OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA SITA
SAYANSI NA TECHNOLOJIA
MUDA:1:30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
MAELEZO
1. Jaza taarifa zako muhimu katika karatasi ya kujibia uliyopewa
2. Jibu maswali yote kulingana na maelekezo ya kila sehemu
3. Zingatia unadhifu wa kazi yako
4. Katika swali la 1-40 andika herufi ya jibu sahihi
5. Kwa swali la 41-45 andika majibu katika nafasi iliyoachwa wazi
Chagua Jibu sahihi kuanzia swali la 1-40 kisha andika jibu katika nafasi uliyopewa.
- Tarakilishi utumika katika maeneo haya isipokuwa (a) Vyuoni (b) Benki (c) Ofisini (d) Yote hapo juu
- Kazi ya pau la mwoneko ni (a) Kuboresha kazi za uandishi (b) Kupanga mwonekano wa ukurasa (c) Kuona nyaraka katika sura mbalimbali (d) Kusahihisha makosa katika waraka
- Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo... (a) joto na unyevu (b) unyevu na mwanga (c) upepo na mwanga wa jua (d) mawingu na upepo (e) unyevu na upepo
- Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha: (a) mmea kukosa madini joto (b) mmea kushindwa kusanisi chakula (c) majani ya mmea kukauka (d) majani ya mmea kuwa njano (e) majani ya mmea kupukutika.
- Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili? (a) Wadudu (b) Mimea (c) Wanyama (d) Virusi (e) Ndege
- Ipi kati ya zifuatazo siyo kazi ya mizizi katika mimea?..............(a) Kusharabu madini ya chumvi. (b) Kusharabu maji (c) kushikilia mmea (d) Kutengeneza chakula cha mmea (e) Kutunza chakula cha mmea
- Ni mmea gani ya hizi hauifadhi chakula katika shina? (a) Miwa (b) Magimbi (c) Viazi (d) Karoti (e) Tangawizi..
- Ipi sio faida ya vituo vya huduma za afya kwa Watoto? (a) Wazazi hupata elimu ya njia bora za kuwalea Watoto (b) Husaidia kupunguza vifo vya Watoto (c) Hutoa hamasa kuhusu wazazi wote kushiriki malezi ya Watoto (d) Husaidia Watoto kupata ushauri juu ya Maisha
- Chakula cha asili na bora zaidi kwa mtoto mchanga ni………….(a) Maziwa ya mama (b) Maziwa ya ng’ombe (c) Maziwa ya kopo (d) Uji wa lishe
- Kuwa na wataalamu wa kutosha ni miongoni mwa sifa muhimu za……………..(a) Kliniki yoyote ya afya ya jamii (b) Kliniki ya ushauri kwa vijana tu (c) Kituo cha kuwahudumia wajawazito tu (d) Kutuo cha watoto yatima tu
- Lengo kubwa la huduma za afya kwa wagonjwa ni………….. (a) Kuwafariji kutokana na matatizo mbalimbali ya kimaisha (b) Kuwasaidia kupona haraka ili warudi kwenye majukumu yao ya kawaida (c) Kuwashauri kuhusu uzalishaji maji (d) Kuwapunguzia gharama za maisha
- Mojawapo ya tahadhari za kuchukua kwa wagonjwa wa anemia selimundu ni (a) Kumpatia mgonjwa mlo kamili(b) Kumpatia chanjo (c) Kufanya mazoezi magumu (d) Kumpatia mgonjwa maji ya kutosha au chakula cha maji maji
- Dawa zinazoongeza damu kuganda wakati mgonjwa wa hemofilia amepata jeraha………(b) Hupunguza athari za hemophilia (b) Huongeza athari za hemophilia (c) Hazina msaada kwa mtu mwenye hemophilia (d) Hutibu tatizo la hemophilia
- Moja kati ya zifuatazo ni dalili ya ugonjwa wa anemia selimundu…………(a) Damu kutoka mfululizo kwenye jeraha (b) Mishipa ya damu kupasuka hasa iliyo kwenye tishu laini (c) Kupata choo chenye damu (d) Kupungukiwa na damu mara kwa mara
- Dalili mojawapo ya ugonjwa wa UKIMWI ni (a) kupungua uzito kwa haraka (b) kuwashwa sehemu za siri (c) kuvimba miguu na tumbo (d) kupoteza uwezo wa kuona (e) kuwa na hasira
- Virusi Vya Ukimwi hushambulia aina gani ya chembe hai katika damu? (a) chembe sahani (b) chembe hai nyeupe (c) Chembe hai nyekundu (d) Hemoglobini (e) Plazima
- Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI? (a Vaa nguo safi (b) Nawa kwa sabuni (c) Vaa glovu (d) Sali (e) Mruhusu apumzike
- UKIMWI husambazwa kwa kupitia: (a) kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI (b) kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI (c) kuongea na mwathirika wa UKIMWI (d) kuwekewa damu (e) kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.
