?> URAIA STANDARD SEVEN EXAMS SERIES
URAIA STANDARD SEVEN EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UMAHIRI KWA SHULE ZA MSINGI

UPIMAJI DARASA LA SABA MTIHANI WA MWIGO

URAIA NA MAADILI

2024

MAELEKEZO:

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali Sita (6) 

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu 

3. Majibu yote yaandikwe katika karatasi hii 

4. Tumia kalamu ya wino wa rangi ya bluu au mweusi 

5, Simu za mikononi na vifaa vingine visivyohitajika haviruhusiwi katika rhumba cha mtihani. 

6. Andika kwa usahihi Jina lako na Jina la Shule kwenye sehemu ulizopewa. 

SEHEMU A:

1. Chagua herufi ya jibu sahihi na andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa. 

i) Chombo cha juu kabisa cha uongozi katika Halmashauri ya wilaya, mji au manispaa ni 

(a) kamati ya kudumu 

(b) baraza la madiwani 

(c) kitengo cha sheria 

(d) mkurugenzi 

(e) mipango na takwimu 

 ii) Ni ishara gani inayoonyesha kwamba Taifa limepatwa na msiba mkubwa? 

(a ) bendera ya CCM kupepea nusu mlingoti 

(b) bendera ya Taifa kupepea nusu mlingoti 

(c) bendera ya shule kupepea nusu mlingoti 

(d) bendera ya CHADEMA kupepea nusu mlingot 

(e) bendera ya Taifa kupandishwa 

iii) Maruma, anaishi na baba, bibi, shangazi yake Sinda pamoja na bibi yake kalamu. Je, Maruma anaishi katika aina gani ya familia? 

(a) familia ya awali 

(b) familia ya mtoto yatima 

(c)familia ya mzazi mmoja 

(d) familia pana 

(e) familia ya baba, mama na watoto 

iv) Mimi ni miongoni mwa alama za Taifa la Tanzania. Ninatumika kuonyesha amani, upendo, umoja na kuitambulisha Tanzania kama nchi huru, mimi ni nani? (a) bendera ya Taifa 

(b) fedha ya Tanzania 

(c) ramani ya Tanzania 

(d) nembo ya Taifa 

(e) mwenge wa uhuru 

 v) Kwa mujibu ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekehisho mwaka 2014. Kwenye sheria hil ufuatao ni wajibu wa mtoto isipokuwa; 

(a) kuwatil wazazi wake 

(b) kutunza na kulmarisha mila na desturi 

(c) kufanya kazi kwa ajili ya kusaidia familia 

(d) kuhudumia jamii yake na Taifa 

(e) kuwanyanyasa watoto katika mazingira yote 

vi) Ni nani kati ya wafuatao sio miongoni mwa watu wenye mahitaji maalumu; 

(a) mwenye ulemavu wa macho

(b) mwenye ulemavu wa akili 

(c) masikini 

(d) mzee 

(e) mgeni 

vii) CCM na CHADEMA vilishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020; Je, ni chombo gani kilisimama uchaguzi huo? 

(a) TAKUKURU 

(b) TARURA 

(c) Tume ya taifa ya uchaguzi 

(d) Tume ya Taifa ya upelelezi 

(e) utawala bora 

viii) Elimu ya zimamoto na uokoaji ni muhimu kutolewa kwa wanajamii iii kukabiliana na majanga ya mato. Je ni namba gani ya dharura hupigwa wakati wa tukio la moto; 

(a) 116 

(b) 113 

(c) 114 

(d) 100 

(e) 102 

ix) Mwenyekiti wa vikao vya baraza la mawaziri ni nani? 

(a) Rais 

(b) makamu wa Rais 

(c) Rais wa Zanzibar 

(d) waziri mkuu 

(e) jaji mkuu 

x) Shughuli mbalimbali za kibinadamu zinachangia uharibifu wa mazingira zifuatazo ni shughuli za utunzaji wa mazingira isipokuwa; 

(a) kupanda miti sehemu zisizo na miti 

(b) kupanda miti ambapo kulikuwa miti 

(c) kukata miti bila kupanda miti 

(d) kupanda miti karibu na vyanzo vya maji 

(e) kilimo cha umwagiliaji 

2. Oanisha vifungu vifuatavyo kwa kuandika herufi za vifungu vya maoeno au majibu kwenye jedwali Ia majibu 

KIFUNGU A

KIFUNGU B: 

  1.                     Ngoma ya kikabila inayochezwa ili kuhamasisha ari ya kufanya kazi
  2.                   Faida ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana
  3.                 Umri sahihi wa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  4.                 Mazungumzo yanayoongozwa na mtu mwenye ujuzi wa kutoa mwongozo na kutatua matatizo au changamoto
  5.                   Utawala wa sheria kama moja ya misingi ya demokrasia

 

A. Miaka 55 na zaidi 

B. Gobogobo toka ardhi ya wasukuma 

C. Kuwasaidia vijana kufanya maamuzi sahihi 

D. Miaka 40 na zaidi 

E. Kunasihi au kutoa ushauri nasaha 

F. Hakuna aye juu ya sheria 

G. Kusababisha momonyoko wa maadili 

H. Mnasihi Lizombe kutoka Songea 

J. Inapunguza ari ya kuwa mzalendo 

 

 

3. Jaza nafasi zilizoachwa wazi

i) Bunge.la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa na Spika ambaye huchaguliwa 

na ……………… 

ii) Kuna sura ngapi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?   

iii) Ni yupi kati ya viongozi wa shule ana wajibu wa kusimamia shughuli za kila siku shuleni? 

iv) Kila mhimili wa serikali una umuhimu na majukumu yake. Ni mhimili upi wa serikali unashughulika na miswada iliyopendekezwa?  

v) Mavazi ya kitamaduni hubeba utambulisho wa jamii fulani. je, vazi gani huvaliwa na wanawake wa kabila Ia Kigogo?  

SEHEMU B: 

4. Jaza taarifa au nafasi zilizoachwa wazi kwenye jedwali lifuatalo 

Na.

TAASISI YA UMOJA WA MATAIFA

KAZI INAYOFANYA

1

UNESCO

…………………………….

2

 

CHAKULA NA KILIMO

3

UNHCR

……………………….

4

……………………….

WAFANYAKAZI ULIMWENGUNI

5

WHO

………………………………………

 

5. Malizia maelezo yafuatayo kwa usahihi 

i) Iwapo Rais aliyepo madarakani akifariki, ni taratibu zipi za kisheria zitachukuliwa kujaza nafasi yake?   

ii) Ni lini Tanzania ilifanya uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi? 

iii) Ni katika jiji gani kuna makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki? 

iv) Afisa Mtendaji wa Kata anapatikanaje?  

 v) Ni chombo kipi maalumu kina wajibu wa kuwalinda raia na mall zao nchini Tanzania? 

SEHEMU C: 

6. Jifunze kwenye picha ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo.

  1.        Ni awamu ipi ya Urais nchini Tanzania ilitumikiwa au kuongozwa na kiongozi ianayeonekana kwenye picha?  
  2.      Ni yupi kati ya Marais sita wa Tanzania alimfuata kiongozi huyo baada ya kumaliza muda wake?
  3.    Ni hatua ipi muhimu ya kujenga uchumi ilichukuliwa au kuruhusiwa na kiongozi huyo kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake?
  4.    Kiongozi aliyeonyeshwa pichani aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ni yupi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wakati huo?
  5.      Sasa hivi kiongozi huyo ni hayati, ni tarehe ipi yalifanyika mazishi yake kitaifa huko Unguja baada ya kupewa heshima za mwisho na watanzania? 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 109

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

JARIBIO LA KUJIPIMA NUSU MUHULA WA KWANZA 2024 

                         SOMO: URAIA NA MAADILI DARASA: VII 

SEHEMU A (ALAMA 20) 

1. Katika kipengele cha i-x chagua herufi ya jibu sahihi 

  1. Ofisa mtendaji wa kata ndiye mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri katika ngazi ya kata. Je, hupatikanaje? A. kwa kuteuliwa na mkurugenzi B. kwa kuteuliwa na diwani C. kwa Kuchaguliwa na wenyeviti wa mitaa D. kwa kuchaguliwa miongoni mwa watendaji wa mitaa E.kuajiriwa na serikali [ ]
  2. Jambo lipi sio huduma inayoweza kutolewa kwa watu wenye mahitaji maalum? A. uadilifu B. msaada wa kisheria C. makazi D. msaada wa kiafya E. ushauri [ ]
  3. Migogoro na mapigano katika jamii ni athari zinazosababishwa na nini? A. kukosekana kwa wasomi B. mahusiano mabaya C. kuwepo kwa matajiri D. ukame E. mafuriko [ ]
  4. Seleman ni mwanafunzi wa darasa la V katika shule ya msingi Mawazo, amebaini kuwepo kwa vitendo visivyofaa shuleni kwao. Utamshauri atumie njia ipi ili kufikisha taarifa au maoni kwa uongozi wa shule? A. mkutano wa wazazi B. sanduku la posta C. sanduku la maoni D. ubao wa matangazo E. aende kituo cha polisi [ ]
  5. Mtaa wa Kihodombi una barabara, zahanati pamoja na shule. Je, kwa jina moja tunaitaje? A. miundombinu ya serikali B. mali za Rais C. miundombinu ya jamii D. rasilimali E. majengo ya umma
  6. Mwongozo unaohusu mbinu za kupanga mipango ya maendeleo ya shule hutumiwa na nani? A. serikali ya mtaa B. uongozi wa shule C. wazazi na walezi D. mwalimu mkuu E. kamati ya shule [ ]
  7. Mkurugenzi wa halmashauri ana majukumu yafuatayo isipokuwa;- A. kusimamia shughuli zote za maendeleo katika halmashauri B. kusimamia shughuli za uchaguzi mkuu katika eneo lake C. kuwa katibu wa vikao vya baraza la madiwani D. kuwasimamia wakuu wa idara katika halmashauri E. kuwawakilisha wananchi katika vikao vya halmashauri [ ]
  8. Ni kwa namna gani mwanafunzi anaweza kupata ufafanuzi wa jambo linalomtatiza wakati wa vipindi darasani? A. kusoma kwa bidii B. kusikiliza upya C. kuandika nukuu za somo D. kuuliza maswali E. kuwasilisha maoni [ ]
  9. Wavuti ambapo watu huujumuishwa pamoja na kutumiana ujumbe au kuwa na nijadala kupitia simu za mkononi au kompyuta huitwaje? A. TEHAMA B. mawasiliano C. mitandao ya kijamii D. uwajibikaji E. teknolojia [ ]
  10. Shule inamahitaji mbalimbali, lipi kati ya haya yafuatayo si miongoni mwa mahitaji ya shule? A. chakula B. fedha C. ardhi D. watoto wa matajiri E. maji [ ]

2. Oanisha kipengele kutoka sehemu A na kipengele kutoka sehemu B ii kupata maana sahihi, kisha andika herufi ya jibu sahihi. 

3. Tumia maneno uliyopewa katika kisanduku cha maneno kujibu kipengele cha i-v 

Kiranja mkuu, uwajibikaji, 114, udadisi, mwanasheria mkuu, uvumilivu, 113,ustahimilivu, ubishi  

  1. Kim ana tabia ya kuhoji kila kitu wakati wa kujifunza darasani au nje ya darasa
  2. Kiongozi anayepatikana kwa njia ya kidemokrasia 
  3. Namba inayotumika kutoa taarifa kwa jeshi la Zimamoto pindi janga la moto linapotokea 
  4. Hayati Lowasa alijiuzulu nafasi ya Waziri mkuu kutokana na kashfa ya kampuni ya Richmond
  5. Manka ni kijana anayeweza kuhimili mambo mazito bila ya kulalamika. Kwa maneno mengine tungeweza kusema Manka ana tabia ipi? 

