FORM FOUR KISWAHILI MIDTERM-2 EXAMS

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA

KIDATO CHA NNE

KISWAHILI 2024-AUG/SEPT

Muda 2:30

MAELEKEZO 

  1.               Jibu maswali yote
  2.               Mtihani huu una sehemu A. B na C (Jumla ya maswali 9)
  3.               Simu za mkononi haziruhusiwi

 

SEHEMUA(Alama16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

 

  1.          Chaguaherufiyajibusahihikatikakipengele(i)hadi(x),Kishaandikaherufiyajibukwenyekijitabuchakochakujibia
  1.                  Kuchezakwakekunafurahisha.Nenolililopigiwamstarilimetumikakamaainaganiyaneno?
    1.                Nomino 
    2.                Kihusishi 
    3.                 Kielezi 
    4.                Kivumishi  
    5.                 Kitenzi

 

  1.                Dhima kuu ya lugha katika mawasiliano ni ipi kati ya hizi zifuatazo?
  1.              Kutambulisha utamaduni
  2.               Kutunza historia
  3.              Kupashana habari
  4.             Kuelimisha jamii
  5.               Kuburudisha jamii

 

  1.             Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja?
  1.              Kaka amefua nguo
  2.               Nipe sahani ya kulia
  3.              Suedi amenunua mbuzi
  4.             Eva amenunua kanga
  5.               Joni amempigia mpira
  1.       Mwalimu Chikoya alimuuliza Suzi kuhusu sehemu za sentensi kutokana na mkabala wa kimuundo lakini alishindwa. Ukiwa   mwanafunzi wa kidato cha nne msaidie Suzi kubainisha sehemu hizo.
    1.          Kirainominonakiraikitenzi
    2.          Kiimanakiarifu
    3.          Kirainominonakiraikivumishi
    4.         Kiraikitenzinakishazitegemezi
    5.           Kiraikivumishi nakishazi tegemezi

 

  1.            Utofauti wa kimatamshi, kimaumbo na matumizi ya maneno ya lugha kuumojakatikamaeneombalimbalihuitwa?
    1.                 Misimu
    2.                  Lafudhi
    3.                 Rejesta
    4.                 Lahaja
    5.                  Simo

 

  1.                   Mimi ni Kiboko, Kila sifa ninastahili mimi. Madaktari chanzo ni mimi, wanasheria chanzo ni mimi. Katika tanzu za fasihi , kipera hiki hupatikana katika utanzu upi?
  1.              Sanaazamaonesho
  2.               Semi
  3.              Hadithi
  4.             Sanaa
  5.               Ushairi

 

  1.     Kuna wakati watumiaji wa lugha hufanya makosa pasipo kukusudia .Sentensi, " Waziri amewakilisha bajeti yake ya mwaka 2022/2023". Ina kosa gani la kisarufi?
    1.         Kosalakimsamiati
    2.          Kosalakimatamshi
    3.         Kosalakimuundo
    4.        Kosalakimaana
    5.          Kosalakilugha

 

 

 

  1.            Uchambuziwakaziyoyoteyafasihihujikitakatikavigezoviwili;faninamaudhui.KwaupandewafaniKunavipengelevifuatavyoisipokuwa:
    1.          Mtindo
    2.          Mandhari
    3.          Muundo
    4.          Migogoro
    5.          Matumiziyakugha

 

  1.             Neno masalamunda limeundwa na silabi ngapi?
    1.              Tano  
    2.               Sita  
    3.               Saba 
    4.             Kumi na moja  
    5.               Nne

 

  1.                Mussa ni mwanafunzi wa Kidato cha nne, alialikwa kwenye sherehe ya matambiko na alipata nafasi ya kuongea ili kuwaelimisha jamii kuhusiana na athari za matambiko na alitoa athari moja ambayo ni:
    1.                   Hukuza na kudumaza ubunifu
    2.                   Sherehe husababisha ugomvi, chuki na uhasama
    3.                   Hujenga dhana potofu katika jamii 
    4.                  Husaidia kukuza uongo na uwoga
    5.                    Huongeza hasira kwa mizimu.

 

  1.      Oanisha mifano ya tamathali za semi katika Orodha A na dhana husika zinazoshabihiana nazo katika Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia. 

ORODHA A

ORODHA B

i. Waridi ni ua lenye kutabasamu linapochanua 

ii. Bibi aliongea na ndugu zake wa Ahera fikirani, “Kaziyangu nimemaliza.Niko tayari sasa siku yoyote kujiunga nanyi.” 

iii. Akina mwalimu Nyerere wa Afrika wanastahili kupongezwa

iv. Mito ya machozi ilionekana katika uso wake usio na hatia.

v. “Jembe bado nainama,sijatulia kulima. 

vi.Mbinu ya kuuliza swali ambalo jibu lake unalo

A. Mubalagha 

B. Ritifaa 

C. Sitiari 

D. Tabaini 

E. Taniaba

F. Tashibiha 

G. Tashihisi 

H. Taashira 

I.Mdokezo

J.Tashititi

K.Tafsida

 

SEHEMU B (Alama 54)

 

Jibu maswali yote katika sehemu hii

 

3. Maneno ya Kiswahili huundwa kwa kutumia njia mbalimbali.Taja njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo na kwa kila neno,tunga sentensi moja tu.

