?> MAARIFA STANDARD SEVEN EXAMS SERIES
MAARIFA STANDARD SEVEN EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI

MTIHANI WA KUJIPIMA

MTIHANI WA UPIMAJI(PRE-NECTA)DARASA LA SABA

[03]MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI

Muda: Saa 1.30 Mwaka: 2024

 

 Maelekezo 

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali saba(7)

2. Majibu yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa. 

3. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu na mweusi. 

4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani. 

5. Andika namba yako ya mtihani na shule katika sehemu ya juu upande wa kulia wa karatasi yako. 

SEHEMU A: (ALAMA 20)

1. Jaza kipengele (i) – (xv) kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi. 

i. Wakati sanga alipokuwa anasafiri kutoka Dar es salaam kwenda Iringa aligundua badiliko la hali ya hewa kwa kuongezeka kwa jotoridi, je hali hiyo ya kijiografia inaitwaje? 

A. Mwinuko kutoka usawa wa bahari 

B. Mabadiliko ya hali ya hewa 

C. Ongezeko la joto 

D. Tabia ya nchi 

E. Usawa wa bahari 

ii. Sheria ya utunzaji wa mazingira ndiyo sheria mama inayotumika kutunza mazingira nchini, je sheria hiyo iliundwa mwaka gani? 

A. 2002 

B. 2012 

C. 2015 

D. 2005 

E. 2004 

iii. Mazingira ni moja ya jambo kuu maalumu katika uhai wa mwanadamu. Je ipi kati ya haya yafuatayo ni matokeo ya uharibifu wa mazingira? 

A. Kutengenezeka kwa mvua 

B. Majira ya mwaka 

C. Kukua kwa mimea 

D. Kuongezeka kwa rutuba 

E. Kukauka kwa vyanzo vya maji 

iv. Kijiji cha Mwanalugali kimekumbwa na upungufu wa mvua kwa muda mrefu, je hali hiyo inaitwaje? 

A. Mafuriko 

B. Njaa 

C. Ongezeko la joto 

D. Ukame 

E. Mlipuko wa volcano 

v. Sophia anataka kutenganisha pumba na nafaka kwa njia ya kupepeta, je ni hali gani ya hewa inafaa kwa kazi hiyo? 

A. Mvua 

B. Radi 

C. Jua 

D. Upepo

E. mawingu 

vi. Darasa la nne walikuwa wanapima kiwango cha mwanga wa jua, je watawasilisha majibu yao katika kizio gani? 

A. Mwanga wa jua 

B. Kipima mwanga 

C. Campbell stock 

D. Masaa 

E. Milimita 

vii. Dunia ina mizunguko miwili ya kujizungusha kwenye mhimili wake na kulizunguka jua. Taja moja ya tokeo la dunia kujizungusha katika muhimili wake? 

A. Afelioni 

B. Kupatwa kwa mwezi 

C. Majira ya mwaka 

D. Kupatwa kwa jua 

E. Usiku na mchana 

viii. Mkutano wa Berlin ulifanyika novemba 1884 hadi February 1885. Je ni mataifa gani kati ya haya yalihudhuria kama watizamaji? 

A. Marekani na Denmark 

B. Ubeligiji na ufaransa 

C. Uingereza na ufaransa 

D. Hispania na Denmark 

E. Ujerumani na ureno 

ix. Mfumo wa jua unajumla ya sayari nane. Je ni sayari ipi inabaridi sana kuliko sayari nyingine? 

A. Dunia 

B. Sumbura 

C. Sarateni 

D. Zohari 

E. Zebaki 

x. Wanafunzi watano waliambiwa waorodheshe tamaduni zisizofaa katika jamii mmoja akataja jibu lisilokuwa sahihi, jibu hilo ni lipi? 

A. Kutahiri wanaume 

B. Ukeketaji 

C. Ndoa za utotoni 

D. Ndoa za kung’ang’aniza 

E. Mauaji ya albino 

xi. Kwenye kila jamii kuna mambo au tabia zilizo katazwa au zisizoruhusiwa, je vitu hivyo vinajulikana kama? 

A. maagano 

B. thamani 

C. miiko 

D. mila

E. desturi

 

 

xii. Mabadiliko ya hali ya hewa yanatokea kwa kasi kubwa sana ulimwenguni, je kupungua kwa barafu kwenye kilele cha milima mirefu pamoja na kuongezeka kwa kina cha bahari ni kiashiria cha janga gani? 

A. Mafuriko 

B. Ongezeko la joto ulimwenguni 

C. Upepo mkali 

D. Tetemeko la ardhi 

E. Msitu mkubwa 

xiii. Umoja wa watu weusi walioungana pamoja katika harakati za kupigania Uhuru, haki na utu wao? 

A. Umajumui 

B. Ukoloni 

C. Ujamaa 

D. Ujima 

E. Kutembea kwa miguu miwili 

xiv. Ni shughuli ipi ya uzalishaji mali inahusisha kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kujifunza au kujiburudisha? 

A. Usafirishaji 

B. Ujasiriamali 

C. Usafari majini 

D. Utalii 

E. Kuburudika. 

 

 

 

xv. Kwanini ardhi inaaminika kuwa ndiyo rasilimali mama wa rasilimali nyingine zote? 

A. Inasaidia kwenye kilimo 

B. Imebeba rasilimali za asili na zisizo za asili 

C.Nimakazi ya viumbe vya majini 

D. Inatumika katika usafirishaji 

E. Inavutia watalii 

 

2.Oanisha kifungu A na B kisha andika majibu kwenye sehemu uliyopewa. 

FUNGU A

MAJIBU

FUNGU B

i. Tabaka la angahewa linaloikinga dunia kugongwa na vimondo

 

A. Angathemo 

B. Angaexo 

C. Angastrato 

D. Tabaka la ozoni 

E. Angatropo 

F. Angahewa 

G. Angameso 

H. Perihelioni 

 

ii. Tabaka la angahewa linalosaidia usafirishaji wa njia ya anga

 

iii. Tabaka linaloikinga dunia dhidi ya miale mibaya ya mwanga wa jua

 

iv. Tabaka la angahewa linaloanzia kilomita 10 hadi kilomita 50

 

v. Tabaka la angahewa linalowezesha mawasiliano ya simu pamoja na mawimbi ya redio

 

 

 

 

 

 

SEHEMU B: (ALAMA 20)

3. (i). orodhesha njia mbili zinazoweza kutumika kutupatia taarifa ya idadi ya watu nchini 

a._________________________ 

b._______________________ 

(ii). Aryan aliwekeza kiasi cha shilingi milioni 10 na akaajiri wafanyakazi 7. 

(a). kiasi cha fedha alichowekeza kwenye biashara kinaitwa ______

(b). je atakuwa kwenye kundi lipi la biashara? ___________________ 

(iii).Juma alichora ramani ya eneo Fulani akatumia kipimio cha sentimita moja kwenye ramani inawakilisha kilomita nne katika ardhi. Andika kipimio hicho kwa njia ya uwiano au sehemu? ________________ 

4. (i). Aina ya ramani inayoonesha mjumuiko wa vitu asilia na vilivyotengenezwa na binadamu hujulikana kama ______________

(ii). Je ni wakati gani mchoraji ramani anatakiwa kutumia kipimio kidogo cha ramani? __________________ 

(iii). Ikiwa ni saa sita kamili mchana katika mji wa Kinshasa unaopatikana nyuzi za longitudo 14 mashariki ,itakuwa ni saa ngapi katika mji wa Tanga unaopatikana nyuzi 39 mashariki ? 

5.(i). Eleza jinsi misitu inavyosaida kupunguza gesijoto angani? 

(ii).Ikiwa mji unaopatikana mita 1500 kutoka usawa wa bahari unajotoridi 300C . tafuta jotoridi la mji unaopatikana mita 500 kutoka usawa wa bahari? 

6. (i). Mwalimu aliwafundisha watoto kuhusu mistari ya kubuni inayochorwa katika ramani. Je ni mstari upi wa kubuni unaigawa dunia katika vizio viwili vilivyosawa cha kusini na kaskazini? ________________ 

(ii).Orodhesha nadharia mbili za uongo kuhusu ujasiriamali? 

 

 

 

SEHEMU C: (ALAMA 10)

7. Soma ramani ifuatayo kisha jibu maswali yafuatayo

Maswali

i Taja jina la tukio linalooneshwa katika mchoro hapo juu?________ 

ii. Taja sababu kuu zinazo sababisha kutokea kwa tukio lililo oneshwa kwenye mchoro hapo juu ? 

iii. Kivuli kamili kinachotokea wakati wa tukio lilioneshwa kwenye mchoro hapo juu huitwa?____ 

iv. Gimba gani huwa halibadili nafasi yake wakati wa kupatwa kwa jua na mwezi?____________ 

v. Kwanini tarehe 21 machi na 23 septemba urefu wa usiku na mchana huwa sawa.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 112

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UMAHIRI KWA SHULE ZA MSINGI

UPIMAJI DARASA LA SABA MTIHANI WA MWIGO

MAARIFA NA STADI

2024

 

MUDA: 1:30                                                                                                         

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una SEHEMU tatu yaani, A,B na C
  2. Maswali yapo manane kwa ujumla
  3. Jibu maswali yote katika kila sehemu
  4. Tumia kalamu ya wino yenye rangi nyeusi au ya bluu
  5. Onyesha kazi yako vizuri
  6. Vifaa vya elektroniki haviitajiki katika chumba cha mtihani

 

MAELEKEZO 

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali Saba (7) 

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu 

3. Majibu yote yaandikwe katika karatasi hii 

4. Tumia kalamu ya wino wa rangi ya bluu au mweusi 

5. Simu za mikononi na vifaa vingine visivyohitajika haviruhusiwi katika chumba cha mtihani. 

6. Andika kwa usahihi Jina lako na Jina la Shule kwenye sehemu ulizopewa. 

SEHEMU A:

1. Chagua herufi ya jibu sahihi na andika herufi yake kwenye mabano uliyopewa

i) Mwalimu wa somo la Maarifa ya jamii aliwafundisha wanafunzi wake juu ya njia bora za utunzaji wa mazingira. Je, takatata za viwandani zifanywe nini iii kulinda mazingira? (a) kufukia (b) kurejeleza (c) kuficha (d) kuchoma (e) kutupa taka hovyo 

ii) Wanahistoria hutumia njia mbalimbali kutunza kumbukumbu za kihistoria. Njia ipi inahusisha kufukua ardhini kutafuta mabaki ya kale ya binadamu, majengo na zana? (a) Athropolojia (b) masimulizi ya mdomo (c) makumbusho ya Taifa (d) Akiolojia (e) machapisho 

iii) Wanafunzi wa darasa Ia tatu walipima kipengele kimojawapo cha hali ya hewa na wakarekodi jibu katika milimita. Je, walipima kipengele gani cha hail ya hewa? (a) jotoridi (b) mwanga wa jua (c) mgandamizo wa hewa (d) upepo (e) mvua 

iv) Mawazo ni mkulima wa zao Ia korosho. Unafikiri mawazo anatoka mkoa gani wa Tanzania unaozalisha zao hilo? (a) Morogoro (b) Singida (c) Dodoma (d) Mtwara (e) Kagera  

v) Maeneo ya milimani na uwanda wa juu ni baridi kuliko maeneno ambayo yapo karibu na usawa wa bahari. Je, unafikiri jotoridi litapungua kiasi gani kila unapopanda meta 1000 kutoka usawa wa bahari? (a) 6 °C (b) 0.6°C (c) 0.06 °C (d) meta 100 (e) 600C 

vi) Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na aina nyingi za madini. Je, ni madini gani hupatikana Manyoni-Singida, Bahi-Dodoma na Namtumbo-Ruvuma? (a) Tanzanait (b) dhahabu (c) urani (d) chumvi (e) chuma  

vii) Wafugaji wanashauriwa kutumia mbinu bora za ufugaji iii kutunza mazingira. Yapi ni madhara ya ufugaji wa mifugo mingi katika eneo dogo? (a) mifugo kunenepa (b) wachungaji kuchoka (c) mmomonyoko wa udongo (d) majani kuongezeka (e) mifugo mingi katika eneo dogo 

viii) Shule ya msingi Mafanikio imepanga kuwa na ziara ya kimasomo kutembelea eneo Ia kihistoria ambalo ni maarufu kwa michoro inayoonyesha mbinu za uwindaji zilizotumiwa na watu wa kale. Je, ni eneo gani la kihistoria watalitembelea? (a) Isimila (b) Engaruka (c) Olduvai Gorge (d) Kilwa (e) Kondoa Irangi 

 ix) Kupungua kwa theluji katika mlima Kilimanjaro kumesababishwa na ongezeko Ia joto katika uso wa Dunia. Ni shughuli ipi inaweza kutumia kukabiliana na tataizo hilo? (a) kuchoma misitu na kukata miti (b) kupanda miti na kutunza mazingira (c) kulima kandokando ya milima (d) uvunaji hovyo wa misitu (e) kufuga mifugo mingi katika eneo dogo

 x) Katika uso wa Dunia kuna pepo zinazovuma kutoka eneo moja kwenda jingine. Je, ni upepo gani unavuma kutoka kusini kuelekea kaskazini? (a) upepo wa kusi (b) upepo wa kaskazini (c) upepo mkavu (d) upepo wa magharibi (e) pepo za monsoon 

xi) Wanafunzi wa darasa Ia nne waijifunza juu ya uhusiano uliopo kati ya jua, mimea na maji juu ya uso wa Dunia. Yapi ni matokeo ya uhusiano huo? (a) kutokea kwa upepo (b) kufanyika kwa mvua (c) kuganda kwa maji (d) kutokea kwa kimbunga (e) kuyeyuka kwa barafu

 xii) Wanafunzi wa darasa is saba walitembelea shamba kubwa Ia ufugaji wa mbuzi wa kisasa. Je, hiyo ni aina gani ya ufugaji. (a) ufugaji wa jadi (b) ranchi (c) ufugaji wa ndani (d) ufugaji wa kuhama hama (e) ufugaji wa sehemu moja 

xiii) Zama za mawe zimegawanyika katika vipindi vitatu. Zama zipi za mawe zilidumu kati ya miaka 3,000,000KK hadi 300,000KK? (a) zama za kale za mawe (b) zama za chuma (c) zama za mwisho (d) zama za kati za mawe (e) zama za kidigitali 

xiv) Wanafunzi watano waliambiwa wataje mila na desturi potofu zinazofanyika katika jamii. Mmoja wa wanafunzi alitaja jibu ambalo si sahihi. Unadhani ni jibu gani Iilitajwa na mwanafunzi huyo? (a) tohara kwa wanaume (b) ukeketaji kwa wanawake (c) ndoa za utotoni (d) mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (e) ndoa za kulazimishwa 

xv) Majaliwa anaishi na mama yake, ndugu zake, mfanyakazi wa ndani na babu yake. Kulingana na uelewa wako hii ni aina gani ya familia? (a) mume na mke (b) familia pana (c) familia ya awali (d) familia ya mzazi mmoja (e) yatima 

2. Oanisha maelezo ya kifungu A yanayoendana na kifungu B 

KIFUNGU A

KIFUNGU B

  1.               Alikuwa ni kiongozi wa kampuni ya kibiashara ya BEACO wakati wa utawala wa Waingereza.
  2.             Kumbukumbu ya mashujaa wa Kiafrika kama vile Isike, Mkwawa na wengine
  3.          Kilikuwa ni chama cha ukombozi nchini Angola chini ya Mzee Augustino Netto 
  4.          Ni tarehe ambayo tukio la Kijiografia hutokea ambapo dunia huwa mbali kutoka kwenye jua.
  5.             Anathubutu na kuwekeza mtaji wa biashara kwa lengo la kujiajiri na kuongeza kipato

 

  1. Ujasiliamali
  2. Tarehe 3 Januari
  3. Karl Peters
  4. ANC
  5. 25 Julai
  6. Wiliam Macknon
  7. Mjasiliamali
  8. Tarehe 1 septemba
  9. Tarehe 4 julai
  10. MPLA
  11. Otto Von Bismark

 

SEHEMU B: MAJIBU MAFUPI

3. Jibu maswali yafuatayo kwa usahihi 

i) Ni yupi kati ya mabaharia wa kwanza kutoka Ureno alifanikiwa kufika Pwani ya Afrika Mashariki mwaka 1498?   

ii) Ni ipi kati ya mistari ya kufikirika huchorwa kwenye ramani kutoka upande wa Kaskazini kuelekea Kusini?  

 iii) Pasi inatumika kunyoosha nguo kuua vijidudu na kuondoa mikunjo au makunyanzi kwenye nguo. je, kuna aina ngapi za pasi?   

4. Malizia maelezo yafuatayo kama ulivyojifunza darasani

i) Ni taasisi ipi ilianzishwa na wakoloni nchini Tanganyika kwa lengo la utafutaji na usimamizi wa vibarua?  

ii) Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za asili na kutengenezwa. Ni rasilimali ipi inabeba rasilimali zote?  

iii) Kuna njia mbalimbali za kutayarisha na kupika vyakula. Ni njia ipi ya kupika chakula inatumia maji mengi?  

5. Jibu maswali yafuatayo kama.ulivyoelekezwa kwenye kila swali 

i) John aliambiwa achore ramani ya mtaa wake. Hivyo alikuwa anatafuta kipimio sahihi cha ramani. Ni aina ipi ya kipimio cha ramani utamshauri aitumie? 

ii) Ni yupi kati ya Marais wa awali barani Afrika alipigania uhuru wa nchi ya Malawi? 

6. Malizia maelezo yafuatayo 

i) Neno uthubutu kama linavyotumika kwenye ujasiliamali linamaanisha 

ii) Mlima Kilimanjaro ni fahari ya nchi yetu na ni chanzo na kivutio cha watalii nchini. Una mwinuko wa mita 5895 juu ya usawa wa bahari. Aina ya mlima huo ni 

SEHEMU C:  RAMANI, MCHORO NA KUKOKOTOA. 

Soma maswali yafuatayo kisha andika majibu sahihi

7. I) Kama dunia inatumia saa 1 kuizunguka nyuzi 15 za longitudo. Itachukua muda gani dunia kuzunguka jua kwa nyuzi 60? 

ii) Kama kipimio cha ramani ni 1:500,000. Ni kilomita ngapi juu ya ardhi zitawakilishwa kwa sentimita 1 kwenye ramani?  

 iii) Jifunze kwenye mchoro ufuatao kisha taja kielelezo cha hali ya hewa kinachopimwa na mchoro huo, kielelezo hicho ni   

iv) Tunaitaje mavazi maalum yanavotumika na wasanii kwenye kuigiza au kucheza ngoma? 

v) Aina gani ya bandari imeonyeshwa kvya herufi B kwenye ramani? 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 104

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

JARIBIO LA KUJIPIMA NUSU MUHULA WA KWANZA 2024 

                         SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI DARASA: VII 

SEHEMU A (ALAMA 20) 

  1. Chagua jibu sahihi na kisha uandike herufi ya jibu sahihi hilo katika nafasi uliyopewa Mpenja ni mjasiliamali ambaye ameajiri watu nane katika shughuli zake. Je, yupo katika kundi gani la ujasiriamali? A. mdogomdogo B. kati C. mkubwa D. wastani E. mdogo [ ]
  2. Wanafunzi wa darasa la sita walijifunza kuhusu mistari ya kufikirika inayochorwa katika ramani. Je, ni mistari ipi huchorwa kutoka upande wa magharibi kuelekea mashariki? A. mstarihi B. kontua C. longitudo D. Ikweta E. latitudo [ ]
  3. Ni kwa jinsi gani Misri na Zanzibar zilipata uhuru wake? A. vita vya msituni B. katiba C. mapinduzi C. mapinduzi na vita D. Mapinduzi na vita E. katiba na vita [ ]
  4. Kwanini ni muhimu kuwa na wimbo wa shule? `A. hukuza vipaji B. huenzi utamaduni wa taifa C. huleta uzalendo katika shule D. ni utambulisho wa shule E. utambulisho wa wazazi na walezi [ ]
  5. Katika kujifunza stadi za ramani, wanafunzi wengi walishindwa namna ya kuanza kusoma mistari ya gridi. Je, ni kwa namna gani mistari ya gridi huanza kusomwa? A. mistari ya ulalo halafu latitudo B. mistari ya ulalo halafu wima C. mistari ya latitudo halafu longitudo D. mistari ya ulalo tu E. mistari ya wima halafu ulalo [ ]
  6. Ni kiongozi yupi kati ya hawa wafuatao aliongoza serikali dhalimu ya makaburu nchini Afrika Kusini mwaka 1989 – 1994? A. Nelson Mandela B. Keneth Kaunda C. Idd Amin D. De Clerk E. Desmond Tutu [ ]
  7. Bunge lina viongozi mbalimbali. Yupi kati ya wafuatao ni kiongozi wa sekretarieti ya bunge? A. Waziri Mkuu B. Spika C. Katibu Kiongozi D. Kiongozi wa upinzani E. Katibu wa bunge [ ]
  8. Wanafunzi walitakiwa kumtaja kiongozi ambaye huhakikisha kuwa shughuli za kila siku shuleni zinatekelezwa, lipi lilikuwa ni jibu sahihi? A. mwalimu wa zamu B. mwenyekiti wa kamati ya shule C. mwalimu mkuu D. kaka na dada mkuu E. mwalimu wa darasa [ ]
  9. Lipi kati ya matukio yafuatayo lilitokea Ulaya kati ya karne ya 18 na 19? A. kuzuka kwa ugonjwa wa ebola B. uvamizi katika nchi za kiafrika C. kukua kwa mapinduzi ya viwanda D. kuzuka kwa vita kuu ya dunia E. Hitler kuitawala dunia [ ]
  10. Wafuatao ni wadudu waharibifu wanaopatikana nyumbani isipokuwa;- A. kunguni, panya na viroboto B. viroboto, nzi na mbu C. mbu, mende na kunguni D. mende, nzi na chawa E. chawa, viroboto na kunguni [ ]
  11. Ni katika tabianchi ipi kati ya zifuatazo ambapo hali ya joto hujitokeza katika miezi ya Juni, Septemba, Novemba na Aprili? A. tropiki B. jangwa C. Ikweta D. pwani E. nusu jangwa [ ]
  12. Katika mfumo wa jua, ni gimba lipi ambalo robotatu ya eneo lake limefunikwa na maji? A. Kausi B. Bahari C. Mirihi D. Zohari E. Dunia [ ]
  13. Majanga ya moto huweza kusababishwa na moto wa asili au shughuli za binadamu. Je, kipi ni chanzo kikubwa cha moto kwenye maeneo yenye misitu minene? A. urinaji wa asali B. uwindaji C. umeme wa radi D. milipuko ya radi E. uvutaji wa sigara [ ]
  14. Ni tukio lipi kati ya haya yafuatayo ni matokeo ya nguvu ya mvutano kati ya dunia na mwezi? A. kupatwa kwa mwezi B. kupatwa kwa dunia C. kupwa na kujaa kwa maji D. mwezi kukaa henamu E. dunia kujizungusha katika mhimili wake [ ]
  15. Kitendo cha kutekeleza wazo jipya kwa lengo la kutengeneza au kuboresha bidhaa au huduma huitwaje? A. ujasiriamali B. akili C. ubunifu D. usanii E. utundu [ ]

2. Katika swali hili umepewa sehemu A na Sehemu B. Oanisha sehemu hizo ili kupata maelezo yenye mantiki. 

Sehemu A

Sehemu B

  1. Tsunami
  1. Nguvu za asili na shughuli za binadamu
  1. Umeme wa radi na joto kali
  1. Moto wa asili
  1. Tetemeko la ardhi na mlipuko wa volikano
  1. Lava
  1. Athari za janga la moto
  1. Mawimbi makubwa ya bahari yanayosababishwa na tetemeko la ardhi la chini ya bahari
  1. Magma
  1. Aina za majanga

 

  1. Hewaukaa kuongezeka

 

  1. Miamba iliyoyeyuka kwa joto kali chini ya ardhi

 

SEHEMU B: (ALAMA 20) 

3. Mwishoni mwa mwaka 2023 wilaya ya Hanang iliyopo mkoani Manyara ilikumbwa na moja ya majanga ya asili ambalo lilipelekea kutokea kwa madhara mbalimbali.

