FORM TWO KISWAHILI MIDTERM-2 EXAMS

OFISI YA RAISI, 

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UTUMILIFU KIDATO CHA PILI

021

Muda: 2:30

KISWAHILI

Mwaka:  AUG/SEPT 2024

Maelekezo 

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10). 

2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa. 

3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alama sabini (70). 

4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali. 

5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi. 

6. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji. 

7. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia. 

SEHEMU A (Alma 15) 

Jibu maswali ,yote katika sehemu hii. 

SEHEMU A (ALAMA 15) 

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. i) Sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo kwa hujulikana kama:-

  1.  sauti 
  2.  Herufi 
  3.  Irabu 
  4.  Konsonanti

ii) Silabi zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi huitwa.

  1.  Vina 
  2.  Mizani 
  3.  Sitiari 
  4.  Vituo

iii) Kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo?

  1.  Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti 
  2.  kuzungumza na kuongea kwa sauti 
  3.  kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti 
  4.  kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti

iv) Dhana ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana Zaidi ya moja?

  1.  Kaka amefua nguo 
  2.  Nipe sahani ya kulia 
  3.  Eva amenunua kanga 
  4.  John amempigia mpira

v) Mkisi ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama

  1.  Kihisishi 
  2.  Nomino 
  3.  Kiwakilishi 
  4.  Kielezi

vi) Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo.

  1.  Fani 
  2.  Falsafa 
  3.  Migogoro 
  4.  Dhamira

 

vii) Ipi ni tofauti ya msingi kati ya mashairi na ngonjera?

  1.  Mpangilio wa vina na mizani 
  2.  Idadi ya mizani na mishororo 
  3.  Majibizano baina ya watu wawili au Zaidi 
  4.  Mpangilio wa silabi na lugha ya mkato.

viii) Bosi samahani kuna barua yako hapa “Mtindo huu wa mazungumzo unatumika wapi”? 

  1.  Ofisini 
  2.  Kiwandani 
  3.  Shambani 
  4.  Kanisani

ix) Sababu zifuatazo husababisha kutokea kwa utata katika tungo isipokuwa

  1.  Neno kuwa na maana Zaidi ya moja 
  2.  Kuzingatia taratibu za uandishi 
  3.  Kutumia maneno yenye maana ya picha 
  4.  Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi

x) Seti ipi ni sahihi kuhusu vipengele vya fani katika fasihi simulizi?

  1.  Dhamira, migogoro, mtindo na mafunzo 
  2.  Ujumbe, matumizi ya lugha, wahusika, mtindo na muundo 
  3.  Wahusika, matumizi ya lugha, muundo, mtindo na mandhari 
  4.  Migogoro, Ujumbe, wahusika, mafunzo na mtindo.

2. Oanisha dhana zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B kasha andika herufi husika katika karatasi ya kujibia

 

ORODHA A

ORODHA B

  1. Upekee wa kundi la watu na shughuli zinazofanyika.
  2. Mitindo tofauti tofauti ya lugha katika miktadha mbalimbali
  3. Mzizi
  4. Kupamba lugha, kuficha ujumbe, kukuza lugha
  5. Mofo huru
  1.  Mkazo
  2.  Rejesta
  3.  Misimu
  4.  Sasa
  5.   –nyw-
  6.   Chanzo cha rejesta
  7.  Dhima za rejesta

 

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika seheme hii.