  1.                  Shule.
  2.               Kandambili

(iii)Washamba.

 

 

  1.         (a)Sehemu ya sentensi inayokaliwa na mtenda au mtendwa wa jambo huundwa kwa vipashio mbalimbali. Thibitisha dai hilo kwa hoja nne (4) na mifano.

(b) Wanafunzi wa kidato cha nne ni hodari sana katika uchanganuzi wa sentensi kwa kuzingatia hatua zote za uchanganuzi kwa njia ya ngoe. Thibitisha uhodari wako katika sentensi ifuatayo kwa kutumia mkabala wa kidhima.

"Mgeni aliyekuja jana ameondoka leo".

 

  1.                     Kuna baadhi ya maneno katika lugha ya kiswahili yasipotumika ipasavyo huweza kuleta utata katika mawasiliano.Toa maana mbili kwa kila neno
  1. Mto
  2. Ota
  3. Shuka
  4. Pepo
  5. Mbuni
  6. Kaa

 

  1.                     Lugha ya Kiswahili inatamalaki na kuvuka mipaka ya dunia. Kwa kutumia hoja madhubuti zenye mifano eleza sababu Tano(5) ambazo zimepelekea kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
  2.                     Kwa kutoa hoja nne zenye mifano madhubuti kutoka katika Tamthiliya ya Kilio chetu fafanua mambo yanayopelekea kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa.

 

8    Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

 

     Rehema aliamka usingizini na kuendelea na safari yake.Awali alishitushwa na mitikisiko iliyotokea karibu na Mbuyu.Hakujua yuko wapi lakini hakuchelewa kujua nia ya safari yake.Aliukamata mkuki wake vizuri na ngao yake pia.Alipiga goti moja na kusimama hali akiuangalia mbuyu.Punde aliwaona nyani wawili wakikimbilia nyasini.Wakasisimama na kumtazama Rehema.Naye alipoona hakuna hatari ya wanyama aliendelea na safari yake.Muda huo wa mchana ulikuwa salama kwani wanyama wakubwa walikuwa Mapangoni mwao ila zilisikika sauti za Panzi,Nyenje na Ndege tu waliojibizana kwa zamu.

     Rehema alipumzika kidogo kwa mara nyingine ili kumnyonyesha mtoto.Hata hivyo vivuli virefu vilimkumbusha kuwa usiku ulikaribia.Lakini hakusikia wala kuona dalili yoyote ile iliyoonesha kuwa binadamu waliishi katika eneo hili.Bado hakuelewa ni wapi alipokuwa.Ni kosa gani alilofanya? Je, mwanae hakuwa binadamu? Ni kweli tofauti yake ni rangi tu? Hakuwa na vidole vya mikono na miguu vilivyomzidi baba yake.Macho yake na masikio yake pia yalikuwa sawa ,alihesabu yote.Mtoto alikuwa karibu sawa na wengine kuliko tofauti yake ya rangi tu.Sasa mbona wanataka kumuua?

      Rehema alianza kukimbia kwa haraka kwani kama hangefika kijiji jirani basi kutoroka kwake kungekuwa kazi bure.Punde si punde alishtushwa na mlio wa vipande vya miti vilivyovunjika.Rehema alisimama akabana pumzi zake akisubiri sauti ile isikike tena.Huyo hakuwa mnyama mkali bali mtu aliyekusanya kuni.Upesi Rehema aliharakisha upande ilikotoka sauti.Ghafla akamwona mzee mmoja akikusanya kuni.Alisogea kiasi ambacho kungetokea hatari angekimbia.Alimsalimia mzee Yule “Tafadhali kuwa mwema ili umsaidie mwanao aliyepotea” alisubiri atakavyojibiwa kwa sauti ile Yule mzee alizunguka na kuinua shoka lake kama ishara ya kutisha.Punde alipogundua kuwa aliyeongea alikuwa ni mwanamke alipata ahueni na kulishika shoka lake chini.Wakati ule Rehema alisita na kuamua kusimama.Tumaini alizinduka usingizini huenda alihisi shaka iliyomkumba mama yake,akaanza kulia.

     Punde si punde Yule mzee alijiandaa kwa Mashambulizi.Aliwaza kuna mtu nyuma ya Yule mama.Iweje mwanamke mwenye mtoto mchanga aranderande msituni bila kuwa na mlinzi? Huenda anatumiwa na kijana imara aliyetaka kumuua.Wakati  huo angefanyaje? Alikusanya kuni chache alizozipasua,akageuka ili aondoke.”Tafadhali usinitupe niliwe na wanyama wa usiku.Nisaidie! La huwezi kunisaidia binti yako basi msaidie mwanangu.Hajaonja maisha bado,na si vyema kufa sasa.Kilio mfululizo cha Yule mtoto na maneno ya Rehema vilimgusa Yule mzee.Ingawa alisita lakini hatimaye aligeuka nyuma.Kutokana na kauli yake alihisi Rehema alikuwa mgeni katika eneo hilo.Akaamua hata iweje angemsaidia.Kwa hadhari kubwa aliwasogelea mama na mtoto wake. “Njooni wanangu,tutakwenda kibandani kwangu”

 

MASWALI

  1.                       Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
  2.                    Unafikiri kwa nini Rehema alitoroka nyumbani kwake na kukimbilia msituni?
  3.             Mwandishi wa habari hii anaichukuliaje jamii ya akina Rehema?
  4.             Kutokana na habari uliyosoma,eleza nafasi ya mwanamke katika jamii kwa 

kutoa  hoja mbili.

