FORM ONE KISWAHILI MIDTERM-2 EXAMS

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

 SCHOOL

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI AGOSTI/SEPTEMBA 2024

KIDATO CHA KWANZA

KISWAHILI 

SEHEMU A (Alama 15)

1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi za kujibia ulizopewa

i.  ”Siri ya mtungi aijuaye kata” huu ni usemi ambao umeundwa na tamathali ya semi ambayo huvipa uwezo wa kibinadamu vitu ambavyo si viumbe hai. Je tamathari hiyo ni ipi kati ya hizi.

  1.              Sitiari 
  2.               Tashibia 
  3.              Tashihisi 
  4.             Takriri

ii.  Kipanya alipoulizwa swali la kutaja dhima tano za viambishi awali, alitoa hoja nne zilizo zahihi na hoja moja haikuwa shihi. Ibainishe hoja ya Kipanya ambayo haikuwa sahihi miongoni mwa hizi

  1.              Kudokeza njeo za vitenzi 
  2.               Kudokeza kauli mbalimbali za vitenzi
  3.              Kudokeza nafsi katika vitenzi 
  4.             Kuonesha ukanushi
  5.               Kudokeza umoja na uwingi

 

iii.  Haule alichezesha vitamkwa vya neno LIMA likawa MALI, LAMI na IMLA. Je Haule alitumia maarifa ya tawi gani la sarufi kufanikisha mchezo huo?

  1.              MOFOLOJIA 
  2.               SINTAKSIA 
  3.              SEMANTIKI 
  4.             FONOLOJIA

iv.  Mwanafunzi mwenyewe hapendi kujisomea mara kwa mara ndio sababu kuu inayomfanya asiazime vitabu. Neno mwenyewe linapatikana kwenye aina gani ya kivumishi kati ya hizi;

  1.              kivumishi cha cha sifa 
  2.               kivumishi cha jina kwa jina 
  3.              kivumishi cha pekee 
  4.             kivumishi cha A-unganifu.

v.  Samata amempigia mpira mwanae” kuna ukweli usiopingwa kwamba tungo iliyotajwa ina uvulivuli ndani yake. Je uvuluvuli huo umetokana na matumizi ya kauli gani miongoni mwa zifuatazo;

  1.              Tendwa 
  2.               Tendewa 
  3.              Tendeana 
  4.             Tendea

vi.  Baada ya mjadala mrefu kuhusu matawi manne ya sarufi, wanafunzi wa mkiu walisahau kisawe cha sintakisia . wasaidie kukibaini hapo chini.

  1.              Sarufi maumbo 
  2.               Sarufi miundo
  3.              Sarufi matamshi 
  4.             Sarufi maana

vii.  Kila changamoto hutatuliwa kulingana na uzito wake kwa kuipatia suluhu inayofaa. Je ipi ni suluhu ya utatata uliopo kwenye tungo isemayo “Baba amenunua mbuzi”

  1.              Kutokutumia maneno yenye maana zaisi ya moja
  2.               Kuzingatia alama za uandishi mfano nukta na mkato
  3.              Kuzingatia mkazo katika matamshi
  4.             Maneno yenye maana zaidi ya moja yafafanuliwe yatumikapo

viii.  Chukulia umeokota kikapu kimejaa vikaratasi vilivyoandikwa vipengere vya maudhui, na kuna kikaratasi kimoja tu, kimeandikwa kipengere cha fani. Je unadhani kikaatasi chenye kipengere cha fani kitakuwa na neno gani miongoni mwa haya yafuatayo;

  1.              Ujumbe 
  2.               Mandhari 
  3.              Dhamira 
  4.             Msimamo

ix.  Mzee Hashimu ni mvuvi maarufu ambaye hupenda kuimba nyimbo tamu za kujiliwaza awapo katika shughuli zake za uvuvi. Je nyimbo za mzee Hashimu kifasihi hufahamika kwa jina gani?

