha kuhusu mazingira kwa wanafunzi wote wa shule za msingi. Na mshindi atapewa zawadi ya kutembelea Zanzibar kwenda kujionea mazingira ya mji mkongwe. Omari na Sara kwa pamoja walikata shauri kushiriki shindano hilo ili ndoto yao ya kutembelea Zanzibar itimie. Walishauriana kwenda kwenye maktaba ya shule yao ili wakatafute vitabu vinavyoeleza zaidi kuhusu mazingira. Sara alipata kitabu kilichoitwa “Tutunze tukutunze” Alimuita rafiki yake, “Omari njoo uone hiki kitabu, inaonekana kitakuwa ni jibu la kile tunachokitafuta” Baada ya Omari kukitazama akasema “Swadakta! Hapa sasa ndio penyewe.” Haraka walikwenda chini ya mti kivulini walijisomea hadi pale waliporidhika kwamba wameelewa vizuri. Baada ya kumaliza kusoma kila mmoja aliandika Insha kivyake na kuipeleka kwenye mashindano. Wote waliandika vizuri lakini Sara alijiongeza kwa kuandika hitimisho zuri. Alishauri serikali kuweka sheria kali ili kuwakomesha wachafuzi wa mazingira. Kipengele hicho ndicho kilimfanya Sara aibuke kidedea kwenye shindano.

Maswali

(i) Kwa unavyofahamu wewe, nini maana ya Mazingira? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(ii) Omari aliona makala kwenye nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... . . . .
(iii) Madhara ya kutotunza mazingira ni pamoja na nini? . . . . . . . . . . . . . . . ... . . . .
(iv) Sara alipata kitabu gani kule maktaba? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(v) Unadhani ni kwa nini Sara aliibuka kidedea kwenye shindano hilo? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

SEHEMU C: (Alama 10)

Umepewa insha yenye sentensi (5) zilizoandikwa bila kufuata mpangilio maalum, zipange sentensi hizo ili zilete mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A-E katika kujibu kipengele cha (i) – (v)

(i) Maendeleo hayo hayakuja kama ndoto bali ni kwa maarifa na juhudi kubwa.
(ii) Katika nchi ya Tanzania, kuna vijiji vingi sana na vingi kati ya hivyo vimepiga maendeleo.
(iii) Hata hivyo bado ipo haja ya kusukuma maendeleo zaidi katika vijiji ambavyo bado vipo nyuma.
(iv) Kwa kufanya hivyo kutasaidia kumwezesha kila mwananchi kufikiwa na huduma za jamii kwa karibu.
(v) Juhudi hizo zilitokana na msukumo wa viongozi wa serikali na kufanya kazi kwa kikoa.

Kisanduku cha majibu

(i) (ii) (iii) (iv) (v)




.

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 36  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 36  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI


MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA SABA FEBRUARI 2024 

SOMO: KISWAHILI

Muda: Saa 1:40

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu mbili: A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu. 
  3. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 35)

Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la 1 - 5, kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya kujibia.

1. Kwa mujibu wa habari uliyosomewa, unadhani kina Juju walijuaje kuwa mahali mashua yao ilipogota kuna karibia kukucha?

A: Walisikia sauti za watu B: Walisikia sauti za ndege C: Walisikia sauti za wanyama D: Walisikia jogoo akiwika E: Walisikia jogoo akilia [     ]

2. Imeelezwa kuwa dhoruba ilitokea katika kisiwa gani?

A: Wete B: Pemba C: Nungwi D: Zanzibar E: Unguja [     ]

3. Kama umesikiliza kwa makini habari uliyosomewa, tuambie jina la mtu aliyekuwa wa kwanza kuhisi mahali mashua yao ilipogota palikuwa panakaribia kukucha.

A: Janja B: Jojo C: Jaja D: Juju E: Jeje [     ]

4. Baada ya dhoruba kutokea, vyombo vingi walivyosafiria wavuvi vilienda mrama. Nini maana ya msemo kwenda mrama?

A: Kupoteza nguvu B: Kwenda kasi C: Kupoteza mwelekeo D: Kwenda taratibu E: Kwenda ovyoovyo [     ]

5. Kwa mujibu wa habari hiyo, unadhani Juju na wenzake walikuwa ni akina nani?

A: Walinzi wa bahari B: Wavuvi C: Wafanyakazi wa melini D: Wafanyabiashara E: Wakulima [     ]

Katika swali la 6 - 35, weka kivuli katika herufi ya jibu lilio sahihi katika karatasi ya kujibia.

6. Mwalimu Masumbuko ana utaratibu wa kuandikiwa majina ya wasumbufu darasani. Bainisha kauli ya utendaji ya sentensi hiyo.

