JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
KIDATO CHA KWANZA
MUDA: SAA 2:30 2025
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Katika vipengele (i) – (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika visanduku ulivyopewa.
(i) Bibi Halima alishuhudia baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha madongo wakitupa taka katika vyanzo vya maji. Katika kutimiza wajibu wake aliwaeleza kuwa wanaharibu urithi wa taifa. Urithi uliokusudiwa na bibi Halima unaingia katika kipengele kipi kati ya vifuatavyo?
(ii) Ulinzi wa Historia ya Tanzania ni jukumu la kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa hili la Tanzania. Ipi ni njia bora na sahihi ya kulinda historia ya Tanzania?
(iii) Nyimbo na ngoma za jadi huimbwa na kupigwa kwa makusudi makubwa kabisa. Ni kipi kati ya yafuatayo huimarishwa pale ngoma na nyimbo zinapohusishwa?
(iv) Michoro inayochorwa maeneo mbalimbali ya kuhistoria ina makusudi makubwa katika nchi yetu ya Tanzania. Nini nia kubwa ya kuchora picha maeneo ya kihistoria?
(v) Nyimbo za jadi huimbwa na makabila mbalimbali hapa nchini Tanzania. Je! Ni wakati gani unaofaa kuimba nyimbo hizi za jadi?
(vi) Katika hotuba yake juuya ustawi wa maadili na maliasili za taifa, waziri mkuu alizungumzia majukumu yanayohusiana na uhifadhi na ulinzi wa urithi wa taifa na maadili. Unadhani ni nani hasa anahusika na ulinzi huo wa maendeleo ya taifa letu?
(vii) Mabadiliko gani yamekuwa yakizingatiwa katika historia ya Tanzania?
(viii) Makundi katika jamii za Kitanzania hujishughulisha na shughuli mbalimbali ambazo huwapatia kipato. Ipi si shughuli ya wanilo kati ya hizi zifuatazo?
(ix) “Kupokea au kutoa mali isiyo halali au kutumia mali ya umma isivyo halali kwa manufaa binafsi.” Maelezo haya yanahitimishwa na neno lipi kati ya haya yafuatayo?
(x) Watanzania wote bila kujali kabila, imani, rangi na dini hatunabudi kuzingatia miongozo, kanuni na sheria zinazoongoza mienendo ya mtu mmoja mmoja katika nchi yetu. Lipi ni jina moja linalojumuisha miongozo hiyo?
MAJIBU
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
2. Oanisha sentensi kutoka kundi A na zile za kundi B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa hapo chini.
| KUNDI A | KUNDI B | ||||
| (i) Njia ya kuhifadhi historia ya jamii (ii) Mfano wa maadili ya kitanzania (iii) Michezo ya jadi (iv) Namna ya kuhifadhi urithi wa taifa (v) Umuhimu wa kulinda na kutunza historia ya taifa |
| ||||
| KUNDI A | i | ii | iii | iv | v |
| KUNDI B | |||||
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Taja shughuli tano (5) za kijamii na kiuchumi zinazofanywa na jamii ya wakichembe katika maisha yao ya kila siku.
4. (a) Eleza maana ya urithi wa Taifa
________________________________________________________________________________________________________________________________________________
(b) Taja njia nne (4) zinazotumika kuhifadhi urithi wa taifa:-
i) ______________________________________________________________________
ii) ______________________________________________________________________
iii) _____________________________________________________________________
iv) _____________________________________________________________________
5. (a) Taja michezo miwili ya jadi inayotumika kuendeleza maadili
(b) Eleza namna michezo hiyo inavyosaidia watoto kujifunza maadili.
i) ______________________________________________________________________
ii) ______________________________________________________________________
iii)______________________________________________________________________
6. Bainisha mifano mitano ya maadili mbalimbali katika jamii za Kitanzania ambayo ingefaa kuigwa na kudumishwa kwa vizazi vijavyo.
7. (a) Bainisha makabila mawili (2) ambayo yanatokana na jamii za wakichembe.
(b) Taja zana tatu (3) zilizotumika katika uwindaji katika jamii ya Wakichembe.
i) __________________________________________________________________
ii) __________________________________________________________________
iii) __________________________________________________________________
8. Jamii za watu wa visiwa vya Zanzibar walinunua na kuuza bidhaa kupitia biashara walizofanya na waajemi, waarabu na watu wa mashariki ya mbali. Taja bidhaa tano (5) zilizohusika katika biashara hiyo.
9. Kwa nini jamii za asili ya Kitanzania zilihama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine? Toa hoja tano (5).
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali hili kwa insha
10. Eleza hoja sita (6) ukionesha matarajio yako ya kujifunza somo la Historia ya Tanzania na Maadili.
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 203
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 203