  1.              Kimai 
  2.               Tendi 
  3.              Wawe 
  4.             Kongozi

x.  “Mshua anaupiga mwingi” katika tungo hii neno anaupiga mwingi lililozuka hivi karibuni likimaannisha kitendo cha kufanya jambo vizuri zaidi linaweza kuingizwa kwenye aina gani ya misimu kati ya zifuatazo;

  1.              Misimu ya kitarafa 
  2.               Misimu zagao 
  3.              Misimu ya kihuni 
  4.             Misimu ya pekee

2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika orodha A na aina za nyimbo kutoka orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

Orodha A

Orodha B

  1.                    Husimuliwa kama mifano ya kuadiri watu 
  2.                  Husimulia chimbuko la asili ya kitu fulani 
  3.             Husimulia kwa nia ya kuchekesha na kukejeli
  4.             Husimulia kwa lengo la kuwaasa watoto 
  5.                  Husimulia kuhusu matukio ya kihistotia
  1.              Soga
  2.               Tarihi
  3.              Vigano
  4.             Visasili
  5.               Hadithi
  6.               Mizungu
  7.              ngano

 

SEHEMU B: (alama 70)

3. Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:

Kwa kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana sana na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo au mawazo tu bali pia katika mambo mengine mengi. Yote haya ni vielelezo vya jinsi kizazi cha leo kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha vizazi vilivyotangulia. Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao si ajabu katu kuwaona vijana wakiwa na mitindo mipya ya maisha yao. Kama vile, wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana ajabu na kudhihirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.

Watu wengi hufikiri kwamba maasi ya vijana wa leo yanayotokana na mambo lukuki, kama vile vishawishi, tamaa, kutaka maisha ya mkato na kupenda vitu vikubwa zaidi ya uwezo wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi hiki kisingelipotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao ambao wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama uaminifu, heshima kwa wazee ama wakuu, kukinai, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia kujitegemea. Mambo haya yote yamesahaulika ama yamepuuzwa katika utamaduni wa kisasa.

Swali lililopo ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au masharti gani? Tuwapime kwa mujibu wa hali ya duniani ya leo ama kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini ili lisije likaegemea upande wowote.

Ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaoathirika na hivyo hubadilika daima. Kwa kweli maendeleo ya elimu, sayansi na hata mawasiliano yameyageuza maisha ya siku hizi. Mathalan leo inawezekana vijana wa barani Afrika wakaona na hata kuzungumza na wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani wakiwa nyumbani kwao. Athari za filamu, video, vitabu, magazeti au majarida haikadiriki. Mambo hayo kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati wao. Isitoshe yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale wanayojifunza ni kweli. Matokeo yake yamekuwa ni wao kuudharau utamaduni wao wa asili na kuvutiwa na ule wa kigeni.

Hivyo wazazi wana wajibu mkubwa wa kuwaongoza na kuwasaidia vijana ili kuwa na uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi mwafaka katika maisha yao.

Maswali

a. Andika kichwa cha habari uliyoisoma, kisichozidi maneno matano

________________________________________________________________

b. Kwa nini kizazi cha leo kinadaiwa kuishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha vizazi vilivyotangulia?

________________________________________________________________________

______________________________________________________

c. Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa “maisha sio jiwe” lina maoni gani?

_______________________________________________________________________

______________________________________________________

d.  Bainisha jambo moja (1) linaloweza kusaidia kizazi cha vijana wa leo kisipotoke

________________________________________________________________________

________________________________________________________________________

e.  Toa mfano mmoja (1) unaoonesha namna maendeleo ya elimu, sayansi na mawasiliano yalivyoyageuza maisha ya vijana wa leo

__________________________________________________________________

__________________________________________________________________

 

4. Ni taarifa gani zinazohusu neno huingizwa katika kamusi? ( Taja tano )

i) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..... 

ii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iii) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

iv) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

v) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

5. Sentensi zifuatazo ni tata. Toa maana mbili kwa kila sentensi ili kudhibitisha utata huo

i) Masudi ameiba kanga

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

ii) Kaka amenunua tai

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

iii) Daktari aliniunga mkono

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

iv) Tausi amemwandikia mama yake barua

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

v) Juma alimpigia mwanangu mpira

a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

6. Sentensi zifuatazo zinabeba maan ya istilahii fulani. Zianishe istilahi hizo kwa kila sentensi. Mfano: Ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi “Mofimu”

  1. Ni aya ndogo kwenye kamusi ambayo huhusisha kidahizo na maelezo yake yote
  2. Ni sauti ambazo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti
  3. Ni mtindo wa lugha wa watu Fulani katika kazi maalumu   
  4. Ni maneno ambayo huonesha hisia za mtenda au mtendwa   
  5. Kamusi huandikwa kwa lugha moja   

7. Kila mhusika ana kazi yake katika kazi ya fasihi. Taja kazi moja moja ya wahusika wafuatao.

  1.               Fanani
  2.               Hadhira
  3.                Wanyama
  4.               Binadamu
  5.               Mahali

8. Toa tofauti tano (5) zilizo kati ya Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi.

LUGHA YA MAZUNGUMZO

LUGHA YA MAANDISHI

i.

