MAARIFA STANDARD FOUR REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA IV TAREHE 23 NA 24 AGOST 2023

MAARIFA YA JAMII

MUDA: SAA 1:30 AGOST 2023

MAELEKEZO

 1. Mtihani huu una maswali manne yenye vipengele vya namba za kirumi
 2. Jibu maswali yote
 3. Andika majina yako kwa usahihi kwenye kila ukurasa

SEHEMU A

1. Kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye maswali yafuatayo

(i) Ukataji miti ovyo ni mojawapo ya . . . . . . . . . . . . wa mazingira.

A. ukarabati B. upendekezaji C. uharibifu D. urutubishaji [     ]

(ii) Haya ni mazingira ya asili  . . . . . . . . .

A. mashamba, barabara, nyumba, milima B. nyumba, wanyama, mimea, maji

C. misitu, milima, chemchemu, bahari D. gari, shule, kabati, kalamu [     ]

(iii) Kitu kinachozunguka kiumbe katika maisha yake ya kila siku ni  . . . . . . . . .

A. mazingira B. mimea C. majengo D. chakula  [     ]

(iv) Moja ya faida tunayoipata kwa kucheza ngoma za utamaduni ni . . . . . . . . .

A. kuendeleza utandawazi B. kuwaburudisha wazungu

C. kukuza mila na desturi D. kudumisha lugha za kigeni [     ]

(v) Madhara yanayoweza kuletwa na mvua nyingi ni

A. kumea mazao B. mafuriko C. ushirikiano D. unyevu anga [     ]

(vi) Kipi kitatokea kwa familia ambayo itashindwa kutunza kumbukumbu za matukio yaliyopita?? 

A. kukumbuka matukio yaliyopita B. kusahau matukio yanayokuja

C. kusahau matukio yaliyopita D. kupata maendeleo [     ]

(vii) Njia zinazotumika kupata taarifa za matukio ni [     ]

A. kiberiti B. simulizi  C. umeme D. mpira [     ]

(viii) Kinjekitile Ngwale aliongoza mapambano ya kupinga uvamizi wa Wajerumani katika mikoa ipi?

A. Mwanza na Shinyanga B. Tabora na Pwani

C. Mtwara na Lindi D. Pwani na Tanga [     ]

2. Oanisha maneno kutoka Fungu A na Fungu B ili kuakamilisha sentensi


FUNGU A

JIBU

FUNGU B

i.

Mfumo wa kwanza kiuchumi ambao watu waliishi na kushirikiana


A. Kifaa kinachotumika kupima uelekeo wa upepo

B. Kinjekitele Ngwale

C. Alimasi

D. Kifaa kitumikacho kupima mwendokasi wa upepo

E. Janga

F. Obiti

G. Ukabaila

H. Kalamu na daftari

I. Ujima

ii.

Anemomita


iii.

Kifaa kinachotumika kurekodi wakati wa kutembelea sehemu maalumu


iv.

Ni mojawapo wa mashujaa waliopinga uvamizi


v.

Njia ya sayari kulizunguka jua huitwa


vi.

Tukio la hatari linalosababisha maafa au balaa huitwa


SEHEMU B:

3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yafuatayo kwa kuandika jibu sahihi

Hali ya joto au baridi ya sehemu au kitu huitwa jotoridi. Kifaa kinachotumika kupima jotoridi huitwa kipima joto. Chanzo cha joto ni jua. Kunapokuwa na joto kali tunasema jotoridi liko juu lakini kunapokuwa na baridi tunasema jotoridi liko chini.

Kunapokuwa na baridi tunashauriwa kuvaa nguo nzito kama sweta na jaketi. Wakati wa joto kali tunavaa nguo nyepesi au nguo za pamba. Hali ya joto husababisha mito na mabwawa kukauka.

MASWALI

i) Hali ya joto au baridi ya mahali huitwaje? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

ii) Mavazi gani huvaliwa wakati wa baridi? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

iii) Ni katika hali gani jotoridi huwa juu? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

iv) Kifaa kinachotumika kupima jotoridi huitwaje?. . . . . . . . .  . . . . . . . . .

v) Chanzo cha joto ni nini?. . . . . . . . .  . . . . . . . . .

vi) Mito na mabwawa hukauka wakati gani. . . . . . . . .  . . . . . . . . .

vii) Nguo nyepesi na za pamba huvaliwa wakati gani?. . . . . . . . .  . . . . . . . . .

4. Chunguza kwa makini picha hii kisha jibu maswali yafuatayo.

image

Maswali

i) Taja kitu kilichopo upande wa kusini . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

ii) Mti upo upande gani wa penseli? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

iii) Kitu gani kipo upande wa kaskazini? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

iv) Kitu gani kilichopo upande ambao jua huchomoza? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .

v) Ukikaa upande uliopo katikati ya nyumba na penseli utakuwa umekaa upande gani? . . . . . . . . .  . . . . . . . . .