A: Kutendewa B: Kutendwa C: Kutendeka D: Kutendana E: Kutendeana [     ]

7. Ningekuwa na hela ningelima shamba lote. Badili sentensi hiyo kuwa katika kauli ya kutendesha?

A: Nikiwa na hela nitalimisha shamba lote B: Ningekuwa na hela ningelimia shamba lote C: Ningekuwa na hela ningelimisha shamba lote D: Ningekuwa na hela ningelimiana shamba lote
E: Ningekuwa na hela shamba lote lingelimika [     ]

8. Tulikwenda kumsalimia mwanafunzi mwenzetu aliyefiwa na wazazi wake na tukampa . . . ..Tumia moja ya nahau zifuatazo kukamilisha sentensi hiyo.

A: mkono wa heri B: mkono wa Idi C: mkono wa buriani D: mkono wa ihsani E: mkono wa pongezi [     ]

9. Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar walikula kiapo ili wasitoe siri ya kambini. Ni nahau ipi inasadifu msemo kula kiapo cha siri?

A: Kata tamaa B: Pata ahueni C: Tia hatiani D: Kaza kamba E: Kula yamini [     ]

10. Utatumia nahau gani kati ya zifuatazo kumuelezea mtu mwenye tabia ya kukasirika kila wakati?

A: Timua mbio B: Kunja ndita C: Chanja mbuga D: Kaa chonjo E: Piga ishara [     ]

11. “Mzee Kondo amekuwa na tabia ya kujisomea magazeti kila siku.” Tambua nafsi ya sentensi hiyo.

A: Kwanza umoja B: Pili umoja C: Tatu umoja D: Pili wingi E: Tatu wingi [     ]

12. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ipo katika nafsi ya pili wingi?

A: Tumekunywa maziwa yote. B: Amekunywa maziwa yote. C: Wamekunywa maziwa yote D: Mmekunywa maziwa yote. E: Umekunywa maziwa yote [     ]

13. Bainisha kauli taarifa ya sentensi hii;- “Nitaimba wimbo wangu kesho”

A: Alisema kuwa ataimba wimbo wake kesho B: Alisema kuwa angeimba wimbo wake kesho C: “Alisema kuwa angeimba wimbo wake siku inayofuata” D: Alisema kesho ataimba wimbo wake
E: Alisema kuwa angeimba wimbo wake siku inayofuata

14. Walikuwa wameanzisha bustani yao. Kama ungeambiwa uibadili sentensi hiyo kuwa katika kauli taarifa, lipi lingekuwa ni jibu lako?

A: “Tutaanzisha bustani yetu B: “Tumeanzisha bustani yetu” C: Tumeanzisha bustani yetu D: “Tulianzisha bustani yetu” E: “Tunaanzisha bustani yetu” [     ]

15. Kama ujuavyo methali huwa na pande mbili zinazokamilishana. Katika muktadha huo, upi ni ukamilisho wa methali ifuatayo? “Mkono uliotia jiwe majini . . . . . . . . . . . ..

A: ndio utakaotia jiwe kichwani B: ndio utakaokatwa C: ule ule utaepua D: ule ule utaopoa E: ndio huo utakaolipasua [     ]

16. Unaye rafiki anayependa kufanya mambo bila kuyajua undani wake na mara zote mambo hayo huishia kumdhuru mwenyewe. Utatumia methali gani kumuonya mtu huyo?

A: Usiibe kabla giza halijaingia B: Usichokula usikichachishe C: Usifunue kinywa kama hukijui ulacho D: Usile na kipofu ukamshika mkono E: Usiache mbachao kwa msala upitao [     ]

17. Methali zifuatazo zinalandana kimaana isipokuwa moja tu. Tumia ujuzi wako kuitambua.

A: Panya wengi hawachimbi shimo B: Kidole kimoja hakiui chawa C: Jifya moja haliinjiki chungu D: Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu E: Mkono mmoja haulei mwana [     ]

18. Chuguza methali zifuatazo kisha ubaini moja unayoweza kuitumia kumuonya mtu mnyimi asiyependa kutoa akiogopa ataishiwa.

A: Mkono usioweza kuukata ubusu B: Mkono utoao ndio upatao C: Mpata radhi hupata hadhi D: Mpanda hila huvuna ufukara E: Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe [     ]

19. Tumia ujuzi wako wa lugha za kifasihi, kubaini kitendawili ambacho jibu lake ni kibatari.

A: Tatu tatu hadi Ulaya B: Napigwa faini kosa silijui C: Natumia nne, mbili, tatu D: Jini mnywa damu, haangazi bila damu E: Mwavuli wa mwitu una nguzo moja [     ]

20. Kwa mfano umepita karibu na shamba la minazi na katika moja ya mnazi ukamuona mtu akichuma na kudondosha nazi chini. Ni kitendawili kipi kitakujia kichwani kutokana na ulichokiona?

