SURA YA KWANZA
MAJANGA KATIKA JAMII
Msamiati
- Jivu la volcano: jivu la moto ltokanalo na mwako wa volkno
- Lava: ujiuji wa moto unaotokea juu ya uso wa dunia baada ya mlipuko wa volcano
- Magma; kimiminika cha mto mithili ya uji mzito, kinachotokana na kuyeyuka kwa iamba kwa sababu ya joto kali
- Mwamba: jiwe kubwa kavu au jabali lililoko majini au nchi kavu au chini ya ardhi
- Nishati: Nguvu ya kuendesha mitambo au nguvu ya kufanya kazi
- Nguvu ya uvutano: nguvu mbili zenye uelekeo tofauti
Dhana ya majanga ya asili
Majanga ya asili ni matukio makubwa ya hatari yanayosababishwa na nguvu za asili ambayo hutokea ghafla na husababisha maafa. Matukio haya ya hatari yanakuwa majanga iwapo to kutokea kwake kutasababisha maafa ambapo rasilimali zilizopo katika jamii haziwezi kuzuia maafa hayo kutokea. Baadhi ya majanga ya asili ni pamoja na tetemeko Ia ardhi, mlipuko wa volkano, maporomoko ya ardhi, tsunami, moto, mafuriko na ukame. Japokuwa mafuriko, ukame na moto ni majanga ya asili, wakati mwingine huweza kusababishwa na shughuli za kibinadamu.
Majanga huweza kutokea ama kwa ghafla au taratibu. Baadhi ya majanga ya asili yanayotokea kwa ghafla ni mafuriko, tetemeko Ia ardhi, mlipuko wa volkano, maporomoko ya ardhi, tsunami na moto. Ukame ni mojawapo ya janga la asili linalotokea taratibu. Majanga haya huweza kutokea sehemu yoyote ile kulingana na asili ya janga hilo. Majanga mengine hutokea kwakujirudiarudia katika eneo moja. Majanga hayo yanapotokea husababisha maafa kama vile vifo vya watu na wanyama, kupotea au kuharibika kwa uoto, mall, miundombinu, na magonjwa ya mlipuko. Yafuatayo ni baadhi ya majanga ya asili na athari zake:
- Kuhusu tetemeko la ardhi lililowahi kutokea.
- Viashirio vya tetemeko la ardhi.
- Mambo ya kufanya kujikinga na tetemeko la ardhi.
Tetemeko Ia ardhi
Tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa ghafla unaotokea katika tabaka Ia juu la dunia. Mtikisiko huu husababishwa na nguvu za asili zinazotokana na nguvu ya mawimbi yapitayo katikati ya matabaka ya miamba ardhini. Miamba iliyopo chini ya use wa dunia inapojongeleana aghalabu husababisha mvutano na msuguano. Mchakato huu mwishowe husababisha mpasuko ambao huachia nguvu ya mtetemo. Nguvu hii husababisha mtikisiko wa ghafla katika tabaka Ia juu Ia dunia unaoitwa tetemeko Ia ardhi. Nguvu hizi za mtetemo pia huweza kusababishwa na mlipuko wa volkano na shughuli za kibinadamu kama vile; milipuko ya nyuklia na uchimbaji wa madini. Ukubwa wa tetemeko la ardhi hupimwa kwa kifaa kiitwacho sesimometa. Kwa kawaida ni vigumu kutambua dalili za kutokea kwa tetemeko la ardhi, hivyo huweza kusababisha madhara makubwa sana endapo litatokea katika makazi ya watu. Madhara hayo ni pamoja na vifo na uharibifu wa mali.
Tetemeko la ardhi
Athari za tetemeko la ardhi
Tetemeko Ia ardhi huleta athari mbalimbali katika mazingira. Ingawa tetemeko Ia ardhi hudumu kwa sekunde chache katika eneo linalohusika, athari zake zinaweza kuwa kubwa sana. Athari za tetemeko Ia ardhi huweza kuwa kubwa, wastani au ndogo kutegemea na ukubwa wa tetemeko, uimara wa majengo na miundombinu mingine, na hali ya asili ya jiolojia ya sehemu inayohusika. Zifuatazo ni baadhi ya athari za tetemeko a ardhi:
- Uharibifu wa mazingira na maeneo ya makazi: Tetemeko la ardhi linapotokea husababisha kupasuka kwa miamba na kuharibika kwa miundombinu kama barabara, reli na viwanja vya michezo. Pia, huweza kusababisha kubomoka kwa majengo, kwa mfano, katika nchi yetu ya Tanzania mnamo mwaka 2016 mkoani Kagera na mwaka 2019 mkoani Katavi, kulitokea matetemeko ya ardhi. Matetemeko hayo yaliharibu miundombinu ya barabara, majengo ya shule, hospitali, na makazi ya watu.