  1. Je, ni janga gani liliikumba wilaya ya Hanang? 
  2. Taja madhara mawili yaliyosababishwa na janga hilo na 
  3. Bainisha njia mbili ambazo jamii inaweza kuzitumia kama tahadhari ili kuzuia kutokea kwa janga kama hilo na 

4. Maendeleo ya binadamu yamepitia katika vipindi mbalimbali ambavyo ni zama za mawe, zama za chuma na zama za teknolojia ya kisasa ya kidigitali. 

  1. Je, ni kitu gani huitambulisha zama husika?  
  2. Zama za mawe zimegawanyika katika zama za kale, za kati na za mwisho. Taja shughuli kuu mbili za kiuchumi ambazo binadamu alianza kuzifanya katika zama za mawe za mwisho. na 
  3. Katika zama za kati za mawe binadamu aliweza kusafiri na kuishi maeneo mbalimbali yenye baridi kali duniani; je, ni nini kilimwezesha kuweza kuishi maeneo hayo? 

5. Tabianchi ni wastani wa hali ya hewa ya eneo fulani iliyorekodiwa kwa kipindi kisichopungua miaka 30. 

  1. Kuna mambo makuu matatu yanayoathiri tabianchi,taja mambo mawili na 
  2. Ukataji wa miti na matumizi ya fueli za kisukuku huweza kusababisha ongezeko la kitu gani duniani? 

6. Kuanzia karne ya 20 Tanganyika iliwekwa chini ya utawala wa Kiingereza;- 

  1. Taja tukio kubwa la kihistoria ambalo lilitokea duniani na athari zake zikapelekea Tanganyika kuwa chini ya utawala wa Kiingereza 
  2. Bainisha aina ya utawala waliotumia Waingereza katika kuitawala Tanganyika 

SEHEMU C : ALAMA 10 

7. Chunguza jedwali ulilopewa likiwa linaonesha matukio ya kihistoria Tanzania kisha jibu maswali kipengele cha a-e 

  1. Taja angalau vifaa viwili vinavyoweza kutumika katika kukusanya taarifa za kihistoria  na 
  2. Wanahistoria hutumia vyanzo mbalimbali katika ukusanyaji na utunzaji wa kumbukumbu, taja angalau vyanzo viwili. na 
  3. Ikiwa umetembelea kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam ili kujifunza zaidi kuhusiana na tukio la kihistoria lililotokea mwaka 1961, bainisha njia mbili utakazotumia katika kukusanya taarifa hizo.
  4. Ni sehemu gani ya makumbusho ambako zinapatikana kumbukumbu za hayati Julius K. Nyerere tu?
  5. Bainisha mataifa ambayo yalihusika katika tukio la kihistoria la mwaka 1978 – 1979.

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 94

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA KWA MSINGI  

NUSU MUHULA WA PILI-AGOSTI-2023

SOMO: MAARIFA YA JAMII NA STADI ZA KAZI 

JINA LA MTAHINIWA ______________________________________ MUDA SAA 1:30

 

SEHEMU A: KUCHAGUA

Chagua jibu sahihi kisha uandike herufi yake katika kisanduku ulichopewa 

  1. Tanganyika ilianza kutawaliwa na Uingereza baada ya tukio lipi?
    1. Mkutano wa Berlin     C. Vita ya pili ya Dunia
    2. Vita ya kwanza ya Dunia  D. Vuguvugu la MAUMAU E. Vita yaMaji Maji  [  ]
  2. Baraza la kutunga sheria nchini Tanganyika lilianzishwa na Donald Cameroon mnamo mwaka:   A. 1919               B. 1945                C. 1926                D. 1920                E. 1954                               [               ]
  3. Chama kilichopigania na kuikomboa Msumbiji kutoka kwa wakoloni kiliitwa:
    1. MPLA   B. SWAPO   C. FRELIMO    D. UNIP   E. TANU     [  ]
  4. Uchaguzi mkuu wa vyama vingi nchini Tanzania ulifanyika mwaka:
    1. 1960   B. 1962   C. 1995   D. 1965     E. 1992     [  ]
  5. Patrice Lumumba ataendelea kukumbukwa kama miongoni mwa mashujaa wa Afrika walioongoza harakati za kuikomboa nchi ya:                                                                                      [              ]
    1. Uganda   C. Ghana   E. South Africa   B. Kenya   D.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  
  6. Kiongozi wa kabila la Wamasai aliitwa nani?
    1. Olaiboni    B. Rubega   C. Laigwanani   D. Ndito   E. Morani     [  ]
  7. Tanganyika ilijipatia Uhuru wake katika karne ya ngapi?
    1. 18          B. 17     C. 20      D. 19     E. 15           [  ]
  8. Bunge la Afrika (PAP) liliundwa mwaka gani?
    1. 1967   B. 1963   C. 2004    D. 2014   E. 2002       [  ]
  9. Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Rais wa Tanganyika mnamo mwaka:
    1. 1967   B. 1964  C. 1962   D. 1977   E. 1961       [  ]
  10. Chama cha siasa kilichoipinga TANU wakati wa harakati za kuikomboa tangayika kilittwa:
    1. ASP   B. TAA   C. UTP  D. CHADEMA  E. CUF     [  ]
  11. Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika lini?           [ ]
    1. Desemba, 1963   C. Januari, 1963  E. Desemba, 1964  B. Aprili, 1964  D.Januari, 1964 
  12. Mistari ya kubuni inayochorwa kwenye ramani kuunganisha sehemu zote zenye kiwango sawa cha mvua huitwa:
    1. Isobars    B. Isotherms    C. Isohels      D. Isohyets    E. Kontua     [  ]
  13. Mkoa maarufu kwa kilimo cha zabibu nchini ni:
    1. Dodoma    B. Morogoro    C. Mtwara  D.Iringa   E. Kigoma     [  ]
  14. Tafuta muda wa mji wa Dar es salaam, Tanzania ikiwa ni saa 2:00 katika mji wa Nairobi, Kenya uliopo nyuzi 45 Mashariki: 
    1. 1:00 jioni    B. 3:00 usiku  C. 2:00 usiku   D. 3:00 asubuhi  E. 2:00 asubuhi  [  ]
  15. Barometa ni kifaa kinachotumika kupima:            [ ]
    1. Kasi ya upepo  B. Jotoridi  C. Mvua  D.Mgandamizo wa hewa  E. Unyevu wa hewa
  16. Jua la utosi katika tropiki ya Kansa hutokea tarehe ngapi?
    1. 22 Desemba  B. 21 Juni   C. 23 Septemba    D. 21 Machi    E. 12 Juni  [  ]
  17. Mvua hupimwa katika kizio kipi?
    1. Kipima mvua   B. Kilomita   C. Millimita      D. Barometa   E. Mita   [  ]
  18. Shuguhuli kuu ya uchumi inayofanywa na watu wanaokaa karibu na fukwe za maziwa na bahari ni:
    1. Uchimbaji madini    B. Uvuvi  C. Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa    D. Biashara    E. Ufugaji wa nyuki                                                                                                                                   [               ]
  19. Joto hupungua kwa kiwango cha nyuzi 0.6 za Sentigredi kwa kila baada ya ongezeko lipi la mwinuko kutoka usawa wa bahari?
    1. Mita 50    B. Mita 100   C. Mita 150  D. Mita 6O   D. Mita 300        [  ]
  20. Kituo cha kuzalisha umeme cha bwawa la Nyumba ya Mungu kipo katika mto gani?

        A. Zambezi      B. Pangani     C. Wami      C.Rufiji 

iji

 

 

 

 

 

21. Nyota iliyo karibu sana na dunia inaitwa:

  

 

 

 

[

]

 A. Sumbula   C. Jua   

E. Zebaki

 

 

 

 

 

 B. Mwezi      D. Asteroidi 

  

 

 

 

[

]













  1. Upi SIYO aina ya usafiri?
    1. Usafiri wa ardhini  C. Usafiri wa majini   E. Usafiri wa nchi kavu
    2. Usafiri wa mdomo  D. Usafiri wa anga            [  ]
  2. Mahitaji ya msingi ya familiani:
    1. Elimu, usafi na afya   B. Maji, kilimo na chakula   C. Hewa, usafi na malazi                            D. Chakula, malazi na mavazi                             E. Heshima, chakula na chakula                             [               ]
  3. Ukabaila ni mfumo wa uzalishaji mali uliolenga katika umilikaji wa:
    1. Mabenki    B. Watumwa  C. Viwanda      D. Ardhi   E. Barabara      [  ]
  4. Kinjekitale Ngwale ni maarufu katika historia ya Tanzania kwa:
    1. Mfumo wake bora wa kuitawala Kilwa
    2. Ushujaa wake wa kuendesha biashara Kilwa
    3. Kuwahamasisha watu kupinga utawala wa Kijerumani
    4. Ufanisi wake wa kukusanya kodi kwa niaba ya wajerumani
    5. Uwezo wake wa kutengeneza na kutumia dawa za mitishamba      [  ]
  5. Karl Peters alikuwa ni wakala wa kikoloni aliyewashawishi viongozi wa kimila kusaini mikataba ya kilaghai ili kuifanya Tanganyika kuwa koloni la:
    1. Wareno        C. Wajerumani       E. Waingerez
    2. Wafaransa     D. Makaburu             [  ]
  6. Gavana wa mwisho aliyekuwa Mwingereza ambaye aliikabidhi Tanganyika mikononi mwa Watanganyika ili wajitawale wenyewe aliitwa:
    1. Donald Cameroon  C. Horace Byatt     E. Richard Turnbull   [  ]
    2. Edward Twinning  D. Julius Von sodden    
  7. Jua huonekana kuwa kubwa kuliko nyota zote kwa sababu:
    1. Lina joto kali zaidi ya nyota zingine
    2. Linang’aa zaidi ya nyota zingine  D. Liko bali sana na Dunia
    3. Hutupatia nishati ya jua    E. Lipo karibu zaidi na Dunia    [  ]
  8. Mwezi unapokuwa katikati ya Dunia na jua huonesha kupatwa kwa:
    1. Dunia  B. Nyota   C. Mwezi       D. Jua   E. Sayari       [  ]
  9. Matokeo makuu ya viwanda katika mazingira ni:
    1. Uchafuzi wa maji na hewa  D. Kumwaga kemikali na kutoa moshi
    2. Kutoa moshi na matumizi makubwa ya nishati E. Uchafuzi wa hewa, maji na ardhi
    3. Uchafuzi wa hewa na udongo               [  ]
  10. Moja ya majanga yanayosababishwa na kani za asili na binadamu ni:
    1. Mlipuko wa volkano  C. Tetemeko la ardhi  E. Mmomonyoko wa udongo[  ]
    2. Sunami     D. Kimbunga 
  11. Jina jumuishi la mito, ardhi, misitu na madini ni:
    1. Bidhaa za nje  C. Uoto wa asili
    2. Dunia           D. Rasilimali za asili   E. Mbuga za wanyama  [  ]
  12. Itakuwa saa ngapi katika mji wa Kagali uliopo 15Mashariki ikiwa ni saa 4:30 asubuhi katika mji wa Mtwara uliopo 300Mashariki?
    1. 3:30 asubuhi  B. 3:30 usiku     C. 5:30 asubuhi   D. 5:30 usiku E. 4:30 usiku   
  13. Jua likiwa katika kizio cha kusini, upepo huvuma kutokea wapi? 
    1. Kusini          C. Mashariki              E. Kaskazini-mashariki
    2. Magharibi               D. Kaskazini          [  ]
  14. Idadi kamili ya watu katika eneo fulani inaweza kupatikanaje?    A.  Kuhesabu idadi ya vizazi      B. Kutathmini eneo husika     C. Kuhesabu vifo       D. Kufanya sensa                                
    1.   Kuhesabu wakimbizi         [ ]
  15. Ipi kati ya hizi zifuatazo ni faida ya kufua nguo?
    1. Kuonekana nadhifu    C. Kuzibadili rangi   E. Kutopendeza   [  ]
    2. Zionekane mpya     D. Zionekane zimechakaa
  16. Kitendo cha kugeuza takataka kuwa bidhaa zinazoweza kutumika huitwa:

A. Sanaa  B. Uharibifu    C. Umwagiliaji D. Urejeleaji    E. Upunguzaji    [  ]

  1. Njia rahisi zaidi ya upishi wa chapatti ni:

A. Kuunguza      B. Kukaanga kwa mafuta machache     C. Kuunga   D. Kufukiza                    E. Kukaanga kwa mafuta mengi                               [               ]

  1. Sanaa ya kupangilia sauti katika namna inayovutia hujulikana kama:
    1. Sanaa   B. Ufinyanzi    C. Kelele   D. Besi   F. Muziki     [  ]
  2. Mashine inayotumika kushonea nguo hujulikana kama:
    1. Oveni  C. Hita  E. Nyenzo   Mashine ya kufulia     D. Cherehani   [ ]

 

SEHEMU B: MAJIBU MAFUPI

Jibu kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi wazi 

  1. Njia ya kupata habari na matukio ya kale kwa njia ya mdomo kupitia vitendawili, hadithi, methali na tamathali za semi hujulikana kama _______________________________
  2. Taja aina mbili za makazi ya binadamu

i.___________________________________________________________________ ii.____________________________________________________________________

  1. Ni tabaka lipi la angahewa ambapo shughuli za kila siku za binadamu hufanyika?

_______________________________________________________________

  1. Ikiwa ni saa 4:00 asubuhi katika mji L uliopo nyuzi 30 Mashariki, Je, itakuwa ni saa ngapi katika mji M uliopo nyuzi za Longitudo 60 Mashariki?

_______________________________________________________________________

  1. Njia haramu inayotumiwa na wajasiriamali kukwepa kulipa kodi kwa kuficha sehemu ambazo bidhaa zao huzalishwa inaitwa __________________________________

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 84

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOGIA

  MTIHANI WA NUSU MUHULA SEPT 2022

DARASA LA VII  

 

SEHEMU A


Chagua herufi ya jibu sahihi

URAIA

  1. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika ngazi ya wilayani: A. Mkurugenzi mtendaji wa wilaya B. Mbunge   C. Katibu tawala wilaya   D. Mkuu wa Wilaya E. Diwani   (         )
  2. Sanaa za maonyesho hujumuisha mambo yafuatayo: A. Nyimbo, hadithi na mashairi.   B. Hadithi, ushonaji nangonjera    C. Ufumaji, michezo na ngonjera D. Uchoraji, ususi na ufinyanzi     E. Maigizo, ususi na ngoma  (        )
  3. Mazao mawili yanayooneshwa kwenye nembo ya taifa ya Tanzania ni: A. Kahawa na katani   B. Katani na karafuu    C. Karafuu na pamba    D. Chai na tumbaku   E. Pamba na kahawa  (       )
  4. Nani msimamizi mkuu wa watumishi wa umma katika ngazi ya mkoa? A. Kamanda wa polisi Mkoa    B. Katibu tawala Mkoa  C. Afisa Elimu Mkoa   D. Mkuu wa Mkoa E. Mganga Mfawidhi wa  Mkoa (      )
  5. Chombo cha serikali chenye mamlaka ya kumuondoa Rais madarakani ni  A. Bunge  B. Jeshi la wananchi    C. Mahakama  D. JajiMkuu   E. Baraza la Mawaziri.
  6. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia Wakimbizi na Elimu, sayansi na utamadunini  A. IMF na ILO B. UNESCO  na UNICEF C. UNHCR  na UNESCO D. WHO na UNHCR  E. UNEP na FAO   (       )
  7. Mkusanyiko wa sheria ambazo huiwezesha serikali kutawala nchini huitwa: A. Kanuni   B. Dira ya taifa    C. Katiba     D. Ilani ya chama tawala   E. Sera ya Nchi     (        )
  8. Ardhi, Misitu, Maji na Madini kwa pamoja huitwa:  A. Uoto wa asili   B. Mahitaji muhimu ya binadamu  C. Hifadhi za taifa  D. Rasilimali za taifa   E. Makazi ya wanyama pori    (         )
  9. Dodoma ilitangazwa kuwa makao makuu ya nchi ya Tanzania mwaka gani? A. 1961    B. 1974   C. 2015  D. 1965   E. 1973    (         )
  10. Kuna jumla ya nchi ngapi zinazounda jumuiya ya Afrika  Mashariki?  A. 3    B. 4    C. 5    D. 6     E. 7
  11. Ni wakati gani bendera ya taifa inaweza kupandishwa nusu mlingoti?  A. Msiba wa kitaifa    B. Ziara ya Rais    C. Uchaguzi wa kitaifa   D. Kuvunjwa kwa Bunge E. Rais kuondolewa madarakani    (        )
  12. Zifuatazo ni mila na desturi zisizofaa kwenye jamii isipokuwa:  A. Ukeketaji    B. Mafunzo ya ulinzi wa jadi     C. Kurithi wa jane     D. Ubaguzi wa kijinsia   E. Ndoa za utotoni    (         )

 

HISTORIA

  1. Muunganiko wa watu wenye uhusiano wa damu na wanaishi pamoja huitwa: A. Kijiji     B. Kabila    C. Familia   D. Ukoo    E. Jamii   (       )
  2. Soko kuu la biashara ya watumwa Afrika Mashariki lilikuwa wapi? A. Bagamoyo    B. Mtwara    C. Kilwa     D. Zanzibar    E. Mombasa   (        )
  3. Nchi nyingi za Afrika zilianza kupigania uhuru wao baada ya tukio lipi kati ya haya: A. Vita ya kwanza ya dunia   B. Vita ya maji maji   C. Uhuru   D. Vita ya pili ya dunia E. Jumuiya ya Mataifa  (       )
  4. Azimio la Arusha lililenga: A. Kilimo    B. Ulinzi na amani    C. Kupinga ubaguzi wa rangi    D. Sera ya Ujamaa na kujitegemea E. Uhuru wa Tanganyika
  5. .Wafanyabiashara wa mwanzo kutoka nje ya Afrika kufika pwani ya Afrika Mashariki walitokea:  A. Ulaya     B. Asia     C. Amerika Kaskazini     D. Amerika Kusini      E. Australia    (        )
  6. Angola ilipata uhuru wake mwaka 1975 chini ya uongozi wa chama gani? A. MPLA      B.FRELIMO    C. SWAPO     D. KANU    E. CPP  (         )
  7. .Nchi mbili za Afrika ambazo hazikutawaliwa kabisa na wakoloni ni zipi? A. Tanganyika na Ghana     B. Liberia na Libya    C. Ethiopia naTanganyika  D. Liberia na Zimbabwe  E. Liberia na Ethiopia (       )
  8. Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanzania alikuwa: A. Julius Nyerere    B. Rashid Kawawa    C. John Malecela   D. Edward Moringe Sokoine E. Mizengo Pinda    (          )
  9. Mwanzilishi wa kampuni ya kibiashara ya Kijerumani Afrika Mashariki (GEACo) aliitwa: A. Karl Peters  B. Cecil Rhodes    C. George Goldie    D. William Macknon   E. Frederick Lugard   (          )
  10. .Binadamu alianza kuchoma misitu ili kuwafukuza wanyama wakali katika zama zipi za mawe?  A. Mwanzo    B. Mwisho     C. Chuma    D. Kale   E. Kati
  11. Ni jamii zipi kati ya hizi zilijihusisha na biashara ya masafa marefu? A. Wayao, Wakamba na Waha   B. Wanyamwezi, Wagogo na Wakamba   C. Wayao, Wanyamwezi na Wakamba  D. Wapare, Wajaluo na Wanyamwezi   E. Wagogo, Wasukuma na Wakamba
  12. Tarehe 12/1/1964 inakumbukwa kwa tukio lipi la kihistoria? A. Uhuru na Jamhuri   B. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar    C. Azimio la Arusha D. Mapinduzi ya Zanzibar  E. Uhuru wa Tanganyika
  13. Dhana mbili zenye kuelezea chimbuko la binadamu ni: A. Dhana ya dini na sayansi   B. Dhana ya maelezo na dini   C. Dhana ya sayansi na maelezo D. Dhana ya dini na uislamu E. Dhana ya dini na ukristo    (           )
  14. Vita vya majimaji vilipiganiwa kuanzia mwaka _______mpaka_______ A. 1906-1907    B. 1904-1908     C. 1905-1907      D. 1903-1906      E. 1906-1908    (            )

 