 

ii.

 

iii.

 

iv.

 

v.

 

 

 

 

 

 

9. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:

“Wanangu chukueni vigoda mketi niwausie ya dunia, maana ya jana sio ya leo na ya leo sio ya kesho. Zama zetu hatukupata kumuona mwanamke akivaa kaptura wala bukta, pia hatukupata kumuona mwanaume katoga masikio wala kusuka nywele. Leo ni jambo la kawaida kuona hayo, tena hayo ni madogo kuna makubwa zaidi ya hayo.

Ukistajaabu ya Musa utaona ya Firauni. Binti yangu angalia sana mwanaume atakayekuoa. Unaweza kudhani umeolewa na mwanaume, kumbe ni mke mwenzio, kwako mumeo huko nje ni mke wa mtu.

Nawe kijana wangu sikuachi pakavu, kuwa makini na mwanamke utakayemuoa. Usije kuoa mwanamke ambaye ndani kwako ni mkeo lakini nje ni mume wa mtu.

MASWALI:

(i) Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyoisoma kisichozidi maneno matatu 

(ii) Toa maana ya maneno yafuatayo:

  1.               Vigoda
  2.               Kutoga 

(iii) Andika methali iliyotumika katika habari hii 

(iv) Mwandishi anazungumzia nini katika wosia wake?

(v) Mwandishi ana maana gani anaposema “Kwako mumeo huko nje ni mke wa mtu”.

 

 

 

SEHEMU C (Alama 15) 

10. Kwa hoja nne (4), fafanua hasara ambazo huweza kumkumba mtu yeyote asiyependa kushiriki mazoezi na michezo hasa kwa wanafunzi shuleni.

 

 

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 183  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 183  


OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

JAMHURI  YA MUUNGANO YA TANZANIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI

KIDATO CHA KWANZA

KISWAHILI 2023

  1. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali

Miaka ya hivi karibuni kumetokea ajali nyingi hapa duniani. Wengi tumesikia taarifa za ajali mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari na baadhi yetu tumeshuhudia kwa macho yetu ajali hizo. Kila aliyesikia au kuona ajali hizo alivaa uso wa huzuni kwani nyingi zilikuwa za kutisha

mno. Wapo watu walio katika miguu, mikono, masikio na hata kunyofokwa macho na wale walionusurika, wapo ndugu na marafiki zetu waliopoteza maisha. Wengi tulipata machungu yaliyo kithiri, tulilia, tulilaumu na kuwalaani wote tulio fikiria ndio walio sababisha ajali hizo.

Waliokufa katika ajali hizo ni watoto wadogo, watu wazima na hata vikongwe wanawake kwa wanaume. Kama ilivyo desturi, kifo hakibagui na kwa kweli huvuna roho za watu wa umri na jinsia zote.

Wazazi wengi wanao fariki katika ajali hizi huacha watoto ambao hawamo katika utaratibu wa kuendelezwa kielimu. Badala yao wanaingia katika utaratibu wa kujitafutia riziki badala ya kujisomea. Watoto wengi hufanya kazi za kubeba mizigo, uvuvi, kuchimba madini migodini,

vibarua mashambani, biashara ndogondogo na hata kazi za nyumbani.

Watoto hao walioachwa na matatizo mengi wafanyapo kazi katika sehemu hizo. Kwa kuwa wengi wao hawana upeo mkubwa wa mambo, hujikuta wakifanya kazi bila kufuata kanuni za kiafya. Hali hiyo huwasababishia magonjwa kama kifua kikuu na hata kupata ajali mbaya, wafanyapo kazi migodini, ambazo zinaweza kusababisha vifo au vilema vya maisha. Wengine huinginzwa kwenye biashara za ukahaba na kupata mimba zisizotarajiwa, tena katika umri mdogo. Wengine huambukizwa magojwa kama vile UKIMWI.

Pamoja na ukweli wa usemi kuwa “Ajali haina kinga”. Ajali nyingi zinatokana na makosa yetu wenyewe. Hizi tukiamua, tunaweza kuzizuia kwani penye nia pana njia. Hivyo hivyo suala la kuwapatia elimu watoto waloathirika na ajali liwe la kufa na kupona. Kama Taifa ni lazima tupige vita ajira kwa watoto, ikiwa kweli tunatakiwa kwenda na wakati vinginevyo tutabaki

nyuma.