STANDARD FOUR MAARIFA EXAM SERIES 31  

STANDARD FOUR MAARIFA EXAM SERIES 31  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

MTIHANI WA UPIMAJI WA DARSA LA NNE

SOMO LA MAARIFA YA JAMII

1. Chagua herufi ya jibu sahihi kasha jaza katika kisanduku.

(i) Ni kiongozi yupi katika Tanzania hupigiwa kura kila baada ya miaka mitano? 

(A) jaji mkuu B) Rais C) Spika Wa Bunge D) Waziri Mkuu [     ]

(ii) Jotoridi hupimwa kwa kifaa kinachoitwa____________________

(A) hygrometa B) kipim ahewa C) kipima joto D) moto.  [     ]

(iii) Bwana na bi Juma walioana mwaka 2014 na walichelewa kupata mototo hadi sasa ,hii famialia inaitwaje? 

(A) ya awali B) ya watoto yatima C) ya mke mjane D) yamakubaliano.  [     ]

(iv) Kipi si chanzo sahihi cha mwanga? 

A) nyota B) jua C) Moto D ) Mwezi  [     ]

(v) Tukio gani lilitokea tarehe 12 Januari 1964? 

A) Uhuru B) Muungano C) Mapinduzi D) Jamhuri.  [     ]

2. Oanisha maneno katika orodha A kutok aorodha B ili kupata maana.

Na

ORODHA A

JIBU

ORODHA B

i.

Tanagnyika ilipata uhuru mwaka


 1. 1962

ii.

Uchaguzi mkuu hufanyika kila baadaya miaka _____


 1. Dr. John PombeMagufuli

iii.

Rais wa awamu ya tano alikuwa anaitwa ____________


 1. 1999

iv.

Mwalimu J.K Nyerere alifariki mwaka _________


 1. 1961

v.

Tanganyika ilikuwa Jamhuri


 1. 5/ Tano
 1. Jazanafasizilizowazi
 1. Ni madhara gani yatatokea kama uhharibifu wamazingira ukiendelea ______________
 2. Joto la binadam hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa _______________________
 3. Waziri mkuu wa Tanzania anaitwa _____________________________
 4. Hatua ya mwanzo ya uchumi katika maisha ya binadamni______________________
 5. Jumana Asha walikuwa wakiishi katika kijiji cha pili baba yake alifariki wa kabaki naama yao, je hiyo ni hiyo ni familia ya aina gani?____________________________
 1. Andika KWELI kwa sentensi sahihi na SI KWELI kwa sentensi isiyo ya kweli.
 1. Ramani ni mchoro wa kitu kama kinavyoonekana kutoka juu_____________
 2. Vitabu, madawati, na chaki ni vitu vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani _______________________
 3. Sindimba ni ngoma ya kiutamaduni inaychezwa na wazaramo______________
 4. Jua ni muhimu katika maisha ya kila siku kwa sababu hutupatia mwanga wakati wa mchana ______________________________
 5. Fursa inayo patikana ukanda wa pwani ni kilimo_________________________
 1. Soma habari kisha jibu maswali yanayofuata.

Wahehe walipigana na wajerumani kuanzia mwaka 1891 hadi mwaka 1898 wakiongozwa na chifu Mkwawa. Mapigano ya kwanza yalitokea mwaka 1891 katika eneo la liitwalo Lugalo. Katika mapigano hayo, wajerumani walishindwa vibaya sana. Pambano la pili lilifanyika mwaka 1894, katika pambano hili Jeshi la Wajerumani lilishambulia ngome ya Mkwawa katika eneo la kalenga hivyo Mkwawa na Jeshi lake walishindwa ,na hatimaye Mkwawa kukimbilia porini na huko aliendeleza vita ya msituni. Mkwawa alipoona amezidiwa na kuwa alikaribia kutekwa na Wajerumani aliamua kujiua kwa kujipiga Risasi mwaka 1898.

MASWALI.

 1. Mkwawa alifariki mwaka gani___________________?
 2. Mkwawa aliposhindwa aliamua kukimbilia wapi_______________________.?
 3. Jeshi la Mkwawa lilipigana na ___________________________________.
 4. Mapambano ya mwanzo ya Wajerumani na Jeshi la Mkwawa yalianza mwaka __________
 5. Pambano la pili kati ya Jeshi la Mkwawa naWaejumani lilifanyika katika eneo la Kalenga mwaka _______________________________________


STANDARD FOUR MAARIFA EXAM SERIES 9  

STANDARD FOUR MAARIFA EXAM SERIES 9  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256