3. Tumia mofimu zifuatazo kuonesha thamani ilizopewa katika paradise Mfano Li-Kuonesha wakati uliopota (Aliondoka)

  1.    ta - kuonesha wakati ujao   
  2.    o - kuonesha mzizi wa neon -  
  3.    ni - kuonesha kitenzi kishirikishi-  
  4.    ku- kuonesha urejesho kwa mtendwa-  
  5.    ki - kuonesha udurushaji -  
  6.    me - kuonesha hali timilifu -  
  7.    kwa - kuonesha mahali -  
  8.    a - kuonesha nafsi -  
  9.    ka - kuonesha kauli ya kutendeka -  
  10.    ku - kuonesha wakati uliopita -  

 

4. (a) Maneno katika lugha yana dhima mbalimbali, bainisha aina ya vivumishi katika tungo zifuatazo :-

  1.    Shamba la bibi limeota nyasi
  1.    Gari dogo limepata ajali
  1.    Nyumba yetu ni nzuri sana
  1.    Kile kiatu ni cha mtoto
  1.    Wanafunzi wangapi wanapenda mayai?
  1.  Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi?
    1.    Wimbo  
    2.    Umbo   
    3.    Kilio   
    4.    Mtoro   
    5.    Mlo   

 

5. (a) Taja alama tano (5) za uakifishi na kisha utoe dhima moja kwa kila alama

(b) Kamilisha mchoro ufuatao wa vipera vya ushairi.

image

 

6. Rafiki yako hakuwepo darasani wakati Mwalimu wa kiswahili alipokuwa anafundisha mada ya uandishi wa barua pepe. Mbainishie rafiki yako vipengele vitano (5) vya msingi anavyopaswa kuvizingatia wakati wa kuandika ujmbe wa barua pepe.

7. Kwa kila methali uliyopewa onesha fundisho lake katika maisha ya kila siku.

  1.    Usiache mbachao kwa msala upitao
  2.    Mgaagaa na upwa hall wali mkavu
  3.    Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
  4.    Mchelea mwana kulia hulia yeye
  5.    Fadhila mfanyie mbuzi mwanadamu atakuudhi

8. Fasihi simulizi huwa na sifa zinazoitofautisha na fasihi andishi.Thibitisha usemi huu kwa hoja tano huku ukizingatia sifa za fasihi simulizi.

 

 

Fasihi simulizi

Fasihi andishi

i.

 

 

ii.

 

 

iii.

 

 

iv.

 

 

v.

 

 

9. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:

(i) Vichekesho 

(ii) Mtindo

(iii) Lakabu

(iv)Soga

(v) Dhamira

 

SEHEMU C (Alama 15)

10. Mwandikie baba yako barua ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Kivukoni SLP 20 Singida kumuomba hela ya safari ya kutembelea mbuga za Wanyama. Jina lako liwe Masumbuko Likoko SLP 345 Mbeya .

 

 

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 188  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 188  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

JAMHURI  YA MUUNGANO YA TANZANIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI

KIDATO CHA PILI

AGOSTI 2023


 

        021                                                KISWAHILI

        Muda: Saa 2:30                                                                        Year: 2023 

 

Maelekezo

1  Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)

2  Jibu msawali yote 

3   Sehemu A ina alama kumi na tano (15) sehemu B ina alama sabaini (70) na sehemu C ina alama kumi na tano (15)

4    Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa

5   Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi

6   Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha upimaji

7    Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia 

 

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1.         Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika visanduku vilivyopo upande wa kulia wa karatasi yako. 

(i)           Sikumpata mofu ‘-ku’ ina dhima gani?

A.    Wakati uliopita  C. Umoja 

B.     Uyakinishi          D. Nzizi wa neno

(ii)        Sitiari ni __________________

A.    Kufananisha vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi

B.     Neno au mistari kadhaa pamoja na silabi hujirudia 

C.     Huusisha kujenga picha akilini 

D.    Kulinganisha vitu viwili au zaidi bila viunganishi

(iii)      Wazo kuu la kimatumizi katika kazi za fasihi huitwa 

A.    Ujumbe  C. Falsafa B. Dhamira            D. Mtazamo

(iv)       Tunaimba vizuri sana kiambishi “Tu” kina dhima ipi?

A.    Huonesha nafsi ya kwanza wingi          C. Huonesha nafsi ya tatu umoja

B.     Huonesha nafsi ya pili wingi     D. Huonesha nafsi ya tatu wingi

(v)         _______________ ni hadithi zinazoelezea asili ya watu vitu na maumbo mbalimbali ulimwenguni katika hali ya kufikirika tu.

