Sura Ya 01 : NGELI ZA NOMINO

Utangulizi

Nomino huweza kugawanywa na kupangwa kwa kuzingatia kigezo cha upatanisho wa kisarufi au kisintaksia, kimofolojia na kisemantiki. Katika sura hii, utajifunza maana ya ngeli, ngeli za nomino, kugawanya ngeli za nomino kwa kutumia kigezo cha upatanisho wa kisarufi au kisintaksia na matumizi ya viambishi vya o-rejeshi katika vitenzi. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kugawanya nomino katika makundi yake na kuwasiliana kwa kutumia Kiswahili sanifu.

Kazi ya 1.1

Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata.

Ninajitanua kwa lugha, zilo tamu za Kibantu,

Kwenye kila uwanja nipo, sayansi na insia,

Mwenzangu nimesikia, watu wakiulizana,

Kuhusu jina la ngeli, mabishano hayakomi,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Wauliza ngeli? Hilo nimetoa kwa wenzangu,

Wenzangu wepi? Nimetoa kwa Wahaya,

Ndege wafananao, huruka pamoja,

Nomino, kama ndege, huruka pamoja pia,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Ngeli za nomino zifananazo, muungano hudumu,

Viumbe hai na visivyo hai, nominoze haziungani,

Ngeli sikai kiholela, mpango nazingatia,

Kisintaksia napangwa, kulingana na viambishi,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Ukitaka kunielewa, kiambishi usikosee,

Ukikosea dhahiri, maana taiharibu,

Utaleta utata, kwa watumiaji wa lugha,

Ukitaka tuendane, vitu na watu sichanganye,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Kisintaksia uhusiano, wa vipashio zingatia,

Maneno yanapendana, upatanisho ni mshenga,

Ukinipanga bila mpango, maana taiharibu,

Anisikilizaye na kunisoma, atapata tabu sana,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Kiswahili najidai, sifa zangu mzomzo,

Wauliza urejeshi, bila ngeli hujinadi,

Uhusiano murua, wa vipashio zingatia,

Ukisahau urafi ki wa ngeli, urejeshi kupotoa,

Hunikuti kwa wageni, ni kwa Wabantu wenzangu tu.

Maswali

1. Unafahamu nini kuhusu asili ya neno ngeli? Fafanua.

2. Katika shairi ulilolisoma, mshairi anaeleza kuhusu nini?

3. Toa maana ya ngeli za nomino kwa mujibu wa mshairi.

4. Ili kubainisha ngeli za nomino ni mambo gani ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa?

5. Katika kituo cha shairi, mwandishi anakusudia kusema nini?

Upatanisho wa kisarufi

Kazi ya 1.2

Chunguza picha zifuatazo, kisha jibu maswali yanayofuata.

Maswali

1. Kwa kila picha, na kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi , tunga sentensi mbili kuonesha umoja na wingi.

2. Bainisha ngeli za nomino kwa kila sentensi uliyotunga.

Kazi ya 1.3

Chunguza orodha ya maneno hapa chini, kisha jibu maswali yanayofuata.

kiti sahani ubani jiko ukuta kuku meno ufa ng’ombe sufuria mtoto Mungu

kikombe karai uzi kalamu dirisha nyumba pembe gari ndege debe tunda uchaguzi

Maswali

1. Andika maneno hayo katika umoja na wingi.

2. Orodhesha viambishi vya umoja na wingi vya maneno hayo.

3. Bainisha maneno yanayofanana, kisha yapange katika ngeli.

Kazi ya 1.4

Chunguza mifano ya sentensi zifuatazo, kisha jibu maswali yanayofuata.

(a) Mtoto anacheza.

(b) Mbuzi yumo zizini.

(c) Mti umeanguka chini.

(d) Changu kizuri kimenunuliwa.

(e) Yule mwembamba ameinama.

(f) Msichana mrembo amewasili.

(g) Mtoto mzuri anacheza.

(h) Mti mfupi umekatwa.

Maswali

1. Bainisha viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa nomino na vitenzi katika sentensi ulizopewa.

2. Je, sentensi ulizopewa zina viambishi vya upatanisho wa kisarufi wa aina moja? Fafanua.

3. Badili sentensi hizo kuwa katika wingi.

4. Bainisha viambishi vinavyoonesha upatanisho wa kisarufi , kwa kuweka pamoja sentensi zenye viambishi vya upatanisho wa kisarufi unaofanana.

5. Kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi , unda sentensi 20 zenye nomino tofautitofauti, kisha panga nomino hizo katika ngeli.

Zingatia

Makundi ya majina ya wanyama, watu, vitu, na mahali kwa kuzingatia sifa zake, huitwa ngeli za nomino. Kisarufi , ngeli za nomino hufafanuliwa kwa kutumia kigezo cha kisintaksia ambacho huangalia upatanisho wa kisarufi baina ya majina na vitenzi.

Upatanisho wa kisarufi hutambulisha ngeli za nomino kwa kuangalia viambishi awali vya umoja na wingi katika nomino au viwakilishi, vivumishi na vitenzi katika sentensi. Kwa mfano:

(a) Mvuvi yupo hapa - Wavuvi wapo hapa.

(b) Mtoto analilia wembe - Watoto wanalilia nyembe.

Viambishi vya upatanisho wa kisarufi ni [yu-] na [a-] katika umoja, na [wa-] katika

wingi. Hivyo, ngeli ya nomino katika mfano huo ni [yu-a-/wa-].

Mfano mwingine wa sentensi za umoja na wingi ni kama ifuatavyo:

(a) Kisu hiki kina makali - Visu hivi vina makali.

(b) Kinanda hiki kinalia vizuri zaidi - Vinanda hivi vinalia vizuri zaidi.

Viambishi vya upatanisho wa kisarufi ni [ki-] katika umoja, na [vi-] katika wingi. Katika mfano huo, ngeli ya nomino ni [ki-/vi-].

Hivyo, uainishaji wa ngeli za nomino kwa kigezo cha upatanisho wa kisarufi huzingatia viambishi awali vya nomino au viwakilishi, vivumishi na vitenzi.

Kazi ya 1.5

1. Kwa kutumia majina kumi ya watu na vitu unavyovifahamu, tunga sentensi kumi zenye umoja na wingi.

2. Kwa kuzingatia mfanano wa viambishi awali vya vitenzi, panga sentensi ulizozitunga katika swali la kwanza kwenye ngeli inayohusika.

Kazi ya 1.6

Chunguza sentensi zifuatazo, kisha jibu maswali yanayofuata.

1. Mvuvi wapo hapa.

2. Uchaguzi zimeahirishwa.

3. Kisu hiki vina makali.

4. Ukuta zimejengwa kwa matofali

5. Ubao huu imechorwa.

6. Kiti itafaa zaidi kukalia.

7. Kinanda hiki vinalia vizuri zaidi.

8. Mikeka hii zimenunuliwa.

9. Mipapai yake yanakatwa.

10. Mihogo zilipikwa.

11. Miti mikubwa una matunda.

12. Madaftari mazuri imechanika leo.

13. Mbwa wakali imepotea

Maswali

1. Bainisha makosa ya upatanisho wa kisarufi kwa kila sentensi uliyopewa.

2. Rekebisha makosa hayo, kisha andika upya sentensi hizo kwa usahihi

Kazi ya 1.7

Zungumza na watu mbalimbali au sikiliza mazungumzo yao, kisha orodhesha sentensi ulizozisikia katika mazungumzo hayo. Bainisha makosa ya upatanisho wa kisarufi yaliyojitokeza. Andika sentensi hizo kwa usahihi, kisha wasilisha kazi hiyo darasani.

Zoezi la 1.1

1. Kwa kuzingatia umoja na wingi, tunga sentensi kumi kwa kila ngeli zifuatazo:

(a) YU-A-WA

(b) KI-VI

(c) U-ZI

(d) I-ZI

(e) LI-YA

2. Kwa kutumia mifano ya nomino 20, zigawe katika aina nyingine za ngeli

tofauti na ulizopewa katika swali la kwanza.

Zingatia

Kwa kutumia kigezo cha kisintaksia au upatanisho wa kisarufi , nomino za Kiswahili

hugawanywa katika ngeli kumi na mbili. Jedwali lifuatalo linaonesha mgawanyo wa ngeli hizo.