Picha: Tetemeko kagera 2016
- Mlipuko wa magonjwa: Tetemeko Ia ardhi husababisha kuharibika kwa miundombinu ya maji. Hii husababisha majitaka kusambaa na kuingia katika mifumo ya majisafi na hivyo kuyachafua. Maji haya ambayo siyo salama yakitumiwa na binadamu kwa kupikia, kunywa, kuogea na kusafishia vyombo, huweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya matumbo, kipindupindu na kuhara. Aidha, tetemeko Ia ardhi husababisha kutimka kwa vumbi na kufuka moshi ambao husambaa katika angahewa. Hali hii huweza kusababisha magonjwa ya macho na athari katika mfumo wa upumuaji.
- Mlipuko wa moto: Tetemeko la ardhi huweza kusababisha mlipuko wa moto ambao hutokana na kuharibika kwa miundombinu ya umeme, kulipuka kwa volkano au kugongana kwa mawe na hatimaye kutokea kwa moto. Moto huu mara nyingi huwa ni vigumu kuuzima kwa sababu ya kuharibika kwa miundombinu na hivyo kushindwa kufika katika maeneo yanayowaka moto.
- Kutokea kwa tsunami: Tetemeko Ia ardhi huweza kusababisha kutokea kwa mawimbi makubwa baharini ambayo huitwa tsunami. Mawimbi haya husambaa na kusafiri hadi katika fukwe za bahari ambapo husababisha maafa ikiwamo vifo vya watu na wanyama pamoja na uharibifu wa mali.
- Kuongezeka au kupungua kwa kina cha bahari: Tetemeko la ardhi linapotokea, husababisha kutikisika kwa sakafu ya bahari na hivyo kuhama au kuachana kwa miamba chini ya bahari. Hali hii huweza kusababisha kusambaa kwa volkano ambayo huganda na kupunguza kina cha bahari. Aidha, tetemeko la ardhi husababisha kubomoka kwa miamba iliyo pembezoni mwa bahari na hivyo kina cha bahari kuongezeka. Pia, kuachana kwa miamba iliyoko chini kwenye sakafu ya bahari kunaweza kusababisha kuongezeka kwa kina cha bahari.
Tetemeko la ardhi pia linasababisha kuinuka kwa miamba pembezoni mwa bahari.
(f) Husababisha vifo kwa viumbe hai: Matetemeko ya ardhi yamekuwa yakisababisha vifo kwa binadamu na viumbe hai wengine. Tetemeko linapotokea, huweza kubomoa majengo na kuharibu miundombinu. Vifusi vya majengo vinapoangukia watu au wanyama huweza kusababisha vifo. Kielelezo namba 1 kinaonesha baadhi ya athari za tetemeko Ia ardhi katika mazingira.
Tahadhari za kuchukua katika kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi
- Ni muhimu kuchukua tahadhari mbalimbali iii kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi.
- Tahadhari mojawapo ni kutoa elimu kuhusu namna ya kuepusha au kupunguza athari iwapo tetemeko Ia ardhi litatokea. Elimu hii ilenge kuwafikia watu wa rika zote yaani watoto, vijana, wenye mahitaji maalumu na wazee.
- Elimu hii pia izingatie chanzo, maeneo hatarishi na yenye historia ya kukumbwa na tetemeko mara kwa mara, madhara yatokanayo na tetemeko Ia ardhi na njia za kukabiliana nayo.
- Kituo cha kuratibu matetemeko ya ardhi kitumie vyombo vya habari na wadau mbalimbali katika kuelimisha jamii na kusambaza elimu kuhusu madhara ya tetemeko la ardhi.
- Wananchi waelimishwe kuhusu kujenga nyumba imara zenye uwezo wa kuhimili mitikisiko inayotokana na tetemeko la ardhi.
- Pia, idara za mipango miji zifanye tathmini ya ardhi kabla ya kugawa maeneo ya ardhi kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi.
- Pia, endapo tetemeko Ia ardhi limetokea au Iinaendelea kutokea unashauriwa kukaa mbali na majengo marefu, miti, nyaya na nguzo za umeme, fukwe za bahari na pembezoni mwa mito mikubwa.
- Kama uko ndani ya nyumba ingia chini ya meza au kitanda na ujifunike kichwa na mwili wako kwa mavazi mazito iii yakukinge na vitu vizito na vyenye ncha kali kama vioo.
- Pia, unaweza kukaa kwenye kona ya chumba kuepuka kuangukiwa na ukuta. Ukisikia tetemeko limetulia paza sauti kuomba msaada.
- Aidha, endapo tetemeko likikukuta nje ya nyumba unashauriwa kulala chini mita kadhaa mbali na nyumba au kimbia na uelekee katika maeneo ya wazi yaliyotengwa na serikali kama viwanja na mashamba makubwa.
Mlipuko wa volkano
- Ndani ya ardhi, chini kabisa ya uso wa dunia kuna joto kali sang na mgandamizo mkubwa wa miamba.
- Joto hill kali huweza kuyeyusha miamba katika eneo hilo na kuifanya iwe katika hali ya kimiminika cha moto mithili ya ujiuji uitwao magma.
Picha: Mlipuko wa volcano Kongo
- Mgandamizo unapozidi huisukuma magma ambayo hupenya katika nyufa zilizo katika tabaka za miamba na kutokeza nje ya uso wa dunia.
