FORM ONE HISTORIA MIDTERM-2 EXAMS

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA ROBO MUHULA AGOSTI

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

KIDATO CHA KWANZA 

MUDA: SAA 2:30 

MAAELEKEZO 1

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moaja(11)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu ya kila swali

SEHEMU A (Alama 16)

1. Katika kipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu saahihi kisha andika herufi ya jibu sahihi.

i.   Jamii za asili ya Kitanzania zilihama kutoka eneo moja na kwenda eneo jingine kwa sababu:

  1. Kufuata wazazi wa asili yao. 
  2. Kufuata elimu ya jadi 
  3. kufuaata ardhi yenye rutuba
  4. kufanya biashara 

ii. Somo la historia a maadili limeundwa na dhana kuu mbili:

  1. Dhana ya Historia ya Tanzania na dhana ya maadili 
  2. Dhana ya makabila na dhana ya utamaduni 
  3. dhana ya jando na ya unyago
  4. dhana ya Sanaa na jamii 

iii. Uhusiano kati ya somo la historia na maadili na chakula na lishe ni:

  1. Kuelewa vyakula vya biashara na kula nyumbani 
  2. Kuelewa vyakula vya asili ya maji na ardhi. 
  3. kuelewa faida ya vyakula vya wanga.
  4. Kuelewa asili ya vyakula, mabadiliko ya mtindo ya kula katika jamii.

iv) jamii za wakushito zinahusisha makabila kama:

  1. Wazaramo na wandengereko 
  2. Wairaki na waburugi 
  3. wangindo na wamatumbi
  4. wachaga na wapare

v) “Rushwa ni adui mkubwa wa haki.Tusipoidhibiti itaangamiza taifa”Baadhi ya madhara ya rushwa ni:

  1. Kushuka kwa tija na fanisi wa taasisi 
  2. Kuapata huduma ya haraka 
  3. usawa na uhalali kupata huduma
  4. kuwajibika kutokana na hongo uliopata 

vi) kulikuwa na sifa maaalumu zilizozingatiwa ili mtu ateuliwe kuwa kiongozi wa ukoo.Miongoni mwa sifa hizo ni:

  1. Ujuzi wa uganga na ushujaa 
  2. Kumiliki wake wengi na mashamba 
  3. awe mkali na anaeogopwa
  4. awe na mali na mfanyabiashara 

vii) Mafunzo katika kujenga tabia njema yalisisitiza mambo yafuatayo:

  1. Kusisitiza kuheshimuu wazazi tu. 
  2. Kufanya kazi kwa maslahi binafsi. 
  3. uwaajibikaji,upendo na ujasiri
  4. kulima na kupika 

viii) Nini maana ya “Urithi wa jamii?”

  1. Mali ya familia pekee 
  2. Mambo ya kisiasa tu 
  3. mila, desturi na tamaduni tunazorithi kutoka kwa wazee.
  4. shuguli za kibiashara.

ix) Maadili ya msingi katika jamii ni Pamoja na:

  1. Urafiki,wizi na heshima 
  2. Heshima,uaminifu na mshikamano. 
  3. Woga,upendeleo na bidi.
  4. Hasira,upendo na chuki

x) Mojawapo ya vyanzo vya Historia visivyoandikwaa ni:

  1. magazeti 
  2. Hati rasmi 
  3. mapokeo ya mdomo
  4. vitabu vya kumbukumbu

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x










.

2. Oanisha maelezo ya maneno kutoka kifungu A na maneno kutoka kifungu B kisha andika herufi ya jibu sahihi

KIFUNGU A

KIFUNGU B

  1. Uadilifu
  2. Utu
  3. Umoja
  4. Usawa
  5. Lugha ya taifa
  6. Uzalendo
  1. Kurahisisha mawasiliano ya watu wa taifa kwasababu inaunganisha watu wa Tanzania.
  2. Kuheshimiana na kujali hali za wengine kwa kuwasaidia na kutunza haki za binadamu.
  3. Unaonganisha watu wa Tanzania kutoka makabila,dini na utamaduni tofauti.
  4. Inahusu watu kuwa waaminifu na nidhamu.
  5. Watu wa Tanzania wanavyotambua haki za kila mtu mbele ya sheria
  6. Inahusu upendo wa watu kwa nchi yao

i

ii

iii

iv

v

vi






.

SEHEMU B (ALAMA 54)

Jibu maswali yote katika seehemu hii.

3. a) bainisha urithi wa asili uliopo maeneo unamoishi na taja manufaa ya urithi huo kwa jamii yako (hoja nne).

b) Urithi waa kihistoria ni eneo pana linalotoa na kazi kumnufaiisha mtu binafsi,jamii na taifa.Taja matumizi ya fursa hizo. (Hoja tano)

4. a) kabla kuingia ukoloni,jaamii za kitanzaniaa zilikuwa zinatumia mifumo maalumu kuelimisha watu. wake.bainisha malengo ya elimu kabla ya ukoloni (hoja nne) 

b) Taja tofauti kati ya jando na unyago. (Hoja tano)

5.a) Ni mambo gani mazuri yaliyopo katika mila ana desturi ya jamii za asili ambayo hayatiliwi mkazo kwa sasa?

b) utamaduni wa jamii za asili uliwandaa vijana kujitegemea kwa sababu ulitilia mkazo i. ii. iii.

6. Jamii za Wabantu,Wakushito,Wakichembe na Wanilo zilikuwa na desturi zilizolenga kukuza maadili katika Nyanja mbalimbali za Maisha yao.Taja malengo yaliojikita katika ujenzi wa maadili katika jamii.(hoja tano)

7. Tunapaswa kufahamu kuwa wajibu wa kulinda na kuifadhi maadili na urithi wa jamii ni jukumu la kila Mtanzania.thibitisha dai hili kwa kutaja matendo yanayokuza na kulinda maadili na urithi wa Tanzania.

8.Elezea maana ya istilahi zifuatazo:

  1. Urithi wa kihistoria
  2. Ol-Aiguanani
  3. Maadili
  4. Wakichembe
  5. Fursa
  6. matambiko

SEHEMU C (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii,swali la tisa (9) ni la lazima na kila swali lina alama 15.

9.Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule yako na mbobezi wa somo la Historia ya Tanzania na maadili Elezea tofaauti wa mfumo wa elimu ya jadi na mfumo wa elimu ya sasa.(hoja tano)

10. kumekuwepo na mmomomyoko wa maadili kwa jamii ya sasa kwa kiasi kikubwa hususani kwa vijana,Ungepewa nafasi ya kutoa maoni kuhusu maadili shuleni mambo gani ungependa yazingatiwe katika ujenzi wa maadili kwa vijana.elezea hoja tano(5) 11.elezea sababu za kujifunza somo la Historia ya Tanzania na maadili

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 225  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 225  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256