Jedwali la 1.1: Mgawanyo wa ngeli za nomino kwa kigezo cha kisintaksia au upatanisho wa kisarufi.

Na.

Ainaya ngeli

Viambishi

Mifano

Umoja

Wingi

1.

YU/A-WA

YU-umoja A-

WA-wingi

Mgeni yumo ndani Mgeni amekuja Ng’ombeamechinjwa

asubuhi

Wageni wamo ndani Wageni wamekuja Ng’ombewamechinjwa

asubuhi

2.

U-I

U-umoja I -wingi

Mkutanoumeanza mchana

Mgomba umekatika

Mikutanoimeanza mchana

Migomba imekatika

3.

LI-YA

LI - umoja

YA- wingi

Jembe limepotea

Papai limeiva

Majembeyamepotea

Mapapai yameiva

4.

KI-VI

KI-umoja

VI - wingi

Kijiko kinang’aa

Kitabu hikikinasomwa

Vijikovinang’aa

Vitabuhivivinasomwa

5.

I-ZI

I - umoja

ZI - wingi

Kazihiiinatosha

Surualiitashonwakesho

Kazi hizizinatosha

Surualizitashonwakesho

6.

U-ZI

U- umoja

ZI - wingi

Uzi umekatika

Ukuta umebomoka

Nyuzi zimekatika

Kuta zimebomoka

7.

U-YA

U- umoja

YA-wingi

Uovuumezidi nchini

Ugonjwa umeenea

Maovu yamezidi nchini

Magonjwayameenea

8.

I-I

I-

Chai imemwagika

Sukari imepanda bei

Chai imemwagika

Sukari imepanda bei

9.

U-U

U-

Uongo umekithiri

Unga umevunda

Uongo umekithiri

Unga umevunda

10.

YA-YA

YA-

Maziwayameuzwa

Maji yamejaa sana

Maziwayameuzwa

Maji yamejaa sana

11.

KU-

KU-

Kusomakunamanufaa

Kucheza kunafurahisha

12.

PA-MU- KU

PA-

MU-

KU-

Hapa petu pamejaa Humundanimnagiza Kule kunaonekana

vizuri

Kazi ya 1.8

1. Orodhesha majina ya vitu vitano vinavyopatikana katika mazingira yako, kisha weka kila jina katika ngeli inayohusika. Hakikisha viambishi vya upatanisho wa kisarufi kama vinakubaliana na ngeli hiyo.

2. Chunguza nomino za ngeli ya nne, ziorodheshe, kisha ziwasilishe darasani.

Kazi ya 1.9

Soma habari ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.

Tanzania ni nchi yenye majira mbalimbali ya mwaka yakiwamo masika, kiangazi, vuli na kipupwe. Masika ni kipindi ambacho mvua nyingi hunyesha sehemu kubwa ya nchi. Kipindi hiki huwa ni lele kwa wanyama na wakulima. Wakulima hupiga vigelegele vya nderemo na vifi jo. Wakulima huwa na ari ya hali ya juu kwani hutifua ardhi kwa jembe la mkono, plau na matrekta ili kupanda mbegu na hutegemea kupata mazao. Wahenga hawakukosea waliposema, “Jembe halimtupi mkulima.” Wakulima huona fahari kutekeleza kauli mbiu isemayo: “Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu.” Licha ya vigelegele na furaha inayotokana na mvua, pia zipo hasara kwani baadhi ya wakulima mambo huenda mrama. Hii ni kutokana na madhara yanayotokana na mvua ambayo ni mafuriko yanayosababisha balaa na maafa.

Mafuriko huleta adha kubwa kwa jamii, kwani nyumba hubomoka, mashamba hujaa maji, mazao na miundombinu huharibika na hufanya watu wengine kuhama makazi yao. Pia, husababisha njaa, magonjwa ya mlipuko na vifo. Kila chenye faida hakikosi kuwa na hasara, ndio maana wahenga walisema “Hakuna masika yasiyo na mbu.” Kipindi hiki, huwapo mazalia ya mbu ambayo ni tatizo kubwa kwa binadamu kwani vifo vingi hutokea kutokana na malaria.