- Je nini utakachokifanya ikiwa utaona nguo alizovaa rafiki yako zinaungua kwa moto?..........(a)Kumpaka mafuta (b) Kumweka maji kwenye jeraha (c) Kumfunika kwa blanketi au nguo nzito (d) Kumpulizia hewa ya oksijeni (e) Kumvua nguo zilizokwisha ungua
- Kifaa kifuatacho siyo muhimu kuwemo katika sanduku Ia huduma ya kwanza (a) Wembe (b) Pimajoto (c) Mkasi (d) Kijiko (e) Kibanio
- Huduma ya kwanza hutolewa kwa lengo gani? (a) Kushusha gharama za matibabu (b) Kuonesha umahiri wa kitabibu (c) Kuokoa maisha ya wagonjwa (d) Kurahisisha matibabu (e) Kupunguza idadi ya madaktari.
- Mojawapo ya huduma ya huduma muhimu ya kumpa mtu aliye ungua moto ni;-(a) kummwagia maji (b) kumfunika nguo (c) kumwagia aside (d) kumfunika blanketi (e) kumpaka asali
- Huduma ya kwanza anayopewa mtu aliyezimia ni (a) kumpa hewa ya oksijeni (b) kumpa juisi ya nazi mbichi (c) kumlaza juu chini na kumbonyeza tumbo (d) kumpa maji yaliyochanganywa na glukosi (e) kumpa juisi ya malimao, sukari na chumvi
- Ni ugonjwa gani unasababishwa na utupaji ovyo wa taka? (a) Malale (b) Homa ya tumbo (c) Kipindupindu (d)malaria
- Njia nzuri ya kutekeza taka za nyumbani kama vyakula ni; (a) Kulisha wanyama (b) Kuziunguza (c)Kuzifukia ardhini (d) Kutumia kama mboji
- wakati wa kufanya usafi wa mazingira glavu huvaliwa ili…………(a) kupunguza uchafu yabisi (b) kuondoa harufu mbaya (c) kujikinga na maambukizi ya magonjwa (d) kuongeza unadhifu kazini
- Lipi sio madhara ya taka katika mazingira yetu? (a) Kuleta magonjwa (b) Kusabisha magonjwa (c) Kupendezesha mazingira (d) Kutoa harufu mbaya
- Hatua ya kwanza ya kuteketeza taka zitokazo mijini ni (a) Kuzichoma (b) Kutenganisha (c) Kuziloweka (d) Kulisha wanyama
- Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......(a) Tumbo (b) Figo (c) Mapafu (d) Moyo (e) Ubongo
- Huduma ya kwanza ni nini? (a) Msaada wa dharura apewao mgonjwa na daktari. (b) Msaadawa awali apewao mgonjwa kabla ya kupelekwa hospitali. (c) Msaada kwa ajili ya mtu aliyeungua moto. (d) Msaada kwa ajili ya mtu aliyeumwa na nyoka. (e) Msaada kwa ajili ya mtu aliyevunjika mfupa.