A: Amchukuapo hamrudishi B: Amekula ncha mbili C: Ajihami bila silaha D: Ana mali lakini nguo havai E: Aliyefuatwa amekuja bali aliyefuata hajaja [     ]

21. Ni kundi lipi la maneno ambalo limebeba nomino za dhahania pekee?

A: Utukufu, Upole, Ungo, Ukarimu B: Uzuri, Shibe, Upendo, Hasira C: Upepo, Njaa, Kima, Kiu D: Mapenzi, Uchungu, Chuma, Chuki E: Ubaya, Zuri, Ukingo, Unyenyekevu [     ]

22. Laiti ningejua kuwa yeye hapendi mayai nisingempikia. Neno yeye limetumika kama aina gani ya neno?

A: Kivumishi B: Nomino C: Kiwakilishi D: Kielezi E: Kiunganishi [     ]

23. Wanafunzi wa shule ya Mapambano wamekwenda ziara ya mafunzo. Maneno yenye ukolezo na mstari yanasifa gani inayofanana?

A: Yote ni nomino B: Yote ni viunganishi C: Yote ni vihisishi D: Yote ni vielezi E: Yote ni vihusishi [     ]

24. Kama ukidondosha silabi ya mwisho katika neno sakafuni, utapata aina gani ya neno?

A: E B: N C: T D: U E: V [     ]

25. Kalulu, mwanafunzi wa darasa la tano alisema “Nimekwenda nyumbani nimemkuta baba hayupo” Unadhani Kalulu alikosea wapi?

A: Kusema alimkuta wakati hakumkuta B: Kusema alimkuta kumbe yupo C: Kusema nilimkuta badala ya nilifika D: Kusema nilimkuta wakati hakwenda E: Kusema hakumkuta wakati hayupo [     ]

26. Mwalimu angalifundisha vizuri . . . . . . ..Kifungu kipi kinakamilisha kwa usahihi sentensi hiyo?

A: tungelifaulu B: tungafaulu C: tungefaulu D: tutafaulu E: tungalifaulu [     ]

27. Mama amenituma mkate uliotengenezwa kwa unga wa nafaka kwa ajili ya kunywea na chai asubuhi. Kwa neno moja unadhani mama amenituma nini?

A: Andazi B: Mofa C: Bumunda D: Chapati E: Kababu [     ]

28. Daktari alitupa ufafanuzi wa ugonjwa uliokuwa unamsumbua babu. Kipi ni kisawe cha neno lenye mstari?

A: Matibabu B: Hotuba C: Fasili D: Chanzo E: Sababu [     ]

29. Garimoshi . . . . .tutaanza safari yetu. Ni muundo upi unafaa kukamilisha sentensi hiyo?

A: ikija B: akija C: vikija D: likija E: kikija [     ]

30. Chunguza maneno yafuatayo kisha ubaini neno lililotofauti na mengine.

A: Kicheko B: Ucheshi C: Kichekesho D: Cheka E: Mchekeshaji [     ]

31. Unaitambuaje Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa hapa nchini Tanzania kati ya taasisi zifuatazo?

A: BAKITA B: MKUKUTA C: MKURABITA D: TAKUKURU E: KIUTA [     ]

32. Shangazi Mage ni mfanyabiashara wa nafaka pale katika soko la Tandika. Unafikiri Shangazi Mage anauza bidhaa gani?

A: Shuka, Vitenge na Khanga B: Viazi, Mihogo na Magimbi C: Mchele, Ulezi na Mahindi D: Mabegi, Mikanda na Viatu E: Machungwa, Maembe na Maparachichi [     ]

33. Mwazani, mwanafunzi wa darasa la sita ameshindwa kuyapanga maneno yafuatayo kialfabeti. Ukiwa kama mjuzi wa matumizi ya kamusi lipi litakuwa ni jibu lako utakalomsaidia Mwazani? [buza, bubu, bunga, bunge, buti]

A: Bubu, Bunga, Bunge, Buza, Buti B: Bubu, Bunge, Buti, Buza, Bunga C: Bunga, Bubu, Bunge, Buti, Buza D: Bubu, Bunga, Bunge, Buti, Buza E: Bunga, Bunge, Bubu, Buti, Buza [     ]

34. Kwa mujibu wa elimu ya viambishi, unafikiri katika neno hili “amemjengea” vipi ni viambishi awali?

A: ame- B: amem- C: a- D: -jeng- E: -ea [     ]

35. Kabla ya uhuru wa nchi yetu, babu zetu walinyanyasika sana chini ya utawala wa kikoloni. Neno lenye mstari lina silabi ngapi?