JIOGRAFIA

  1. Dunia inapolizunguka jua hutokea nini? A. Majira ya mwaka    B. Usiku na mchana    C. Mwezi mwandamo     D. Kupwa na kujaa kwa maji  E. Kiangazi na usiku    (         )
  2. Afrika mashariki inapatikana kwenye longitude ipi? A. 45 Magharibi B. 0C. 15 MagharibiD. 45 MasharikiiE. 30 Mashariki    (             )
  3. Nchi ya Misri huzalisha nguvu za umeme kutoka katika bwawa lipi? A. Akasombo    B. Aswan   C. Kabora Bassa   D. Owen   E. Mtera   (         )
  4. .Jua la utosi kwenye latitude ya ikweta hutokea miezi ipi? A. Januari na Februari  B. Aprili na Julai   C. Machi na Septemba   D. Julai na Februari E. Mei na Juni       (         )
  5. Picha inayoonesha misitu minene na mazao kama michikichi itakuwa imepigwa kutoka katika eneo lenye hali gani? A. Kitropiki   B. Jangwa   C. Kimeditrenian    D. Kiikweta    E. Kimonsuni (         )
  6. Sehemu ya ardhi iliyo tambarare kati ya vilele au safu za milima huitwaje? A. Bonde   B. Kigongo    C. Genge    D. Pitio   E. Uwandawajuu     (          )
  7. Maziwa yanayopatikana katika bonde la ufa la Afrika Mashariki upande wa mashariki ni: A. Natron, Eyasi na Manyara B. Natron,NyasanaRukwa C. Manyara ,Nyasa na Tanganyika D. Rukwa,Natronna Victoria E. Victoria,Tanganyikana Nyasa   (          )
  8. Kifaa maalum kinachotumika kupima mwendo kasi wa upepo huitwaje? A. Haigromita    B. Kipima upepo    C. Themometa    D. Barometa   E. Anemometa     (         )
  9. Ni tukio gani hutokea mwezi ukiwa kati kati ya jua na dunia?  A. Kupatwa kwa dunia  B. Kupatwa kwa jua  C. Kupatwa kwa mwezi  D. Mvua kubwa E. Tetemeko la ardhi      (           )
  10. Yafuatayo ni majanga ya asilii sipokuwa: A. Vita na ajali   B. Mafuriko   C. Mlipukowa volcano  D. Tetemeko la ardhi   E. Ukame   (           )
  11. Ikiwa ni saa 2 asubuhi katika mji A uliopo kwenye nyuzi 30 mashariki, je itakuwa ni saa ngapi katika mji B uliopo kwenye nyuzi 90 mashariki? A. 12 asubuhi B. 3 Asubuhi    C. 6 adhuhuriD. 9 usiku E.  9 mchana      (            )
  12. Mistari ya gridi husomwa kwa tarakimu sita, je zipi ni tarakimu za mstari wa ulalo katika gridi 375746?  A. 375    B. 574    C. 746     D. 375746     E. 346 (         )
  13. Mwinuko, mito, maziwa ,mabwawa na mabonde ni vitu vinavyounda nini? A. Uoto wa asili    B. Bonde la ufa     C. Tabia ya nchi     D. Vyanzo vya maji   E. Sura ya nchi      (          )
  14. Iwapo kipimio cha ramani ni 1:600,000. Je, Sentimeta1 inawakilisha Kilometa ngapi? A. Km 60   B. Km 0.6   C. Km 1    D. Km 6    E. Km 6000 (       )

 

SEHEMU B:

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI

  1. Mhimili wa serikali unaohusika kupokea, kujadili na kupitisha bajeti ya serikali  huitwa:......
  2. Mfumo wa Ukabaila ambao msingi wake mkuu ulikuwa ni ardhi uliosha mirima eneo ya kanda ya ziwa  hulijulikana kama______
  3. Lengo kuu la kusaini wa kwa mkataba wa Freire kati ya sultani wa Zanzibar na Freire mwaka 1873 lilikuwa_____________
  4. Unyevu hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwacho______________________________
  5. Badili nyuzi 45 za sentigred kuwa faren haiti_______________________________



LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 66

WIZARA YA ELIMU

MTIHANI WA I MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA. JAN, 2021

JINA LA MTAHINIWA:______________________________________________________________

SEHEMU:  A CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI ZAIDI NA UIANDIKE KATIKA KARATASI YAKO YA KUJIBIA.

  1. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 – 1885 uliitishwa na _____ A. Carl Peters B. Johann Krapf C. Henry Stanley D. Otto Von Bismark                                                                                                [    ]
  2. Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka _____ A. 1961 B. 1962 C. 1977 D. 1964                   [    ]
  3. Ipi kati ya nchi zifuatazo ilipata uhuru kwa njia ya vita?_____ A. Ghana B. Tanganyika C. Msumbiji D. Zambia                                                                                                                                          [    ]
  4. Vita vya Majimaji vilipiganwa kati ya mwaka _____ A. 1908 – 1909 B. 1907 – 1905 C. 1905 – 1097 D. 1807 – 1905                                                                                                                                  [    ]
  5. Chama kilichokuwa kinapigania uhuru wa kweli Tanganyika ni _____ A. UTP B. ASP C. TANU D. TAO                                                                                                                                                   [    ]
  6. Rais wa kwanza wa chama cha TANU alikuwa _____ A. Julius K. Nyerere B. Nkwame Nkurumah C. Oscar Kambona D. Jomo Kenyatta                                                                                              [    ]
  7. Kiongozi wa Wahehe aliyepinga uvamizi wa Wajerumani nchini Tanganyika aliitwa _____ A. Mkwawa B. Gwasa C. Mtemi Isike D. Mangi Sina                                                                          [    ]
  8. Harakati za kudai uhuru kamili barani Afrika zilianza baada ya mwaka_____ A. 1945 B. 1961 C. 1884 D. 1960                                                                                                                                     [    ]
  9. Familia zenye asili moja huitwa _____ A. Ukoo B. Jamii C. Familia D. Ndugu                             [    ]
  10. Nchi zipi hazikutawaliwa na wakoloni barani Afrika?_____ A. Ethiopia na Liberia B. Liberia na Kenya C. Rwanda na Uganda D. Tanganyika na Liberia                                                                 [    ]
  11. Shirika la umoja wa mataifa linaloshughurikia wakimbizi linaitwa_____ A. UNICEF B. UNHCR C. FAO D. WHO                                                                                                                                   [    ]
  12. Chimbuko la Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ilikuwa mnamo mwaka_____ A. 1967 B. 1963 C. 2002 D. 1977                                                                                                                                [    ]
  13. Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka_____ A. 1977 B. 1967 C. 1948 D. 1917                                    [   ]
  14. Nchi za kwanza kuanzisha uhusiano na Tanganyika wakati wa ukoloni ni _____ na _____ A. Kenya na Msumbiji B. Uganda na Rwanda C. China na Msumbiji D. Kenya na Uganda                          [    ]
  15. Baadhi ya vyombo muhimu vinavyosaidia kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki ni _____ na _____ A. Bunge na Spika wa Bunge B. Bunge na Mahakama C. Mahakama na Majaji D. Soko la pamoja na ushuru wa forodha                                                                                                           [    ]
  16. Mojawapo ya shughuli zinazofanywa na binadamu zinaweza kuharibu mazingira ni _____ A. Uchimbaji wa madini B. ufugaji wa ndani C. Ukusanyaji takataka D. urejelezaji                           [    ]
  17. Kipimio kidogo cha ramani hutumika kuchorea_____ A. maeneo makubwa B. maeneo madogo C. maeneo ya kati D. maeneo madogo na ya kati                                                                                  [    ]
  18. Ni kitu gani muhimu katika ramani kinachotumika kutafsiri vitu vyote vilivyomo kwenye ramani? _____ A. Dira B. Ufunguo C. Kipimio D. Fremu                                                                             [    ]
  19. Yafuatayo ni majanga ya asili ispokuwa_____ A. onezeko la watu na tsunami B. kimbunga na mafuriko C. tetemeko la ardhi na mafuriko D.vita na njaa                                                               [    ]
  20. Majira ya mwaka hutokea kutokana na _____ A. kupatwa kwa mwezi B. mwezi kuizunguka dunia C. dunia kulizunguka jua D. kupatwa kwa jua                                                                                  [    ]
  21. Kupwa na kujaa kwa maji husababishwa na _____ A. dunia kuwa kati ya jua na mwezi B. kupatwa kwa jua C. uvutano kati ya mwezi na dunia D. kupatwa kwa mwezi                                               [    ]
  22. Mto Ruvuma upo upande gani mwa Tanzania? _____ A. Kusini B. Kaskazini C. Mashariki D. Magharibi                                                                                                                                          [    ]
  23. Haigrometa ni kifaa kinachotumika kupima _____ A. unyevu B. Jotoridi C. Mvua D. mwanga    [    ]
  24. Latitudo, mwinuko na umbali kutoka baharini ni mambo muhimu yanayoathiri _____ A. tabia ya nchi B. mfumo wa jua C. hali ya hewa D. mikondo ya bahari                                                         [    ]
  25. Kitu muhimu katika ramani kinachotumika kuonesha uwiano wa umbali katika ramani na umbali halisi kwenye ardhi huitwa _____ A. Kipimio B. Dira C. Ufunguo D. Fremu                                [    ]
  26. Nishati gani kati ya zifuatazo inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira? _____ A. mkaa B. jua C. maji D. upepo                                                                                                                               [    ]
  27. Sherehe za mafunzo yanayotolewa kwa vijana wa kiume ili kuwa wanajamii bora ni _____ A. jando B. unyago C. semina D. skauti                                                                                                   [    ]
  28. Bomba la kusafirishia mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Zambia linaitwa _____ A.TAZAMA B. TAZARA C. KAPIRIMPOSHI D.TANZANAITI                                                                           [    ]
  29. Miongoni mwa mashujaa wa Afrika waliopinga uvamizi ni _____ A. Agostino Neto, Kwame Nkurumah na Otto von Bismack B. Kwame Nkurumah, Isike, na Seyyid Said C.Otto von Bismack, Isike na Agostino Neto D. mfalme Menellik wa II, Msisiri na Mkwawa                                         [    ]
  30. Mkutano wa kuigawa Afrika ulifanyika katika nchi ya _____ A. Uingereza B. Marekani C. Ujerumani D. Ufaransa                                                                                                                     [    ]
  31. Vita ya kwanza ya dunia ilipiganwa kati ya mwaka _____na _____ A. 1939 -1945 B. 1905 – 1907 C. 1914 – 1918 D. 1884 – 1885                                                                                                    [    ]
  32. Sayari yenye viumbe hai ni _____ A. Sumbura B. Mihiri C. Zuhura D. Dunia                               [    ]
  33. Dunia hulizunguka jua kwa muda wa _____ A. saa 24 B. siku 300 C. Usiku na Mchana D. Siku 365.25 au 366                                                                                                                                    [    ]
  34. Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ni mlima _____ A. Meru B. Kilimanjaro C. Elgon D. Himalaya                                                                                                                                           [    ]
  35. Mgandamizo wa hewa katika mazingira hupimwa kwa chombo kinachoitwa _____ A. Anemometa B. Barometa C. Kipimaupepo D. Haigrometa                                                                                  [    ]

SEHEMU: B CHUNGUZA RAMANI IFUATAYO KISHA JIBU MASWALI

C:UsersKYAMBODocumentsmocks and assorted examsMap-of-East-Africa-showing-six-regions-of-the-EMBLEM-study-area.jpg

  1. Ziwa kubwa Tanganyika limeoneshwa kwa herufigani? _____
  2. Ziwa lenye kina kirefu limeoneshwa kwa herufi gani? _____
  3. Herufi G inaonesha nchi gani? _____
  4. Nchi ya Burundi imeoneshwa kwa herufi ipi? _____
  5. Bahari ya Hindi ipo upoande upi mwa ramani ya Afrika Mashariki? _____

SEHEMU: C JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI

  1. Ni nchi gani ilikuwa ya kwanza kujipatia uhuru wake toka kwa wakoloni Barani Afrika _____
  2. Chama kilichoipatia uhuru nchi ya Msumbiji kinaitwa _____
  3. Shughuli ya uzalishaji mali ambayo imeajiri watu wengi kuliko shughuli nyingine Tanzania ni _____
  4. Mji mkuu wa nchi ya Tanzania unaitwa _____
  5.            Shirika la kimataifa linaloshughulikia watoto linaitwa _____

 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 60

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOGIA

  JARIBIO  LA  WIKI  MAARIFA YA JAMII

DARASA LA VII  - 2021

 

SEHEMU A


Chagua herufi ya jibu sahihi

URAIA

  1. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika ngazi ya wilayani: A. Mkurugenzi mtendaji wa wilaya B. Mbunge   C. Katibu tawala wilaya   D. Mkuu wa Wilaya E. Diwani   (         )
  2. Sanaa za maonyesho hujumuisha mambo yafuatayo: A. Nyimbo, hadithi na mashairi.   B. Hadithi, ushonaji nangonjera    C. Ufumaji, michezo na ngonjera D. Uchoraji, ususi na ufinyanzi     E. Maigizo, ususi na ngoma  (        )
  3. Mazao mawili yanayooneshwa kwenye nembo ya taifa ya Tanzania ni: A. Kahawa na katani   B. Katani na karafuu    C. Karafuu na pamba    D. Chai na tumbaku   E. Pamba na kahawa  (       )
  4. Nani msimamizi mkuu wa watumishi wa umma katika ngazi ya mkoa? A. Kamanda wa polisi Mkoa    B. Katibu tawala Mkoa  C. Afisa Elimu Mkoa   D. Mkuu wa Mkoa E. Mganga Mfawidhi wa  Mkoa (      )
  5. Chombo cha serikali chenye mamlaka ya kumuondoa Rais madarakani ni  A. Bunge  B. Jeshi la wananchi    C. Mahakama  D. JajiMkuu   E. Baraza la Mawaziri.
  6. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia Wakimbizi na Elimu, sayansi na utamadunini  A. IMF na ILO B. UNESCO  na UNICEF C. UNHCR  na UNESCO D. WHO na UNHCR  E. UNEP na FAO   (       )
  7. Mkusanyiko wa sheria ambazo huiwezesha serikali kutawala nchini huitwa: A. Kanuni   B. Dira ya taifa    C. Katiba     D. Ilani ya chama tawala   E. Sera ya Nchi     (        )
  8. Ardhi, Misitu, Maji na Madini kwa pamoja huitwa:  A. Uoto wa asili   B. Mahitaji muhimu ya binadamu  C. Hifadhi za taifa  D. Rasilimali za taifa   E. Makazi ya wanyama pori    (         )
  9. Dodoma ilitangazwa kuwa makao makuu ya nchi ya Tanzania mwaka gani? A. 1961    B. 1974   C. 2015  D. 1965   E. 1973    (         )
  10. Kuna jumla ya nchi ngapi zinazounda jumuiya ya Afrika  Mashariki?  A. 3    B. 4    C. 5    D. 6     E. 7
  11. Ni wakati gani bendera ya taifa inaweza kupandishwa nusu mlingoti?  A. Msiba wa kitaifa    B. Ziara ya Rais    C. Uchaguzi wa kitaifa   D. Kuvunjwa kwa Bunge E. Rais kuondolewa madarakani    (        )
  12. Zifuatazo ni mila na desturi zisizofaa kwenye jamii isipokuwa:  A. Ukeketaji    B. Mafunzo ya ulinzi wa jadi     C. Kurithi wa jane     D. Ubaguzi wa kijinsia   E. Ndoa za utotoni    (         )

 

HISTORIA

  1. Muunganiko wa watu wenye uhusiano wa damu na wanaishi pamoja huitwa: A. Kijiji     B. Kabila    C. Familia   D. Ukoo    E. Jamii   (       )
  2. Soko kuu la biashara ya watumwa Afrika Mashariki lilikuwa wapi? A. Bagamoyo    B. Mtwara    C. Kilwa     D. Zanzibar    E. Mombasa   (        )
  3. Nchi nyingi za Afrika zilianza kupigania uhuru wao baada ya tukio lipi kati ya haya: A. Vita ya kwanza ya dunia   B. Vita ya maji maji   C. Uhuru   D. Vita ya pili ya dunia E. Jumuiya ya Mataifa  (       )
  4. Azimio la Arusha lililenga: A. Kilimo    B. Ulinzi na amani    C. Kupinga ubaguzi wa rangi    D. Sera ya Ujamaa na kujitegemea E. Uhuru wa Tanganyika
  5. .Wafanyabiashara wa mwanzo kutoka nje ya Afrika kufika pwani ya Afrika Mashariki walitokea:  A. Ulaya     B. Asia     C. Amerika Kaskazini     D. Amerika Kusini      E. Australia    (        )
  6. Angola ilipata uhuru wake mwaka 1975 chini ya uongozi wa chama gani? A. MPLA      B.FRELIMO    C. SWAPO     D. KANU    E. CPP  (         )
  7. .Nchi mbili za Afrika ambazo hazikutawaliwa kabisa na wakoloni ni zipi? A. Tanganyika na Ghana     B. Liberia na Libya    C. Ethiopia naTanganyika  D. Liberia na Zimbabwe  E. Liberia na Ethiopia (       )
  8. Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanzania alikuwa: A. Julius Nyerere    B. Rashid Kawawa    C. John Malecela   D. Edward Moringe Sokoine E. Mizengo Pinda    (          )
  9. Mwanzilishi wa kampuni ya kibiashara ya Kijerumani Afrika Mashariki (GEACo) aliitwa: A. Karl Peters  B. Cecil Rhodes    C. George Goldie    D. William Macknon   E. Frederick Lugard   (          )
  10. .Binadamu alianza kuchoma misitu ili kuwafukuza wanyama wakali katika zama zipi za mawe?  A. Mwanzo    B. Mwisho     C. Chuma    D. Kale   E. Kati
  11. Ni jamii zipi kati ya hizi zilijihusisha na biashara ya masafa marefu? A. Wayao, Wakamba na Waha   B. Wanyamwezi, Wagogo na Wakamba   C. Wayao, Wanyamwezi na Wakamba  D. Wapare, Wajaluo na Wanyamwezi   E. Wagogo, Wasukuma na Wakamba
  12. Tarehe 12/1/1964 inakumbukwa kwa tukio lipi la kihistoria? A. Uhuru na Jamhuri   B. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar    C. Azimio la Arusha D. Mapinduzi ya Zanzibar  E. Uhuru wa Tanganyika
  13. Dhana mbili zenye kuelezea chimbuko la binadamu ni: A. Dhana ya dini na sayansi   B. Dhana ya maelezo na dini   C. Dhana ya sayansi na maelezo D. Dhana ya dini na uislamu E. Dhana ya dini na ukristo    (           )
  14. Vita vya majimaji vilipiganiwa kuanzia mwaka _______mpaka_______ A. 1906-1907    B. 1904-1908     C. 1905-1907      D. 1903-1906      E. 1906-1908    (            )

 

JIOGRAFIA

  1. Dunia inapolizunguka jua hutokea nini? A. Majira ya mwaka    B. Usiku na mchana    C. Mwezi mwandamo     D. Kupwa na kujaa kwa maji  E. Kiangazi na usiku    (         )
  2. Afrika mashariki inapatikana kwenye longitude ipi? A. 45 Magharibi B. 0C. 15 MagharibiD. 45 MasharikiiE. 30 Mashariki    (             )
  3. Nchi ya Misri huzalisha nguvu za umeme kutoka katika bwawa lipi? A. Akasombo    B. Aswan   C. Kabora Bassa   D. Owen   E. Mtera   (         )
  4. .Jua la utosi kwenye latitude ya ikweta hutokea miezi ipi? A. Januari na Februari  B. Aprili na Julai   C. Machi na Septemba   D. Julai na Februari E. Mei na Juni       (         )
  5. Picha inayoonesha misitu minene na mazao kama michikichi itakuwa imepigwa kutoka katika eneo lenye hali gani? A. Kitropiki   B. Jangwa   C. Kimeditrenian    D. Kiikweta    E. Kimonsuni (         )
  6. Sehemu ya ardhi iliyo tambarare kati ya vilele au safu za milima huitwaje? A. Bonde   B. Kigongo    C. Genge    D. Pitio   E. Uwandawajuu     (          )
  7. Maziwa yanayopatikana katika bonde la ufa la Afrika Mashariki upande wa mashariki ni: A. Natron, Eyasi na Manyara B. Natron,NyasanaRukwa C. Manyara ,Nyasa na Tanganyika D. Rukwa,Natronna Victoria E. Victoria,Tanganyikana Nyasa   (          )
  8.                                                                                                                                                                                Kifaa maalum kinachotumika kupima mwendo kasi wa upepo huitwaje? A. Haigromita    B. Kipima upepo    C. Themometa    D. Barometa   E. Anemometa     (         )
  9.                                                                                                                                                                                Ni tukio gani hutokea mwezi ukiwa kati kati ya jua na dunia?  A. Kupatwa kwa dunia  B. Kupatwa kwa jua  C. Kupatwa kwa mwezi  D. Mvua kubwa E. Tetemeko la ardhi      (           )
  10.                                                                                                                                                                                Yafuatayo ni majanga ya asilii sipokuwa: A. Vita na ajali   B. Mafuriko   C. Mlipukowa volcano  D. Tetemeko la ardhi   E. Ukame   (           )
  11.                                                                                                                                                                                Ikiwa ni saa 2 asubuhi katika mji A uliopo kwenye nyuzi 30 mashariki, je itakuwa ni saa ngapi katika mji B uliopo kwenye nyuzi 90 mashariki? A. 12 asubuhi B. 3 Asubuhi    C. 6 adhuhuriD. 9 usiku E.  9 mchana      (            )
  12.                                                                                                                                                                                Mistari ya gridi husomwa kwa tarakimu sita, je zipi ni tarakimu za mstari wa ulalo katika gridi 375746?  A. 375    B. 574    C. 746     D. 375746     E. 346 (         )
  13.                                                                                                                                                                                Mwinuko, mito, maziwa ,mabwawa na mabonde ni vitu vinavyounda nini? A. Uoto wa asili    B. Bonde la ufa     C. Tabia ya nchi     D. Vyanzo vya maji   E. Sura ya nchi      (          )
  14.                                                                                                                                                                                Iwapo kipimio cha ramani ni 1:600,000. Je, Sentimeta1 inawakilisha Kilometa ngapi? A. Km 60   B. Km 0.6   C. Km 1    D. Km 6    E. Km 6000 (       )

