SURA YA KWANZA
ALAMA ZA USALAMA KATIKA MAZINGIRA
Msamiati
Dhana ya alama za Usalama katika mazingira
Aina za alama za usalama
Zipo aina kuu nne za alama za usalama, ambazo ni alama za:
Jedwali
Na | Aina za alama za usalama | Rangi | Maelekezo. | Sifa. | Mfano. |
1 | Alama za Nyekundu kuzuia au kukataza |
| Zina umbo la duara au pembe nne, picha nyeusi kwenye msingi mweupe na kingo nyekundu. Baadhi ya alama hizi zirla mstari mwekundu wa kiegema | ||
2 | Alama za onyo au tahadhari | Njano. |
| Zina umbo la pembe tatu, picha nyeusi kwenye msingi wa nano na kingo nyeusi | |
3 | Alama za lazima au amri | bluu | Husisitizatabia au vitendo fulani | Zina umbo la duara, picha nyeupe kwenye msingi wa bluu | |
4 | Alama za dharura | Kijani. |
Huduma ya kwanza au vifaa vya kujiokoa | Zina umbo la pembe nne (mstatili au mraba), picha nyeupe kwenye msingi wa kijani au picha ya kijani ______ kwenye msingi |
Tafsiri za alama za usalama
Alama za usalama hubeba ujumbe ambao hutoa tahadhari kwa walengwa. Ni vema kutambua alama hizo na tafsiri zake, iii kuepuka hatari au ajali zinazoweza kutokea kwa kutozingatia tahadhari iliyotolewa. Miongoni mwa alama hizo ni kama zinavyooneshwa kwenye Jedwali namba 2.
1. Hairuhusiwi kuingia
Alama zinapatikana wapi?
Sehemu ambazo haziruhusiwi kuingia au kupita, mfano, maabara
Athari ya kutochukua tahadhari
Huweza kupata madhara ya kiafya endapo mtu ataingia au kupita
2. Hairuhusiwa kuvuta sigara
Alama zinapatikana wapi?
Kwenye vituo vya kujaza mafuta ya magari, kwenye ndege, kwenye migahawa, shule na katika maeneo mengine ya umma
Athari ya kutochukua tahadhari
Moto huweza kutokea mtu akivuta sigara sehemu hiyo. Husababisha madhara ya kiafya kwa mtu asiyevuta ambaye yupo karibu na mvutaji wa sigara.
Matumizi ya alama za usalama katika mazingira
Alama za usalama hutumika katika maeneo na vitu mbalimbali vilivyopo kwenye mazingira yetu, Miongoni mwa matumizi ya alama za usalama ni haya yafuatayo:
Kuonesha hatari
Kuna maeneo au vitu ambavyo huwekwa alama za usalama, iii kuonesha hatari ambayo mtu huweza kukutana nayo endapo hatachukua tahadhari. Kwa mfano, alama zinazotahadharisha kuwa kung mionzi ya eksirei, kemikali yenye kulipuka au mkondo unaopitisha umeme mkubwa. Alama hizi humfanya mtu achukue tahadhari anapokaribia mazingira hayo.
Kuepusha magonjwa
Alama za usalama hutumika kuonesha namna mtu anavyoweza kuepuka
magonjwa au kutoathiri afya yake akizingatia tahadhari iliyotolewa. Mfano, vitu vyenye alama ya vimelea vya magonjwa, kama vile mapipa ya taka za hospitali hutahadharisha kutovigusa. Alama hiyo huepusha magonjwa yanayosababishwa na vimelea.
Kuepusha ajali
Alama nyingine za usalama husaidia kuepusha ajali. Mfano, gari linalobeba mafuta huwa na alama ya usalama inayoonesha vitu vinavyoshika moto na kuwaka kwa haraka. Hivyo, matumizi ya alama hii husaidia kuepusha ajali za moto ambazo zingeweza kutokea.
Kutoa tahadhari na maelekezo
Alama nyingine hutahadharisha na kutoa maelekezo ya namna ya kutumia au kufanya kitu fulani kwa uangalifu. Kwa mfano, vitu vinavyovunjika kwa urahisi huwekewa alama ya maelekezo kumsaidia anayebeba kuwa mwangalifu. Baadhi ya vivatilifu vya kuua wadudu au magugu huwekwa alama ya sumu au hatari. Alama hizi humfanya mtumiaji kutumia vifaa vya kujikinga wakati wa kutumia kemikali hizo ill asidhurike. Vifaa hivyo ni pamoja na glovu, miwani, vazi maalumu au ovalori, buti na kofia ngumu. Vilevile, kwenye chupa za dawa za kupuliza za kuua wadudu na manukato huwekwa alama ya kushika moto. Hivyo, hutahadharisha kukaa mbali na vyanzo vya moto wakati wa kutumia vitu hivyo.
www.learninghubtz.co.tz