FORM THREE KISWAHILI ANNUAL EXAMS

 

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI

KISWAHILI

KIDATO CHA TATU

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3                                                       2024 OCTOBER

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11). 

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima 

3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B ina alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30)

4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali

5. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha Mtihani. 

6. Andika Namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia. 

 

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika kipengele (i) – (x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia. 

 

(i) Mshititi Dkt. Yahya A. Sovu alialikwa kwenye Kongamano la Wanaisimu lililofanyika katika Viwanja vya Nyamagana. Katika kongamano hilo aliwasilisha mada ya “Uchanganuzi wa sentensi”, ambapo alibainisha hatua na vipengele vyote vya uchanganuzi wa sentensi kwa kutumia mikabala husika. Je, katika uwasilishaji wake kipengele cha “Chagizo” alikitaja kutumika katika mkabala gani? 

A. Kisintaksia 

B. Kiupatanishi 

C. Kisasa 

D. Kimapokeo 

E. Kimuundo 

 

(ii) Wanaopewa kazi ya kujenga ndio hao hao wanaobomoa badala ya kujenga. Kwa kupitia riwaya ya Joka la Mdimu ni mhusika gani mwenye sifa hiyo? 

A. Shiraz Bhanj 

B. Brown Kwacha 

C. Cheche 

D. Amani 

E. Tino 

 

(iii) Lipi kati ya maandiko yafuatayo huandikwa kwa lengo la kueleza mahitaji mbalimbali kwa mtu anayehusika? 

A. Kumbukumbu za mikutano 

B. Risala 

C. Hotuba 

D. Barua 

E. Insha 

 

(iv) Pamoja na kujifunza darasani maana na aina za lahaja bado rafiki yako Oko ameshindwa kubainisha ni wapi lahaja ya Kimtang’ata inazungumzwa katika jumuiya ya watu wa Pwani ya Afrika Mashariki. Msaidie kubaini sehemu inayozungumzwa lahaja hiyo. 

A. Kaskazini mwa Tanga 

B. Kaskazini mwa Mafia 

C. Kaskazini mwa Unguja 

D. Kaskazini mwa Lamu 

E. Kaskazini mwa Somalia 

 

(v) Usomaji upi husaidia kupima uwezo wa kutamka maneno kwa ufasaha na kutumia lafudhi ya lugha husika? 

A. Kusoma kwa makini 

B. Kusoma kwa ziada 

C. Kusoma kwa sauti 

D. Kusoma kwa burudani 

E. Kusoma kimya 

 

(vi) Mdogo wako wa Kidato cha Pili amepewa kazi ya kutunga hadithi, mwisho wa hadithi hiyo ni “Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.” Je, hiki ni kipera gani cha hadithi? 

A. Tarihi 

B. Soga 

C. Visasili 

D. Ngano 

E. Vigano 

 

(vii) Wanafunzi wenzako wa kidato cha Nne wanabishana juu ya sifa za tangazo rasmi. Tumia maarifa uliyoyapata kwenye mada hiyo kumaliza ubishani huo kwa kubainisha ipi si sifa ya tangazo hilo. 

A. Hutolewa baada ya kuratibiwa na mamlaka 

B. Hutolewa kwa kufuata taratibu maalumu 

C. Hutolewa na kubandikwa siku maalumu 

D. Hutolewa na mashirika ya serikali, binafsi au dini 

E. Hutolewa kwenye maeneo maalumu 

 

(viii) Mauja alimwambia Mabala “Ili uwe mahiri wa lugha ya mazungumzo huna budi kuwa mtumwa huru katika lugha husika.” Ukiwa kama mtaalam wa lugha ya Kiswahili Mauja anamaanisha nini kwa Mabala? 

A. Mabala azingatie muundo, misimu na mitindo ya lugha 

B. Mabala azingatie mandhari, ujumbe, dhamira na mada 

C. Mabala azingatia umri, mada, muktadha na muundo 

D. Mabala azingatie mada, lengo, muktadha na uhusiano 

E. Mabala azingatie, lengo, rika, muundo na mila 

 

(ix) Makundi ya ngeli za Nomino hayatofautiani na makundi ya matunda sokoni kwani kila ngeli hupangwa katika kundi lake. Je, ni ngeli ipi inayohusiana na viumbe vyenye uhai tu? 