 

SEHEMU C (ALAMA 30%)

Jibu maswali mawili tu kutoka katika sehemu hii. swali la 9 ni la lazima 

 

  1.                     "Pamoja na mwanamke kutumika kama kivutio katika kazi nyingi za Sanaa pia ameonekana kubeba uhalisia wake" Kwa kutumia diwani mbili thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu.

 

  1.   Ni wazi kuwa waandishi hutumia mitindo mbalimbali katika uandishi wa kazi zao ili   kuonesha upekee wa kazi zao.Thibitisha dhahiri kauli hiyo kwa kuonesha Mitindo mitatu toka katika riwaya mbili ulizosoma.

 

  1.         Fasihi simulizi ni hai na halisi zaidi kuliko fasihi andishi.Jadili

 

ORODHA YA VITABU

 

USHAIRI:

-Wasakatonge   -MS.Khatibu (DUP)

-Malenga Wapya  - TAKILUKI (DUP)

-Mashairi ya Chekacheka – T.A.Mvungi (EP & LTD)

 

RIWAYA:

-Takadini – Ben J.Hanson (MBC)

-Watoto wa Mama Ntilie – E.Mbogo (HP)

-Joka la Mdimu – A.J.Safari (HP)

 

TAMTHILIYA:

-Orodha – Steve Reynold (MA)

-Ngoswe Penzi Kitovu cha uzembe – E.Semzaba (ESC)

-Kilio Chetu – Medical Aid Foundation (TPH)

 

 

 

 

 

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 197  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 197  

OFISI  YA   RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI

KISWAHILI KIDATO CHA NNE

    021                                                         KISWAHILI 

MUDA:  SAA:3                                                                              AUG, 2023

                                                         Maelekezo.

  1.               Mtihani huu una sehemu tatu A, B na C.
  2.               Jibu maswali yote katika sehemu A, B na maswali mawili (2) kutoka katika sehemu C .Swali namba tisa (9) ni lazima.
  3.               Zingatia maagizo ya kila swali.
  4.               Andika namba yako ya Mtihani kwenye kila karatasi ya kujibia.

 

                                           SEHEMU A. ( Alama 16 )

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

 

  1.               Chagua herufi ya jibu sahihi, kisha andika jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

 

  1. Nomino inapokwenda likizo ni aina gani ya neno huchukua pahala pake ?


  1.              Kivumishi          
  2.               kiwakilishi       
  3.              kielezi
  4.             Nomino za kawaida   
  5.               kitenzi 


 

  1. Ubeti wa shairi wenye mistari mitatu huitwa


  1.              Sabilia    
  2.               Takhimisa   
  3.              Tathilitha 
  4.             Tathnia 
  5.               Tamolitha


 

  1. Dhana mojawapo kati ya hizi huwa na dhima ya kuokoa muda


  1.              Fasihi 
  2.               Ufahamu  
  3.              Hadithi  
  4.             Masimulizi  
  5.               Lugha fasaha


 

  1. Kategoria ya kisarufi inayowakilisha wakati katika kitenzi ni?


  1.              Njeo  
  2.               Shina   
  3.              Kiambishi awali  
  4.             Leksimu 
  5.               Mtendwa


 

  1. Zifuatazo ni tanzu za fasihi simulizi isipokuwa


  1.              Ushairi  
  2.               Maigizo  
  3.              Semi  
  4.             Hadithi  
  5.               Shairi


  1. Upi ni mzizi wa neno “watakapopambanisha


  1.              Pambana 
  2.               Pambanish 
  3.              Pambani
  4.             Pamban 
  5.               Pamb


 

  1. Sitaki, sitaki, nasema sitaki kabisa kusikia. Katika lugha ya kisanii sentensi hii ina


  1.              Tashihisi   
  2.               Sitiari  
  3.              Takriri  
  4.             Tafsida  
  5.               Tashibiha


 

  1. Kipi kati ya vipengele vifuatavyo hakibainishi muundo katika shairi la kimapokeo


  1.              Mizani   
  2.               Vina  
  3.              Beti  
  4.             Kituo  
  5.               Kina


 

  1. Ni kauli ipi iliyotumika katika kuunda neno “ Hawakupotea
  1.              Kauli ya kutendea  
  2.               Kauli ya kutenda  
  3.              Kauli ya kutendeana 
  4.             Kauli ya kutendewa  
  5.               Kauli ya kutendana

 

