JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA UPIMAJI – KISWAHILI
KIDATO CHA NNE- MACHI 2024
Muda : Saa 3
Maelekezo
SEHEMU A (ALAMA 16)
Orodha A | Orodha B |
|
|
SEHEMU B
ALAMA 54
(b) bainisha mzizi katika maneno ya sentensi zifuatazo (vitenzi)
“Ndugu wazazi kumbe safari yenu inahusu harusi ya Zaituni?”. Mkuu wa shule aliwauliza wazazi, “Ndiyo”, wazazi walijibu kwa pamoja bila aibu. “Inategemewa kufungwa lini”?. Mkuu aliendelea kuhoji.
“Harusi hii ilikua ifanyike wakati Zaituni alipofika kidato cha nne, lakini Zaituni huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa na kijiji kizaima na kudharauliwa na kila mtu. Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha, hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishe. Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii”. Mzee Abdalah aluelezea. Muda wote huu mkuu wa shule alikua akimtazama mzee kwa chati sana. Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi “ Zaituni ana kiburi kumbe?”
Mama Zaituni hakutaka hilo limpite, himahima akatoa maelezo yake “ Mama wee, Zaituni usimwone hiivi, Zaituni manangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuoelewa. Zaituni ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haioni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na Elimu mliyompa”. Mtoto sasa ameharibika, anafanya apendavyo. Hii Elimu gani isiyojali adabu wala utii? Mama Zaituni alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka.
Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya mwisho. Alikwisha tambua kwamba wazazi wa Zaituni walikua wameachwa nuuma na wakati. Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.
Maswali
SEHEMU C
ALAMA 30
Jibu maswali mawili kutoka katika sehemu hii
ORODHA YA VITABU.
USHAIRI.
Wasakatonge – M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya – TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya ChekaCheka T.A. Mvungi (EP&D LTD)
RIWAYA
Takadini – Ben J Henson (MBS)
Watoto wa Mama Ntilie – E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu – A. J. Safari (H.P )
TAMTHILIYA
Orodha – Stebe Reynolds (M.A)
Kilio Chetu – Medical Aid Foundation (TPH)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe – E. Semzaba (ESC)
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 181
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 181
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
MUDA: SAA 3:00 MACHI : 2023
MAELEZO
SEHEMU A (alama 15)
Jibu Maswali yote Katika sehemu hii
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia.
(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza hisia za mtenda au mtendwa
(ii) Lahaja ya kimtang’ata huongelewa sehemu gani ya Pwani ya A.Mashariki?
(iii) Kategoria ya kisarufi inayowakilisha wakati katika kitenzi.
(iv) Zifuatazo ni dhima za picha na mchoro katika kamusi isipokuwa ipi?
(v) Ipi ni maana ya nahau “mbiu ya mgambo” kati ya maana hizi hapa chini.
(vi) Upi ni mzizi wa neno anakula?
(vii) Mama Zita anakuja” Tungo hii ni tata, utata huo umesababishwa na nini?
(viii) Kwa vipi ngonjera ni igizo?
(ix) Kifungu cha maneno ambacho hujibu maswali ya ziada kuhusu tendo katika sentensi huitwa. _______________
(x) Ili mzungumzaji wa lugha aweze kuwasiliana kwa usahihi anahitaji mambo manne ambayo ni _______________
2. Oanisha dhana zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B. kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.
ORODHA A | ORODHA B |
(i) Hatua ya kwanza ya uchanganuzi wa sentensi (ii) Kanda (iii) Shamirisho (iv) Mofimu ni kiambishi (v) Wingi wa shule |
|
SEHEMU B. (Alama 40)
Jibu maswali yote
3. Uteuzi mzuri wa maneno ni lazima uzingatie unaongea nini unaongea na nani? unaongea wapi? Na kwa nini? Eleza kwa ufupi hoja nne.
4. Andika methali inayohusiana na mambo yafuatayo.
5. (a) Sentensi zifuatazo zinamakosa kisarufi ziandikwe upya kwa usahihi.