- Mojawapo ya athari za kupaka mafuta kwenye jeraha la moto ni: (a) kuongeza joto kwenye jeraha (b) kuongeza maumivu kwenye jeraha (c) kuruhusu hewa kupita kwenye jeraha (d) kusababisha vijidudu kuingia kwenye jeraha (e) kuongeza malengelenge.
- Huduma ipi ya kwanza kati ya zifuatazo hutolewa kwa mtu aliyekazwa na misuli? (a) Kumfanyisha mazoezi ya viungo (b) Kumpumzisha kitandani (c) Kufunga misuli kwa bandeji (d) Kumpa dawa ya kutuliza maumivu (e) Kuchua polepole misuli husika
- Ipi kati ya sentensi zifuatazo inatoa maana ya huduma ya kwanza?.............(a) Msaada wa haraka anaopewa mtu kabla ya kwenda hospitali. (b) Msaada wa haraka anaopewa mtu baada ya kufika hospitali.(c) Msaada wa haraka unaotolewa kwa mtu na mtaalamu wa afya. (d) saada unaotolewa kwa mtu aliyezirai. (e) Msaada unaotolewa kwa mtu aliyeumwa na nyoka.
- UKIMWI husambazwa kwa kupitia: (a) kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI (b) kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI (c) kuongea na mwathirika wa UKIMWI (d) kuwekewa damu (e) kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.
- Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI? (a) Vaa nguo safi (b) Nawa kwa sabuni (c) Vaa glovu (d) Sali (e) Mruhusu apumzike
- Kipi kati ya vifuatavyo ni maarufu kwa kuchangia maambukizi ya WU katika jamii? (a) Uchangiaji wa sindano, miswaki, damu na ngono zembe. (b) Kanda za video, nyimbo, muziki na maigizo. (c) Televisheni, magazeti na vipeperushi kuhusu WU. (d) Kondomu, wataalamu wa afya, semina na taasisi za UKIMWI. (e) Tohara kwa wanaume na wanawake.
- Mgonjwa wa UKIMWI anastahili kupata mlo maalumu ili; (a) aweze kupona haraka (b) asiambukize watu VVU (c) awe na nguvu ya kufanya kazi (d) mwili upambane na maradhi (e) VVU viangamie kabisa
- Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI? (a) Kuvimba kwa matezi (b) Kupoteza uzito (c) Kuharisha kusikokoma (d) Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida. (e) Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.
- Moja kati ya zifuatazo ni dalili ya ugonjwa wa anemia selimundu…………(a) Damu kutoka mfululizo kwenye jeraha (b) Mishipa ya damu kupasuka hasa iliyo kwenye tishu laini (c) Kupata choo chenye damu (d) Kupungukiwa na damu mara kwa mara
- Mojawapo ya tahadhari za kuchukua kwa wagonjwa wa anemia selimundu ni; (a) Kumpatia mgonjwa mlo kamili (b) Kumpatia chanjo (c) Kufanya mazoezi magumu (d) Kumpatia mgonjwa maji ya kutosha au chakula cha maji maji
Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu maswali yafuatao

Chunguza picha kisha jibu maswali yafuatao;
- Onyesha sehemu ambayo hutoa mbegu za kiume
- Taja umuhimu wa sehemu yenye nambari 5
- Onyesha sehemu inayoshikilia na kukinga ua
- Sehemu yenye nambari 4 inaitwaje?
- Ni sehemu gani inapokea mbegu za kiume?
LEARNINGHUBTZ.CO.TZSAYANSI STANDARD SIX EXAM SERIES 53
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA KWANZA DARASA LA SITA
SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MUDA:1: 30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
MAELEKEZO:
- Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
- Kumbuka kuandika majina yako.
- Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
SEHEMU A. CHAGUA JIBU SAHIHI
- Mishipa ya damu, neva za fahamu una tezijasho hupatikana kwenye sehemu gani ya Ngozi?