- Magma pia huweza kuishia chini ya ardhi kabla ya kutokeza juu ya uso wa dunia na kuganda. Magma hii ikitokeza juu ya uso wa dunia huitwa lava.
- Volkano huweza kutoka nje ya uso wa dunia kwa mlipuko au kwa kufuka taratibu. Mlipuko wa volkano unategemea kiasi cha joto katika miamba iliyo chini ya tabaka la ardhi, pamoja na nguvu ya msukumo au mgandamizo iliyoko chini ya ardhi.
- Magma hii huweza kutoka kwa mlipuko mkubwa na kuruka hewani mita kadhaa, kisha humwagika na kutiririka juu ya uso wa dunia kama Kielelezo namba 2 kinavyoonesha. Lava hii hutiririka na kutapakaa juu ya uso wa dunia na kuganda. Kitendo cha magma kutoka nje kwa kasi kubwa huitwa mlipuko wa volkano.
- Mlipuko wa volkano pia huambatana na kurusha jivu Ia volkano ambayo husambaa katika angahewa. Mlipuko wa volkano huwa na mchanganyiko wa gesi kama salfadioksidi ambayo ni hatari kwa maisha ya viumbe hai.
Oldonyo Lengai- Volcano hai
- Mlipuko wa volkano huweza kutoa lava inayotapakaa katika eneo dogo au kubwa na baadaye hupoa na kuganda, kisha hutengeneza mlima au mwinuko wa lava.
- Nchini Tanzania, ipo milima yenye asili ya volkano. Baadhi ya milima hiyo hulipuka mara kwa mara na huitwa milima yenye volkano hai kama vile mlima wa Oldonyo-Lengai uliopo mkoani Arusha.
- Milima mingine ni ile iliyowahi kulipuka zamani, lakini bado inaonesha dalili kwamba huenda ikalipuka katika miaka ijayo.
- Milima hii huitwa milima yenye volkano tuli kama vile mlima Kilimanjaro na mlima Meru. Pia, ipo milima ya volkano iliyokufa au volkano mfu. Milima hii haina dalili za kulipuka tena japo iliwahi kulipuka miaka ya zamani sang kama vile mlima Rungwe.
Athari za mlipuko wa volkano
Volkano inapolipuka juu ya use wa dunia husababisha athari mbalimbali kwa viumbe hai na mazingira kwa ujumla. Zifuatazo ni baadhi ya athari za mlipuko wa volkano:
- Vifo kwa viumbe hai: Volkano inapolipuka hurusha lava ambayo hufunika eneo Ia ardhi. Lava hiyo inaweza kuua viumbe hai kama vile wanyama, binadamu, na bakteria muhimu wa mfumo wa ikolojia. Pia, inaweza kukausha mimea.
- Matatizo ya kiafya katika mfumo wa upumuaji, macho na ngozi: Volkano inapolipuka hutoa moshi mzito, vumbi na majivu ambavyo huweza kusababisha matatizo ya kiafya kwa viumbe hai hususani wanyama na binadamu. Mfano, majivu yenye sumu yanaposambaa huweza kutua kwenye ngozi na kusababisha muwasho na kubabuka. Moshi mzito wenye gesi ya ukaa unaposambaa na kuvutwa na viumbe hai huweza kuathiri mfumo wa upumuaji na hata kusababisha vifo.
- Uharibifu wa mall kama vile miundombinu na makazi ya watu: Mlipuko wa volkano unapotokea kwa kiwango kikubwa hufunika miundombinu zikiwemo barabara kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 3 (a), reli na maeneo ya wazi ikiwamo viwanja vya michezo na uharibifu wa mall kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 3 (b).
- Uchafuzi wa vyanzo vya maji: Volkano huweza kutiririka katika vyanzo vya maji na kusambaza kemikali zenye sumu. Kemikali hizi huweza kusababisha magonjwa na vifo kwa viumbe hai kama binadamu, wanyama, mimea na wadudu. Aidha, volkano huweza kuziba vyanzo vya maji na kusababisha ukosefu wa maji.
- Kutikisika na kuporomoka kwa ardhi: Mlipuko wa volkano huambatana na kutikisika kwa ardhi ambako kunaweza kusababisha kutokea kwa maporomoko ya ardhi na tetemeko.
- Kutokea kwa janga la moto: Lava inaposambaa juu ya nyasi, huweza kusababisha muwako wa moto. Muwako huo unaweza kusababisha kutokea kwa janga Ia moto linaloweza kuunguza misitu na makazi ya watu.
(g) Athari kwa tabianchi: Majivu na gesi ya salfadioksidi hupunguza jotoridi duniani kwa kuakisi mwanga wa Jua. Pia mlipuko wa volkano unaweza kusababisha ongezeko la gesijoto angani, hivyo huchangia kusababisha mabadiliko ya tabianchi.
(h) Mawingu yatokanayo na majivu ya volkano na vumbi ni hatarishi kwa usafiri wa anga na huweza kuharibu injini za ndege.