SEHEMU B (ALAMA 20) 

4. Umepewa vipengele vya mpangokazi wa kujitolea, tumia herufi A-E kuzipanga sentensi hizo kwa kuzingatia mpangilio wa vipengele hivyo. 

A. Malengo B. Muda C. Mahitaji D. Utekelezaji E. Tathmini 

  1. Miche ya matunda na kivuli, samadi na majembe 
  2. Je, miche na maua yaliyopandwa imetunzwa vyema?
  3. Kuboresha mazingira ya shule yetu.
  4. Wanafunzi kuandaa maeneo kwa ajili ya kupanda miti, kulima eneo hilo, kukusanya samadi, kupanda na kuimwagilia kila siku
  5. Kufikia mwezi Aprili shule yetu iwe na miti ya matunda na kivuli yakutosha

5. Katika kipengele cha i-v andika jibu lako kwa maelezo mafupi

  1. Mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa yamekuwa na changamoto mbalimbali. Zitaje tunu mbili za taifa ambazo zinaweza kutumiwa katika mapambano hayo. na 
  2. Ni muhimu kila shule kufanya vikao vya baraza la wanafunzi ili kuruhusu kila mwanafunzi kutoa maoni yake. Je,nani huwa mwenyekiti wa baraza la wanafunzi?
  3. Ikiwa wewe ni mwanafunzi wa darasa la VII ambaye umepata elimu ya Uraia na Maadili; ni nini utapaswa kufanya katika matukio haya?
  1. Unapowakosea wengine bila kujua 
  2. Unapokosewa na wengine kwa bahati mbaya 
  1. Utamsaidiaje mwanafunzi mwenzako mwenye tabia ya kugombana na rafiki zake?
  2. Tarehe 19.03.2021 Tanzania ilishuhudia kuandikwa historia mpya ya kuapishwa kwa Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuambiea;-
  1. Nini kilitokea na kupelekea Dr. Samia Suluhu Hassan kuapishwa na kuwa Rais?
  2. Ikiwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hufanyika kila baada ya miaka mitano, je, ni lini Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi huo kama Rais aliyopo madarakani aliapishwa mwaka 2021?

SEHEMU C (ALAMA 10) 

6. Chunguza kwa makini picha ulizopewa kisha tumia picha hizo kujibu kipengele cha i-v 

  1. Picha hii inawakilisha baadhi ya vitu ambavyo hulitambulisha taifa letu kwa mataifa mengine. Je, kwa jina moja huitwaje?
  2. Ni alama ipi kati ya hizo hutumika kama mhuri wa nyaraka za serikali?
  3. Mwenge wa uhuru hukimbizwa nchi nzima kila mwaka kwa lengo la kukagua miradi yote inayotekelezwa na serikali. Je, kilele cha mbio za mwenge huo huwa ni tarehe ngapi?
  4. Ikiwa umeona shuleni kwenu bendera ya taifa inapepea nusu mlingoti;

a). Je, inakua inaashiria nini?  

b). Ni nani mwenye mamlaka ya kutoa tamko la bendera kupepea nusu mlingoti?  

v. Je, picha ya twiga huashiria uwepo wa nini nchini kwetu?  

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 99

 

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA SHULE ZA MSINGI

NUSU MUHULA WA PILI

AGOSTI – 2023 

SOMO: URAIA NA MAADILI 

JINA ____________________________________TAREHE_________________ DRS 7

MUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una jumla ya maswali arobaini na Tano (45)
  2. Jibu maswali yote katika kila sehemu
  3. Soma maelekezo kabla ya kujibu maswali
  4. Swali la 1 – 40 chagua jibu sahihi na swali la 41 – 45, jibu maswali katika nafasi uliopewa.
  5. Tumia kalamu ya bluu na nyeusi
  6. Simu za mkononi, vikokotozi, na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU: A

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichowekewa

  1. Dola ina mihimili mikuu mitatu ambayo ni _____ A. serikali, bunge na mahakama B. Rais, waziri mkuu na spika C. Rais, bunge na mahakama D. Rais, diwani na spika                                                                                [                            ]
  2. Namba gani ya simu hutumika kutoa taarifa ya rushwa TAKUKURU? A. *1134# B. *113# C. *114# D. *103# [     ]
  3. Mtendaji mkuu katika kamati ya shule ni _____ A. wazazi B. wajumbe C. Mwalimu mkuu D. Mwenyekiti      [       ]
  4. Rushwa inaweza kugawanyika katika makundi mawiliambayo ni _____ A. rushwa ya ngono na rushwa fedha B. rushwa ya taasisi za umma C. rushwa ya kisiasa nay a kijamii B. rushwa kubwa na rushwa ndogo                    [       ]
  5. Kulipa kodi ni wajibu wa kila _____ A. MtanzaniaB. Mfanyabiashara C. Mtumishi wa serikali D.Mjasiriamali [      ]
  6. _____ ni kitendo cha mtu kufanya jambo kinyume na anavyosema. A. ufisadi B. unafiki C. uadui D. uhalifu [          ]
  7. _____ ni vitu muhimu na vya thamani vinavyomilikiwa na nchi. A. pesa B. miundombinu C. rasilimali D.viwanda               [               ]
  8. _____ chombo chenye jukumu la kutangaza mshindi wa nafasi ya Urais. A. mahakama B. dola C. bunge D. tume ya Taifa ya uchaguzi                                                                                                                                     [            ]
  9. Kazi kuu ya Bunge ni _____ A. kutunga sheria B.kutafsiri sheria C. kumchagua waziri mkuu D. kutoa siri za serikali    [            ]
  10. Mfumo wa utawala unaotumika Tanzania ni wa__ A. kiimla B. kidemokrasia C. kidikteta D. kifisadi [            ]
  11. Uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine ya kiafrika umekua kutokana na nini? _____ A. utunzaji wa mazingira B. jumuiya zilizopo C. utandawazi D. uhusiano wa michezo                                                 [            ]
  12. Uwezo wa kukabiliana na changamoto huitwa_____ A. uadilifu B. kipaji C. kuaminika D. ujasiri       [            ]
  13. Rais John Pombe Magufuli ni wa awamu ya ngapi hapa Tanzania? _____ A. 3 B. 4 C. 5 D. 6              [            ]
  14. Moja ya alama za Taifa la Tanzania ni pamoja na _____ A. bendera ya Taifa B. bendera ya Rais C. wimbo wa shule D. ramani ya shule                                                                                                                       [            ]
  15. _____ ni uharibifu au wizi wa mali alizokabidhiwa mtu. A. ufisadi B. riba C. ubadhirifu D. ufujaji     [            ]
  16. _____ ni hali ya kutetea jambo bila kutetereka. A. ukorofi B. msimamo C. utundu D. ukali           [            ]
  17. Muktadha ni ____ yanayosababisha mahali jambo lilikofanyika. A. maeneo B. mahali C. mazingira D. chuo   [    ]
  18. Lipi kati ya yafuatayo hutambulisha marafiki wema? _____ A. kuishi eneo moja B. kusoma shule moja C. kulala pamoja D. tabia njema na upendo                                                                                                 [            ]
  19. Moja kati ya hizi si athari za rushwa katika jamii _____ A. kuongezeka kwa gharama za kiutawala B. kushindwa kufikia kiwango cha juu cha uaminifu C. kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato D. serikali kushindwa kufika mlengo yake                                                                                                                                                     [            ]
  20. Moja ya njia za kupapambana na matumizi mabaya ya mali za umma ni _____ A. kuelimisha watu B. kuwaajiri watu C. kuwapa watu fedha nyingi D. serikali kutotimiza wajibu wake.                                                 [            ]
  21. Watu wanaoishi katika sehemu Fulani wanaitwa _____ A. wateja B. wakazi C. makazi D. walowezi      [            ]
  22. Maneno yaliyomo katika ngao ya Taifa ni _____ A. umoja na nguvu B. uhuru na umoja C. uhuru  na kazi D. uhuru na Amani                                                                                                                              [            ]
  23. Raia mwenye umri wa miaka kumi na tano _____ A. haruhusiwi kupiga kura B. anaruhusiwa kupiga kura C. anagombea udiwani D. anaweza kujiandikisha kugombea Urais                                                         [            ]
  24. Utii wa sheria _____ A. haubagui kiongozi au mwananchi B. bila shuruti haiwezekani C. unasababisha uchelewashaji wa majukumu D. unawahusu viongozi                                                                             [            ]
  25. Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina sura ngapi? _____ A. 9 B. 10 C. 11 D. 12                  [            ]
  26. Uhuru wa kutoa maoni ni moja ya nguzo za _____ A. kutii sheria B. uwajibikaji C. demokrasia D. utawala [        ]
  27. Uhuru wa mtu kuishi mahali popote nchini ni mfano wa nini? ______ A. haki za binadamu B. njia za kupata maadui wengi C. mbinu za kuzuia uzururaji D. hakuna jibu sahihi                                                                   [            ]
  28. Umoja wa mataifa ulianzishwa mwaka _____ A. 1945 B. 1991 C. 1997 D. 1977                                    [            ]
  29. Uhusiano wa Tanzania na Kenya umesaidia _____ A. kuboresha uchumi wa nchi hizo mbili B. kuporomosha uchumi wa nchi C. kuzua vita D. kuongeza uadui                                                                                             [            ]
  30. _____ ni chombo chenye mamlaka ya kuendesha utawala au siasa ya nchi. A. Dola B. Bunge C. Serikali D. Diplomasia                                                                                                                                                  [            ]
  31. Mkusanyiko wa sheria ambazo huwezesha serikali kutawala huitwa ___ A. katiba B. kanuni C. sheria D. dira[   ]
  32. _____ ni mambo muhimu kwa maendeleo ya nchi yeyote ile. A. wasomi wengi B. ardhi na watu C. ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora D. fedha na mikopo                                                                                [            ]
  33. Mji mkuu wa nchi ya Nigeria ni upi? _____ A. Lagos B. Abuja C. Cairo D. Biafra                            [            ]
  34. Azimio la Arusha hapa Tanzania lilianzishwa mwaka _____ A. 1985 B. 1967 C. 1977 D. 1997            [            ]
  35. Mwenge wa Uhuru uliwashwa mwaka 1961 katika kilele cha mlima _____ A. Meru B. Kilimanjaro C. Usambara D. Rungwe                                                                                                                                                    [            ]
  36. Viongozi wafuatao huteuliwa na Rais isipokuwa _____ A. mkuu wa mkoa B. katibu tawala wa mkoa C. waziri mkuu D. diwani                                                                                                                          [            ]
  37. Mtu anyetaka kugombea nafasi ya ubunge sharti awe na sifa zifuatazo isipokuwa _____ A. Raia mwenye umri usiopungua miaka 21 B. anajua kusoma na kuandika C. awe na akili timamu D. aliyewahi kuwa diwani  [      ]
  38. Alama ya Taifa inayoonesha Amani na upendo wa watu wa Tanzania ni _____ A. bendera ya Rais B. mwenge wa uhuru C. bendera ya Taifa D. ngao ya Taifa                                                                              [            ]
  39. Chombo cha serikali kinachoshughulika na kuamua kesi kinaitwa _____ A. bunge B. mahakama C. baraza la kata D. Tume ya Taifa                                                                                                                                        [            ]
  40. Ni lini Tanganyika ilikuwa  Jamhuri? _____ A. 26/4/1964 B. 9/12/1961 C. 9/12/1962 D. 5/12/1967     [            ]

SEHEMU: B – Jibu maswali yafuatayo kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi.