A: Saba B: Nane C: Tano D: Kumi na nne E: Sita [     ]

SEHEMU B: (Alama 5)

Umepewa insha yenye sentensi (5) zilizoandikwa bila kufuata mpangilio maalum, zipange sentensi hizo ili zilete mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E. Siliba herufi ya jibu sahihi.

36. Bundala aliwaona wanyama wawili kwa mbali wakitembea kuelekea upande wao. [     ]

37. Bibi alinyanyua shingo ili awatazame vizuri, akasema, “Wale sio ng’ombe ni tembo. [     ]

38. Wakiwa wanakaribia kufika shambani, [     ]

39. Bundala aliuliza, “Umejuaje kuwa wale ni tembo?” Bibi akajibu nimeona masikio na mikonga [     ]

40. Alimshika bibi yake kwa woga, huku akisema, “Bibi! bibi! Unawaona wale ng’ombe?” [     ]

SEHEMU C: (Alama 10)

Soma kwa makini utenzi ufuatao kisha jibu swali la 41 - 45 kwa kuandika jibu katika fomu ya kujibia.

Kuwajuza natamani,
Na ukweli ujueni,
Somo kuwapatieni,
Faida yake mjue.

Dunia kama Kijiji,
Ni TEHAMA usihoji,
Marekani Msumbiji,
Ni mafupi masafae.

Utandawazi hakika,
Dunia kuunganika,
Kotekote kwafikika,
Hili ulizingatie.
Teknolojia hizi,
Faidaze kwa vizazi,
Ubunifu ugunduzi,
Himahima twendelee.

Palipo mwanya wa rushwa,
TEHAMA huteremshwa,
Kodi nyingi huzalishwa,
Mapato yasipotee.

Utenzi mwisho mefika,
Chini kalamu naweka,
Somo limekamilika,
Tijaye mzingatie.

Maswali.

41. Ukiusoma vizuri utenzi huo unagundua kuwa malenga alitaka kutoa ujumbe gani kwa hadhira? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..
42. Utenzi huu una jumla ya beti ngapi? . . . . . . . . . . . ...
43. Kila mshororo wa utenzi huu una jumla ya mizani mingapi? . . . ... . . . . . . .
44. Andika kina cha kiishio cha utenzi huu . . . . . . . .
45. Kipi ni kirefu cha neno lililoandikwa kwa herufi kubwa katika beti za utenzi huu? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... . . . . . . . . . .. . .

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 30  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 30  

OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKAKI ZA MITAA, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

 

MTIHANI WA KUJIANDAA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023

SOMO: KISWAHILI DARASA: VII MUDA: SAA 1:40 

MAELEKEZO:

  • Mtihani huu una maswali 45
  • Jibu maswali yote kama ulivyoelekezwa  

SEHEMU A

Sikiliza habari itakayosomwa na msimamizi kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi

1. Habari hii inahusu nini? _______

A. umoja B. Tanzania C. utamaduni D. wageni E. ulaya [       ]

2. Nchi gani inasifika kuwa na ukarimu?

A. Asia B. Ulaya C. Amerika D. Tanzania E. India [       ]

3. Ni vipengele vipi vya utamaduni vimetajwa katika habari hii? _______

A. amani na desturi B. upendo na mila C. amani na upendo D. upendo E. mila na desturi [       ]

4. Wageni wanaotoka Tanzania hutoka katika jamii za nchi gani? ______ 

A. Ulaya tu B. wenyeji wa Tanzania C. Umerika asia na Ulaya D. Uganda na Ulaya E. Asia tu [       ]

5. Kichwa cha habari hii cha faa kiwe ______

A. Mila B. Desturi C. Utamaduni D. Umoja E. Amani [       ]

 Katika swali la 6 – 35 chagua herufi ya jibu sahihi kisha iandike kwenye mabano uliyopewa.

6. Katika maneno yafuatayo ipi ni nomino ya dhahani? ________

A. unakuja B. umeenia C. utalima D. uelewe E. ulisoma

7. Neno lipi ni tofauti na mengine?_____ 

A. embe B. chungwa C. ndizi D. ng’ombe E. papai [       ]

8. “Nitatetema kama Mayele” Kiambishi cha njeo katika neno nitatetema ni kipi? _____