- Sehemu ya ndani b. Sehemu ya nje c. Sehemu ya ndani na nje d. Sehemu zote za ngozi
- Kazi ya tezijasho ni A. Kutengeneza maji B. Kutengeneza jasho C. Kutoa damu mwilini D. Kusafisha damu
- Athari za joto kwenye utoaji takamwili kwa njia ya Ngozi ni A. Kufanya vitundu vya jasho kutanuka na kutoa jasho kwa wingi B. Kufanya vitundu vya jasho kusinyaa na kutoa jasho kwa wingi C. Kufanya vitundu vya jasho kutanuka na kutoa jasho kidogo D. Kupiteza fahamu
- Mfumo wa utoaji takamwili unajumuisha ogani kuu nne ambazo ni A. Figo, ini, Ngozi na mapafu B. Figo, ulimi, Ngozi na mapafu C. Ini, utumbo mpana, Ngozi na mapafu D. Ini, ngozi, moyo
- Seli nyekundu za damu zilizokufa hutolewa mwilini kupitia
- Mkojo
- Jasho
- Kinyesi
- hewa
- Mtu anayeishi na VVU hutumia dawa
- Kwa miezi 6 mfululizo
- Kila anapohisi maumivu
- Kwa Maisha yake yote
- Kwa miaka miwili
- Moja ya faida ya kutumia “ARV” ni
- Kurudisha na kuongeza kinga mwilini
- Kuweza kuongeza usugu wa virusi
- Kuongeza kasi ya kuzaliana kwa VVU mwilini
- Kuangamiza virusi
- Ipi kati ya hizi sio njia ya kuambukiza VVU?
- Kukumbatiana
- Kufanya ngono bila kinga
- Kuekewa damu yenye virusi
- Kutumia vifaa vya kukata vilivyotumiwa na mtu mwenye virusi
- Kwa nini ni muhimu kuosha matunda kabla ya kula?
- Kuondoa sumu
- Kuondoa vimelea
- Kuondoa utomvu
- Kuondoa harufu mbaya
- Kuondoa chumvichumvi
- Magonjwa yapi kati ya yafuatayo huzuiliwa kwa chanjo?................
- Surua na kifaduro
- Kichocho na malaria
- Kuhara na mkamba
- Ukimwi na kisukari
- Kifua kikuu na tetekuwanga
- Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa
- UKIMWI
- Trikomona
- Kaswende
- Klamedia
- Trakoma
- Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?
- Wote walioko hewani
- Basili
- Plasimodiamu
- Fungi
- Amiha
- Kipi kati ya vimiminika vifuatavyo kianaweza kusababisha ajali ya kuungua moto?
- Uji wa moto
- Juisi
- Asali
- Soda
- Mtu aliyeungua moto hupewa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa……………
- Nyumbani
- Shule
- Kulala
- Hospitalini
- Ipi sio faida ya huduma ya kwanza
- Kupunguza maumivu
- Kuponya mgonjwa
- Kuokoa Maisha
- Kumpa mgonjwa matumaini
- Kipi akipaswi kufanyiwa mtu aliyeungua moto?
- Kumwagilia maji
- Kumtoa kwenye chanzo cha moto
- Kumfunika na blanketi kama nguo zimeshika moto
- Kumpatia huduma ya kwanza
- Kutokuoga kunaweza kukasababisha;
- Ugonjwa ngozi
- Homa
- Minyoo
- Kuharisha
- Maji katika chakula husaidia;
- Kutoa uchafu
- Mmeng’enyo wa chakula
- Kusafisha damu
- Kuondoa uchafu
- Ipi sio kanuni ya usafi?
- Lishe bora
- Usafi wa mwili
- Mazoezi
- Kulewa
- Kazi ya mafuta mwilini ni;
- Kuleta nguvu na joto
- Kulinda mwili
- Kujenga mwili
- Kujenga mifupa
- Sehemu ipi katika nyenzo daraja la kwanza huwa katikati?
- Mzigo
- Jitihada
- Egemeo
- toroli
- Jozi ifuatayo ni mfano wa nyenzo daraja la pili
- Opena na toroli
- Sepeto na toroli
- Mizani na mlango
- Mlango na sepeto
- Mojawapo ya vifaa vifuatavyo ni mfano wa kabari:
- Mtange
- Toroli
- Patasi
- opena
- Gesi hii utumia kuunda mbolea.