Maswali

Andika herufi ya jibu sahihi katika maswali yafuatayo

i. Mwandishi anafahamisha kuwa wanaokufa kwa ajali ni......................................

  1. Watu wa aina zote
  2.  Watoto wadogo
  3.  Watu wazima
  4.  Vikongwe, wanawake na wanaume

ii. Ipi si kweli kuhusu maeneo wanako ajiriwa watoto?

  1. Kwenye machimbo ya madini
  2. Kwenye biashara ndogondogo
  3. Kazi za nyumbani
  4. Kwenye ofisi za serikali

iii. Ajira kwa watoto husababishwa na......................................

  1.              Kutokuwepo kwa shule za kutosha
  2.               Vifo vya wazazi na ugumu wa maisha
  3.              Kampeni za vyama vya siasa
  4.             Madeni ya nchi

iv. Ili watoto waweze kufanikiwa katika maisha yao ya badaye, lazima jamii...................

  1. Ipige vita rushwa
  2. Ifuate siasa ya ujamaa na kujitegemea
  3. Iwape watoto elimu
  4. Ijenge barabara nzuri

v. Moja ya haya yafuatayo sio ajali yakujitakia....................

A. Gari kuanguka kutokana na mwendo kasi

B. Kuzidisha uwezo wa uzito katika vyombo vya usafiri

C. Kuendesha vyombo vya usafiri pasipo kuzingatia kanuni na sheria

D. Kuzuka kwa vimbunga vinavyoleta maafa makubwa.

vi. Mwandishi anaamini kuwa tunaweza kuzuia ajali zisitokee kwa

A. Kuomba Mungu atuepushe na jali hata kama sheria na kanuni hazifuatwi

B. Kutoendesha magari katika barabara mbaya

C. Kuwa makini katika kuendesha vyombo vya usafiri

D. Kutowaruhusu wazazi wenye watoto kutumia vyombo vya usafiri

Vii. Kipi kati ya vifuatavyo chafaa kuwa kichwa cha habari uliyosoma

  1. UMUHIMU WA ELIMU
  2. VYOMBO VYA USAFIRI
  3. AJALI BARABARANI
  4. AJALI KWA WATOTO

Viii. Msemo huu una maana gani “Alivaa uso wa huzuni”

  1. Alikuwa na hasira 
  2. Alikuwa mchoyo
  3. Alikuwa mvivu
  4. Alitia huruma au alikuwa na masikitiko

ix. Kati ya misemo ifuatayo upi haukutumika katika habari

  1. Alivaa uso wa huzuni
  2. Anamkono wa birika
  3. Liwe lwa kufa na kupona 
  4. Penye nia pana njia

x. Habari hii ina aya ngapi?

  1. Moja
  2. Sita

C. Tano 

D. Tatu

2. Oanisha safu ya maneno A na B

ORODHA A

ORODHA

I. Maghani

II. Semi

III. Methali

IV. Lakabu

V. Rara

A. Ni hadithi fupi nyepesi ya kishairi yenye visa vya kusisimua; rara

huimbwa au kughanwa ikiambatana na ala za muziki

B. Hizi ni hadithi za mapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama,

miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha

C. Istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa

kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa.

D. Tungo au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au

mafunzo muhimu ya kijamii.

E. Semi fupi fupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo,

mazito yaliyotokana na uzoefu wa kijamii

F. Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa

au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au

kimatendo.

G. Usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili iufumbue.

H. Ghani ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa yenye uzito

kijamii au kitaifa.

 

3. Juma alibishana na Hassani kuwa kamusi haina maana na ni upotevu wa muda kusoma kamusi, Wewe kama mwanafunzi mtete hassani.

 

4. Kwa kuzingatia lafudhi na matamshi sahihi, bainisha maneno yenye makossa katika sentensi zifuatazo

a) Nimepata ujumbe wa simu wenye taarifa mbaya _______________

b) Ntoto wangu anaumwa ____________

c) Rafiki yangu naja ______________

d) Ama kweri elimu haina mwisho ________________

e) Kurara badara ya kutafuta kazi ya kufanya kunasababisha maisha kuwa

magumu _________________

5. Chunguza sentensi zifuatazo, kisha bainisha vivumishi vilivyotumika kwa kutaja ni aina gani ya kivumishi

a) Watu wachache waliumia ______________________

ii) Gari lao limegongwa natrekta _______________________

iii) Familia imemtakia la heri mtoto wao mpendwa __________________________

iv) Wanafunzi wachache wamechelewa darasani ____________________

v) Nyumba ngapi zimebomolewa na mafuriko ______________________

6. Eleza kwa kutoa mifano tofauti iliyopo baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi kwa kuzingatia vipengele vya umri, uhifadhi, uwasilishwaji, mabadiliko na umiliki.