A.    Tarihi      C. Visasili

B.     Ngano    D. Soga

(vi)       Mambo yanayojenga umbo la ndani la kazi ya fasihi ni yapi?

A.    Falsafa, mtazamo, ujumbe, dhamira, wahusika

B.     Dhamira, ujumbe, mtazamo, migogoro, matumizi ya lugha 

C.     Dhamira ujumbe, mandhari, mgogoro, mtazamo

D.    Mtazamo, falsafa, dhamira, ujumbe na mgogoro

(vii)    Ni kutamkaji unaotambulisha asili ya mtu, 

A.    Kiimbo  C. Lafudhi

B.     Mkazo    D. Silabi

(viii)  Kwa maneno mengine fonolojia tunaweza kuiita…

A.    Sarufi muundo   C. Sarufi matamshi

B.     Pragmatiki          D. Sarufi maumbo 

       

(ix)       “Mungu yu mwema” Je, neno “yu” katika tungo hapo juu linabeba dhima ya aina gani ya neno.

A.    Nomino C. Kitenzi kisaidizi

B.     Kiwakilishi        D. Kitenzi kishirikishi

(x)         Vizuri vimeibiwa, viatu vizuri vimeibiwa na anacheza vizuri. neno vizuri limetumika kama

A.    Nomino, kiwakilishi na kivumishi        C. Kiwakilishi, kielezi na kivumishi 

B.     Kiwakilishi, kivumishi na kielezi          D. Kielezi, kiwakilishi na kiwakilishi

2.         Oanisha dhana zifuatazo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya maelezo husika katika Orodha B kisha andika herufi hiyo katika sehemu ya majibu kama inavyoonekana katika jedwali.

ORODHA A

MAJIBU

ORODHA B

i. Tashibiha  ii. Tashihisi iii. Tafsida  iv. Takriri

v. Mdokezo 

 

image

 

image

 

image

 

image

 

A.    Mayra alitembea, alitemea, alitembe hadi akafika 

B.    Mtoto wa mzee juma aliaga dunia katika vita vile vya makabila 

C.    Mayra akasema nitaku…………. nitakup…….

D.    Mayra alipokuwa msituni alipokelewa na sauti nyororo za ndege wakiimba. 

E.     Mzee Juma aliongea kwa hasira mithili ya mbogo aliyejeruhiwa.

 

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3.         Kwa mifano thabiti eleza maana ya maneno yafuatayo 

(a)      Mofolojia

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

(b)      Shadda

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

 

(c)      Fonimu

………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

(d)      Alofoni

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

(e)      Shina

………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………

4.         (a) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendwa 

i) Imba  ……………………………………………………………………………………. 

ii) Ruka  ……………………………………………………………………………………. 

iii) Piga  ……………………………………………………………………………………. 

iv) Soma  …………………………………………………………………………………….

 v) Omba  …………………………………………………………………………………….

(b) Onesha kivumishi katika tungo zifuatazo kisha bainisha aina gani ya kivumishi. 

i)       Mti mkavu umeanguka 

                        Kivumishi      …………………………………...………

                        Aina                …………………………………...……… 

 

ii)     Mbwa ambaye amekuja ameondoka

                        Kivumishi      …………………………………...……… 

                        Aina                …………………………………...………

 

iii)   Mwanafunzi mwingine ameletwa 

                        Kivumishi      …………………………………...……… 

                        Aina                …………………………………...……… 

iv)   Mtoto amejenga banda la kuku

                        Kivumishi      …………………………………...……… 

                        Aina                …………………………………...………

v)      Kikombe hiki kimevunjika

                        Kivumishi      …………………………………...……… 

                        Aina                …………………………………...………

5.         (a) Kitenzi kishiriki ni neno linaloonesha tabia au hali iliyokuwepo au isiyokuwepo kwa kitu au  mtu fulani. Tunga sentensi tano (05) kwa kutumia vitenzi vishirikishi tofauti na pigia  mstari  vitenzi hivyo. 