  1. Kauli mbiu ya Watanzania iliyomo kwenye nembo ya Taifa ni __________________________________________
  2. Utamaduni ni ________________________________________________________________________________
  3. Taja nguzo tatu za Dola
  1. ______________________________
  2. ______________________________
  3. ______________________________
  1. Kirefu cha neno “TAKUKURU” ni ___________________________________________________________
  2. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika mwaka __________________________________________

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 79

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA SEPT 2022

URAIA NA MAADILI DARASA LA SABA. 

 

  1. Kila nchi inaaminika kwa kuwa na amani na utulivu na inaffuata misingi ya demokrasia iliyowekwa duniani. Ili nchi iwe na demokrasia ya kweli inatakiwa iwe na ________(a) mfumo wa chama kimoja cha siasa (b) mfumo wa vyama vingi vya siasa (c) kutawaliwa kijeshi (d) mapinduzi ya mara kwa mara
  2. Kiongozi mkuu wa serikali katika wilaya ni ____(a) mkurugenzi wa wilaya (b) katibu tawala (c) mkuu wa wilaya
  3. Bunge haliongozwi kiholela holela. Shughuli zake husimamiwa na Spika wa bunge. Ila za uongozi wan chi husimamiwa na kiongozi gani? (a) waziri mkuu (b) makamu wa Rais (c) Jaji kiongozi (d) mwanasheria mkuu
  4. Kuna msemo unaosema kuwa “Rushwa ni adui wa haki”.Chombo kinachopambana na watu wanaokengeuka kauli hii kinaitwaje? (a) tume ya uchaguzi (b) TANESCO (c) TAKUKURU (d) TBC
  5. Raisi wa kwanza baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini Tanzania alichaguliwa mwaka gani?(a) 1962 (b) 1992 (c) 1995 (d) 2000
  6. Mpaka sasa Chama Cha Mapinduzi ndiyo mama lao katika kila chaguzi tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini, hivyo basi tunaweza kusemaje kuhusu kauli hii? (a) chama cha upinzani (b) kisichofuata katiba ya nchi (c) humiliki vitu vyote isipokuwa jeshi na elimu (d) chama Tawala
  7. Kwa Tanzania bara ni msimamizi wa shughuli zote za serikali. Je Zanzibar ni nani?(a) waziri kiongozi (b) makamu wa rais (c) jaji kiongozi (d) meya wa jiji
  8. Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji au Halmashauri ya jiji huitwa___ (a) mkurugenzi (b) mratibu (c) meya (d) mrajisi
  9. Kelvin alimuua mkewe pasina kukusudia. Baada ya kesi yake kusikilizwa kwa kina Kelvini alifungwa jela. Taasisi gani ilifunga Kelvin?(a) mahakama ya mwanzo (b) mahakama ya wilaya

(c) mahakama ya Rufaa (d) Mahakama kuu

  1.                   Alama ya mke na mume iliyoko kwenye ngao ya Taifa huwakilisha ____ (a) jinsia (b) ubaguzi

(c) umoja wetu (d)Taifa mchanganyiko

  1. Mwaka ujao tunatarajia kufanya Sensa ya makazi na watu ka kawaida ya nchi yetu.Kabla ya sensa ya mwaka kesho iliyotangulia ilikuwa mwaka gani? (a) 1992 (b) 2012(c) 2002 (d) 1982
  2. Mwenge wa uhuru ni katika alama za nchi yetu. Mwenge huu ulianza kuimulika nchi yetu kwa mara ya kwanza mwaka gani?(a) 9.12.1961 (b)9.12.1962 (c) 1.5.1964 (d) 9.10.1963
  3. Mwaka huu shule yako ilipata bahati ya kutembelewa na kiongozi wa vikao vya halmashauri. Je mgeni huyu hutokana na nini?(a) wakuu wa idara (b) wajumbe wa kuteuliwa (c) wabunge (d) madiwani
  4. Hatimaye siku ya harusi yake Halima alifurahi sana. Aliiomba na kucheza kwa madaha. Pia mumewe kadhalika. Wazazi hawakuwa nyuma walifurahi kwa kuwa walipewa zawadi na mume wa motto wao. Je wazazi walipewa nini?(a) mahali (b) tozo (c) mhari (d) uchumba
  5. Kila desturi ina faida na hasara. Mitala au ndoa za wake wengi ni miongoni mwa mila potofu kwa kuwa (a) zinazotakiwa (b) zinazokwenda na wakati (c) za watu wa mjini (d) zinanyima uhuru wa wanajamii na wanandoa kwa ujumla.
  6. Ili tuendelee tunahitai mipango madhubuti. Mipango ya maendeleo ya nchi yoyote inatokana uimara wa nyaraka muhimu. Tubainishie nyaraka hiyo inaitwaje? (a) sera (b) katiba (c) ilani (d)sekta
  7. Kigezo kimojawapo cha utumiaji mbaya wa madaraka ni ____ (a) Rushwa (b) umoja (c) vyama vingi (d)uchaguzi
  8. Moja ya Nyanja muhimu kwa maendeleo ya taifa ni Nyanja ya habari na mawasiliano. Zifuatato si shughuli za Nyanja ya habari na mawasiliano ISIPOKUWA___ (a) ulinzi na usalama (b) kusimamia sheria (c) kuunda mashirikia (d) kukosoa serikali
  9. Ukiwa kama bin adamu na unatakiwa utoe msaada wa haraka katika jamii. Katika makundi yafuatayo lipi utalipa kipaumbele?

(a) viongozi wa dini, madiwani na wazee (b) wagonjwa, watoto, wazee na walemavu (c) watoto, vijana, wagonjwa na wazee (d) viongozi, watoto na wafanyakazi

  1.                                                                                                                                                                                                                                                    Zifuatazo ni njia za kujenga uhusiano mwema na watu katika jamii isipokuwa..

          (a) kudumisha umoja na amani (b) kutatua matatizo ya familia

     (c) kuzuia maradhi ya kuambukiza (d) kushiriki katika kazi za pamoja

  1.         Kuheshimu jamii, kuwajali wengine, kuwa mkweli na kuwajibika kwa jamii inasaidiaje watu? (a) kuleta maendeleo duni (b) kujenga uadui baina ya watu katika jamii

(c) kujenga uhusiano mzuri katika jamii (d) kujenga hofu na kuogopa wanaokuzidi umri

  1. Katika vitabu vya historia ya mwanadamu kuna mifumo mbalimbali inayomwezesha kufika malengo yake ya kila zama. Je ni upi wa kiuchumi usiozingatia mipaka ya kijogafia? (a) ujamaa (b) ujima (c) ukabaila (d) utamaduni
  2. Nchi yetu imebrikiwa rasilimali tofauti tofauti. Rasilimali hizi zinazunguka ardhini, majini na angani. Bainisha kati ya zifuatazo ipi si rasilimali?(a) kilimo (b) watu(c) ardhi (d) msitu
  3. Shabaha ya kuanzishwa kwa serikali za mitaa mchini ni ____ (a) apatikane diwani (b) CCM iwe na nguvu (c) pawe na uchaguzi (d) kupeleka madaraka kwa wananchi
  4. Bunge ni sehemu za taasisi zinazoundwa serikali. Ina majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye katiba. Tuambie kuaznia (a) mpala (d) lipi si jukumu la bunge?(a) kutunga sheria (b)kutafsiri sheria (c) kuchagua spika (d)kusimamia serikali
  5. Mashirika na makampuni kumilikiwa na mtu au taasisi zisizo za kiserikali ni dhana ya ____(a) urasimishaji (b) utandawazi (c) ubinafsishaji (d) tasafu
  6. Shirika la afya la ulimwengu ni lipi? _____ (a) WHO (b) FAO (c) IMF (d)UNDP
  7. Yeye ndiyo anahakikisha mkoa una amani na utilivu wakati wote. Mttu huyu anaitwa nani?(a) mkuu wa polisi (b) mbunge (c) katibu tawala za wa mkoa (d) mkuu wa mkoa
  8. Baada ya rasi Samia kuwateua amemkasimisha majukumu ya kuwaapisha wakuu wa wilaya. Je aliyekasimisha majuku haya anaitwa nani? (a) mkuu wa wilaya (b) kamishina wa magereza (c) spika wa bunge (d)mkuu wa mkoa
  9. Baada ya bwana Luka kuhukumiwa na mahakama alipelekwa kwenye chombo maalumu ili wajifunze. Je bwana Luka alipelekwa kwenye chombo gani?(a) bunge (b) magereza (c) mahakama (d) polisi
  10. Katiba ya sasa ya Tanzania litungwa mwaka. (a) 1977 (b) 1962 (c) 1965 (d) 1964
  11. Ndiyo kila kitu kina utambulisho wake. Waislamu wanatambulishwa na msikiti na wakiristo wanatambulishwa na kanis. Unafikiri ni kitu gani kinatambulisha katiba ya Tanzania?(a) Katiba (b) jalada (c) malengo (d)utangulizi
  12. Andishi na mapokeo ni mifumo ya......(a) katiba (b) bunge (c) mahakama (d) maoni
  13. Nenda popote fanya lolote kuwa huru na nchi yako maana unalidwa na katiba yako. Hii hali inatokana na uwepo wa kitu gani nchini?(a) udikteta (b) uchwara (c) demokrasia (d) maoni
  14. .... Huundwa na watu kwa ajili ya kushika madaraka ya serikali katika nchi (a) serikali (b) bunge (c) chama cha siasa (d) mahakama
  15. Denis Kibu mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya jiji la Mbeya kwa sasa anachezea timu ya Simba. Alizua utata sana kwakuwa alikosa sifa za kurithi, kuandikishwa na kuzaliwa Tanzania. Je Denis Kibu alikosa sifa za kitu gani? (a) uraia wa Tanzania (b) Madhumuni ya katiba ya Tanzania (c) sifa za uraia wa Tanzania (d) haki za raia wa Tanzania
  16. Shirika la umoja wa mataifa linalshughulikia wakimbizi ni ...(a) UNESCO (b) FAO (c) WHO (d) UNHCR
  17. Mtu anayewakilisha nchi yake katika nchi zingine huitwa ....(a) Mwanadiplomasia (b) Balozi (c) Mlowezi (d) Mtwana
  18. Mwenyekiti wa tume ya mapendekezo ya katiba mpya ya Tanzania ya mwaka 2013 alikuwa .... (a) Piusi Msekwa (b) Anna makinda (c) Samweli sita (d) Joseph Walioba
  19. Katika orodha ifuatayo ya maraisi kuna raisi anatofauti na maraisi wenzake. Je unaweza kumtambua? (a) J.M. KIKWETE (b) A.H.MWINYI (c) S.S. HASSANI (d) J.J.MAGUFURI

 

SEHEMU B

Jaza sehemu zilizo wazi

41. Juma ni mwanafunzi wa darasa la VI katika shule ya msingi LUMBUGU. Mwaka 2020 maendeleo yake

yalikuwa mazuri. Ila mwaka huu maendeleo yake yamekuwa mabaya. Taja njia tatu utakazozitumia kumsaidia mwanafunzi huyu.

