OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA
KIDATO CHA KWANZA
KISWAHILI NOVEMBA 2023
Muda: 2:30
MAELEZO
SEHEMU A (Alama 30)
1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo;
2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika Orodha A na aina za nyimbo kutoka Orodha B. Kisha andika herufi ya Jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.
ORODHA A | ORODHA B |
|
|
3. Tumia mofimu zifuatazo kuonesha thamani ilizopewa katika paradise Mfano Li- Kuonesha wakati uliopita (Aliondoka)
(b) Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi
(b)Kamilisha mchoro ufuatao wa vipera vya ushairi
9. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:
(i) Vichekesho
(ii) Mtindo
(iii) Lakabu
(iv)Soga
(v) Dhamira
SEHEMU C (ALAMA 15)
10. Mwandikie baba yako barua ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Kivukoni SLP 20 Singida kumwomba hela ya safari ya kutembelea mbuga za wanyama. Jina lako liwe Mwaluko likoko SLP 350 Dodoma.
FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 156
FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 156
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA
KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA
NOVEMBA 2022
Maelekezo:
SEHEMU A: (Alama 15)
Jibu maswali yote kwenye sehemu hii
1.Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzunguka kiumbe katika maisha yake. Vitu hivyo vinaweza kuwa vyenye uhai kama vile wanyama, wadudu na mimea au visivyo na uhai kama vile milima, maziwa, mabonde, mito na bahari.
Uharibifu wa mazingira ni uzoroteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa, maji, mimea, udongo na hata kupotea kwa wanyamapori. Mara nyingi, uharibifu wa mazingira husababishwa na vitendo vya binadamu kuangamiza viumbe vinavyomzunguka. Vitendo hivyo ni kama vile kukata miti hovyo, kulima kandokando ya vyanzo vya maji, kutupa taka hovyo na kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji.
Uharibifu wa mazingira hutokana na shughuli mbalimbali za binadamu kama vile kilimo. Binadamu hupanua mashamba kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Ukataji wa miti ovyo na uchomaji wa misitu husababisha vifo vya viumbe hai vinavyoishi katika miti hiyo kama vile nyani, tumbili na sokwe.
Utupaji wa taka huweza kuharibu mazingira. Taka hizo hutoa harufu mbaya na kuvutia wadudu kama vile nzi. Wadudu hao husababisha magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu.
Viwanda kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji ni sababu nyingine ya uharibifu wa mazingira. Maji yanayotiririshwa huchafua maji yanayotumiwa na binadamu kutoka kwenye mito na maziwa hivyo husababisha magonjwa kwa binadamu kama vile kansa. Viwanda pia hutoa moshi ambao huchafua hewa inayovutwa na watu hivyo watu hupata madhara kama vile ugonjwa wa mapafu.
Maswali
i. Kichwa kinachofaa kwa habari hii ni:
A. Hali ya hewa
B. Kutunza mazingira
C. Sababu za uharibifu wa mazingira
D. Ukataji miti ovyo
E. Athari za mazingira
ii. Kwa nini ni muhimu kutunza mazingira yetu?
A. Ili kuepukana na magonjwa, vita na njaa
B. Ili kupata mazao mengi, wanyama wengi na miti.
C. Ili kupendezesha mazingira, kupata majalala na maziwa
D. Ili kuepuka magonjwa, kupata mvua za kutosha na afya bora
E. Ili kuondoa mmomonyoko wa udongo, kupata miti mingi na kuondoa unyevuunyevu
iii. Shughuli zingine zinazofanywa na binadamu na hupelekea uharibifu wa mazingira ni:
A. Kufuga wanyama wengi katika eneo dogo
B. Kujenga nyumba nzuri
C. Kusafisha maziwa yetu
D. Kuuza madini
E. Kufua nguo
iv. Ugonjwa wa mapafu unaoweza kusababishwa na kuvuta hewa kutoka kwa mtu mwingine hujulikana kama vile_______
A. Athma
B. Kifua kikuu
C. Pumu
D. Kipindupindu
E. Kansa
v. Magonjwa mengine yanayoweza kutupata baada ya kutupa taka ovyo ni pamoja na __
A. Upele
B. Amiba
C. Pumu
D. Kuhara
E. Homa
vi. Ni ugonjwa gani wa mlipuko unaozungumziwa na mwandishi katika habari hii?
A. Korona
B. Kipindupindu
C. Kansa
D. Homa ya mapafu
E. Maji machafu
vii. Waziri wa tanzania mwenye dhamana ya kusimamia mazingira anaitwa _______
A. Umi Mwalimu
B. Tundu Antipasi Lisu
C. Godbless Lema
D. Majaliwa kasimu majaliwa
E. Seleman Jafo
viii. Kutokana na habari uliyoisoma, Rasilimali ni nini?