i. ……………………………………………………………………………………………… 

ii. ………………………………………………………………………………………………

 iii. ……………………………………………………………………………………………… 

iv. ……………………………………………………………………………………………… 

v. ………………………………………………………………………………………………

(b) Kwa muundo wa jedwali tambulisha nomino tano (5) zisizo na umbo dhahiri la wingi na uzipange kwa umoja na wingi wake. 

i. ……………………………………………………………………………………………… 

ii. ……………………………………………………………………………………………… 

iii. ……………………………………………………………………………………………… 

iv. ……………………………………………………………………………………………… 

v. ………………………………………………………………………………………………

6.         Kila tasnia ya uandishi ina hatua zake. Andika barua kwa mkuu wa shule ukiomba ruhusa ya kwenda hospitali kutibiwa. Barua yako ipite kwa mwalimu wako wa darasa. 

……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

7.      “Misemo mingi hutumika kwa madhumuni ya kulinda na kuvuta umakini wa mtu.” Fafanua usemi huu kwa kutumia misemo mitano”

i.        …………………………………………………………………………………………………..

 ii. ………………………………………………………………………………………………….. 

iii. …………………………………………………………………………………………………..

 iv. …………………………………………………………………………………………………..

v. …………………………………………………………………………………………………..

8.      Soma ngonjera ifuatayo kisha jibu maswali 

1.      Hodi! hodi! naingia  Nyamazeni nawaambia,

Nataka kuwaelezea,

Sababu za kuhesabia, Sensa ni ukombozi, Kwa kila mtanzania. 

2.      Hesabu isipotimia,

Serikali isipojua,

Mipango itazimia, Sensa ni ukombozi, Kwa kila mtanzania.

3.      Serikali ikishajua,

Idadi ikatambua, 

Kila raia kumpatia,

Sensa ni ukombozi,

Kwa kila mtanzania

4.      Shule itatujengea, Hospitali zitaenea,

Maji itapanua,

Na barabara pia,

Sensa ni ukombozi,

Kwa kila mtanzania

       

5.      Elimu imeitoa, Kwenu watanzania,

Hongera mlojitoa 

Vituoni kusogea,

Nyumbani kusubiria 

Sensa ni ukombozi,

Kwa kila mtanzania

Maswali 

i.        Nini dhamira ya fanani katika utungo huu? ……………………………………………………..

ii.      Je, mtambaji ana msimamo gani kwa jamii?

………………………………………………………………………………………………….. iii) Kwa mujibu wa mwandishi ni athari gani zinaweza kujitokeza endapo sensa haitafanyika?

…………………………………………………………………………………………………..

…………………………………………………………………………………………………..

iv) Mtunzi wa utungo huu ana imani gani na falsafa ipi kuhusu sensa?

…………………………………………………………………………………………..………

 v) Taja jina la muhusika mkuu katika utungo huu.? ……………………………………………….

9.      Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi simulizi siku hizi huhifadhiwa katika vinasa sauti kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye. Bainisha athari tano (5) hasi zinazojitokeza fasihi simulizi inapohifadhiwa katika njia tajwa.

i.        ………………………………………………………………………………………………….. 

ii. ………………………………………………………………………………………………….. 

iii. ………………………………………………………………………………………………….. 

iv. …………………………………………………………………………………………………..

v. …………………………………………………………………………………………………..

       

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10) katika sehemu hii.