- Licha ya kwamba mlipuko wa volkano una athari nyingi, lakini pia una faida kama vile; kuzalisha udongo wenye rutuba na udongo mpya wa asili, pamoja na kumwaga vipande vidogovidogo vya madini kama dhahabu na almasi kutoka ardhini. Pia, mlipuko wa volkano huweza kusababisha kutokea kwa chemichemi za maji na kupatikana kwa visiwa baharini.
Tahadhari za kuchukua katika kukabiliana na athari za mlipuko wa volkano
- Mlipuko wa volkano ni moja kati ya majanga ya asili ambayo yanahitaji umakini na maandalizi ya mapema kabla hayajatokea.
- Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, itoe elimu kwa wananchi juu ya athari za mlipuko wa volkano. Wananchi waelimishwe kuhusu madhara ya kujenga makazi yao karibu na maeneo au milima yenye asili ya volkano.
- Inashauriwa kujenga au kuanzisha makazi umbali wa takribani kilomita 50 kutoka kwenye vyanzo vya milipuko ya volkano.
- Aidha, mamlaka zinazohusika zitoe tahadhari mapema kuhusu viashirio vya mlipuko wa volkano kabla ya janga kutokea.
- Hata hivyo, endapo mlipuko wa volkano utatokea katika eneo unaloishi unashauriwa kukimbia na kwenda umbali mrefu ambako ujiuji wa volkano hautafika.
- Zingatia kuvaa barakoa (kichujahewa) iii usivute hewa yenye sumu itokayo katika moshi mzito wa volkano. Wakati unatembea kuelekea sehemu salama, epuka kukanyaga madimbwi ya maji au kupita katika mito na vijito vitokavyo milimani kwani huenda ukakanyaga ujiuji wa moto au maji ya moto yatiririkayo kutoka katika mlima unaolipuka volkano.
- Iwapo mlipuko wa volkano utatokea ukiwa ndani ya nyumba, unashauriwa kubaki ndani na kuhakikisha hakuna vitu vinavyoweza kukudondokea na kukudhuru hadi pale timu ya uokoaji itakapofika kukusaidia.
Maporomoko ya ardhi
- Maporomoko ya ardhi ni mmeguko wa ghafla wa mwamba au kipande cha ardhi kutoka katika mwinuko.
- Maporomoko ya ardhi huchochewa na nguvu ya uvutano. Kadiri mteremko unavyozidi kuwa mkali ndivyo kasi ya kushuka kwa mwamba au kipande cha ardhi inavyozidi kuongezeka. Kielelezo namba 4 kinaonesha maporomoko ya ardhi.
- Maporomoko ya ardhi husababishwa na vyanzo mbalimbali kama vile mlipuko wa volkano, tetemeko la ardhi, mvua kubwa, na mafuriko.
- Mlipuko wa volkano husababisha kutikisika kwa tabaka la juu la ardhi na hivyo huweza kukatika na kuporomoka. Hii inachangia sana kutokea kwa maporomoko ya udongo kwani ardhi iliyotikiswa huwa dhaifu na yenye mikatiko na nyufa nyingi.
- Hali hii huifanya ardhi ya maeneo haya kuporomoka kirahisi. Aidha, mitetemo ya ardhi inapotokea huharibu muunganiko wa udongo na miamba. Ardhi huwa dhaifu, hivyo kuwa rahisi kuporomoka. Mafuriko pia huchangia kutokea kwa maporomoko.
- Kiwango cha maji yaliyoko ardhini kinapoongezeka kutokana na mvua kubwa au kuyeyuka kwa barafu, uzito wa udongo huongezeka na kushikamana kwake hupungua.
- Kadiri kiasi cha maji kinavyozidi kufyonzwa na kuongezeka katika udongo, hupunguza uwezo wa udongo kushikamana. Hali hii husababisha maporomoko ya ardhi kutokea.
- Nchini Tanzania maporomoko makubwa ya ardhi yaliwahi kutokea mkoani Kilimanjaro, wilaya ya Same na Morogoro wilaya ya Kilosa mnamo mwaka 2014.
Athari za maporomoko ya ardhi
Maporomoko ya ardhi yanapotokea huweza kuleta athari mbalimbali. Athari hizi ni kama zifuatazo:
- Uharibifu wa miundombinu, mali na makazi: Maporomoko ya ardhi huweza kuharibu na kuziba barabara
Pia, huweza kuharibu reli, madaraja, nguzo za umeme na simu, mabomba ya mafuta na mifereji ya maji. Hali hii huweza kusitisha shughuli za uzalishaji mali kwa kipindi fulani. Aidha, maporomoko ya ardhi yanapotokea huweza kuharibu mali na makazi hivyo kuwaletea wananchi umaskini.
- Uharibifu wa mimea na vifo vya wanyama: Maporomoko ya ardhi yanapotokea huporomosha vifusi vya udongo ambavyo vinaweza kuwafunika wanyama na mimea katika maeneo ya bondeni. Hii huweza kusababisha vifo vya wanyama na kuharibu mimea katika eneo linalohusika.
- Kuondolewa kwa tabaka Ia udongo wenye rutuba: Maporomoko ya ardhi husababisha kuondolewa kwa tabaka Ia ardhi lenye rutuba na kurundikwa bondeni. Maeneo yaliyoondolewa tabaka Ia juu Ia ardhi hubaki bila rutuba hivyo kuathiri uoto na shughuli za -kilimo. Hali hii huweza kusababisha kutokea kwa baa Ia njaa katika eneo linalohusika.