  1. Serikali iliamua kuanzisha mahakama ya ufisadi ili kuweza kukabiliana na watu wenye matumizi mabaya ya ofisi za umma. Kitendo hiki kinaitwaje?
  2. Unafikiri ni kwanini Raisi JOHN POMBE MAGUFULI alipofariki, SAMIA SULUHU HASSANI alikuwa raisi bila ya kufanyika uchaguzi mkuu?
  3. Bwana Kanduru ni MEYA wa jiji. Taja majukumu yake mawili
  4. Nini maana ya neon MAADILI kama linavyotumika kwenye somo la URAIA NA MAADILI?

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 63

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA SABA

URAIA NA MAADILI

MUDA:1:30                                                             

JINA_____________________________________SHULE_________________________

MAELEZO

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

 

Chagua Jibu sahihi katika swali la 1-40. Kisha andika jibu lake atika nafasi uliopewa

  1. Mojawapo ya njia ambazo wananchi wanaweza kushiriki katika ulinzi na usalama ni...............(a) kupiga wahalifu (b) kufanya mazoezi ya viungo(c) kuwaua wahalifu  (d) kuwafichua wahalifu (e) kuwa rafiki na wahalifu
  2.  Jukumu la kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao lipo mikononi mwa; (a) Jeshi la Wananchi la Tanzania (b) Idara ya Usalama wa Taifa (c) Jeshi la Magereza (d) Jeshi Ia Mgambo (e) Jeshi la Polisi
  3.  Vyanzo vya mapato ya serikali za mitaani pamoja na: (a) kodi ya kichwa na kodi ya rasilimali (b) ruzuku, kodi na michango mingine (c) kodi ya ardhi, na kodi ya rasilimali (d) tozo katika mazao ya mali asili (e) tozo za leseni za biashara
  4. Ipi kati ya vifuatavyo si miongoni mwa vitendo vya kulinda nchi yetu? (a) Kutoa taarifa za uhalifu (b) Kulinda mipaka ya nchi (c) Kutoa taarifa kwa wahalifu kuhusu rasilimali zilizopo nchini (d) Kusimamia sheria na kulinda rasilimali zetu
  5. ipi kati ya zifuatazo ni oja ya mbinu stahiki za kulinda rasilimali za Umma? (a) Kuzuia kwa wageni ili kupata fedha (b) Kutoa elimu ya utunzaji wa rasilimali za nchi (c) Kuzigawa kwa wananchi wazitumie (d) Kuzuia zisitumike kabisa
  6. Ni mataifa yapi kati ya yafuatayo yalianzisha umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote?  (a) Ulaya Mashariki. (b) Nchi zinazoendelea (c) Ulaya Magharibi.  (d) Amerika ya Kusini (e) Amerika ya Kaskazini
  7. Tanzania inapata faida gani kwa kuongeza biashara yake ya kimataifa?(a) Kuongeza majengo (b) Kupunguza wajasiriamali wa ndani (c)Kuongeza deni (d) Kupunguza mikataba ya kibiashara  (e) Kuongeza fedha za kigeni
  8. Upi si umuhimu wa kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine? (a) Kupata utaalamu na teknolojia (b) Kudumisha utamaduni wa Mtanzania (c) Kukuza migogoro kati ya nchi na nchi (d) Kupata pesa za kigeni
  9. Tanzania imefanya nini katika kujenga jamii inayoheshimu utamaduni wake? (a) Kuwakinga raia wake na utandawazi (b) Kufundisha lugha za asili (c) Kuwa na vyombo vya kuendeleza utamaduni (d)Kuzuia tamaduni zote za kigeni
  10. Moja ya mambo yafuatayo si kweli kuhusu mambo ambayo mgonjwa wa ukimwi anapaswa kutendewa: (a) kustaafishwa kazini (b) kula pamoja (c) kucheza naye  (d) kujadiliana naye kuhusu maendeleo yake (e) kupewa tiba kwa magonjwa nyemelezi
  11. Mambo ambayo kila mwanadamu anastahili kupata bila kujali kabila, utaifa au jinsia huitwa: (a) Utawala bora. (b) Haki za binadamu. (c) Utawala wa sheria.  (d) Demokrasia.  (e) Usawa wa kijinsia
  12. Moja ya matukio yanayokiuka Haki za Binadamu nchini Tanzania ni.............(a) Mauaji ya vikongwe na maalbino (b)Ukataji na upandaji mid (c) kuwafungulia mashtaka wahalifu (d) kufukuzwa kazi viongozi wasio waadilifu(e) Serikali kusimamia ukusanyaji kodi
  13. Kuzingatia sheria, haki za bianadamu, ukweli na uwazi, na uhuru wa vyombo vya habari ni misingi ya (a)Urasimu (b) Utawala wa sheria (c) Ujamaa wa kiafrika (d)Demokrasia ya Uwakilishi (e) utawala bora
  14. Haki za binadamu zinapaswa kutolewa kwa watu wote bila kujali .(a)vyama vya siasa. (b) katiba ya nchi.(c)haki za makundi maalumu. (d) umri wa mtu. (e) rangi, dini, jinsi na kabila.
  15.   Mambo yote ambayo watu wote wanastahili bila ya kujali kabila, utaifa au jinsia ya huitwa(a) utawala bora (b) haki za binadamu (c) utawala wa sheria (d) demokrasia (e) usawa wa kijinsia
  16. Chombo cha juu katika maamuzi kwenye serikali ya kijiji ni ..................(a)  Serikali ya kijiji (b) Kamati ya ulinzi na usalama(c) Mkutano mkuu wa kijiji (d) Afisa Mtendaji wa kijiji(e) Kamati ya Maendeleo ya kijiji
  17. Nani mwenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa mabalozi wa kuiwakilisha Tanzania nchi za nje? (a) Baraza la mawaziri (b) Wabunge wa bunge la jamuhuri ya Tanzania (c) Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania (d) Waziri mkuu
  18. Ipi ni kazi kubwa ya mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje? (a) Kukuza ushirikiano wa kidiplomasia, uchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiteknolojia na mataifa mengine (b) Kufanya biashara za kimataifa (c) Kuandaa ziara za viongozi nje ya nchi (d) Kuunda umoja wa mataifa ya kigeni
  19. Ni kwa namna gani mhimili wa Mahakama hutumia makongamano na mihadhara katika kusimamia haki za binadamu nchini? (a) Hutoa elimu kwa wananchi ili kupata haki zao bila kubughudhiwa au kuonewa kwa namna yoyote (b) Hutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kuacha watumishi wa mahakama kufanya uamuzi wa utashi wao tu (c) Hutoa elimu kwa wananchi juu ya kutokukemea vitendo vya rushwa na ufisadi (d) Hutoa elimu juu ya namna ya watu kudai haki zao kwa woga
  20. Ipi kati ya yafuatayo si majukumu ya serikali katika kusimamia haki za binadamu? (a) Kutoa huduma za kijamii (a) Kuzuia haki isitendeke kwa wahalifu (b) Kulinda amani na utulivu (c) Kulinda rasilimali za nchi
  21. Ipi kati ya vitendo vifuatavyo kinaonesha umuhimu wa kuheshimu Imani na itikadi za wengine? (a) Kubeza Imani za wengine (b) Kuchonganisha watu kwenye jamii (c) Kuishi bila kubaguana kwa misingi ya kiimani na kiitikadi (d) Kuishi kwa raha bila ykujali vurugu za kiitikadi
  22. Ipi ni mojawapo ya ishara ya kuheshimu sheria za shule? (a) Kuchelewa shule (b) Kuchonganisha wanafunzi wenzako (c) Kufuata sheria za shule (d) Kuheshimu wakubwa tu
  23. Mwanafunzi hutegemea nini anapowajibika na kujituma katika shughuli zake? (a) Hisia zake (b) Hisia za watu wengine (c) Hisia za wazazi (d) Hisia za walimu
  24. Mijadala kwa vikundi ni njia ya majadiliano yenye faida gani kwa mwanafunzi? (a) Humwezesha kuuliza maswali (b) Humfanya kuwa huru kujadili (c) Humsaidia kupoteza muda (d) Hujifunza namna ya kujenga hoja bora
  25. Ipi kati ya zifuatazo si hatua za kufanya uamuzi sahihi? (a) Kufahamu tatizo (b) Kutengeneza mikakati (c) Kutathmini (d) Kutokubaliana na changamoto
  26. Njia ipi kati ya zifuatazo Ni njia za kuelimisha jamii juu ya kutekeleza mipango? (a) Kujitenga na watu (b) Kujitenga na watu wasiokujua (c) Kushirikiana na watu wengine (d) Kujitenga na watu wasiokupenda
  27. Ipi ni hatua mojawapo muhimu katika kutatua changamoto wakati wa kutekeleza mipango? (a) Kubaini kiini na ukubwa wa changamoto (b) Kuwekeza Zaidi katika utekelezaji wa mipango (c) Kupata ushauri wa namna ya kutekeleza mipango (d) Kuvumilia changamoto katika utekelezaji wa mipango
  28. Lipi kati ya mambo yafuatayo si muhimu katika kujiwekea malengo katika Maisha? (a) Ujuzi wa kutathmini (b) Kuandaa rasilimali (c) Kujua kiingereza (d)Ari ya kufikia lengo
  29. Kwa nini mihemko humfanya mtu ashindwe kufanya uamuzisahihi? (a) Hutanguliza faida mbele (b) Hana muda wa kufanya tathmini ya athari za uamuzi wake (c) Huongozwa na mihemko kutenda jambo (d) Hutafakari sana na kutenda jambo baadaye
  30. Ipi kati ya zifuatazo si faida za kubuni njia mbadala katika kukabiliana na tatizo? (a) Husaidia kutatua changamoto iliyoshindikana (b) Husaidia kushughulikia tatizo lililokosa ufumbuzi (c) Husaidia kupata utatuzi wa tatizo jipya (d) Husaidia kupata muda wa ziada wa kujifurahisha na kutafakari
  31. Ipi kati ya zifuatazo ni maana sahihi ya neno mawasiliano? (a) Mfumo wa kupashana habari na ujumbe (b) Taaluma ya utafutaji habari (c) Kazi ya kujitolea kutafuta habari (d) Mfumo wa kujua habari zilizofichwa
  32. Ipi kati ya njia zifuatazo ni sahihi kuepuka kufanya makosa ya mitandao ya mawasiliano? (a) Kufungua kesi polisi (b) Kutii sheria na kanuni (c) Kutotumia mitandao (d) Kutotumia simu za mikononi
  33. Ipi kati ya yafuatayo siyo matumizi sahihi ya fedha kwa mwanafunzi kutekeleza majukumu yake katika jamii? (a) Kutumia fedha kwa ajili ya matembezi na kula vyakula vizuri (b) Kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kama kilimo (c) Kununua vifaa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kilimo (d) Kutumia fedha kujifunza mafunzo ya ujasiriamali ili kupata maarifa ya uwekezaji
  34. Kutunza vyanzo vya maji kama mito, maziwa na bahari huleta faida gani katika jamii? (a) Husaidia wasiojiweza kupata huduma za maji (b) Kufanya maji yaishe haraka ili kutafuta vyanzo vingine (c) Kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya uhakika (d) Hupunguza upatikanaji wa maji na shughuli za uzalishaji mali
  35. Mwanafunzi anawezaje kushiriki kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara? (a) Kuendesha mitambo ya kujenga barabara (b) Kulima barabara na kufukia mashimo katikati ya barabara (c) Kukagua na kubaini mashimo ya barabara tu (d) Kuwaelimisha mafundi ujenzi namna ya kujenga barabara
  36. Kwanini mitazamo tofauti ya madhara ya rushwa katika jamii hutokea? (a) Utendaji duni wa kazi (b) Elimu duni juu ya rushwa (c) Ukosefu wa mipango (d) Watoaji na wapokeaji wa rushwa kutoshitakiwa
  37. Taasisi zisizo za kiserikali zina wajibu gani katika jamii? (a) Kuelimisha walioathiriwa na rushwa tu (b) Kuwapa msaada wa kifedha walioathiriwa na matukio ya rushwa (c) Kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya rushwa (d) Kupambana na wanaotoa taarifa za rushwa kwenye jamii
  38. Kuendelea kwa tatizo la rushwa ni changamoto inayozikabili taasisi za Serikali na asasi zisizo za kiserikali kwa sababu gani? (a) Wananchi wana Imani kwamba rushwa ni nzuri (b) Wananchi wa Tanzania ni wakarimu (c) Maadili na uadilifu unakosekana (d) Watu wanataka kuwa na maendeleo binafsi na ya nchi
  39. Ni lipi jukumu lako katika kudumisha umoja miongoni mwa wanafunzi wenzako? (a) Kutoa kauli mbalimbali au kushiriki shughuli zinazodumisha umoja kama vile kusoma Pamoja (b) Kuongoza wanafunzi wengine kuandamana na kudai haki pale wanapokosa uji au chai shuleni (c) Kutetea wavivu na wazembe katika shughuli za darasani (d) Kujitenga na wanafunzi wenzako ili uweze kufanya vizuri darasani
  40. Ni njia ipi kati ya zifuatazo hujenga umoja na mshikamano katika jamii? (a) Kuwa mvivu na kujenga chuki kwa wanaokuchukia (b) Kuchagua marafiki wenye akili timamu na wenye fedha tu (c) Kuwapenda Zaidi ndugu zako na kuwapendelea kuliko watu usiowafahamu (d) Kuheshimu kila mtu bila kujali rika lake, itikadi yake au dini yake