10.  Siku zote uwapo na sherehe hualika watu tofauti ambao ni ndugu, jamaa na marafiki. Ukiwa kama kijana wa familia ya Mtunda Maembe, mwalike mama yako mdogo aitwae Neema Juma katika sherehe ya harusi ya kaka yako Paulo Maembe itakayofanyika tarehe 20/12/2023. Jina lako Omari Maembe 

………………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

 

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 159  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 159  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA

FOMATI MPYA YA NECTA

KISWAHILI KIDATO CHA PILI

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehumu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
  2. Jibu maswali yote
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15) sehemu B ina alama sabini (7)) na sehemu C ina alama kumi na tano (15)
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha upimaji.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo:
  1. Ni kiambishi kipi kinachodokeza ukanushi kati ya vifuatavyo
  1. Wa-
  2. Sh-
  3. –a
  4. Si-
  5. Na-
  1. Neno lipi kati ya haya ni mofu huru?
  1. Uji
  2. Uzuri
  3. Uchache
  4. Ufa
  5. upweke
  1. unyumbulishaji katika lugha ya Kiswahili huhususha uchapikaji wa viambishi
  1. kabla ya mzizi wa neno
  2. katikati ya mzizi wa neno
  3. Baada ya mzizi wa neno
  4. Kabla na baada ya vitenzi
  5. Kabla, katikati na baada ya mzizi
  1. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halitokani na utohoaji
  1. Posta
  2. Kompyuta
  3. Polisi
  4. Boksi
  5. Achali
  1. Utokeji wa misimu katika jamii hutegemea na
  1. Uchaguzi wa viongozi
  2. Mabadiliko ya kijamii
  3. Shughuli itendekayo
  4. Utani uliopo miongoni mwa wanajamii
  5. Kutumika na kudumu kwa muda mrefu
  1. Nyenzo kuu za lugha ya mazungumzo ni
  1. Usimuliaji
  2. Mdomo
  3. Maandishi
  4. Vitendo
  5. Ishara
  1. Utoshelezi wa muwala ni vipengele vya
  1. Mtindo
  2. Matumizi ya lugha
  3. Muundo
  4. Ujumbe
  5. falsafa
  1. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halihusiani na ushahiri
  1. Mshororo
  2. Kipande
  3. Bahari
  4. Dayalojia
  5. Muwala
  1. Vipi ni ubora wa njia ya kuhifadhi kazi ya fasihi simulizi kwa kichwa?
  1. Ni kongwe
  2. Ina uhai
  3. Ina gharama
  4. Hukutana chini ya mti
  5. Ni rahisi kubadilika
  1. Vipengele vifuatavyo hutumiwa katika uandishi wa barua rasmi na barua pepe isipokuwa
  1. Anuani ya mwandishi na mwandikiwa
  2. Lengo
  3. Mada na kichwa
  4. Saini
  5. Jina la mwandishi
  1. Onesha dhana zilizopo fungu A na mifano iliyopo fungu B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.

FUNGU A

FUNGU B

  1. Mzizi
  2. Mofu huru
  3. Kiambishi awali
  4. Kiambishi cha kauli
  5. Kiambishi tamati
  1. Mtu
  2. Sasa
  3. –cham-
  4. –chok-
  5. –an-
  6. –ji.
  7. u-

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Tumia mofimu zifuatazo kuonesha thamani zilizopewa katika paradise

Mfano: Li-Kuonesha wakati uliopita (Aliondoka)

  1. ta  - Kuonesha wakati ujao -___________________
  2. o -  Kuonesha mzizi wa neno -_________________
  3. ni  -  kuonesha kitenzi kishirikishi - _____________
  4. ku - Kuonesha urejesho kwa mtendwa - __________
  5. ki  - Kuonesha hali udurushaji -_________________
  6. me - Kuonesha hali timilifu -___________________
  7. kwa – kuonesha hali mahali -____________________
  8. a –   kuonesha nafsi -_________________________
  9. ka – kuonesha kauli ya kutendeka -______________
  10. ku –  Kuonesha wakati uliopita -_________________
  1. (a)Maneno katika lugha yana dhima mbalimbali, bainisha aina ya vivumishi katika tungo zifuatazo.
  1. Shamba la bibi limeota nyasi _____________________
  2. Gari lililoondoka limepata ajali ______________
  3. Nyumba yetu ni nzuri sana ________________
  4. Kile kiatu ni cha mtoto __________________
  5. Wnafunzi wangapi wanapenda mayai? __________

(b) Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi?