Tahadhari za kuchukua katika kukabiliana na athari za maporomoko ya ardhi
- Zipo tahadhari ambazo mtu anapaswa kuzizingatia iii kupunguza kiwango cha kutokea kwa maporomoko na kukabiliana na athari zake.
- Tahadhari zinaweza kuchukuliwa kwa kupanda miti na mimea mbalimbali katika maeneo ya wazi na yenye mteremko mkali.
- Pia, kuzuia uvunaji hovyo na uchomaji holela wa misitu. Wananchi kutofanya shughuli za ujenzi wa makazi kwenye maeneo yenye mteremko mkali na kwenye mabonde.
- Kwa sababu kwa kufanya hivyo huchochea kuongezeka kwa athari zitokanazo na maporomoko ya ardhi. Aidha, mamlaka zinazohusika zinapaswa kutoa elimu kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na maporomoko ya ardhi na maeneo hatarishi.
- Pia, kuwahimiza wananchi kufuatilia vipindi vya utabiri wa hall ya hewa kupitia redio na televisheni iii kuchukua tahadhari stahiki.
- Wananchi wanapaswa kuzingatia sheria zinazohusu matumizi ya ardhi hasa katika maeneo yenye mteremko mkali.
- Mwananchi yeyote anapaswa kupata ushauri kutoka kwa wataaiamu endapo atataka kuishi na kufanya shughuli za kibinadamu kama vile uchimbaji madini na kilimo kwenye maeneo yenye mteremko mkali.
- Pia, inashauriwa kufukia mashimo na kupanda miti mara baada ya shughuli za uchimbaji madini kukamilika iii kupunguza athari zinazoweza kutokea kutokana na maporomoko ya ardhi.
- Mara baada ya kutokea kwa maporomoko ya ardhi, unashauriwa kuzibua mifumo ya maji ambayo itakuwa imeziba kutokana na uchafu kama tope na taka nyingine ngumu zinazoletwa na udongo.
- Ondoa kifusi, miti au takataka nyingine kwa kusafisha eneo ambalo limeathirika iii kulirejesha katika hall yake ya awali.
- Sawazisha tope na mrundikano wa udongo ulioporomoka ili kupata msawazo wa ardhi husika. Tunashauriwa kurejesha makazi yaliyoharibika katika hall yake ya awali.
Tsunami
- Tsunami ni neno Ia kijapani lenye maana ya "wimbi Ia bandarini". Tsunami ni mawimbi makubwa ya bahari yanayosababishwa na tetemeko is ardhi chini ya sakafu ya bahari au mitikisiko mingine ya dunia kama vile milipuko ya volkano na kuanguka kwa vimondo baharini.
- Tsunami pia husababishwa na kupishana kwa eneo kubwa la sakafu ya bahari pamoja na ujaribishaji na matumizi ya mabomu ya nyuklia.
- Tetemeko Ia ardhi au mitikisiko mingine ya dunia husababisha kutokea kwa mawimbi makubwa baharini ambayo husafiri na kusambaa kwa kasi katika eneo kubwa Ia bahari. Mitikisiko hii inapotokea hutengeneza nguvu katika sakafu ya bahari ambayo husababisha mawimbi makubwa juu ya use wa bahari.
- Mawimbi haya huanza kusafiri na kuongezeka nguvu kwa kasi kuelekea katika fukwe za bahari. Mawimbi ya tsunami yang nguvu na uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilomita 10 hadi 800 kwa saa, na huweza kudumu kwa wastani wa saa moja. Mawimbi haya huweza kufikia urefu wa mita 10 hadi 30.
- Tsunami inaweza kutokea muda wowote usiku au mchana. Bahari ya Pasifiki nchini Indonesia na Japan ni baadhi ya maeneo ambayo hupatwa na majanga ya tsunami mara kwa mara.
- Kutokea kwa matetemeko makubwa ya ardhi chini ya Bahari ya Pasifiki ndiyo chanzo kikubwa cha tsunami katika eneo hilo. Kielelezo namba 6 kinaonesha muonekano wa wimbi Ia tsunami.
Picha: tsunami
Athari zinazotokana na tsunami
- Vifo kwa wakazi na watumiaji wa maeneo ya fukwe za bahari: Mawimbi ya tsunami huathiri sang maeneo ya fukwe za bahari. Kwa mfano, tukio Is tsunami ambapo ni kubwa kuliko yote yaliyowahi kurekodiwa, lilitokea katika bahari ya Hindi, Mashariki mwa Asia, mnamo Disemba 26 mwaka 2004. Tukio hili lilihusisha nchi kama, Indonesia, Singapore, Malaysia na India katika Bara Is Asia, na linaloaminika kusababisha vifo vya watu zaidi ya 230 000 katika nchi 14. Athari hizi zilihusisha pia nchi za Afrika ya Mashariki ambapo takribani watu 11 nchini Tanzania na 1 nchini Kenya walipoteza maisha baada ya kusombwa na maji walipokuwa wakiogelea katika Bahari ya Hindi.