 

SEHEMU B:

JAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI

  1.                                                                                                                                                                                Mhimili wa serikali unaohusika kupokea, kujadili na kupitisha bajeti ya serikali  huitwa:......
  2.                                                                                                                                                                                Mfumo wa Ukabaila ambao msingi wake mkuu ulikuwa ni ardhi uliosha mirima eneo ya kanda ya ziwa  hulijulikana kama______
  3.                                                                                                                                                                                Lengo kuu la kusaini wa kwa mkataba wa Freire kati ya sultani wa Zanzibar na Freire mwaka 1873 lilikuwa_____________
  4.                                                                                                                                                                                Unyevu hupimwa kwa kifaa maalumu kiitwacho______________________________
  5.                                                                                                                                                                                Badili nyuzi 45 za sentigred kuwa faren haiti_______________________________


LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 58

WIZARA YA ELIMU

 MAARIFA YA JAMII                                                                                

MUDA: SAA 1:30                                                                                     

 

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina maswali ishirini na tano (45)
  2. Jibu maswali yote kwa kujaza nafasi wazi au kuandika herufi ya jibu sahihi

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

  1. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wa sasa anaitwa mheshimiwa __________(A)Dr.Ally Mohamed Shein (B)Samia Suluhu Hassan (C) Dr. john Pombe Magufuli (D)Kasimu Majaliwa kasimu ( D) Hussein Ally Mwinyi  (     )
  2. Muswada wa sheria huandaliwa na ________(A)wabunge (B)spika wa bunge (C) waziri wa sheria   (D) Mahakama  (E) Watanzania  (     )
  3. kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania raia anaweza kugombea urais akiwa na umri wa miaka ______(A)21 na Zaidi   (B)50 na Zaidi  (C) 18 na Zaidi  (D) 60 na zaidi  (D)40 na zaidi   (     )
  4. Nembo  ya taifa ina vitu vifuatavyo isipokuwa _________(A)Pembe za ndovu   (B) Pamba na mahindi  (C) Mwanamke na motto  (D) Jembe na nyundo (E) Mwanamke na mwanaume  (     )
  5. Vita vilivyotokea Rwanda 1994 vilitokana na _____(A)Uchaguzi  (B)Ukabila  (C) Rushwa  (D) Ukabaila  (E) Utajiri
  6. Kundi la familia anuai lenye chimbuko moja huitwa ___________ (A) jamaa  (B)Baba  na watoto  (C)Ndugu (D)Familia  ( E) Ukoo        (     )
  7.  _______________ni kipindi Fulani cha wakati katika maisha.  (A) zama (B) zana  (C)zama za mawe ( D) zama za chuma  (E) zama za ukoloni     (     )
  8. Janga kubwa linaloitikisa dunia mpaka sasa lililotokea mwishoni mwa mwaka 2019 ni _______(A) Vuguvugu la vita vya tatu vya dunia(B) Maradhi ya UKIMWI (C)Virusi vya korona (COVID 19)  (D) Moto uliotokea katika msitu wa amazon  (E) ukame          (      )
  9. Wareno wallijenga ngome ya yesu huko ______(A)Kilwa   (B) Mombasa  (C) Bagamoyo    (D)Zanzibar  ( E) Isimila
  10. Wafuatao ni mifano ya wapelelezi isipokuwa __________(A)Joseph Thompson  (B)Dr. David Livingstone  (C) Richard Burton  (D) Carl-Peters    (E) Sir. Richard Tanbull      (     )
  11. Mashamba makubwa ya kufugia wanyama huitwa?_______________(A)Ranchi (B) kongwa (C) kiborioni (D) Ufugaji (E) zizi            (     )
  12. Mtemi isike alikuwa kiongozi wa _________(A) Bunyoro (B)Wazaramo (C)Wanyamwezi (D)Maasai  (E) wahehe  (     )
  13. Utawala wa wajerumani Tanzania ulichukuliwa na____________ (A)Waarabu (B)Waingereza (C)Waafirika (D)Wabantu (E) Waburushi    (     )
  14. Ni ziwa gani linaitenganisha Tanzania na Malawi? _____(A)Nyasa (B)Victoria (C)Rukwa (D)Tanganyika ( E) Manyara                        (    ) 
  15. Mashine ndogo inayotumika kusaga vyakula na matunda huitwa ________ (A)cherehani (B)kitasa (C)blenda (D)jokofu (E) kisu na panga        (     )
  16. Mtu anayetengeneza kikapu kwa kutumia kili huitwa ______ (A)msani (B)msusi (C)mchoraji (D)mtengenezaji    (E) mwimbaji                                 (     )
  17. Mwelekeo kati ya kusini na magharibi huitwa__________(A)Kusini-kusini-magharibi (B)Kaskazini magharibi (C)Magharibu-Kusini-Magharibi (D)Kusini-magharibi  (E)  Magharibi -Kusini     (     )
  18. Ugonjwa mojawapo unaosumbua kuku ni  {a} upele {B mahepe [C] Ukurutu {D} Kichwa {E} Manjano  (     )
  19. Ni  chanzo gani cha nishati hutumika zaidi maeneo ya kijijini (A)Umeme (B)Kuni (C)Gesi asilia (D)Mafuta ya taa (E) Mkaa   (     )
  20. Biashara ya utumwa iliazishwa na __(A)Waingereza(B) Wajerumani (C) Waswahili (D)Wareno (E) Waarabu (     )
  21. Jua la utosi katika tropiki ya kansa hotokea__(A) 21 mwezi wa tatu (B) 21mwezi wa sita (C) 23 mwezi wa tisa (D) 22 mwezi wa saba (E) 20 Mwezi wa tisa (     )
  22. Kupatwa kwa mwezi  kutokea pale dunia inapokuwa katikati ya __(A)J ua namwezi (B) Sayari na nyota(C)Jua na sayari(D)Mwezi na dunia (E) Sayari na mwezi (     )
  23. Mambo yafuatayo husababisha kutokea kwa janga la Tsunami isipokuwa__(A) Mlipuko wa volcano (B) Kuanguka kwa vimondo baharini (C) Tetemeko la ardhi(D)Mafuriko (E) Maporomoko ya ardhi (     )
  24. Ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Afrika ni (A)Nyasa (B) Turkana (C) Victoria (D)Tanganyika (E) Kyoga  (     )
  25. Sayari yenye pete katika mfumo wa jua ni; (A) Sumbura (B) Sarateni (C) Zebaki (D) Zuhura (E) Dunia (     )
  26. Kahawa, chai, pareto na pamba ni (A) Mazao ya chakula (B) Madini (C) Mazao ya muda (D) Uvuvi (E) Mazao yua biashara (     )
  27.  Kifaa kinachotumika kuwekea pasi wakati wa kupiga pasi nguo  ni (A) kibao (B) farasi (C) kiti (D) meza (E) kabati (     )
  28. Mkataba wa mwaka------ ulijulikana kuwa mkataba wa heligoland uliofanyika kati ya serikali ya Uingereza na Ujerumani (A)1886(B)1990 (C)1890 (D)1907 (E) 1884 (     )
  29. Makumbusho ya mkwawa yanapatikana__(A)Isimila (B) Amboni (C) Kalenga(D) Ruaha (E) Bagamoyo (     )
  30. Kipindi cha miaka 1000 huitwa___(A)Milenia (B)Karne(C)Mlongo(D)Kalenda (E) Zama (     )
  31. Tanzania ni mwanachama wa jumuiya zifuatazo isipokuwa __(A) SADC (B)AU ( C) ECOWAS (D) EAC  (E) NAM (     )
  32. Mikoa inayoonyesha dalili ya jangwa Tanzania ni ipi?(A)Tanga na Iringa (B) Iringa na Mbeya (C) Mwaza na mara (D) Shinyanga na Dodoma (E)  Njombe na Ruvuma (     )
  33. Watu  walio wengi Tanzania ni _(A)Waajiriwa serikalini (B)Wavuvi (C) Wakulima (D)Wafanyakazi wa benki (E) Wafanyabiashara (     )
  34. Migogoro kati ya wakulima na wafugaji husababishha na upungufu wa __(A)Eneo la kuchugia na kulima   (B)Ujuzi    (C)Vifaa vya kisasa   (D)Elimu (E) Upungufu wa wakulima (     )
  35. Madini ambayo yanaweza kuwa chanzo cha nishati ni kama__(A) Dhahabu na almasi  (B) Tanzanite na shaba  (C) Chuma na chumvi   (D) Makaa ya mawe na gesi asilia (E) Dhahabu na shaba (     )
  36. Kitendo cha kutembelea sehemu kwa ajili ya kujifunza na kustarehe huitwa (A)Vivutio vya watalii (B) Utalii (C) Biashara (D)Mtalii (E) Mpelelezi (     )
  37. Hifadhi zote za wanyama zinasimamiwa na chombo kinachoitwa (A) TRA (B) TAMWA (C)TANAPA (D)NEMC (E) TANROAD (     )
  38. Mfumo wa jua hujumuisha sayari __(A)Tisa(B)Nane(C)Themanini (D)  Kumi (E) Nne (     )
  39. Lipi kati ya yafuatayo siyo bwawa? __(A)Aswam  (B)Mtera (C) Nyumba ya mungu (D)Kidatu       (     )
  40. Njia ambayo inatumika na sayari kulizunguka jua huitwa __(A)Latitude (B)Mhimili (C)Ikweta (D)Obiti  ( E) mfumo  (     )

SEHEMU :B JAZA NAFASI WAZI

  1. ____________________ni taulo ambayo hutumika na mwanamke kujisitiri wakati wa hedhi
  2. Mistari ya kufikirika ya ulalo ambayo huchorwa juu ya uso wa dunia kaskazini na kusini mwa Ikweta hujulikana kama________________
  3. Mtu aliyefanya mambo makubwa mazuri katika nchi yake anaitwa _____________________
  4. Sanaa inayotumika kutengeza maumbo mbalimbali kwa kutumia udongo  inaitwa _________
  5. Ikiwa ni saa 3:00 asubuhi katika mji A unaopatikana longitude 300 mashariki; Je itakuwa saa ngapi katika mji B unaopatikana longitude 600mashariki?

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 57

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA SABA

MAARIFA YA JAMII

MUDA:1:30                                                             

JINA_____________________________________SHULE_________________________

MAELEZO

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

 

Chagua jibu sahihi kuanzia swali la 1-40, kisha andika kwenye nafasi zilizo wazi

  1.    Kundi lipi linaonesha sayari?(a)  Zebaki, Mwezi na Zuhura (b)  Dunia, Nyota na Mihiri (c)  Zebaki, Serateni na Zohari (d)  Zuhura, Dunia na Kimondo (e) Utaridi, Jua na Mwezi
  2.    Vitufe vidogo kuliko sayari vilivyoundwa kwa miamba migumu ambavyo ulizunguka jua huitwa; (a) Kometi (b) Vimondo (c) Asteroid (d) Gimbi
  3.    Nyota iliyokaribu na dunia huitwa (a) Jua (b) Mwezi (c) Venus (d) Zebaki
  4.    Jumuiya ya Africa Mashariki inaundwa na nchi ngapi? (a) 3 (b) 5 (c) 6 (d) 7
  5.    Nyumba ya Mungu inatumika kuzalisha umeme, Je inapatikana mkoa gani? (a) kigoma (b) Morogoro (c) Kilimanjaro (d) Mbeya
  6.    Ukataji  wa miti hovyo husababisha; (a) mafuriko (b) jangwa (c) Ukame (d) mvua
  7.    Mito, maziwa, bahari, na chemchem ni vyanzo vya; (a) mvua (b) maji (c) uhai (d)biashara
  8.    Lugha ambayo inawaunganisha watanzania wote ni; (a) Kiingereza (b) kiitaliano (c) kibantu (d) kiswahili
  9.    Sudan ya Kusini ilipata Uhuru wake mnamo mwaka? (a) 2010 (b) 2011 (c) 2007 (d) 2016
  10. Kati ya viongozi hawa nani hakuwa mwanzilishi wa umoja wa Afrika? (a) Kwame Nkrumah (b) Ahmed sekou (c) Nelson Mandela (D) Julius Nyerere
  11. Zifuatazo ni njia za uzalishaji mali isipokuwa? (a) kuabudu (b) biashara (c) uvuvi (d) utalii
  12. Chanzo kikukuu cha mwanga duniani ni; (a) upepo (b) Jenereta (c) Jua (d) Maji
  13. Rais wa awamu ya tano wa muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  alifariki mwaka? (a) 2015 (b) 2020 (c) 2000 (d) 2021
  14. Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka? (a) 1967 (b) 1927 (c) 1947 (d) 1977
  15. Zao la kibiashara linaolimwa Unguja na Pemba ni? ( a) pareto (b) pamba (c) karafuu (d) mihogo
  16. Kipimo kidogo cha ramani hutumika kuchorea (a) maeneo madogo (b) maeneo makubwa (c) maeneo ya kati tu (d) maeneo madogo na ya kati (e) maeneo madogo na makubwa
  17. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya ramani? (a) Huonesha pande zote za kitu (b) Urefu wa kitu huoneshwa (c) Umbo la asili la kitu hubakia (d) Rangi ya asili ya kitu huonekana (e) Huonesha sura ya juu ya kitu.
  18. Baadhi ya Maitafa yenye haki ya kura ya Veto katika Umoja wa Mataifa ni: (a)  Ufaransa, Uturuki na Marekani (b)  Marekani, Uingereza na China (c)  Marekani, China na India (d)  Brazili.Ufaransa na Italia (e) Urusi, China na India
  19. Viongozi wafuatao walikuwa waanzilishi wa umoja wa Nchi za Mistari wa mbele katika ukombozi wa Kusini mwa Afrika isipokuwa (a) Hayati Julius Nyerere  (a) Hayati Augustino Neto (c) Hayati Samora M. Machel  (d) Mzee Kenneth Kaunda  (e) Hayati Laurent D.Kabila
  20. Njia iliyotumiwa na mataifa ya Afrika kujikwamua kiuchumi baada ya uhuru ni: (a) kuanzisha dini. (b) kuongeza bei za pembejeo.  (c) kudumisha utawala wa kikabila. (d) kuboresha kilimo.  (e) kusisitiza ukabila.
  21. Nchi zipi zilihudhuria mkutano wa Berlin mwaka 1884 - 1885 kama watazamaji? (a) Marekani na Uholanzi (b) Kanada na Marekani (c) Hispania na Marekani (d) Polanda na Marekani
  22.  Sababu mojawapo ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa ilikuwa: (a) Huruma ya wazungu juu ya mateso ya watumwa (b)  Waafrika kupigania uhuru wao (c) Kupata masoko ya bidhaa za ulaya(d)  Wazungu kujali juu ya usawa wa watu wote (e) Udhaifu wa watumwa kutoka Afrika.
  23. Rais wa kwanza wa nchi ya Msumbiji alikuwa (a) Edwardo do Santos            (b)  Samora Machel (c)  Edward Mondlane  (d) Joachim Chissano  (e) Grace Machel
  24. Aliyekuwa Rais wa Tanganyika kabla ya muungano alikuwa: (a) Abeid Karume (b) Benjamin Mkapa (c) Jakaya Kikwete  (d) Julius Nyerere  (e) Rashid Kawawa
  25. Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni: (a)  kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi (b)  Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa (c) baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu (d)  kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu (e)  kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama
  26. Wanachama waanzilishi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) walikuwa: (a) nchi huru za Afrika ya Kati (b) nchi huru za Afrika          (c) nchi huru za Afrika ya Kaskazini  (d) nchi huru za Afrika ya Magharibi  (e) nchi huru kusini mwa Afrika.
  27. Kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuanzisha uhusiano na nchi husaidia nini? (a) Kufahamu utajiri wa nchi inayohusika ili kufaidika (b) Kubaini usalama wa nchi inayohusika na tahadhari za kuchukua (c) Kusaidia wananchi wanaopata shida (d) Kutekeleza makubaliano
  28. Ipi siyo faida ya utamaduni katika Jamii? (a) Kudumisha umoja wa kitaifa (b) Kulinda rasilimali za taifa (c) Kuiga utamaduni mpya (d) Kulinda rasilimali za Taifa
  29. Yapi sio mafunzo yatolewayo wakati wa sherehe za Jando?(a) Kujitegemea (b) Elimu stadi za Maisha (c) Kupenda na kuthamini kazi (d) Ibada za kanisani
  30. Ipi siyo faida ya utamaduni katika Jamii? (a) Kudumisha umoja wa kitaifa (a) Kulinda rasilimali za taifa (c) Kuiga utamaduni mpya (d) Kulinda rasilimali za Taifa
  31. Ngoma gani ambayo haiowani na kabila linalocheza ngoma (a) Ngoma ya sindimba- Wamakonde (b) Ngoma ya Kasimbo- wahaya (c) Ngoma ya Mganda- Pare (d) Ngoma ya Mdundiko- wazaramo
  32. Yapi sio mafunzo yatolewayo wakati wa sherehe za Jando? (a) Kujitegemea (b) Elimu stadi za Maisha (c) Kupenda na kuthamini kazi (d) Ibada za kanisani
  33. Ipi sio utamaduni wa mtanzania? (a) Kucheza ngoma za asili (b) Vyakula vya asili (c) Sherehe za jando (d) Wanawake kuvaa suruari na sketi fupi
  34.  Mojawapo ya changamoto za kumbukumbu kwa njia ya maandishi ni (a) Huharibika haraka (b) Unahitaji masharti magumu (c) Uandishi huchukua muda mrefu (d) Ni rahisi kufanyia marekebisho
  35. Michoro ya mapangoni iliyoko Kondoa Irangi inasadikiwa kuchorwa wakati wa zama za (a) mwanzo za mawe (b) Kati za mawe (c) Mwisho za mawe (d) Chuma (e) Ugunduzi wa moto
  36. Uchafuzi wa hewa katika maeneo ya makazi unaweza kuthibitiwa kwa:  (a) matumizi ya vyoo  (b) kuchoma takataka (c)  kumwaga maji taka mitaani  (d) kuchemsha maji ya kunywa (e) kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki
  37. Wakati wa mvua kubwa inayoambatana na radi, watu hawaruhusiwi (a) kuvaa nguo nyekundu....... (b)  kutumia miavuli  (c) kufungua milango na madirisha (d) kujificha chini ya mti  (e)kufunga luninga na redio
  38. Ipi kati ya zifuatazo ni njia ya kuzuia mafuriko? (a) Kujenga nyumba imara. (b) Kupanda miti.(c) Kukata miti.(d) Kuchoma misitu.(e) Kujenga nyumba mabondeni.
  39. Ili kupunguza/kuondoa ongezeko la joto la dunia tunapaswa ......... (a) tuongeze utoaji wa hewa ya kabonidayoksaidi (b) tuongeze hewa ya kabonidayoksaidi inayotolewa na wanyama (c) tutumie vyanzo vya nishati vilivyo rafiki kwa mazingira (d) tuchome vichaka, misitu na nyasi(e)  tukate miti ili kupata eneo la kilimo
  40. Pepo huvuma kutoka pande zipi jua liwapo upande wa kusini mwa dunia?(a)  Kusini        (b) Magharibi  (c) Mashariki     (d) Kaskazini (e) Kaskazini-mashariki

Soma kwa makini Ramani ifuatayo; kisha jibu maswali yafuatayo;

  1. Taja jina la nchi iliyooneshwa kwa herufi R
  2. Bandari iliyoonesha kwa herufi T ipo nchi gani?
  3. Ni zao gani la biashara hulimwa katika eneo liliooneshwa kwa herufi S huitwaje?
  4. Kituo cha kuzalisha  umeme kilichooneshwa kwa herufi S huitwaje?
  5. Uchumi wa nchi iliyooneshwa kwa herufi Q hutegemea aina ipi ya madini?

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 51

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA DARASA LA SABA

MAARIFA YA JAMII

MUDA:1: 30                                                             

JINA_____________________________________SHULE_________________________

MAELEKEZO:

  1. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
  2. Kumbuka kuandika majina yako.
  3. Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.