- Agoni
- Nitrojeni
- Kabonidayoksaidi
- Amonia
- Ipi sio sifa ya hewa
- Ina harufu
- Haina rangi
- Haionekani
- Inachukua nafasi
- Ipi kati ya hizi sio sehemu ya hewa
- Oksijeni
- Hydrogeni
- Agoni
- Nitrojeni.
- Shina la mmea likiwa jembamba, refu na majani kuwa na rangi ya manjano ni ukosefu wa:-
- Madini
- Maji
- Jua
- Hewa
- Kipi kati ya hivi haviongezi hewa ya kabonidayoksaidi kwenye angahewa?
- Moshi wa magari
- Shughuli za viwandani
- Ukataji miti
- Gesi ya kupikia.
- Ipi sio kazi ya maji katika mimea?
- Kuyeyusha virutubisho
- Kubeba kabohaidreti kutoka kwenye majani kwenda kwenye sehemu zingine.
- Kufanya mimea kuwa imara
- Husaidia mimea kutengeneza chakula
- Mimea kudumaa na majani kukosa rangi yake husababishwa na:-
- Potasi
- Naitrojeni
- Kolisiama
- Fosiforasi
- Udongo unaopitisha maji sana unaitwa?
- Udongo kichanga
- Udongo tifutifu
- Udongo changarawe
- Udongo wa mfinyanzi
- Udongo unaofaa kwa kufinyanga ni
- Udongo tifutifu
- Udongo laini
- Udongo wa mfinyanzi
- Udongo wa kichanga
- Wakulimia hupendelea udongo gani?
- Udongo tifutifu
- Udongo wa kichanga
- Udongo wa mfinyanzi
- Udongo changarawe
- Akyumuleta ni muungano wa seli zilizoungwa pamoja na hutumika kutoa umeme mkondo mnyoofu kwa matumizi ya:
- baiskeli, pasi na simu
- magari, matrekta na simu
- friji, pasi na feni
- baiskeli, friji na jiko la umeme.
- Seli kavu, jiko la mkaa na pasi
- Vyanzo asilia vya nishati katika maisha ya kila siku ni:
- kuni, moto na maji
- umeme, sumaku na gesi asili
- kuni, jua na upepo
- moto, upepo na sumaku
- umeme, upepo na maji
- Uhusiano kati ya sumaku na umeme ni................
- Chanzo cha sumaku ni nguvu ya atomiki
- Umeme huzuia mvutano wa sumaku.
- Popote penye usumaku pana umeme.
- Popote penye umeme pana usumaku.
- Sumaku huzuia umeme.
- Faili lenye mkusanyiko wa mkekakazi mmoja au Zaidi huitwa?
- Laha
- Kitabukazi
- Seli
- Sarafu
- Seli inayosisimuliwa kwenye screen ambayo ndiyo inashughulikiwa kwa wakati huo huitwa?
- Kiolezi
- Kikasha jina
- Seli amilifu
- Seli mtandao
- Tofauti ya potenshali kati ya ncha za way ani volti 12. Kiasi cha mkondo wa umeme unaopita ni ampia 0.4. Je waya huo una ukinzani wa ohm ngapi?
- 25
- 4.8
- 30
- 20
- Mashine ipi kati ya hizi zifuatazo ni mashine tata?
- Kabari
- Wenzo
- Cherehani
- Mteremko.
SEHEMU B:
Jibu maswali yafuatayo kwa ufasaha.
- Eleza maana ya maneno haya:
- Ufanisi
- Manufaa ya kimakanika
- Ikiwa mzigo wenye kilogramu 60 utanyanyuliwa mita 1 juu, jitihada itavuta mita 1 chini kwa kutumia roda tuli.
- Je, jitihada ina kilogramu ngapi?