  1. Wimbo ____________
  2. Umbo ______________
  3. Kilio ______________
  4. Mtoro ______________
  5. Mlo _______________
  1. Toa maana mbili kwa akila neno
  1. Mbuni _______________
  2. Mto _________________
  3. Ota __________________
  4. Pepo ________________
  5. Shuka ________________
  1. Sentensi zifuatazo zinabeba maana ya istilahi Fulani. Zianishe istilahi hizo kwa kila sentensi.

Mfano: Ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi “Mofimu”

  1. Ni aya ndogo kwenye kamusi ambayo huhusisha kidahizo na maelezo yake yote
  2. Ni sauti ambazo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti
  3. Ni mtindo wa lugha wa watu Fulani katika kazi maalumu
  4. Ni maneno ambayo huonesha hisia za mtenda au mtendwa
  5. Kamusi huandikwa kwa lugha moja
  1. Kila mhusika ana kazi yake katika kazi ya fasihi. Taja kazi moja ya wahusika wafuatao.
  1. Fani
  2. Hadhira
  3. Wanyama
  4. Binadamu
  5. mahali
  1. katika kazi ya fasihi simulizia viungo vya mwili kama vile macho, mdomo, kichwa, miguu hata mikono husaidia kufanikisha kazi hiyo na kufikisha ujumbe kwa jamii. Taja na eleza kwa kifupi faida tano (5) za kutumia viungo hivyo vya mwili vilivyotajwa hapo juu katika kazi ya fasihi simulizi.
  2. Kila kitu kina faida na hasara zake. Kwa kila kipengele kifuatacho eleza faida moja na hasara moja.
  1. Utani
  1. Faida
  2. Hasara
  1. Matambiko
  1. Faida
  2. Hasara
  1. Miviga
  1. Faida
  2. Hasira
  1. Michezo ya watoto
  1. Faida
  2. Hasara
  1. Michezo ya jukwaani
  1. Faida
  2. Hasara

SEHEMU C (Alama 15)

  1. Kwa hoja nne (4), fafanua hasara ambazo huwezi kumkumba mtu yeyote asiyependa kushiriki mazoezi na michezo hasa kwa wanafunzi shuleni.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 115  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 115  

THE PRESIDENT'S OFFICE

MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT

AUGUST-SEPTEMBER   EXAMINATION SERIES

KISWAHILI  FORM-2

2020

TIME: 2:30 HRS

SEHEMU A

1.  Soma hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:

Katika nchi ya ughaibuni kulikuwa na mfalme mwenye dharau na maringo sana, aliwaona wananchi wake kama wajinga. Watu wake waliishi bila amani na walichukia vitendo vya mfalme wao. Mfalme huyo alikuwa anajigamba kuwa yeye ni tajiri kuliko wafalme wote katika nchi za jirani. Kwa ujumla mfalme huyo alikuwa mnyanyasaji na mwenyekebehi nyingi.

imageimageMfalme alikuwa mwenye kufuru sana, hata alidiriki kutamka kwenye mkutano wa hadhara kuwa hajawahi kuona njaa. Mzee mmoja mwenye busara aitwaye Bwana Adili alimwambia mfalme kuwa asihofu atampeleka mahali njaa inakopatikana. Bwana Adili kwa kukubaliana na mfalme walipanga siku ya safari ya kwenda kumwonesha mahali ilipo njaa. Safari hiyo ilikuwa na masharti kuwa hakuna kula chochote asubuhi na hakuna kubeba masurufu yoyote yakiwemo maji, ingawa Bwana Adili kwa ujanja wake alibeba.