SEHEMU A: CHAGUA JIBU SAHIHI KUTOKA YALE ULIOPEWA

  1. Ni tabia gani inachangia kuuwa biashara? A. Kukopa benki b. Usimamizi mzuri c. Kuajiri ndugu d. Kutumia pesa kwa utaratibu uliopangwa e. kuwa na bajeti
  2. Ipi sio tabia ya mjasiriamali? A. Kufanya kazi kwa bidi b. Ubunifu c. Kujiburudisha baada ya kazi d. Kutokata tamaa e.ujasiri
  3. Serikali inaweza kusaidia wajasiriamali wanao chipukia kwa; a. Kuwapa mtaji b. Kuboresha mazingira ya kufanya biashara c. Kuwafungulia biashara d. Kuwazawadia wanaofanya vizuri e. kuwatoza kodi kubwa
  4. Pareto hutumika kutengenezea: a. manukato b. dawa za kuulia wadudu c. vipodozi d. jeli e. mapambo
  5. Aina kuu mbili za biashara ni: a. biashara ya mkopo na ya malipo b. biashara ya mkopo na kubadilishana c. biashara ya mtaji na fedha d. Biashara ya hisa na ya mitaji e.biashara ya ndani na ya nje
  6. Mikoko ni aina ya uoto upatikanao pembezoni mwa: a. mito  b.  maziwa c. bahari d. mabwawa e. visima
  7.  Biashara ya ndani ni ile inayohusisha bidhaa ... a. zinazotengenezwa nje ya nchi. B. zinazotengenezwa na kuuzwa ndani ya nchi. C. zinazozalishwa ndani ya nchi. D. zinazotengenezwa na kuuzwa nje ya nchi. E. zinazouzwa nje ya nchi.
  8. Vitu viwili vinavyopatikana katika mazingira ya nyumbani ni: a. vitanda na madawati b. madarasa na maktaba c. vitanda na vyombo vya jikoni d. mlingoti wa bendera na vitanda e. viwanja vya michezo na madarasa
  9. Watu wanaoishi kandokando mwa bahari na maziwa hujihusisha na shughuli za: a. kilimo b. uvuvi c. uvunaji magogo d. ufugaji e. usafirishaji
  10.  Mbuga za wanyama zinazopatikana Tanzania ni: a. Serengeti, Ruaha na Mikumi b. Tarangire, Katavi na Ngorongoro c. Serengeti, Manyara na Ngorongoro d. Selous, Serengeti na Mikumi e. Mkomazi, Selous na Ngorongoro
  11. Uvuvi usio endeleevu waweza kusababisha yafuatayo kasoro: a. vifo vya watu b. vifo vya Samaki c. uchafuzi wa maji d. umaskini e. utajiri
  12. Mikoa inayolima zao la ndizi Tanzania ni: a. Kagera, Kilimanjaro na Mbeya b. Mbeya, Kagera na Lindi c. Kagera, Singida na Shinyanga d. Arusha, Morogoro na Shinyanga e. Singida, Lindi na Kagera
  13. Ranchi ni eno lililotengwa kwa: a. kilimo cha mazao a. machinjio ya ngombe c. ufugaji wa ngombe d. josho la ngombe e. kuotesha majani
  14. Jua la utosi katika mwezi Disemba huwa katika .  a. Kizio cha Kusini.   B. Tropiki ya Kansa.          C.  Ikweta.  D. Kizio cha Kaskazini.        E. Tropiki ya Kaprikoni.
  15.  Kundi lipi linaonesha sayari? A.  Zebaki, Mwezi na Zuhura b.  Dunia, Nyota na Mihiri c. Zebaki, Serateni na Zohari d. Zuhura, Dunia na Kimondo d.Utaridi, Jua na Mwezi
  16.  Majira ya mwaka hutokea kutokana na ... a. kupatwa kwa mwezi b. mwezi kuizunguka dunia c. dunia kulizunguka jua  d. kupatwa kwa jua e. kuongezeka kwa joto.
  17. Chanzo kikuu cha mnishati katika fumo wa jua ni:a. Dunia  b.  Sayari  c.  jua  d. Mwezi  e. Nyota
  18.  Ni sayari zipi kati ya zifuatazo zina miezi? A. Dunia, Kamsi, Mihiri na Zuhura. B. Dunia, Zohari, Zuhura na Kamsi. C. Dunia, Sumbula, Sarateni na Kamsi. D. Sarateni, Zebaki, Dunia na Kamsi. E. Dunia, Sumbula, Sarateni na Zebaki.
  19. Sehemu ya muhimu ya ramani inayoelezea kuhusu alama zilizotumiwa katika ramani ni a. ufunguo b. fremu c. dira d. kipimio e. kichwa cha ramani
  20.  Katika kuonesha mahali kwa kutumia mistari ya gridi katika ramani huanza kusomwa namba za mstari gani? . a. Ulalo halafu wima. B. Wima halafu ulalo. C. Kushoto halafu kulia. D. Kulia halafu juu. E Kulia halafu kushoto.
  21.  Iwapo umbali wa kilometa 25 kwenye ardhi unawakilishwa na urefu wa sentimeta 5 kwenye ramani. Kipimo cha ramani ni ... a. 1:20000 b. 1:100000 c. 1:50000 d. 1:500000 e. 1:10000
  22.  Picha iliyopigwa katika uoto wa savanna huonesha ... a. misitu minene. B. nyasi ndefu. C. miti iliyochongoka juu. D. miti yenye umbile la mwavuli. E. nyasi fupi.
  23. Njia iliyotumiwa na mataifa ya Afrika kujikwamua kiuchumi baada ya uhuru ni: a. kuanzisha dini. B. kuongeza bei za pembejeo.  C. kudumisha utawala wa kikabila. D. kuboresha kilimo.  E. kusisitiza ukabila.
  24. Kitendo cha nchi changa kulazimika kuzingatia matakwa na maslahi ya nchi za kibeberu huitwaje? A. ukoloni mkongwe  b. ukoloni mamboleo c. ubepari d. umangimeza  e.utandawazi
  25. Viongozi wafuatao walikuwa waanzilishi wa umoja wa Nchi za Mistari wa mbele katika ukombozi wa Kusini mwa Afrika isipokuwa a. Hayati Julius Nyerere  b. Hayati Augustino Neto c. Hayati Samora M. Machel  d. Mzee Kenneth Kaunda  e. Hayati Laurent D.Kabila
  26. Lipi kati ya yafuatayo ni miongoni mwa madhara ya ukoloni? A. kuzorota kwa viwanda vya serikali b. kukua kwa utamaduni wa Kiafrika c. kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi d. kuwepo kwa demokrasi e. elimu ilitolewa bure
  27.  Wakati wa mvua kubwa inayoambatana na radi, watu hawaruhusiwi a. kuvaa nguo nyekundu....... b. kutumia miavuli c. kufungua milango na madirisha d. kujificha chini ya mti e. kufunga luninga na redio
  28. Janga la kimazingira linalosababishwa na nguvu za asili pekee linaitwa a. Ukame b. Tetemeko la ardhi c. Mmomonyoko wa udongo d. Njaa e. Uchafuzi wa mazingira
  29. Lipi kati ya majanga yafuatayo husababishwa na binadamu a. Vita b. Ukame c. Milipuko ya volcano d. Tetemeko la ardhi e. Kimbunga
  30.  Moja ya majanga yanayoletwa na nguvu za asili na kazi za binadamu ni: a. miipuko wa volcano b. tsunami. C. kitropiki. D. radi. E. mmomonyoko wa udongo.
  31. Chanzo kikuu cha wakimbizi Afrika Mashariki na Kati ni:a. uchochezi wa mataifa ya kijamaa yaliyosambaratika b. migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe c. tamaa ya makundi yenye uwezo wa kupigana d. uvivu, njaa, ukame na kukosa demokrasia e. kuzaliana kwa wingi kwa kundi moja dhidi ya mengine
  32. Moja ya mbinu iliyotumika kudhoofisha teknolojia ya Waafrika wakati wa ukolono ni  a. kufundisha masomo ya sayansi. b.  kuanzisha viwanda vya kisasa katika Afrika. C. kubinafsisha viwanda vya Afrika. D.  kuleta bidhaa za viwandani kutoka ulaya. E. kufundisha Waafrika teknolojia ya Ulaya.
  33. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885 uliitishwa na ..a. Carl Peters  b.Johann Krapf  c. Henry Stanley  d. David Livingstone e. Otto Von Bismarck.
  34. Mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma katika Afrika alikuwa ... a. Horace Byatt b. Friedrick Lugard c. Richard Turnbull d. Donald Cameroon e. Edward Twinning
  35. Ni Taifa lipi la kibepari liliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1891 hadi 1918? A.  Ujerumani  b.  Uingereza c.  China  d.  Ureno  e. Ufaransa
  36. Tanzania ipo kusini mwa a. lkweta  b. Tropiki ya kaprikoni c. Greenwich  d. Ncha ya kaskazini e. Muhimili wa dunia
  37. Yafuatayo ni mambo yalisababishwa na uharibifu wa uoto isipokuwa: a. Kimbunga na tufani b. upungufu wa maji na nusu jangwa c. mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa viumbe hai d. njaa na mifugo mingi kufa e. Uchimbaji madini na utengenezaji barabara
  38. Bainisha njia sahihi ya kuzuia athari za mazingira zinazotokana na kilimo: a. Kulima kilimo cha zao moja. B. Kulima kwenye vyanzo vya maji. C. Kilimo cha kuhamahama. D. Kukata miti kandokando ya shamba. E. Kutumia mbolea ya asili.
  39. Viashiria vya utandawazi ni pamoja na............... a. kupungua kwa tofauti ya kipato b. uchumi wa soko huria c. kupungua kwa umaskini d. kuwepo kwa ushindani wa kutengeneza silaha e. kuwepo kwa bidhaa nyingi toka viwanda vya ndani
  40. Biashara ya kimataifa inahusisha............... a. uingizaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi  b. uingizaji bidhaa kutoka nje ya nchi tu c. usafirishaji bidhaa kwenda nje ya nchi tu d. kufanya biashara kwa kutumia pesa e. kukopa fedha kutoka nje ya nchi

SEHEMU B: JIBU MASWALI KWA UFASAHA

Jaza nafasi zilizoachwa wazi

  1. Wapiganaji wa chama cha FRELIMO walipata mafunzo ya kijeshi katikanchi ya ……………………….. na kufanikiwa kuleta uhuru wa kweli Msumbiji
  2. Mwalimu Julius Nyerere alifanikiwa kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika akiwa kiongozi wa chama cha……………………………
  3. Katika    harakati za kudai uhuru, baadhi ya nchi za Afrika zilizopata uhuru wake kwa njia ya mapinduzi ni ………………………… na ………………………………………….
  4. Ni mkoa upi nchini Tanzania ni maarufu kwa ukulima wa pamba?...........................................
  5. Binadamu aliweza kutembea kwa miguu miwili aliitwa?..........................................................

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 41

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINIDARASA LA VII JULAI 2021

MAARIFA YA JAMII

Muda: saa 1 : 30

MAELEKEZO:

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

SEHEMU : A 

CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI 

1. Ardhi ni rasilimali ambayo isipotunzwa vizuri inaweza kusababisha hatari katika maisha ya viumbe hai na rasilimali nyingine. Ipi ni njia bora itakayotumika kutunza rasilimali hiyo kati ya zifuatazo? ______

  1. Kuongeza idadi ya wakulima mashambani
  2. Kutoa elimu juu ya matumizi sahihi yaardhi
  3. Kuhimiza wafugaji kuongeza idadi ya mifugo
  4. Kuwahimiza wananchi kutumia mbolea za viwandani
  5. Kuhimiza upandaji miti katika maeneo ya wazi     [     ]

2. Katika sikukuu ya wakulima kauli mbiu iliyotolewa na Waziri Mkuu ilikuwa ni, “Kilimo ni uti wa mgongo katika uchumi wa Tanzania”. Kauli mbiu hiyo inamaana gani? ______________________________

  1. Ni shughuli inayofanywa na watu matajiri
  2. Hufanyika kwa kutumia matrekta na majembe ya kukokotwa na ng’ombe
  3. Ndio shughuli kuu ya uzalishaji mali
  4. Hufanyika sehemu zenye vyanzo vya maji pekee
  5. Mazao yanayovunwa huuzwa nje ya nchi     [     ]

3. Mwalimu Kazimoto alifundisha kuhusu shughuli ya kilimo cha mazao ya biashara kilichofanywa Tanganyika kabla ya uhuru. Je, wanafunziwalibaini mazao yapi ya biashara? _____________________

  1. Korosho, maharage,mkonge na pareto
  2. Mahindi, kahawa, chai na pareto
  3. Kahawa,pareto,mkonge na chai
  4. Zabibu, kahawa,chai na maharage
  5. Pareto, korosho,chai na mahindi     [     ]

4. Wakulima wengi nchini Tanzania hupeleka mazao sokoni kuuza. Ninjia zipi kuu za usafirishaji zinazotumika? ___________________________

  1. Barabara na Reli
  2. Anga na Barabara
  3. Maji na Anga
  4. Reli na Anga
  5. Maji na Barabara     [     ]

5. Shughuli za kilimo huweza kuharibu ardhiikiwa hazikufanyika kwa uangalifu. Ni kwa namna gani kilimo kinaweza kuharibu ardhi? ______

  1. Kwa kutumia mbolea ya asili
  2. Kwa kulima kwa kubadilisha mazao
  3. Kwa kulima matuta ya kukinga mteremko
  4. Kwa kutumia mbolea za viwandani
  5. Kwa kupanda miti karibu na shamba     [     ]

6. Ukurasa wa 3kati ya 96.Shamba la Bwana Tembo ambalo lipo pembeni ya mlima Pina limepungukiwa na rutuba kutokana na momonyoko wa udongo. Kama mtaalam wa mazingira ninini chanzocha momonyoko huo? _________________________________

  1. Shamba kuwa katika mteremko mkali
  2. Shamba kuwa na miti mingi
  3. Samadi kuwekwa shambani
  4. Shamba kupandwa mazao mengi ya mizizi na nafaka
  5. Mazao kubadilishwa shambani kila mwaka     [     ]

7. Shughuli za kibinadamu kandoya mto Matumaini huleta madhara kwa jamii inayouzunguka. Ni madhara gani yanasababishwa na shughuli za ukataji miti ovyo pembeni mwa mto huo? _________ 

  1. Ukosefu wa maji viwandani 
  2. Uchafuzi wa hewa 
  3. Ardhi kupoteza rutuba 
  4. Kukauka kwa vyanzo vya maji 
  5. Kupungua kwa uvuvi     [     ]

8. Wazo ni mkulima ambaye anataka kuanzisha kilimo katika eneo ambalo ni nusu jangwa. Kama Afisa kilimo niushauri gani utampa?________ 

  1. Kulima mazao yanayovumilia ukame 
  2. Kuachana na shughuli za kilimo 
  3. Kulima msimu wa mvua tu 
  4. Kutumia mbolea ya viwandani tuwakati wa kilimo
  5. Kutumia samadi peke yakewakati wa kilimo     [     ]

9. Ukiwa ni kiongozi wa klabu ya kutunza mazingira, utampa ushauri gani mtu anaye kata miti ovyo kwa ajili ya kupata nishati? ___________________

  1. Kutumianishati mbadala rafiki kwa mazingira 
  2. Kujificha asikamatwe na Maafisa Misitu 
  3. Kuhifadhivyema mabaki ya miti iliyokatwa 
  4. Kuuzakuni na mkaa kujiongezea kipato 
  5. Kukatamiti ya ndani ya misitu ili asijulikane     [     ]

10. Ni tukio lipi la kihistoria lilitokea Tanganyika mwaka 1926? _______

  1. Kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia
  2. Kuanzishwa kwa chama cha African Association
  3. Kuanzishwa kwa Baraza la Bunge 
  4. Uhuru wa Tanganyika 
  5. Kuanzishwa kwa vyama vingi     [     ]

11. Ukurasa wa 4kati ya 911.Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mwenge wanapanga safari ya kimasomokwenda kuona mabaki yamifumo ya kilimo cha umwagiliaji iliyotumiwa na watu wa kale. Ni eneolipi la kihistoria utawashauri kutembelea? _________ 

  1. Engaruka 
  2. Amboni
  3. Isimila 
  4. Olduvai Gorge 
  5. Kondoa Irangi     [     ]

12. Maeneo yafuatayo ya kihistoria yanapatikana Tanzania isipokuwa _________________________________ 

  1. Rusinga 
  2. Olduvai Gorge 
  3. Engaruka 
  4. Kondoa Irangi 
  5. Kaole     [     ]

13. Historia ya ukombozi wa Tanzania ilianza na vyama vya ustawi wa wafanyakazi kama vile TTACSA mwaka 1922 kilichobadilishwa kuwa TAA mwaka 1929 na baadae kuwa TANU mwaka 1954. Je, ni kwa nini TAA ilibadilishwa kuwa chama cha TANU mwaka 1954? ____________

  1. Kuwaunganisha watu wote katika kudai uhuru 
  2. Kuwa chama cha kisiasa kwa ajili ya wafanyakazi tu 
  3. Kuwaunganisha watu wote kupigana vita vya ukombozi 
  4. Kuunganisha vyama vyote vya siasa katika harakati za ukombozi 
  5. Kuwa chama cha kutetea ustawi wa wakulima     [     ]

14. Wanafunzi wa Darasa la Sita walirekodi viwango vya jotoridi kuanzia Jumatatu hadi Jumapili kama ifuatavyo: 200C, 320C, 300C, 240C, 270C, 270C na 220C mtawalia. Je,upi ni wastani wa jotoridi kwa wiki? ___________ 

  1. 200C 
  2. 320C 
  3. 270 C
  4. 26.20 C 
  5. 260     [     ]

15. Umepewa jukumu la kutoa mafunzo kwa wanakijiji wa Kijiji cha Juhudi juu ya fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zinaweza kufanyika katika vipindi mbalimbali vya mwaka. Je, ungewashauri kufanya biashara ya kuuza miavuli katikakipindi gani? __________________ 

  1. Wakati wa Kiangazi 
  2. Wakatiwa Kipupwe 
  3. Wakati wa Vuli 
  4. Wakati wa Masika 
  5. Wakati wa Baridi     [     ]

16. Wanafunzi wa Darasa la Nne walifundishwa kuhusu vipengele mbalimbalivya hali ya hewa. Ni kundi lipilinawakilisha vipengele vya hali ya hewa walivyojifunza? ___________________________________ 

  1. Jotoridi, udongo, mvua na unyevuanga 
  2. Anga, mwangajua, mgandamizohewa na upepo 
  3. Maji, udongo, jotoridi na mawingu 
  4. Mgandamizohewa, jotoridi, mvua na mwangajua 
  5. Mvua, jotoridi mgandamizohewa na anga     [     ]

17. Baraka anatafuta msaada wako kumwezesha kujibu swali kuhusu dhana ya “utamaduni”. Je, ni vielelezo vipi vya utamaduni utakavyo-mpa Baraka ili aweze kuielewa vizuri dhana hiyo? ________ 

  1. Lugha, mila na tohara 
  2. Mila, desturi na lugha 
  3. Mila, desturi na miiko 
  4. Tohara, mila na desturi 
  5. Lugha, mila na makumbusho     [     ]

18. Ngoma za asili, uchongaji, uchoraji na maigizo ya jadi ni miongoni mwa mambo ya kitamaduni yanayovutia watalii. Ni neno gani lifaalo kwa vipengele hivi vya utamaduni? ___________________________ 

  1. Mila
  2. Sanaa 
  3. Michezo 
  4. Lugha 
  5. Miiko     [     ]

19. Kiongozi kutoka Wizara inayosimamia Utamaduni aliwataka vijana kuacha kushabikia tamaduni za kigeni na kudharau tamaduni za Kiafrika. Je, nini lengo la ushauri huo? __________________________ 

  1. Kulinda maslahi ya wageni
  2. Kulinda maslahi ya viongozi 
  3. Kupata fursa ya kutembelea nchi za nje
  4. Kulinda rasilimali za Taifa
  5. Kufurahiarasilimali za Taifa     [     ]

20. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Harambee husisitiza wanafunzi wake kushiriki katika michezo ya jadi. Lipi katiya yafuatayo ni lengo lake kuu? __________________________ 

  1. kukuza kufikiri na kucheza 
  2. kuwezesha maamuzi na kuwa mbinafsi 
  3. kukuza kufikiri na kufanya maamuzi 
  4. kuongeza uzuri wa nyimbo na kufikiri 
  5. kutanua utawala wa sheria nakufanyamaamuzi     [     ]

21. Fikiria umeteuliwa kuongea na mojawapo ya makundi rika katika jamii yako kuhusu mahusioano mema miongoni mwao. Lipi kati ya yafuatayo ungelisisitiza? ________ 

  1. Kuheshimiana na kusaidiana
  2. Kusaidiana na kugombana 
  3. Kusalimiana na kudharauliana 
  4. Kuheshimiana na kubaguana 
  5. Kuelewana na kuogopana     [     ]

22. Kama kuna wazazi na watoto, hii ni familia ya awali. Je, familia hii itaitwaje baada ya vifo vya wazazi wao? _________________________ 

  1. Familia pana 
  2. Familia ya watoto 
  3. Familia ya watoto yatima
  4. Familia tegemezi 
  5. Familia ya watoto wa mitaani     [     ]

23. Ukoloni katika nchi nyingi za Kiafrika ulikuwa na hasara zaidi kuliko faida. Kama mwanahistoria, ipi unadhani ni athari ya kijamii iliyotokana naukoloni katika Tanganyika? ________________________ 

  1. Kusaini mikataba na watawala wenyeji na kuleta mazao mapya
  2. Kuanzishwa kwaelimu rasmi na kueneza Ukristo 
  3. Kusaini mikataba na watawala wenyeji na kujenga barabara
  4. Kuanzishwa kwa mazao mapya na kuteua machifu kama watawala
  5. Kuleta elimu rasmi na kusaini mikataba na watawala wenyeji     [     ]

24. Nchi nyingi za Afrika kuwa wanachama wa jumuiya mbalimbali inadhihirisha umuhimu wa jumuiya hizokwa nchi husika. Unadhani nini kitatokea endapo nchi itavunja uhusiano huo? ________ 

  1. Kutakuwa na maendeleo makubwa katika nchi 
  2. Kushuka kwa uchumi na kudorora kwa amani 
  3. Kutumia bidhaa za nchi nyingine na kukua kwa maendeleo 
  4. Kuongeza wajuzi katika nchi na dunia 
  5. Kupata fursa ya kuungana na mataifa tajiri     [     ]

25. Mnamo robo ya mwisho ya karne ya 19, Mataifa ya Ulaya yaligombea maeneo ya Afrika kwasababu walitaka malighafi, masoko, wafanyakazi na sehemu ya kuweka vitega uchumi. Maeneo yafuatayo yaligombaniwa isipokuwa ___________________

  1. Maeneo ya kando kando ya Bahari au Ukanda wa Pwani 
  2. Maeneo yenye hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutuba 
  3. Maeneo yenye maziwa na mito mikuu
  4. Maeneo yenye utajiri wa madini na rasilimali nyingine 
  5. Maeneo yenye viwanda vingi vya kuzalisha bidhaa     [     ]

26. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anatambulika kuwa ni shujaa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Ni nini kinachomfanya atambulike hivyo? _______________ 

  1. lihudhuria vikao vya UNO huko Ulaya 
  2. Alipinga vikali aina zote za ubaguzi wa rangi na kidini 
  3. Alipinga vikali urejeshwaji wa mfumowa vyama vingi 
  4. Aliwahamasisha Watanganyika kutumia mapambano ya silaha
  5. Alihamasisha mapinduzi katika kupigania uhuru     [     ]

27. Kuanzia mwaka 1985 hadi 2015 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliongozwa na marais watatu. Ipi ni orodha sahihi ya Marais hao? _________

  1. Julius K. Nyerere, Ali H. Mwinyi and Bejamin W. Mkapa 
  2. Julius K. Nyerere, Ali H. Mwinyi na Jakaya M. Kikwete 
  3. Ali H. Mwinyi, Benjamin W. Mkapa na Jakaya M. Kikwete 
  4. Julius K. Nyerere, Abeid A. Karume na John P. Magufuli 
  5. Benjamin W. Mkapa, Jakaya M. Kikwete na John P. Magufuli     [     ]