  1. “Waandishi wa fasihi huzungumzia watu wenye mienendo isiyokubalika katika jamii ili kukemea mienendo hiyo.”Katika tamthiliya ulizosoma , ni wahusika wepi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika ?
  1.              Ngoswe, Baba Anna na Suzi
  2.               Joti, Ngoswe na Mama Furaha
  3.              Mazoea, Mama Furaha na Joti
  4.             Ngoswe, Joti na Padre James.
  5.               Padre James, Ngoswe na Baba Anna

 

 

 

 

  1.               Chagua kifungu cha maneno kutoka orodha B kinachotoa maelezo sahihi ya maneno kutoka orodha A. Andika herufi ya jibu sahihi katika jedwali hapo chini.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Sehemu ya neno ambayo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
  2. Viambajengo vya sentensi.
  3. Semantiki
  4. Pangaboi
  5. Mkazo
  6. Fonolojia
  1.               Miamabatano ya maneno
  2.               Silabi
  3.              Mkato
  4.             Konsonati
  5.               Kiima na Kiarifu
  6.               Sarufi  maana katika sentensi
  7.              Shadda
  8.             Sarufi matamshi
  9.                  Irabu
  10.                 Kiimbo 

 

 

 

SEHEMU B ( Alama 54 )

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

  1.               Eleza  maana ya kielezi na mazingira manne ambayo kielezi huweza kujipambanua. Kisha tunga sentensi moja kwa kila aina ya mazingira .
  2.               Onesha mzizi wa maneno yafuatayo
  1. Mapigano
  2. Walitumikishwa
  3. Onesha
  4. Amekula
  5. Alimnong”oneza
  6. Walipokunywa

 

  1.               Lugha ya Kiswahili hutumia njia mbalimbali katika kujipatia msamiati wake. Onesha ni njia ipi iliyotumika kuunda maneno yafuatayo.
  1. Divai
  2. Hataza
  3. UDA
  4. Bahasha
  5. Imla
  6. Cherehani

 

  1.               Chama cha Kiswahili cha Afrika ( CHAKA) ni miongoni mwa taasisi zilizojitahidi katika kukuza na kueneza Kiswahili Barani Afrika . Eleza majukumu sita  ya chama hiki katika kufanikisha azma hiyo.

 

  1.               Kwa kutumia Riwaya ya Takadini na Watoto Wa Mama Ntiliye, onesha namna mwanamke alivyochorwa kama mtu mwenye huruma na fadhila. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia wahusika wawili kutoka katika kila kitabu kwa kutoa hoja tatu kwa kila Riwaya.

 

  1.               Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata

TOHARA

Tohara, kwa mwanamke, ni hatari,

Madhara, kwa wake uke, hushamiri,

Hasara, ya peke yake, hudhiri,

                  Zinduka

Epuka, hao ngariba, wajuaji,

Hufika, navyo viroba, wachinjaji,

Kumbuka, hawana tiba, wauwaji,

                  Zinduka.

Kiwembe, kilichofuka, na kibutu,

Viumbe, huathirika, ni kwa kutu, 

Siombe, ya kakufika, mwanakwetu.

                 Zinduka.

Mzazi, kujifunguwa, idhihali,

Huwezi, kujitanuwa, ni muhali,

Ni wazi, husumbuliwa na misuli,

                  Amka.

    Maswali

  1.               Umepata ujumbe gani katika utanzu huu wa shairi .    
  2.               Unafikiri mwandishi anasisitiza nini katika shairi hili.    
  3.                Taja dhamira mbili zinazopatikana katika shairi hili.    
  4.               Eleza kwa ufupi muundo uliotumika katika shairi hili.    
  5.               Mwandishi amtumia mtindo gani katika utanzu huu wa ushairi.        
  6.                 Taja kituo katika ubeti wa kwanza mpaka wa tatu.    

 

 

 

 

                                                        SEHEMU C ( Alama 30 )

Jibu maswali mawili tu  (2)  kutoka sehemu hii swali la (9) ni lazima.

  1.               Katika jamii yeyote ile kuna watu wanaokwamisha maendeleo kusonga mbele na hatimaye kujiangalia wao wenyewe na kuacha wengine kuhangaika katika maisha ya kila siku. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma eleza athari wanazozisababisha katika jamii. Toa hoja tatu katika kila diwani.
  2.          Kwa kutumia Riwaya ya Takadini na Watoto Wa Mama Ntiliye , eleza ni jinsi gani mwanaume ameonekana kuwa kikwazo cha maendeleo katika jamii.
  3.          Jadili jinsi wasanii wawili wa Tamthiliya mbili ulizosoma  walivyotumia mbinu ya kicheko kutoa ujumbe  waliokusudiwa kwa wananchi.                                                                                                                                                                                                                                                

                                                  ORODHA YA VITABU                

  USHAIRI

Wasakatonge                                                 M.S Khatibu ( DUP)

Malenga Wapya                                            TAKILUKI ( DUP )

Mashairi ya Chekacheka                              T.A Mvungi ( EP & DLTD)

 

 RIWAYA

Takadini                                                          Ben Hanson ( MBS )

Watoto Wa Mama Ntiliye                            E. Mbogo ( H.P)

Joka la Mdimu                                              A.J Safari ( H.P)

 

TAMTHILIYA

Orodha                                                            Steve Raynolds (M.A )

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe                 E.Semzaba ( ESC)

Kilio Chetu                                                       Medical Aid Foundation ( TPH)

 

 

1

 

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 165  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 165  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MKOA NA SERIKALI ZA MTAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI

SEPTEMBA-2022 

KISWAHILI KIDATO CHA NNE

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani
  5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi utakayojibia.