A. KI-VI 

B. LI-YA 

C. U-YA 

D. I - ZI 

E. A-WA 

 

(x) Ufupishaji wa Habari una misingi yake ambayo haipaswi kukiukwa. Ni upi msingi wa kazi hiyo? 

A. Kuzingatia wazo kuu 

B. Kuzingatia lugha yenye mvuto 

C. Kuzingatia muundo wa kazi hiyo 

D. Kuzingatia mtindo wa kazi hiyo 

E. Kuzingatia mbinu za kisanaa 

 

2. Oanisha maana za dhana mbalimbali za tungo katika orodha A na dhana husika katika orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia. 

ORODHA A 

ORODHA B 

i) Sehemu ya sentensi inayokaliwa na nomino au kikundi nomino 

(ii) Sehemu ya sentensi ambayo huarifu tendo linalotendeka 

(iii) Sehemu ya sentensi inayokaliwa na mtenda wa jambo 

(iv) Sehemu ya sentensi inayokaliwa na kielezi au kikundi kielezi 

(v) Sehemu ya sentensi inayokaliwa na kitenzi chenye O-rejeshi 

(vi) Sehemu ya sentensi inayokaliwa na kitenzi au kikundi kitenzi 

A. Kiarifu 

B. Chagizo 

C. Shamirisho 

D. Prediketa 

E. Kiima 

F. Kirai 

G. Kishazi tegemezi 

H. Kishazi huru 

 

SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Ili ikue lugha ina tabia ya kujiongezea msamiati wake kwa njia kadha wa kadha. Thibitisha dai hili kwa hoja sita (6) kisha toa mfano mmoja kwa kila hoja. 

 

4. Joti ni mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Gezaulole aliyeteuliwa kuwasilisha mada ya uandishi wa baruapepe kwenye maadhimisho ya siku ya teknolojia duniani. Muelekeze Joti vipengele muhimu katika uandishi huo. (Toa hoja 6) 

 

5. Suala la kufaa au kutofaa kuigwa haliangalii rika wala jinsi. Thibitisha dai hili kwa kutumia wahusika sita (6) wa rika na jinsi mbili tofauti kutoka katika tamthiliya ya Kilio Chetu kuonesha namna wasivyofaa kuigwa na jamii. 

 

6. Lugha ya Kiswahili inatamalaki na kuvuka nje ya mipaka ya dunia. Onesha mchango wa lugha hiyo katika maendeleo ya sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi. Toa hoja sita. 

 

7. (a) Rais Samia Suluhu Hassan aliwahutubia Watanzania siku ya sherehe ya Muungano. Ukiacha aina hiyo iliyotumika, bainisha aina nyingine tatu za hotuba. 

(b) Kila uandishi una muundo wake. Fafanua kwa mifano vipengele vikuu vitatu vya kuzingatia katika uandishi wa kumbukumbu za mikutano. 

 

8. Soma kifungu cha Habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata: 

 

Kiasi katika matendo huwapa watu maisha yasiyo wasiwasi. Dunia yao ya ajabu, kwa desturi, imejigawa katika viasi vingi sana. Ina mchana wa nuru na usuku wa giza, hari na baridi, na mengine mengi. Hapana mfalme awezaye kudai kuwa mchana ni wake peke yake, wala raia mwenye haki ya kusema kuwa usiku ni wake peke yake. Vitu hivi ni milki ya watu wote. Kama mchana na hari vingefululiza kuwako bila ya kiasi maisha yangechujuka na kuyabisika na kama usiku na baridi vingefululiza kuwako bila ya mpaka maisha yangevia na kuganda. 

Basi kama wanadamu wana tabia ya kunung’unika mara kwa mara juu ya hari nyingi au baridi kali – mambo yanayotokea kwa kudura Hapana shaka kuwa wana haki pia ya kunung’unika juu ya mamlaka yasiyo kiasi, heshima isiyo wastani, uhuru usio kadiri na nguvu isiyo mpaka. 

Si halali mwenye mamlaka kuyatumia ovyo; ni haramu Mheshimiwa kuwavunjia wengine heshima zao; hakuna uhuru wa matendo maovu. 

