SURA YA KWANZA.

MAZINGIRA

Mazingira hujumuisha vitu vyote vinavyotuzunguka, vikiwemo viumbe hai na vitu visivyo hai. Viumbe hai ni pamoja na wanyama, mimea na wadudu. Vitu visivyo hai ni pamoja na mchanga, mawe, hewa na maji.

Usalama wa mazingira

Mazingira salama kwa viumbe hai ni yale ambayo hayajaathiriwa kutoka katika uhalisia wake. Mazingira hayo hufanya viumbe hai waishi na kukua vizuri. Mazingira yasiyo salama kwa viumbe hai ni yale yaliyoathiriwa kutoka katika uhalisia wake. Mazingira hayo huathiri afya na ukuaji wa viumbe hai.

Mfano wa mazingira yanayofaa kwa ukuaji wa viumbe hai ni udongo, maji ya mito, maziwa na bahari. Halikadhalika hewa pia ni muhimu kwa viumbe hai. Mazingira hayo yakiathiriwa huwa sio salama kwa viumbe hai.

Uharibifu wa udongo

Soma habari ifuatayo kwa makini, kisha fanya zoezi la 1.

Siku moja mwalimu wa Shule ya Msingi Kidete aliwapa kazi wanafunzi. Kazi hiyo ilikuwa ni kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vinavyosababisha uharibifu wa udongo katika mazingira yanayowazunguka. Wanafunzi waliandaa daftari pamoja na kaiamu kwa ajili ya kuandika matokeo ya uchunguzi. Mwalimu aliwasisitiza wanafunzi kuwasilisha kazi zao mara baada ya kumaliza uchunguzi. Baada ya kuwasilisha kazi, mwalimu alimchagua Shukrani na kufanya naye mazungumzo darasani. Mazungumzo hayo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwalimu: Katika uchunguzi ulioufanya, ulibaini vitendo gani vinavyohatarisha usalama wa udongo?

Shukrani: Nilibaini kuwepo kwa utupaji na uchomaji ovyo wa takatak

Mwalimu: Sawa Shukrani, vitu gani ambavyo uliviona vimetupwa, ukagundua vinasababisha uharibifu wa udongo?

Shukrani: Niliona mifuko ya plastiki, makopo, chupa za plastiki na misumari. Vitu vingine ni nyembe, vipande vya bati na vipande vya chupa. Vitu hivi vilikuwa vimezagaa ovyo kila mahali.

Mwalimu: Vitu hivyo unadhani vina madhara gani kwa viumbe hai?

Shukrani: Vitu hivyo huathiri afya za wanyama na mimea. Pia, husababisha kuwepo kwa mazalio ya vijidudu vya magonjwa kama vile malaria. Vilevile, husababisha maambukizi na kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na homa ya matumbo.

Mwalimu: Vizuri sana. Nini kifanyike ili kuondoa tatizo hilo?

Shukrani: lnatubidi kukusanya takataka na kuziweka kwenye
pipa kisha kuzitupa mahali salama au kuzichoma.
Pia, kuchimba shimo na kufukia takataka zinazooza.

Mwalimu: Ni sehemu gani salama ya kuchoma takataka zilizokusanywa?

Shukrani: Ni kwenye shimo la takataka au tanuru maalum.

Mwalimu : Sawa Shukrani, njia salama ni kuzichoma takataka. Lakini moshi wake ni hatari kwa afya., hivyo zichomwe mbali na makazi ya watu. Je, unafikiri takataka gani nyingine zinaweza kuharibu udongo?

Shukrani: Uchafu unaotoka kwenye makazi ya watu kama maji machafu na majitaka yanayotoka vyooni ambayo hutiririka ovyo.

Mwalimu: Kweli kabisa, vilevile umwagaji wa mafuta yanayotoka kwenye magari, mitambo na vifaa mbalimbali huharibu udongo.

Shukrani: Asante sana mwalimu, ninaahidi kuwa balozi wa mazingira.

Mwalimu: Asante sana Shukrani. Naamini, wewe pamoja na wenzako mtakuwa mabalozi mazuri wa mazingira. Mazingira salama, ukiwemo udongo ni makazi ya wadudu wanaosaidia mmeng’enyo wa virutubisho vya mimea katika ardhi. Hivyo, hatuna budi kuutunza.

Kielelezo namba 1. Uchafuzi wa udongo

Uchafuzi wa maji

Ukichunguza maeneo unayoishi, kung baadhi ya watu hutupa takataka katika mikondo ya maji. Pia, watu hutiririsha majitaka kutoka vyooni, viwandani na migodini kuelekea kwenye vyanzo vya maji. Maji yanayotoka viwandani na migodini yanaweza kuwa na kemikali zenye sum. Utiririshaji wa majitaka husababisha uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji.

Aidha, shughuli za kila siku za binadamu huweza kuchafua vyanzo vya maji. Shughuli hizo ni kama kufua, kuoga, kujisaidia ovyo na kulima kandokando ya vyanzo vya maji. Vilevile, wanyama wanapotumia mito, mabwawa na maziwa huchafua maji. Uchafuzi wa vyanzo vya maji husababisha madhara kwa binadamu na viumbe wengine.

Maji yaliyochafuliwa huweza kusababisha magonjwa ya homa ya matumbo, kichocho na kipindupindu. Halikadhalika, maji yaliyochafuliwa kwa kemikali kutoka viwandani, shambani na migodini huweza kusababisha saratani.

Kielelezo namba 2. Uchafuzi wa maji

Uchafuzi wa hewa

Hewa ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali zinazopatikana angani. Hewa inaweza ku'iva safi au chafu. Hewa safi ni lie ambayo haina vihatarishi vya afya na mazingira.