A. nita B. -ta C. te D. –a- E. tema [       ]

9. Walimu walifundisha masomo vizuri. Sentensi hii ipo katika wakati gani? ____ 

A. uliopita B. ujao C. uliopo D. mazoea E. usiodhihirika [       ]

10. Neno “paka” lina silabi ngapi? _____ 

A. mbili B. nne C. tano D. moja E. sita [       ]

11. Umoja wa neno nyaraka ni _________

A. waraka B. nyaraka C. miwaraka D. wawaraka E. kanyaraka [       ]

12. Hadi sasa hakuna mtu_________ aliyekamatwa kuhusika na wizi. 

A. yoyote B. wowote C. yeyote D. yote E. vyovyote [       ]

13. Mahali ambapo anaishi Rais wa nchi huitwa? _______

A. nyunbani B. makao ya Rais C. ikulu D. ngome E. banda [       ]

14. Neno “kitongoji” lina konsonati ngapi? _______ 

A. moja B. mbili C. tano D. tatu E. kumi [       ]

15. Wahenga walisema “hakuna marefu yasiyokuwa na ncha” nini maana ya methali hii? ______

A. hakuna kitu kisicho kirefu B. hakuna kitu kisicho na ncha C. hakuna jambo lenye mwanzo mrefu

D. hakuna jambo lisilokuwa na mwisho E. hakuna marefu yasiyokuwa na mafupi [       ]

16. “Angeliamka” mapema asingeliachwa na ndege. Kipi ni kiambishi cha masharti katika sentensi hii? _______

A. –a- B. –nge- C. –ngeli- D. angel E. –ili- [       ]

17. Mzee Juma ameishi Morogoro ____miaka kumi. 

A. toka B. kwa C. tangu D. kipindi E. tangia [       ]

18. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo lipo katika kundi la majina?_______ 

A. mlimani B. peponi C. mweusi D. utoto E. kwaya [       ]

19. Kama ungeliimba vizuri _____ zawadi.

A. ungelipewa B. ungepewa C. ungalipewa D. ungapewa E. ukipewa [       ]

20. Kitabu chako ni kizuri ukienda dukani nami ninunulie ________. Ni kifungu kipi cha maneno kinakamilisha sentensi hiyo? ___ 

A. kama hivyo B. kama hiko C. kama hicho D. kama iko E. kama icho [       ]

21. John husafisha eneo lake mpaka muda wa kuingia darasani unapowadia. Neno wadia lina maana gani? ___

A. kuwasili B. kuisha C. kufika D. kusogea E. rejea [       ]

22. Kila mtu atalipitia darasa hili apende asipende. Darasa hili ni lipi ? ________ 

A. kifo B. elimu ya msingi C. elimu ya awali D. dini E. semina [       ]

23. Mzee Mpili alizunguka mbuyu, nini maana ya nahau zunguka mbuyu? _______ 

A. kutoa rushwa B. kupiga rushwa C. kupokea rushwa D. kuleta rushwa E. kula rushwa [       ]

24. Mihogo iliyotoka Kidahwe haipikiki, imekaa sana. Neno lililopigiwa mstari liko katika kauli gani ya utendaji?__

A. Kutendeana B. Kutendewa C. Kutenda D. Kutendana E. Kutendeka [       ]

25. Asha anapia uvivu maana yake maneno yaliyopigiwa mstari ni ______ 

A. kutabili kazi B. kula uvivu C. kukaa raha  D. kuamka na uvivu E. kukaa huku ukifanya kazi [       ] 

26. __________________ mbele kiza. Methali hii inakamilishwa na maneno yapi kati ya haya yafuatayo?

A. Usiku B. Ujinga mwingi C. Werevu mwingi D. Ubishi mwingi E. Upendo [       ]

27. Malizia methali hii. “Mwenda tezi na omo ________” 

A. ni mnafiki B. marejeo ngamani C. hafai kwenye raha D. uakufa naye E. hufaidi siku ya iddi [       ]

28. “Gari lile liliendeshwa na mdogo wangu.” Hii ni kauli ya ______ 

A. kutendeka B. kutendewa C. kutenda D. kutendwa E. kutendana [       ]

29. Tegua kitendawili kisemacho Kondoo wetu ana nyama nje ngozi ndani. ________ 

A. Nywele na kichwa B. Katani C. Uyoga D. Chungwa E. Filigisi [       ]

30. Siwema ni msichana mzuri lakini ana mkono wa birika. Maana ya nahau iliyokolezwa ni ipi? _____

A. Mchoyo B. Mwizi C. Muongo D. Kusengenya E. Msahaulifu [       ]

31. Tegua kitendawili hiki “bomu la machozi baridi” _______

A. nywele B. moshi C. miguu D. ngozi E. gesi [       ]

32. Maana ya nahau “kufa moyo” ni ipi ? _______

A. kufariki B. kuugua sana C. kuchoka sana D. fia ndani ya moyo E. kukata tama [       ]

33. Samaki mkunje angali mbichi. Methali ipi kati ya hizi ina maana sawa na hii ? ______ 

A. samaki huanza kuoza kichwani B. ukitaka riba ziba C. jino la pembe si dawa ya pengo D. sikio la kufa halisikii dawa E. ngozi ivute ingali maji [       ]

34. Methali ipi haifanani na zingine kati ya hizi? ________

A. sikio la kufa halisikii dawa B. chombo cha kuzama hakina usukani C. siku ya kufa nyani miti yote huteleza D. maji yakimwagika hayazoleki [       ]

35. Maana ya “fuja mali” ni ________

A. kuiba mali B. kutumia mali ovyo C. kuhifadhi mali D. kutumia mali kibali E. kuitumia mali [       ]

 SEHEMU B: UTUNGAJI

 Panga sentensi zifuatazo katika mfuatano sahihi kwa kizipa herufi A, B, C, D na E.