 

Maswali: 

(a) Andika kichwa cha Habari kinachofaa kwa habari uliyoisoma. 

(b) Nini kitatokea kama usiku na baridi vitafululiza ulimwenguni? 

(c) Fafanua maneno yaliyopigiwa mstari kama yalivyotumika katika habari. 

(d) Je, kuna ujumbe gani unaopatikana katika habari hii? (Toa hoja 2). 

 

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima.

 

ORODHA YA VITABU 

Ushairi 

Wasakatonge - M.S Khatibu 

Malenga Wapya - TAKILUKI 

Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi 

 

Riwaya 

Takadini - Ben J. Hanson 

Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo 

Joka la Mdimu - A.J. Safari 

 

Tamthiliya 

Orodha - Steve Reynolds 

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba 

Kilio Chetu - Medical Aid Foundation

 

9. Malenga ni askari wa kupambana na maadui mbalimbali wanaoshambulia ustawi wa jamii na silaha zao ni kalamu na karatasi. Fafanua maadui sita (6) ambao Malenga wawili uliowasoma hupambana nao katika kazi zao. Onesha hoja tatu kwa kila diwani. 

 

10. Kutowajibika kwa baadhi ya wanajamii kumekuwa ni kichocheo cha matatizo ndani ya jamii zao. Thibitisha usemi huu kwa riwaya mbili na kutoa hoja tatu kwa kila riwaya. 

 

11. “Uteuzi wa mandhari huakisi mawazo ya msanii.”Tumia tamthiliya mbili (2) kati ya ulizosoma kutathmini kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu. 

 

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 187  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 187  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

MTIHANI WA MWISHO MWAKA

KIDATO CHA TATU

KISWAHILI NOVEMBA 2023

Muda 2:30

MAELEKEZO

  1. Jibu maswali yote
  2. Mtihani huu una sehemu A. B na C (Jumla ya maswali 9)
  3. Simu za mkononi haziruhusiwi

SEHEMU A (16)

  1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo
  1. Neno lipi kati ya haya ni mofimu huru
  1. Uji
  2. Uzuri
  3. Uchache
  4. Ufa
  5. Upweke
  1. Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na iliyopo kwenye maneno yale.
  1. Mafumbo
  2. Nahau
  3. Misemo
  4. Semi
  5. Hadithi
  1. Utokeji wa misimu katika jamii hutegemea na
  1. Uchaguzi wa viongozi
  2. Mabadiliko ya Kijamii
  1. Shughuli itendekayo
  2. Utani uliopo miongoni mwa wanajamii
  3. Kutumia na kudumu kwa muda mrefu
  1. Nyenzo kuu za lugha ya Mazungumzo ni
  1. Usimuliaji
  2. Mdomo
  3. Maandishi
  4. Vitendo
  5. Ishara
  1. Kipi kipengele kinachohusu mjengeko wa kazi za fasihi?
  1. Muundo
  2. Wahusika
  3. Mtindo
  4. Mandhari
  5. Lugha
  1. Kikundi cha maneno kinachoonesha jambo lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikanaje?
  1. Kikundi kivumishi
  2. Kikundi kitenzi
  3. Nomino
  4. Chagizo
  5. Shamirisho
  1. ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa neno “Nitamfitinisha”
  1. Kutendeana
  2. Kutendesha
  3. Kutenda
  4. Kutendea
  5. Kutendewa
  1. Dhima Kuu ya Misima katika lugha ni ipi?
  1. Kuficha jambo kwa wasiohusika
  1. Kuongeza ukali wa maneno
  2. Kupatanisha maneno
  1. Kutambulisha aina za maneno
  2. Kuhimiza shughuli za maendeleo
  1. Ipi ni jozi sahihi ya vipera vya semi?
  1. Soga, nyimbo na nahau
  2. Methal mizungu na vitendawili
  3. Mafumbo, soga, maghani
  4. Misemo, mafumbo na vigano
  5. Mashairi mafumbo na mizungu
  1. Shule zetu zimeweka mikakati kabambe ya kutokomeza daraja la pili ili zibaki na daraja la kwanza pekee. Neno ‘ili’ katika tungo hii ni aina gani ya neno?
  1. Kiunganishi
  2. Kivumishi
  3. Kielezi
  4. Kitenzi
  5. Kihusishi
  1. Oanisha maelezo yaliyo katika Orodha A na dhana husika katika Orodha B. Kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Mada, Uhusiano, Malengo na Muktadha
  2. Umeupiga mwingi
  3. Nani Ugali mbuzi choma
  4. Baba Juma amefariki
  5. Hupokea mabadiliko ya papo hapo
  6. Kutumia lugha kulingana na kaida za jamii
  1. Tungo tata
  2. Utumizi wa lugha
  3. Lugha ya mazungumzo
  4. Simo
  5. Rejesta
  6. Humsaidia mzungumzaji kuteua lugha kwa usahihi
  7. Sababu ya utata
  8. Lahaja
  9. Lugha ya maandishi