 

SEHEMU A

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) had (x), kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
  1. Bainisha tabia ya umbo lililopigiwa mstari katika kitenzi ib-w-a
  1. Kaulitendeka
  2. Kaulitendea
  3. Kaulitendeana
  4. Kaulitendwa
  5. kaulitendesha
  1. “Kiti cha mfalme kinaheshimiwa” katika sentensi hii neno lililopigiwa msitari ni aina gani ya neno katika uainishi wa maneno?
  1. Kiunganishi
  2. Kihusishi
  3. Nomino
  4. Kiingizi
  5. kivumishi
  1. ipi ni fasili sahihi kuhusu “Vina” miongoni mwa fasili zifuatazo?
  1. Mstari wa mwisho wa shairi unaobadilika ubeti mmoja hadi mwingine.
  2. Mistari ya mwisho wa ubeti wa ushairi wenye kujirudia kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
  3. Idadi ya silabi zinazopatikana katika mstari wa ubeti wa ushairi
  4. Silabi za kati na mwisho wa mstari wa ubeti wa shairi zenye mlio unaofanana
  5. Kifungu cha maneno kinachobeba wazo kuu mojawapo la ushairi.
  1. Mang’winda amekuwa mtoro sana. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina gani ya neno?
  1. Kitenzi kikuu
  2. Kiunganishi
  3. Nomino
  4. Kitenzi kisaidizi
  5. Kitenzi kishirikishi
  1. Ipi kati ya zifuatazo si sifa ya fasihili simulizi?
  1. Kuwa na hali ya utendaji
  2. Kuonana kwa fanani na hadhira ana kwa ana
  3. Kutopokea mabadiliko ya papo kwa papo
  4. Kuwa kongwe Zaidi
  5. Kutolewa kwa njia ya mdomo
  1. Ipi ni maana ya Nahau “Mbinu ya mgambo” kati ya maana hizi hapa chini:
  1. Tangazo maalumu
  2. Tia aibu
  3. Fanya tashtiti
  4. Mluzi wa mgambo
  5. Sare za mgambo
  1. Kategoria ya kisarufi inayowakilisha wakat katika kitenzi
  1. Leksiumu
  2. Kiambishi awali
  3. Shina
  4. Mtendwa/Mtendwa
  5. Njeo
  1. Kila lugha duniani inakua kwa kuiongezea msamiati wake. Ikiwemo Kiswahili. Kuna njia mbalimbali zinazotumika katika kuunda msamiati wa Kiswahili. Je unafikiria maneno wayarehema,dukapapainakorosho yamepatikana kwa njia gani kati zifuatazo?
  1. Kukopa maneno
  2. Kutohoa maneno
  3. Kuangalia kitu/kufananisha umbo
  4. Kudondosha maneno
  5. Kuambisha maneno
  1. Dhana mojawapo kati ya hizi huwa na dhima ya kuokoa muda:
  1. Ufahamu
  2. Fasihi
  3. Lughafasaha
  4. Masimulizi
  5. Hadhithi
  1. Zifuatazo ni tanzu za fasihi simulizi isipokuwa:
  1. Ushairi
  2. Maigizo
  3. Shairi
  4. Hadhithi
  5. semi
  1. Oanisha maana za dhana zilizo katika Orodha Akwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B, kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Kueleza jambo kwa maneno machache bila kuipoteza maana yake ya msingi.
  2. Alama ya uandishi inayotenga maneno yaliyo katika orodha Fulani.
  3. Lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu na si lazima kuwa na vitabu vyote anavyohitaji msomaji kuvisoma.
  4. Hutumika katika kukariri maneno yaliyosemwa na mtu mwingine
  5. Huhifadhi msamiati. Ni chanzo cha tahajia, ni chanzo cha sarufi ya lugha na hutumika katika utafiti has wahistoria ya lugha
  1. Ufahamu
  2. Mkato
  3. Ufupisho
  4. Ni aina za ufahamu
  5. Kamusi
  6. Lugha fasaha
  7. Mtajo
  8. Kusoma kwa burudani

 

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

  1. Weka majina yafuatayo katika ngeli zake
  1. Ugonjwa
  2. Kipofu
  3. Mchungwa
  4. Uovu
  1. Andika methali inayohusiana na mambo yafuatayo:
  1. Vidole vya binadamu
  2. Ukulima
  3. Imani ya binadamu kwa Mungu
  4. ulevi
  1. (a) Taja njia nne zinazotumika kuunda misimu.