Safari ilianza asubuhi mapema huku mfalme akiwa na furaha kubwa ya kwenda kuona njaa. Walitembea mwendo wa saa zisizopungua ?ita, mfalme akawa amechoka sana akamwomba Bwana Adili wapumzike. Uchovu huo imageulitokana na ukweli kwamba mfalme hakuwahi kwenda mwendo mrefu kwa miguu. Wakati wa mapumziko mfalme alimwomba Bwana Adili maji na mkate lakini Bwana Adili alimnyima, walipumzika kwa muda wa saa moja na safari ikaendelea. Ilipofika jioni mfalme alikuwa amechoka kabisa kwani mwendo ulikuwa mrefu na njaa ilimuuma mno. Walipumzika chini ya mti, mfalme alimuuliza Bwana Adili, mbona hatufiki safari yetu? Bwana Adili hakumjibu chochote bali alichukua mkate akala na kunywa maji, mfalme alihisi njaa kali, alimwomba Bwana Adili mkate na maji lakini alimnyima.

Hali ya mfalme ilizidi kuwa mbaya sana, ndipo Bwana Adili akamwambia nitakupa maji na mkate ule lakini uahidi kwa maandishi kuwa utaacha dharau na majivuno kwa watu. Mfalme alipiga magoti mbele ya Bwana Adili na kuchukua karatasi na kalamu aliyopewa na Bwana Adili na kuahidi kwa maandishi kuwa ataacha kabisa tabia ya dharau na majivuno. Bwana Adili alipokea maelezo ya mfalme na akampa mkate na maji. Mfalme alipomaliza kula alimshukuru sana, ndipo Bwana Adili alipomgeukia mfalme na kumweleza kuwa hakuna maskani ya njaa bali hali aliyokuwa nayo mtu asipokula chakula. Waliporudi mfalme aliitisha mkutano wa hadhara. aliwaomba radhi wananchi wake na tangu siku hiyo mfalme aliishi kwa upendo na wananchi wote.

Maswali

(a)(i)     Bwana Adili alitoa masharti gani ya safari?.........................................

(ii)    Kwa nini Bwana Adili alitoa masharti uliyoeleza katika kipengele

(b)     Toa methali moja inayolingana na fundisho linalopatikana katika hadithi uliyosoma.

(c)     Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika hadithi uliyosoma:

(i)Anajigamba ..................

(ii)Kebehi .....................

(iii) Kufuru ..................

(iv)Masurufu . .......................

 (v) Maskani....................

2.   Andika ufupisho wa habari uliyosoma kwa maneno 60.

SEHEMU B

SARUFI

3. (a) Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika tungo zifuatazo: Mfano: Sisi tunacheza mpira uwanjani. image

Jibu: Kiwakilishi ... .... ..... ......

(i)Kuku yu bandani . .............

(ii)Maskini! Ameumia! ...............

(iii)Wako hatakiwi hapa .................

(iv)Dagaavva Kigoma ni watamu ................

(v)Mtoto alikuwa anacheza mpira . ..................

(b) Unda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo:

(i) Kiumbe                                                

(ii) Pigo  

(iii)Mteule  

(iv)Mlinzi    

(v)Kiongozi

(vi) Mchezo 

(vii) Adhabu

(viii) Muundo  

(ix) Chakula 

(x)  Mtego 

4. Tunga sentensi kwa kutumia aina za maneno zifuatazo:

Mfano: Jina usiku litumike kama kielezi

Wote wawili waliondoka jana usiku image 

(i) Mimi litumike kama kiwakilishi . ................

(ii) Letu litumike kama kivumishi . ...............

(iii) Tutaendelea litumike kama kitenzi kisaidizi .................. 

(iv) Na litumike kama kiunganishi . ..........................

(v) Upendo litumike kama nomino dhahania ..................

SEHEMU C

MATUMIZI YA LUCHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

5. (a) Andika kwa usahihi maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumka katika tungo zifuatazo:

(i) Mashirikiano ni muhimu kwetu .................

(ii) Mimi ni mwanainji wa Tanzania ...............