Mwezi uliopita wakati wa usiku, Juma akiwa amelala usingizi alishitushwa na kelele za watu. Baada ya kuamka, aliona maji mengi yamejaa ndani ya chumba alichokuwa amelala. Watu wengi walikuwa wamelala fofofo. Ghafl a kelele na mayowe vilisikika, maji! Maji! Maji! Nakufaaa! Uwiii! Msaaaada! Watu walitapatapa wakikimbia huku na huko. Mafuriko yaliathiri watu, wanyama, na kuharibu makazi, mashamba, na miundombinu, mfano: barabara na madaraja. Pia, yalikata mawasiliano baina ya pande mbili za kijiji. Shughuli za uchumi zilizoroteshwa. Wakazi wa eneo hilo hawakuamini macho yao jinsi mto ulivyojaa na kufurika hadi kufi kia makazi yao, hata kwa wale wanaoishi mbali kidogo na mto. Usiku huo kulikuwa na patashika nguo kuchanika. Kila mmoja alipambana kunusuru maisha yake. Kesho yake, serikali na watu binafsi, walifanya jitihada za kuokoa waathirika wa mafuriko. Vijana na wapigambizi walikuwa bega kwa bega kusaidia kuokoa watu na mali zao. Waathirika wengine walibebwa mgongoni, mabegani na wengine kwenye chombo maalumu. Mimea iliyokuwa ikinesanesa usiku na mchana kwa shukurani, ilionekana kupoteza matumaini kwani yote ilikuwa imemezwa na maji. Mazao mengi mashambani yaliharibika na kufanya hali ya uchumi kudorora. Hivyo, wananchi walikuwa na wakati mgumu sana kimaisha. Methali isemayo, “Jembe halimtupi mkulima,” haikufua dafu. Wananchi waliomba msaada kutoka serikalini na kwa watu binafsi

Haya yote yalisababishwa na baadhi ya wananchi kuvunja sheria ya mazingira kwa kujenga makazi karibu na vyanzo vya maji hasa mito. Kile walichokipuuza sasa kimetokea. Walikumbuka maneno yenye hekima yaliyowahi kusemwa na wahenga, “Mdharau mwiba mguu huota tende” na “Sikio la kufa halisikii dawa.” Pamoja na juhudi zilizofanyika kuokoa maisha ya wananchi serikali ilifanya kazi bega kwa bega na wananchi kukarabati miundombinu iliyoharibiwa kwa mafuriko.

Maswali

1. Neno “wakulima” lipo katika ngeli ipi?

2. Ainisha ngeli zilizomo kwenye vifungu vya maneno “mambo huenda mrama,” “yowe limepigwa.”

3. “Mimea iliyokuwa ikinesanesa.” Kifungu hiki cha maneno kipo katika aina ipi ya ngeli?

4. Kwa kutumia habari uliyoisoma, andika kifungu cha maneno chenye ngeli ya I-ZI.

5. Kwa kutumia vifungu viwili vya maneno katika aya ya pili, onesha ngeli ya kwanza.

6. Onesha ngeli za nomino zilizojitokeza katika aya ya mwisho.

7. Kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi , andika ngeli sita za nomino zinazotokana na habari uliyoisoma.

Kazi ya 1.10

1. Kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi , andika habari yenye maneno yasiyozidi 250 na yasiyopungua 200 katika mojawapo ya mada zifuatazo:

(a) Usalama barabarani

(b) Haki za mtoto

(c) Utunzaji wa mazingira ya shule

2. Kwa kuzingatia kigezo cha kisintaksia, andika majina ya vitu mbalimbali vinavyopatikana shuleni, darasani, nyumbani au mtaani kwenu, kisha panga majina hayo katika ngeli inayohusika

Kazi ya 1.11

1. Orodhesha majina ya vitu vitano ambavyo vinapatikana darasani, shuleni au nyumbani, kisha panga majina ya vitu hivyo katika ngeli inayohusika.

2. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata.