Jibu maswali yafuatayo kwa umakini.

  1. Taja mihimili mitatu ya dola
  2. Taja kazi mbili za bunge la taifa
  3. Kiongozi mkuu katika bunge ni nani?
  4. Taja misingi miwili inayoweza saidia mihimili ya dola kufanya kazi vizuri
  5. Ni nini maana ya mahakama?

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 49

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA- MACHI-2022

URAIA NA MAADILI   DARASA LA SABA.

SEHEMU A: CHAGUA JIBU SAHIHI KUTOKA YALE ULIOPEWA

  1. Msaidizi wa mkuu wa mkoa katika shughuli zake za utendaji ni nani? A. ofisa elimu mkoa B. katibu tawala wa mkoa C. mkuu wa idara ya utawala na utumishi mkoa D. ofisa afya wa mkoa
  2. Mwenyekiti wa halmashauri ngazi ya wilaya huongoza akina nani? A. wenyeviti wa mtaa B. makatibu tawala C. madiwani wa halmashauri D. mtendaji wa kata
  3. Katika ofisi ya kata, nani ni mtendaji mkuu? A. Diwani D. Ofisa mtendaji wa kata C. Ofisa mazingira wa kata D. Ofisa maendeleo wa kata
  4. Wanachama wa vyama tofauti vya siasa wanapokosoana na kushindana kwa misingi ya haki, ukweli na amani, hali hii tunaweza kuiita: A. Utulivu na kisiasa B. Uvumilivu wa kisiasa C. Changamoto za kisiasa D. Ukomavu wa kisiasa
  5. Mtu anapata uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa, kurithi na: A. Kuwatembelea wazazi wanaoishi Tanzania B. Kutumia kitambulisho cha mpiga kura C. Kujiandikisha D. Kubatizwa
  6. Sifa mojawapo ya mtu anayeomba uraia wa Tanzania: A. Aukubali uraia wanchi alikotoka kwa maandishi B. Sio lazima kutangaza kwenye vyombo vya habari C. Awe hajawahi kukutwa na kosa lolote la jinai toka aingie nchini. D. Awe Tajiri
  7. Ni kitendo kipi sio sahihi? A. Kuheshimu sala za wakristo B. Kudharau mavazi ya kiislamu C. Kutopiga kelele darasani D. Kutumia lugha ya taifa
  8. Tunapopata changamoto katika maisha tunapaswa? A. Kulia B. Kukata tama C. Kuwa mvumilivu na kutafuta suluhisho D. Kudai haki
  9. Lengo la uvumilivu ni A. Kuvumilia mateso B. Kukata tama C. Kutafuta njia sahihi za kutatua shida D. Kufikia malengo
  10. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali maji? A. Kukata miti kwenye vyanzo vya maji B. Kutochoma moto misitu C. Kutotiririsha maji machafu D. Kutunza miti
  11. Ni kitendo gani kati ya hivi huchangia kuharibu rasilimali ardhi? A. Kulima matuta kwa kukinga mteremko B. Kuchoma misitu wakati wa kusafisha mashamba C. Kuweka mbolea ya samadi shambani D. Kutumia mbolea ya dukani
  12. Upi si umuhimu wa kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine? A. Kupata utaalamu na teknolojia B. Kudumisha utamaduni wa Mtanzania C. Kukuza migogoro kati ya nchi na nchi D. Kupata pesa za kigeni
  13. Lugha ya Kiswahili imejenga uhusiano na mataifa mengine katika nyanja zifuatazo isipokuwa:A. Biashara za ndani na nje ya nchi B. Michezo ya kimataifa  C. Utalii na utamaduni wa Kitanzania  D. Kuharibu ushirikiano
  14. Umoja wa hiari wa nchi huru zilizowahi kutawaliwa na Uingereza hufahamika kama: A. Jumuiya ya Madola B. Umoja wa Mataifa C. Nchi zinazoendelea    D. Umoja wa Afrika E. Shirikisho la Mataifa
  15. Kwa nini tunajaribu nadharia mbalimbali kwa vitendo? A. Kuthibitisha ukweli wake B. Kuzitofautisha C. Kuzifanya ziweze kukubalika kimataifa D. Kubaini zisizofaa
  16. Tunawezaje kudhibitisha mambo tuliyojifunza? A. Iwapo tutafaulu katika mitihani B. Iwapo tutaeleza wengine C. Iwapo tutayatumia katika maisha yetu D. Iwapo tutayakiri
  17. Tunapojifunza na wenzetu tunapata faida zifuatazo isipokuwa: A. Kujenga kumbukumbu ya muda mrefu B. Kujenga tabia ya uvumilivu C. Kupendelea wengine D. Kujenga urafiki
  18. Unawezaje kuongeza ufanisi katika kujifunza? A. Kubeba vitabu vingi B. Kusoma kwa vikundi C. Kucheza na wenzako D. Kufanya mtihani
  19. Ni hatua zipi wanafunzi wanatakiwa kuchukua wanapoona katika eneo la shule wageni wanaowatilia shaka? A. Kutoa taarifa kwa jeshi la Wananchi la Tanzania. B.  Kutaarifu Kamati ya Shule kuhusu uwepo wa wageni. C.  Kuwapiga wageni kabla ya kuwafikisha Mahakamani. D. Kuwakamata wageni na kuwahoji. E. Kutaarifu Walimu kuhusu uwepo wa wageni.
  20. Jukumu la kuwalinda raia wa Tanzania na mali zao lipo mikononi mwa A. Jeshi la Wananchi la Tanzania B. Idara ya Usalama wa Taifa C. Jeshi la Magereza D. Jeshi Ia Mgambo E. Jeshi la Polisi
  21. Huduma za kisheria kwa wahitaji huweza kupatikana sehemu gani? A. Asasi binafsi za utetezi wa haki za binadamu, mahakamani na magereza B. Kwa mwanasheria, mahakamani, na asasi binafsi za utetezi wa haki za binadamu C. Shuleni, vituo vya polisi na vituo vya afya D. Mahakamani, ofisi za vijiji na magereza
  22. Nini umuhimu wa kuwahudumia na kuwafariji wahitaji katika jamii? A. Kujenga upendo na kuthamini utu B. Kudumisha udugu na kujitangaza C. Kulinda haki za binadamu na haki za kisiasa D. Kukuza utegemezi kwa wahitaji
  23. Kati ya vitendo vifuatavyo kimojawapo si kitendo cha kusaidia kuhamasisha amani kwenye jamii A. Kubishana na majirani zako B. Kutumia mitandao ya kijamii kupinga ubaguzi C. Kutumia mikutano na semina kujadili umoja D. Kuandaa kisamafunzo na ngonjera kuhamasisha upendo katika jamii
  24. Kujisitiri na kuwasitiri wengine vinasaidiaje jamii? A. Kuhamasisha amani katika jamii B. Kuthamini utu C. Kutokujipenda sana D. Kujipenda kwanza na wengine baadaye
  25. Ipi ni hatua ya hadhari ya kuchukua kabla ya janga la moto kutokea? A. Kuziba mdomo na blanketi Kuwapa majeruhi matibabu B. Kujenga nyumba zenye milango na madirisha ya mbele C. Kujenga nyumba zenye milango na madirisha ya dharura
  26. Ni jaribio lipi hatari Zaidi linaloweza kuleta na kusababisha mlipuko wa moto katika maeneo yetu? A. Matumizi ya mkaa wa kisasa B. Kutumia jiko la mafuta ya taa kwa uangalifu C. Kuwasha jiko la gesi bila kuzingatia taratibu za kiusalama D. Majibu a, b na c yote ni sahihi
  27. Taasisi zisizo za kiserikali zina wajibu gani katika jamii? A. Kuelimisha walioathiriwa na rushwa tu B. Kuwapa msaada wa kifedha walioathiriwa na matukio ya rushwa C. Kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya rushwa D. Kupambana na wanaotoa taarifa za rushwa kwenye jamii
  28. Kuzuia na kupambana na rushwa nchini husaidia kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika uboreshaji wa jambo lipi katika Taifa? A. Miundombinu B. Masilahi ya watu wachache C. Watoa rushwa D. Afya za wapokea rushwa
  29. Mwanafunzi anawezaje kushiriki kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara? A. Kuendesha mitambo ya kujenga barabara B. Kulima barabara na kufukia mashimo katikati ya barabara C. Kukagua na kubaini mashimo ya barabara tu D. Kuwaelimisha mafundi ujenzi namna ya kujenga barabara
  30. Kutunza vyanzo vya maji kama mito, maziwa na bahari huleta faida gani katika jamii?A. Husaidia wasiojiweza kupata huduma za maji B. Kufanya maji yaishe haraka ili kutafuta vyanzo vingine C. Kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya uhakika D. Hupunguza upatikanaji wa maji na shughuli za uzalishaji mali
  31. Kati ya vitendo vifuatavyo kimojawapo si kitendo cha kusaidia kuhamasisha amani kwenye jamii A. Kubishana na majirani zako B. Kutumia mitandao ya kijamii kupinga ubaguzi C. Kutumia mikutano na semina kujadili umoja D. Kuandaa kisamafunzo na ngonjera kuhamasisha upendo katika jamii
  32. Kujisitiri na kuwasitiri wengine vinasaidiaje jamii? A. Kuhamasisha amani katika jamii B. Kuthamini utu C. Kutokujipenda sana D. Kujipenda kwanza na wengine baadaye
  33. Kutenda haki husaidia kulinda uhuru na umoja wa taifa kwa sababu gani? A. Viongozi wa nchi hutoa maagizo B. Watu huwa na uhuru wa kufanya lolote walipendalo C. Raia huwa huru kufanya ugaidi D. Wananchi huipenda nchi yao
  34. Ipi kati ya zifuatazo ni njia za haraka za kutangaza fursa zilizopo Tanzania katika nchi za kigeni? A. Tovuti, mitandao ya kijamii, majarida, na vipeperushi B. Simu za mkononi C, Mikutano ya kisiasa D. Redio
  35. Ipi kati ya njia zifuatazo hukuza uhusiano Zaidi miongoni mwa mataifa? A. Usafirishaji wa bidhaa B. Uwekezaji C. Utalii D. Utandawazi
  36. Ni kwa namna gani mhimili wa Mahakama hutumia makongamano na mihadhara katika kusimamia haki za binadamu nchini? A. Hutoa elimu kwa wananchi ili kupata haki zao bila kubughudhiwa au kuonewa kwa namna yoyote B. Hutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kuacha watumishi wa mahakama kufanya uamuzi wa utashi wao tu C. Hutoa elimu kwa wananchi juu ya kutokukemea vitendo vya rushwa na ufisadi D. Hutoa elimu juu ya namna ya watu kudai haki zao kwa woga
  37. Ni jukumu la nani kuimarisha haki za binadamu, ulinzi na usalama nchini? A. Serikali B. Vyombo vya dola C. Mihimili ya dola D. Raia wote
  38. Uchambuzi wa mahitaji kama hatua ya kuandaa mpangokazi huhusisha kuandaa kitu gani? A. Nyaraka za mpangokazi B. Sura za mpangokazi C. Tathmini ya malengo ya taasisi D. Kubainisha na kuandaa rasilimali zinazohitajika
  39. Ni jinsi gani mpangokazi wa kujitolea husaidia kugawa majukumu shuleni? A. Kila mmoja hutambua na kutekeleza majukumu yake kutokana na mpangokazi B. Kila mtu kutekeleza mambo yake binafsi C. Kila mmoja kutekeleza kila jukumu lililo ndani ya mpangokazi kwa muda wake mwenyewe D. Kila mmoja ataamua ni kwa namna gani atatimiza majukumu bila kupangiwa
  40. Tarehe saba mwezi wan ne kila mwaka tunaadhimisha sikukuu gani hapa Tanzania? A. karume day B. Nyerere day C. Siku ya wakulima D. Siku ya Muungano