- Uharibifu wa makazi na miundombinu: Kutokana na mawimbi makubwa ya tsunami ambayo hugonga fukwe za bahari na kusambaa, maeneo ya makazi na miundombinu huathiriwa kama Kielelezo namba 7 kinavyoonesha. Hii ni pamoja na majengo ya makazi, hoteli na migahawa, vibanda vya huduma za utalii, barabara na viwanja vya michezo pamoja na maeneo mengine ya starehe. Pia, tsunami hubomoa reli na viwanja vya ndege pamoja na kuharibu vyanzo vya nishati ya umeme.
- Mafuriko na kuchafuka kwa vyanzo vya maji: Hali hii husababishwa na mawimbi makubwa ya maji yanayoletwa na tsunami katika fukwe za bahari. Maji haya husambaa na kujaa katika maeneo jirani na bahari na hivyo kusababisha mafuriko. Pia, maji haya huenea na kutuama katika maeneo mbalimbali ya makazi, hivyo kusababisha kuenea kwa magonjwa kama vile malaria, homa ya matumbo, kipindupindu na kuhara.
- Uharibifu wa makazi ya viumbe hai kama samaki na wanyama: Mawimbi ya tsunami yanapopiga katika maeneo ya kutagia mayai ya samaki kama vile matumbawe, huharibu na huathiri mazalia ya samaki. Hali hiyo inaweza kusababisha samaki kufa. Pia, mawimbi ya tsunami huweza kuharibu miundombinu ambayo inaweza kutiririsha sumu baharini na kuua viumbe wa baharini wakiwemo samaki. Kwa upande wa wanyama, tsunami inaweza kuathiri uoto ambao ni makazi ya wanyama na pia huweza kusomba wanyama na kufa.
- Kuharibu uoto wa asili: Mawimbi ya tsunami huweza kung'oa miti na mimea mingine. Hii husababisha kupoteza uasilia wa mwonekano wa eneo na hatimaye kuharibika kwa ikolojia katika eneo husika.
Tahadhari za kuchukua katika kukabiliana na athari za tsunami
- Tsunami haitokei mara kwa mara, ingawa inapotokea huweza kusababisha maafa makubwa.
- Zipo tahadhari ambazo mtu anapaswa kuzizingatia iii kupunguza kiwango cha kutokea kwa tsunami na kukabiliana na athari zake. Moja ya tahadhari hizo ni kudhibiti urutubishaji, ujaribishaji, matumizi ya mabomu ya nyuklia na vilipuzi katika bahari. Hii itasaidia kupunguza kiwango cha matetemeko yatokanayo na shughuli za wanadamu. Epuka kujenga au kuishi maeneo ya kando ya fukwe za bahari.
- Kama ujenzi unafanyika basi uzingatie ushauri wa kitaalamu kuhusu umbali sahihi kutoka fukwe za bahari na kina sahihi kutoka usawa wa bahari.
- Mamlaka inayohusika wakiwamo wataalamu wa jiolojia watoe tahadhari pindi to viashirio vya tsunami vinapojitokeza, kama vile, tetemeko Ia ardhi, na kupwa na kujaa kwa maji kusiko kwa kawaida.
- Hii iende sambamba na utoaji wa elimu kwa umma juu ya dalili za kutokea kwa janga Ia tsunami, madhara na jinsi ya kujikinga.
- Aidha, endapo tsunami imetokea katika eneo ulilopo, unashauriwa kujihifadhi kwa kusimama katika eneo lililoinuka. Kwa kufanya hivyo ni vigumu maji kukufikia na kukusomba, pia hurahisisha uokoaji.
- Epuka kujaribu kukatisha au kuogelea katika mikondo ya maji inayotiririka kurejea baharini, huenda mikondo hiyo ya maji ikawa bado ina nguvu na hivyo kukusomba.
Majanga ya moto
- Moto ni muwako ambao hutoa joto na mwanga. Moto pia huelezwa kuwa ni matokeo ya mgongano wa kikemikali kati ya kitu kinachoweza kuwaka, oksijeni na joto.
- Majanga ya moto ni miongoni mwa majanga yanayotokea juu ya use wa dunia, ambayo hutokana na mlipuko wa moto.
- Majanga haya yamekuwa yakitokea sehemu mbalimbali duniani na kusababisha madhara makubwa katika jamii. Majanga ya moto yanaweza kuwa ya asili au yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu.
- Majanga ya moto wa asili mara nyingi hutokea kwenye misitu minene mfano, msitu wa Amazon uliopo nchini Brazil na misitu ya upande wa Mashariki na Kaskazini Mashariki mwa jimbo Ia Victoria nchini Australia.
- Majanga haya hutokea hasa kipindi cha kiangazi ambacho huwa na joto kali. Chanzo cha moto wa asili chaweza kuwa milipuko ya volkano na umeme wa radi ambao ni chanzo kikubwa hasa katika maeneo ya misitu minene.