7. Unapowasiliana kwa lugha ya kisahili ni muhimu kuzingatia mambo gani?

8. kihusishi ni moja kati ya aina za maeneno, onesha matumizi matano ya kihusishi ‘’kwa’’

9. Lugha hutumika kama chombo, zana, kifaa au njia ya kufikia lengo Fulani. Onesha kwanini lugha inatumika katika jamii

10. Wananchi wa kijiji cha Fungafunga wanasifika kwa utaalamu wa kuchonga vinyago kutokanana na uwepo wa misitu katika kijiji cha Fungafunga. Ukiwa kama Afisa misitu tumia hoja sita (6) kuwaeleza wananchi wa kijiji cha Fungafunga kuhusu umuhimu wa misitu kwa kutunga insha isiyozidi maneno 250 .

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 142  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 142  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI AUG 2021

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA                    MUDA : SAA 2:30

MAAGIZO

  1.            Mtihani huu una sehemu nne (04) A, B, C na D
  2.          Jibu maswli yote
  3.        Fuata maagizo ya kila sehemu na swali.
  4.        Andika majina yako matatu.
  5.          Mpangilio mzuri wa kazi uta zingatiwa

 

SEHEMU A (Alama 10).

UFAHAMU

  1.          Soma kwa makini habari ifuatayo kasha jibu maswali yanayo fuata;

Ugonjwa hatari wa UKIMWI umeenea kwa kasi sana katika nchi masikini  ikiwepo nchi ya Tanzania.Kuna sababu mbalimbali zinazo changia hali hii. Sababu kubwa ni umasikini .

   Wasichana na wanawake wengi hupenda kujiuza kama bidhaa sokoni ili wapate fedha ya kujikimu  katika maisha yao . Hufanya hivyo kwa kuji rahisisha kwa wanaume wenye bulungutu  la fedha.Wanawake hawa ujipeleka kwenye mabaa au kwenye vilabu vya pombe, wakisha kunywa na kuvaa miwani wote huingia katika ulimwengu mwingine ambako huanza kuambukizana virusi vya UKIMWI.

      Sababu nyingine ni raha na starehe ambayo watu wengi huifurahia.Hufanya hivyo ili kujistarehesha wao wenyewe . Hutumia miili yao kama sehemu ya burudani katika maisha yao. Hukumbatiana ili kujisahaulisha taabu na misukosuko katika maisha.

  Sababu nyingine ni ukosefu wa elimu juu ya ugonjwa huu, watu wengi hawajafundishwa adhari za ugonjwa huu kwa jamii . Hivyo hawa jui maana ya UKIMWI,wao hufikiri kwamba UKIMWI ni ndoto na hakuna ugonjwa wa aina hii hali hiii imesababisha baadhi ya vijana ………..

    Njia zinazo eneza ugonjwa huu ni nyingi nikitaja nitaonekana  mmbea kwani kila mmoja anazifahamu.Athari za UKIMWI katika jamiii nikama vileb kifo,kushuka kwa shughuli za uzalishaji mali n.k.

 

MASWALI

  1.            Eleza maana ya maneno yaliyo pigiwa mstari.
  1.           ……………………………………………………………………………………………………
  2.          ……………………………………………………………………………………………………
  3.           ………………………………………………………………………………………………….
  4.          ……………………………………………………………………………………………………
  5.           ……………………………………………………………………………………………………
  1.             Ni kwa vip UKIMWI huchangia kushuka kwa shughuli za uzalishaji mali?.........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  2.           Taja sababu nne zinazo eneza ugojwa wa UKIMWI
  1.              ……………………………………………………………………………………………….
  2.          ……………………………………………………………………………………………….
  3.                 ……………………………………………………………………………………………..
  4.                                                                                                                                                                                                                                  ……………………………………………………………………………………………….
  1.           Fafanua sababu kuu inayo changia kuenea kwa ugonjwa huu katika nchi masikini kama Tanzania………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
  2.          Andika kichwa cha habari kisicho zidi maneno matano(05)

……………………………………………………………………………………………………….