28. Mwalimu aliwaambia wanafunziwakekuwa mistari ya latitudo huwa na mizingo tofauti tofauti kutegemea na mahali ulipo. Ni mstari upi wenye mzingo mrefu kati ya hii ifuatayo?_______________________________

  1. Tropiki ya Kaprikoni 
  2. Mzingo wa Aktiki
  3. Mstari wa Ikweta 
  4. Tropiki ya Kansa 
  5. Mzingo wa Antaktiki     [     ]

29. Wakati wa kipindi cha somo la Maarifa ya Jamii mwalimu aliwapa wanafunzi ramani ya Tanzania yenye vitu vya asili na vilivyotengenezwa na binadamu kwa lengo la kujifunza. Je, hiyo ilikuwa ni ramani ya ainagani? _________________________________ 

  1. Ramani za takwimu 
  2. Ramani za kisiasa 
  3. Ramani za kontua
  4. Ramani za topografia 
  5. Ramani za miji     [     ]

30. Mtalii aliwasili nchini Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kuelekea moja kwa moja katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro bila ya kupokelewa na mwenyeji yeyote. Ni kifaa kipikati ya vifuatavyo kilimwezesha kufika huko? _______________ 

  1. Skeli
  2. Hali ya hewa
  3. Ramani 
  4. Mwelekeo wa jua
  5. Picha 3     [     ]

31. Bahati alichora ramani ya kijiji chao bila kuonesha kipimio cha ramani. Ni adhari ipi atakayoipata mtumiaji wa ramani hiyo? _______________________ 

  1. Kushindwa kufahamu mipaka ya kijiji
  2. Kutofahamu ukubwa halisi wa kijiji
  3. Kutozitambua alama zilizotumika
  4. Maudhui ya ramani kutoeleweka 
  5. Mazao ya chakula yaliyo kijijini kutoonekana vizuri     [     ]

32. Fikiria kuwa umealikwa kamamtaalamu wa mambo ya hali ya hewakuelezea umuhimu wa tabaka la ozoni kwajamii. Je,ungeelezanini? __ 

  1. Huzuia kansa ya ngozi 
  2. Huzuia mmomonyoko wa udongo 
  3. Huongeza idadi ya watu
  4. Husababisha kutengenezeka kwa mvua 
  5. Huongeza uoto wa asili     [     ]

33. Rafiki yangu alisafiri kwenda Ulaya kumtembelea shangazi yake kipindi cha likizo. Kulikuwa na baridi kali iliyoambatana na mchana kuwa mfupi kuliko usiku. Je, hali hiyo inawakilisha msimu upi wa mwaka? __________ 

  1. Kiangazi 
  2. Masika 
  3. Kipupwe 
  4. Vuli 
  5. Mvua     [     ]

34. Wanafunzi wa Darasa la Tatu walijifunza kuwa,kuna sayari nane zinazounda mfumo wa jua ambazo baadhi zipo mbali na nyingine zipo karibu na jua. Je, ni Sayari ipi miongoni mwa zifuatazo ipo karibu zaidi na jua? ___________ 

  1. Sumbula
  2. Kausi 
  3. Zuhura
  4. Zebaki
  5. Dunia     [     ]

35. Tanzania ni nchi iliyojaaliwa kuwa na madini ya aina mbalimbali. Ni kundi lipi kati ya yafuatayo hujumuisha madini ya vito? _________ 

  1. Dhahabu, chumvi na chuma 
  2. Almasi, rubi na tanzanaiti 
  3. Almasi, dhahabu na chuma 
  4. Cobalt, rubi na tanzanaiti 
  5. Chumvi, dhahabu na almasi     [     ]

36. Wanafunzi wa Darasa la Saba walipewa aina mpya ya vifungo kwa ajili ya mashati yao. Ni kanuni ipi wanapaswa kuzingatia wakati wakushona vifungo hivyo? ____________________________________ 

  1. Kuchagua uzi wenye rangi tofauti na vifungo walivyopewa 
  2. Kuchagua sindano inayoendana na kitambaa cha shati 
  3. Kuanza kushona mshono wa kushikiza 
  4. Kutumia sindano kubwa kuliko tundu la kifungo 
  5. Kupitisha uzi upande wa juu ya kitambaa cha shati     [     ]

37. Umemtembelea shangazi yako na kupewa chumba kichafu cha kulala. Ni magonjwa gani unaweza kuyapata kwa kulala kwenye chumba hicho? ___________ 

  1. Kuharisha na kutapika 
  2. Kukohoa na kutapika 
  3. Mafua na kifua 
  4. Malaria na kifua 
  5. Kuharisha na mafua     [     ]

38. Bwana Nzima amepanga kusafiri na amedhamiria kufungasha nyama kwa ajili ya safari yake. Ungemshauri kutumia mojawapo ya njia zipi kuandaa nyama hiyo ili kuzuia kuharibika? ___________________ 

  1. Kukaanga, kuchemsha na kuchoma 
  2. Kuchemsha, kubanika na kukaanga 
  3. Kutokosa, kukaanga na kuchoma 
  4. Kuchoma, kukaanga na kubanika 
  5. Kuchoma, kubanika na kupika kwa mvuke     [     ]

39. Mwalimu wa Stadi za Kazi aliwaongoza wanafunzi kufinyanga chungu na kuwapa mbinu za kukikausha vizuri. Je, kuna umuhimu gani wa kukikausha chungu hicho? ____________________________________ 

  1. Kukifanya kiwe imara 
  2. Kukifanya kiwe na rangi nyeusi 
  3. Ili kuweza kukiweka nakshi 
  4. Kukifanya kuwana harufu ya kuungua 
  5. Kukifanya kiwe chepesi     [     ]

40. Mimi ni mbunifu, mwenye uthubutu na ninajituma katika kutimiza malengo yangu. Je, mimi ni nani? ______________________________ 

  1. Mjasiriamali 
  2. Mtu mwenye ujuzi 
  3. Mfanyabiashara 
  4. Mnunuzi 
  5. Muuzaji     [     ]


SEHEMU B

JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA KUELEZA KWA KIFUPI

41. Eleza kwa kifupi tofauti kati ya mjasiriamali mtumishi na mjasiriamali mfanyabiashara? __ ____________________________________

42. Mlipuko wa volkano katika kijiji cha Kikuu umeleta madhara kwa jamii. Bainisha madhara chanya mawili ya mlipuko huo ___________

43. Bi Atupele aliwataka wanafunzi waorodheshe tabia ya nchi ya maeneo waliyotoka. Mmoja wa wanafunzi alitaja kuwepo kwa mvua nyingi, kiwango cha juu cha jotoridi na uwiano mdogo wa joto kwa mwaka mzima. Je, eneo hilo lina tabia gani ya nchi? __________

44. Tabu alitembelea kituo cha hali ya hewa kilichopo uwanja wa ndege wa Mwanza kuchukua takwimu za hali ya hewa ya eneo hilo, na kuwasilisha takwimu hizo katika Jedwali kama ifuatavyo:

Mwezi
Jan. Feb. Mach Apr Mei Juni Juli Agu. Sep Okt Nov Dis.
Joto(0 C) 22.5 25 25 25.5 25.5 25.5 25.5 25.5 26.1 26.1 26.1 26.6
Mvua (mm) 198 340 431 350 280 230 160 71 15 12 15 66
  1. Ni mwezi upi ulikuwa na mvua na jotoridi kubwa? __________________________
  2. Ni aina ipi ya tabia ya nchi inawakilishwa na taarifa zilizopo kwenye jedwali? _________________________________________

45. Ni kwa nini Chifu Mkwawa alijulikana kama shujaa katika jamii yake ___________________________________________________________________________________________________________________________ 


LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 37

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YAK RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA TATHMINIDARASA LA VII MAY 2020

MAARIFA YA JAMII

Muda: saa 1

MAELEKEZO:

1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa

2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu

3. Zingatia unadhifu wa kazi yako

4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi

5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi

SEHEMU A: MASWALI YA KUCHAGUA 

Chagua jibu sahihi kisha siliba herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia uliyopewa

1. Shughuli zifuatazo zinasababisha uchafuzi wa mazingira, ISIPOKUWA:

  1.            Ukataji miti ovyo C. Kuchoma misitu na vichaka E. Kutupa taka ovyo [ ]
  2.            Kupanda miti D. Shughuli za viwanda

2. Njia mojawapo ya kuzuia mafuriko ni:

  1.            Kujenga nyumba kwenye mabonde C. Kilimo cha mzunguko E. Kujenga nyumba zinazohamishika
  2.            Kukata miti D. Kupanda miti [ ]

3. Mtetemo wa ghafla unaotokea juu ya uso wa dunia hujulikana kama:

  1.                 Tetemeko la ardhi C. Maporomoko ya ardhi E. Tufani [ ]
  2.                 Mlipuko wa volkano D. Tsunami

4. Joto la Dar es salaam, Tanga, Lindi na Mtwara ni kubwa kuliko la Njombe, Arusha na Mbeya kutokana na tofauti ya: 
A. Latitudo B. Mwinuko C. Mtazamo D. Mvua E. Longitudo [ ]

5. Zifuatazo ni faida za kufahamu hali ya hewa ya eneo fulani, ISIPOKUWA:

  1.            Kuchagua aina ya mavazi ya kuvaa
  2.            Kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya hali ya hewa
  3.            Kupanga shughuli za kilimo
  4.            Huwasaidia marubani kuchukua tahadhari kabla ya kurusha ndege au kutua [ ]
  5.            Kujua matukio ya kihistoria yaliyotokea hapo zamani

6. Karne moja ni sawa na miaka mingapi?

A. 10 B. 20 C. 100 D. 50 E. 1000 [ ]

7. Miongoni mwa majanga yanayosababishwa na kuongezeka kwa joto duniani ni:

  1.            Tetemeko la ardhi na vita C.Ajali na mlipuko wa volkano E. Ukame na mafuriko
  2.            Radi na mafuriko D. Maporomoko ya ardhi na mmomonyoko wa udongo [ ]

8. Hali ya upungufu au ukosefu wa mvua kwa kipindi cha muda mrefu hujulikana kama:

A. Ukame B. Mafuriko C. Njaa D. Kipupwe E. Majanga [ ]

9. Njia ipi ya kuhifadhi kumbukumbu za matukio ya kihistoria hutumiwa zaidi na watu wasiojua kusoma na kuandika? A. Vitabu              B. Maandishi C. Mazungumzo ya mdomo D. Maktaba E. Nyaraka              [              ]

10. Fuvu la kichwa cha mtu wa kale zaidi liligunduliwa katika bonde la Olduvai na:

  1.            Dk. Louis Leakey C. Dk. Livingstone E. Karl Peters [ ]
  2.            Dk. Charles Darwin D. Vasco Da Gama

11. Eneo la kihistoria ambalo ni maarufu kutokana na michoro ya mapangani nchini Tanzania ni:

A. Isimila B. Kilwa C. Engaruka D. Olduvai Gorge E. Kondoa Irangi [ ]

12. Binadamu wa kale alianza kilimo na ufugaji katika kipindi cha:

  1.            Zama za Mawe za Kale C. Zama za Chuma E. Zama za Kidijitali
  2.            Zama za Mawe za Kati D. Zama za Mawe za Mwisho [ ]

13. Mkwawa anakumbukwa kama miongoni mwa mashujaa wa nchi yetu kwa sababu:

  1.              Aligundua fuvu la kichwa cha mtu wa kale zaidi katika bonde la Olduvai
  2. Alisaini mikataba ya ulaghai na Waingereza [ ]
  3.              Aliongoza vita vya Majimaji dhidi ya Wajerumani
  4.              Alipambana na Wajerumani kwa ujasiri mkubwa
  5.              Aliasisi nadharia ya chimbuko la mwanadamu

14. Nchi ngapi zilikuwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia mwaka 1967 hadi1977?

A. Mbili B. Tano C. Tatu D. Sita E. Saba [ ]

15. Utawala wa Wajerumani nchini Tanganyika ulifika kikomo mwaka gani?

  1. Baada ya mkutano wa Berlin C. Baada ya vita vya Kwanza vya dunia E. Baada ya vita vya Maji Maji
  2. Baada ya kuundwa kwa TANU D. Baada ya vita vya pili vya dunia

16. Mgawanyo wa Afrika Mashariki kati ya Wajerumani na Waingereza ulikamilika mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Helgoland mwaka:

A. 1840 B. 1842 C. 1896 D. 1886 E. 1890 [ ]

17. Kundi gani la vitangulizi vya ukoloni lilifika Afrika kwa lengo kuu la kueneza dini ya Ukristo?

A. Wafanyabiashara B. Wapelelezi C. Wamisionari D. Walowezi E. Waarabu [ ]

18. Gavana wa kwanza wa Waingereza nchini Tanganyika alikuwa nani?

  1.                   Julius Von Soden C E.dward Twinning E. Donald Cameron [ ]
  2.                   Horrace Byatt D. Richard Turnbull

19. Chama cha ANC wakati wa harakati za kudai uhuru nchini Tanganyika kiliongozwa na nani?

  1.                   John Rupia C. Martin Kayamba E. Zuberi Mtemvu [ ]
  2.                   Oscar Kambona D. Mohammed Shamte

20. Maigizo,nyimbo na filamu ni mifano ya aina gani ya sanaa?

  1.                   Sanaa ghibu C. Sanaa za ufundi E. Sanaa zisizoonekana
  2.                   Sanaa za maonyesho D. Sanaa za fasihi [ ]

21. Ngoma za asili zina faida gani kwa jamii?

  1.     Huchochea uvivu D. Husababisha maambukizi ya magonjwa
  2.     Huleta utengano E. Huimarisha utamaduni wa jamii husika [ ]
  3.    Husababisha ndoa za utotoni

22. Mtemi Isike na Mirambo walikuwa ni viongozi wa kabila gani?

A. Gogo B. Yao C. Nyamwezi D. Hehe E. Ngoni [ ]

23. Nchi nyingi za Afrika zilianza kupata uhuru wao katika miaka ya:

A. 1950 B. 1960 C. 1900 D. 1970 E. 2000 [ ]

24. Bomba la mafuta linaloanzia Dar es salaam hadi Ndola nchini Zambia linaitwa:

A. TANAPA B. TAZARA C. TAZAMA D. SONGAS E .TIPER [ ]

25. Kuna tofauti gani ya muda kati ya mji wa Kigali uliopo nyuzi 300 Mashariki na mji wa Mogadishu uliopo nyuzi 600 Mashariki?

A. Dakika 30 B. Dakika 15 C. Masaa 3 D.Saa 1 E. Masaa 2 [ ]

26. Alama ipi ya ramani kati ya hizi zifuatazo huwakilisha kilele cha mlima?

  1.        Ni aina ipi ya kipimio cha ramani inaweza kutumika kuchora ramani ya darasa?

A. Kipimio cha uwiano B. Kipimio cha kati C. Kipimio cha mstari D. Kipimio kidogo E. Kipimio kikubwa                                                                                                                                                                  [              ]

  1.        Ni gimba lipi kati ya magimba yafuatayo huwa katikati ya magimba mengine wakati wa kupatwa kwa mwezi?
  1.            Jua
  2.            Mwezi
  3.            Dunia
  4.            zebaki
  5.             Kausi.

    29. Mstari wa latitude wenye nyuzi 231/2 kaskazini mwa ikweta hujulikan a kama;

  1.            Tropiki ya kansa
  2.            Meridani kuu
  3.            Mzingo wa antaktiki
  4.            Tropiki ya kaprikoni
  5.             Mzingo wa aktiki

30. Urefu wa mchana na usiku huwa sawa wakati jua linapokuwa la utosi katika;

  1.            Ikweta
  2.            Tropiki ya kaprikoni
  3.            Ncha ya kusini
  4.            Meridian kuu
  5.             Mzingo wa aktiki

         31. Urefu wa mchana na usiku huwa wakati jua linapokuwa la utosi katika;

  1.            Ikweta
  2.            Tropiki ya kaprikoni
  3.            Ncha ya kusini
  4.            Meridian kuu
  5.             Tropiki ya kansa.
  1.        Yafuatayo ni mazao ya chakula, ISIPOKUWA:

A. Mahindi B. Ndizi C. Mihogo D. Ulezi E. Pareto [ ]

  1.        Madini magumu zaidi ambayo hutumika katika mapambo na kukatia vioo hujulikana kama:

A. Dhahabu B. Shaba C. Tanzanaiti D. Chokaa E. Makaa ya mawe [ I

33. Shughuli ipi ya uzalishaji mali kati ya hizi zifuatazo hufanyika zaidi katika maeneo yenye udongo wenye rutuba na mvua za kutosha?

A. Uchimbaji wa madini B. Uvuvi C. Viwanda D. Kilimo E. Ufugaji [ I

34. Zifuatazo ni faida za utalii, ISIPOKUWA:

  1.              Hutupatia fedha za kigeni C. Kuongezeka kwa pato la taifaa              E. Kukua kwa uchumi wa taifa
  2.              Hutupatia ajira D. Uchafuzi wa mazingira [ I

35. Mtibwa, Kilombero, Kagera na Moshi ni maeneo maarufu kwa kilimo cha:

A. Chai B. Mkonge C. Kahawa D. Pamba E. Miwa [ I

36. Shughuli inayohusisha kuuza na kununua bidhaa hujulikana kama:

A. Utalii B. Biashara C. Uchukuzi D. Uuzaji E. Ununuzi

37. Sanaa ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile mikeka, mazuria na vikapu kwa kutumia majani au magome ya miti hujulikana kama:

  1.              Uchongaji
  2.               Ufinyanzi
  3.               Ufumaji
  4.              Upakuaji
  5.               Uchapaji

38. Miongoni mwa dalili za kubalehe kwa wanawake ni:

  1.              Kuwa na sauti nzito
  2.               Kuota ndevu
  3.               Kupanuka kwa kifua hedhi
  4.              Kutoa harufu nzuri

39. Kwanini unashauriwa kufunua jiko mara wakati wa kuoka mikate?

  1.              Kuongeza ladha
  2.               Kuongeza chumvi
  3.               Kuondoa sukari
  4.              Kufanya mikate ichemke haraka
  5.               Kuepuka kuunguza mikate

40. Kiasi cha fedha kinachobakia kwa mjasiriamali mara baada ya kulipa gharama za mtaji wa biashara hujulikana kama: A. Matumizi              B. Mtaji              C. Mauzo              D. Akiba              E. Faida              

SEHEMU B: MASWALI YA MAJIBU MAFUPI 

Jibu swali la 41-45 kwa kuandika majibu sahihi katika karatasi ya kujibia uliyopewa

  1.   Kwanini tunashauriwa kukausha maji mwilini mara baada ya kuoga?
  2.   Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni nani?
  3.   Eleza kwa kifupi ni kwa jinsi gani shughuli za uchukuzi huchangia katika maendelelo ya taifa
  4.   Makamu mkuu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa nani?
  5.   Eleza athari mbili za majanga ya moto 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 30

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA MSINGI

MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA -MACHI 2021

MAARIFA YA JAMII – DARASA LA SABA

FOMATI MPYA

MUDA1:30 MASAA MACHI 2021

JINA …………………………...SHULE ………………………...

MAELEZO

  1. Mtihani huu una sehemu Mbili A na B na jumla ya maswali matano
  2. Sehemu ya A ina alama 40 na sehemu B ina alama 10
  3. Jibu maswali yote kulingana na maelezo ya kila swali
  4. Mtihani wote una alama 50

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

KIPENGELE I: URAIA

  1. Katika muundo wa kiutawala wa serikali za mitaa, wilaya na manispaa zinaongozwa na:
  1. Chama tawala
  2. Mkurugenzi mtendaji
  3. Mkuu wa wilaya
  4. Kamati yenyewe
  5. Afisa utawala wa wilaya
  1. Mwenye wajibu wa kulinda Uhuru na mipaka ya nchi ni ……….
  1. Mwananchi mwenyewe
  2. Serikali
  3. Jeshi la wananchi wa Tanzania
  4. Rais
  5. Waziri mkuu
  1. Katika muundo wa kiutawala wa serikali za mitaa, wilaya na manispaa zinaongozwa na:
  1. Chama tawala
  2. Mkurugenzi mtendaji
  3. Mkuu wa wilaya
  4. Kamati yenyewe
  5. Afisa utawala wa wilaya
  1. Jeshi linalohusika kurekebisha tabia za wahalifu ni:- ………
  1. Mgambo
  2. Polisi
  3. JWTZ
  4. Magereza
  5. Uhamiaji
  1. Utamaduni katika Jamii unaweza kuonekana katika yote isipokuwa:- …..
  1. Chakula
  2. Mavazi
  3. Kufanyakazi
  4. Ngoma
  5. Utalii
  1. Chombo chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania ni:
  1. Jeshi la polisi
  2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  3. Mahakama Kuu
  4. Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
  5. Ofisi ya Waziri Mkuu
  1. Njia nzuri unapotaka kuanza biashara mpya ni…………
  1. kuiga mikakati ya biashara kutoka kwa majirani
  2. kuhusisha Ndugu katika biashara zako
  3. Kuangalia upatikanaji wa bidhaa na soko
  4. Kuwa na mtaji mkubwa
  5. Kuwa na makazi ya watu.
  1. Ulinzi na usalama wa taifa letu ni jukumu la:
  1. Jeshi Wananchi wa Tanzania
  2. kitengo cha Usalama wa Taifa
  3. Jeshi la Polisi
  4. mgambo
  5. kila mwananchi
  1. Maliasili ya Taifa huwakilishwa kwenye nembo ya Taifa kwa kutumia alama ya _______________
  1. Mlima Kilimanjaro
  2. mkuki
  3. karafuu
  4. mawimbi ya bahari
  5. pembe za tembo
  1. Utandawazi ni mfumo unao hamasisha:
  1. teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi zinazoendelea
  2. haki sawa kwa kila mmoja duniani
  3. mfumo wa vyama vingi katika nchi zinazoendelea
  4. biashara huria baina ya mataifa
  5. sekta binafsi katika nchi zinazoendelea
  1. Nini maana ya ujasiriamali?
  1. Bishara yoyote yenye faida
  2. Uwekezaji kwenye biashara
  3. Biashara ndogondogo
  4. Sekta binafsi
  5. Ujasiri wa kumiliki mali
  1. Kiongozi anayeshughulikia shughuli za Serikali Bungeni ni;_______
  1. Spika wa Bunge
  2. Waziri Mkuu
  3. mwanasheria Mkuu wa Serikali
  4. Wabunge wote
  5. Rais wa Jamhuri ya Muungano
  1. Eneo la kiutawala ambalo ni kubwa kuliko kata lakini ni dogo kuliko Wilaya linaitwa____
  1. Kijiji
  2. Mkoa
  3. Jimbo
  4. Ukanda
  5. Tarafa
  1. Katika bendera ya Taifa rangi ya njano huwakilisha nini__________
  1. Uoto wa Asili
  2. Watu wa Tanzania
  3. Madini
  4. Maji
  5. Kilimo
  1. Mahitaji ya msingi ya familia ni kama _________A.chakula , malazi, na magari (B.chakula, nguo na televisheni C. Nguo, malazi na chakula D chakula, malazina televisheni E.Chakula, malazi mavazi na ngoma za Asili.