SEHEMU C. JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA UFASA

  1. Rais wa Muungano wa Jamhuri wa Tanzania anaapishwa na nani?............................
  2. Pendekeza njia mbili za kukabili ufisadi………………………………………………
  3. Taja njia mbili ya kulinda rasilimali maji………………………………………….
  4. Je mazingira ni nini?...............................................................................................
  5. Taja faida mbili za uhusiano wa Tanzania na Mataifa Mengine……………………

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 43

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YAK RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINI DARASA LA VII MAY 2020

URAIA NA MAADILI

Muda: saa 1

MAELEKEZO:

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

SEHEMU A: MASWALI YA KUCHAGUA 

Chagua jibu sahihi kisha siliba herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia uliyopewa

1. Kitendo cha kuonesha tabia njema kwa watu hujulikana kama:

A. Kuomba msamaha B. Heshima C. Ustahimilivu D. Usaliti .E. Unafiki 

2. Jukumu la kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu ni la nani?

  1.  Viongozi wa serikali pekee        D. Viongozi wa dini na wa serikali
  2.   Wanafamila pekee                     E. Wazazi 
  3.   Serikali na kila mtu ndani ya jamii

3. Alama ya taifa inayowakilisha mamlaka ya Rais wa Tanzania ni ipi?

  1. Picha ya Rais      C. Ngao ya taifa            E. Mwenge wa uhuru 
  2. Ikulu                   D. Bendera ya Rais

4. Picha ya shoka na jembe katika ngao ya taifa huwakilisha nini?

  1.                   Ulinzi na usalama C. Rasilimali za taifaE. Uhuru na umoja
  2.                   Amani na upendo D. Wafanyakazi na wakulima [ ]

5. Nchi ipi kati ya hizi zifuatazo haipakani na Tanzania katika upande wowote?

A. Rwanda B. Burundi C. Kenya D. Zambia E. Somalia [ ]

6. Uzalendo, ujamaa, umoja, amani na utu wa watu ni miongoni mwaza taifa.

  1.                   Alama              C. Tamaduni E. Haki
  2.                   Tunu              D. Rasilimali [ ]

7. Hali ya mtu kuipenda nchi yake na kuwa tayari kuilinda hujulikana kama:

A. Uadilifu B. Ustahimilivu C. Uzalendo D. Demokrasia E. Ujamaa 

8. Shughuli ambazo watu hufanya kwa kupenda wao wenyewe pasipo kulazimishwa au kutarajia malipo hujulikana kama:

  1. Tabia hatarishi                   C. Nidhamu binafsi       E. Majukumu
  2. Shughuli za kujitolea         D. Kazi za shuruti 

9. Uhusiano wa kijamii au kiutamaduni uliopo kati ya mwanamke na mwanaume hujulikana kama:

A. Jinsia B. Jinsi C. Utamaduni D. Mila E. Desturi

10. Kiongozi wa juu zaidi katika muundo wa utawala wa shule ni nani?

  1. Mlezi wa shule            C. Mwalimu mkuu    E. Mwalimu mkuu msaidizi
  2.  Meneja wa shule        D. Mwalimu wa taaluma

11. Ratiba ya masomo shuleni huandaliwa na nani?

  1.  Mwalimu mkuu            C. Mwalimu wa taaluma          E. Kiranja mkuu
  2.  Mwalimu wa nidhamu D. Mwalimu mkuu msaidizi 

12. Mila na desturi zipi kati ya hizi zifuatazo zinafaa kuhifadhiwa na kuenziwa?

  1. Kuheshimu wazee            C. Kurithi wajane              E. Ndoa za utotoni
  2. Kubagua walemavu          D. Ndoa za kulazimishwa 

13. Kitendo cha kujifanya mwema machoni mwa watu lakini kiuhalisia siyo mwema hujulikana kama:

A. Unafiki B. Uvumilivu C. Heshima D. Uwazi E. Uadilifu 

14. Mtu anayetoa ushauri nasaha kwa watu wenye matatizo mbalimbali katika jamii hujulikana kama:

A. Mkufunzi B. Muwezeshaji C. Wakili D. Mnasihi E. Mzalendo                                                                          

15. Kitendo gani kati ya hivi vifuatavyo hakionyeshi heshima miongoni mwa wanajamii?

  1. Kusalimia                      C. Kuvaa mavazi ya heshima          E. Kuwasidia wazee
  2. Kutumia lugha ya staha D. Kutukana 

16. Mtu aliyesoma ana sifa zifuatazo, ISIPOKUWA:

A. Ni muadilifu B. Ni mtafiti C. Ni mgunduzi D. AnajiaminiE. Unafiki 

17. Jambo gani kati ya haya yafuatayo linaashiria matumizi mabaya ya rasilimali za taifa?

  1.   kushiriki katika uchaguzi                 C. Kula rushwa E. Uadilifu 
  2.  Kutii sheria za nchi                           D. Uaminifu

18. Mtu anayetumia nguvu za kijeshi kuvuruga amani ya nchi fulani hujulikana kama:

A. Mkimbizi B. Mzalendo C. Balozi D. Gaidi E. Jangili 

19. Sheria inayokataza uzalishaji, uingizwaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini Tanzania ilianza kutumika lini?

  1.  1 Juni 2019                            C. 25 Aprili 2017                           E. 26 Januari 2006
  2.  1 Julai 2000                            D. 18 Machi 2018 [ I

20. Kuna faida gani kutii sheria za nchi bila shuruti?

  1.  Husababisha vita                            D. Huleta uoga na utengano
  2.  Huvuruga amani ya nchi                E. Huleta umoja na utengano 
  3.   Huleta umoja na mshikamano

21. Ulinzi na usalama wa taifa letu na rasilimali za taifa ni jukumu la nani?

  1. Viongozi wa serikali   C. Watanzania wote       E. Serikali za mitaa
  2. Jeshi la polisi              D. Jeshi la Wananchi wa Tanzania 

22. Chombo kinachohusika na ukusanyaji wa kodi na mapato mengine ya serikali nchini Tanzania  hujulikana kama: A. TANAPA              B. BASATA              C. TAA              D. TRA              E. TBS           

23. Chombo kinachohusika na utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ya kijiji ni:

  1. Mwenyekiti wa kijiji            C. Mkutano mkuu wa kijiji      E. Kamati ya kijiji
  2.  Halmashauri kuu ya kijiji    D. Mkutano mkuu wa kata 

24. Kiongozi anayechaguliwa na wananchi katika ngazi ya kata hujulikana kama:

  1.  Mwenyekiti wa kijiji                    C. Mbunge E. Afisa mtendaji wa kijiji
  2. Diwani                                           D. Afisa mtendaji wa kata 

25. Viongozi wafuatao wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ISIPOKUWA: 

  1. Waziri Mkuu .                        C. Mkurugenzi wa wilaya     E. Inspekta mkuu wa polisi
  2. Wakuu wa Mikoa                   D. Kamanda wa polisi wa mkoa 

26. Jambo lipi kati ya haya yafuatayo haliimarisha utawala bora shuleni?

  1. Kuchagua viranja                          D. Kulinda rasilimali za shule
  2. Kufanya vikao vya darasa             E. Kuwashirikisha wanafunzi katika maamuzi           
  3. Kutoheshimu sheria za shule

27. Kiongozi mkuu wa shughuli za kila siku bungeni ni nani?

  1. Rais                      C. Spika              E. Makamu wa Rais
  2. Waziri mkuu        D. Naibu spika 

28. Mashauri yanayohusu kesi za uhaini au mauaji husikilizwa katika ngazi ipi ya mahakama?

  1. Mahakama ya mwanzo         C. Mahakama kuu E. Mahakama ya wilaya
  2. Mahakama ya Rufaa            D. Mahakama ya Hakimu Mkazi 

29. Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa jina lingine hujulikana kama:

  1.  Mahakama kuu                 C. Mahakama ya wilaya      E. Mahakama ya Rufaa
  2.  Mahakama ya mwanzo    D. Mahakama ya mkoa 

30. Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mwaka gani?

  1. 1975                         C. 1964                    E. 2005
  2.  1979                        D. 1996 

31. Tathmini ya mpango kazi wa hiari inahusiana na nini?

  1. Kutathmini malengo              C. Nyaraka za mpango kazi          E. Kuweka malengo
  2. Kuandaa rasilimali                 D. Sura za mpango kazi

32. Tukio la kuuza bidhaa za kampuni au taasisi kwa njia ya kushindanisha bei hujulikana kama:

  1. Biashara ya magendo  C. Biashara ya ndani  E. Mnada

      B. Uwekezaji D. Harambee

33. Msaada upi kati ya hii ifuatayo hauna manufaa kwa maendeleo ya shule?

  1. Samani                        C. Soda na bia           E.Vitabu
  2. Vifaa vya kujifunzia    D. Sare za shule 

34. Msaada wa kisheria hutolewa wapi zaidi?

A. Shuleni B. Nyumbani C. Mahakamani D. Gerezani E. Kanisani             

35. Hali ya kuwa na utulivu pasipo kuwa na vita katika nchi hujulikana kama:

A. Amani B. Ulinzi C. Sheria D. Uhusiano E.Heshima 

36. Kipi kati ya vitendo vifuatavyo huimarisha amani na usalama wa nchi?

  1.  Kuvunja sheria C. Kutotii sheria E. Kutii sheria bila shuruti
  2.   Kugombana na wengine D. Kuendeleza matendo maovu 

37. Kitendo cha kutoa siri ya mtu kwa adui yake hujulikana kama:

  1. Kusengenya  C. Usaliti E. Unafiki
  2. Nidhamu binafsi D. Umbea 

38. Majanga ya moto pamoja na shughuli za uokoaji nchini Tanzania hushughulikiwa na:

  1. Jeshi la polisi C. Jeshi la Mgambo E. Sungusungu
  2.  Jeshi la zimamoto D. Jeshi la Zimamoto na uokoaji 

39. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Tanzania liliundwa mwaka gani?