(b) Kwa kutumia mifano, andika miundo mine (4) ya sentensi shurutia.
6. Wewe na msaidizi wako mmehudhuria kikao cha kupanga mahafali ya kumaliza kidato cha nne. Andika kumbukumbu ya kikao kilichofanyika katika shule kilichokuwa na wajumbe nane.
7. Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili, umepitia vipindi vingi tofauti, fafanua kwa mifano mambo manne (4) yaliosaidia kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru.
8. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yafuatayo:
Nchi ya Tanzania hufanya uchaguzi wake kila baada ya miaka mitano, uchaguzi mkuu huhusisha uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani. Octoba 2020 watanzania wote walikuwa katika pilikapilika za kuwapata viongozi wa kuwawakilisha katika matatizo yao.
Mtanzania aliyekuwa huru kuchagua viongozi wake alitakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-
Awe amejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, awe na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea, awe raia wa Tanzania na awe na akili timamu.
Uchaguzi ulifanyika kwa amani, wananchi waliweza kuelemishwa kupitia vyombo vya habari kama redio, magazeti, Runinga pamoja na majarida. Kwa kutumia vyombo hivyo vya habari zilifika sehemu zote za nchi yaani mijini na vijijini, kila mtanzania alijua uchaguzi ni muhimu kwake kwani hutupatia viongozi bora kuendeleza demokrasia, kuleta mabadiliko nchini na kutatua migogoro mbalimabli katika jamii pamoja na kuondoa ubaguzi. Watanzania tushikamane kuendeleza amani nchini.
MASWALI:
SEHEMU ‘C’ Alama (45)
Jibu maswali matatu tu kutoka sehemu hii
9. Umealikwa kwenda kuelimisha jamii yako juu ya “madhara ya mapenzi katka umri mdogo”. Tunga mchezo mfupi wa kuigiza usiozidi maneno (300) mia tatu kuhusu mada hiyo.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
RIWAYA
TAMTHILIA
10. Mashairi siku zote hukemea uonevu katika jamii. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja 3 kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizo soma.
11. Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma, fafanua namna ambavyo waaandishi wametumia kipengele cha mtindo kuumba kazi zao. Eleza hoja tatu kwa kila kitabu.
12. Kwa kutumia hoja tatu kutoka kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma. Jadili kufaulu kwa mwandishi katika kipengele cha matumizi ya lugha.
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 138
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 138
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
MUDA: SAA 3:00 APRILI: 2022
MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, na D
2. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
3. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi.
4. Jibu maswali yote katika sehemu A, B, C na maswali matatu sehemu D, swali la tisa ni lazima.
SEHEMU A (Alama 10)
1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herefu ya jibu hilo.
i) Ni jambo gani linalodhihirisha umbo la nje ya kazi ya fasihi?
ii) Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
iii) leta wali kuku.hii ni aina gani ya rejista?
A. Rejesta ya Hotolini
B. Rejesta ya Hospitalin
C. Rejesta ya Mtaani
D. Rejista ya Shambani
iv) Ipi maana inayoelekeana na methali hii? ‘chanda chema huvikwa pete’
v) ..........ni hadithi zinazozungumzia matukio ya kihistoriya.
vi) Mara nyingi fasihi simulizi huzingatia uwepo wa;
vii)Upi ni mzizi wa neno anakula?
viii)Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi Fulani ya kifasihi?
ix) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
x) Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi?
SEHEMU B (Alama 5)
2. Oanisha sentensi za kifungu A, kwa kuchagua jibu sahihi katika kifungu B, andika jibu lako kwa usahihi katika kisanduku ulichopewa hapo chini;
KIFUNGU A | KIFUNGU B |
|
|
KIFUNGU: A | I | II | III | IV | V |
KIFUNGU B |
|
|
|
|
|
SEHEMU C: ALAMA 40
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.
4. Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni kielezi cha aina gani?
i) Darasani kuna utulivu mkubwa.
ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.
iii) Mwalimu amerudi tena.
iv) Nitaondoka wiki ijayo.