A. Ni jumla ya mali aliyonayo mtu au nchi
B. Vyanzo vya maji
C. Upepo
D. Barabara
E. Mali inayopatikana kutokana na njia isiyo sahihi
ix. Zifuatazo ni njia za kutunza mazingira
A. Kulipua mabomu, kupanda miti na kuchimba vyoo.
B. Kupanda miti, kutupa taka ovyo na kutiririsha maji machafu
C. Kupanda miti, kutoa elimu dhidi ya mazingira na kuchimba mashimo ya kuhifadhi taka. D. Kuendesha magari makubwa, kujenga nyumba nzuri na kunawa mikono kabla ya kula
E. Kuwafundisha wanafunzi, kuchoma taka na kupanda maua.
x. Ni uharibifu gani wa mazingira kati ya yafuatayo husababisha mmomonyoko wa ardhi?
A. Kutupa vinyesi vya watoto ovyo
B. Kupanda ukoka
C. Kuchoma misitu
D. Kufuga wanyama wengi
E. Mikusanyiko ya watu
2. Oanisha safu ya maneno A na B.
SEHEMU B: (Alama 70)
Jibu maswali yote kwenye sehemu hii
3. Fafanua maana ya istilahi zifuatazo kama zinavyotumika kwenye lugha ya Kiswahili
(a) Shina la neno
…………………………………………………………………………………………………
(b) Sarufi
…………………………………………………………………………………………………
(c) Vielezi
…………………………………………………………………………………………………
(d) Sintaksia
…………………………………………………………………………………………………
(e) Viambishi
…………………………………………………………………………………………………
4.Bainisha dhima tano (5) za viambishi awali katika lugha ya Kiswahili. Kwa kila dhima toa mfano mmoja.
5.a) Sentensi zifuatazo ni tata. Tunga sesntensi mbili kila sentensi ondoa utata huo.
i. Mama amenunua mbuzi
....................................................................................................................................................
ii. Baba Amina ameondoka
…………………………………………………………………………………………………
iii. Mwajuma ametumwa na Rama
…………………………………………………………………………………………………
iv. Kaka amevunja kijiko chake
…………………………………………………………………………………………………
v. Ali amempigia Asha ngoma
…………………………………………………………………………………………………
b) Taja mifano ya kauli zinazoonyesha muktadha wa rejesta zifuatazo:
i. Hotelini
…………………………………………………………………………………………………
ii. Sokoni
…………………………………………………………………………………………………
iii. Bandarini
…………………………………………………………………………………………………
iv. Darasani
…………………………………………………………………………………………………
v. Ndani ya basi
…………………………………………………………………………………………………
6. (a) Panga maneno yafuatayo kama yanavyokuwa katika kamusi
Kafeli, Tosha, Zaituni, Buriani, Roho, Paroko, Kaheshimu, Amina, Amani
…………………………………………………………………………………………………………………………………….
(b) Fafanua dhima tano za kamusi
7. Taja methali moja ambayo ungeweza kuitumia kuonya au kuadilisha kulingana na tukio lililoelezwa hapo chini
Mfano: Mtoto alilelewa vibaya hatimaye ajawa jambazi
Methali: Samaki mkunje ingali mbichi
i. Ndege alijenga kiota kwa kuchukua jani moja moja na hatimaye baada ya siku tatu kiota kikakamilika kujengwa.
Methali: ………………………………………………………………………………..…….
ii. Wastara alikuwa masikini, akajibidisha sana kufanyakazi usiku kucha, hatimaye akafanikiwa kupata utajiri na kuishi maisha yenye hadhi.
Methali: ……………………………………………………………………………………….
iii. Simba alivamia zizi la Mzee Mahende na kukamata ng’ombe mmoja, alipotoka na mkuki kumkabili, alishindwa akarudi nyuma kwa hofu kisha yowe wanakijiji wakakusanyika wakiwa na mikuki na mapanga na marungu wakampiga na kumuua.
Methali: ……………………………………………………………………………………….
iv. Dereva aliendesha gari kwa kasi na kusababisha ajari mbaya
Methali: ……………………………………………………………………………………….
v. Baba alipofiwa na mtoto wake alilia sana hadi akazimia
Methali: ………………………………………………………………………………………..
8. Amina ni mwanafunzi wa darasa la saba anayesoma shule ya msingi Majimengi, tatizo la Amina alikuwa anaamini kuwa lugha haina umuhimu wowote katika jamii. Wewe kama mwanafunzi wa kidato cha pili unamshawishi vipi Amina aweze kubadili imani yake? Kwa hoja tano (05)
9. Wahusika ni kipengele muhimu sana katika kazi yoyote ile ya fasihi. Onyesha aina ya wahusika katika fasihi simulizi (05).
SEHEMU C: (Alama 15)
10. Andika insha yenye maneno 150 na yasiyozidi 200 inayohusu madhara ya mimba za utotoni
FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 111
FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 111