JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU
MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA IV TAREHE 23 NA 24 AGOST 2023
URAIA NA MAADILI
MUDA: SAA 1:30 AGOST 2023
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 26)
1. Chagua herufi ya jibu sahihi
(i) Katika sarafu zifuatazo ipi ina picha ya Hayati Abeid Amani Karume?
A. Shilingi 5000 B. Shilingi 100 C. Shiling 1000 D. Shilingi 200 [ ]
(ii) Kiongozi mkuu wa serikali ya kijiji ni
A. Mkurugenzi wa Wilaya B. Mwenyekiti wa Kijiji C. Diwani D. Mwenyekiti wa Kitongoji [ ]
(iii) Uoto wa asili kwenye bendera ya taifa huwakilishwa na rangi ya
A. Bluu B. Njano C. Nyeusi D. Kijani [ ]
(iv) Ni alama gani hupatikana katika ya bendera ya Rais?
A. Fedha ya taifa B. Bendera ya taifa C. Ngao ya taifa D. Sikukuu za taifa [ ]
(vv) Waziri mkuu wa Tanzania anaitwa nani?
A. Tulia Ackson. B. Ummy Mwalimu C. Dr. Philipo Mpango D. Majaliwa Kassim [ ]
2. Oanisha maneno kutoka Kifungu A na Kifungu B ili kuleta maana sahihi
KIFUNGU A | JIBU | KIFUNGU B |
i. Demokrasia | A. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar B. Uhuru wa Tanganyika C. Ni eneo la mjini D. Ni haki ya watu kuchagua viongozi wao E. Muungano wa Tanzania na Zanzibar F. Kuzaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere | |
ii. 1922 | ||
iii. 1964 | ||
iv. Serikali za mitaa |
3. Jibu maswali yafuatayo kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye mabano
(i) Katibu wa vikao vya kamati ya shule huitwa (Mwalimu mkuu, Mtendaji wa kijiji, Diwani, Mzazi)
(ii) Kitendo cha uvunjifu wa sheria za nchi huitwa. (uhalifu, uovu, katiba, haki)
(iii) Mazao yanayopatikana katika nembo ya taifa ni ( karafuu na pamba, mtama na mahindi, ndizi)
(iv) Mambo ambayo mtu anastahili kuyapata yanaitwa (wajibu, sheria, malazi, haki)
SEHEMU B (Alama 24)
4. Jedwali hili linaonesha makabila mbalimbali na mikoa yanakopatikana Tanzania. Jaza nafasi zilizoachwa wazi.
KABILA | MKOA |
i. | Tabora |
ii. | Dodoma |
Makonde | iii. |
iv. | Singida |
5. Soma picha ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo namba (i) – (iv)
MASWALI
(i) Jina la sehemu inayooneshwa kwenye picha inaitwa
(ii) Ni nembo ipi ya taifa inaonekana mbele ya wanafunzi?
(iii)Kiongozi mkuu wa jamii inayooneshwa kwenye picha ni
(iv) Kutokana na uelewa wako, ni muda gani bendera ya taifa hupandishwa?
6. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo
Ukatili wa watoto ni tabia ambayo hufanywa na watu wazima makusudi kuwaumiza watoto kwa njia ya ukatili na kuwafanyia vurugu. Ukatili wa watoto unahuusisha kuwapuuza watoto, ngono au unyanyasaji wakijinsia. Ukatili wa watoto pia hujulikana kama Ukiukwaji wa haki za watoto. Ni ukiukwaji kufanya kitendo ambacho kipo kinyume na haki za watoto. Ukiukwaji wa haki ni ukosefu wa haki na usawa. Ukiukwaji wa haki za watoto ni kutokuwatendea haki watoto. Ni uvunjifu wa haki za watoto.
Ukiukwaji wa haki za watoto ni kitendo cha kuwanyima haki zao watoto. Jamii inapaswa kufanya kila njia kulinda haki za watoto.