- Tafuta thamani ya manufaa ya kimakinika
- Tafuta uwiano wa mwendo Dhahiri
- Tafuta ufanisi wa roda tuli
- Eleza kanuni ya ohm
- Taja mahitaji manne ya usanishaji wa chakula
- Eleza athari za kukosekana maji ya kutosha katika mimea
LEARNINGHUBTZ.CO.TZSAYANSI STANDARD SIX EXAM SERIES 41
LEARNINGHUBTZ.CO.TZSAYANSI STANDARD SIX EXAM SERIES 39
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
SAYANSI- MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
DARASA LA SITA
MUDA: 1.30
MAELEKEZO
- Mtihani huu unasehemu mbili
- Jibu maswali yote 45
- Hakikisha kazi yako ni safi
SEHEMU A. Chagua jibu sahihi.
1. Ukuaji wa viumbe hai unahusu uongezekaji wa yafuatayo isiopokuwa;
- Kimo
- Uzani
- Unene
- Umbo la seli
2. Kipi sio mahitaji muhimu ya ukuaji wa mimea
- Gesi ya kabonidayoksaidi
- Maji
- Gesi ya Nitrojeni
- Mwanga na joto
3. Kazi ya umbijani ni:-
- Kutengeneza chakula
- Kunasa nishati ya jua
- Kuchanganya maji na nishati ya jua
- Kupatia mmea rangi ya kujani
4. Kitendo cha mimea kusanisi chakula kwa kutumia nishati ya mwanga wa jua huitwa
- Usanisi
- Fotosinthesis
- Usanisuru
- Husharabu
5. Shina la mmea likiwa jembamba, refu na majani kuwa na rangi ya manjano ni ukosefu wa:-
- Madini
- Maji
- Jua
- Hewa
6. Kipi kati ya hivi haviongezi hewa ya kabonidayoksaidi kwenye angahewa?
- Moshi wa magari
- Shughuli za viwandani
- Ukataji miti
- Gesi ya kupikia.
7. Ipi sio kazi ya maji katika mimea?
- Kuyeyusha virutubisho
- Kubeba kabohaidreti kutoka kwenye majani kwenda kwenye sehemu zingine.
- Kufanya mimea kuwa imara
- Husaidia mimea kutengeneza chakula
8. Mimea kudumaa na majani kukosa rangi yake husababishwa na:-
- Potasi
- Naitrojeni
- Kolisiama
- Fosiforasi
9. Tishu inayopitisha maji na virutubisho kutoka kwenye mizizi kwenda sehemu zote za mimea huitwa?
- Floemi
- Zailemu
- Vinyelezi
- Vinywele
10. Gesi ambayo mimea hutumia kusanisi chakula ni:-
- Oksijeni
- Kabonidayoksaidi
- Nitrogen
- Agoni.
11. Moto unahitaji gesi gani ili kuwaka?
- Kabonidayoksaidi
- Agoni
- Oksijeni
- Nitrojeni
12. Gesi mojawapo kati ya hizi hutumia kusindika vinywaji
- Nitrojeni
- Agoni
- Kabonidayoksaidi
- Nioni
13. Gesi ambayo inachangia asilimia 0.003 ya hewa kwenye angahewa ni:-
- Nitrojeni
- Kabonidayoksaidi
- Agoni
- Oksijeni
14. Ni lipi ambalo sio matumizi ya kabonidayoksaidi?
- Kuzima moto
- Kuhifadhi chakula
- Kuunguza
- Kusanisi chakula
15. Gesi hii hutumika kwenye taa za umeme
- Agoni
- Helium
- Krypton
- Oksijeni
16. Ni yapi sio matumizi ya Oksijeni?
- Kuwasha moto
- Kutengeneza kula
- Kuhifadhi chakula
- Hospitali kwa wagonjwa waliozidiwa
17. Gesi hii utumia kuunda mbolea.
- Agoni
- Nitrojeni
- Kabonidayoksaidi
- Amonia
18. Ipi sio sifa ya hewa
- Ina harufu
- Haina rangi
- Haionekani
- Inachukua nafasi
19. Ipi kati ya hizi sio sehemu ya hewa
- Oksijeni
- Hydrogeni
- Agoni
- Nitrojeni.
20. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...