A. 1997 B. 2003 C. 2007 D. 2013 E. 2017 

40. Nyumba ya Sozi ilikuwa inaungua moto kutokana na kupata hitilafu ya umeme. Je, ni namba gani ya simu Sozi angeweza kuipigia ili kuomba msaada kwa jeshi linalohusika na uzimaji wa moto na uokoaji?

A. 112 B. 114 C. 114 D. 100 E. 113                                                                                                                [              ]
SEHEMU B: MASWALI YA MAJIBU MAFUPI 

Jibu swali la 41-45 kwa kuandika majibu sahihi katika karatasi ya kujibia uliyopewa

41. Ni kwa namna gani mpango kazi wa hiari humsaidia mwanafunzi kufaulu vizuri katika masomo yake?

42. Chombo kikuu kinachosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kata hujulikana kama

43. Baada ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania Rais mteule huapishwa na nani?

44. Ni chombo kipi cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kina kazi sawa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

45. Taja faida mbili za kuwa na wimbo wa shule

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 28

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021

URAIA NA MAADILI – DARASA LA SABA

FOMATI MPYA

MUDA1:30 MASAA       MACHI 2021

JINA …………………………...SHULE ………………………...

MAELEKEZO 
  • Jibu maswali yote
  • Tumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41-45
  • Hakikisha kazi yako inakuwa safi
  • Tumia penseli kuweka kivuli kwa majibu sahihi

SEHEMU A:Chagua jibu sahihi.

1. Mtu anayedhibiti mwenendo wa wanafunzi shuleni ni..

  1.  Mwenyekiti wa kamati ya shule 
  2.  Mwalimu wa nidhamu
  3.  Mwalimu mkuu msaidizi 
  4.  Mwalimu wa taaluma
  5.  Mwalimu wa somo
  1. Tunaposema sheria mama tunamaanisha nini?
  1. sheria zinazohusu akina mama,
  2. katiba ya nchi,
  3. bunge,
  4. Baraza la Mawaziri
  5. baraza la madiwani.
  1. Chombo cha juu katika maamuzi kwenye serikali ya kijiji ni ..................
  1. Serikali ya kijiji 
  2. Kamati ya ulinzi na usalama
  3. Mkutano mkuu wa kijiji 
  4. Afisa Mtendaji wa Kijiji
  5. Kamati ya Maendeleo ya kijiji
  1. Chombo cha kitaifa kinachotunga sheria za nchi ni;
  1. Bunge,
  2. Mahakama,
  3. Jeshi la polisi,
  4. Baraza la madiwani
  5.  baraza la wawakilishi Zanzibar.
  1. Ipi kati ya sarafu zifuatazo ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar?.................
  1. Sarafu ya shilingi mia moja 
  2. Sarafu ya shilingi mia mbili
  3. Sarafu ya shilingi hamsini 
  4. Sarafu ya silingi ishirini
  5. Sarafu ya shilingi kumi
  1. Sheria ambayo imepitishwa na bunge ila bado haijasainiwa na Rais ni_________
  1. katiba,
  2. maoniyawananchi,
  3. muswada,
  4. mawaidha
  5. mjadala.
  1. Maliasili zinazovutia watalii na kuchangia katika kukuza uchumi wa Tanzania ni..................
  1. ardhi 
  2. mito 
  3. mifugo
  4.  madini 
  5.  mbuga za wanyama
  1. Chombo ambacho kimepewa mamlaka yakuendesha utawala wanchi kwamisingi maalumu__________
  1. Bunge,
  2. Chama cha siasa,
  3. Serikali,
  4. Jeshi 
  5. polisi.
  1. Kiongozi anayepatikana kwa kuchaguliwa katika ngazi ya kata ni________
  1. OfisaMtendaji,
  2. Diwani,
  3. Mwenyekiti,
  4. Kitongoji
  5. Mwenyekitiwahalmashauri.
  1. Wajibu wa serikali katika kujenga maadili ya viongozi ni....................
  1. Kuwakopesha magari viongozi wote
  2. Kuimarisha mfumo wa chama kimoja cha siasa
  3. Kusimamia sheria za utumishi wa umma
  4. Kuhamisha watumishi wasio waadilifu
  5. Kuajiri watumishi wenye elimu ya juu to
  1. Nyimbo,ngoma,mashairi na masimulizi kwa neon moja huitwa_______.
  1. burudani, 
  2. mazoezi, 
  3. sanaa za maonyesho,
  4. elimu
  5. asili
  1. Maana ya utamaduni ni:-
  1. Ushabiki wa kitu au jambo unalolipenda
  2. Mtindo wa jumla wa maisha ya watu katika jamii au taifa Fulani
  3. Shughuli za asili zinazofanywa na watu
  4. Yote sahihi
  1. Baadhi ya alama zipatikanazo kwenye fedha ya Tanzania ni
  1. Twiga Tembo, Nembo ya taifa na sura ya rais
  2. Nembo , nyumbu na kifaru
  3. Mwenge , twiga na sokwe
  4. Mwenge wa uhuru
  1. Umuhimu wa bendera ya rais ni
  1. Kutembelea katika ziara mbalimbali tu
  2. Kuonyesha mamlaka ya rais
  3. Kuhamasisha mwenge wa uhuru
  4. Kuonyesha heshima kwa rais
  1. Chimbuko la sheria zote nchini Tanzania ni;
  1. Fedha ya Tanzania
  2. Katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania.
  3. Vyama vya siasa
  4. Bunge
  1. Rangi ya bluu iliyopo katika bendera ya taifa uwakilisha;
  1. Watanzania
  2. Madini
  3. Maji ambayo ni mito, maziwa na bahari nchini Tanzania
  4. Uoto wa asili
  1. Alama ambayo hutumika kuonyesha umiliki wa mali na nyaraka za serikali tu ni;
  1. Picha ya makamu wa rais
  2. Bendera ya taifa
  3. Nembo ya Taifa
  4. Ndege ya Taifa
  1. Ni ishara gani inayoonyesha kwamba taifa limepatwa na msibu mkubwa?
  1. Bendera zote kupepea nusu mlingoti
  2. Bendera ya taifa kupepea nusu mlingoti
  3. Bendera ya taifa kutopandishwa kabisa siku ya tukio
  4. Watu kutokwenda kazini
  1. Ni siku ambazo viongozi hupata fursa kueleza mafanikio na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi
  1. Siku za kukimbizwa mwenge wa uhuru tu
  2. Sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar tu
  3. Sikukuu za kitaifa
  4. Sikukuu ya krismas
  1. Zipi kati ya hizi ni mila zisizofaa katika jamii?
  1. Kufanya kazi kwa ushirikiano
  2. Kuwakeketa wasichana
  3. Kuhamasisha wanaume na wanawake kushirikiana kufanya kazi za nyumbani hili kujiongezea kipato.
  4. Kuoa jinsia moja
  1. Mifano ya vikundi vinavyoweza kuundwa shuleni ni kama;
  1. Skauti, klabu za mazingira, klabu ya TAKUKURU.
  2. Klabu za masomo
  3. Upatu, ushirikiano na vyama vya siasa
  4. Skauti, singeli na ngoma za asili.
  1. Maendeleo yafamilia huletwa na_
  1. Baba
  2. Mama
  3. Mama na Baba
  4.  Wanafamiliawote
  5. babunabibi
  1. Kipi ni miongoni mwa tabia za kiutamaduni huchangia kuenea kwa vvu/ukimwi ---------
  1. Ndoa za utotoni na ukeketaji
  2. Kurithi wajane na ukeketaji
  3. Ngoma za asili na ndoa za kulazimishwa
  4. Imani za vyakula na ngoma za asili
  5. Ukeketaji na mauaji ya vikongwe
  1. Alama inayowakilisha wafanyakazi katika Nembo yaTaifa ni? ------------
  1. Jembe
  2. Mkuki
  3. Pembe za ndovu
  4. Mwenge wa uhuru
  5. Shoka
  1. Mwenenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya,Miji,manispaa na Jiji huchaguliwa na ;
  1. Wajumbe wa Bunge
  2. Mkuu wa Mkoa
  3. Madiwani
  4. Rais
  5. Ofisi ya Waziri Mkuu.
  1. Bunge limeundwa na sehemu kuu mbili nazo ni; ---------
  1. Spika na wabunge
  2. Waziri wa sheria na Wabunge
  3. Rais na Wajumbe wa Bunge
  4. Waziri Mkuu na Spika 
  5. Mwanasheria Mkuu wa  Serikali na Spika.
  1. Waendao kwamiguu barabarani wanashauriwa kutembeakwa -----------
  1. Kutumia upande wakulia wa barabara
  2. Kutumia upande wa kushoto wa barabara
  3. Kuangalia upande wa kulia na kushoto wa barabara
  4. Kushikana mikono
  5. Kuangalia taa za usalama barabarani
  1. Jukumumojawapo la Baraza la madiwanini ……
  1. Kupitisha bajeti ya wizara
  2. Kumshauri Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
  3. Kuhudhuria vikao vya Bunge
  4. Kuteua mkuu wa Wilaya 
  5. Kuapishawatendajiwavijiji.
  1. mkurugengezi wa halmashauri huteuliwa na …… 
  1. Rais
  2. mkuu wa mkoa 
  3. madiwani
  4. mkuu wa wilaya
  1. Maana ya utamaduni ni
  1. ushabiki wa kitu
  2. mtindo wa jumla ya maisha ya watu watu
  3. shughuli za asili zinazo fanywa na watu
  4. ngoma na filimbi
  5. mila na desturi
  1. Ufundi wa kuwasilisha hisia na mawazo yaliyomo katika fikra huitwa:
  1. Mila
  2. Desturi
  3. Sanaa
  4. Utamaduni.
  1. Asili, mila, jadi Imani na desturi za jamii Fulani huitwa?
  1. Utamaduni
  2. Desturi
  3. Sanaa
  4. Mila
  1. Jambo la kawaida linalotendwa kila siku na jamii huitwa?
  1. Lugha
  2. Sanaa
  3. Desturi
  4. Mila
  1. Wareno walifika pwani ya Africa Mashariki mwaka?
  1. 1540
  2. 1498
  3. 1497
  4. 1690
  1. Lengo la waarab wa Omani kuja pwani ya afrika ilikuwa
  1. Kilimo
  2. Uvuvi
  3. Biashara
  4. Upagazi.
  1. Mreno wa kwanza kufika katika pwani ya Afrika mashariki alijulikana kama
  1. William Mackinnon
  2. Charles Stokes
  3. Vasco Dagama
  4. Karl Peters
  1. Wareno walifika katika Mji wa kilwa mnamo karne ya
  1. 15
  2. 16
  3. 19
  4. 18
  1. Nini maana ya uhusiano?
  1. Hali ya watu wawili na Zaidi wenye malengo ya Pamoja
  2. Hali ya kugombana baina ya mt una mtu
  3. Hali ya kufanya kazi peke yako
  4. Mshikamano
  1. Kipi kati ya vifuatavyo ni chombo cha sheria kinasimamiahaki?
  1. Polisi
  2. Bunge
  3. Shule
  4. Mahakama
  5. Jeshi
  1. Wajumbe wa Kamati ya Shule huchaguliwa na ………..
  1. Mwalimu mkuu 
  2. Wazazi 
  3. Walimu shuleni 
  4. Mtendaji wa kijiji 
  5. Diwani.