MASWALI
(i) Ukatili wa watoto ni tabia ambayo
(ii) Ukatili wa watoto kama ilivyoelezwa katika habari unahusisha ngono, ukatili wa kijinsia na
(iii) Mwandishi amesema ukiukwaji wa haki ni kitendo kisichokubalika dhidi ya
(iv) Jina jingine la Ukiukwaji wa haki za watoto kutokana na habari uliyosoma ni
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 36
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 36
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
UPIMAJI WA UTAMILIFU DARASA LA NNE
MKOA WA NJOMBE
06 URAIA NA MAADILI
Muda: Saa 1:30 Mwaka :2023
MAELEKEZO
KWA MATUMIZI YA UPIMAJI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MPIMAJI |
1 | ||
2 | ||
3 | ||
4 | ||
5 | ||
JUMLA | ||
SAINI YA MHAKIKI |
SEHEMU : A Chagua herufi ya jibu sahihi
1. i. Kuwahi shuleni ni moja ya ____________________
ii. Baadhi ya matendo ya kujijali ni pamoja na_________________
iii. Watoto waliokosa adabu wanaweza kuwa _________________
iv. Ni rangi gani katika bendera ya Taifa inawakilisha mali asili Tanzania?
v. Kufanya kazi kwa pamoja humaanisha ___________________
2. Oanisha kifungu A na B:ili kupata maana sahihi.
Na | Kifungu A | Kifungu B | Jawabu |
i. | Kundi la watu wanaoishi katika eneo moja | A: Mazingira | |
ii. | Matendo ya uaminifu | B: Kufichua Uovu | |
iii. | Moja ya haki ya watoto | C: Kupata elimu bora | |
iv. | Ni jumla ya vitu vyote vinavyotuzunguka | D: Ukoo | |
v. | Kuhakikisha wanakijiji wanapata huduma za Kijamii kama vile maji, umeme na barabara | E: Kazi mojawapo ya serikali ya kijiji |
SEHEMU : B
3. Andika neno HAKI au WAJIBU mbele ya kila sentensi.
i. Kujifunza kutokana na makosa__________________________________
ii. Kupata elimu bora____________________________________________
iii. Kuthamini watu wenye ulemavu_________________________________
iv. Mtoto kucheza_______________________________________________
v. Kusoma kwa bidii_____________________________________________
4. Jaza nafasi zilizo wazi
i. Makazi ya Rais huitwa ________________________________________
ii. Alama inayotambulisha shule au Taifa huitwa ______________________
iii. Mtu mwenye mapenzi na nchi yake huitwa________________________
iv. Bendera ya Taifa hupandishwa saa ngapi?_________________________
v. Katibu wa kamati ya shule anaitwa ______________________________
5. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata.
Maria na Tina ni wanafunzi wa darasa la IV katika shule ya msingi Chambalo. Marafiki hawa walifanya vibaya katika masomo yao.Walisoma kwa bidii lakini hawakufaulu mitihani yao.
Maria hakukata tamaa aliamini kuwa atafikia malengo aliyojiwekea ya kufaulu mitihani yake. Aliwashawishi wenzake kwenda kuunda kikundi cha kujisomea. Siku ya Jumamosi waliamka mapema kufanya shughuli za nyumbani na kila ilipotimu saa 5 asubuhi walikutana nyumbani na kujisomea. Baada ya Miezi sita tu. Maria alikuwa wa kwanza katika masomo, Maria aliongoza darasani.
Maswali
i. Maria hakukata tamaa kwa kuwa aliamini _______________________________________
ii. Maria na rafiki yake waliweza kufanya vizuri baada ya kuamua kufanya nini? __________________________________________
iii. Siku ya Jumamosi Maria na rafiki zake waliamka ___________________ ili wafanye majukumu yao ya nyumbani.
iv. Baada ya miezi sita maria alikuwa wa_____________________________ katika masomo yake.
v. Maria aliwashawishi wenzake kuunda kikundi cha _________________________________________
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 26
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 26
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI
MTIHANI WA UPIMAJI WA DARASA LA NNE
URAIA NA MAADILI
SEHEMU A
1.Chagua herufi ya jibu sahihi na kisha andika katika kisanduku
(i)Ni alama ipi kati ya zifuatazo inapatikana katikati ya bendera ya raisi wa Tanzania?