SEHEMU B (Alama 20)

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

  1.                 (a)  Taja mambo makuu manne(04) ambayo yana jenga lugha.
  1.               ………………………………………………………………………………..
  2.             ………………………………………………………………………………………
  3.              ………………………………………………………………………………………..
  4.               ……………………………………………………………………………………….

b.  Lugha ni chombo muhimu sana katika jamii. Nini umuhimu wake katika jamii?

  1.               ...........................................………………………………………………………..
  2.                ………………………………………………………………………………………………………
  3.              ……………………………………………………………………………………………………..
  4.               ………………………………………………………………………………………………………..
  5.              ………………………………………………………………………………………………………..

c. Eleza maana ya dhana zifuatazo;

  1.            Ufasaha……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2.                Mawasiliano………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  3.              Lugha…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  4.           Matamshi sahihi ……………………………………………….......................................................................................................................................................
  5.          Lugha fasaha …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

SEHEMU C (Alama 20)

SARUFI

  1.          a) Taja matawi manne (04) ya sarufi;
  1.            ……………………………………………………………..
  2.          …………………………………………………………….
  3.        ……………………………………………………………………
  4.        ……………………………………………………………….

b) Tunga sentensi kwa kutumia  vipashio vifua tavyo

  1.                  mfano; N+t+N=  Mtoto   ni    Mgonjwa  

                                 N        t          N

  1.              N+V+E=…………………………………………………………………………………
  2.          W+TS+T+E=…………………………………………………………………………..
  3.           N+t+N+V=……………………………………………………………………………
  4.          H+N+T=………………………………………………………………………………..

 

SEHEMU D (Alama 50)

                                   FASIHI KWA UJUMLA

  1.          a) Taja sifa tano (05) za faihi simulizi
  1.            ……………………………………………………………………………………………………..
  2.          …………………………………………………………………………………………………….
  3.        ……………………………………………………………………………………………………..
  4.        …………………………………………………………………………………………..
  5.          ……………………………………………………………………………………………..

b)  Eleza maana ya maneno yafuatayo

  1.                  Maigizo …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  2.                Sanaa ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  3.              Methali …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  4.               Fasihi…………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  5.                 Majigambo…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

c) Taja vipengele vitano (05) muhimu vya fasihi simulizi.

  1.                  ……………………………………………………………………………………………………
  2.                ………………………………………………………………………………………………
  3.              ……………………………………………………………………………………………………
  4.               …………………………………………………………………………………………………..
  5.                 …………………………………………………………………………………………………..

d) Kamilisha methali zifuatazo

  1.                Mgaagaa na upwa………………………………………………...................
  2.                Dua la kuku halimpati mwewe……………………………………………..
  3.                Kizuri cha jiuza …………………………………………………………………….
  4.                Heri nusu shari……………………………………………………………………
  5.                Usimlaumu dobi………………………………………………………………..

e) Taja vipengele vitano vya fani

  1.                …………………………………………………………
  2.                ……………………………………………………….
  3.                ………………………………………………………..
  4.                ………………………………………………………….
  5.                …………………………………………………………..

FASIHI SIMULIZI

FASIHI ANDISHI

  1.                                                                                                                                                                                                                                    

  1.                                                                                                                                                                                                                                  

ii

  1.                                                                                                                                                                                                                                

iii

  1.                                                                                                                                                                                                                                

iv

  1.                                                                                                                                                                                                                                   

V

f) Taja tofauti tano (05) kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi

 

 

 

 

                                                                                                                                                                                         

                            

1 | Page

 

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 70  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 70  

THE PRESIDENT'S OFFICE

MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT

AUGUST-SEPTEMBER   EXAMINATION SERIES

KISWAHILI

2020

TIME: 2:30 HRS

SEHEMU A

1.  Soma hadithi ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:

Katika nchi ya ughaibuni kulikuwa na mfalme mwenye dharau na maringo sana, aliwaona wananchi wake kama wajinga. Watu wake waliishi bila amani na walichukia vitendo vya mfalme wao. Mfalme huyo alikuwa anajigamba kuwa yeye ni tajiri kuliko wafalme wote katika nchi za jirani. Kwa ujumla mfalme huyo alikuwa mnyanyasaji na mwenyekebehi nyingi.

imageimageMfalme alikuwa mwenye kufuru sana, hata alidiriki kutamka kwenye mkutano wa hadhara kuwa hajawahi kuona njaa. Mzee mmoja mwenye busara aitwaye Bwana Adili alimwambia mfalme kuwa asihofu atampeleka mahali njaa inakopatikana. Bwana Adili kwa kukubaliana na mfalme walipanga siku ya safari ya kwenda kumwonesha mahali ilipo njaa. Safari hiyo ilikuwa na masharti kuwa hakuna kula chochote asubuhi na hakuna kubeba masurufu yoyote yakiwemo maji, ingawa Bwana Adili kwa ujanja wake alibeba.