(iii)Mama anakaaga jikoni anapopika ............

(iv) Hakuna mapungufu yaliyojitokeza ........

(v) Hajafika mwanafunzi yoyote leo ..................

(vi) Huyu ni rafiki angu.................................

(b)     Eleza maana mbili kwa kila tungo.

(i) Mama anaota.

(ii)Tafathali nipe sahani ya kulia.

(iii)Vijakazi wanalima barabara.

(iv)Amekanyaga mtoto.

(v) Shangazi anawachezea wanangu.

6. (a)     Andika KWELI kama sentensi ni sahihi au SIO KWELI kama sentensi si sahii
 (i) Tafadhali mpikie ugali. Hii ni tungo tata ......... 

(ii) Kifaa kinachotumika kulia chakula kiitwacho uma wingi wake ni uma ... ... ...

(iii) Rejesta ni misimu ya Kiswahili . 

(iv) Amekula chumvi nyingi. Hii ni nahau 

(v) Mbili kutwa mara tatu. Ni rejesta ya kujifunza hesabu ........

(b) Eleza kwa kifupi dhima tano za lugha katika jamii.

 

SEHEMU D

FASIHI SIMULIZI

7. (a) Eleza kwa kifupi maana ya dhana zifuatazo:

(i) Shairi .............

(ii)Vichekesho ... ... ...

(iii)Ngonjera ... ......

(iv)Visasili .............

(v) Mapingiti ..............

8.   Jaza nafasi iliyoachwa wazi kukamilisha methali zifuatazo:

(i) Samaki mkunje ........................

(ii) ............njaa mwana malegeza. 

(iii) ..........hutanda na kuyeyuka. 

(iv)  Ajidhaniaye kasimama .........

 (v) ...........usiilalie mlango wazi.

 9.  Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Mwanafunzi ikibali, mbeleya wako mwalimu.

Katika siku si mbali, utakuwa aalimu,

Kujitia baradhuli, baadaye ulaumu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Usijifanye kiburi, kujifanya chakaramu,

Hiyo wanaita shari, ndaniyake ina sumu,

Hivi hauna habari, heshima kitu adimu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Katika hii sayari, namba moja ni elimu,

Usiipate sufuri, kisha hapo ulaumu,

Maisha haya safari, mwana kitu adimu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Ni walezi mashuhuri, hivyo wana umuhimu, 

Wameishika nambari, kutokana na kalamu, 

Usimwendeshe chuchuri, uidumishe nidhamu, 

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Mwalimu baba na mama, hilo wazi ufahamu,

Hivyo tazama ndarama, zisisababishe-ghamu, 

Neno hili ni la zama, shika nakupajukumu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Sitapenda kukuchosha, kwa mengi kukushutumu, image

Nakutakia maisha,ya shuleyenye utamu,

Ili upate bashasha,na mema kutakadamu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

MASWALI

(i)Mtunzi wa shairi hili anatoa ujumbe gani?

(ii)Ni mambo gani matatu ambayo mwanafunzi unatakiwa imagekuyaepuka kama yalivyoelezwa katika shairi ulilosoma?

(iii) Bainisha kituo bahari katika shairi ulilosoma.

(iv)Bainisha vina vya kati na vya mwisho vya shairi ulilosoma.

(v)Mshairi ana maana gani anaposema, Neno hili ni la zama, shika nakupa jukumu.”

(vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma:

  • Ikibali ..... ... .
  •  Baradhuli ...........
  • Kutakadamu .........
  •  Chuchuri .........
  • Bashasha .........

SEHEMU E : UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

10. Wewe ni miongoni mwa Watanzania wanaopenda kuishi maisha marefu, hivyo unakerwa sana na tatizo la ajali za barabarani. Andika barua kwenye gazeti la Uhuru ukipendekeza kwa serikali hatua gani zichukuliwe iii kuthibiti ajali za barabarani. Toa hoja tatu tu.

 

 

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 34  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 34  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256