Vitu vinavyoweza kuchafua hewa ni vumbi, harufu mbaya, kemikali au vimeiea vya magonjwa. Pia, shughuli mbalimbali za kibinadamu zinachangia katika uchafuzi wa hewa. Shughuli hizo ni kama uchomaji takataka na misitu. Vilevile, moshi wa sumu kutoka viwandani na kwenye magari chakavu huchafua hewa.

Kielelezo namba 3. Uchafuzi wa hewa

Soma habari ifuatayo kwa makini, kisha fanya zoezi la 4.

Siku moja mwalimu wetu alimwalika mtaalamu wa mazingira wa kata ya Mima. Lengo iilikuwa kutueleza athari za uchafuzi wa mazingira. Mtaalamu alieleza kuwa, uchafuzi wa mazingira husababisha vifo vya wanyama na mimea. Vifo hivyo husababishwa na kuchafuka kwa hewa, maji na udongo. Vilevile, utiririshaji wa majitaka kutoka kwenye makazi ya watu na viwandani, huathiri viumbe hai wanaoishi majini.

Aliendelea kusema kuwa, magonjwa kama kichocho na kipindupindu husababishwa na uchafuzi wa mazingira. Magonjwa mengine ni kikohozi, mafua na homa ya matumbo.

Mtaalamu alieleza vitendo vya ukataji miti ovyo husababisha kuongezeka kwa hewa ya kabonidioksidi katika anga. Hewa hii ingetumiwa na mimea kutengeneza chakula na kutoa hewa safi ya oksijeni ambayo hutumiwa na viumbe hai.

Wanafunzi walimuuliza mtaalamu kuhusu madhara ya moshi wa viwandani kwenye mazingira. Mtaalamu alieleza kuwa, moshi wenye sumu huathiri mapafu na kusababisha magonjwa kama vile saratani ya mapafu.

Mtaalamu aliwashukuru wanafunzi kwa kumsikiliza na kuwataka wafanye hadhari iii wasichafue mazingira. Mwalimu alimshukuru mtaalamu kwa ufafanuzi wake mzuri uliowafanya wanafunzi kufurahia somo.

Kutunza mazingira

Ni muhimu kutunza mazingira yetu iii yawe safi na salama. Uchafu wenye takataka mchanganyiko na zisizooza kama mifuko ya plastiki, nyembe na sindano unatakiwa utenganishwe. Pia, vigae vya chupa, sahani na vikombe vichomwe kwenye tanuri au zifukiwe kwenye shimo la Takataka kama mabaki ya chakula, karatasi na majani yaliyopukutishwa na miti zifukiwe kwenye shimo. Baada ya iticpda takataka hizi huoza na kuwa mbolea. Takataka zinazoraa-lkwa urejelezaji zipelekwe viwandani kwa ajili ya kutengeneza vitu vingine.

Kielelezo namba 4. Tanuri

Ni vema majitaka yaelekezwe katika mfumo rasmi wa kutiririsha na kutunza majitaka. Pale ambapo hakuna mfumo huo, maji hayo yahifadhiwe katika mashimo ya majitaka. Mashimo yakijaa majitaka yanyonywe kwa gari maalumu na kupelekwa sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo. Sehemu ambapo hakuna gari maalumu la kunyonyea majitaka, shimo lililojaa lifukiwe na Iichimbwe shimo jingine.

Neema na Musa ni wanafunzi wa Shule ya M.singi Miembeni. Siku moja wakiwa njiani kutoka shuleni, Neema alianzisha mazungumzo kama ifuatavyo:

Neema: Kwa nini tunashauriwa kupanda miti katikamazingira yetu?

Musa: Kwa sababu miti ni muhimu katika maisha yetu yakila siku.

Neema:Je, ni umuhimu gani huo?

Musa: Miti hutupatia kuni, mkaa, hewa ya oksijeni,matunda na kivuli. Halikadhalika, miti hutupatia dawa, mbao na pia ni makazi ya ndege, wanyama na wadudu.

Neema:Asante Musa! Kumbe kuna umuhimu wa kupanda na kutunza miti katika mazingira yetu. Hivi kwa nini watu wanakata miti?

Musa: Watu wanakata miti kwa ajili ya matumizi mbalimbalikama kuni, kuchoma mkaa

na kujengea nyumba.

Neema:Kama watu watakata miti kwa wingi kwa ajili ya kuchoma mkaa nini kitatokea?

Musa: Ukataji wa miti kwa wingi utasababisha kiwango chahewa ya kabonidioksidi kuongezeka. Kuongezeka kwa hewa ya kabonidioksidi kuna madhara kwa viumbe hai na anga. Pia, uchOmaji wa mkaa ukizidi utasababisha jangwa na uchafuzi wa hewa.

Neema:Asante Musa kwa maelezo yako. Je, ni uchomaji wa mkaa pekee ndiyo unaochafua hewa?

Musa: Hapana, vipo vyanzo vingine vinavyochafua hewa.Vyanzo hivyo ni pamoja na vumbi na harufu mbaya kutoka kwenye mifumo ya majitaka iliyoharibika.

Vilevile, moshi kutoka viwandani, magari chakavu na mitambo inayotumia nishati mbalimbali hasa fueli huchafua hewa.

Neema:Nashukuru Musa kwa maelezo yako. Ni vyema tuchukue hatua za kuelimisha jamii iii kudumisha usalama wa hewa.

Musa : Kweli kabisa, jamii ina jukumu la kuhakikishainadumisha usafi na usalama wa hewa. Pia, isichome misitu, ipunguze uchomaji wa mkaa na itumie nishati mbadala kama gesi na umeme.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256