- Chanzo kingine cha moto wa asili ni joto kali kutoka angani ambalo husaidia moto kuwaka kwa urahisi. Umeme wa radi na joto kali kutoka angani husababisha kutokea kwa moto na kuunguza vumbi la mbao, majani makavu na nyasi.
- Moto huu huenea na kuchoma eneo kubwa Ia msitu.
- Mbali na vyanzo vya asili, majanga ya moto pia husababishwa na shughuli za binadamu, kama vile; uchomaji wa makusudi wa misitu, urinaji asali kwa kutumia moto, shughuli za uwindaji, uvutaji hovyo wa sigara na matumizi yasiyo sahihi ya nishati ya gesi, mafuta na umeme.
- Moto unaosababishwa na shughuli za binadamu mara nyingi hutokea mashambani, misituni, shuleni, kwenye maeneo ya makazi na biashara. Mfano wa majanga ya moto ya aina hii, ni ule uliotokea mwaka 2017 na kuteketeza soko Ia SIDO mkoani Mbeya, na kusababisha hasara kubwa na uharibifu wa mali na majengo ya biashara kama inavyoonekana katika Kielelezo.
- Janga lingine Ia moto lililosababishwa na shughuli za binadamu ni lile lililotokea mkoani Morogoro mwaka 2019 ambapo loll Ia mafuta lilianguka na kumwaga mafuta. Watu walipokuwa wakichota mafuta hayo ghafla kukatokea hitilafu katika mfumo wa umeme wa gari uliosababisha moto kulipuka na kusabisha vifo vya watu zaidi ya 100 na uharibifu wa mall na mazingira kama inavyoonekana katika Mfano mwingine ni moto ulioteketeza shule ya sekondari Mihayo, mkoani Tabora mwaka 2018.
Athari za majanga ya moto
Mato ni miongoni mwa majanga yenye uwezo mkubwa wa kusababisha madhara katika jamii. Zifuatazo ni athari za mato katika jamii:
- Husababisha vifo na ulemavu wa muda au wa kudumu kwa binadamu na viumbe wengine. Moto huathiri maisha ya binadamu na wanyama, kwa mfano, moto uliotokea Morogoro mwaka 2019 ulisababisha kupoteza maisha ya watu zaidi ya 100.
- Janga Ia moto huharibu mali na miundombinu kama vile, nguzo za umeme, visima vya mafuta na gesi, na kusababisha hasara kubwa miongoni mwa jamii husika. Moto uliotokea Morogoro mwaka 2019 ulisababisha kuungua kwa mali kama vile pikipiki, baiskeli na magari.
- Tabaka Ia juu la udongo kupoteza uwezo wa kufyonza na kuhifadhi maji kwa muda mrefu. Hii husababisha ardhi kuwa kame na yenye nyufa nyingi, hivyo kushindwa kuhifadhi maji. Ardhi hupoteza hali ya kushikamana na hivyo kuchochea mmomonyoko wa udongo na kutokea kwa maporomoko ya ardhi na mafuriko kwa urahisi.
- Kuongezeka kwa hewaukaa katika angahewa. Misitu inapoungua, hutoa moshi mzito wenye gesi ya kabonidioksidi ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gesijoto angani zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi.
- Kuharibu makazi ya wanyama pori na Bayoanuai. Majanga ya moto wa msituni huweza kuhatarisha maisha ya viumbe hai. Mfano mioto ya mara kwa mara kwenye hifadhi ya mlima Kilimanjaro na mbuga zingine za wanyama huharibu makazi ya wanyama na kusababisha vifo.
- Kusitishwa kwa huduma za kijamii kama shule, viwanja vya ndege, na hospitali. Hivyo, jamii husika huathirika.
- Kukosekana kwa ajira endapo mahali pa kazi patateketea kwa mato, mfano soko la Mwanjelwa na SIDO mkoani Mbeya, na soko la Samunge mkoani Arusha.
Kanuni za kuzima moto na uokoaji
- Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania namba 14 ya mwaka 2007 ya Zimamoto na Uokoaji, Jeshi Ia Zimamoto na Uokoaji lina wajibu wa kuzima na kuokoa maisha na mali, pamoja na kushughulikia dharura zozote ambazo si za kihalifu.
- Kanuni za uokoaji katika janga la moto zimetengenezwa kwa lengo la kusaidia pande mbili yaani, mwokoaji na mwokolewaji.
- Pamoja na hayo ili kufanikisha jukumu hill jeshi linashirikisha wananchi. Zifuatazo ni kanuni za kufuata iii kuokoa mall na maisha ya watu wakati wa janga la moto:
- Piga kengele, king'ora au mayowe kuomba msaada na kuashiria watumiaji wengine wa jengo waliomo ndani kuwa kuna moto.
- Toka nje na piga simu namba ya dharura ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ill kuweza kupata msaada zaidi. Namba hiyo ni 114.
- Inawezekana kuanza kuzima moto kwa kutumia vizimia moto vilivyopo endapo to vinalingana na asili ya moto huo.
- Kumbuka kwamba, hairuhusiwi kuzima moto ambao chanzo chake ni umeme kabla ya kuzima swichi kuu. Iwapo imeshindikana kuzima swichi kuu tumia mchanga mkavu, mtungi wa hewa ya ukaa au poda kavu kuzima moto.