Safari ilianza asubuhi mapema huku mfalme akiwa na furaha kubwa ya kwenda kuona njaa. Walitembea mwendo wa saa zisizopungua ?ita, mfalme akawa amechoka sana akamwomba Bwana Adili wapumzike. Uchovu huo imageulitokana na ukweli kwamba mfalme hakuwahi kwenda mwendo mrefu kwa miguu. Wakati wa mapumziko mfalme alimwomba Bwana Adili maji na mkate lakini Bwana Adili alimnyima, walipumzika kwa muda wa saa moja na safari ikaendelea. Ilipofika jioni mfalme alikuwa amechoka kabisa kwani mwendo ulikuwa mrefu na njaa ilimuuma mno. Walipumzika chini ya mti, mfalme alimuuliza Bwana Adili, mbona hatufiki safari yetu? Bwana Adili hakumjibu chochote bali alichukua mkate akala na kunywa maji, mfalme alihisi njaa kali, alimwomba Bwana Adili mkate na maji lakini alimnyima.

Hali ya mfalme ilizidi kuwa mbaya sana, ndipo Bwana Adili akamwambia nitakupa maji na mkate ule lakini uahidi kwa maandishi kuwa utaacha dharau na majivuno kwa watu. Mfalme alipiga magoti mbele ya Bwana Adili na kuchukua karatasi na kalamu aliyopewa na Bwana Adili na kuahidi kwa maandishi kuwa ataacha kabisa tabia ya dharau na majivuno. Bwana Adili alipokea maelezo ya mfalme na akampa mkate na maji. Mfalme alipomaliza kula alimshukuru sana, ndipo Bwana Adili alipomgeukia mfalme na kumweleza kuwa hakuna maskani ya njaa bali hali aliyokuwa nayo mtu asipokula chakula. Waliporudi mfalme aliitisha mkutano wa hadhara. aliwaomba radhi wananchi wake na tangu siku hiyo mfalme aliishi kwa upendo na wananchi wote.

Maswali

(a)(i)     Bwana Adili alitoa masharti gani ya safari?.........................................

(ii)    Kwa nini Bwana Adili alitoa masharti uliyoeleza katika kipengele

(b)     Toa methali moja inayolingana na fundisho linalopatikana katika hadithi uliyosoma.

(c)     Toa maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika hadithi uliyosoma:

(i)Anajigamba ..................

(ii)Kebehi .....................

(iii) Kufuru ..................

(iv)Masurufu . .......................

 (v) Maskani....................

(d)     Andika ufupisho wa habari uliyosoma kwa maneno 60.

SEHEMU B

MATUMIZI YA LUCHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Andika kwa usahihi maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumka katika tungo zifuatazo:

(i) Mashirikiano ni muhimu kwetu .................

(ii) Mimi ni mwanainji wa Tanzania ...............

(iii)Mama anakaaga jikoni anapopika ............

(iv) Hakuna mapungufu yaliyojitokeza ........

(v) Hajafika mwanafunzi yoyote leo ..................

(vi) Huyu ni rafiki angu.................................

(b)     Eleza maana mbili kwa kila tungo.

(i) Mama anaota.

(ii)Tafathali nipe sahani ya kulia.

(iii)Vijakazi wanalima barabara.

(iv)Amekanyaga mtoto.

(v) Shangazi anawachezea wanangu.

(c)     Andika KWELI kama sentensi ni sahihi au SIO KWELI kama sentensi si sahii
 (i) Tafadhali mpikie ugali. Hii ni tungo tata .........

(ii) Kifaa kinachotumika kulia chakula kiitwacho uma wingi wake ni uma ... ... ...

(iii) Rejesta ni misimu ya Kiswahili . 

(iv) Amekula chumvi nyingi. Hii ni nahau 

(v) Mbili kutwa mara tatu. Ni rejesta ya kujifunza hesabu ........

SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Nyumbua maneno yafuatayo na kuunda maneno manne kwa kila neno:

(i) Angalia ... ... ...

(ii)Chukua ...............

(iii)Oga ... ... ...

(iv)Kata . . ................