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI;

41.Kiongozi mkuu wa shughuli za kila siku  Bungeni ----------

42.Ni nani mwenyekiti wa baraza la mawaziri…………………….

43._____________ni kiongozi mkuu wa kisiasa katika kata………..

44.Bendera ya taifa ina rangi ngapi?_________________-

45.Katibu wa vikao vya baraza la madiwani katika Ngazi ya Halmashauri  ni_________________

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 24

OFISI YA RAISTAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINI YA AWALIDARASA LA SABA (VII) -2021

SOMO:URAIA NA MAADILIMUDA: SAA 1:30

MAELEKEZO 

  • Jibu maswali yote
  • Tumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali la 41-45
  • Hakikisha kazi yako inakuwa safi
  • Tumia penseli kuweka kivuli kwa majibu sahihi

SEHEMU A:Chaguajibusahihi.

  1. Waziri mkuu huteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa______________.a)madiwani, b)wenyeviti wa mitaa,                     c) wabunge, d)katibu wa wizara (e) wakuu wa mikoa[       ]
  2. Tunaposema sheria mama tunamaanisha nini? a)sheria zinazohusu akina mama, b)katiba ya nchi, c)bunge, d)Baraza la Mawaziri (e) baraza la madiwani.[     ]
  3. Mwakilishi wawananchi katika halmashauri ya wilaya au manispaa ni _______.a)mbunge, b) diwani, c)ofisi ya Mtendaji, d)mwenyekiti wa kijiji (e) diwani viti maalumu [       ]
  4. Chombo cha kitaifa kinachotunga sheria za nchi ni; a)Bunge, b)Mahakama, c)Jeshi la polisi, d)Baraza la madiwani (e) baraza la wawakilishi zanzibar[       ]
  5. Uchaguzi mkuuwa Rais,Wabunge na Madiwani utafanyika mwaka_____a)2019, b)2020, c)2022, d)2023 (e) 2025 [       ]
  6. Sheria ambayo imepitishwa na bunge ila bado haijasainiwa na Rais ni_________ a)katiba, b)maoniyawananchi, c)muswada, d)mawaidha (e) mjadala.[       ]
  7. Nchi yetu nimuungano wanchi mbili zenye serikali ngapi? A)Tatu,b)mbili, c)moja, d)nne (e) nne[       ]
  8. Chombo ambacho kimepewa mamlaka yakuendesha utawala wanchi kwamisingi maalumu__________a)Bunge, b)Chama cha siasa, c)Serikali, d)Jeshi  (e) polisi.[       ]
  9. Kiongozi anayepatikana kwa kuchaguliwa katika ngazi ya kata ni________a)OfisaMtendaji,b)Diwani, c)Mwenyekiti, d)Kitongoji ( e ) mwenyekitiwahalmashauri[       ]
  10.                     Mapato ya serikali zamitaa hutokanananini? a)Misaada ya nchi wahisani, b)Mikopo katikamabenki, c)Ruzuku , kodi mbalimbali na michango yawananchi, d)Wizi ( e) faini.[       ]
  11.                     Nyimbo,ngoma,mashairi na masimulizi kwa neon moja huitwa_______.a)burudani,  b)mazoezi,  c)sanaa za maonyesho, d)elimu (E) asili.[       ]
  12.                     Zoezi la kuhesabu watu huitwa_________.a)hesabu, b)makazi, c)idadi, d)sensa (e) jumla kuu y a watu.[       ]
  13.                     Kiongozi mkuu wa shughuli za serikali katika bunge ni________.a)Jajimkuu, b)Mwanasheriamkuu, c)Spikawabunge, d)MakamuwaRai (E) maziri mkuu.[       ]
  14.                     Chama kilicholeta uhuru wa Tanganyika kilikuwa __________a)TAA, b)ZANU, c)ZANUPF, d)TANU ( e) ccm[       ]
  15.                     Hatua yamwisho ya maendeleo ya kiuchumi yamaisha ya binadamu ilikuwa___________.a)ujima, b)ujamaa, c)ukabaila, d)ubepari (e) umwinyi.[       ]
  16.                     Uchaguzi mkuu husimamiwa na chombo kipi kati ya hivi?a)Takukuru, b)Tume ya ofisi yaWaziriMkuu, c)ofisi ya utumishi, d)Tume yaTaifa ya uchaguzi( e) tamisemi[       ]
  1.                     Mawazo yajumla kuhusu namna yakukuza uchumi huitwa _______a)mipango ya uchumi, b)sera ya uchumi, c)ujasiriamali wa uchumi, d)mbinu za kukuza uchumi (e) kujiajili.[       ]
  2.                     ____________nikuzalisha,kusambaza na kutumia mali ili kuwaletea wananchi maendeleo.a)Rasilimali, b)Maliasili, c)Uchumi, d)Ujasiriamali.(e) kujiajili[       ]

19.Uwezo wakukabiliana na changamoto huitwa (a) uadilifu (b) ujasiri (c) kipaji (d) kuaminika (e) nguvusana [  ]

20.Nembo ya taifa nikielelezo cha_______(a)uhuru wanchi yetu(b )umoja,uwezonanguvuzataifaletu(c)uzalendo (d) hapakazitu (e) kupiganiauhuru

21.Maendeleo yafamilia huletwa na_(a) Baba (b) Mama(c) Mama na Baba(d) Wanafamiliawote (e )babunabibi

22.Kipi ni miongoni mwa tabia za kiutamaduni huchangia kuenea kwa vvu/ukimwi ---------(a)Ndoa za utotoni na ukeketaji (b)Kurithi wajane na ukeketaji (c) Ngoma za asili na ndoa za kulazimishwa (d) Imani za vyakula na ngoma za asili (e)Ukeketaji na mauaji ya vikongwe

23.Alama inayowakilisha wafanyakazi katika Nembo yaTaifani? ------------(a)Jembe (b)Mkuki (c) Pembezandovu ( d) Mwengewauhuru ( e) Shoka

24.Mwenenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya,Miji,manispaa na Jiji huchaguliwa na ;A.)Wajumbe wa Bunge B.)Mkuu wa Mkoa C.)Madiwani D.)Rais E.)Ofisi ya Waziri Mkuu.

25.Bunge limeundwa na sehemu kuu mbili nazo ni; ---------(a)Spika na wabunge (b) Waziri wa sheria na Wabunge (c) Rais na Wajumbe wa Bunge (d) Waziri Mkuu na Spika  (e)Mwanasheria Mkuu wa  Serikali na Spika.

26.Waendao kwamiguu barabarani wanashauriwa kutembeakwa -----------(a)Kutumia upande wakulia wa barabara (b)Kutumia upande wa kushoto wa barabara (c)Kuangalia upande wa kulia na kushoto wa barabara (d)Kushikana mikono ( e)Kuangalia taa za usalama barabarani

27. Jukumumojawapo la Baraza la madiwanini ……A. Kupitisha bajeti ya wizara B. Kumshauri Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya C. Kuhudhuria vikao vya Bunge D. Kuteua mkuu wa Wilaya  E. Kuapishawatendajiwavijiji. 

28 mkurugengezi wa halmashauri huteuliwa na ……  A. Rais (b) mkuu wa mkoa  (d)madiwani (E) mkuu wa wilaya

29.Maana ya utamaduni ni(a)ushabiki wa kitu(b)mtindo wa jumla ya maisha ya watu watu (c) shughuli za asili zinazo fanywa na watu(d) ngoma na filimbi (e )mila na desturi

30.Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza lini? (a) 9/12/1962(b)9/12/1961(c)26/4/1964(d) 9/12/1960( E)10/12/1968

31.Katiba ni nini?(a) ratiba ya Tanzania (b)uhuru wa kufanyajambo(c)kitabu cha sheria(d) jumla ya kanuni, taratibu au sheria(E ) Ni mwongozo wa maisha ya kila raia watanzania

32.Kiongozi mkuu katika wilaya ni (a)mkurugenzi(b) katibu tawala(c)mkuu wa wilaya(d) afisa mtendaji( e)afisa mipango wawilaya

33.Katika ofisiya kata nani ni mtendajimkuu?(a) diwani (b) afisamtendajiwa kata  (c)mtendaji wa kijiji( d)afisa elimu kata (e) afisa tarafa

34.Ukataji wa miti ovyo na uchomaji misitu unawezakusababisha ___(a)mvua nyingi(b)kuchafua mazingira(c)ukame na bala la njaa(d)mavuno mengi(e ) vifo

35.Watu,misitu,madini ardhi,maji na wanyamaporini ___(A)maliasili(B)vitu vya thamani(C)rasilimali za taifa(D)mazao(e)  misitu

36.Kiongozi bora anatakiwa awe nasifa ipi kati yahizi?(a)anayependwa na watu wengi(b)anayetawala kwa kufuata haki(c)aliyechaguliwa kwa kazi nyingi( d  )asiyependa makuu (e) mpenda starehe na anasa

37.Kanuni zinazowekwa shuleni na nyumbani husaidia (a)kufuata utaratibu na kudhibiti nidhamu(b)ukiukwaji wa haki za mototo ubabe wa wazazi(c) kuletafujo(d) kuletaupendonyumbani (e) amaninautulivu

38.Kipi kati ya vifuatavyo ni chombo cha sheria kinasimamiahaki?(a)polisi(b)bunge(c)shule(d)mahakama(e) jeshi

39. Kuna ainatatuzaUraia, yaaniUraiawaKuandikishwa, KuzaliwanaUraiawa               A. Kupewa B. Kuokota C. Kurithi D. Kukubali E. kulazimishwa. 

40. Wajumbe wa Kamati ya Shule huchaguliwa na ………..A.)Mwalimu mkuu B.)Wazazi C.)Walimu shuleni D.)Mtendaji wa kijiji E.)Diwani.

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI;

41.Kiongozi mkuu wa shughuli za kila siku  Bungeni ----------

42.Mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za serikali katika Ngazi ya Wilaya ni____________________

43._____________ni kiongozi wa kuchaguliwa katika kata.

44.Bendera ya rais ina rangi ngapi?_________________-

45.Katibu wa vikao vya baraza la madiwani katika Ngazi ya Halmashauri  ni_________________

MUONGOZO WA MAJIBU YA URAIA NA MAADILI : DARASA LA SABA 2021

1.

C

26

A

2.

B

27

B

3.

B

28

A

4.

A

29

B

5.

E

30

B

6.

C

31

D

7.

B

32

C

8.

A

33

B

9.

B

34

C

10.

C

35

C

11.

C

36

B

12.

D

37

A

13

E

38

D

14

D

39

C

15

B

40

B

16

D

41

SPIKA WA BUNGE

17

B

42

KATIBU TAWALA (DAS)

18

C

43

DIWANI

19

B

44

MBILI

20

B

45

MKURUGENZI

21

D

22

B

23

E

24

C

25

C

LEARNINGHUBTZ.CO.TZURAIA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 20

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256