SEHEMU B (ALAMA 54)

  1. (a)Unaelewa nini dhana ya misimu

(b) Onesha vyanzo viwili vya Msimu

(c) Misimu huweza kuundwa kwa njia tofauti tofauti

  1. Demu
  2. Kumzimikia
  3. Disco
  4. Ferouz ni twiga
  5. Mataputapu
  1. Batuli alitaka kuhifadhi methali na vitendawili kwa njia ya Kichwa tu kwa ajili ya kizazi kijacho. Lakini Kibutu alimkataza asifanye hivyo badala yake atumie njia nyingine
  1. Toa hoja nne (4) kama sababu ya katazo hilo
  2. Taja njia tano (5) sahihi ambazo unahisi kibuyu angemshawishi batuli atumie.
  1. Eleza kinagaubaga tofauti zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo.
  1. Uwasilishaji
  2. Uhifadhi
  3. Manadiliko
  1. Lugha ina tabia ya kujiongeza msamiati wake kwa njia kadha wa kadha; kwa kuthibitisha dai hilo, tambulisha njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo.
  1. Kuku
  2. Mpangaji
  3. Kifaurongo
  1. TATAKI
  2. Fedha
  3. Msikwao
  1. Kitivo
  2. Pilipili

ix. Imla, mali, mila, lami

  1. Maendeleo ya Sayansi na Teknologia ni ndumi la kuwili kwa fasihi simulizi. Kwa hoja sita thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja mbili.

8. Soma kifungu habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

"Ndugu wazazi, kumbe safari yenu inahusu harusi ya Maria ?".Mkuu wa shule aliwauliza wazazi."Ndiyo," wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu."inategemewa kufugwa lini ."Mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati Maria anapofika kidato cha nne, Lakini Maria huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha ;hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishie .Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii,"Mzee Abdallah alieleza." Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama Mzee kwa chati sana .Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi: Maria ana kiburi kumbe?"

Mama Maria hakutaka hilo limpite ,hima hima akatoa maelezo yake ."Mama wewe ,Maria usimuone hivi. Maria mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Maria ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haiyoni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa.

Mtoto sasa ameharibika .Anafanya apendavyo elimu gani isiyojali adabu.wala utii?" Mama Maria alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka".

Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya mwisho.Alikwishatambua kwamba wazazi wa Maria walikuwa wameachwa nyuma na wakati .Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.

Maswali

(i)Bainisha dhima nne (04) zilizotokana na habari uliyosoma.

Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 70 na kuzidi 80.

SEHEMU C: (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili katika sehemu hii swali la 11 ni lazima

ORODHA YA VITABU

ORODHA YA VITABU.

USHAIRI.

  • Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP).
  • Malenga wapya -TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekacheka - T.A.Mvungi(EP&D.LTD)

RIWAYA.

  • Takadini -Ben J.Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N'tilie - E.Mbogo(HP)
  • Joka la Mdimu - A.J.SaiTari (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds(MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
  1. Fasihi ya Kiswahili imemuweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti. Thibitisha Usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya
  2. Lugha ni mhimili katika kazi yoyote ya fasihi. Watunzi hutumia lugha kiufundi ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Kwa kutumia jazanda au taswira tatu kutoka katika diwani mbili ulizosoma na uonyeshe namna zinavyofikisha ujumbe kwa jamii.
  3. “Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo au mambo hayapo sawa. Kauli hii inaweza kuwiana na waandishi wa riwaya Juu ya jamii inavyowazunguka, kwa kutoa hoja tatu kutoka kila riwaya katika riwaya mbili ulizosoma, jadili kwa nini wasanii hao hulia?

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 152  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 152  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA 2020

021KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 DECEMBER 2020


Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, B na chagua maswali matatu (03) kutoka sehemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.

SEHEMU A, (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.

(i) Ni kanuni, sheria na taratibu zipi zinazozingatiwa na wazungumzaji wa lugha fulani?

A Mofimu, Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi

B Herufi, Sauti, Mofimu,Silabi na neno.

C Sarufi Maana, Sarufi Miundo, Sarufi Maumbo na Sarufi Matamshi.

 Sarufi maana, Mofimu, Neno na Kirai

E Silabi, Neno, Kirai na Sentensi.

(ii)………………. Ni sauti zinazotamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

 A Sauti B Herufi

 C irabu D  Silabi

 E Konsonanti

(iii)  Zipi ni nyenzo za lugha yoyote duniani?

A Sarufi na Fasihi B Irabu na Konsonanti

C Sarufi, Irabu na KonsonantiD Fasihi, Irabu na Konsonanti

E Sarufi, Fasihi, Irabu na Konsonanti

(iv) Mpangilio sahihi wa ngeli za kisintaksia ni upi?

A YU/A-WA, I-ZI,LI-YA,U-I,KI-VI,U-ZI,U-YA, KU,PA-MU-KU

B U-ZI, I-ZI,LI-YA,U-I, KU, YU/A-WA,U-YA, KI-VI, PA-MU-KU

C YU/A-WA, I-ZI, LI-YA,U-YA, KI-VI,U-ZI,U-I, KU,PA-MU-KU

D YU/A-WA,I-ZI, LI-YA,U-I,KI-VI, U-ZI,U-YA, PA-MU-KU, KU

E YU/A-WA, I-ZI,LI-YA, U-I, KI-VI,U-ZI, U-YA,KU, PA-MU-KU

(v)  Ni upi mpangilio sahihi wa mjengo wa Tungo?

A Kirai, Neno, Sentensi na Kishazi

B Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi

 Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno

E Sentensi, Neno. Kishazi na Kirai

(vi)  Ni lugha mseto ya muda inayozuka pindi makundi mawili yenye lugha mbili tofauti yakutanapo.

 Lugha ya vizalia B Pijini

C Kibantu D Kiswahili

E Kiunguja

(vii)Mambo muhimu yanayopatikana katika maana ya lugha ni kama yafuatayo, isipokuwa;

A Ni sauti za nasibu B Ni mfumo

C Lugha hufurahisha na kufundisha D Lugha inamuhusu binadamu

E Lugha ni chombo cha mawasiliano

(viii)  Ni sentensi ipi sio sentensi huru?

A Juma anacheza mpira B Anaimba vizuri

C Mtoto aliyepotea jana amepatikana. D Asha ni mtoto mzuri

EYule alikuwa anataka kucheza mpira.

(ix)  ……………. Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au kileksika;

 Isimu B Shina

C Mzizi D Kiimbo

E Mofimu

(x) Ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?

A Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba.

B Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani.

C Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama.

 Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba

E Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani.

2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha ‘’A’’ ambayo ni aina ya tungo na orodha ‘’B’’ ambazo ni aina za maneno yanayounda tungo hizo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA “A”

ORODHA “B”

i.Wale waliamini maneno yangu

 ii. Salama alikuwa mwanafunzi wangu

 iii. Walikuwa wanataka kwenda kulima

 iv.Alikuwa anajisomea darasani polepole

 v. Loo! Yule anapenda ugomvi

A. N + t +N +V

B. H + w +T + N

C. W + T + N + V

D. Ts + T + E +E

E. Ts + Ts + Ts + T

F. N + V + t +E

G. N + U+ N+ T

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswaliyote katika sehemu hii

3.Tunga sentensi moja kwa kila alama kuonesha matumizi ya alama zifuatazo.F4

i. Mkato

ii. Mabano

iii. Alama za mtajo

iv. Nukta pacha

4.Andika maana ya methali zifuatazo;

  1. Kikulacho ki nguoni mwako.
  2. Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
  3. Mchumia juani hulia kivulini.

5.(a) Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo. Tumia alama ya mkwaju (/) na kuweka herufi “K” juu ya kiima na herufi “A” juu ya kiarifu.

i. Mdogo wangu anaongea sana

ii. Yule kijana aliyekuja hapa juzi amefariki dunia

iii. Frank ni kijana mpole sana

iv. Mama amelala sakafuni

(b) Changanua sentensi zifuatazo kwa njia yamatawi kwa kutumia mkabala wa kimapokeo

i. Fisi mkubwa ameuawa kichakani jana alfajiri.

ii. Mtoto aliyekuwa anacheza uwanjani amevunjika mguu.

6.(a) Kwa kutumia mifano miwili kwa kila kipengele, fafanua kwa ufupi jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoonesha kuwa vitenzi vya Kiswahili na lugha za kibantu vina asili moja.

  1. Mpangilio wa viambishi katika vitenzi
  2. Kiambishi tamati katika vitenzi

b) Eleza kwa ufupi juu ya nadharia zifuatazo kwa jinsi zinavyoelezea asili ya Kiswahili

a)Kiswahili ni pijini au krioli

b)Kiswahili ni kiarabu

7. Kwa kutumia mifano, fafanua dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi

a)Tashibiha

b)Takriri

c)Sitiari

d)Tashihisi

e)Mubaalagha

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata;

Wanangu, toka zamani bara letu la Afrika lilikuwa na mambo yaliyohitilafiana na haya tunayoyaona sasa. Hadithi, vitimbi, na visa vilivyotokea zamani katika bara letu vinatofautiana sana na mabara yoyote mengine. Vyetu ni vitamu na bora kuliko vyote vile vilivyotokea katika mabara hayo.

Miujiza ya mambo yaliyotokea ina mizizi ambayo viini vyake hubenua waziwazi mila na desturi za asili tangu zamani, hivyo, hadithi hizo zina tija ya makumbusho ya daima milele. Kwa hiyo, katika hali yoyote yatupasa kuhifadhi hazina za mila zetu. Mila zetu zidumishwe; kwa mfano watu kuzunguka moto huku kizee kikongwe au ajuza akisimulia hadithi za mambo ya kale liwe ni jambo la kawaida kabisa. Katika dunia ya leo simulizi hizo za ujasirina uzalendo zimeenea kutoka vizazi hadi vizazi. Mambo mengi yamebadilika kutoka mitindo aina aina, hivyo mabadiliko hayo yasitufanye sisi kusahau simulizi zetu katika mitindo yetu. Ni wajibu utupasao kuendeleza tabia hizi ili tubenue mbinu za masimulizi hata kwa vitabu.

Maswali

  1. Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
  2. Bara la Afrika lina mambo gani mawili mazuri.
  3. Mwandishi anatuhimiza tudumishe mila ipi?
  4. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 60.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu(3) kutoka katika sehemu hii.

9.Wewe kama afisa Manunuzi wa kiwanda cha mbao cha Mshikamao S. L. P 100 Chamwino, andika barua kwa mfanyabiashara yeyote mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la vifaa vifuatavyo; Misumeno 5, gundi ya mbao lita 20, misumari ya nchi sita Kg 25, na kofia ngumu 40. Jina lako liwe Shukrani Kazamoyo.

10. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

11. “Kazi ya fasihi ina radha kwa sababu inamzungumzia pia mwanamke kwa namna tofautitofauti” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.

12. Chagua wahusika wawili katika tamthiliya teule mbili ulizosoma na uoneshe ujumbe unaowasilishwa na waandishi kupitia matendo yao.

ORODHA YA VITABU 

USHAIRI

Wasakatonge ---------------------------- M. S Khatibu (DUP)

Malenga wapya-------------------------- TAKILUKI (DUPU)

Mashairi ya Chekacheka---------------- T. A. Mvungi (EPdD.LTD)

RIWAYA

Takadini ----------------------------------- Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie ----------------- E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu ---------------------------- A. J. Safari ( H.P)

TAMTHILIYA

Orodha ------------------------------------ Steve Reynolds ( M. A)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ----- E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu --------------------------------- Medical Aid Foundation (TPH)

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 37  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 37  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256