5. Toa maana tano (5) za neno “Kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana ulitoa.
6.Taja njia nne (4) zitumikazo kuunda misamiati na utoe mfano kwa kila njia.
7. Taja aina mbili za Mashairi na maana zake.
8. Soma shairi lifuatalo kisha jibu sehemu hii.
Utu wa binadamu, ni kama yai na kuku,
Utu niile nidhamu, mola aliyo mtunuku,
Ubinadamu ni damu, ya utu wa kila siku,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
Yeyote mwanadamu, ana asili ya mtu,
Yaani kwenye yake damu, hakikosi hiki kitu,
Utu sifa maalum, ya mtu kuitwa mtu,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
Utu ni kiumbe hai, tunacho chaonekana,
Utu kamwe haudai, tabia ya kujivuna,
Utu ni ule uhai, ushikao uungwana.
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake
Utu unayo aibu, na tabia ya muhali,
Utu huenda na jibu, kila imani na ukweli,
Utuwe hauna tabu, tabia ya ujalili,
Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.
MASWALI
SEHEMU D (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii swali la 9 ni lazima
9. Ukiwa kiongozi wa michezo katika shule ya Sekondari Kizota S L P 30 Dodoma, andika barua kwa mkuu wako wa shule kupitia kwa mwalimu wa michezo kuomba kuongezewa siku za michezo shuleni. jina lako liwe Siku njema Afya.
10 “Msanii ni kinda la jamii husika anayoandika kuihusu jamii hiyo”. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa.
11. “Wahusika katika kazi za fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila mhusika kutoka katika tamthilliya mbili zilizoorodheshwa.
12.Elimu ni ufunguo wa maisha. Fafanua kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kati ya vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A.Mvungi (EP & D.LT.D)
RIWAYA
Takadini Ben J. Hanson (Mbs)
Watoto Wa Mama N’tilie E. Mbogo (H.P)
Joka La Mdimu A.J.Safari (H.P)
TAMTILIYA
Orodha Steve Reynolds (Ma)
Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe E.Semzaba (Esc)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (Tph)
1
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 80
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 80
OFISI YA RAIS
WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULU- MACHI-2020
KISWAHILI
SEHEMU A (Alama 10)
UFAHAMU
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata;
Nchi yetu ya Tanzania imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko ulaya.
Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi ya chanikiwiti na maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha. Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya manjano na kisha yakawa mviringo.
Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa meusi ambamo wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata watundu kama tumbili na kima huonekana humo.
Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kujali wapita njia.
Zaidi ya pwani zetu, watalii huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa wanyama katika mbuga zetu huwa na ngozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru, utadhani amekasirika na kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote.
Basi mambo kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu. Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.
Maswali
2. Fupisha habari ulioisoma kwa maneno yasiozidi arobaini (40)
SEHEMU B (Alama 25)
SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. (a) Eleza maana ya utohoaji.
(b) Maneno yafuatayo yametoholewa kutoka lugha gani.
4. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.
5. (a) Eleza maana ya urejeshi katika kitenzi.
(b) Tunga sentensi tatu zinazoonesha urejeshi wa:
6. Bainisha tabia za maumbo yaliyokolezwa wino katika vitenzi ulivyopewa.
7. (a) Eleza maana na dhima ya kiunganishi katika sentensi.
(b) Tunga sentensi mbili kwa kila kiunganishi kifuatacho;
8. Jifanye kuwa mfanyabiashara wa mchele na unataka kuitangaza biashara yako nje na ndani ya nchi. Andika tangazo kuhusu biashara hiyo na jina lako liwe Pera Mlavi.
SEHEMU C. (Alama 45)
FASIHI KWA UJUMLA
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
ORODHA YA VITABU:
USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatiby (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya ChekaCheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9. “Waandishi wa tamthiliya wameshindwa kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa.” Kanusha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kotoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
10. “Mshairi ni mwalimu wa viongozi wa nchi.” Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ilizosoma.
11. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 4
FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 4