FORM ONE EDK ANNUAL EXAMS

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA WA PILI

KIDATO CHA KWANZA

ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Muda: Saa 2 Novemba, 2026

MAELEKEZO

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye karatasi ya kujibia.
  3. Andika kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  4. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  5. Andika jina lako katika kila ukurasa wa karatasi ya kujibia.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU.
NAMBA YA SWALI ALAMA SAINI YA MTAHINI
1.    
2.    
3.    
4.    
5.    
6.    
7.    
8.    
9.    
10.    
JUMLA    
SAINI YA MHAKIKI    

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele (i) – (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake.

i. Kwanini elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?

  1. Kuleta maendeleo katika jamii

  2. Kutatua changamoto za wanadamu

  3. Kufuata mwenendo wa Mitume (A.S)

  4. Kumuabudu Allah (S.W) ipasavyo.

ii. Ni itikadi gani ya maisha iliyojengwa katika kujitenga na vitu vizuri na kumletea mwanadamu maendeleo miongoni mwa itikadi za dini?

  1. Ukafiri

  2. Utawa

  3. Ushirikina

  4. Upagani.

iii. Mtume Muhammad (S.A.W) alishushiwa aya tano za mwanzo akiwa katika pango la Hira. Aya hizi zinapatikana katika sura gani?

  1. Surat Al – Faatih’a

  2. Surat Al - Lahabi

  3. Surat Al – A’laq

  4. Surat Al – Falaq.

iv. Gomwa Mponda na wenzie wamekuwa na ubishani juu ya mgawanyo wa elimu katika uislamu hasa elimu ambayo ni faradhi ‘Ain. Ni ipi elimu ambayo ni Faradhi ‘Ain kati ya hizi?

  1. Elimu ya Mazingira

  2. Elimu ya Mwongozo

  3. Elimu ya Akhera

  4. Elimu ya Dunia

v. Qur’an ni kitabu cha Allah (S.W) kilichoteremshwa kwa ajili ya wanadamu wote. Bainisha kusudio la kuteremshwa kitabu hiki.

  1. Kusomwa mara kwa mara katika swala

  2. Kuongoza maisha ya mwanadamu

  3. Kufukuzia majini na mashetani

  4. Kuhifadhiwa katika vifua vya Waislamu.

vi. Bainisha sura inayowafunza Waislamu adabu za kuomba dua kwa Allah (S.W).

  1. Surat Al – Ikhlas’

  2. Surat Annas

  3. Surat Al – Faatih’a

  4. Surat Al – Maau’n.

vii. “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano”. Ni ipi nguzo ya Nne ya uislamu?

  1. Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani

  2. Kutoa Zakat

  3. Kusimamisha Swala

  4. Kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo.

viii. Kwa sababu gani ni muhimu kufuata Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W)?

  1. Sunnah ni sehemu ya Qur’an tukufu

  2. Huwezi kuitekeleza Qur’an ipasavyo bila Sunnah

  3. Kuacha Sunnah ni sababu ya kupata dhambi

  4. Sunnah ni sababu ya kuingia peponi.

ix. Muislamu analazimika kutekeleza swala tano za faradhi katika maisha yake. Bainisha kusudio la swala hizi.

  1. Kinga ya maovu na machafu

  2. Tiketi ya kuingia peponi

  3. Kupata thawabu na heshima

  4. Kumtambulisha Muislamu.

x. Kwa nini Waislamu wanafunga mwezi wa Ramadhani?

  1. Kutafuta Ucha Mungu

  2. Kufutiwa dhambi

  3. Kuingia peponi

  4. Kudumisha historia.

2. Oanisha maelezo kuhusu shahada katika orodha A na istilahi husika kutoka katika orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwa kila kipengele katika karatasi yako ya kujibia.

Orodha A
Orodha B
  1. Mafungamano ya Allah na Mtume wake
  2. Ahadi ya kufuata mwenendo wa Mtume (S.A.W)
  3. Ahadi ya kuchunga mipaka ya Allah (S.W)
  4. Kuikanusha shahada kivitendo katika maisha
  5. Kiingilio cha dini ya Uislamu
  1. Ushirikina
  2. Shahada ya kwanza
  3. Dalili ya shahada mbili
  4. Chimbuko la shahada
  5. Utawa
  6. Shahada ya pili
  7. Kutamka shahada mbili

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Imani ya kweli ya Muislamu inakamilika kwa kuzingatia mambo sita ya msingi sana kwa kila muumini. Orodhesha mambo hayo katika mpangilo sahihi.

4. (a) Kwa kuzingatia Sheria, nini maana ya Shahada?

(b) Mtume Muhammad (S.a.W) anatufundisha kuwa shahada ya kweli imegawanyika katika hatua kuu tatu, bainisha sehemu tatu za shahada.

5. (a) Janaba ni nini kisheria?

(b) Kwa kurejea kutoka katika Qur’an (4:43), taja mambo manne yaliyoharamishwa kufanya kwa mwenye janaba.

6. Surat Al – Fatihah ni sura inayosomwa mara kwa mara na hasa katika ibada ya swala. Fafanua kwa ufupi mafunzo manne ya sura hii.

7. (A) Mitume na Manabii wa Mwenyezi Mungu walitumia mbinu mbalimbali katika kuwalingania watu wao. Ni mbinu zipi walizozitumia katika kuwalingania watu wao?

(B) Ndani ya Qur’an Tukufu imetaja na kuelezea Mitume ishirini na tano. Wewe kama msomaji wa kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu (Qur’an) taja Mitume kumi na mbili waliotajwa ndani ya kitabu hicho.

8. Baadhi ya Waislamu wanapuuza Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kudai kwamba ukiitekeleza unapata thawabu na ukiicha hupati dhambi. Wabainishie hasara nne watakazopata duniani na akhera kutokana na mwenendo huu.

9. Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W), Muislamu bora ni yule mwenye tabia njema na mwenye kuepuka tabia mbaya. Bainisha tabia mbaya tano utakazoziepuka katika maisha yako ya kila siku.

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10).

10. “Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumtakatisha mja kutokana na mambo maovu na machafu.” Qur’an (29:45). Kwa kuzingatia aya tajwa fafanua kwa utaratibu sharti nne (4) za kusimamisha swala. Wabillah Tawfeeq

FORM ONE EDK EXAM SERIES 307  

FORM ONE EDK EXAM SERIES 307  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256