36. Zima taa ulale, kuna radi sana. [       ]

37. Nilikuwa chumbani kwangu nikisoma kitabu cha hadithi. [       ]

38. Ilikuwa ni wakati wa usiku. [       ]

39. Mara nilimsikia baba akiniita, Bura! Bura! [       ]

40. Siku hiyo kulikuwa na mvuya kubwa iliyoambatana na radi. [       ]

SEHEMU C: USHAIRI - Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo Ukiwepo darasani, mwalimu msikilize,

Kisichotiwa mizani, angalia usimeze, 

Kilopita kipimoni, ndicho ukitekeleze, 

Elimu ni ufunguo, kila mtoto sikia.

Mazoezi darasani, yatakufanya uweze,

La kufanya akilini, kuchagua ipendeze, 

Uzio ubaini, jamii usipumbaze,

Elimu ni ufunguo, kila mtoto sikia.

MASAWALI

41. Shairi hili lina jumla ya beti ngapi? ......................................................................

42. Taja vina vya mwisho katika ubeti wa kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

43. Kila ubeti wa shairi hili una mishororo mingapi? ....................................................

44. Ubeti wa pili una mizani mingapi? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

45. Mstari unaojirudiarudia katika kila ubeti unaitwaje? . . . . . . .. ... . . . . . . . .




HABARI YA KUSOMA

Utamaduni ni mfumo wa maisha ya watu na jinsi wanavyoishi na taratibu zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Tanzania ni moja ta kati ya nchi zinazosifika duniani kwa ukarimu, amani na upendo kwa wageni, licha ya kuwa na makabila zaidi ya mia moja na ishirini ambayo yote hutunza mila na desturi zao, watanzania wanaishi kwa umoja, upendo na mshikamano. Hali hiihuwavutia watu wa mataifa mengine na wengine na wengine hupenda kuishi Tanzania.

Wageni hawa hutoka katika jamii za nchi tofauti zikiwemo zile za Asia, Ulaya na Amerika.

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 21  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 21  

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

 MTIHANI WA UTAMILIFU KATA 
 KISWAHILI DARASA LA SABA – MACHI, 2023

 MUDA: SAA 1:30

 MAELEKEZO 

  1. Mtihani huu una maswali arobaini na tano (45) tu.
  2. Jibu maswali yote
  3. Soma maelekezo kwa kila kurasa uliyopewa
  4. Kumbuka kuandika Jina lako, Namba yako ya mtihani na Jina la shule yako katika karatasi ya kujibia.
  5. Tumia penseli ya HB tu.
  6. Simu hazihitajiki katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A: UFAHAMU WA KUSIKILIZA

Sikiliza kwa makini habari utakayosomewa na msimamizi kisha jibu swali 1- 5 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu sahihi katika fomu yako ya kujibia. 

1. Kutokana na habari uliyoisikiliza, ni nani aliyezungumziwa?

(A) Amani (B) Bibi (C) Wananchi (D) Bibi na Amani (E) Kilole [     ]

2. Amani alimuuliza swali gani bibi yake? 

(A) kama unajua kusoma na kuandika (B) kama unajua kuandika (C) kama unajua kusoma (D) kama unajua kuimba na kuandika (E) kama unajua kuimba [     ]

3. Amani anaishi katika kijiji cha Kilole. Je, Amani anaishi na nani?

(A) Bibi (B) Babu (C) Shangazi (D) Mjomba (E) Babu na bibi [     ]

4. Kwa mujibu wa habari uliyoisikiliza. Amani ana tabia gani?

(A) mvivu (B) mdadisi (C) mkarimu (D) mchapakazi na mdadisi (E) mpole [     ]

5. Kichwa cha habari hii kinafaa kiwe kipi miongoni mwa hivi?

(A) kijiji cha Kilole (B) Amani (C) Amani na bibi yake (D) Kilole (E) Bibi [     ]

Katika Swali la 6 – 35 weka kivuli katika herufi ya jibu sahihi 

6. Neno machweo lina maana ipi kati ya hizi zifuatazo?

(A) wakati jua linapozama (B) wakati jua linapochomoza (C) wakati jua linapokuwa la utosi

(D) wakati jua linapokuwa kati (E) wakati jua linapokuwa pembeni [     ]

7. “Kazi mbaya si mchezo mwema” methali inayofanana na methali hii ni ipi kati ya hizi zifuatazo?