Baba yake Zawadi ni mkulima mkubwa katika Kijiji cha Tuungane. Yeye hulima aina mbalimbali za matunda katika shamba lake, yakiwamo mapapai, mapera, machungwa na maembe. Pia, ana bustani kubwa ya mbogamboga ambayo inaweza kulisha kijiji kizima. Wanakijiji huenda kwake kununua mchicha, kabichi, bamia, nyanya na biringanya. Pamoja na kilimo, pia hujishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, mbuzi, na kuku. Aidha, Baba Zawadi ana punda watatu anaowatumia kubebea mizigo kwenda sokoni. Wakati wa kurudi nyumbani, punda hao humsaidia kubeba mahitaji mbalimbali ya nyumbani. Hakika, Baba Zawadi ananufaika sana na shughuli za kilimo na ufugaji

Maswali

1. Orodhesha majina ya mbogamboga, wanyama na matunda yaliyojitokeza katika kifungu cha habari ulichokisoma kwenye ngeli inayohusika.

2. Andika ngeli za majina hayo. Umewezaje kupata ngeli hizo ? Fafanua.

3. Kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi , andika habari yenye maneno yasiyozidi 250 na yasiyopungua 100, kisha ainisha

O-rejeshi katika ngeli

Kazi ya 1.12

somo kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata.

Masopano alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtengeshari. Yeye ni miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa taifa mwaka jana. Walimu waliomfundisha mwanafunzi huyo, walijigamba kwa kuwa shule yao ilitoa mwanafunzi bora. Kila shule iliyofanya vizuri kitaifa ilipata zawadi ya kikombe na shilingi milioni tano zilizoahidiwa. Waziri aliyetoahotuba siku hiyo, alizitaka shule zingine kuiga mfano wa walimu hao. Waziri aliahidi kuwa mwanafunzi atakayefanya vizuri mtihani wa taifa mwaka ujao atasomeshwa hadi chuo kikuu. Walimu na wazazi waliokuwapo kwenye hafl a hiyo, walimshangilia Masopano. Pia, wazazi waliipongeza shule yake kwa juhudi ilizozifanya mpaka kutoa mwanafunzi bora. Waziri alipomaliza hotuba yake, alipanda gari lake lililokuwa linaongozwa na msafara wa polisi.

Maswali

1. Bainisha sentensi zenye o-rejeshi katika kifungu cha habari ulichokisoma.

2. Tunga sentensi kumi zenye vitenzi vyenye o-rejeshi.

3. Fasili istilahi ya o-rejeshi.

Zoezi la 1.2

1. Fafanua dhana ya o-rejeshi katika upatanisho wa kisarufi .

2. Tunga sentensi tatu, kila moja iwe na kiambishi rejeshi {-mo-}.

3. Tunga sentensi katika umoja na wingi zenye viambishi vya o-rejeshi kwa kutumia maneno yafuatayo: embe, nyumba, kitanda, mtu, kitabu, jembe na kabati.

4. Orodhesha maneno sita yaliyobeba viambishi rejeshi vya ngeli ya KI-VI.

Zingatia

O-rejeshi hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi. O-rejeshi hufuata mfumo wa upatanisho wa kisarufi katika ngeli. Angalia mifano ya o-rejeshi katika sentensi zifuatazo:

(a) Wagonjwa waliopimwa walitibiwa.

(b) Jambo lililokusudiwa silo lililotendeka.

(c) Mwanafunzi atakayechelewa ataadhibiwa.

(d) Kitambaa kilichopelekwa kitarudishwa.

(e) Tuliingia mahali tulimopangiwa.

(f) Mitungi iliyotolewa shuleni inavuja.

Katika urejeshi, vitenzi hubeba viambishi ngeli vyenye kiambishi -o-, isipokuwa kama nomino iliyotajwa, ni ya ngeli ya kwanza umoja. Urejeshi wa ngeli hiyo hutumia {-ye-} badala ya {-o-}.

Jedwali la 1.2: Matumizi ya o - rejeshi katika ngeli za upatanisho wa kisarufi

Ainaya ngeli

Viambishi vya ngeli

Viambishi vya -o-rejeshi

Mifano

1.

YU/A-WA

YU-

A-

WA-

-YE-

-YE-

-O-

Mbuzi anayetafutwa yumo zizini

Mbuzi wanaotafutwa wamo zizini

Mzazi aliyekuja ametoa zawadi

Wazaziwaliokujawametoazawadi

2.

U- I

U-

1-

-O-

-YO-

Mti ulionipa umestawi

Mitiuliyonipa imestawi

3.