(b)Msimu huwa na sifa za kuendana na wakati, taja misimu mine iliyozuka kipindi cha serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania 

  1. Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili umepitia vipindi vingi tofauti. Fafanua kwa mifano mambo manne (4) yaliyosaidia kuikuza na kuieneza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru.
  2. Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadini na watoto wa mama Ntilie, kwa kifupi ukitumia hoja nne, mbili kutoka kila riwaya. Eleza ni jinsi gani mwanaume ameonekana kuwa kikwazo cha maendeleo katika jamii. Tumia mzee lomolomo na Mzee Makwati.
  3. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata:

Amani. Amani!

Amani huyu ndio wimbo unaohitajika kusikika masikioni mwa vizazi vyetu vilivyopo lakini na vijavyo. Huu ndo ulikuwa wosia alikuwa akiutoa mzee mmoja aitwae Majanga kwa watoto wake. Lakini pia kwa wajukuu zake. Baada ya maneno hayo mjukuu mmoja alimuuliza babu yake, kwa nini unapenda tuimbe Amani siku zote? Mzee Majanga alisema yafuatayo : Amani ndio kila kitu Amani huleta umoja na mshikamano, Amani huleta maendeleo, Amani hufanya watu kulipa hata maduhuli ya serikali, Amani hufanya watu kutunza na kulinda miundombinu mbalimbali, Amani huwafanya watu kulala fofofo, Amani huwafanya watu kujenga majumba ya kifahari, Amani huwafanya watu kula chakula na kushiba, Amani inawafanya watu kuongeza familia. Amani ni kila kitu mjukuu wangu.

Baada ya maelezo hayo yote mjukuu wa pili wa mzee Majanga alimuuliza babu yake swali tena. Kwani babu Amani kutoweka inasababishwa na nini? Mzee majanga alimueleza mjukuu wake yafuatayo. Kuna vitu na mambo mengi yanayoweza kufanya Amani ipotee miongoni mwao ni pamoja na ufisadi wa viongozi, uongozi mbaya, ukosefu wa haki miongoni mwa watu, matumizi. Matumizi mabaya ya rasimali za nchi, ukabila, vifo vya watu na hudumu mbovu kwa wananchi. Punde si punde mjukuu wa tatu aliuliza swali kwa babu yake kuwa kwani Amani ikipotea kunatokea madhara gani? Babu alimjibu mjukuu wake kwa kusema kuwa, kwanza usiombe Amani hata ya familia ikipotea maana madhara yake huwezi kuyamudu hata siku moja.

Kwanza watu hugeuka na kuwa watumwa nchini mwao. Pili vifo kuongezeka, uharibifu wa miundombinu mfano barabara, reli n.k njaa kali, nchi kumwaga damu, maandamano yasiyoisha, hudumu zote za kijamii kuzorota kwa ujumla na hakuna awezaye kufanya lolote lenye tija sehemu ambayo haina Amani. Babu alihitimisha wosia wake kwa kuwakumbusha wajukuu zake kuwa wawe mstari wa mbele kuziunga mkono juhudi za mfalme wao anazozifanya ikiwa ni pamoja na kupiga vita rushwa na ufisadi, kujenga uchumi, kujenga aina zote za miundombinu, kuboresha usafiri wa angani na majini lakini kikubwa zaidi kutumia fursa ya elimu bila malipo

Kabla babu hajakataa roho aliwambai wajukuu zake kuwa “Amani ikipotea huwezi kuirudisha kwa urahisi ni bora njaa ya tumbo kuliko njaa ya akili.”

Maswali

  1. Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
  2. Unafikiri kwa nini mzee Majanga anahitaji vizazi vitunze Amani?
  3. (i)Taja mambo matatu yanayoweze kufanya Amani itoweke katika nchi

(ii) Je unahisi Amani ikipotea madhara yake huwa ni makubwa sana? Taja mawili tu.

  1. Unahisi ni kwa nini mzee Majanga anaiona njaa ya tumbo ina unafuu kuliko ile ya akili? Toa sababu mbili tu.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

  1. Wewe ukiwa ni mfanya biashara mashuhuri wa simu kutoka kampuni ya NOKIA, andika tangazo kwa wananchi katika gazeti la Uhuru ili kuwajulisha wateja wako na wananchi kwa ujumla juu ya simu mpya unazozileta msimu wa kiangazi.

 

ORODHA YA VITABU TEULE KWA SWALI LA 10 – 12

 

USHAIRI

Wasakatonge     - M.S Khatibu (DUP)

Malenga Wapya    - TAKILUKI (DUP)

Mashari ya Chekacheka  - T.A Mvungi (EP & D.LTD)

 

RIWAYA

Takadini     - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie   - E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu    - A.J.Safari (HP)

 

TAMTHILIYA

Orodha     - Steve Raynolds (MA)

Ngoswe Penzi kitovu cha Uzembe - E.Semzaba (ESC)

Kilio chetu     - Medical Aid Foundation

 

  1. “Mshairi siku zote kukemea uonevu katika jamii” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.
  2. “Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha kwa jamii husika.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma
  3. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 123  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 123  


THE PRESIDENT'S OFFICE

MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT

PRE-NATIONAL  EXAMINATION SERIES-1

KISWAHILI  FORM-4

2020

TIME: 3:00 HRS

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.