(v)Omba ... ... ..........

(b) Tumia maneno yafuatayo kama nomino na utunge sentensi moja kwa kila neno:

(i) Starehe . ..............

(ii) Ukweli .........

(iii)Utaalamu ...... .. 

 (iv) Umoja ... ... ...

(v) Uzembe ...........

(vi) Ukarimu .... ..... image

(viii) Upweke .. .....

(vii) Ushujaa . .........

(ix) Upendo ... ... ...    

(x) Furaha . .............

(c) Kitenzi kikuu huweza kutumika sambamba na kitenzi kingine kukamilisha sentensi. Katika sentensi zifuatazo bainisha vitenzi vilivyotumika. Sentensi ya kwanza ni mfano:

(i) Aliyekuja atasafiri kesho.

(ii) Mgeni wangu amekwisha kuwasili.

(iii) Amina hakutaka kumuudhi.

(iv)Mafundi wangali wanashona viatu. image

(v)Wataendelea kumsubiri hadi kesho.

(vi) Gari lilikuwa limeharibika mlimani Kitonga 

SEHEMU D : FASIHI SIMULIZI

4.Eleza kwa kifupi maana ya dhana zifuatazo:

(i) Maigizo 

(ii) Semi ......... 

(iii) Tarihi .

(iv) Majigambo ..........

(v) Mizani . . . . . . . ..

(b) Jaza nafasi iliyoachwa wazi kukamilisha methali zifuatazo:

(i)Hamadi kibindoni ... ... ...

(ii).. ......yasiyokuwa ncha.

(iii)......... si mwisho wa uhunzi.

(iv)Mwenye shibe .............

(v)......... embe tunda la msimu.

(c) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Kweli kito mahabubu, Muweza mjaze kweli,

Kweli siriya ajabu, huwapa watufadhili,

Kweli chimbo la dhahabu, linahimili kweli,

Kweliyajambo hekima, na mifanoya akili.

Kweli nguvuya imani, moyoni muwe na kweli,

Kweli kitu cha thamani, fahariyetu ni kweli,

Kweli itupe makini, tutoe majibu kweli,

Kweli kwa mtu ni tija, woga huvunjwa na kweli.

Kweli huniadabisha, utu huletwa na kweli,

Kweli hunielimisha,jinsiya kuwa kamili,

Kweli hunipa maisha,ya mwangaza wa kandili,

 Kweli haina kiwango, manufaa yake kweli.

Kweli katika baraza, maongeziyawe kweli, 

Kweli au hupendeza,zamaza kujibu swali, 

Kweli itakuongoza, uweze kufanya kweli,

Kweli huwa mfaulu, katika pambono kali.

Kweli leo iwe pambo, upambile kweli kweli,

Kweli ikujaze mambo,yoteyaliyoya kweli,

Kweli ikupe kiimbo, chenye majibu ya kweli,

Kweli tatua mafumbo, uwemahiri wa kweli.

Kweli hapa kaditama, ni mimi mtunzi kweli, Kweli ikujaze mema, ufaulu kweli kweli, Kweli itakupa chema, Kidato cha tatu kweli, Kweli mhimili wako, pokea kwa dhati kweli.

MASWALI

(i) Mtunzi wa shairi hili anatoa ujumbe gani?

(ii)Katika ubeti wa pili mshairi anasisitiza jambo gani?

(iii)Bainisha kina bahari katika shairi ulilosoma.

(iv) Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi ulilosoma huitwaje? Toa sababu moja. (v) Mshairi ana maana gani anaposema," Kweli mhimili wako, pokea kwa dhati kweli."

(vi) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma.

  •   Mahabubu
  •    Fahari            
  •    Kandili
  •    Zama
  •     Mahiri

SEHEMU E 
 UANDISHI WA INSHA/UTUNGA)I

5. Andika mazungumzo au dayalojia kati ya mzazi na mwanawe juu ya rnatokeo ya mtihani wa muhula yasiyoridhisha ukilenga mzazi kutoa ushauri wa jinsi ya kupata ufaulu bora muhula unaofuata.

Mzazi: ............................................................................... 

Mtoto: ................................................................................

Mzazi: ............................................................................... 

Mtoto: ................................................................................

Mzazi: ............................................................................... 

Mtoto: ................................................................................

Mzazi: ............................................................................... 

Mtoto: ................................................................................ 

Mzazi: ............................................................................... 

Mtoto: ................................................................................

 

 

 

 

 

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 24  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 24  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256