HISTORIA

  1. Azimio la Arusha lilihusu…………
  1. Uhuru na kazi
  2. siasa na kilimo
  3. Elimu kwa wote
  4. Siasa ya ujamaa na kujitegemea
  5. mfumowavyamavingi
  1. Wafanyabiashara kutoka bara la Asia walifika Tanganyika kwa mara ya kwanza mnamo
  1. Karne ya 15
  2. Karne ya 19
  3. Karne ya 8
  4. Karne ya 9
  5. Karne ya 12
  1. Kundi la familia anuai Lenye chimbuko moja huitwa ………
  1. Baba na watoto
  2. ukoo
  3. ndugu
  4. wanandugu
  5. familia
  1. Kabla ya ukoloni majukumu ya kiongozi wa ukoo yalikuwa ni pamoja na:
  1. kutatua migogoro
  2. kusaini mikataba na wakoloni
  3. kuongeza idadi ya mifugo
  4. kujenga nyumba
  5. kuanzisha vijiji vya ujamaa
  1. Azimio la Arusha lililenga zaidi:
  1. uhuru na kazi
  2. siasa na kilimo
  3. elimu kwa wo?e
  4. ujamaa na kujitegemea
  5. mfumo wa vyama vingi
  1. Zipi kati ya Nchi zifuatazo zilipata uhuru kwa njia ya mtutu wa bunduki?................
  1. Angola, Ghana na Kenya
  2. Zimbabwe, Angola na Msumbiji
  3. Msumbiji, Liberia na Zimbabwe
  4. Uganda, Rwanda na Tanzania
  5. Kenya, Uganda na Liberia
  1. Mwanadamu alianza kutembea kwa miguu miwili katika hatua gani ya mabadiliko?
  1. Primate
  2. Homo sapiens
  3. Homo habilis
  4. Zinjanthropus
  5. Homo erectus
  1. Dhamira ya kuligombea na kuligawa bara la Afrika karne ya 19 ilichochewa zaidi na jambo gani kati ya hayo yafuatayo?
  1. ili kuwastaarabisha waafrika
  2. matakwa ya kiuchumi ya Nchi za kibeberu
  3. matakwa ya kiuchumi ya Nchi za kijamaa barani Asia
  4. mapinduzi ya viwanda barani Afrika
  5. Nchi za kibepari kutaka zionekane bora zaidi kuliko zingine
  1. _________ ni mfumo wa uzalishaji mali uliodumu kwa muda Mfupi kuliko mifumo mingine yote barani Afrika.
  1. Ujima
  2. Ujamaa
  3. Ukabaila
  4. Utumwa
  5. Ubepari
  1. Inasadikika kuwa Binadamu wa kwanza aliishi.......
  1. Afrika
  2. Ulaya
  3. Australia
  4. Amerik26.
  1. Watangulizi wa kwanza wa ukoloni kuwasili Zanzibar na Tanganyika walikuwa:
  1. wafanya biashara
  2. Wamisionari
  3. Wapelelezi
  4. Walowezi
  5. Waarabu
  1. Jamii za Afrika ya Mashariki zilizopinga ukoloni kwa silaha ni pamoja na:
  1. Wanandi na Wahehe
  2. Wasangu na Wabena
  3. Waha na Wakamba
  4. Waganda na Wabena
  5. Wabena na Wapare
  1. Michoro ya mapangoni Nchini Tanzania inapatikana ______
  1. Olduvai Gorge
  2. Russinga
  3. Kondoa Irangi
  4. Isimila Iringa
  5. PanganiTanga
  1. Mapambano ya kudai Uhuru katika bara la Afrika yalianza baada ya:
  1. Kuundwa kwa Umoja wa Mataifa
  2. Kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti
  3. Vita Kuü ya Pili ya Dunia
  4. Kupigwa marufuku biashara ya watumwa
  5. Kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi
  1. Sehemu ya ardhi iliyozungukwa na maji pande zote huitwa________
  1. Penisula
  2. Kisiwa
  3. Rasi
  4. Ghuba
  5. Bara
31. Tunapataje idadi ya watu katika sehemu fulani?
  1. Kwa kuhesabu watoto wachanga
  2. Kwa kuhesabu wafu
  3. Kwa kuhesabu wakimbizi
  4. Kwa kukokotoa eneo Ia sehemu
  5. Kwa kufanya sensa
  1. Vitu viwili vinavyounda mazingira ni __________
  1. mimea na wanyama
  2. milima na mabwawa
  3. vitu vyenye uhai na visivyo na uhai
  4. binadamu na wanyama
  5. maji na hewa
  1. Uharibifu wa mazingira unaweza kudhibitiwa kwa________
  1. matumizi ya mifuko ya plastiki
  2. utupaji taka ovyo
  3. matumizi ya mbolea za viwandani
  4. ufugaji wa wanyama
  5. kuchakata taka
  1. Dunia inajizungusha yenyewe katika Muhimili wake tuapata ;___
  1. Usiku na mchana
  2. Majira mbalimbali ya Mwaka
  3. Kupatwa kwa Jua
  4. Kupungua kwa jotoridi Duniani
  5. Kutofautiana kwa nyakati katika Longitudo moja.
  1. Maji ya mvua yanaweza kukingwa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye kwa kutumia:
  1. Ndoo na mabomba
  2. Chupa na majaba
  3. Visima na chupa
  4. Visima na mapipa
  5. Ndoo na chupa
  1. Mojawapo kati yak maziwa yafuatayo lipo katika bonde la ufa la mashariki__
  1. Turkana
  2. Albert
  3. Kyoga
  4. Tanganyika
  5. Edward
  1. Nchi ambayo hustawisha zao la mpira kwa wingi katika bara la Afrika ni .…….
  1. Liberia
  2. Ghana
  3. Nigeria
  4. Burundi
  5. Gabon
  1. Picha inayoonesha msitu mnene na mazao kama minazi yawezakuwa inawakilisha eneo lenye:
  1. Hali ya hewa ya kiikweta
  2. Hali ya hewa ya kitropiki
  3. Hali ya hewa ya kimonsun
  4. Hali ya hewa ya kimediteranian
  5. Hali ya hewa ya baridi
  1. Kabila lililojishughulisha na biashara ya masafa marefu kusini mwa Tanganyika kabla ya ukoloni Afrika Mashariki ni ____________
  1. maasai
  2. kamba
  3. chagga
  4. nyakyusa
  5. hehe
    1. Mojawapo ya sababu za kuongezeka kwa idadi ya watu na kuzaliana ni:
    1. uhamiaji na kuzaliana
    2. watu kukosa elimu ya maisha
    3. Kuzaliana na afya
    4. Ndoa za watu wenye umri mdogo
    5. Ongezeko Ia wakimbizi


    TUMIA RAMANI IFUATAYO KUJIBU SWALI LA 41-45

    41. Herufi F inawakilisha kisiwa cha…………………………

    42. Herufi D inawakilisha ziwa :-………………..

    43. Herufi A ninchi ya:- ……………………

    44. Herufi G ni mbuga ya …………………………

    45. Herufi B ni reli ya:- ……………….

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 21

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MAARIFA YA JAMII DARASA LA SABA 2021

TATHIMINI YA AWALI

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

KIPENGELE I: URAIA 

  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaitwa mheshimiwa……(A) Dr.Ally Mohamed Shein (B)Bakili Mluzi  (C)  Edgar Rungu (D) Dr John Pombe Magufuli     (E)Kasimu Majaliwa Kasimu (  )
  1. Mwenye wajibu wa kulinda Uhuru na mipaka ya nchi ni ……….(A) Mwananchi mwenyewe (B)Serikali (C) Jeshi la wananchi  wa Tanzania   (D) Rais  (E) Waziri mkuu
  1. Muswada wa sheria huandaliwa na …………..(A) Spika wa Bunge (B) Wabunge (C)    Waziri wa sheria (D) Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali E.Mahakama.
  1. Jeshi linalohusika kurekebisha tabia za wahalifu ni:- ………(a) Mgambo (B) Polisi (C) JWTZ (D) Magereza  (E) Uhamiaji
  1. Utamaduni katika Jamii unaweza kuonekana katika yote isipokuwa:- …..(A)Chakula (B) Mavazi (C) Kufanyakazi (D) Ngoma (E)  Utalii
  1. Kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania raia anaweza kugombea Urais akiwa na umri wa miaka ………(A) 21 na zaidi (B) 40 na zaidi (C)18 na zaidi (D) 50 na zaidi (E) 61 na zaidi
  1. Njia nzuri unapotaka kuanza biashara mpya ni…………(A)kuiga mikakati ya biashara kutoka kwa majirani (B) kuhusisha Ndugu katika biashara zako C.Kuangalia upatikanaji wa bidhaa na soko D.)Kuwa na mtaji mkubwa E.)Kuwa na makazi ya watu.
  1. Kiongozi anayeteuliwa na Rais ili aongoze shughuli  zote za Serikali katika Wilaya anaitwa __________________ (a) Mkuu wa  Wilaya (b) Mwenyekiti wa Halmashauri  (c) KatibuTawala Wilaya   (d) Diwani     (e) Mkurugenzi wa Halmashauri.
  1. Maliasili ya Taifa huwakilishwa kwenye nembo ya Taifa kwa kutumia alama ya _______________ (a) Mlima Kilimanjaro (b) mkuki (c) karafuu (d) mawimbi ya bahari (e) pembe za tembo
  1. Jumuiya ya Madola ni Muungano wa hiari wa Nchi zilizowahi kuwa chini ya Utawala wa __ (a) Ujerumani (b) Ufaransa (c) Italia (d)  Ureno (e) Uingereza
  1. Vitu vinavyounda utamaduni  wa Taifa ni pamoja na______A. Sanaa na Lugha B. Makazi na fedha C. Sheria na Mila D. Sanaa na walimu E. jeshi na Serikali
  1. Kiongozi anayeshughulikia shughuli za Serikali Bungeni ni;_______ A. Spika wa Bunge B. Waziri Mkuu  C.mwanasheria Mkuu wa Serikali D. Wabunge wote E. Rais wa Jamhuri ya Muungano
  1. Eneo la kiutawala ambalo ni kubwa kuliko kata lakini ni dogo kuliko Wilaya linaitwa____A. Kijiji B. Mkoa C. Jimbo D. Ukanda E. Tarafa
  1. Katika bendera ya Taifa rangi ya njano huwakilisha  nini__________ A.Uoto wa Asili B. Watu wa Tanzania C. Madini D. Maji E. Kilimo
  1. Mahitaji ya msingi ya familia ni kama _________A.chakula , malazi, na magari  (B.chakula, nguo na televisheni   C. Nguo, malazi na chakula D chakula, malazina televisheni E.Chakula, malazi mavazi na ngoma za Asili.

HISTORIA

  1. Azimio la Arusha lilihusu………… (a) Uhuru na kazi (b) siasa na kilimo (c) Elimu kwa wote (d)Siasa ya  ujamaa na kujitegemea (e) mfumowavyamavingi
  1. Hatua ya mwanzo aliyopitia binadamu katika harakati za kupambana na mazingira yake ni ___ (A) Mshikamano (B) Utumwa (C)Umoja (D) Ujima (E) Ujamaa
  1. Kundi la familia anuai Lenye chimbuko moja huitwa ………(A)Baba na watoto (B) ukoo   (C) ndugu                   (D)  wanandugu   (E) familia
  1. Historia ya Maisha ya binadamu inaweza kugawanywa katika zama kuu mbili nazo ni…… (A) zama za mawe na Sayansi na Teknolojia (B) zama za chuma na zama za mawe(C) zama za mawe za kale (D) zama za mawe za kale na zama za  mawe za kati(E) zama za chuma na zama za mwisho
  1. Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika aliitwa ____ (A) RashidiKawawa

(B)Julius K. Nyerere (C) Abeid Karume (D) Edward Sokoine (E) Ahamed Salimu

  1. Zipi kati ya Nchi zifuatazo zilipata uhuru kwa njia ya mtutu wa bunduki?................

(A)Angola, Ghana na Kenya (B) Zimbabwe, Angola na Msumbiji 

(C) Msumbiji, Liberia na Zimbabwe (D) Uganda, Rwanda na Tanzania  

(E) Kenya, Uganda na Liberia    

  1. Vita vilivyotokea Rwanda mwaka 1994 vilitokana na ________

              (A) Ukabila (A) Utajiri (C)   rushwa (D) ukabaila (E) ubepari

  1. Dhamira ya kuligombea na kuligawa bara la Afrika karne ya 19 ilichochewa zaidi na jambo gani kati ya hayo yafuatayo?A.ili kuwastaarabisha waafrika B.matakwa ya kiuchumi ya Nchi za kibeberu  C.matakwa ya kiuchumi ya Nchi za kijamaa barani Asia D.mapinduzi ya viwanda barani Afrika E.Nchi za kibepari kutaka zionekane bora zaidi kuliko zingine
  1. _________ ni mfumo wa uzalishaji mali uliodumu kwa muda Mfupi kuliko mifumo mingine yote barani Afrika. A.  Ujima                 B. Ujamaa C.Ukabaila D.Utumwa  E. Ubepari
  1. Inasadikika  kuwa Binadamu wa kwanza aliishi.......A.frika B. Ulaya  C.Australia D. Amerika


  1. Uongozi katika koo mbalimbali ulianza binadamu alipoanzisha A.Makazi ya muda B. Makazi ya kudumu C.Makazi ya kuhamahama D.Mfumo wa kutembea E.Makazi ya pangoni
  1. Alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii za Wahaya………… A.Abatwazi B.Omukama C.Abatwale D. Abankole E.Mukama
  1. Michoro ya mapangoni Nchini Tanzania inapatikana ______A.Olduvai Gorge  B.Russinga   C.Kondoa Irangi   D.Isimila Iringa E.PanganiTanga
  1. Historia ya Pwani ya  Afrika Mashariki inaonesha kuwa bandari ya Kilwa na Sofala zilikuwa zinasafirisha dhahabu ng’ambo. Dhahabu hiyo ilitoka……A. Zambia B. Botswana  C. Zimbabwe  D. Congo E.Angola
  1. Sehemu ya ardhi iliyozungukwa na maji pande zote huitwa________(A) Penisula (B) Kisiwa (C) Rasi(D) Ghuba              (E) Bara [              ]
  2. Mfumo wa umwagiliaji wa Gezira ni maarufu  kwa uzalishaji wa________(A) Pamba  (B) Chai   (C) Katani                            (D) Ndizi              (E) Mpunga              [              ]
  3. Vitu viwili vinavyounda mazingira ni __________(A) mimea na wanyama (B) milima na mabwawa      (C) vitu vyenye uhai na visivyo na uhai(D) binadamu na wanyama(E) maji na hewa              [              ]
  4. Uharibifu wa mazingira unaweza kudhibitiwa kwa________ (A) matumizi ya mifuko ya plastiki  (B) utupaji taka ovyo(C) matumizi ya mbolea za viwandani (D) ufugaji wa wanyama (E) kuchakata taka
  1. Dunia inajizungusha yenyewe katika Muhimili wake tuapata ;___ (A) Usiku na mchana (B) Majira mbalimbali ya Mwaka (C) Kupatwa kwa Jua (D) Kupungua kwa jotoridi Duniani (E) Kutofautiana kwa nyakati katika Longitudo moja.              [              ]
  1. Nchi yenye watu wengi barani Afrika ni ___________ (A) Algeria (B) Nigeria (C) Tanzania (D) Libya              (E) Ghana                                          [              ]
  1. Mojawapo kati yak maziwa yafuatayo lipo katika bonde la ufa la mashariki__(A) Turkana  (BAlbert      (C) Kyoga              (D) Tanganyika (E) Edward                            [              ]
  1. Nchi ambayo hustawisha zao la mpira kwa wingi katika bara la Afrika ni .…….(A) Liberia (BGhana (C) Nigeria              (D) Burundi                            (E) Gabon                            [              ]
  2. Ni mikoa ipi kati ya hii ifuatayo ni maarufu kwa uzalishaji wa kahawa____(A) Shinyanga na Dodoma (B) Morogoro na Iringa              (C) Iringa na Mbeya              (D) Kagera na Kilimanjaro (E) Kagera na Mbeya
  1. Kabila lililojishughulisha na biashara ya masafa marefu kusini mwa Tanganyika kabla ya ukoloni Afrika Mashariki ni ____________
  1. Mfanyabiashara maarufu wa Kijerumani aliyesaini mkataba wa kilaghai na Chifu Mangungo wa Musovero aliitwa……………………….A) William Maknnon B.)Karlpeters C.)David Livingstone D.)Vasco da Gama E.)John Speke

TUMIA RAMANI IFUATAYO KUJIBU SWALI LA 41-45

  1. Herufi F inawakilisha kisiwa cha…………………………
  2. Herufi D inawakilisha ziwa :-………………..
  1. Herufi A ninchi ya:- ……………………
  2. Herufi G ni mbuga ya …………………………
  3. Herufi B ni reli ya:- ……………….

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 18

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MAARIFA YA JAMII - MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA

DARASA LA SABA

MUDA: 1.30      

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una maswali 50
  2. Jibu maswali yote katika nafasi uliopewa
  3. Hakikisha kazi yako ni safi
  4. Usijaribu kuibia

SEHEMU A.

1. Ni madini yapi yanayopatikana Tanzania pekee?

  1.  Dhahabu 
  2.  Urani
  3.  Almasi
  4. Tanzanaiti 
  5.  Makaa ya mawe

2. Uvuvi usio endelevu hufanyika kwa kutumia:

  1. Mitego
  2. Meli kubwa
  3. Nyavu mraba ndogo
  4. Ugwe
  5. Nyavu mraba kubwa

3. Kuna makundi mangapi ya uoto wa asili?

  1.  Matatu 
  2.  Manne 
  3.  Mawili 
  4.  Matano 
  5.  Sita

4. Lengo kuu la mabadiliko ya katiba ya Tanzania mwaka 1962 yalikuwa

  1. kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
  2. kuunda serikali ya shirikisho
  3. kuunda serikali ya mtaa
  4. kuunda serikali ya jamhuri
  5. kuunda serikali ya mpito.

5. Umoja wa Afrika ulianzishwa rasmi mwaka gani?

  1.  2002 
  2.  2001 
  3.  1963 
  4.  1945 
  5.  1999

6. Ubugabire ni mfumo wa Umwinyi uliajengwa juu ya umiliki wa:

  1.  ngombe 
  2.  viwanda 
  3.  ardhi
  4.  wafanyakazi wa kigeni 
  5.  watumwa

7. Mfumo wa kwanza ambapo jamii ilimiliki njia zote za uzalishaji kijamaa huitwa :.............

  1.  Umwinyi 
  2.  Ukomunisiti 
  3.  Ujamaa
  4.  Urafiki 
  5.  Ujima

8. Ipi ni athari ya ongezeko kubwa la watu?.................

  1. Kupungua kwa uhalifu
  2. Ongezeko la ajira
  3. Kupungua kwa maji
  4. Kupungua kwa biashara ndogondogo
  5. Kutotosheleza kwa huduma za jamii

9. Tatizo kubwa linalowakabili wakulima wengi wa Afrika Mashariki ni pamoja na ................

  1. uwepo wa mvua nyingi mwaka mzima •
  2. mvua zisizoaminika
  3. uwepo wa masoko ya uhakika
  4. uhaba wa maeneo ya kulima
  5. matumizi ya mbolea za chumvi

10. Milima mikunjo hutokea katika maeneo yenye...............

  1.  miamba tabaka 
  2.  miamba ya volkano na moto
  3.  miamba geu 
  4.  miamba mato
  5.  miamba volcano

11. Janga la kimazingira linalosababishwa na nguvu za asili pekee linaitwa

  1.  Ukame 
  2.  Tetemeko la ardhi
  3.  Mmomonyoko wa udongo 
  4.  Njaa
  5.  Uchafuzi wa mazingira

12. Wakati wa mvua kubwa inayoambatana na radi, watu hawaruhusiwi

  1.  kuvaa nguo nyekundu.......
  2.  kutumia miavuli 
  3.  kufungua milango na madirisha
  4.  kujificha chini ya mti 
  5.  kufunga luninga na redio

13. Rais Julius Kambarage Nyerere na Kwame Nkurumah walikuwa

  1. waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  2. waanzilishi wa Umoja wa Mataifa.
  3. waanzilishi wa Jumuiya ya Mataifa.
  4. waanzilishi wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika.
  5. waanzilishi wa Jumuia ya Madola.


14. Kwa nini vita vya Maji Maji vilitokea?..............

  1. Wareno waliwapeleka Watanganyika utumwani.
  2. Kinjekitile alikasirisha na uhasama wa Wajerumani na Waarabu.
  3. Watanganyika walipigwa mijeledi na Waingereza.
  4. Wajerumani waliwalazimisha watu kufanya kazi katika mashamba ya pamba.
  5. Sultani Seyyid Said aliwatesa na kuwatumikisha Waafrika.

15. Binti wa shangazi yako huitwa................

  1.  Mpwa 
  2.  Binamu 
  3.  Mama mkwe 
  4.  Shemeji 
  5.  Dada

16. Ni lini binadamu alianza kuchoma misitu iii kuwafukuza wanyama wakali?.................

  1. Wakati wa Zama za Chuma
  2. Wakati wa Zama za Mwanzo za Mawe
  3. Wakati wa Zama za Kale za Mawe
  4. Wakati wa Zama za Mwisho za Mawe
  5. Wakati wa Zama za Kati za Mawe

17. Mwanzilishi wa mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma katika Afrika alikuwa ...

  1. Horace Byatt
  2. Friedrick Lugard
  3. Richard Turnbull
  4. Donald Cameroon
  5. Edward Twinning

18.  Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885 uliitishwa na ..