(A)Bendera ya taifa (B)Wimbo wa taifa (C)Nembo ya taifa(D)Katiba ya taifa ( )
( ii)Ni sarafu ipi kati ya zifuatazo ina picha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?
(A)Shilingi 100(B) Shilingi 50(C)Shilingi 200(D)Shilingi 500 ( )
(iii)Mojawapo ya vitu ambavyo vinaanza vinaonyesha upendo miongoni mwa wanajamii ni;
(A)Kusema uongo (B)Kupigana (C)Kuiba vitu vya wengine (D)Kuheshimiana ( )
(iv)Ni tarehe gani tunasherehekea muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar?
(A)9 disemba (B)12 Januari (C) 14 Oktoba (D) 26 Aprili ( )
(v)Wimbo wa Taifa unapoimbwa tunatakiwa
(A) Tulale (B) Tupige magoti (C)Tusimame wima (D) Tutembee ( )
SEHEMU B
Oanisha fungu A na Fungu B ili kupata maana kamili kutoka fingu A
| FUNGU A | JIBU | | FUNGU B |
i | Rangi nyeusi katika bendera ya tanzania | | A | Ardhi maji na mifugo |
ii | Lugha,mavazi na chakula | | B | Uaswa wa kijinsia |
iii | Kutunga sheria | | C | Utamadauni |
iv | Mwanamke na mwanaume katika nembo ya Taifa | | D | Watu wa Tanzania |
v | Maliasili | | E | Bunge |
SEHEMU C
3.Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku
Nne,Tano, Mazingira, J.K Nyerere, Kipaji, Utamaduni |
i.Rais wa kwanza wa Tanzania …………………………………….
ii…………………….ni jumla ya vitu vyote vinavyomzunguka mwanadamu
iii.Uwezo wa kutenda jambo kwa ustadi ……………………………………………………………..
iv.Uchaguzi mkuu wa Tanzania hufanyika kila baada ya miaka …………………………
v.Bendera ya Taifa ina jumla ya rangi …………………………………………………………………
4.Kamilisha kifungu cha hapo chini kwa kutumia maneno sahihi na uyaandike kwenye nafasi zilizoahwa wazi.Kipengere namba moja (i) imetolewa kama mfano
Tanganyika ilipata uhuru wake (i) 9 disemba 1961.Tarehe (ii)……………………………..ikawa jamhuri .Raisi wa kwanza wa Tanganyika alikuwa anaitwa (iii)………………………………….Alihudumu kama raisi wa Tanganyika kuanzia mwaka 1962 mpaka mwaka 1964 na amekuwa raisi wa jamhuri ya muungao wa Tanzania kuanzia mwaka 1964 mpaka (iv)……………………………Raisi wa awamu ya pili wa Tanzania alikuwa anaitwa(v)…………………………………………………….
5.Soma kifungu cha habari kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo
Mtu mtiifu mwaminifu na mkweli katika jamii yake kila wakati hufanya vitu kwa usahihi hata kama hakuna mtu anayemwongoza kuwa mtiifu.Inamaana unakuwa mkweli na mwaminifu hata kwako wewe mwenyewe. Kama mtu mtu akitaka kufanikiwa katika maisha yake anatakiwa awe mwaminifu na mkweli.
MASWALI
i………………ni mtu anayefanya vitu kwa usahihi wakati wote
ii.Kichwa cha habari chafaa kiwe ……………………………………………………….
iii.Umejfunza nini kutokana na habari hii…………………………………………..?
iv.Ili uweze kufanikiwa katika jamii unatakaiwa kuwa ………………………
v.Kuwa mtiifu inamaana unakuwa ……………………………………………………..
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 12
STANDARD FOUR URAIA EXAM SERIES 12