- Watu ambao hawashiriki katika uzimaji wa moto wanashauriwa kukaa sehemu maalumu ya kukusanyikia ill kuwezesha kufahamu kwa urahisi nani yupo na nani hayupo. Ni muhimu kuhakiki watu wote kama wapo ili kuwa na taarifa kamili punde waokoaji wa Zimamoto watakapowasili.
- Unapozima moto hakikisha miango upo nyuma yako na uwe wazi iii ukishindwa kuzima moto uweze kutoka kwa urahisi.
- Moshi unapozidi, jaribu kutambaa kwa magoti na mikono ukiwa unaelekeza use chini iii kuzuia moshi wenye sumu kuingia puani kwa wingi, ikiwezekana tumia kichuja hewa na vumbi (barakoa).
- Hairuhusiwi kurudi ndani ya jengo linalowaka moto kama hall bado si salama.
(i)Iwapo jitihada za kutoka nje zimeshindikana kabisa, funga miango na
ziba sehemu ya chini ya miango kwa kutumia kitambaa kilicholowa.
(j) Simama kando ya dirisha na punga kitambaa cheupe kuashiria uwapo wako na kuomba msaada wa kutoka kuokolewa.
Namna ya kushiriki katika kuzuia janga Ia moto
- Katika kuzuia majanga ya moto, njia mbalimbali zimekuwa zikitumika kulingana na mahali na chanzo cha moto.
- Unashauriwa kuzingatia kanuni za kimazingira na tahadhari zilizowekwa iii kuepuka kusababisha moto. Mfano, uvutaji wa sigara katika maeneo hatarishi, kama vile kwenye vituo vya mafuta, maghala ya chakula, vyombo vya usafiri na katika misitu mikubwa.
- Pia vichungi vya sigara vyaweza kuzusha moto endapo havikuzimwa ipasavyo na kutupwa katika vyombo maalumu kwa ajili hiyo.
- Ni vema kuhakikisha vifaa vyote vya umeme na gesi ni imara na vinafaa kwa matumizi kabla ya kuvitumia.
- Epuka kutumia vifaa vya umeme visivyo na ubora au vilivyochakaa. Matengenezo yote yanayohusu umeme na gesi yafanywe na mtaalamu anayehusika.
- Tunashauriwa kutumia vifaa vya umeme vilivyoidhinishwa na kutambulika kimataifa na kitaifa kwa ubora, mfano wa vifaa hivi ni kama, pasi, mtungi wa gesi, birika Ia umeme, simu za viganjani, redio, runinga na majokofu. Inashauriwa kufanya ukaguzi wa mfumo wa umeme kwenye majengo mara kwa mara.
- Vilevile, unashauriwa kuwa makini na matumizi yote yanayohusisha moto ulio wazi kama vile mshumaa, kibatari na jiko Ia mkaa.
- Tunapaswa kuwa na vifaa kinga dhidi ya radi, vizimia moto na viashirio vya moto. Wakulima wanashauriwa kuepuka kuwasha moto shambani wakati wa upepo mkali na nyasi zikiwa kavu sana ill kuzuia moto kusambaa.
- Kuhakikisha uwapo wa miundombinu ya barabara au njia zinazorahisisha ufikaji wa eneo endapo moto utatokea. Elimu itolewe kwa jamii iii kufahamu wajibu na namna ya kukabiliana na janga la moto.
- Maeneo maalumu yatengwe kwa wafugaji ili kupata malisho ya mifugo yao kwa urahisi na kuepukana na tabia ya kuchoma misitu ill kupata malisho ya mifugo yao. Elimu kuhusu urinaji bora na salama wa asali itolewe.
- Warinaji waelekezwe njia bora kama kutumia bomba la moshi au kifaa cha moshi kufukuza nyuki badala ya moto ambao ni hatari kwa mazingira.
- Uchomaji holela wa taka pia ni chanzo cha moto, inashauriwa taka zichomwe katika maeneo maalumu, mbali na vitu vinavyoweza kushika moto kwa haraka kama gesi, mafuta, pumba za mazao na mabaki ya shughuli za useremala.
- Shughuli za uchomeleaji vyuma zifanywe kwa tahadhari mbali na vitu vinavyoweza kushika na kusambaza moto kama vile karatasi, mafuta, mbao na nguo.
- Vilevile, uchomaji wa mkaa upate kibali kutoka mamlaka inayohusika, pamoja na kupewa elimu ya kutosha jinsi ya kutumia teknolojia bora ya uchomaji mkaa.
- Wananchi waelezwe umuhimu wa kuzima mabaki ya moto baada ya kufukua mkaa au kupika. Moto wa mkaa huzimika taratibu hivyo ni muhimu kuzima mabaki hayo.
- Kwa upande wa shule, kanuni hapo juu zinapaswa kuzingatiwa. Udhibiti wa kutumia mishumaa na vibatari unahitajika, pia kutoruhusu kutumia vifaa vya umeme kama hita kwenye mabweni au kujiunganishia umeme kiholela.