  1. Carl Peters 
  2. Johann Krapf 
  3. Henry Stanley 
  4. David Livingstone
  5. Otto Von Bismarck.

19. Familia hujumuisha

  1. marafiki, watoto na ndugu
  2. baba, mama na watoto
  3. majirani, ndugu na watoto
  4. majirani watoto na marafiki
  5. baba, mama na majirani

20. Moja ya athari mbaya ya utandawazi kwa Tanzania ni ...

  1. kuongezeka kwa idadi ya wageni nchini
  2. kumomonyoka kwa maadili katika jamii
  3. kuongezeka kwa uhasama baina ya vyama vya siasa
  4. kuongezeka kwa uhuru wa vyombo vya habari
  5. ongezeko la matumizi ya teknolojia ya habari

21. Utawala wa sheria maana yake ni ...

  1. wananchi kujichukulia sheria mkononi
  2. polisi kuadhibu wanaovunja sheria
  3. sheria kuchukua mkondo wake
  4. mahakama kukamata wanaovunja sheria
  5. mamlaka ya mahakama kutunga sheria

22. Kuzingatia sheria, haki za bianadamu, ukweli na uwazi, na uhuru wa vyombo vya habari ni misingi ya

  1. Urasimu
  2. Utawala wa sheria
  3. Ujamaa wa kiafrika
  4. Demokrasia ya Uwakilishi
  5. utawala bora

23. Mwenyekiti wa kikao cha maendeleo katika kata ni .

  1. Diwani wa kata
  2. Afisa Huduma za ugani
  3. Afisa Maendeleo wa kata
  4. Mratibu Elimu wa kata
  5. Afisa Mtendaji wa kata

24. Mto uliooneshwa kwa herufi E unaitwa:

  1.  Tana           
  2.  Galana
  3.  Naili         
  4.  Malagarasi 
  5.  Ruaha

 25. Mlima maarufu unaopatikana katika eneo lenye herufi C huitwa:

  1.  Kilimanjaro               
  2.  Rungwe
  3.  Meru    
  4.  Usambara 
  5.  Uluguru

26.  Nchi inayooneshwa kwa herufi B ni maarufu kwa uzalishaji wa madini yanayoitwa:

  1.   Dhahabu
  2.  Tanzanaiti
  3.  Makaa ya Mawe
  4.   Almasi
  5.   Shaba

27. Ongezeko Ia joto duniani, ukame, mafuriko na vimbunga ni matokeo ya athari zitokanazona

  1.  uharibifu wa mazingira
  2.  tsunami iliyotoka Asia
  3.  ongezeko kubwa Ia watu katika nchi za Ulaya
  4.  matumizi ya mabomu ya nyuklia
  5.  Mvua nyingi

28.  Faida ya ushirikiano kati ya shule na jumuiya inayozunguka shule ni pamoja na:

  1.  ulinzi na usalama wa shule kuimarika
  2.  ongezeko Ia idadi ya watoto wanaoandikishwa shule
  3.  nafasi za ajira kwa jamii inayozunguka shule kuongezeka 
  4.  shughuli za biashara kuzunguka eneo Ia shule kuongezeka
  5.  walimu wengi kupata nyumba za kupanga jirani na shule

29. Ni hatua zipi wanafunzi wanatakiwa kuchukua wanapoona katika eneo la shule wageni wanaowatilia shaka? 

  1.  Kutoa taarifa kwa jeshi la Wananchi la Tanzania. 
  2.  Kutaarifu Kamati ya Shule kuhusu uwepo wa wageni.
  3.  Kuwapiga wageni kabla ya kuwafikisha Mahakamani.
  4.  Kuwakamata wageni na kuwahoji.
  5.  Kutaarifu Walimu kuhusu uwepo wa wageni.


 30. Uchumi wa soko huria, ushindani wa kidemokrasia katika siasa na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano ni viashiria vya

  1.  ujasiriamali 
  2.  utawala bora 
  3.  utawala wa sheria 
  4.  utandawazi 
  5.  haki za binadamu

31.  Rangi nyeusi katika bendera yetu huwakilisha:

  1.  Mimea      
  2.  Madini
  3.  Watu   
  4.  Ardhi 
  5.  Mbuga za wanyama

32.  Sababu kubwa ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi Tanzania ni:

  1.  kutekeleza matakwa ya wahisani
  2.  kulinda haki za makundi maalumu katika jamii
  3.  kuvutia wawekezaji wa nje
  4.  kutekeleza maelekezo ya Umoja wa Mataifa
  5.  kupanua demokrasia

33.  Haki ya kumiliki mali iko katika kipengele kipi cha haki za binadamu?

  1.  Kijamii na kiuchumi   
  2.  Kisiasa na kiuchumi
  3.  Kikatiba na kisiasa               
  4.  Kijamii na Kisiasa 
  5.  Kijamii na Kiutamaduni

34.  Ulinzi na usalama wa taifa letu ni jukumu la:

  1.  Jeshi Wananchi wa Tanzania 
  2.  kitengo cha Usalama wa Taifa
  3.  Jeshi la Polisi
  4.  mgambo
  5.  kila mwananchi

35. Utandawazi ni mfumo unao hamasisha:

  1. teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi zinazoendelea
  2. haki sawa kwa kila mmoja duniani
  3. mfumo wa vyama vingi katika nchi zinazoendelea
  4. biashara huria baina ya mataifa
  5. sekta binafsi katika nchi zinazoendelea . 

36. .Mojawapo ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa ni:

  1.  kushindwa kuzuia kuenea kwa Utandawazi
  2.  Waafrika hawajawahi kupata nafasi katika uongozi wa juu katika Umoja wa Mataifa
  3.  baadhi ya watu tu ndio wenye kura ya turufu
  4.  kushindwa kupitisha maazimio ya haki za binadamu
  5.  kutokushirikishwa kwa Waafrika katika vikao vya baraza la usalama

37. Mkutano wa kuligawa bara la Afrika ulifanyika:

  1. Berlin
  2. London
  3. Roma
  4. Paris
  5. New York

38. Katika zama za mawe za mwisho ugawanyaji majukumu katika jamii ulifanyika kwa misingi ya:

  1. hekima na utajiri
  2. hekima na umri
  3. uzoefu na hekima 
  4. umri na jinsia 
  5. utajiri na umri

39.Utawala waWaingereza nchini Tanganyika uliisha mnamo .....

  1. karne ya 15 
  2. karne ya 19 
  3. karne ya 20 
  4. karne ya 18 
  5. karne y 17

40. Watangulizi wa kwanza wa ukoloni kuwasili Zanzibar na Tanganyika walikuwa:

  1.  wafanya biashara   
  2. Wamisionari  
  3. Wapelelezi
  4. Walowezi                            
  5. Waarabu

41. Mataifa ya Ulaya yaliyokuwa yakipigania Mto Nile yalikuwa:

  1.  Ufaransa na Ubelgiji
  2.  Uingereza na Ujerumani
  3.  Ufaransa na Ureno
  4.  Uingereza na Ufaransa 
  5.  Ubelgiji na Ureno

42. Tunapataje idadi ya watu katika sehemu fulani?

  1. Kwa kuhesabu watoto wachanga
  2. Kwa kuhesabu wafu
  3. Kwa kuhesabu wakimbizi
  4. Kwa kukokotoa eneo Ia sehemu 
  5. Kwa kufanya sensa

43. Mojawapo ya sababu za kuongezeka kwa idadi ya watu na kuzaliana ni:

  1. uhamiaji na kuzaliana
  2.  watu kukosa elimu ya maisha
  3.  Kuzaliana na afya
  4. Ndoa za watu wenye umri mdogo
  5. Ongezeko Ia wakimbizi

44.  Ni yapi kati ya madini yafuatayo ambayo ni chimbuko Ia nishati ya kinyuklia? 

  1. Makaa Yã mawe              
  2.  Uraniam           
  3.  Shaba
  4.  Almasi                                          
  5.  Dhahabu

45.  Mikoko ni aina ya uoto upatikanao pembezoni mwa:

  1.  mito
  2.  maziwa
  3.  bahari 
  4. mabwawa 
  5. visima

SEHEMU B

Jibu maswali yafuatayo kwa kuandika jibu lililo sahihi.

46. Nini maana ya ujasiriamali?

47. Taja tabia mbili za wajasiriamali

48.Taja changamoto mbili zinazowakumba wajasiriamali Tanzania.

49. Taja fursa za kibiashara zinazopatikana katika ufuo wa bahari

50. Mfanyabiashara sio mjasiriamali, eleza.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 10

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI YA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA SABA

MUDA : 2:30

MAARIFA YA JAMII

MAELEZO KWA MTAHINIWA

  1. Mtihani huu unamaswali 50
  2. Jibu Maswali Yote
  3. ANDIKA Majibu yako kwa Herufi kubwa
  4. Hakikisha kazi yako inasomeka vyema

Chagua Jibu sahihi.

1. Katibu kata anachaguliwa na:

  1. Wanachama wa chama tawala
  2. Mkutano mkuu wa kata
  3. Wananchi wa kata ile
  4. Mkutano wa kijiji wa mwaka
  5. Kamati ya kijiji

2. Kamati ya maendeleo ya kata inaundwa na wafuatao isipokuwa:

  1. Katibu kata
  2. Afisa mtendaji wa Kata
  3. Katibu Kata wa viti maalumu
  4. Afisa mtendaji wa Mkoa
  5. Kamanda wa Polisi wa Mkoa

3. Mwakilishi wa Rais katika ngazi ya mkoa ni:

  1. Katibu tawala wa Mkoa
  2. Mkurugenzi mtendaji wa manispaa
  3. Mkuu wa Mkoa
  4. Afisa mtendaji wa Mkoa
  5. kamanda wa Polisi wa mkoa

4. Kauli mbiu ya Tanzania iliyopo kwenye nembo ya taifa ni:

  1. uhuru na maendeleo
  2. uhuru na kazi
  3. uhuru na umoja
  4. uhuru na amani
  5. umoja na amani

5. Wimbo wa taifa una beti ngapi?

  1. Tatu
  2. Mbili
  3. Nne
  4. Tano
  5. Sita

6. Kazi ya kamati ya shule ni:

  1. Kusimamia maendeleo ya taaluma
  2. Kutoa ushauri juu ya maambukizi ya UKIMWI
  3. Kuidhinisha uteuzi wa waalimu
  4. Kusimamia nidhamu ya waalimu
  5. Kusimamia ujenzi na maendeleo ya shule.

7. Chombo chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani Tanzania ni:

  1. Jeshi la polisi
  2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
  3. Mahakama Kuu
  4. Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
  5. Ofisi ya Waziri Mkuu

8. Haki ya kumiliki mali iko katika kipengele kipi cha haki za binadamu?

  1. Kijamii na kiuchumi
  2. Kisiasa na kiuchumi
  3. Kikatiba na kisiasa
  4. Kijamii na Kisiasa
  5. Kijamii na Kiutamaduni

9. Ulinzi na usalama wa taifa letu ni jukumu la:

  1. Jeshi Wananchi wa Tanzania
  2. kitengo cha Usalama wa Taifa
  3. Jeshi la Polisi
  4. mgambo
  5. kila mwananchi

10.Mojawapo ya kazi za mgamboni:

  1. kukamata wahalifu na kuwapeleka kwenye kituo cha polisi
  2. kuadhibu wanaovunja sheria mijini
  3. kuzuia ajali za moto
  4. kukusanya kodi ya maendeleo mijini
  5. kuzuia na kupambana na rushwa

11. Utandawazi ni mfumo unao hamasisha:

  1. teknolojia ya habari na mawasiliano katika nchi zinazoendelea
  2. haki sawa kwa kila mmoja duniani
  3. mfumo wa vyama vingi katika nchi zinazoendelea
  4. biashara huria baina ya mataifa
  5. sekta binafsi katika nchi zinazoendelea .

12.Nini maana ya ujasiriamali?

  1. Bishara yoyote yenye faida
  2. Uwekezaji kwenye biashara
  3. Biashara ndogondogo
  4. Sekta binafsi
  5. Ujasiri wa kumiliki mali

13. Mtumishi wa umma ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa nafasi yake katika utumishi wa umma ni ....

  1. Jaji Mkuu
  2. Katibu Mkuu Kiongozi
  3. Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
  4. Msajili wa vyama vya siasa.
  5. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

14. Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?

  1. Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa.
  2. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
  3. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
  4. Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
  5. Mahakama Kuu ya Kimataifa.

15. Chimbuko la familia ni:

  1. babu na bibi
  2. baba na mama
  3. shangazi na mjomba
  4. watoto na wazazi
  5. kaka na dada

16. Kiongozi mkuu wa shule ni:

  1. mwalimu mkuu msaidizi
  2. mwalimu wa taaluma
  3. kiranja mkuu
  4. mwalimu mkuu
  5. mwalimu wa nidhamu

17. Nini faida ya mgawanyo wa kazi katika familia?

  1. Hudhoofisha familia
  2. Huchochea utengano
  3. Huleta udikteta
  4. Huleta maendeleo
  5. Huleta mitafaruku

18. Moto uligunduliwa katika:

  1. Zama za Mawe za Kale
  2. Zama za Mawe za Kati
  3. Zama za Chuma
  4. Zama za Mawe za Mwisho
  5. Zama za Viwanda

19. Uchoraji wa wanyama katika mapango ulianza kufanywa na binadamu katika:

  1. Zama za Chuma
  2. Zama za Mawe za Kati
  3. Zama za Mawe za Kale
  4. Zama za Mawe za Mwisho
  5. Zama za Mavve za Mwanzo

20. Mabaki ya Zinjanthropus yaliyopatikana katika bonde la Olduvai mwaka 1959 yaligunduliwa na:

  1. David Livingstone
  2. Fredrick Lugard
  3. Louis Leakey
  4. Carl Peters
  5. Charles Darwin

21.Utawala waWaingereza nchini Tanganyika uliisha mnamo .....

  1. karne ya 15
  2. karne ya 19
  3. karne ya 20
  4. karne ya 18
  5. karne y 17

22.Vita vilivyozuka nchini Ruanda mwaka 1994 vilisababishwa na:

  1. ukabila
  2. ubaguzi wa rangi
  3. rushwa
  4. ukabaila
  5. ubepari

23. Watangulizi wa kwanza wa ukoloni kuwasili Zanzibar na Tanganyika walikuwa:

  1. wafanya biashara
  2. Wamisionari
  3. Wapelelezi
  4. Walowezi
  5. Waarabu

24. Makoloni ya Ujerumani katika Afrika yalikuwa ..

  1. Naijeria, Namibia na Togo.
  2. Gambia, Togo na Namibia.
  3. Kameruni, Togo na Namibia.
  4. Namibia, Tanganyika na Naijeria.
  5. Kameruni, Tanganyika na Senegal.

25.Ni mataifa yapi kati ya yafuatayo yalianzisha umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote?

  1. Ulaya Mashariki.
  2. Nchi zinazoendelea
  3. Ulaya Magharibi.
  4. Amerika ya Kusini
  5. Amerika ya Kaskazini

26. Wajerumani walitawala Tanganyika baada ya .....

  1. Vita Kuu ya Kwanza.
  2. Vita Kuuya Pili.
  3. Mkutano wa Berlin.
  4. Kuundwa kwa UNO.
  5. Kushindwa kwa Wareno.

27.Katika Zama za Mwanzo za Mawe binadamu .....

  1. alianza kufuga wanyama na ndege.
  2. aligundua moto.
  3. alijihusisha na kilimo na biashara.
  4. aliongeza uwezo wa kuzalisha chakula.
  5. aliishi kwa kutegemea mazingira.

28. Jamii zilizokuwa maarufu kwa kufua chuma hapa Tanganyika ni pamoja na ...

  1. Wapare na Wazinza.
  2. Wapare na Wagogo.
  3. Wazinza na Wasukuma
  4. Wapare na Wajaluo.
  5. Wazinza na Wagogo.

29. Soko kuu la watumwa Zanzibar lilifungwa mwaka ......

  1. 1873
  2. 1822
  3. 1845
  4. 1820
  5. 1900

30. Mojawapo ya athari za kugawanywa kwa bara la Afrika ilikuwa .........

  1. kukua kwa viwanda vya Afrika.
  2. kudumaa kwa viwanda vya Afrika.
  3. kuboreshwa kwa uchumi wa jadi.
  4. kudumisha utamaduni wa Kiafrika.
  5. kuanza kwa biashara ya utumwa

31.Taifa la pili kuitawala Zanzibar lilikuwa ......

  1. Uingereza.
  2. Ujerumani.
  3. Ureno.
  4. Oman.
  5. Ufaransa.

32. Bidhaa zilizoletwa Tanganyika kutoka Bara la Asia kuanzia karne ya nane zilikuwa ni pamoja na ....

  1. pembe za ndovu na dhahabu.
  2. Ngozi na bunduki
  3. Chumvi na shaba
  4. Nguo na ngano
  5. Nguo na watumwa

33. Pepo huvuma kutoka pande zipi jua liwapo upande wa kusini mwa dunia?

  1. Kusini
  2. Magharibi
  3. Mashariki
  4. Kaskazini
  5. Kaskazini-mashariki

34. Tunapataje idadi ya watu katika sehemu fulani?

  1. Kwa kuhesabu watoto wachanga
  2. Kwa kuhesabu wafu
  3. Kwa kuhesabu wakimbizi
  4. Kwa kukokotoa eneo Ia sehemu
  5. Kwa kufanya sensa

35. Mojawapo ya madhara ya ongezeko kubwa Ia watu nchini Tanzania ni:

  1. Kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe
  2. Ongezeko Ia utegemezi
  3. Uhaba wa huduma za kijamii
  4. Kupungua kwa eneo Ia nchi
  5. Upungufu wa wasomi

36. Maji ya mvua yanaweza kukingwa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye kwa kutumia:

  1. Ndoo na mabomba
  2. Chupa na majaba
  3. Visima na chupa
  4. Visima na mapipa
  5. Ndoo na chupa

37. Jua la utosi katika mwezi Disemba huwa katika .

  1. Kizio cha Kusini.
  2. Tropiki ya Kansa.
  3. Ikweta.
  4. Kizio cha Kaskazini.
  5. Tropiki ya Kaprikoni.

38. Bainisha vyanzo vya umeme kati ya vifuatavyo: ....

  1. Nguvu ya maji, madini na nyaya.
  2. Upepo, nguvu ya maji na transfoma.
  3. Nguvu ya maji, upepo na jua.
  4. Makaa ya mawe, nyaya na transfoma.
  5. Nguvu ya maji, transfoma na makaa ya mawe.

39. Picha iliyopigwa katika uoto wa savanna huonesha ...

  1. misitu minene.
  2. nyasi ndefu.
  3. miti iliyochongoka juu.
  4. miti yenye umbile la mwavuli.
  5. nyasi fupi.

40. Athari kuu za viwanda katika mazingira ni .....

  1. kuchafua maji, hewa na harufu mbaya.
  2. kutoa moshi na matumizi makubwa ya nguvu ya nishati.
  3. uchafuzi wa hewa, udongo na harufu mbaya.
  4. kumwaga kemikali na kutoa moshi.
  5. uchafuzi wa hewa, maji na ardhi.

41. Zao la mkonge hulimwa katika mikoa ipi Tanzania? ....... .

  1. Tanga na Mbeya.
  2. Morogoro na Pwani.
  3. Morogoro na Tanga.
  4. Kilimanjaro na Manyara.
  5. Mtwara na Singida

42. Nchi za Kusini mvva Afrika ni pamoja na:

  1. Angola, Afrika Kusini na Namibia
  2. Afrika Kusini, Burundi na Malawi
  3. Malawi, Msumbiji na Rwanda
  4. Zimbabwe, Botswana na Tanzania
  5. Swaziland, Lesotho na Nigeria

43. Ni mikoa ipi nchini Tanzania imeonesha dalili za kuenea kwa jangwa?

  1. Shinyanga, Tabora na Mwanza
  2. Kilimanjaro, Iringa na Mbeya
  3. Lindi, Morogoro na Tabora
  4. Shinyanga, Dodoma na Singida
  5. Arusha, Ruvuma na Manyara

44. Kundi lipi linaonesha sayari?

  1. Zebaki, Mwezi na Zuhura
  2. Dunia, Nyota na Mihiri
  3. Zebaki, Serateni na Zohari
  4. Zuhura, Dunia na Kimondo
  5. Utaridi, Jua na Mwezi

45. Ongezeko Ia joto duniani, ukame, mafuriko na vimbunga ni matokeo ya athari zitokanazona

  1. uharibifu wa mazingira
  2. tsunami iliyotoka Asia
  3. ongezeko kubwa Ia watu katika nchi za Ulaya
  4. matumizi ya mabomu ya nyuklia
  5. Mvua nyingi

46. Kitu muhimu katika ramani kinachotumika kuonesha uwiano wa umbali katika ramani na umbali halisi kwenye ardhi huitwa.

  1. Skeli
  2. Dira
  3. Ufunguo
  4. Fremu
  5. Jina la ramani

47. Nishati gani kati ya zifuatazo inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira?

  1. Jua
  2. Upepo
  3. Maji
  4. Mkaa.
  5. Kinyesi cha wanyama

48. Ufugaji wa kisasa wa wanyama huzingatia nini? ..

  1. Utamaduni wa jamii
  2. Ubora wa wanyama na mazao yao.
  3. Kuwepo kwa ardhi ya kutosha.
  4. Mbuga za asili za kulishia mifugo.
  5. Hali ya hewa.

49. Majira ya mwaka hutokea kutokana na ...

  1. kupatwa kwa mwezi
  2. mwezi kuizunguka dunia
  3. dunia kulizunguka jua
  4. kupatwa kwa jua
  5. kuongezeka kwa joto.

50. Mikoa ipi ina mashamba makubwa ya Chai?

  1. Pwani, Njombe na Iringa
  2. Ruvuma na Morogoro
  3. Morogoro, Njombe na Iringa.
  4. Kilimanjaro na Mbeya
  5. Mbeya, Njombe na Iringa

LEARNINGHUBTZ.CO.TZMAARIFA STANDARD SEVEN EXAM SERIES 6

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256