(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

  1. Kiunganishi   
  2. Kivumishi
  3. Kihisishi 
  4. Kiwakilishi 
  5. Kielezi

 

(ii) Ni sentensi ipi haina kitenzi kisaidizi?

  1.  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtiifu.
  2. Watoto wanatakiwa kulala mapema ili wawahi shuleni.
  3. Paka alikuwa anataka kula chakula cha mbwa.
  4. Juma alikuwa anasoma kitabu cha hadithi za mapenzi.
  5. Robert Kelly anataka kuja kutumbuiza mwezi Desemba.

(iii)  Ni sentensi ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?

  1. Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba.
  2. Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani.
  3. Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani. 
  4. Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama.
  5. Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba.

 

(iv)  Bainisha seti ya maneno inayofaa kuingizwa kwenye kamusi kwa kuzingatia mpangilio wa alfabeti.

  1. Jabali, jadhibika, jabiri, jadi, jalada
  2. Jabali, jabiri, jadhibika, jadi, jalada
  3. Jabali, jadi, jadhibika, jalada, jabiri 
  4. Jabiri, jabali, jalada, jadi, jadhibika
  5. Jabali, jalada, jabiri, jadhibika, jadi

 

(iv) Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno? 

  1. Kivumishi 
  2. Kielezi 
  3. Kiwakilishi 
  4. Kivumishi cha sifa 
  5. Kihisishi 

 

(v) Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:- 

  1. Kinaongewa na wabantu wengi 
  2. Ni lugha ya Taifa 
  3. Kina maneno mengi ya kibantu 
  4. Kimethibitishwa kiisimu na kihistoria 
  5. Wasomi wengi wamethibitisha hivyo.  


(vi) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi? 

  1. Muundo 
  2. Mtindo 
  3. Wahusika 
  4. Jina la mtunzi  
  5. Jina la kazi husika 

(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo? 

  1. Maneno yanayoonesha uhusiano baina ya neno moja na jingine. 
  2. Kipashio kidogo katika lugha kinachotumika kama dhana ya kuchambulia lugha Fulani. 
  3. Matokeo ya kuweka na kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi. 
  4. Kipashi cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea 
  5. Maneno yenye kutoa maana kamili


(viii) Nini maana ya sentensi sahili. 

  1. Ni sentensi yenye kishazi kuu kimoja au zaidi pamoja na kishazi tegemezi.
  2. Ni sentensi yenye kishazi huru 
  3. Ni sentensi yenye kuonesha masharti 
  4. Ni sentensi yenye maana nyingi 
  5. Ni sentensi yenye vishazi vingi 


(ix) Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa 

A.      Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi

B.      Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja 

            ana lugha yake

C.      Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi 

            mawasiliano

D.     Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana 

           ishara

  E.       Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza

 

2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika karatasi ya kujibia. 

 

Orodha    A

Orodha   B

  1. Sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolea aina zote za viambishi. 
  2. Hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi 
  3. Mzizi unaobakia baada ya kuondondewa viambishi tamati maana. 
  4. Mzizi wowote yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyumbuliko 
  5. Sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti 
  1. Mzizi asilia 
  2. Irabu 
  3. Mzizi/ kiini 
  4. Silabi 
  5. Mzizi wa mnyumbuliko 
  6. Shina la kitenzi 
  7. Mzizi asilia maana 
  8. Kitenzi 
  9. Mnyumbuliko 
  10. Uambishaji  

 

3.   (a) Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.

(b) Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni cha aina gani.
 (i) Darasani kuna utulivu mkubwa  

(ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
(iii) Mwalimu amerudi tena.
 (iv)  Nitaondoka wiki inayokuja. 

4. Moja ya faida ya misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mfano mmoja wa misimu zagao iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo:
(a) Muda mfupi baada ya kupata uhuru.
(b) Miaka ya Azimio la Arusha.
(c) Njaa ya mwaka 1974/1975.
(d) Miaka ya vita vya Kagera.
 (e)   Kipindi cha hali ngumu ya maisha baada ya vita vya Kagera.

5. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.

  1. Maisha ni safari ndefu.
  2. Ukisoma kwa bidii utafaulu kwa kiwango cha juu.
  3. Mtoto aliyelazwa hospitalini ameruhusiwa kwenda nyumbani.
  4. Nitakuja leo ingawa nitachelewa sana.
  5. Alinunua madaftari lakini kitabu cha Kiswahili alipewa na mwalimu.

6. (a) Eleza maana ya Kiambishi.

(b) Bainisha viambishi vilivyopo katika vitenzi vifuatavyo:

  1. Tunalima.
  2. Wanatembea.
  3. Godoro.

7. Katika kila sentensi andika neno moja lenye maana sawa na maelezo ya sentensi husika.

  1. Mtu anayechunguza uhalifu.
  2. Ng’ombe dume aliyehasiwa.
  3. Chombo cha usafiri kinachopita juu ya vyuma.
  4. Mti unaozaa matunda yanayotengenezwa kinywaji cha kahawa.
  5. Sehemu ndogo ya nchi iliyochongoka na kuzungukwa na bahari katika sehemu zake tatu.