(A) hewala haigombi (B) mchezea tope humrukia (C) mcheka kivu asiyefikwa na jeraha (D) lila na fila havitengamani (E) mcheza kwao hutunzwa [     ]

8. Wanafunzi wale wanapenda kucheza mpira. Katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kivumishi? 

(A) wanafunzi (B) wale (C) wanapenda (D) mpira (E) kucheza [     ]

9. Katika lugha ya Kiswahili neno “staftahi” lina silabi ngapi?

(A) sita (B) tano (C) nne (D) tatu (E) saba [     ]

10. “Ukitaka kuruka agana na nyonga”. Sentensi hii iko katika aina gani ya sentensi kati ya hizi?

(A) sahihi (B) ambatano (C) changamano (D) tegemezi (E) shurutia [     ]

11. Ipi ni maana ya kitedawili “nyumba yangu imeungua mwamba wake umebaki”

(A) mfupa (B) njia (C) kaburi (D) kisima (E) mlima [     ]

12. Kuwa na nyota ya jaha maana yake ni___________ 

(A) jua la mchana (B) nyota ya asubuhi (C) bahati nzuri (D) bahati mbaya (E) bahati nasibu [     ]

13. Wewe ni mtoto mdogo sana. Sentensi hii iko katika nafsi gani?

(A) ya kwanza umoja (B) ya pili umoja (C) ya tatu wingi (D) ya pili wingi (E) ya kwanza umoja na wingi [     ]

14. Watu hufanya kazi mbalimbali ili kuweza kujipatia kipato. Mtu anayefanya kazi ya kutunza na kuazima vitabu maktaba anaitwa Mkutubi. Je! mtu anayefanya kazi ya kuzibua vyoo anaitwa nani? 

(A) kuli (B) topasi (C) toinyo (D) chepe (E) zubaifu [     ]

15. Bwana Afya aliuliza, kuna umuhimu gani wa kuchemsha maji ya kunywa? Je! sentensi hii iko katika kauli ipi kati ya zifuatazo? 

(A) taarifa (B) halisi (C) tata (D) tungo huru (E) kutenda [     ]

16. Asha ana gari. Neno “ana” ni aina gani ya neno?

(A) kitenzi (B) nomino (C) kiunganishi (D) kielezi (E) kihusishi [     ]

17. Baba amelima shamba kubwa sana. Silabi inayoonesha nafsi ni ipi?[     ]

(A) –li– (B) –a– (C) –me– (D) –i– (E) –lim–[     ]

18. Ngumi  zilipigika vilivyo, Neno lililopigiwa mstari lipo katika kauli gani?

(A) kutenda (B) kutendewa (C) kutendwa (D) kutendeka (E) kutendesha [     ]

19. __________ Kamilisha methali ifuatayo. Akikalia Kigoda

(A) huanguka (B) usimtukane (C) mtii (D) mfukuze (E) harudi [     ]

20. _______________ Ali anakula wali maharage.

(A) na (B) kwa (C) ni (D) ya (E) pamoja [     ]

21. Simba mkali amepita shuleni kwetu. Mchanganuo wa sentensi hii ni upi kati ya michanganuo ifuatayo? 

(A) T+N+V+W+E (B) N+E+V+T+W (C) V+E+T+W+N (D) N+V+T+E+V (E) N+V+E+T+V [     ]

22. ________ Kinyume cha methali isemayo; “Ngoja ngoja yaumiza matumbo” ni

(A) bendera hufuata upepo (B) mtu hujikuna hajipatiapo (C) mwisha hadhuru maiti (D) haraka haraka haina Baraka (E) asiyesikia la mkuu huvunjika guu [     ]

23. ______ Wakoloni walitunyanyasa lakini hatimaye unyanyasaji huo ulifika ukingoni kwani Ni methali ipi kati ya zifuatazo inamalizia sentensi hii?

(A) hakuna marefu yasiyokuwa na ncha (B) mchumia juani hulia kivulini (C) ukiona vyaelea ujue vimeundwa (D) umoja ni nguvu utengano ni udhaifu (E) bandubandu humalia gogo [     ]

24. Kazi ya Daudi ni kazi ya kijungujiko. Je! kazi ya kijungujiko ni kazi ya aina gani?

(A) kazi ya kuchimba vyoo (B) kazi ya kujitolea (C) kazi ya kufundisha wanafunzi (D) kazi isiyo rasmi au inayotosha mahitaji ya mlo tu (E) kazi ya kikoa [     ]

25. Ikiwa mzizi wa neno “PIK” tukiunda neno litakalokuwa katika wakati uliopita nafsi ya kwanza
umoja hali ya kutenda tunapata neno.

(A) alipika (B) nilipika (C) walipika (D) tulipika (E) nimepika [     ]

26. Akikosekana maana inakosekana. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?

(A) kitabu (B) kamusi (C) magazeti (D) shairi (E) vipeperushi [     ]

27. Mashairi ya kimapokeo yamegawanyika katika aina mbalimbali. Je ubeti wa shairi wenye mistari minne huitwaje?

(A) mshororo (B) tarbia (C) kituo (D) kibwagizo (E) mizani [     ]

28. _______ Mnyama ambaye amekuwa laini bado hajazaa anaitwa

(A) mtamba (B) mbuguma (C) maksai (D) fahali (E) beberu [     ]

29. Nenda ukawasikilize watakachokueleza uniletee mrejesho. Katika sentensi hii mtenda ni nafsi ya ngapi? 

(A) ya kwanza umoja (B) ya pili umoja (C) ya tatu wingi (D) ya kwanza wingi (E) ya pili wingi [     ]

30. _______________________ Ali ni askari kanzu. Ali ni 

(A) trafiki (B) kanga (C) bunduki (D) mpelelezi (E) askari mwenye cheo cha juu [     ]

31. Jambazi alihukumiwa kwa kuua mfanyabiashara. Sentensi hii iko katika hali gani?

(A) hali timilifu (B) hali ya kuendelea (C) hali isiyodhihirika (D) hali ya mazoea (E) hali tata [     ]

32. Tungo changamano ni tungo yenye vishazi vingapi?

(A) vitatu (B) viwili (C) vinne (D) vitano (E) kimoja [     ]

33. _______ Kisawe cha jogoo ni jimbi, kisawe cha beseni ni karai. Je kisawe cha kinyonga ni

(A) bombo (B) hua (C) lumbwi (D) kelbu (E) baghala [     ]

34. Katika neno anacheza. Kipi ni kiambishi njeo?

(A) –a– (B) –na– (C) –chez– (D) –a– (E) –cheza– [     ]

35. Lipi kati ya maneno yafuatayo si kivumishi likiambatanishwa na nomino?

(A) Yule (B) nzuri (C) polepole (D) huyo (E) hawa [     ]

 SEHEMU B:

 Panga sentensi zifuatazo kwa kuzipa herufi A – E ili zilete maana kamili kwa kujibu swali la 36 – 40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi

36. Niliogopa lakini nilipiga moyo konde  [    ]

37. Nilirudi nyuma kidogo nikaokota fimbo na kumpiga   [    ]

38. Jumamosi iliyopita mama alinituma sokoni   [    ]

39. Nilipokuwa njiani nilimwona nyoka   [    ] 

40. Aliniambia ninunue nyanya, vitunguu, sukari na mafuta   [    ]


 SEHEMU C: 

 Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo 

Masebo ni mwalimu anayefundisha katika shule ya Msingi Maendeleo iliyoko wilaya ya Masasi. Anakaa katika kitongoji cha usafi kilichopo umbali wa kilometa tano kutoka shuleni. Siku moja mwalimu Masebo alikuwa anakwenda shuleni. Pembezoni mwa msitu wa kijiji aliwaona vijana watatu, vijana hao walikuwa wakikata miti kwa kutumia mapanga na mashoka na kuivundika pembeni. Aliwatambua vijana hao kuwa ni Juma, Sadiki na Joseph. Mwalimu Masebo alisikitika sana. Alisimamisha pikipiki yake haraka na kwenda katika eneo lile. Alianza kuwafokea vijana wale kwa kukata miti mingi kiasi kile. Vijana wale walishangaa sana.

 Maswali 

41. Juma, Sadiki na Joseph walikuwa wanafanya nini msituni?

42. Mwalimu Masebo aliona nini pembezoni mwa msitu wa kijiji?

43. Je! ukikuta watu wanaoharibu mazingira utafanya nini?

44. Kwa nini mwalimu Masebo alisikitika sana?

45. Kwa nini tunashauriwa kutokata miti ovyo?



UFAHAMU WA KUSIKILIZA

Amani anaishi na bibi yake katika kijiji cha Kilole. Anamsaidia bibi yake shughuli za nyumbani. Anamsaidia kusafisha nyumba, kupika, kuosha vyombo na kufua. Juzi Amani alimuuliza bibi yake; bibi unajua kusoma? Bibi akajibu ninajua kusoma na kuandika. Amani akasema sawa bibi, kesho nitaleta kitabu changu ili tusome pamoja.



STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 3  

STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 3  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256