- joto na unyevu
- unyevu na mwanga
- upepo na mwanga wa jua
- mawingu na upepo
- unyevu na upepo
21. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:
- mmea kukosa madini joto
- mmea kushindwa kusanisi chakula
- majani ya mmea kukauka
- majani ya mmea kuwa njano
- maj ani ya mmea kupukutika.
22. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:
- osmosis
- difyusheni
- msukumo
- mgandamizo
- mjongeo
23. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?
- Wadudu
- Mimea
- Wanyama
- Virusi
- Ndege
24. Ipi kati ya zifuatazo siyo kazi ya mizizi katika mimea?..............
- Kusharabu madini ya chumvi.
- Kusharabu maji
- kushikilia mmea
- Kutengeneza chakula cha mmea
- Kutunza chakula cha mmea
25. Gesi ipi hupunguzwa angani na mimea?..................
- Kabondioksaidi
- Oksijeni
- Haidrojeni
- Kabonimonoksaidi
- Naitrojeni
26. Ni mmea gani ya hizi hauifadhi chakula katika shina?
- Miwa
- Magimbi
- Viazi
- Karoti
- Tangawizi..
27. Katika jani, umbijani hupatikana kwa wingi wapi?
- Epidamisi ya juu
- Epidamisi ya chini
- Seli linzi
- Stomata
- Selisafu za kati
28. Ni sehemu gani ya jani yenye seli zenye kloroplasti?
- Kikonyo
- Lamina
- Kingo
- Kishipajani
- Vena kuu
29. Usanishaji chakula hufanyika katika sehemu gani kuu ya mimea?
- Mizizi
- Majani
- Shina
- Ua
- Jani
30. ………….Huruka juu kwa mabawa yenye manyoya
- Ndege
- Popo
- Mbu
- Kipepeo
- Panzi
31. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?
- Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini.
- Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
- Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
- Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
- Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.
32. Kundi lipi limeainisha wanyama wenye uti wa mgongo?
- Konokono, mjusi na kenge
- Papasi, panzi na mbungo
- Chura, mamba na mchwa
- Kuku, popo na bata
- Nyoka, panzi na mbuzi
33. …………..hutaga mayai majini hata kama yeye huishi nchi kavu
- Kobe
- Kasa
- Chura
- Mamba
- Nyangumi
34. …………………huishi majini lakini hutaga mayai yake nchi kavu
- Papa
- Kobe
- Mjusi
- Kasa
- Mamba
35. ……………ni mammalian lakini hana tezi za jasho
- Popo
- Nyangumi
- Mbwa
- Panya
- Sungura
.36. ………………hunatoa mbegu lakini hautoi maua
- Mchungwa
- Mvinje
- Mhindi
- Mwembe
- Mpera
37. Wakati unatoahuduma ya kwanza kwa mtu aluyeungua moto, hairuhusiwi kupaka….kwenye jeraha.
- Maji
- Mafuta
- Asali
- Dawa
38. Kipi kati ya vimiminika vifuatavyo kinaweza kusababisha ajali ya kuungua moto?
- Uji wa moto
- Juisi
- Asali
- Soda
39. Mtu aliyeungua moto hupewa hudumaya kwanza kabla ya kupelekwa………………..
- Nyumbani
- Shule
- Kulala
- Hospitalini.
40. Tunafanya mazoezi kwa kucheza ili…………………………..
- Kuwa na nguvu
- Kuwafurahisha walimu
- Tuendelee kusoma
- Tuimarishe afya ya mwili.
SEHEMUB. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia neno sahihi.
41. Kirutubisho cha aina ya _____________ husaidia katika ukuaji wa maua.
42. Kirutubisho kinachosaidia katika ukuaji wa majani huitwa________________
43. Kirutubisho cha aina ya_________________ husaidia katika ukuaji wa mizizi
44. Maji na virutubisho husafirishwa kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani kwa njia ya___________
45. Kitendo cha mimea kujitengenezea chakula huitwa______________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZSAYANSI STANDARD SIX EXAM SERIES 16
LEARNINGHUBTZ.CO.TZSAYANSI STANDARD SIX EXAM SERIES 5