FORM ONE HISTORIA MIDTERM EXAMS

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUMALIZA NUSU MUHULA KIDATO CHA KWANZA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI 2025

MUDA 2:30

MAELEKEZO

1. Karatasi hii Ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi 10

2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa 

3. Sehemu A na C Zina alama kumi na Tano (15) Kila na sehemu B Ina alama sabini (70)

4. Zingatia maelezo ya Kila sehemu na ya Kila swali 

5. Andika jina lako juu ya karatasi hii.

 

SEHEMU A. Alama 15

1. Chagua jibu sahihi kutoka machuguzi uliopewa kwa vipengele (i)- (x) kasha andika jibu lake katika nafasi uliopewa.

i) Somo la historia ya Tanzania na maadili linaundwa na dhana kuu mbili nazo ni

  1. Historia ya Tanzania na maadili
  2. Historia kuhusu mambo au matukio yaliyopita
  3. Historia ya Tanzania na Tehama
  4. Historia ya Tanzania na utu

 ii) Ni miongozo inayotawala tabia na matendo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla. dhana hii imebebwa na neno

  1. Maadili
  2. Huruma
  3. Tanzania
  4. Historia

iii) Neno maadili linapotumika huweza pia kuashiria au kuimarisha Tunu za jamii au taifa ni zipi Kati ya zifuatazo

  1. Uhuru na Amani
  2. Amani na furaha
  3. Furaha na unyenyekevu
  4. Unyenyekevu na upendo

vi) Tunaweza kuwakaribisha wageni kwa furaha na kuwapa heshima kubwa ikiwa pamoja na kukirimiwa kwa 

  1. Chakula na malazi
  2. Chakula na malezi
  3. Chakula na kuoga
  4. Chakula na heshima

v) Mazingira ya kiliografia yanaweza kuathiri shughuli za binadamu kama vile 

  1. Biashara,utamaduni,kilimo na uhamaji wa watu
  2. Biashara,uchumi,siasa, na mazingira
  3. Uchumi,jamii,uvuvi, na uwindaji
  4. Uwindaji,ukusanyaji,ulinzi na mazingira

vi) Kwa kutumia uchambuzi wa makabila Tanzania ni nchi yenye makundi ya makabila yote yanayopatikana barani Afrika makundi hayo ni

  1. Wabantu ,wakichembe,wakushito na wanilo
  2. Wabantu,wangoni,wamakonde na wazaramo
  3. Wakichembe,Wabantu,wahaya na wanyakyusa
  4. Wanilo,wakushito,wakichembe,na wapemba

vii) Kihistoria kundi kubwa la tatu la watanzania ambalo ni jamii ya wafugaji walioingia nchini Tanzania wakitokea kusini mwa sudani ni 

  1. Wabantu
  2. Wanilo
  3. Wakushito
  4. Wakichembe

viii) Jamii za wakushito zinahusisha makabila kama 

  1. Wairaki,wagorowa, na waburugi
  2. Wamasai,wapare na Wairaki
  3. Wameru,Wamasai na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga, na Wairaki

ix) Kwa hapa Tanzania jamii za Wanilo ni kama 

  1. Wamasai,wajaluo, na wadatoga
  2. Wamasai Wairaki, na wadatoga
  3. Wadatoga,wajaluo na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga na Wairaki

x) Morani ni kundirika katika jamii ya kimasai la vijana wenye umri Kati ya miaka

A) 18 na 35

B)18 na 40

C)18 na 60

D) 18 na 80

 

2. OANISHA JIBU LA ORODHA 'A' NA JIBU LA ORODHA 'B'

ORODHA A

ORODHA B

  1.                     Wakichembe
  2.                   Wanilo
  3.                 Wabantu
  4.                 Mitala

 

  1. Hutumia lugha ya kugongagonga ulimi
  2. Wairaki na wagorowa
  3. Wadatoga na Wamasai
  4. Wahadimu,watumbatu na wapemba
  5. Ndoa za wake wengi

 

 

SEHEMU B. Alama 70

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Mkude ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wavulana buingu . Ameshindwa kuelewa maana ya maneno yafuatayo kwenye somo la historia ya Tanzania na maadili. Msaidie kumuelezea maana ya maneno hayo.

a) Tunu za taifa

b) maadili

c) Jiografia

d) Jamii

e) wajibu

4. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkondo A waelezee wanafunzi wenzako umuhimu wa kuwa na maadili katika jamii na taifa kwa ujumla.

5.Warioba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza alichaguliwa na jamii yake kuelezea namna ambavyo vijana wanaweza kujengwa kwa kuwa na tabia njema. Msaidie warioba katika kuwaeleza vijana vitu vinavyojenga tabia njema katika jamii zetu nukta Tano.

6. Ukiwa Kama mwanafunzi kutoka shule ya sekondari chekeleni. waelezee wanafunzi wenzio kwanini jamii za Asili ya kitanzania zilihama kutoka eneo Moja kwenda eneo jingine nukta Tano

7. Kwa kutumia nukta Tano tofautisha jamii za Asili za wakichembe na jamii za Asili za kibantu.

8. Kwa kumtumia mtaalamu "EMILE DURKHEIM" (1884) Toa dhana ya neno 'Jamii'

9. Eleza Tofauti iliyopo Kati ya maadili yaliyojengwa katika jamii za Asili na jamii za sasa za kitanzania

SEHEMU C Alama 15

Jibu swali la kumi

Bainisha changamoto za kukuza maadili katika jamii unamoishi na Kisha toa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua.

 

 

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256