NGELI ZA NOMINO
Baada Ya Kusoma Mada Hii Utaweza :
UPATANISHI WA KISARUFI KATIKA SENTENSI
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Mfano:
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
NGELI | UFAFANUZI | MIFANO |
A-WA | Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.k | Sungura mjanja ameumia, Sungura wajanja wameumia Mkuu anawasili |
LI-YA | Majina yenye kiambaisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hii | Jambia la babu limepotea, Majambia ya babu yamepatikana |
KI-VI | Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima | Chakula kimekwisha, Vyakula vimekwisha, Kijito kimekauka Vijito vimekauka |
U-I | Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kewa mfano mkono, mguu, mkia n.k | Mlima umeporomoka, Milima imeporomoka, Mkono umevunjika, Mikono imevunjika, Mto huu una mamba wengi, Mito hii ina mamba wengi |
U-ZI | Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/ k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa | Ukuta umebomoka, Kuta zimebomoka, Wimbo huu unavutia, Nyimbo hizi zinavutia, Ufa umeonekana, Nyufa zimeonekana |
I-ZI | Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). | Nyumba imejengwa, Nyumba zimejengwa, Salam imefika Salam zimefika |
U-YA | Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi. | Ukuu umekuponza, Makuu yamekuponza, Unyoya unapepea, Manyoya yanapepea |
KU | Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina) | Kusoma kwako kumekusaidia, Kuchelewa kumemponza |
PA/MU/KU- | Huonesha mahali | Amekaa pale palipo na wadudu wengi Amelala mule mulimojaa siafu. Amepita kule mbali |
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
HABARI ZENYE UPATANISHI WA KISARUFI
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo: