OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MITIHANI YA KUJIPIMA KWA SHULE ZA SEKONDARI
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA-NOVEMBER-2025
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
MUDA: Saa 2:30
MAELEKEZO
1. Mtihani huu una sehemu tatu: A, B na C .
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B.
3. Sehemu C jibu swali moja (1) la insha .
4. Andika majibu yako kwa kalamu ya wino wa buluu au mweusi .
5. Hakikisha maandishi yako ni safi na nadhifu.
SEHEMU A (15 Alama)
SWALI LA 1: Chagua Jibu Sahihi (i – x)
Chagua jibu sahihi na andika herufi yake katika kijisanduku kilichotolewa.
(i) Jamii kubwa ya Wabantu inasadikika ilitoka katika eneo la: A. Bonde la Naili B. Afrika Magharibi C. Afrika Kaskazini D. Kongo
(ii) Kundi la watu waliokuwa na lugha za Kisudani na walihamia Tanzania ni: A. Wabantu B. Wanilo C. Wakushito D. Wakichembe
(iii) Kazi kuu ya jamii za asili za Kitanzania ilikuwa: A. Kilimo, Ufugaji, na Uvuvi B. Biashara ya Kitalii C. Ufugaji pekee D. Uchimbaji wa madini