 

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Ustaarabu ni jambo jema ambalo hupendwa na kila jamii yenye utashi hapa duniani. Kila jamii yenye ustaarabu mambo yake huendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazoeleweka. Maamuzi na mafanikio mbalimbali miongoni mwa wanajamii hutolewa bila hamaki wala kukurupuka. Kanuni na taratibu hizo huiongoza jamii kufikia upeo wake kimaendeleo kuanzia ngazi za chini kabisa ambayo ni familia mpaka ngazi ya juu kabisa ambayo ni taifa. Taratibu na kanuni hizo huwekwa katika chombo kimoja maalumu kinachoitwa katiba.

Katiba ni jumla ya sheria, kanuni na taratibu fulani zilizokubaliwa kuwekwa na jamii au taifa fulani kama dira ya maisha ya kila siku ya jamii au taifa hilo. Taifa bila katiba ni sawa na behewa la garimoshi bila injini. Hivyo katiba ina umuhimu wa kipekee katika taifa lolote lile.

Katika nchi zenye utamaduni wa kidemokrasia, katiba huundwa kutokana na maoni ya wananchi wake kwa utaratibu maalumu uliowekwa na serikali. Aghalbu, maoni na mawazo yaliyotolewa na wananchi huwa ni chimbuko la katiba hiyo. Wananchi hujiona ni sehemu ya utawala. Kwa upande wa pili wa sarafu, nchi zenye utaratibu wa kiimla, katiba hutayarishwa na watawala kwa maslahi yao binafsi. Katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala. Maoni na mawazo ya wananchi hayazingatiwi katika kuunda katiba.

Umuhimu wa katiba huonekana na kujidhihirisha waziwazi katika maisha ya kila siku ya nchi yoyote ile. Kwanza, katiba huelekeza wajibu wa ila mwanajamii kwa taifa lake na wajibu wa viongozi walio madarakani kwa wananchi au raia. Pili, katiba huonesha na kuainisha haki ambazo kila raia anastahili kupata na pia taratibu za kufuata katia kudai au dupewa haki hizo. Mbali na hayo, katiba hutoa utaratibu wa jinsi ya kuwapata viongozi wetu katika ngazi mabalimbali za kisiasa na kijamii. Pia uhuru wa mtu binafsi hulindwa na katiba. Hivyo, katika nchi ambayo ina katiba inayokidhi matarajio ya wananchi wote mambo huwa mazuri na kamwe chombo hakiwezi kwenda mrama.

Aidha, wananchi hawana budi kuelewa maana ya katiba ili waweze kutoa maoni na mapendekezo ya kuunda katiba mpya au kuimarisha iliyopo. Ni muhali kwa mtu asiyejua maana ya katiba kutoa maoni kuhusu katiba. Wananchi hupaswa kuelimishwa kupita semina, warsha na makongamano mbalimbali ili kujua katiba zao na kutoa maoni kuhusu uundaji wa katibu mpya.

Hata hivyo, wananchi wengi hasa vijana hawajitumi katika kuzijua katiba za nchi zao au kutoa maoni ya uundaji wa katiba mpya. Athari zake ni kutojua haki zao za msingi na kuburutwa kama mkokoteni na watawala katika mambo mbalimbali. Vilevile hulalamikia mambo ambayo hawakuchangia mawazo.

Hivyo basi, ni vizuri kwa wananchi kutambua, kuthamini na kuheshimu uwepo wa katiba kama kiongozi kizuri katika kuonesha njia muafaka ya kujiletea maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa nchi husika.

Maswali

(a)  Toa maana ya maneno yote yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.

(b) Kwa mujibu wa habari uliyosoma, taja mambo mazuri mawili yatokanayo na uwepo wa katiba katika nchi.

(c)  Kwanini mwandishi anasema katiba hutumiwa kama sera kwa maslahi ya watawala?

(d) Je, ni hofu gani aliyonayo mwandishi dhidi ya vijana kuhusu katiba?

(e) Andika kichwa cha habari uliyosoma kisichozidi maneno matano (5).

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

9.   Andika insha ya hoja isiyopungua maneno mia mbili na hamsini (250) na isiyozidi maneno mia tatu (300) kuhusu ‘Madhara ya Madawa ya Kulevya nchini Tanzania’.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12

USHAIRI

Wasakatonge   -  M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya  - TAKILUKI (DUP) 

Mashairi ya Chekacheka  -  T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

 Takadini     -   Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie  -  E. Mbogo (H.P) 

Joka la Mdimu   -   A.J .Safari (H.P.)

TAMTHILIYA

Orodha   -    Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu  -  Medical Aid Foundation (TPH)

10. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

11. “Ustadi wa msanii hudhihirishwa na fani”. Dhihirisha kauli hiyo kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma.

12. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma eleza jinsi taswira tatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256