LI-YA

LI-

YA-

-LO-

-YO-

Koti lililofuliwa limekauka

Makotiyaliyofuliwayamekauka

4.

Kl-VI

KI-

VI-

-CHO-

-VYO-

Kiaziulichopandakimeota

Viaziulivyopandavimeota

5.

I-ZI

I-

ZI-

-YO-

-ZO-

Kalamu iliyonunuliwa imepotea

Kalamuzilizonunuliwazimepotea

6.

U-ZI

U-

ZI-

- O-

-ZO

Uzi ulioshonea umekwisha

Nyuziulizoshoneazimekwisha

7.

U-YA

U-

YA-

-O-

-YO-

Ugonjwa ulioingia hauna dawa

Magonjwayaliyoingiahayanadawa

8.

I-I

I-

-YO-

Chai iliyopikwa imeuzwa Sukariiliyonunuliwaimetumika

9.

U-U

U-

-O-

Uongoanaozungumzautamgharimu Unga ulioanikwa umenyeshewa

10.

YA-YA

YA-

-YO-

Maziwayaliyouzwayameganda Maji yaliyoletwa yanavuja

11.

KU-

KU-

-KO-

Kucheza kulikonifurahisha ni kwa Kiba Kuchorakulikopendekezwakutazingatiwa

12.

PA-MU-KU

PA-

MU-

KU-

-PO-

-MO-

-KO-

Hapo ulipokaa pamelowa

Humo ulimoingia mmejaa

Huko unakokwenda hakuna kitu

Zoezi la marudio la 1.

1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo:

(i) Mende anapenda kula uchafu. Neno lililopigiwa mstari lipo katika ngeli ipi?

(a) KI-VI

(b) U-I

(c) A-WA

(d) KU

(e) LI-YA

(ii) _________ mna watu wengi.

(a) Aliingia

(b) Alipoingia

(c) Alikoingia

(d) Alivyoingia

(e) Alimoingia

(iii) Neno “papai” linaingia katika ngeli ya _________

(a) PA-MU-KU

(b) U-ZI

(c) U-YA

(d) KI-VI

(e) LI-YA

(iv) “Shangazi yupo shambani kwake.” Kifungu hiki cha maneno kipo katika ngeli gani?

(a) I-ZI

(b) YU-A-WA

(c) PA-MU-KU

(d) KI-VI

(e) U-I

2. Jaza nafasi zilizoachwa wazi.

(i) Ng’ombe amekula mahindi shambani. Neno “ng’ombe” lipo katika ngeli ya _________

(ii) Kigezo cha uainishaji wa ngeli za nomino kwa kuangalia ushikamani wa maneno katika sentensi huitwa _________

(iii) ________ ni neno lenye asili ya lugha ya Kibantu inayozungumzwa na jamiii ya Wahaya.

(iv) Maumbo “-ye-, -cho-, -o-, -mo-” yanajulikana kama maumbo ya _________

(v) Upepo ulivuma kwa kasi. Neno “upepo” lipo katika ngeli ya _________

3. Eleza maana ya upatanisho wa kisarufi .

4. Tunga sentensi kumi zenye o-rejeshi ukitumia ngeli mbalimbali, kisha onesha kiambishi cha urejeshi kwa kila sentensi.

5. Kwa kutumia viambishi ngeli vya o-rejeshi, tunga sentensi kumi, kisha onesha matumizi ya viambishi ngeli vya [yu-a-/wa-] katika sentensi hizo.

6. Ngeli za nomino zinakusaidiaje katika maisha ya kila siku?

7. Tunga sentensi kumi, kisha zipange katika ngeli za kisintaksia zinazohusika.

8. Kwa kuzingatia kigezo cha kisintaksia, tunga dayalojia isiyozidi ukurasa mmoja, kisha pigia mstari kila ngeli iliyojitokeza.

9. Fafanua dhana ya ngeli za nomino.

10. Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kinachounda ngeli za nomino. Kwa kutumia ngeli zifuatazo, tunga sentensi mbili kuthibitisha usemi huu:

(a) U-I

(b) LI-YA

(c) I-ZI

(d) A-WA

(e) U-ZI

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256